Dalali aliwatafutia jamaa chumba Buguruni karibu na reli, nyumba nzuri sana. Jamaa na mkewe wakahamia kwa furaha, lakini furaha yao iliisha walipokuja gudundua nyumba ile iko karibu mno na reli treni ikipita mpaka kitanda kinacheza.
Siku hiyo dalali akapita mke akamwita na kumwambia tatizo wakati treni inapita, wakaanza kubishana, yule mama akamwambia dalali kwa kuwa kuna treni itapita sasa hivi… njoo ndani uone mwenyewe.
Bahati mbaya wakiwa wamejilaza kitandani ili dalali aone adhabu wanayopata, Mzee mwenye mali alirudi ghafla, akauliza,
‘Nyie mnafanya nini hapa?’
Masikini dalali kwa woga mkubwa akajibu’ Tunangoja treni’
Nimecheka hadi machozi yanatoka! 🤣😭
Hii ni kali kabisa! Siwezi kushiba! 😂
Hii ni bomba sana! 🤣👍
Lazima niihifadhi hii, ni kichekesho kali sana! 😆
Hii imenichekesha sana! 🤣😆