Vichekesho Vya Asubuhi Hii

Kweli shilingi yaua, Huyu jamaa kapatikana, angalia anachomjibu mke wake,

Jamaa alikuwa anagombana na mkewe,hatimae
akamwambia kwa ukali
“Unajua nimechoka sasa, haya kusanya nguo
zako na……..

Kabla hajamalizia sentensi simu
ya mkewe ikaita, kumbe alikuwa ni baba yake.
Basi mzee akaanza kuongea na binti yake huku
jamaa anasikia

“Aisee mwanangu nimebahatika kuuza ile
nyumba yangu sasa nimeona niwatumie milioni
20 mjaribu kuanzisha mradi na mwenzio.
Haya mwambie yeye nitampigia kesho kama
ana mradi mwingine nimpe hela kidogo”.Baada
ya simu kukatwa mke akamgeukia jamaa
akamuuliza,”eeenhee!!! ulikuwa unasema
umenichoka nikusanye nguo zangu halafu
iweje? Jamaa kwa upole akajibu “Nilikuwa
nasema ukusanye nguo zako na unipe nifue”.

Hii mitoto mingine mijinga, cheki alichokifanya huyu

Nimeamka asubuhi nikiwa na elfu 1 tu mfukoni, nikamtuma mtoto wa jirani akaninunulie maandazi nipate kunywa chai. Baada ya muda namuona anarudi huku analamba askrimu ya AZAM kama Simba vile. Nikamuuliza maandazi yako wapi? Akanijibu eti wakati anafika yanapouzwa maandazi akagundua kuwa kapoteza hela yangu, hivyo akaanza kurudi, ila bahati nzuri wakati anarudi ili kuja kunitaarifu kuhusu kupotea kwa hela yangu, njiani akaokota elfu 1 ambayo kuna mtu alipoteza ndio akaamua kununua askrimu….kwa sasa niko polisi na mtoto yuko dispensari na mamake😀😀😀😀😀😀😀

Angalia huyu jamaa alivyowafanyia watu uhuni bar

Jamaa kaingia Bar;
Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji. Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,

Jamaa: Muhudumu nipe supu na kila mtu humu ndani mpe supu maana ninapokunywa supu kila mtu lazima anywe supu. Watu wakapewa supu tena safari hii wakapiga makofi.
Jamaa: Muhudumu nipe bili, na kila mtu humu ndani mpe bili maana wakati nalipa bili yangu kila mtu lazima alipe yake. Zogo lilianzia hapo…….

Ameniomba nimfungulie akaunt facebook cheki nilichomjibu

Leo nimechoka zangu alafu shangazi amekuja anataka nimuunganishe facebook. Imebidi nimwambie
lazima awe na picha passport size 4 kwaajili ya kuweka profile picture, barua kutoka kwa afisa mtendaji na Atm card ya nmb bank. Alafu awe na marefa wanne ambao wamekuwa facebook for more than 3 years. Amesema
hataki tena kujiunga fb!

😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Saa ivi niko zangu nimelala naendelea kupunguza uchovu

Baadhi ya misemo mikali ya leo

1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.

2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.

3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?

4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.

5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.

6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.

7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.

8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.

9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.

10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi kufunika sufuria.

Shopping Cart
3
    3
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About