Omba omba sio barabarani tuu
Boy:- baby ivi nikifa utakuja msibani?
Girl:-ntakuja ukinitumia nauli.
Hapo ndo unagundua kuwa sio kila omba omba yuko barabarani.
๐ค๐ค๐ค๐ค๐ค๐ค
Boy:- baby ivi nikifa utakuja msibani?
Girl:-ntakuja ukinitumia nauli.
Hapo ndo unagundua kuwa sio kila omba omba yuko barabarani.
๐ค๐ค๐ค๐ค๐ค๐ค
Hakuna m2 mwenye ndugu wengi kama konda wa daladala.
Utasikia,
“HAYA, DADA HAPO MBELE, MJOMBA KULE MWISHO.
MA-MDOGO UNAENDA?,
NGOJA ASHUKE BIBI.
HAYA SHEMEJI UMEIKUTA YA KUWAH.
Babu njoo ukae!
Baba angu hapo tusogee kidogo,
Shangazi maliza ngazi,
Swaiba geukia mbele,
Kaka hapo shika upande wa pili,
Mdogo wangu mpishe Ma Mkwe akae.
Subiri Shemeji yako apandeโฆ
Duhโฆ makonda nomaโฆ!!
Juzi nikitoka church nilipanda kihiace na kulikuwa na mrembo mkali hujawahi kuona,kila kijana alikuwa akimtupia macho,so me nilikuwa na wepesi wa kuongea naye kirahisi coz nilikuwa kando yake,,, Sasa kama unavyojuwa wanaume kwa kujikosha Nikaimigine mtto ananiangalia so nikaamuwa kupiga fake phone
“Hello Mr. Supervisor,nitachalewa kidogo coz kuna mahali nitapitia, so nipelekee tu hyo Ferrari yangu nyumbani”
Nikaona mrembo ameniangalia kwa macho ya husda apo nkajua nimeuwa ndege kwa jiwe moja, nkaamua kujikosha mtt wa kiume , “niaje mrembo”, akanikazia macho kisha akaniambia,
“Shika battery yako uliangusha ukitoa simu”
Icho kicheko watu walicheka hujawahi ona jooo adi ikabidi dereva aegeshe gari watu wacheke kwanza ๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Nikaona isiwe tabu nikashukia pale pale๐ถ๐ฟ๐ถ๐ฟ๐ถ๐ฟ
Tujifunze kusema ukweli kwani uongo sio mzuri hata kwa Munguโฆ ๐๐๐๐๐
Mtoto ni wa baba au wa mama?
Mume alimpa mkewe talaka wakaenda mahakamani ili hakimu aamue nani akae na mtoto.
MME: Akasimama akauliza hivi: Mheshimiwa hakimu hivi nikichukua ATM card nikaingiza kwenye mashine ikatoa pesa, sasa pesa zitakuwa ni za ATM au zakwangu?
MKE: Akasimama na kusema: Mheshimiwa hakimu hivi ukimwaga mbegu ktk shamba la mtu mti ukiota utakuwa wa kwako au wa mwenye shamba?.
Hebu tumsaidie hakimu aamue kesi hiiโฆ
Akina dada mpenzi wako akikuita MAMITO usikubali
na yeye mwite MAFORONYA kama mbwai na iwe mbwai๐คช๐คช๐คช๐คช๐คช๐คช
Et jana usiku mwiz kavunja mlango kwangu akaanza kutafuta kitu kila kona ikabid na mie niamke namuuliza unatafuta nini ananijibu hela ndipo nilipoanza na mie kutafuta nae maana hta hela ya kula Jana sikua nayo alichoka zaid nilipomuliza una uhakika uliweka humu? sipendagi ujinga๐ถ๐ป na kitu hela mm!
MUME wakati anakata roho huku mkewe akiwa amemshikilia alisema mke wangu, mi natubu kwako, kwani nilifanya mapenzi na dada yako, mdogo wako, rafiki yako na mama yako
MKE akamnong’oneza mume wake na kumwambia mbona mimi nayafahamu yote, ndio maana nimekupa sumu ili na wewe ujue uchungu wake. JE NANI ZAIDI?
Mfalme Sulemani alikuwa na wake 700 na alichepuka(cheated)na vimada 300 . Mpenzi wako/Mume wako unamfumania na kimada mmoja tu ugomvi na amani imapotea ndani ya nyumba,unasimulia kuanzia padri,mchungaji,ukoo wako mzima,mashoga, stress,vidonda vya tumbo,inapelekea mpaka unaokoka,eti kisa kamuonjesha mmojaโ sasa akionjesha 700 si utakutwa Mirembe๏ฟฝ
Wadada acheni HIZO
๐๐๐๐๐๐.
Kitambo tukiwa watoto ulikuwa unaitwa uje ule kwa lugha tofauti kulingana na chakula kilichopikwa siku na muda husika
1. UGALI NA KUNDE
Mwitaji : ๐ฃJoniiiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Uje ukule
2. UGALI NA SAMAKI
Mwitaji: ๐ฃ we Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Unaitwa na Mama
3. WALI NA NYAMA/KUKU
Mwitaji: ๐ฃ Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Shauri yako!
๐๐๐๐๐๐
Jamaa kaenda kwa mke wa rafiki yake:
JAMAA: Shem nakupenda!
MKE: Hebu toka hapa! Je rafiki
yako akijua? tena koma!
JAMAA: Ntakupa milioni 1!
MKE: Basi njoo kesho mchana
mume wangu akiwa kazini!
Kesho yake Jamaa kaja
na milioni 1 wakamalizana na mke wa rafki yake,
jioni ilipofika
Mume akarudi home na
kumuuliza Mkewe, “Rafki yangu SAM kaleta hela yangu milioni 1?”
MKE akajibu kwa unyonge, “Ndio!”
MUME: Yes! Ndio maana nampenda SAM kanikopa asubuhi jioni karejesha!!!!
Mke hoiโฆโฆ
๐๐๐๐๐๐
Hili nalo neneo.
Ukimuona mbwa๐ถ harusini usimpige mawe wala kumfukuza inawezekana kilichomleta pale ndicho kilichokupeleka na wewe hapo
Ka ni wewe?
DOGO: baba mi siendi tena shule inaonekana walimu hawana uhakika na majibu yao.
BABA: Kwanini unasema hivyo?
DOGO: juzi walisema 3+4= 7, jana wakasema 1+6=7, halafu leo wanasema 5+2=7 sasa huoni kama wanatuchanganya.
ungekua wewe ungemjibu nini
Miaka 13: Usipende wavulana ni wabaya.
Miaka 18: Sitaki nikuone na yule mvulana tena!
Miaka 23: Lini utatuletea mchumba wako?
Miaka 26: Wenzio wanaolewa.
Miaka 30: Tumekuambia kwamba acha
kuchagua sana wanaume, hutaki kusikia!
Miaka 33: Kuna mtu wa Mungu yupo kule
anaombea unaweza kupata mchumba
Miaka 36: At least pata mtoto mmoja.
Miaka 39: We will take care of all the wedding
billsโฆyeyote ni sawa sisi tutagharamia kila kitu mwanetu wee mlete tu .
Miaka 45: hivi kweli nani alikuroga.?
๐๐๐ changamkia fulsa umri ukifika
Jamaa kaenda kumtembelea rafiki yake Levi, kule sehemu za kwetu, akakaribishwa bonge ya ugali na nyama nyingi tu, wakati anakula akagundua kuwa shemeji yake, mke wa rafiki yake hali nyama;
JAMAA: Aise hili ni bonge ya lanchi hii, lakini Levi mbona sisi tu tunakula nyama shemeji Gulo hagusi kabisa anaishia mchicha tu? Tabia gani hii?
LEVI: Hapana sijamkataza, ila shemeji yako Mngoni halagi nyama ya FISI kama sisi
Recent Comments