Tumaini kwa Mungu
Mtumainie Mungu kwa maana Mungu hawatupi wale wamtumainiao na kumgoja. Mkono wake upo tayari kwa ajili ya kuwaokoa wale wanaomwelekea.
Mtumainie Mungu kwa maana Mungu hawatupi wale wamtumainiao na kumgoja. Mkono wake upo tayari kwa ajili ya kuwaokoa wale wanaomwelekea.
Tunda asili yake ni sehemu za Mashariki mwa Europe na pia Magharibi mwa Asia, na tunda hili linajulikana kwa miaka ya zamani mno katika miji ya Old China, Babulon na Egypt. Tunda hili hutumiwa na lina faida kubwa katika mwili wa mwanaadamu. Lina dawa ya maradhi tofauti:
Apple lina wingi wa iron, arsenic na phosphorus, kwa mtu mwenywe ugonjwa huu inafaa kufanya juice ya apple iwe fresh. Ni vizuri kunywa juice hiyo glass moja kabla kula chakula (nusu saa kabla) na pia kabla ya kwenda kulala usiku.
Mwenye kutokezewa na ugonjwa huu ni vizuri sana kutumia tunda hili (iwe bivu). Kila siku ale 2 pia kama yatapikwa au kuchomwa ni mazuri zaidi kwani hulainisha cellulose.
Kuna matatizo tofauti ya tumbo, kwahivo tunda hili limekusanya matatizo yote ya tumbo na kuondoa matatizo hayo. Changanya apple, asali kidogo na ufura kidogo na kula kabla chakula hii husaidia kuondoa matatizo ya tumbo kama vile usagaji mdogo wa chakula na mengine.
Tunda hili lina faida katika maradhi yote ya kichwa. Apple lilowiva limenye maganda yake, halafu ule kwa kutia chumvi kidogo kila siku asubugi kabla ya kula kitu chochote, na uendelee kufanya hivi kwa muda wa wiki 2.
Apple ya wingi wa potassium na phosphorus lakini sodium inapatikana kidogo sana.Kwa wakai wa zamani watu walikuwa wakila matunda haya na asali, kwa ajili ya maradhi ya moyo na research imefanyika imeonekana kwa wale watu wanotumia vyakula venye potassium kwa wingi huepukana na maradhi ya moyo. Kwahili ni uzuri kula tunda hili pamoja na asali.
Apple linasaidia katika kuongeza kutoa (secreation) mkojo ambayo hii inasaidia kurudisha blood pressure katika hali ya kawaida, pia inasaidia kupungua kwa sodium chloride katika figo..
Matunda ya maepo yanasaidia sana meno katika kuyasafisha na kuyaepusha na vijidudu na kuoza, kila baada chakula kula apple moja.
Njia hizo ni kama ifuatayo!!
1. Mtaji mbadala
Mtaji mbadala unarejelea rasilimali au mbinu ambazo zinaweza kutumika badala ya fedha katika kuendeleza biashara au mradi fulani. Ni muhimu kuelewa kwamba si kila hatua inahitaji matumizi ya fedha taslimu. Kuna nyakati ambapo unaweza kutumia rasilimali zingine ulizonazo ambazo zinaweza kuchukua nafasi ya fedha. Kwa mfano, mtu anaweza kutumia nguvu zake mwenyewe katika kutengeneza kitu kama bidhaa au katika kutoa huduma, hivyo kuokoa gharama ambayo angehitaji kulipa mtu mwingine kufanya kazi hiyo.
Ujasiriamali unahusisha pia kutumia maarifa na uzoefu ambao mtu amepata katika fani au sekta fulani. Maarifa haya yaliyotokana na mafunzo au uzoefu yanaweza kugeuzwa kuwa bidhaa au huduma bila ya gharama za ziada. Halikadhalika, mtaji mbadala unaweza kujumuisha kutumia umaarufu au jina lako kuvutia wateja au wabia bila haja ya matangazo ya gharama.
Kukopa au kuazima ni njia nyingine ya mtaji mbadala. Badala ya kutumia akiba yako ya fedha au kuchukua mkopo wa riba kubwa, unaweza kuazima vifaa au pata mikopo isiyo na riba kutoka kwa marafiki, familia, au taasisi zinazotoa mikopo midogo midogo.
Ubunifu ni sehemu muhimu ya mtaji mbadala. Kwa kutumia ubunifu, mtu anaweza kubuni njia mpya na tofauti za kutekeleza miradi ambazo hazihitaji fedha nyingi. Hii inaweza kujumuisha kufanya biashara kwa njia ya kubadilishana bidhaa na huduma (barter trade) au kuanzisha njia mpya ambazo zinapunguza gharama za uendeshaji.
Kipaji ni rasilimali nyingine ambayo inaweza kutumika kama mtaji mbadala. Kwa mtu mwenye kipaji kikubwa katika sanaa, muziki, riadha, au tasnia nyingine, kipaji hicho kinaweza kuwa njia ya kujipatia kipato bila haja ya kuwekeza fedha nyingi. Uwezo binafsi uliojengwa kama vile uongozi, mawasiliano na uwezo wa kushawishi watu, pia ni mali ambazo zinaweza kutumika kama mtaji mbadala.
Kwa ujumla, dhana ya mtaji mbadala inasisitiza umuhimu wa kuchangamkia rasilimali na vipawa tulivyonavyo, na kutafuta njia mbadala za kufanikisha malengo bila kutegemea fedha taslimu pekee.
2. Kupata mtaji kwa ndugu, jamaa na marafiki
Watu wengi wanakuwa kwenye umaskini wakati wamezungukwa na ndugu matajiri kisa wanaona aibu kuomba msaada, lakini amini usiamini watu wengi wametajirika kupitia ndugu, jamaa na marafiki, mfano mtu tajiri kuliko wote barani Afrika kutoka Nigeria ndugu Dangote yeye alivyotaka kuanza ujasiriamali aliomba msaada toka kwa mjomba wake ambaye alimuazima kama milioni 3 hiv , kwa kuwa aliona fursa kwenye mambo ya ujenzi (cement) yeye akaanza kununua cement na kuuza leo hii ndugu Dangote amekuwa bilionea ambaye amewekeza sana barani Afrika anauza cement, unga , mchele, mafuta, sukari na saa hivi anauza mafuta kule Africa Magharibi hata hapa Tanzania tuna kiwanda chake kule Mtwara,
Kuomba msaada sio ishara ua udhaifu bali ni ishara ya nguvu kwamba unajiamini ndio maana unaomba msaada. kumbuka kwenye neno UJASIRIAMALI kuna neno Jasiri pia, huwezi kuwa na mali bila kuwa jasiri.Umezungukwa na watu waliobarikiwa usisite kuwaambia wakusaidie ,.
3. Kwa kujiwekea akiba.
Watu wengi sana hapa kwetu Tanzania ukiwaambia weka akiba wanakwambia mimi siwezi kuweka akiba, sina utamaduni wa kuweka akiba, hivyo mi nakushauri anza leo kujifunza kuweka akiba, ni ngumu sana kufika juu bila kuweka akiba kwa mfano kama umeajiriwa na unajua biashara fulani inataka milioni 2 ili kuifanya na wewe mshahara wako ni laki 4, kwa nini basi kila mwezi usiweke laki 1 pembeni, ndan ya miaka miwili utakuwa na milioni 2.4 huo ni mtaji wako wewe mwenyewe.
Usisite kuanza kidogo kwa kuweka akiba polepole mpaka ufike huko unakoenda.
4. Pata kazi ya ziada
Kama kipato unachopata hakitoshi unaweza kujitafutia kazi ya ziada kwa muda wako wa jioni au weekend ili uweze kupata ziada ya akiba kwa ajili ya mtaji.
Watu wengi wanatumia muda vibaya, Je baada ya kazi yako unafanya nini? ile saa 10 hadi saa 4 usiku unatumiaje muda wako? Jinsi unavyotumia muda huu itakupelekea kuwa tajiri au maskini
5. Pata Mtaji kwa njia ya kudunduliza
Hii njia ya kudunduliza ndio njia ambayo ni nyepesi kabisa ambayo watu wengi hawaioni, ukiamua kutumia njia hii kamwe huwezi kukosa mtaji, hii ina maana unaanza katika hali ya chini kabisa ya kufanya kitu chochote halafu ile faida unayoipata hauitumii bali unaiwekeza kwenye biashara yako.Tuone mfano wa dada Christine ambaye ni mfano mzuri wa mtaji wa kudunduliza
Christine Momburi alikuwa amejifungua na mume wake walikuwa wamemuachisha kazi kwa hivyo maisha hayakuwa mazuri sana,
Sasa siku moja walitembelewa na mgeni nyumbani kwao yule mgeni alipotaka kuondoka alimpa Christina shilingi 700 ili anunue maziwa ya mtoto, baada ya yule mgeni kuondoka Christina alijiuliza Je aitumie ile sh 700 kununua maziwa au afanyie nini hasa ili iweze kubadili maisha yake? kwa hiyo alijiuliza sana baadae akaamua kuichukua ile hela aende sehemu akanunue nyanya chungu na mboga mboga kwa bei ya jumla. Akazinunua akaenda kuuza, kwa siku ya kwanza ikatoka sh 700 kwenda 1500 akaongeza mtaji wake, ilikufupisha stori baada ya wiki moja Christina akawa na mtaji wa sh 25000/=.
Siku moja akasikia kuna mahali wanajenga wanataka mama lishe wa kuwapelekea chakula akachukua ile tenda akawa anawapelekea chakula, baadae akasikia kuna sehemu wanataka mtu wa kuwapelekea sare za shule. akawa anazidi kukua na kukua na hivi sasa Christina amekuwa ni mjasiriamali mkubwa pale Moshi ana maduka makubwa sana na amehojiwa na vyombo vya habari mbalimbali na yeye amekiri kwamba kudunduliza ndio kuliko mtoa.
Sasa swali la msingi nalotaka nikuulize ni swali lifuatalo:
Swali, Ni je ni Sh 700 ngapi zimepita mikononi mwako? Je ni Sh 7000 ngapi zimepita mikononi mwako? Je ni Sh 70000 zimepita mikononi mwako? vipi kuhusu laki 7 au milioni 7 ngap zimepita mikononi mwako? mara nyingi tumeidharau fedha na kuona ni ndogo lakini kumbuka nilishasema siku za nyuma kuwa kila shilingi inayopita mikononi mwako ni itazame kwa jicho la kimilionea.
Nikukumbushe kuwa tajiri kuna maumivu ambayo utayapitia, watu wengi hawataki kupitia maumivu ndio maana watu wachache sana wanakuwa matajiri., watu wengi wanapenda utukufu lakini hawataki kubeba msalaba.
Hivyo usidharau pesa bali fikiria kwa ubunifu jinsi ya kuizalisha fedha hiyo.
6. Pata Mtaji mdogo kupitia wawekezaji
Wakati mwingine kutokana na mazingira uliyonayo unaweza ukagundua kwamba una wazo zuri sana la biashara lakini hauna mtaji, hapa jambo la msingi ni kuangalia unaweza kumpata vipi muwekezaji ambaye atataka faida, ni afadhali ukawa na wazo ukawashirikisha wengine wakakupa mtaji halafu mkagawana faida kuliko kufa na wazo lako zuri,.
Sisi watanzania tupo nyuma sana katika suala la kufanya biashara pamoja ( Partinership) tofauti na wakenya.
mfano mzuri ni rafiki yangu anaitwa Elisha Edson yuko Iringa, yeye aliwaza kuanzisha kiwanda cha mbao hizi nguzo za umeme, bahati mbaya hakuwa na mtaji wa kutosha akaamua kuongea na marafiki zake zaidi ya 10 akamshawishi kila rafiki yake awekeze kiasi kadhaa cha fedha na kumpatia hisa kwenye kile kiwanda chake, rafiki zake walikusanyika waktoa fedha na sasa kiwanda kimeanzishwa na kinakaribia kutoa nguzo wakati wowote kuanzia sasa.
Je wewe una weza ukatumia njia hii? je una wazo ambalo unajua kabisa hili wazo nikipata wawekezaji wa nanmna hii? masharti yake yanaweza kuwa magumu sababu unaweza kuambiwa uandike mchanganuo wa biashara unao eleweka, na wazo lako la biashara lionekane limetulia kabisa.
Lakini ni afadhali ukapitia mchakato huu kuliko kuwa na wazo zuri halafu wewe huna fedha. na kumbe ungeweza kutoa ajira na kulipa kodi kwa nchi hii na kufanya wenzako wakanufaika na wazo ulilonalo.
7. Mtaji kwa njia ya Mgavi ( Supplier Financing)
Hii ni njia ya uhakika ya kupata mtaji wako. Naomba nitoe stori halisi , Miaka mingi iliyopita kijana mmoja anayeitwa Reginald alikuwa anatafuta kalamu za kuandikia mtaani kwake, lakin bahati mbaya baada ya kutafuta sana kwa muda mrefu alikosa kalamu pale mtaani kwake, jambo hilo lilimfanya aweze kushangaa sana na kujiuliza hivi kweli inawezekana vipi hakuna kalamu hapa mtaani? kwa hyo hilo likamfanya aanze kutafuta mbinu na maarifa ya yeye kuwa mtu ambaye analeta kalamu Tanzania. baada kufanya uchunguzi kwa marafiki mbalimbali wakati huo yeye alikuwa muhasibu tu, akaambiwa Mombasa kuna mtu ana kiwanda cha kalamu na baada ya kufanya mazungumzo na yule ndugu ikaonekana bwana Reginald angeweza kuwa anaingiza kalamu hapa Tanzania lakini hakuwa na mtaji, ndipo hapo ilibidi atumie mali kauli yaani awshawishi wale watu wampatie zile kalamu azilete hapa, aziuze halafu aweze kurejesha fedha na kuchukua faida yake.
Hivyo akaanza hiyo biashara kwenye chumba chake kidogo sebuleni akisaidiwa na familia yake baadae wahamia nje wakatengeneza banda la mabati tayari ikawa ndio kiwanda kwa ajili ya kupaki zile kalamu kwa pamoja. mwaka huo huo wa kwanza bwana Reginald alipata faida kubwa sana takriban bilion ya shilingi
8.Kupitia Taasisi za kifedha
Mada hii ni ndefu sana lakini tutajifunza huko mbele mada inayoitwa Jinsi ya kuishawishi benki ikukopeshe hata kama hukopesheki. hii mada tutaiongelea zaidi huko mbele , lakini nataka tu ujue ili benki ikukope inahitaji uwe na biashara ambayo imeshakuwepo kwa takribani miezi 6 au zaidi, pia watahitaji uwe na mzunguko mzuri wa fedha unaoeleweka, uwe na dhamana ambayo unaiweka ili kama unashindwa kulipa waweze kuichukua ile dhamana, watahitaji uwe umefanya usajili rasmi wa biashara yako., uwe na account ya benk n.k
Sasa basi kwa kuwa watu wanaogopa kwenda benki kutokana na yote haya ndipo unaweza kujaribu kutumia microfinances, hizi ni taasis za kifedha ambazo hutoa mikopo midogo midogo, kwa hiyo angalia kama huko ndiko unapoweza ukaponea. Zaidi ya hayo, taasisi hizi za kifedha zinajulikana kwa kutoa huduma zilizobinafsishwa zaidi, ambazo zinaweza kuwa na manufaa hasa kwa wajasiriamali wadogo na wa kati, watu binafsi, na biashara ndogo ndogo ambazo zinatafuta fursa za kukuza mitaji.
Microfinance institutions (MFI) zina sifa ya kuwa na mifumo inayoweza kufikiwa kwa urahisi, kwani mara nyingi hawana vikwazo vikali vya kielimu au kiuchumi kama vile benki kubwa. Wanaweza kutoa mikopo kwa riba nafuu na wakati huo huo kutoa mafunzo na ushauri wa kibiashara, ambayo yanaweza kuwa na manufaa makubwa kwa wakopaji.
Pia ni muhimu kufahamu kwamba MFI zinaweza kuwa na mitandao mikubwa inayowezesha huduma kufika hata vijijini ambako benki kubwa haziwezi kufika. Hii ina maana kwamba watu wanaoishi maeneo ya vijijini wanaweza kupata huduma za kifedha bila ya kuwa na ulazima wa kusafiri masafa marefu kwenda kwenye miji mikubwa.
Kwa kutumia huduma za microfinance, unaweza kupata fursa ya kuongeza mtaji, kuboresha biashara yako, na hata kupata elimu ya kifedha ambayo inaweza kusaidia katika kufanya maamuzi bora ya kibiashara na kifedha. Ni muhimu kuchunguza chaguzi zilizopo, kulinganisha tofauti za riba na masharti ya mkopo kabla ya kuchukua uamuzi wa kutumia taasisi fulani ya microfinance.
Mchele 3 Magi
Mafuta 1/4 kikombe
Karoti unakata refu refu 3
Vitunguu maji kata vikubwa vikubwa 1 kikubwa
Pilipli manga 1/2 kijicho chai
Hiliki 1/2 kijiko chai
Karafuu ya unga 1/4 kijiko cha chai
Mdalasini wa unga 1/2 kijiko cha chai
Zaafarani (ukipenda) roweka katika maji 1 kijiko cha chai
Zabibu kavu (ukipenda) 1/4 kikombe
Chumvi kiasi
1. Kwenye sufuria tia mafuta na kaanga karoti kidogo.
2. Tia vitunguu kisha tia bizari zote.
3. Tia maji kiasi (kutegemea aina ya mchele) na chumvi
4. Tia mchele upike uwive.
5. Karibu na kuwvia tia zabibu ukipenda.
6. Funika endelea kuupika hadi uwive.
Nyama 2 Ratili (LB)
Chumvi Kiasi
Mafuta 1/4 kikombe
Kitunguu (kata virefu virefu) 1 Kikubwa
Pilipili mboga kubwa 2
(ukipenda moja nyekundu moja kijani)
unazikata vipande virefu virefu.
Figili mwitu (celery) kata vipande Miche miwili
virefu virefu
1. Chemsha nyama hadi iwive
2. Ikaange kwa mafuta hadi iwe nyekundu
3. Weka vitunguu, pilipili mboga na figili mwitu
4. Kaanga kidogo tu kama dakika moja.
Watu wengi hulitumia tunda la papai kwa sababu ya utamu wake. Hata hivyo mbali na kuwa na ladha nzuri, tunda la papai lina faida lukuki kwa afya ya mwanadamu.
Tunda la papai lina vitamini A,B,C,D, na E jambo linalo liweka tunda hili katika kundi la matunda na vyakula vyenye utajiri mkubwa wa vitamin.
Tunda la papai lina faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kuwa na uwezo wa :
1. Kutibu tatizo la Shida ya kusaga chakula tumboni.
2. Kutibu Udhaifu wa tumbo.
3. Kutibu Kisukari na asthma au pumu.
4. Kutibu Kikohozi kitokacho mapafuni.
ยท Kutibu Kifua kikuu
ยท Tunda hili huleta afya nzuri ukitumia kila siku
ยท Maziwa yanayotoka katika jani lake huponya vidonda
ยท Vilevile yanasaidia kutibu sehemu palipoungua moto
ยท Kama hiyo haitoshi, maziwa yanayotoka katika jani la mpapai yanatibu kiungulia na Ugonjwa wa colon (njia ya haja kubwa ndani)
ยท Pia yanasaidia kutofunga choo
ยท Maganda ya tunda la papai yanasaidia kutibu tatizo la kuungua, vipele na saratani ya ngozi.
ยท Mbegu zake zinatibu ini zikitafunwa 10 โ 12 kwa siku 5.
ยท Majani yake yakaushie ndani, yanatibu pumu. Inapoanza kubana yachome majani yaliyokaushwa kisha jifukize, kule kubanwa kutakisha.
ยท Majani yake yanasaidia katika kutibu shinikizo la damu.
ยท Papai likimenywa na kupondwa linafaa Sana katika masuala ya urembo kwani linaweza kutumika Kama vile unavyotumia lotion kulainisha uso.
ยท Mbegu za papai zina uwezo wa kutibu homa. Meza mbegu za papai kiasi cha kijiko cha chakula mara 3 kwa ajili ya kutibu homa.
ยท Mbegu za papai zilizokaushwa ndani kisha zikasagwa kuwa unga zinatibu malaria, tumia kijiko 1 cha chai changanya na uji, kunywa mara 3 kwa siku 5 Mgonjwa wa kifua kikuu akila matunda haya kwa muda mrefu atapona bila dawa nyingine.
ยท Mizizi yake ikipondwa na kulowekwa katika maji yaliyochemshwa, lita 2 na nusu kwa dakika 15, yanatibu figo, bladder, yanazuia kutapika.
Anakuja Mchina anasema anahitaji Paka๐,
ananunua mmoja kwa bei ya 20,000/=, basi
wanakijiji wanahaha kusaka Paka๐,
wanawaleta mchina ananunua wote anasepa
nao. Anarudi tena anasema vipi, naona
wameadimika, sasa ntanunua kwa bei ya
35,000 Paka๐ mmoja, wanakijiji wanaenda
deep zaidi msituni, kamata Paka๐, leta kwa
mchina, mchina anasepa nao.
Afu wiki
mnayofuatia Mchina anasema bado anataka
Paka๐, saivi atanunua kwa Laki. Wanakijiji
macho yamewatoka, hawana tena paka๐.
Mchina anasema basi ntaftieni kwa Laki na
Nusu. Keshoake inasikika kuwa kuna Mchagga
anauza Paka kijiji cha pili, anauza kwa
100,000/=, wanakijiji wanawahi fasta
wanaenda nunua Paka๐๐๐๐ wote wa kijiji cha
pili. Wanarudi kijijini hawana pesa ila wana
Mapaka ๐๐๐ wakijua watamuuzia mchina fasta kwa
laki na nusu, Mchina hatokei Ng’oooo!!!!
Infact, yule mchina alikuwa anawakusanya tu
na kuwahifadhi kule kijiji cha pili akijua ataja
wauza kwa 100,000/= kwa hawa hawa wa kijiji
hiki.
This is what called business strategy.๐
Korosho zina faida hizi zifuatazo;
1. Zinakinga Maradhi ya Saratani Haswa kwenye matumbo mapana.
2. Korosho zinasaidia Afya ya moyo kufanya kazi vizuri.
3. Korosho zinasaidia Kuzifanya nywele na ngozi ya mwili kuwa na Afya nzuri.
4. Korosho zinasaidia mifupa yako kuwa imara na afya nzuri.
5. Korosho ni nzuri kula kwa ajili ya mishipa ya mwilini mwako.
6. Korosho zinakukinga usipatwe na mawe kwenye nyongo yako.
7. Korosho ukila zinapunguza uzito mwilini.
Kati ya wanawake na wanaume wote wawili wanahitaji kuvutiwa na wenza wao ili wadumu katika mahusiano. Kama mwanaume lazima upate wakati wa kujua unatakiwa kufanya nini kwa ajili ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua.
Hali kadhalika kama bado haupo Kwenye mahusiano kuna mambo ambayo ni ya msingi kufanya au kuwa nayo ili uweze kuwa na mvuto zaidi kwa wanawake.
Wanawake wanapenda sana wanaume wanaojali wao kama wao, wanaojali kile wanachokifanya na watu wao wa karibu kama ndugu na wazazi. Wanapenda wanaume wanawaona wao ni kila kitu na wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mwanamme anatakiwa amjali mpenzi wake kwa kila hali. Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa sana ya kuendelea kudumu katika uhusiano hai. Vile vile kuonyesha kujali mambo yake na watu wake wa karibu kunamvutia mwanamke.
Mwanamke huvutiwa sana na mtu ambaye yupo karibu nae na ambaye anapatikana wakati anapohitajika. Kati ya vitu vinavyowapa wapendeza sana wanawake ni pamoja na kusogezwa karibu. Hapa ni kuwa naye katika mambo mengi unayoyafanya kila siku na kushiriki katika mambo yake hata kwa mawazo kama ukishindwa kwa matendo. Ni vizuri kuwa naye au kuwasiliana naye wakati wa kula, ukitaka kujua aina ya chakula alichokula siku hiyo au ikiwezekana mchagulie. Ni mambo madogo sana lakini yanayoongeza nakshi katika mapenzi na ambayo ni muhimu sana kwa wanawake. Yapo mengi sana ambayo kwa kuyafanya utakuwa umemsogeza mpenzi wako karibu yako, mfano kutembea pamoja, kuangalia movie pamoja, nakadhalika. Tumia ubunifu wako ili uweze kuteka hisia za mwenzi wako kisawasawa kwani mwanamke anavutiwa sana na mtu aliye karibu nae.
Wanawake wanapenda kusifiwa na kuonekana kuwa bora. Mwanamke akisifiwa anahisi kupendwa kupita kiasi. Anajiona kamili, peke yake na mwenye nguvu kwako. Anajiamini na unamfanya azidi kukupenda kwa kuwa anaamini yupo na mwanaume ambaye anajivunia kuwa naye. Vilevile kumsifia mwanamke kwake ni njia ya kuonyesha upendo na Ishara ya kuonyesha kumjali kupita kiasi.
Mwanamke anavutiwa zaidi na mtu anayeonyesha kumpa kipaumbele na kupewa nafasi. Kuna wakati wanawake huwa na mambo yao binafsi. Kazini au kifamilia. Inawezekana akatatizika katika eneo fulani ambalo kwa namna moja ama nyingine atahitaji usaidizi wako. Ikitokea mwanamke akawa katika hali hiyo, msikilize.
Mathalani ana tatizo la kifamilia, amekuambia mmoja wa wazazi wake anaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini kuonesha kujali kwako tu, kutampa matumani kwamba anaishi na mtu sahihi. Acha kupuuza mambo yake; hata yale madogo, kama ya โmtoto wa dada amerudishwa ada shuleniโ.
Msikilize, mshauri panapofaa kufanya hivyo na ukiweza msaidie hata kifedha. Katika upande wa pili ni hivyo hivyo. Labda una tatizo binafsi, kazini kwako au kifamilia, mshirikishe.
Unaweza kushangaa jambo ambalo uliamini unaweza kulimaliza peke yako, kwa kumshirikisha likawa jepesi zaidi na mambo yakaendelea vyema. Kipaumbele kwa namna yoyote ile, kunaongeza mapenzi zaidi kwa mwanamke.
Wanawake wanapenda mwanamme ambaye ni msafi, hii ni kwa sababu kiasili wamejaliwa kupenda usafi ndio maana ni nadra sana kukutana na mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana wanaitwa mapambo ya nyumba au la nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya kupenda sana usafi. Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako, lazima uishi katika nyumba safi. Hata anapokuja kukutembelea, anakuta mazingira masafi kuanzia sebuleni hadi chumbani. Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa rahisi zaidi yeye kuanzia hapo alipokukuta na kuendelea mbele.
Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini yaani mwenye uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza sawia pale anapotakiwa kufanya hivyo au wakati wowote ule. Siyo anayebabaika na kuyumba yumba. Suala la msimamo binafsi, kwa mwanamke ni kubwa kuliko hata kumnunulia nguo mpya.
Mwanamke anapenda kukuona ukiwa katika hali halisi ya maisha yako, usiyeyumbishwa na mwenye kutoa maamuzi yasiyoyumba.
Wakati mwingine, mwanamke anaweza kukupima hata katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia unavyotoa maamuzi yako, lakini pia atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha.
Anataka kuona msimamo wako muda wote. Mwanamke hapendi mtu anayebadilikabadilika Kwenye maamuzi na misimamo yake.
Mwanamke anapenda mwanaume mwenye malengo na anayemshirikisha katika mipango yake. Mwanamke anavutiwa na mwanamke mwenye malengo katika maisha yake. Vilevile anapenda mtu anayemshirikisha katika malengo yake na kumuweka katika mipango yake. Faida ya kumshirikisha katika malengo yako ni pamoja na kunampa nguvu na nafasi ya kujiona mama katika familia yenu. Msaidizi kamili wa nyumba yenu. Mweleze juu ya malengo yako, wakati mwingine anaweza kukusaidia sehemu ambayo hukutarajia.
Mwanamke hupenda mwanamme anayeweza kujitetea. Mwanaume aliye โfitiโ ni chaguo la wanawake wengi. Si mnyonge. Mpole kupitiliza na aliye tayari kuonewa! Huyu hana nafasi.
Wanawake hawapendi kuwa na wanaume ambao wapo tayari kuonewa. Wanataka wenye uwezo wa kusimama kidete kuona haki zao hazichukuliwi kirahisi. Hili si suala la kutetea tu haki yako pekee kama mwanaume, bali inapobidi kusimamia haki ya mwanamke wako. Nisieleweke vibaya katika hili, lakini mwanaume imara ni yule ambaye ana nguvu โ anafanya mazoezi na ambaye yupo tayari kwa lolote! Inapowezekana, uwe na uwezo wa โkuzichapaโ ikiwa mtakutana na vibaka au watu wabaya wenye lengo wa kukudhuru/kuwadhuru au kumdhuru mpenzi wako.
Mwanamke anavutiwa zaidi na mwanamme anayeweza kumridhisha katika tendo la ndoa. Anataka mwanamme anayeweza kufanya kile anachotaka yeye na kile anachokipenda. Mwanamke hapendi mwanamme anayemkomoa katika tendo la ndoa au anayefanya mambo asiyoyapenda. Mwanamke anataka kuridhishwa na kujaliwa katika tendo la ndoa.
Wanawake wengi siku hizi hawajui au hawataki kuonesha mahaba
Nimefanya kautafiti kangu kadogo nimegundua wanawake wengi siku hizi hawaonyeshi mahaba yani kwa ujumla hawako “Romantic”. Wanawake wengi siku hizi akipata mwanaume anaona amepata mtu wa kumsaidia shida zake kwa hiyo hata akiwa ndani ya mahusiano anafikiria zaidi kutatuliwa shida zake kuliko mahusiano yenyewe.
๐
Wanawake wa siku hizi wengi, kwa mfano umemtoa out kidogo mkapate walau msosi sehemu nzuri, mkianza kula mpaka mnamaliza hakumbuki hata kukulisha kidogo kimahaba. Unakuta anakula msosi kimpango wake utafikiri anakula na kaka yake. Mnatoka kidogo mnatembea unakuta anatembea na wewe utafikiri anatembea na kaka yake; yani unaweza ukamuacha nyuma kidogo au akawa mbele yako anashindwa kujiongeza kupitisha mkono wake kwenye kikwapa chako na kukushika kimahaba.
๐
Wakati mwingine anakuona jasho linakutoka usoni anashindwa hata kukufuta kimahaba anakutazama tu utafikiri wewe ni kinyago cha mpapure. Wakati anakuaga anaondoka utafikiri anamuaga kaka yake hakupigi hata busu. Mwanamke unazungumza nae hakushiki hata ndevu zako kimahaba, mwanamke unakuwa nae hakufunyii massage wala hakukati mara moja moja kucha zako kimahaba.
๐
Wakati mwingine unakuta umekaa nae mwaka mzima kwenye mahusiano lakini hajawahi kukwambia neno “Nakupenda”mpaka wewe uanze kumwambia kwanza.
๐
Wanawake wengi wa siku hizi wanapenda kudekezwa, kubembelezwa na kupewa pesa ndio maana wengi utasikia wakisema “nataka mwanaume Romantic na mwenye pesa” lakini hawajiulizi je, wao ni Romantic? Au sisi wanaume hatuhitaji hayo mahaba ya wanawake?
๐
Asili ya mwanamke ni mfariji mkuu wa mwanaume lakini siku hizi wanawake wengi wamekuwa stress kwa wanaume.
๐
Note: Hakuna mwanaume mbahili kwa mwanamke Romantic.
Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke
Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.
AMINI UNA AKILI YENYE UWEZO MKUBWA WA KUBUNI WAZO LA KUWEZA KUKUSAIDIA KUFANIKIWA KIMAISHA.
Huwa nikikaa na kufikiri ni namna gani binadamu aliweza kubuni ndege, meli kubwa hasa za mizigo, gari na vitu vinginevyo na badae kuja kuwa msaada mkubwa katika dunia yetu ya siku leo hata kurahisisha maisha katika eneo fulani lililokuwa na ugumu kwetu, basi nauona uwezo wa Mungu aliouweka ndani ya binadamu huyu ingawa yeye binafsi kama binadamu wakati mwingine hatulitambui hilo na kama tunalitambua basi ni wachache na wakati mwingine hatujakaa vizuri kuitumia hii fursa ya uwezo huo tuliopewa. Hii inaonyesha ni jinsi gani binadamu alivyo na uwezo mkubwa wa kufanya ubunifu kwa kupitia akili aliyonayo na kuleta mageuzi na mshangao mkubwa katika ulimwengu tunaoishi.
Hebu tazama wengi wa wabunifu waliojitoa kwa kuumiza akili na kubuni vitu vipya katika ulimwengu huu tunaoishi leo hii, ndio tunaowaona matajiri katika dunia hii ya leo kuliko watu wengine waliokataa kutumia uwezo na akili zao walizopewa na Mwenyezi Mungu na zaidi sana kubakia kulalamikia watu wengine wanaofanikiwa. Nataka nikuambie unauwezo mkubwa sana ndani yako unaoweza kuutumia ili kubuni jambo kubwa litakaloleta matokeo chanya na kuwa msaada mkubwa katika jamii yako unayoishi na kwako pia.
Ndio. Una uwezo mkubwa sana tena sana unaoweza kuleta matokeo chanya na makubwa katika ulimwengu wako na ukasahau hata habari ya kuajiriwa na kuanza kujiajiri binafsi kupitia jambo ulilobuni. Tatizo ni kwamba hupendi kutumia akili yako kufikiri kwa upana na kwa kiwango cha juu kwa hofu ya kupoteza muda, kuumiza akili, kutokutaka matatizo (stress), nakadhalika. Kila siku umekuwa ni mtu wa kusema โmimi sitaki kuumiza akili yanguโ mara unasema โmimi masuala yanayochosha akili yangu siyatakiโ unataka kufanya mambo marahisi marahisi ili utoke kimaisha, ni gumu sana kwa namna hiyo rafiki.
โIf you do what is easy your life will be hard, but if you do what is hard your life will be easy.โ โ Les Brown
Nataka nikuambie akili yako inauwezo mkubwa sana, narudia โinauwezo mkubwa sanaโ tena sana wa kubuni biashara ya kukutoa kimaisha, kutatua matatizo yaliyo magumu kwa jamii iliyokuzunguka, kuleta mbinu na mikakati mipya kwenye kazi au ofisini ili kusaidia kampuni kusimama, nakadhalika. Tatizo unajitetea na kujenga hofu kubwa ndani yako ya kujitoa na kufikiri ili kuhakikisha unaleta matokeo mapya na makubwa mahali ulipo muda huu. Hebu fikiri kama binadamu huyu huyu unayemjua na aliye kama wewe alibuni balbu za umeme anaitwa Thomas Edison kutoka nchini Marekani; na zaidi sana binadamu huyu huyu kama wewe aliweza kugeuza historia ya muonekano wa magari na kuja na kitu kipya zaidi anaitwa Henry Ford, na binadamu huyu huyu aliweza kubuni biashara ya kuuza kuku walioandaliwa kama chakula na hatimaye kuwa na mgahawa mkubwa wa KFC uliosambaa karibu nchi 123 duniani kote anaitwa Harland Sanders. Na wengine wengi sana ambao sitaweza kuwamaliza kwa kuwataja wote mahali hapa siku ya leo.
Naamini wapo watu wanaoweza kujitetea na kusema kwa kuwa hao ni watu weupe yaani wazungu na sijaona mtu mweusi hata mmoja hapo. Hebu fikiri ni watu wangapi wanabiashara ambayo leo hii inawaingizia mabilioni ya pesa na wakati mwingine biashara wanazozifanya ni za kawaida na zilizokuwa zikidharaulika na watu kwenye jamii zao na wapo hapa afrika. Angalia mtu kama Aliko Dangote kwa sasa zaidi ya kujishughulisha na uzalishaji wa cement na bidhaa nyingine za ujenzi na hata biashara zake kubwa nyingine kwa sasa ameenza kuzalisha nyanya na kuuza kwenye nchi yake huko nchini Nigeria. Ulitegemea mtu kama huyu ambaye ni tajiri wa kwanza afrika kuwaza kufanya biashara kama hiyo ya nyaya kwa sasa? Yawezekana wewe ulipoambiwa kuuza nyanya uliona ni biashara kichaa na haina maana ya kuifanya. Ukweli ni kuwa usipende kuanzia pakubwa bali anza na madogo ili kukupeleka kwenye kilele chako cha mafanikio na kutimiliza ndoto yako uliyonayo.
Hivyo hivyo kwa Bakhresa, Mengi, Dewji, Sheria Ngowi na wengine wengi tunaowaona nchini mwetu Tanzania wamefanikiwa kiuchumi, hii yote ni kutokana na kuamua kubuni kitu kipya kilichoweza kuwa msaada mkubwa kwenye jamii yao na kuweza kuwaletea wao mafanikio makubwa katika maisha yao. Sheria Ngowi pamoja na kusomea masuala ya Sheria nchini India lakini alijua bado ana kitu cha ziada ndani yake kinachoweza kumlipa na kumfanya awe na uhuru wa kifedha na maisha mazuri sawa na anavyotaka. Leo hii ni mbunifu wa mavazi Africa nzima inamjua na kumtazama. Jiulize kama asingetumia akili yake kwa kufikiri zaidi na kufuata ndoto yake aliyokuwanayo leo hii ingekuwaje kwake na kwenye jamii yake iliyohitaji mchango wake?
Nataka nikuambie huwezi kutoka kwa siku moja ni lazima uumize kichwa na akili yako leo hii na kujua ni nini cha kufanya kinachoweza kukupa uhuru unaoutaka kesho. Na suala la kuumiza kichwa chako na akili ni sasa na si kesho, narudia tena suala la kuumiza akili yako kwa ajili ya kubuni wazo la kukutoa kimaisha โni sasa na si keshoโ kama unavyofikiri. Usiridhike na maisha yako unayoishi leo, usiridhike na kipato unachokipata huku sema ukweli ndani ya moyo wako na kwa uhalisia hakikutoshelezi kabisa kufikia kwenye kilele cha mafanikio makubwa unayoyataka. Usikubali kuwa mvivu wa kuumiza kichwa na kutumia akili yako kwa ajili ya kuja na kitu kipya kinachoweza kuleta manufaa kwako na kwa jamii yako iliyokuzunguka, anza kuwa mbunifu ili uweze kufikia ndoto yako ya maisha.
Umiza kichwa kuanzia sasa na amini katika wazo (idea) utakayoipata ndani ya moyo na akili yako ili kukusaidia na wewe kuwa miongoni mwa watatuzi wa matatizo katika ulimwengu huu. Unaweza kutumia matatizo yaliyopo kwenye jamii yako kama sehemu ya kukupatia wazo jipya na baada ya hapo kubuni njia na mkakati wa kulitatua tatizo ili kuleta matokeo chanya katikati ya watu waliokuzunguka na kwako pia. Mwombe Mungu akupe mwongozo wa kukusaidia kulitimiza na kulifanya hilo wazo (idea) kuwa wazi katika ulimwengu wa nje ili usibaki na wazo lililo kwenye akili na kichwa tu pasipo kuleta matokeo na mchango wowote makubwa kwa watu wako.
Nakusihi usisubiri kesho. Usione una siku nyingi za kuwaza au kuleta matokeo (ku_implement) ya hilo wazo lako (idea) uliyonayo au ndoto ya siku nyingi unayotembea nayo kila kukicha pasipo kuweka vitendo vya kuifanya izae faida na matunda kwako. Anza leo kuhidhilishia dunia kuwa nawe unauwezo mkubwa aliouweka Mungu ndani yako. Usijikatae wala usiogope kukataliwa na wengine pale utakapofanya uamuzi wa kuja na kitu chako kipya kwenye jamii yako, kumbuka kukataliwa ni sehemu ya kukupeleka katika mafanikio. Kadri unavyoongeza kukataliwa ndio unavyoongeza kufanikiwa.
Kama unahitaji kuwa mbunifu wa mavazi kama sheria ngowi anza kubuni leo hii au ikibidi mtafute na uwe chini yake na afanyike kuwa msaada na mshauri wako (mentor) wa hicho kitu unachotaka kukifanya. Amini inawezekana kwani watu waliofanikiwa si wachoyo unapojishusha na kuonesha uhitaji wa kujifunza kutoka kwao. Kama unataka kuwa mfanyabiashara mkubwa kama Dangote lakini bado huna wazo la biashara. Basi elewa una uwezo mkubwa wa kuumiza kichwa na akili kuanzia sasa na ukapata wazo linaloweza kuishangaza dunia yote hapo badae.
Lakini kumbuka si lazima ukaja na kitu kipya kabisa kwani tambua unauwezo pia wa โkuboresha wazoโ au kitu fulani kinachofanyika na watu wengine ila wewe ukaleta ubunifu mpya kwenye hicho kitu na kuleta utofauti mkubwa kwenye eneo (industries) hiyo. Na hii ndio njia inayofanyika kwenye makampuni ya simu, magari, televisheni, nakadhalika. Leo hii samsung akileta simu yenye kamera yenye uwezo wa mega pixel 16 kesho yake utasikia Iphone ametoa simu yake mpya yenye kamera yenye uwezo wa mega pixel 20. Huu ni ubunifu tu ili kuzidi kutawala soko na kuteka wateja wa soko la simu ulimwenguni kote. Nataka nikuambie nawe unauwezo wa kufanya ubunifu mkubwa kwenye jambo lolote lile ili kukuletea mafanikio makubwa na hatimaye ukafanikiwa kufikia katika ndoto yako.
Nataka nikuambie una mawazo milioni na zaidi ndani yako ambayo hadi sasa dunia inayasubiri ili yaweze kuwa msaada kwa watu wengi na kufanyika kuwa faraja kubwa hata kwa watu waliokata tamaa. Ndio. usishangae wala sijakosea kusema ni mawazo โmilioni na zaidiโ uliyonayo ndani yako. Ni wewe tu umejidharau, ni wewe unajiona huwezi kuwaza na kutoka na kitu kipya au kilichojaa ubunifu, ni wewe tu unajaa hofu ya kukataliwa kisa unaona utaonekana unaiga, huigi kwani hata waandishi wanaoandika kama mimi wanaandika kutokana na walichokipitia kwenye maisha na kujifunza kwa wengine, ni wewe tu unajiona huna lolote na si chochote katika ulimwengu huu hivyo huwezi kufanya mambo makubwa. Unajikosea heshima kwa kujiwiza mawazo hayo ya chini na kumkosea Mwenyezi Mungu yeye aliyekuumba na kukupa akili zote timamu ili uzitumie kwa ajili ya kuwaza na kubuni mambo mapya yanayoweza kuwa msaada mkubwa kwako na kwa jamii yako iliyokuzunguka. Anza kuwaza na kuumiza akili na kichwa chako leo hii, na amini kesho utafanikiwa.
JIAMINI NA AMINI UNAWEZA. ISHI NDOTO YAKO.
Dalali aliwatafutia jamaa chumba Buguruni karibu na reli, nyumba nzuri sana. Jamaa na mkewe wakahamia kwa furaha, lakini furaha yao iliisha walipokuja gudundua nyumba ile iko karibu mno na reli treni ikipita mpaka kitanda kinacheza.
Siku hiyo dalali akapita mke akamwita na kumwambia tatizo wakati treni inapita, wakaanza kubishana, yule mama akamwambia dalali kwa kuwa kuna treni itapita sasa hiviโฆ njoo ndani uone mwenyewe.
Bahati mbaya wakiwa wamejilaza kitandani ili dalali aone adhabu wanayopata, Mzee mwenye mali alirudi ghafla, akauliza,
‘Nyie mnafanya nini hapa?’
Masikini dalali kwa woga mkubwa akajibu’ Tunangoja treni’
Leo wapendwa nitaenda kuzungumzia mapishi ya mchuzi wa kuku (chicken curry).
Kuku mzima
Nyanya kubwa 3
Karoti mbili
Pilipili hoho
Kotmiri
Tangawizi
Kitunguu maji
Kitunguu saumu kidogo
Ndimu
Mafuta ya kupikia
Chumvi (pilipili ukipenda)
1. Menya vitunguu saumu na tangawizi na uvitwange pamoja.
2. Katakata kuku vipande vidogo kisha ukamulie ndimu na kupaka mchanganyiko wa tangawizi na vitunguu saumu (kiasi tu).
3. Katakata vitunguu maji na pilipili hoho uweke pembeni.
4. Grind (Kwangua) kwenye grater nyanya na karoti pia uweke pembeni.
5.Katakata kotmiri vipande vidogo uweke pembeni.
6. Andaa kikaango na jiko.
1. Bandika kikaango jikoni na mafuta kiasi, yakishachemka weka vitunguu maji na kaanga hadi vimelainika na kuiva (hakikisha haviungui).
2. Weka pilipili hoho na karoti na endelea kukoroga hadi vyote viive na kulainika, Kisha weka chumvi.
3. Sasa weka vipande vya nyama koroga na funikia kwa dakika 3, kisha weka nyanya zako ulizo grind na koroga ili zichanganyike vizuri, vikishachanganyika weka kotmiri na pilipili kama utapenda. Acha vichemke kwa dakika 5. Hakikisha moto sio mkali sana.
4. Angalia kama nyama zimeiva vizuri kisha epua mchuzi wako.
5. Pakua kwenye bakuli na katakata kotmiri uweke kwa juu.
Unaweza kula kwa ugali, wali, ndizi rost au chipsi.
Kuacha kitu chochote kabisa moja kwa moja ni rahisi sana kuliko kufanya kitu hicho kidogokidogo kwa wastani. Usijidanganye utafanya kidogo au utaacha kidogo. Acha Kabisa na usifanye tena.
Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka. Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.
Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.
Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.
Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.
Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.
Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.
Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.
Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.
Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.
Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.
Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote โ binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!
Kuwa na nywele zenye afya nzuri ni muhimu kwa wote bila kujali jinsi, hali hii husababisha wengi kutumia madawa ya aina mbalimbali ya kuhakikisha nywele zao zinastawi na kuwa na muonekano mzuri.
Kwa bahati mbaya, wengi waliotumia madawa yanayotengenezwa kwa kemikali hujikuta katika wakati mgumu siku za usoni wakikabiliwa na matatizo ya nywele kukatika na hata kupata madhara katika ngozi ya kichwa.
Njia bora na salama zaidi ya kustawisha nywele, kuzifanya ziwe na mvuto wa aina yake bila kujali wewe ni mtu wa asili ya bara Asia, Afrika au Marekani, ni kula vyakula vyenye virutubisho muhimu kwa afya ya nywele.
Vifuatavyo ni sehemu ya vyakula ambavyo hupatikana kirahisi barani Afrika na kwa bei nafuu, ambavyo vitakupa afya bora zaidi ya nywele zako.
Nywele za binadamu zina protini ambayo zimeumbiwa. Hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa zina protini ya kutosha, na hilo hufanyika kupitia vyakula. Protini ni nguzo kuu ya nywele za binadamu, na yai ni moja kati ya vyakula vyenye utajiri mkubwa wa protini. Hakikisha unakula yai angalau mara tatu kwa wiki.
Nywele zinahitaji madini ya chuma ili ziweze kuwa katika hali nzuri ya afya. Kukosekana kwa madini ya chuma husababisha nywele kunyonyoka. Mwili unapokosa madini ya chuma, hewa ya oxygen na virutubisho hushindwa kufika vizuri kwenye mizizi ya nywele hivyo hufanya nywele kuwa dhaifu na zisizo na muonekano mzuri.
Mboga za majani aina ya spinachi ni suluhisho, kwakuwa zina madini ya chuma kwa wingi ambayo seli za nywele huhitaji.
Mwili wa binadamu huhitaji vitamini C ambayo husaidia kuhuisha utendaji wa madini ya chuma. Hivyo, unapaswa kuongeza matunda ya jamii ya โcitrusโ, kama vile machungwa, chenza, balungi na limao. Pia, unaweza kutumia na asali pamoja.
Vitamini C husaidia katika ukuaji wa nywele kusaidia usambaaji wa virutubisho na ukuaji wa haraka wa nywele.
Ni muhimu sana kuhakikisha unakunywa juice ya karoti kila siku, kama unataka nywele zako zikue haraka zikiwa na mwonekano mzuri wenye afya. Vitamini A inayopatikana kwenye karoti ni muhimu sana kwa ukuaji wa seli za nywele. Kumbuka nywele zina tishu ambazo hukua haraka zaidi katika mwili.
Karoti ina mafuta asili yanayofahamika kama โsebumโ na mizizi ambayo husaidia kukuza nywele kwa haraka.
Tunda aina ya parachichi lina kazi nyingi sana mwilini kama matunda mengine, lakini hili ni tunda la kipekee amnbalo lina utajiri wa vitamini E ambayo husaidia mzunguko wa damu na katika hilo husaidia mfumo wa ukuaji wa nywele kwa haraka.
Tunda hili husaidia kuhuisha na kurekebisha mafuta na kiwango cha PH (inayosafisha kemikalii mwilini) ambavyo kama vitazidi kwenye mwili vinaweza kusababisha kusimama kwa ukuaji wa nywele, yaani nywele hudumaa.
Kwa faida zaidi, vitamin E inayopatikana kwenye parachichi kwa wingi husaidia zaidi afya ya moyo wa binadamu na zaidi ngozi. Hakikisha unapata tunda hili kadiri iwezekanavyo.
Hivi ni baadhi tu ya vyakula na matunda kwa ukuaji mzuri wa nywele zako. Kama unatumia vizuri mlo wako, utakuwa adimu sana kutumia mafuta yenye kemikali ambayo yanaweza kukuletea madhara mabaya.
Sala yoyote ili iwe SALA lazima itolewe kwa Imani, Upendo, Unyenyekevu na kwa Matumaini. Sala kama hii ndiyo ipendezayo mbele ya Mungu.
Recent Comments