Omba omba sio barabarani tuu
Boy:- baby ivi nikifa utakuja msibani?
Girl:-ntakuja ukinitumia nauli.
Hapo ndo unagundua kuwa sio kila omba omba yuko barabarani.
๐ค๐ค๐ค๐ค๐ค๐ค
Boy:- baby ivi nikifa utakuja msibani?
Girl:-ntakuja ukinitumia nauli.
Hapo ndo unagundua kuwa sio kila omba omba yuko barabarani.
๐ค๐ค๐ค๐ค๐ค๐ค
Ni kwa nini tunapata Mateso na shida katika Maisha? Kwa nini Mungu ameruhusu tuteseke?
Mungu hapendi mtu Ateseke lakini ni kwa njia ya ya Mateso mtu anaweza akapimwa IMANI yake, UNYENYEKEVU, UTII na Matumaini yake kwa Mungu.
Mateso na shida katika maisha ni nafasi ya kujifunza na Kuonyesha unyenyekevu, Imani na Matumaini ya mtu.
Mtu anaweza kujitesa au kukubali Mateso huku akiyachukulia kama malipizi ya dhambi zake au dhambi za wengine.
Sio rahisi kwa mtu wa kawaida kuweza kukubali au kujitesa kwa ajili ya dhambi hasa kwa dhambi zisizokua zake, Ni watu wachache Wenye fadhila hii. Mfano Watakatifu kama Mt. Faustina aliweza kuchukua Mateso kama malipizi ya dhambi hasa za watu wengine ambapo alikubali magonjwa shida na Kudharauliwa kama malipizi ya dhambi.
Kware au Kwale au Kereng’ende ni jamii ya ndege ambao kwa sasa wanafugwa majumbani na wanaotaga mayai kama kuku ama bata na kwa wingi sana.
Ndege hawa ni wadogo 280gm – 300gm, rangi ya kwale ni kahawia au kijivu na wana michirizi au madoa. Mara nyingi miguu yao ni myekundu au rangi ya manjano na koo lao ni jekundu, jeupe, jeusi au rangi ya manjano.
1. Kware anakula chakula chochote anachoweza kula kuku ikiwemo chakula cha broiler. Kama utaamua kuwapa chakula cha broiler unawapa โstarterโ kware wenye umri kuanzia siku moja hadi wiki ya tatu baada ya hapo unawapa Falcon au hill.
2. Ukiweza kuwatengenezea chakula chako mwenye kutumia pumba nk. Ni vizuri zaidi kwa mayai yenye lishe 100%
3. Kware 100 wenye umri wa mwezi hutumia kiroba cha kilo 20 kwa wiki 3.
4. Kware hawamalizi chakula kama kuku.
5. Pia kware hupewa majani kama mchicha nk.
Kware dume humpanda jike kwa muda kidogo, Hapo jike anakuwa tayari kutaga na hutaga mayai 290 hadi 310 kwa mwaka (hii hulingana na lishe nzuri atakayopatiwa).
Mayai ya Kware huatamiwa kwa siku 18 na huanza kuanguliwa vifaranga kwa muda wa siku 2, kuanzia siku ya 18 na hadi 20.
Njia bora ya kutotolesha mayai ya Kware ni kwa kutumia incubator ambapo mayai huatamiwa kwa wingi ndani ya siku 18.
Vifaranga wapatiwe chakula โSTARTER PELLETโ na maji masafi ya kutosha. Siku ya 1 wawekee โGLUCOSEโ kwenye maji, Packet moja kwa lita 20 za maji, na siku ya pili hadi ya tano wawekee Amin Total kwenye maji, Wape maji pekee siku ya sita na siku ya saba wapatie chanjo ya Newcastle. Utawapatia joto kwa njia ya umeme kwa โBULBโ mbili (2) za 200watts kwa kila vifaranga 300, ama unaweza kuweka taa ya โEnergy Serverโ pamoja na jiko la mkaa uliofunikwa na majivu ambao utakidhi kuwapatia joto sawia kwa masaa 24 kwa siku 7. (Majivu yanasaidia moto kukaa kwa muda mrefu)
Banda/box lako liwe la ukubwa wa 1.5m x 1.5m (au eneo la ukubwa huo ndani mwa banda kubwa la kufugia kuku) lazima uzingatie usalama wa vifaranga dhidi ya panya, paka au vicheche. Unatakiwa kuweka magazeti au mabox chini kwenye sakafu yatakayosaidia usafi. Kwa week ya kwanza chakula kitawekwa chini na tunashauri utumie chakula cha pellet ili kusaidia vifaranga wasiteleze na kuathiri miguu. NOTE: Weka gololi au mawe kwenye drinkers zako ili kuzuia vifaranga wasizame ndani ya (drinkers) maji na kufa.
Vifaranga wataendelea kupewa chakula โSTARTER PELLETโ na maji safi. Wataendelea kuhitaji โmwangaโ wa kutosha muda wote na joto la wastani bulb 2 za watts 100 au moja ya watts 200
Uhitaji wa joto utapungua, ila ni kipindi ambacho wanakula chakula zaidi kwa ajili ya kukua. Ni vizuri waendelee kupata taa ili kupata mwangaza utakayowawezesha kula mchana na usiku.
Kware wako hawatahitaji joto tena wawekee taa tu za energy server kipindi cha usiku, wape chakula na maji ya kutosha zaidi kwa ajili ya kukua.
Wiki ya sita kuelekea ya saba Kware wako wataanza kutaga mayai kila siku, kwa wastani Kware mmoja hutaga mayai 300 kwa mwaka.
Kware ni ndege wenye kinga kubwa na ni vigumu sana kushambuliwa na magonjwa kama kuku na mara wanapougua ni rahisi sana kutibika. Magonjwa yanayoweza kuwapata Kware ni typhoid, mafua na kuharisha .
Vifuatazo ni vitu vya asili vinavyotumika kutibu magonjwa mbali mbali kwa Kware na yanayopatikana kwa wingi katika maeneo ya mfugaji. Madawa haya hutumika kwa kiwango cha wastani na hayana kipimo maalum kwani hata ukiyazidisha hayana madhara.
Madawa haya hutumika kutibu kuharisha damu pamoja na mafua kwa vifaranga vya Kware. Chukua kiasi kidogo cha mwarubaini kisha twanga vizuri kupata maji maji. Kamua maji yale, kisha weka katika maji uliyoandaa kuwanywesha vifaranga wako. Kata vipande vidogovidogo vya aloe vera (jani moja laweza kutosha) na tia katika maji yaliyochanganywa na mwarobaini, kisha wapatie vifaranga wanywe (Aloe Vera itaendelea kujikamua yenyewe ikiwa ndani ya maji huku vifaranga wakiendele kunywa).
Hii hutumika kukinga na kutibu vifaranga vya kware wanaosumbuliwa na kuharisha damu. Unachukua kitunguu swaumu na kuondoa maganda ya nje kisha kusafisha na kukata vipande vidogo sana, na kuwawekea kama chakula. Vifaranga wanapenda sana vitunguu hivyo na watakula kwa kasi kama chakula lakini ni tiba tayari. Unaweza kuwapatia kila siku hadi watakapo pona.
Maziwa yanayotokana na ngโombe pia hutumika kutibu ugonjwa wa kuhara pamoja na kuwapa nguvu Kware waliolegea. Mnyweshwe maziwa hayo Kware anayeumwa bila kuyachemsha na umnyweshe maziwa ya kutosha kiasi cha kushiba. Unamnywesha mara tatu kwa siku. Hakikisha maziwa unayotumia yanatoka kwa ngโombe wanaotibiwa kila mara.
Siyo lazima Kware waugue ndipo uwapatie tiba hizi. Hakikisha unawapa tiba kabla hata hawajaugua hivyo utawakinga na magonjwa hayo. Waweza kuchanganya madawa hayo yote kwa wakati mmoja kwani hayana madhara.
Endapo madawa ya asili hayapatikani katika eneo la mfugaji basi waweza kuwatibu Kware kwa madawa yafuatayo ambapo vipimo huelezwa moja kwa moja kwa maandishi katika madawa hayo au kuelezwa na muuzaji pale utakaponunulia; Amprolium kwa ugonjwa wa kuharisha damu (Coccidiosis), Fluban,Coridix au Doxyco kutibu mafua (Coryza) na Esb3,Trisulmycine au Trimazine hutumika kwa homa ya matumbo (Typhoid).
Wanapokosa madini ya kutosha kwenye chakula huweza kupata madhara yafuatayo:-
1. Kuharisha
2. Kunyonyoka manyoya
3. Kupunguza kasi ya kutaga mayai.
Siku ya 7 lazima vifaranga wapatiwe chanjo ya โkideri/mdondoโ
(respiratory & digestive diseases) kwa dawa inayoitwa โnewcastleโ. Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi na pia husababishwa na virusi kwa njia ya hewa.
Siku ya 14 lazima wapewe chanjo ya โgumboroโ. Chanzo cha
maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi na pia husababishwa na virusi kwa njia ya hewa.
Siku ya 21 lazima warudie chanjo ya โNewcastle (aina ya IBDL)โ. Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi na pia husababishwa na virusi kwa njia ya hewa.
Siku ya 35 lazima wapate chanjo ya โNduiโ.
1. Trei ya (mayai 30) ya KWALE inauzwa shilingi 30,000 .
2. Kifaranga wa Kware wa siku moja anauzwa shilingi 2500 โ 3000
3. Kware wa week 4 (mwezi mmoja) anauzwa kwa shilingi 10,000โ 12,000
4. Kware aliyeanza kutotoa (week 6) huuzwa shillingi 20,000 โ 25,000
5. Kware kwa aliyekomaa kwa ajili ya kitoweo huuzwa kwa shilingi 25,000
6. DROPING za Kware huuzwa kwa shilingi 10,000 kwa 50kg kwa wafugaji wa samaki
Soko la KWALE liko juu sana kwa mayai na nyama. KWALE pia hutofautiana bei kwa jike na dume.
Ufugaji wa kwale hua na faida ukilinganisha na ufugaji wa ndege wengine
ยท Chanzo cha kipato kwa wafugaji.
ยท Hawana gharama sana katika suala kufuga.
ยท Hawataji utaalam sana katika kuwafuga.
ยท Mayai yake ni tiba ya magonjwa mbalimbali.
ยท Mayai yake hayakosi soko.
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.
MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.
MWAL: Na wewe James??
JAMES: mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiweโฆโฆ”
Akameza mate kisha akaendeleaโฆ.
“Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali.”
MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??
JENNY: Nataka kuwa mke wa James.!!
Mchele – 2 Mugs
Viazi – 3
Nyama ya Kusaga – 1 Pound
Mboga mchanganyiko za barafu – 1 Mug
(Frozen vegetable)
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi – 2 vijiko vya supu
Garam masala – 1 kijiko cha supu
Nyanya – 1
Kitungu maji – 1
Mdalasini nzima – 1 vijiti
Karafuu – 3 chembe
Pilipili mbichi – 1
Chumvi – kiasi
Maji – 2 ยฝ Mugs
Mafuta – 3 vijiko vya supu
Osha mchele na uroweke kiasi kutegemea aina ya mchele.
Katakata viazi kaanga katika mafuta, toa weka kando.
Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
Tia nyama ya kusaga, thomu na tangawizi, pilipili, bizari zote na chumvi. Kaanga hadi nyama iwive.
Katakata nyanya uliyokatakata itie katika mchanganyiko wa nyama na endelea kukaanga kidogo tu.
Tia mboga ya barafu (frozen vegetables)
Tia maji, kidonge cha supu.
Yatakapochemka tia mchele.
Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa ยฝ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.
Mwanamke unywele hasa ukiwa nao, hii ni kauli upya ambayo Muungwana blog inakupa siku ya leo. Miongoni mwa maswali ambavyo huwa tunaulizwa na wasamoaji wetu ni pamoja ni kwa jinsi gani naweza kutengeneza nywele zangu ili ziwe za kuvutia?
Basi nasi bila ya haiana yeyote ile tunakuletea somo hili maalum kwa ajili ya watu wote ambao wanatamani kujua namna ya kuzifanya nywele zako zivutie. Kwanza kabisa kuna vitu vingi vinavyoweza kufanya nywele zako zikakosa afya na mvuto, vitu kama vumbi, upepo, mvua, jua, maji na madawa tunayoweka kwenye nywele zetu pamoja na vyakula tunavyokula ni chanzo kikuu cha nywele zetu kuharibika na kukosa afya na mvuto
Hivyo zifuatazo ndizo njia ya kufanya nywele zako zivutie:
Tumia shampoo inayoendana na nywele zako, kuna nywele za aina tofauti. kuna nywele kavu, zenye mafuta, mchanganyiko, na pia kuna nywele nyepesi, laini, ngumu na nzito. zipo aina tofauti za shampoo zinazoendana na aina ya nywele zilizopo . hivyo basi ni vyema unapotaka kuosha nywele ukajua ni aina gani ya shampoo utumie, pia kwenye condition napo unatakiwa kufanya hivyo hivyo.
Jaribu kuzichana nywele kwa kichanuo kikubwa, au jaribu kuziacha mpaka zikauke ndo uzichane. unapochana nywele mbichi tumia kitana kikubwa na chana taratibub ukianzia nyuma kuja mbele. kuchan nywele zikiwa mbichi bila kufuata utaratibu kutafanya nywele zako zikatike na ziharibike.
kula vyakula venye protin na matunda kutasaidia kuimalisha afya ya nywele zako na kuzifanya ziwe nzuri na za kuvutia.
kukata ncha za nywele zako kunasaidia kufanya nywele zako kujizaa upya, mara nyingi seli katika ncha za nywele hufa. seli zinapokufa huzui nywele zinazozaliwa kushindwa kustawi vyema na hivyo kuzifanya nywele zako kukosa afya. japo wanawake wengi huwa hawapendi kukata ncha za nywele zao wakihofia nywele zao kuonekana fupi. lakini ukweli ni kwamba unapokata ncha za nywele zako unasaidia nywele zako kupata nafasi ya kukua vizuri na kuwa zenye afya nzuri na kuvutia.
kuosha nywele zako angalau mara moja kwa wiki kutasaidia kuzifanya nywele zako ziwe na afya. Hata kama uko busy sana basi jitahidi isipite wiki mbili bila kuonsha nywele zako.
Unapotaka kulala hakikisha unazifunga nywele zako, unaweza kuzisuka mabutu au kuzifuna vizuri na kuzibana. kulala huki ukiwa umeziachia nywele zako hufanya nywele zikatike na kuharibika
Badala ya kutumia mafuta yenye kemikali nyingi kutoka viwandani, jaribu kutumia mafuta ya asili katika kutunza nywele zako. tumia mafuta kama ya nazi au parachichi kupaka nywele zako.
W akati utakapokuwa unaelekea kwenye sehemu yenye jua kali, vumbi au upepo. zilinde nywele zako kwa kuzifunika na kofia, scarf au mtandio. Pia unaweza kuzipaka sunscreen.
Ili kuongeza mbegu za kiume zingatia haya yafuatayo;
Chakula unachokula kina mchango mkubwa katika kutibu tatizo hili. Vyakula vingi vya kisasa havina uwezo wa kuongeza uwingi wa mbegu.
Punguza matumizi ya sukari na vyakula vya ngano. Ongeza zaidi matunda, mboga za majani na mafuta yenye afya.
Acha kutumia kahawa, vinywaji na vyakula vyenye kaffeina.
Kama una tatizo la kuwa na mbegu chache ni vizuri ukaacha kutumia vinywaji au vyakula vyote vyenye kaffeina kwanza.
Kitunguu swaumu kina Selenium na pia kinaondoa sumu mwilini vitu hivi viwili ni mhimu kwa ajili ya kuongeza spidi ya mbegu.
Vile vile Kitunguu swaumu kina โAllicinโ ambayo huongeza msukumo wa damu kwenda kwenye uume.
Kujitibu unaweza kuongeza kitunguu swaumu kwenye chakula unachopika. Pia unaweza kutafuna punje 2 au 3 kila unapoenda kulala au unaweza kukatakata hizo punje 3 vipande vidogo vido (chop) kisha unywe na maji.
Usile zaidi ya punje 3 kwa siku.
Mayai yanachukuliwa kama mbadala wa uhakika zaidi katika kuongeza uwingi wa mbegu pamoja na kuongeza spidi au kasi yake. Yana vitamini E nyingi na protini ya kutosha vitu viwili mhimu katika kuongeza mbegu. Tumia mayai ya kienyeji zaidi na sio ya kisasa.
Mboga hii ina Folic asidi ambayo ni mhimu katika kuongezeka kwa mbegu za kiume.
Ndizi zina Magnesiamu, Vitamini B1 na Vitamini C, vitu ambavyo ni mhimu sana kwa ajili ya kutengeneza mbegu za kiume. Vile vile Ndizi zina kimengโenya kimoja adimu sana kijulikanacho kama โBromeliadโ ambacho husaidia kuziweka sawa homoni zinazohusiana na tendo la ndoa.
Mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya Zinki ambayo ni mhimu katika kuundwa au kutengenezwa kwa mbegu za kiume na homoni ya testosterone.
Vile vile mbegu hizi zina vitamini B, C, D, E, na K ambazo zote ni vitamini mhimu katika kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa na nguvu kwa ujumla.
Mboga za majani zinapunguza homoni ya โestrogenโ na hivyo kufanya homoni ya โtestosteroneโ ipatikane kwa wingi na kiurahisi zaidi na hivyo mbegu zako ziweze kuongezeka bila vipangamizi vyovyote. Homoni hii ndiyo inayohusika na kuzalishwa kwa mbegu
Kutokunywa maji ya kutosha kila siku kuna uhusiano wa moja kwa moja na kupungua kwa uwingi wa mbegu. Mbegu zako zimetengenezwa kwa maji, zipo kwenye hali ya kimiminika.
Kunywa maji ya kutosha kunasaidia kutengenezwa kwa mbegu nyingi.
Kutegemea na uzito wako unaweza kuhitaji maji lita 2 mpaka 3 kila siku.
Vyakula hivi ni pamoja na tunda la parachichi na karoti, mbegu za maboga, ufuta, alizeti, maharage, chungwa, papai, bamia nk
Mtoto alimwuuliza baba yake,
Mtoto: Baba unaweza kumwachia hilo gari lako house boy/girl akaliendesha?
Baba: siwezi kumwachia gari langu hili aliendeshe ni ghali sana.
Mtoto: je mnaweza kumwachia chumba chenu house boy/girl kikiwa wazi na mkaenda kazini?
Baba: haiwezekani kamwe kuna vitu vya gharama na pia heshima haitakuwepo.
Mtoto: unaweza ukampa house boy/girl ATM CARD yako na namba ya siri ukakuchulie pesa?
Baba: mtoto unatafuta balaa sasa, unataka siku akiiba hii card akachukue pesa zote tuwe maskini, sithubutu.
Mtoto: aahaaaaaa, kumbe hauwezi kumkabidhi chochote chenye thamani house boy/ girl, sasa kwa nini mnanikabidhi mimi kwa house boy/girl na nyie mnaenda kazini mpaka mnarudi kumbe mimi sina thamani kwenu eeeeh!
Katika Jamii nyingi duniani, dhana ya urembo imekuwa na mitazamo tofauti kwa watu wengi. Kila mmoja anautafakari urembo kwa namna yake kulingana na malezi na tamaduni za mahali husika. Wako wanaoamini kuwa mrembo ni lazima awe na ngozi nyeupe, wengine hudhani kuwa ili kuonekana mrembo, lazima uwe na nywele ndefu, lakini pia wapo wanaodhani kwamba ili uwe mrembo ni lazima uwe na umbo namba nane na wapo wanaojua urembo ni kuwa mwembamba (kimbaumbau au Miss) au kuwa mrefu na wapo wanaoamini urembo ni kuwa mnene.
Hiyo yote ni mitazamo tu, lakini tafsiri halisi kutoka kwa wataalamu wa urembo ni kwamba; urembo ni hali ya kuwa na afya bora.
Je, Mpenzi msomaji ulikuwa unajua hili? Nakuomba Kabla hujafanya chochote kuhusu afya yako, unatakiwa kuamini kwamba wewe ni mrembo. Ikiwa utasimama katika hilo ni kweli utakuwa mrembo siku zote. Basi ili kubaki kuwa mrembo tujifunze haya machache leo ya kufanya:
Hakikisha ngozi yako inakuwa safi muda wote. Unaweza kutumia njia mbalimbali kama vile kuondoa ngozi zilizokufa mara kwa mara. Kuondoa mafuta yaliyogandamana katika ngozi kwa kufanyia masaji ngozi yako ili kurahisisha mzunguko wa damu yako.
Ikiwa hili litafanyika kwa umakini ni wazi kuwa matatizo ya kuwa na chunusi au weusi katika ngozi yako havitakuwepo kwako.
Tumia bidhaa za nywele, ambazo zinaendana na nywele zako na hakikisha unazingatia mambo muhimu katika uboreshaji wa nywele zako.
Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kutokutumia vifaa vinavyounguza vywele.
Epuka kuosha nywele kwa maji ya moto, pia kuchana nywele zikiwa na maji, kwani unaweza kusababisha kukatika kwa nywele zako.
Tumia vipodozi pale inapobidi, usipendelee kutumia vipodozi mara kwa mara kwani wakati mwingine matumizi ya mara kwa mara ya vipodozi, husababisha madhara katika ngozi yako, hasa unapotumia bila kufuata maelekezo ya wataalamu.
Hakikisha unapata usingizi wa kutosha kila siku. Kwa mujibu wa wataalamu, unatakiwa kulala si chini ya saa nane kila siku. Ikiwa utapata usingizi wa kutosha ni wazi kuwa macho yako yataonekana yenye nuru siku zote. Pia utazidi kuonekana kuwa mrembo zaidi.
Hakikisha mazoezi yanakuwa sehemu ya maisha yako, hii itasaidia kukufanya uonekane siyo tu mrembo, bali pia mwenye kujiamini.
Usafi wa meno pia ni miongoni mwa mambo ya kuzingatia unapoamua kuboresha urembo wako. Hakikisha unapiga mswaki walau mara mbili kwa siku kila siku au kila baada ya kula.
Haya yameorodheshwa na wataalamu mbalimbali kuwa ni mambo yanayochangia urembo wa asili na mvuto wa ngozi na mwili.
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.
MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.
MWAL: Na wewe Nehemiah ??
Nehemiah : mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiweโฆโฆ”
Akameza mate kisha akaendeleaโฆ.
“Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali.”
MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??
JENNY: Nataka kuwa mke wa Nehemiah .!!
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuniโฆunaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuniโฆ๐๐๐๐
Unga – 2 Vikombe
Cocoa ya unga – 1 Kijiko cha supu
Sukari ya hudhurungi – 1 Kikombe
Siagi – ยพ Kikombe
Yai – 1
Molasses – ยผ Kikombe
Baking soda – 2 vijiko vya chai
Mdalasini wa unga – 1 kijiko cha chai
Tangawizi mbichi – 1 kijiko cha supu
Karafuu ya unga – ยฝ kijiko cha chai
Chumvi ยฝ kijiko cha chai
Vanilla ยฝ kijiko cha chai
Katika bakuli, chunga unga, baking soda, chumvi na cocoa. Weka kando.
Washa oven lipate moto huku unatayarisha biskuti.
Katika bakuli jengine, mimina siagi na sukari upige kwa mashini ya keki hadi mchanganyiko uwe laini kama dakika mbili.
Mimina molasses na yai ndani ya mchanganyiko wa siagi na sukari uchanganye vizuri.
Mimina unga kidogo kidogo huku unachanganya na mwiko hadi unga wote umalizike.
Mimina mdalasini, karafuu na tangawizi, changanya vizuri.
Weka mchanganyiko wako ndani ya friji kama masaa mawili. (Ukipenda unaweza kuhifadhi mchanganyiko wako ndani ya mfuko wa freezer na uoke siku nyengine.)
Tengeneza viduara vidogo vidogo.
Chovya kila kiduara katikati sukari, kisha panga kwenye treya ya kuoka
Rudisha viduara katika friji kama nusu saa.
Oka katika oven 350ยบF kwa muda wa dakika 15.
Toa biskuti kwenye oven na uache zipoe kama dakika kumi.
Panga kwenye sahani tayari kuliwa.
Wakati mafuta ya nazi yakiwa yamemengโenywa na mwili huhamasisha uundwaji wa nguvu mpya za ubongo zijulikanazo kama โketonesโ.
Ketones zina uwezo wa kusambaza nguvu katika ubongo hata kama insulin itakuwa chini ya kiwango kama matokeo ya ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
Insulin kazi yake kubwa ni kuishughulikia sukari (glucose) na hivyo kuzipa nguvu seli za ubongo.
Ubongo wa mtu mwenye ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu hauwezi kujitengenezea insulin yake kwa usahihi na vya kutosha. Kwa hiyo inashauriwa kutumia mafuta haya.
Mafuta ya nazi yanao uwezo wa kupigana na seli za kansa. Tafiti za karibuni zinasema kitu chochote chenye uwezo wa kuuongezea nguvu ubongo husaidia pia kuzuia kusambaa kwa seli za kansa katika mwili.
Zaidi ni kuwa mafuta haya yana uwezo wa kumdhibiti bakteria ajulikanaye kama โhelicobacter pyloriโ ambaye husababisha vidonda vya tumbo.
Kuongeza kinga ya mwili ni moja ya faida za mafuta ya nazi sababu ni mafuta ambayo hupigana dhidi ya bakteria, fangasi na virusi mbalimbali.
Paka moja kwa moja juu ya ngozi au kuyanywa pia kuchanganya kwenye vyakula mbalimbali kwa ajili ya kuongeza kinga yako ya mwili.
Mafuta ya nazi yana asidi mafuta nzuri zenye uwezo wa kusaidia na kuzilinda seli za ubongo na kuziwezesha kufanya kazi kwa ufasaha zaidi.
Mafuta ya nazi yanajulikana vizuri kwa uwezo wake wa kukuongezea uvumilivu yaani stamina.
Mafuta ya nazi ni dawa ya mba na mara nyingine hutumika kwa kuchanganywa na mafuta mengine
Ni mazuri kwa ngozi na yanatibu magonjwa mbalimbali ya ngozi.
Mfuta ya nazi yanaweza kuzuia mpaka asilimia 20 ya miale ya jua kushindwa kukufikia moja kwa moja kwenye ngozi yako kama utayafanya kuwa ndiyo mafuta yako ya kupakaa.
Wengi mnapenda kufanya scrub hasa usoni (facial). Kwa lugha nyepesi ni kitendo cha kusugua ngozi kwa dawa maalumu ili kuondoa uchafu wote na kuifanya ionekane nyororo na yenye kupendeza.
Sasa huhitaji dawa zenye kemikali kwa ajili hiyo wakati mafuta ya nazi yanaweza kukusaidia hilo bila madhara yoyote mabaya.
Fanya hivi changanya nusu kikombe (mln125) cha mafuta ya nazi na sukari kikombe kimoja na ufanye dawa ya kusugua na kusafisha uso wako.
Unaweza pia kutumia nazi yenyewe moja kwa moja kabla hujapata mafuta yake.
Tumezoea kutumia nazi jikoni kwenye mapishi, lakini nazi pia inaweza kutumika kama scrub ya asili ya ngozi yako.
Fuata hatua hizi zifuatazo ili kufanya ngozi ya uso wako iwe laini, nyororo na kufanya uso wako uwe laini, nyororo na wenye mvuto.
Scrub hii unaweza pia kuitumia kwa mwili mzima, lakini hapa nitaelezea namna ya kutumia kwa uso wako.
*Safisha uso wako kwa maji safi na sabuni ya kawaida isiwe sabuni ya dawa (medicated)
*Ukishamaliza hapo, utakaa hivyo bila kuuosha uso wako kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.
Ili kupata matokeo mazuri fanya hivi kwa muda wa siku 5 mfululizo bila kuacha, yaani mara moja kwa siku.
Amini nakuambia utapata matokeo mazuri mpaka mwenyewe utaifurahia ngozi yako na hata vocha utaninunulia kunipongeza.
Unatakiwa kupakaa tu sehemu yenye tatizo moja kwa moja huku ukinywa kijiko kidogo kimoja kila siku na hutakawia kupona hivyo vidonda.
Yanangarisha kucha na kuzikinga na wadudu.
Mafuta ya nazi Yanaweza kutumika kama dawa ya asili ya kufukuza wadudu (insect repellent) wakiwemo mbu. Unachohitaji ni kuchanganya pamoja na kiasi kidogo cha mafuta ya karafuu au ya mnanaa (mint) na ujipake juu ya ngozi yako na hakuna mdudu yoyote akiwemo mbu atakayekusogelea.
Mafuta ya nazi yana viondoa sumu vyenye nguvu zaidi ambavyo vinaweza kuulinda mwili wako dhidi ya vijidudu nyemelezi.
Zaidi, matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kurahisisha umengโenywaji wa madini ya kalsiamu tumboni mwako.
Upungufu wa madini ya kalsiamu mwilini husababisha mifupa kuwa hafifu jambo linaloishia kuleta ugonjwa wa mifupa (osteoporosis).
Kuzuia ugonjwa wa mifupa unahitaji kuongeza mafuta ya nazi kuwa sehemu ya chakula chako. Hii ndiyo faida ya mafuta ya nazi ambayo niliona si vema kama sitakuambia.
Watu wenye vitambi au unene uliozidi wanatakiwa kuongeza mafuta ya nazi kwenye milo yao na miili yao itakaa sawa yenyewe.
Matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kusaidia mafuta kuchomwa zaidi mwilini huku kiasi chako cha njaa kikishuka.
Mifadhaiko ni jambo lisiloweza kuepukika katika maisha yetu. Kazi ya mfadhaiko au stress ni kukufanya uwe imara zaidi, mpole na unayejiamini zaidi.
Unapofadhaishwa mwili wako huwa unajiongeza na kuwa na shauku ya kufanikiwa zaidi. Hata hivyo mfadhaiko unapodumu kwa muda mrefu unaweza kuleta madhara makubwa kwa mhusika kihisia na hata kimwili pia.
Mfadhaiko wa muda mrefu unaweza kupelekea huzuni mbaya na hatimaye kuathiri muonekano wako.
Watu wenye mifadhaiko (stress) ya muda mrefu huonekana ni wenye umri mkubwa hata kama umri wao bado ni mdogo.
Tafiti za karibuni zimeonyesha uhusiano wa karibu uliopo kati ya matumizi ya mafuta ya nazi na kupungua kwa mfadhaiko wa akili.
Tunaweza kusema kuwa, kitendo hiki cha kuondoa mfadhaiko au stress ni moja ya kazi ya kustajaabisha kabisa ya mafuta ya nazi. Asidi mafuta zilizomo ndani ya mafuta haya ndizo zinazohusika na kazi hii mhimu.
Ili mwili wako ubaki ni wenye afya na kuzuia usipatwe na magonjwa unahitaji kuwa na mfumo mzuri wa mmengโenyo wa chakula na wakati huo huo mfumo imara wa uchukuwaji wa viinilishe, madini na vitamini mbalimbali kutoka kwenye chakula unachokula.
Kwa bahati nzuri, kuuongezea nguvu mfumo wa mmengโenyo wa chakula ni kazi nyingine ambayo mafuta ya nazi yanaweza kukusaidia bila madhara mengine mabaya.
Matumizi ya mafuta ya nazi yatakuwezesha kuongeza uchukuwaji wa viinilishe mhimu kutoka kwenye chakula sababu mafuta haya yana madini ambayo huweza kuyeyuka kwenye mafuta kama kalsiamu na magnesiamu.
Zaidi, mafuta haya yanaweza kusaidia umengโenywaji wa mafuta mengine magumu ndani ya mwili kama matokeo ya kuimarishwa kwa vimengโenya vinavyohusiana na mmengโenyo wa chakula.
Kama unapata maumivu au matatizo yoyote katika kongosho au kibofu cha mkojo unahitaji kuongeza matumizi ya mafuta ya nazi.
Ukiendelea kutumia mafuta ya nazi kila mara utaweza kujitibu pia tatizo la mawe katika kibofu cha mkojo na kuondoa hali ya kutojisikia vizuri kutokana na magonjwa katika kongosho au kibofu cha mkojo.
Faida kubwa ya mafuta ya nazi haiishii katika uwezo wake wa kuchoma mafuta, bali yana kazi nyingine ya kushangaza zaidi nayo ni kutengeneza misuli ya mwili.
Kwenye bidhaa nyingi zinazouzwa zaidi duniani za kutengeneza virutubishi vya kutengeneza misuli ya mwili mafuta ya nazi lazima yawemo.
Kama unataka kuongeza misuli mingi mwilini kirahisi zaidi changanya tui zito la nazi kikombe kimoja (robo lita), ongeza vanilla vijiko vikubwa vitatu, ongeza maji maji ya chungwa vijiko vikuwa viwili na ndizi zilizoiva mbili.
Saga na mashine ya kusagia matunda jikoni (blender) mchanganyiko huu kwa pamoja na ule wote kutwa mara 1 kila siku.
Kuzuia kuoza kwa jino na magonjwa ya fizi ni moja ya kazi nyingine nzuri ya kushangaza ya mafuta ya nazi ambayo nimependa kukufahamisha kupitia makala hii.
Mafuta ya nazi ni dawa inayoweza kudhibiti bakteria wabaya na hivyo kuzuia kuoza kwa jino na maumivu mengine katika fizi. Ili kuzuia haya unahitaji tu kutumia mafuta yako ya nazi kama dawa yako ya mswaki kila siku.
Unaweza pia kuongeza kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto ili kutengeneza dawa ya kusafisha mdomo (mouthwash).
Kwa mjibu wa madaktari wengi, kuna uhusiano wa karibu kati ya madhara ya figo na kushindwa kufanya kazi kwa ogani hii mhimu.
Kama tatizo la kufeli kwa figo halitapatiwa ufumbuzi linaweza kupelekea kifo. Figo na Ini ni ogani mhimu zaidi katika mwili ambazo zinatakiwa kupewa uangalizi wa karibu kila mara zisipatwe na madhara yoyote.
Kwa bahati nzuri, mafuta ya nazi yanayo uwezo wa kulinda figo na Ini visipatwe na madhara yoyote mabaya moja ya kazi ya mafuta ya nazi mwilini ulikuwa huijuwi bado.
Wanasayansi wameviona viinilishe katika mafuta ya nazi ambavyo ni mhimu sana kwa afya ya Ini na figo katika mwili wa binadamu.
Nazi pamoja na mafuta ya nazi huwa na asidi mafuta mhimu sana ambazo huhamasisha uundwaji wa โMonooctanoinโ ambayo hufanya kazi ya kuyeyusha mawe katika kibofu cha mkojo na figo.
Wagonjwa ambao hawawezi kumudu gharama za upasuwaji kuondoa mawe katika figo na katika kibofu cha mkojo wanaweza kujitibu hilo kwa kutumia mafuta ya nazi kama dawa mbadala.
Unachohitaji kufanya ni kunywa tu kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi kila siku kutwa mara 1 mpaka utakapokuwa umepona.
Mafuta ya nazi hudhibiti uvimbe na kuondoa sumu mwilini, kazi hizi mbili zinayafanya kuwa dawa bora ya kutibu ugonjwa wa baridi yabisi.
Unahitaji kijiko kidogo kimoja cha mafuta haya kila siku ili kujitibu na ugonjwa wa baridi yabisi.
Faida za mafuta ya nazi zinahusu pia kurekebisha kazi za ogani za mwili kama kuweka sawa mapigo ya moyo, kupumua na kuzalisha homoni mhimu.
Tezi koromeo huzalisha homoni mbili ambazo huwa na msaada mkubwa katika kuongeza nguvu katika mfumo wa mmengโenyo wa chakula.
Ufanisi mzuri wa tezi hii huweza kuhakikisha mapigo ya moyo ni sawa, uzito sawa wa mwili, na usawa ulio sawa wa homoni.
Kutibu kisukari aina ya kwanza ni moja ya kazi nyingine nzuri za mafuta ya nazi sababu mafuta haya yanao uwezo wa kuiweka sawa damu sukari (blood glucose) ndani ya mwili.
Mafuta ya nazi yamethibitika siyo katika kushusha kisukari aina ya kwanza tu bali pia katika kuweka sawa aina mbalimbali za homoni mwilini.
Kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi kwa siku kinatosha kwa kazi hii.
Mafuta ya nazi ni moja ya dawa nyingine nzuri kwa ajili ya kutibu maambukizi ya fangasi kwa sababu moja kuu kwamba ni mafuta yanayoweza kuua bakteria na virusi mbalimbali.
Hii ni kazi ya mafuta haya ambayo isingekuwa vema kama nisingekujulisha kupitia makala hii. Hii ni matokeo ya kuwa na โlauric acidโ na โcapric acidโ.
Tafiti mbalimbali zimeonyesha uhusiano uliopo baina ya matumizi ya mafuta yenye afya na kushuka kwa maambukizi ya fangasi.
Kwa fangasi yoyote juu ya ngozi unaweza kutumia mafuta haya kama mafuta yako ya kupakaa kila siku pia unaweza kunywa kijiko kidogo kimoja kila siku kuongeza kinga zaidi ya mwili.
Maradhi mengi mwilini huja kama sababu ya homoni zako kutokuwa sawa. Ni bahati kufahamu kuwa mafuta ya nazi ni moja ya dawa za asili nzuri katika kuziweka sawa homoni zako.
Hii ni kwa sababu mafuta ya nazi yana mafuta mazuri yajulikanayo kama โlauric acidโ. Mafuta ya nazi huiweka sawa homoni mhimu sana kwa upande wa uzazi kwa mwanamke homoni ijulikanayo kama โestrogenโ. Chanzo kingine kizuri cha homoni hii ni pamoja na tunda la parachichi.
Kuzeeka mapema ni jambo lisilopendwa karibu na watu wote. Kuzeeka mapema hakuathiri muonekano wako tu bali huathiri pia afya yako.
Tunapozungumzia juu ya faida za kushangaza zilizomo katika mafuta ya nazi lazima ujuwe kuwa mojawapo ni hili la kukufanya usizeeke mapema.
Viuajivijasumu vilivyomo kwenye mafuta ya nazi hufanya kazi mhimu katika kupunguza vijidudu nyemelezi na matatizo mengine katika ini.
Kuzuia magonjwa ya ubongo ni faida nyingine ya mafuta ya nazi ambayo unapaswa kuijua.
Asidi mafuta zilizomo kwenye mafuta ya nazi hubadilishwa na kuwa โketonesโ ambazo huzuia kutokea tatizo la kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
Kupoteza kumbukumbu ni matokeo ya kuongezeka kwa kemikali ijulikanayo kwa kitaalamu kama โamyloid beta peptidesโ.
Kwenye mafuta ya nazi kuna kitu mhimu sana kijulikanacho kama โPhenolic compoundsโ ambacho hudhibiti ile kemikali ya โamyloid beta peptidesโ na hivyo kukuondolea tatizo la kupoteza kumbukumbu kirahisi zaidi.
Mafuta ya nazi yanaweza kukupunguzia hitaji lako la kutaka kula chakula kila mara kwa kuwa hufanya kazi ya kupunguza njaa ndani ya mwili.
Kutumia mafuta ya nazi kutakufanya ujisikie umeshiba kwa kipindi kirefu na kama matokeo yake kutakusaidia kupunguza kiasi cha nishati unaingiza ndani ya mwili wako kila siku.
Kuna uhusiano wa karibu kati ya mafuta safi kwa afya na kuwa na njaa ya wastani.
Tafiti mbalimbali Zimeonyesha kwamba Msongamano wa juu wa lipoprotini kolesto (high-density lipoproteins -HDL) unao uwezo wa kulinda moyo wako.
Hivyo mafuta ya nazi yanaweza kupunguza hatari kwako ya kupatwa na ugonjwa wa moyo moja ya kazi nyingine mhimu sana ya mafuta haya.
Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo โlauric acidโ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla.
Lauric acid huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalamu kama High Density Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalamu wa lishe wa Lifesum.
Tafiti zimeendelea kuonyesha uhusiano uliopo kati ya matumizi ya mafuta ya nazi na kuimarika kwa mfumo mzuri wa mmengโenyo wa chakula.
Mafuta ya nazi yanapokuwa yamemengโenywa ndani ya mwili wako hutumika kama nguvu yako moja kwa moja.
Watu wanaotumia mara kwa mara mafuta ya nazi kwenye vyakula vyao kila siku wanakuwa na mfumo mzuri wa mmengโenyo wa chakula jambo ambalo ni mhimu katika kuchoma mafuta na nishati ndani ya mwili.
Mafuta ya nazi yanasaidia kuimarisha kinga yako ya mwili kwani mafuta ya nazi yana kiasi cha kutosha cha viuajivijasumu (antioxidants) dhidi ya vijidudu mbalimbali nyemelezi.
Tafiti zimeonyesha kwamba matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kuwa msaada mkubwa katika kuotesha na kukuza nywele.
Mafuta ya nazi ni mazuri kwa kupaka mdomoni. Vilevile kama una tatizo la midomo kukauka basi uwe unapakaa mafuta ya asili ya nazi kila mara.
Mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa wa kuungua na bado yakabaki na viinilishe vyake kama kawaida hata baada ya kuunguzwa au kuchomwa katika moto.
Mafuta ya nazi hubaki katika hali yake hata katika joto la kawaida tofauti na mafuta mengine.
Mafuta ya nazi ni mafuta mazuri kwa ajili ya masaji na kukupatia hali ya utulivu unaouhitaji kupitia masaji.
Pakaa mafuta ya nazi katika uke kulainisha. Faida nyingine unapopaka mafuta haya ukeni ni kutibu fangasi na bakteria tena bila madhara.
Mafuta ya nazi yanaweza kudhibiti dalili za ugonjwa wa aleji. Kila siku pakaa mafuta ya nazi ndani ya pua zako na hauta piga chafya unapokuwa karibu na kile kinachokuletea aleji/mzio.
Hakuna mtu duniani ambaye hajawahi kukutana na hali ya kukataliwa. Yaani kukataliwa katika hali yoyote ile. Waweza kuwa umekataliwa katika kupata ajira, umekataliwa katika mahusiano, umekataliwa kupata nafasi ya kusoma, umekataliwa kupata mtaji wa biashara, umekataliwa tuu..umekataliwa.
โ-= Unaweza kuwa umekataliwa katika ajira moja kumbe kuna ajira nyingine tena yenye maslahi zaidi inakusubiri.
โ-= Umekataliwa na mteja mmoja na kumbe kuna wateja wengi wanakusubiri.
โ-= Umekataliwa katika chuo kimoja mwaka huu kumbe mwakani kuna nafasi yako inakusubiri.
โโ= Umekataliwa na mpenzi ulioamini kabisa atakua wako wa maisha kumbe aliye wako haswaa anakusubiri ufike.
Watu wengi kinachowarudisha nyuma, “ni kuacha kuboresha fikra zao ili kuwa watatuzi wa matatizo_(problem solvers)_ ila wameamua kuwa walalamikaji tu kila siku, ili tuendelee ni lazima tujikite katika kutafuta majibu ya matatizo yanayotuzunguka.” Yaani, mara zote jiulize ” *sasa nifanye nini? Na sio kwa nini mimi?”*
Mtaalamu mmoja aliwahi kusema ” _Life is 10% of what happens to you and 90% of how you respond to it_”. Yaani _yale yanayokutokea maishani yanachangia asilimia kumi tu kuboresha au kuharibu maisha yako na asilimia 90 ya maisha yako ni jinsi wewe unavyoyachukulia maisha hayo_. Kwa nini ukate tamaa baada ya kukataliwa. Yape maisha yako maana sana thamani ya juu kabisa ili kukataliwa kwako iwe ni kukupa nguvu ya kufanya vizuri zaidi. Tambua utakacho na unachoweza kukifanya. Jifunze vizuri na ubobee ili kuuhakikishia ulimwengu kwamba wewe sio mzigo ila ni sehemu ya wenye majibu ya matatizo yanayotuzunguka.
Kukataliwa, ni mtaji. Kila jambo lina wakati wake.
Mtoto wako atakapofikisha miezi sita, ataanza kuota meno. Watoto wengi wanapotaka kuota meno humwaga mate sana na hutaka kutafunatafuna vitu. Wakati mwingine watoto hutapika au kuhara wakiota meno.
Kwa kawaida kuota meno hakufanyi mtoto kupandwa na joto. Kama mtoto wako atapata joto, yaweza kuwa jambo lingine. Hakikisha umemwona daktari wa watoto.
ยทWakati wa kulala, weka kitambaa safi chini ya kichwa cha mwanao ambapo ute utamwagika. Unaweza kibadilisha kitambaa hichi kitakapo loweka ute.
ยทMpatie mtoto kitu cha kutafuna ambacho hakitamdhuru. Usimpatie kitu kidogo sana kwani anaweza kukimeza. Unaweza kumpatia vidunde vya mpira visivyokuwa na majimaji ndani kwani vyaweza kupasuka.
ยทUsifungilie kidunde cha kutafuna kwa shingo ya mwanao. Kinaweza kushikwa na kummyonga.
ยทKuna dawa nyingi dukani za kupiunguza maumivu wakati mwanao anaota meno. Hata hivyo, mwone daktari wa watoto kabla jujampa mwanao dawa yoyote
ยทBaada ya mwanao kuota meno hakikisha unayatunza vizuri
Recent Comments