Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Mambo ya Msingi unayotakiwa kufahamu kuhusu Sakramenti ya Daraja

Daraja na ndoa ni tofauti na sakramenti nyingine kwa sababu gani?
Daraja na ndoa ni tofauti na sakramenti nyingine kwa sababu hazilengi hasa faida ya mtu anayezipokea, bali huduma zake kwa ajili ya Kanisa na jamii. Daraja inatia uwezo wa Kristo kwa ustawi wa Kanisa, Bibi arusi wake. Ndoa inatia upendo wake mwaminifu kwa ustawi wa familia, kanisa dogo la nyumbani.
“Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe” (Mdo 20:28).
“Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa. Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa” (Ef 5:29-32).


Je, daraja takatifu zinahitajiwa kabisa na Kanisa?
Ndiyo, daraja takatifu zinahitajiwa kabisa na Kanisa kwa sababu kazi ya wokovu haimtegemei binadamu, bali Mungu.
“Hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni. Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu” (Eb 5:4-5),
Yesu alisisitiza alivyopewa na Baba uwezo wa kutuokoa. “Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake” (Yoh 3:35).
“Kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele” (Yoh 17:2)
.
Kisha kufufuka alitumia mamlaka hiyo kuwatuma wanafunzi kumi na mmoja waliobaki:
“Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa dahari” (Math 28:18-20).
Mpaka mwisho wa dunia uwezo huo wa Kimungu utatolewa tu kwa sakramenti ya daraja, inayounganisha mtu na Mitume kupitia mlolongo usiokatika wa kuwekewa mikono ili kushirikishwa mamlaka. Bila yake, kuna upungufu katika ufundishaji, utoaji wa sakramenti na uongozi.


Je, wenye daraja wanastahili heshima?
Ndiyo, wenye daraja wanastahili heshima kwa sababu ya mamlaka ya Kiroho waliyonayo kutoka kwa Kristo.
“Amin, amin, nawaambieni: Yeye ampokeaye mtu yeyote nimpelekaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi ampokea yeye aliyenipeleka” (Yoh 13:20).
“Jaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Kristo Yesu” (Gal 4:14).
“Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii” (Tito 3:1).
Wenye daraja wanaotimiza kazi zao vizuri wanastahili heshima kwa uaminifu wao pia.
“Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu, hasa hao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha” (1Tim 5:17).


Je, wenye daraja wanaweza wakatenda dhambi?
Ndiyo, wenye daraja wanaweza wakatenda dhambi kwa sababu ni binadamu kama sisi sote. Yesu alionja ukosefu wa Mitume hasa wakati wa mateso.
“Je, mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, na mmoja wenu ni shetani?” (Yoh 6:70).
“Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao, na kuniacha mimi peke yangu” (Yoh 16:32).
Paulo alionya mapadri, “Katika ninyi wenyewe watainuka watu, wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao” (Mdo 20:30).


Ili tuwe na wachungaji wengi waaminifu tunapaswa kufanya nini?
Ili tuwe na wachungaji wengi waaminifu tunapaswa hasa kusali.
“Mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake” (Math 9:38).
Halafu yanahitajika maandalizi ya muda mrefu, juhudi na ushirikiano wa kidugu.
“Asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi… Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia… Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine” (1Tim 3:6; 4:16; 5:22).


Je, wanawake wanaweza kupewa daraja?, Mwanamke anaweza kuwa padri?
Hapana, wanawake hawawezi kupewa daraja, kwa sababu kwa karibu miaka elfu mbili mfululizo Kanisa limejiona halina mamlaka ya kufanya tofauti na Yesu. Yeye alichagua wanaume tu kuwa Mitume wake, ingawa walikuwepo wanawake waaminifu kuliko wengi wao, hasa Maria, mtakatifu kuliko wote.
“Petro, na Yohane, na Yakobo, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo wa Alfayo, na Simoni Zelote, na Yuda wa Yakobo. Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake… Wakaweka wawili, Yusufu, aitwaye Barsaba, aliyekuwa na jina la pili Yusto, na Mathiya… kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja” (Mdo 1:13-14,23,26).
“Walimchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia; ambao wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao” (Mdo 6:5-6).


Je, kutoa daraja kwa wanaume tu ni kuwakosea haki wanawake?
Hapana, kutoa daraja kwa wanaume tu si kuwakosea haki wanawake, kwa kuwa hizo ni huduma zinazofaidisha wote.
“Maana aliye mkubwa ni yupi? Yeye aketiye chakulani, au yule atumikaye? Siye yule aketiye chakulani? Lakini mimi kati yenu ni kama atumikaye” (Lk 22:27).
Mwenye daraja anahudumia Kanisa kwa kumwakilisha Yesu; hivyo anatakiwa kuwa mwanamume kama yeye mbele ya Bibiarusi wake. Kukubali mgawanyo wa majukumu maishani ni kusifu hekima ya Mungu aliyetuumba watu wa jinsia mbili tofauti ili kustawisha familia, jamii na Kanisa.
“Walakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwana… Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake” (1Kor 11:11; 12:27).


Je, mwenye daraja anaweza kuwa na ndoa?
Ndiyo, mwenye daraja anaweza kuwa na ndoa.
“Hatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke aliye ndugu, kama wao mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?” (1Kor 9:5).
Paulo, akiwa mseja, hakudai kila mmojawao aoe, ila asiwe ameoa mara mbili, bali “mume wa mke mmoja” (1Tim 3:2; Tit 1:6), kama alivyoagiza mjane aandikishwe akiwa tu “mke wa mume mmoja” (1Tim 5:9).
Polepole mang’amuzi yakaelekeza Kanisa kubana nafasi hiyo kwa Maaskofu, na katika majimbo mengi kwa mapadri pia. Useja mtakatifu unawalinganisha zaidi na Yesu na kuwaachia uhuru wa moyo na wa muda kwa ajili ya huduma.
“Wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee” (Math 19:12).


Ni zipi Sakramenti za Huduma ya ushirika na utume?
Ni Sakramenti mbili ambazo ni Sakramenti ya Daraja na Sakramenti ya Ndoa


Sakramenti ya Daraja ndiyo nini?
Sakramenti ya Daraja ndiyo Sakramenti ambayo mwanamme mkatoliki aliyeitwa na Mungu hupata mamlaka na neema ya kuendeleza ndani ya Kanisa Utume Kristo aliowakabidhi Mitume wake


Ni kwa nini inaitwa Sakramenti ya Daraja?
Inaitwa Sakramenti ya Daraja kwa sababu mtu anapata Sakramenti hii kwa kuweka wakfu kwa ibada ya pekee inayomwezesha kwa nguvu ya Roho Mtakatifu atumie uwezo Mtakatifu kwa niaba na mamlaka ya Yesu Kristo ili kuhudumia Taifa la Mungu


Sakramenti ya Daraja ina ngazi ngapi?
Sakramenti ya Daraja inazo ngazi tatu, nazo ni Ushemasi, Upadre, Uaskofu


Ibada ya kutolea Daraja ya uaskofu ina matokeo gani?
Ibada ya kutolea Daraja ya uaskofu ina matokeo yafuatayo;
1. Inampa utimilifu wa SSakramenti ya Daraja Takatifu
2. Askofu anakuwa Mwandamizi rasmi wa Mitume
3. Inampa Askofu ushirika na Papa na maaskofu wengine wa kuwajibikia Makanisa yote
4. Inampa uwezo wa kufundisha, kutakasa na kuongoza


Askofu ni nani?
Askofu ndiye mchungaji mkuu wa kanisa Mahalia au Jimbo lake


Askofu ana kazi gani katika Jimbo lake?
Askofu katika Jimbo lake anamwakilisha Kristo akitimiza kazi ya kichungaji akisaidiwa na mapadri na mashemasi wake.
Askofu ni kiongozi wa kiroho katika jimbo mahalia. Na sio mambo ya kiroho tu ila hata ya kijamii lakini watu/mtu akiitaji ufafanuzi na msaada toka kwake.
Kazi zake ni:-
1. Kuliongoza taifa la Mungu alilopewa yaani wakristo/wengineo pia
2. Kusimamia na kuongoza Litrujia katika eneo husika.
3. Kueneza amani kwa kupitia karama na wadhifa aliopewa na Mungu.
4. Kueneza upendo katika eneo/jimbo mahalia.
5. Mtoa kauli ya mwisho kwa mambo ya kikanisa katika jimbo.
6. Kusimamia miito ya kanisa na kuchochea bila kukata tamaa
7. Kusimamia baraza la walei na kulishauri kwa kutolea kauli ya Mwisho kabla ya kwenda kwingine
8. Kuwashauri watu waliokata tamaa au kushindikana katika ngazi za chini
NB. Hivyo ndani ya kanisa kuna miogozo ili kupata nafasi zisizokinzana


Ni nani ampaye padri Daraja la Uaskofu?
Ni Baba Mtakatifu pekee au humteua Askofu mmoja akisaidiwa na maaskofu wengine wawili humweka wakfu Padri huyo kuwa Askofu (Mt 13:2-3)


Baba Mtakatifu ni nani?
1. Ndiye Askofu Mkuu wa Maaskofu wote
2. Ndiye mchungaji mkuu wa Wakatoliki wote hapa duniani
3. Ni Wakili wa Yesu Kristo hapa duniani. (Mt 16:18-19; Yoh 21:15-17).


Ibada ya Daraja inachapa alama gani nafsini mwa aliyepewa?
1. Ibada ya Daraja inatia rohoni alama isiyofutika
2. Inamlinganisha mpokeaji na Kristo Kuhani
3. Inamwezesha mwenye Daraja kutenda kwa Jina la Yesu aliye Kichwa cha Kanisa


Kwa Sakramenti ya Daraja Padri anapata mamlaka gani?
Kwa Sakramenti ya Daraja Padri anapata mamlaka ya
1. Kuadhimisha sadaka ya Misa Takatifu na kutakasa watu kwa njia ya Sakramenti.
2. Kuhubiri neno la Mungu
3. Kuwaongoza watu (Ebr 5:1-4)


Ni nani wenye uwezo wa kutoa Sakramenti ya Daraja?
Wanaotoa Sakramenti ya Daraja Katika ngazi tatu Uaskofu, Upadre, Ushemasi ni Maaskofu waliopewa Daraja halisi kama waandamizi wa Mitume.


Ni nani aweza kupewa kihalali Sakramenti ya Daraja Takatifu?
Mwenye kupewa kihalali Sakramenti ya Daraja Takatifu ni Mwanaume peke yake aliyebatizwa, akiwa na wito nasifa zinazotakiwa na kukubaliwa na Mamlaka ya Kanisa. Ndivyo Yesu Kristu alivyotaka mwenyewe


Alama wazi ya Sakramenti ya Daraja Takatifu ni nini?
Alama wazi ya Sakramenti ya Daraja Takatifu ni kuweka mikono juu ya yule anayepewa Daraja na kutamka maneneo ya sala ya wakfu.


Anayetaka kuwa padri yampasa nini?
Yampasa;
1. Awe na tabia njema, akili za kutosha na afya nzuri.
2. Apende sana wokovu wa watu na kujitolea kwa huduma ya Mungu
3. Awe tayari kuishi hali ya useja maisha yake yote


Kwa sababu gani cheo cha Padri ni kikubwa sana?
Kwa sababu Padri anashiriki Upadri wa Yesu Kristo na ni mjumbe kati ya Mungu na Mwanadamu


Yatupasa nini kwa wenye Daraja Takatifu?
Yatupasa
1. Kuwaheshimu
2. Kuwasikiliza na kufuata mafundisho yao
4. Kuwasaidia katika utumishi wao kwa Sala na sadaka zetu


Matokeo ya Sakramenti ya Daraja ni yapi?
1. Inaleta mmiminiko wa kipekee wa Roho Mtakatifuambao unamlinganisha mhusika na Kristo
2. Inatia alama ya kiroho isiyofutika. kwa hiyo haiwezi kurudiwa au kutolewa kwa muda tuu.

Safari ni safari

FUNDISHO : SAFARI NI SAFARI

Maisha ni ya ajabu sana, wakati mwingine maisha ni mazuri na mwingine ni mabaya, katika maisha yetu tumeshapitia safari nyingi sana na za aina mbalimbali kwa nyakati mbalimbali. Lakin kiukweli kila safari ni safari tuu.

Japokua kila safari ina changamoto zake lakini mwisho wake ni ule ule , kila safari ina uzuri na upekee wake.

Vile vile kila safari ina ubaya wake, kwa mfano kila safari ina gharama yake kulingana na upekee wake.

Usiwe na wasiwasi na mashaka na aina ya safari ulionayo, jipe moyo utaimaliza na kupata ulichokitarajia. Haya ndio maisha na wote tunatakiwa tuyafurahie.

Ingawa kila mtu ana safari yake bado wote tunatakiwa tufurahie pamoja kwa safari tuliyo nayo. Hata Uwe Na safar ya aina gani wewe furahi tuu. Hii ni kwa sababu safari mwisho wake ni mmoja kwa wote burudani ni ile ile

Safari🍺 ni safari 🍺hata kama ni ya chupa au ya kopo mwisho wake 💤💤

😋😜😜😂😂😂
Ulijua ni nn??

Maswali na Majibu kuhusu Biblia

Neno Bwana lina maana gani katika Biblia?
Neno Bwana Katika Biblia linamaanisha “Mungu Mtawala”

Mapokeo ya Mitume ndiyo nini?
Mapokeo ya Mitume ndiyo yale yote ambayo Yesu aliwakabidhi Mitume wake, na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu yatadumu hata mwisho wa dunia katika mafundisho, liturujia na maisha ya Kanisa.
“Nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vilevile kama nilivyowatolea… Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe” (1Kor 11:2; 15:3).
“Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu… Mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine” (2Tim 1:14; 2:2).
Tukikata huo mnyororo wa mapokeo, hata kama ni kwa kisingizio cha kushikilia Biblia, tunaachana na asili ya Kanisa.
“Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu… Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu” (2Thes 2:15; 3:6).

Maandiko Matakatifu ndiyo nini?
Maandiko Matakatifu ndiyo vitabu vyote 73 ambavyo viliandikwa na watu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu vikakusanywa na Kanisa kwa jina la “Biblia”, yaani “Vitabu”.
Hao “wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu” (2Pet 1:21).

Je, Biblia zote ni sawa?
Hapana, Biblia zote si sawa. Tujihadhari na matoleo mapungufu ambamo vimenyofolewa vitabu 7 vizima na sehemu kadhaa za vitabu vingine vilivyotumiwa na Wakristo wa kwanza.
“Amin, nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie” (Math 5:18). “Na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki” (Ufu 22:19).
Je wakristo Wakatoliki wanasoma Biblia kwenye Ibada ya Misa? Biblia inanukuliwa mara ngapi Kwenye Ibada ya misa ya Wakatoliki?
Ndiyo, Wakatoliki wanasoma Biblia kila siku wanapoadhimisha Ibada ya Misa wakati wa Liturujia ya Neno.
Wakatoliki wananukuu Biblia mara Tano kwenye Ibada ya Misa. Wananukuu wanaposoma somo la Kwanzaa, Somo la pili, wimbo wa katikati, Shangilio na Injili.

Tunatambuaje Maandiko Matakatifu kati ya maandishi yote ya binadamu?
Tunatambua Maandiko Matakatifu kati ya maandishi yote ya binadamu kwa njia ya Mapokeo, yaani kwa sababu yametumiwa na Kanisa tangu mwanzo kwa kulisha kwa hakika imani yake.
Tunahitaji Mapokeo kwa kuwa Maandiko yenyewe hayataji orodha ya vitabu vyake vyote, Sanasana Yesu alividokeza baadhi akisema yanamzungumzia na kutimia ndani yake,
“Ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii, na Zaburi” (Lk 24:44).
Halafu Barua ya Pili ya Mtume Petro ikalinganisha “na Maandiko mengine” nyaraka zote ambazo Paulo aliziandika “kwa hekima aliyopewa” (2Pet 3:15-16).

Sababu nyingine za Biblia kutojitosheleza ni zipi?
Sababu nyingine za Biblia kutojitosheleza ni kwamba mambo mengi muhimu hayakuandikwa,
“Kuna mambo mengine mengi aliyoyafanya Yesu, ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa” (Yoh 21:25).
Tena barua ni nusu tu ya kuonana; hivyo Yesu hakuandika lolote, nao Mitume hawakupenda kuandika yote.
“Kwa kuwa ninayo mambo mengi, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini nataraji kuja kwenu, na kusema nanyi mdomo kwa mdomo, ili furaha yetu iwe imetimizwa” (2Yoh 12).
“Nalikuwa na mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa wino na kalamu. Lakini nataraji kukuona karibu, nasi tutasema mdomo kwa mdomo” (3Yoh 13-14).
Hasa ibada haziwezi kufanyika kwa barua; k.mf. kuwekea mikono ili kumshirikisha Roho Mtakatifu. Paji la namna hiyo halipitii Maandiko, bali Mapokeo tu. Hatimaye Biblia ikipotoshwa haipingi, kwa kuwa si mtu hai anayeweza kujitetea.

Biblia iliandikwa kwa kusudi gani?
Biblia iliandikwa kusudi tupate “kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini” tuwe “na uzima wa milele” (Yoh 20:31).
“Tangu utoto umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. Kila Andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki” (2Tim 3:15-16).
Si lengo lake kutufundisha historia, jiografia wala sayansi: kuhusu elimu hizo na kuhusu ufasaha wa lugha Biblia ilitegemea ujuzi na vipawa vya watu walioiandika.

Je, vitabu vya Biblia vinatofautiana?
Ndiyo, vitabu vya Biblia vinatofautiana kwa kuwa Mungu alijifunua hatua kwa hatua; hivyo vitabu 46 vilivyoandikwa kabla ya Yesu vinaitwa Agano la Kale na 27 vilivyomfuata vinaitwa Agano Jipya.
“Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka” (Eb 8:13).
Mungu “ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha” (2Kor 3:6).

Je, vitabu vyote vya Biblia vinahusiana?
Ndiyo, vitabu vyote vya Biblia vinahusiana kwa kuwa vinaangaziana na kuunda kitabu kimoja ambacho ni Neno la Mungu yuleyule, ingawa katika hatua tofauti: Agano la Kale ndiyo maandalizi na Agano Jipya ndio utimilifu wake.
Yesu alisema, “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua Torati au Manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza” (Math 5:17).
Tunahitaji Agano la Kale ili tuelewe vizuri Agano Jipya katika maandalizi yake, na tunahitaji Agano Jipya ili tuelewe Agano la Kale lilivyotimilizwa na Yesu.

Je, inafaa tushike neno lolote la Agano la Kale kama Wayahudi?
Hapana, haifai tushike neno lolote la Agano la Kale kama Wayahudi wasiozingatia jinsi Yesu alivyolitimiliza kwa maneno na matendo hata wakamshutumu kutenda kinyume:
“Mtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato” (Yoh 9:16).
Alipofafanua amri 10 za Mungu alikariri:
“Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa… lakini mimi nawaambieni…” (Math 5:21,27,31,33,38,43).
Alipouliziwa unajisi wa vyakula kadhaa, alisisitiza,
“’Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi; kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni?’ Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote” (Mk 7:18- 19).
“Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo” (Kol 2:16-17).
Hakika, mwili ni mzito kuliko kivuli chake.
Vile vile katika Warumi 4:16. Tunasoma “Kwa sababu hiyo, jambo hili lategemea imani, hivyo kwamba ahadi hiyo yatokana na neema ya Mungu, na kwamba ni hakika kuwa ahadi hiyo ni kwa ajili ya wote:si kwa wale tu wanaoishika sheria, bali kwa wale waishio kwa Imani kama Abrahamu. Yeye ni Baba yetu sote.”
Wakristo wengine wanachanganywa na wale wasioyajua maandiko na kuwataka washike sheria na Torati,basi tukisema ni lazima kushika sheria tutakua tunakataa kua Abrahamu hakuwa mtu wa Mungu maana kwa Abrahamu hatukuwa na Sheria wala Torati na alipata kibali machoni Pa Mungu tuu kwa Imani. Kumbuka pia Abrahamu alitahiriwa baada ya Kuwa tayari mtu wa Mungu kwa Imani yake na sio kwamba Kutahiriwa ndio kulifanya mtu wa Mungu.
Tumekombolewa kwa Imani na sio kwa Sheria. Wagalatia 5:18 “Lakini Mkiongozwa na Roho hampo chini ya sheria”
Hatumtumikii Mungu ili tuwe watu wa Mungu bali tukishakua watu wa Mungu ndio tunamtumikia Mungu.

Yesu alitimiliza Agano la Kale kwa namna isiyotarajiwa hasa lini?
Yesu alitimiliza Agano la Kale kwa namna isiyotarajiwa hasa aliposulubiwa, akionekana na Wayahudi wenzake kama kwamba amelaaniwa:
“Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa: ‘Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti’; ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani” (Gal 3:13-14).

Kati ya vitabu vya Biblia, vilivyo bora ni vipi?
Kati ya vitabu vya Biblia, vilivyo bora ni Injili 4 zilizoandikwa na Mathayo, Marko, Luka na Yohane.
Ndio moyo wa Maandiko Matakatifu yote, kwa kuwa ndizo shuhuda kuu juu ya maisha na mafundisho ya Yesu.
Yeye “amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora. Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili” (Eb 8:6-7).

Tueleweje Maandiko Matakatifu?
Tuelewe Maandiko Matakatifu kwa kuzingatia hasa Mungu alitaka kusema nini kuhusu wokovu wetu kupitia waandishi wengi aliowaongoza kuyatunga kwa lugha na mitindo mbalimbali.
Lakini ebu, “Yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na Maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe” (2Pet 3:16).
Utitiri wa madhehebu yanayoshindana yakidai kushikilia Biblia tu unathibitisha uwekezano mkubwa wa kuipotosha kwa namna moja au nyingine.
“Utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia walimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo” (2Tim 4:3-4).
Njia pekee ya kukwepa fujo hiyo ni kuelewa Maandiko ndani ya Kanisa, kadiri ya Mapokeo yake hai.
“Lakini mtu yeyote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu” (1Kor 11:16).
Biblia nje ya Kanisa ni kama samaki nje ya maji.

Tupokeeje ufunuo wa Mungu?
Tupokee ufunuo wa Mungu kwa kusadiki mafundisho ya Kanisa lake, ili tuzidi kumjua na kuambatana naye bila ya kudanganyika. Yesu aliwaambia Mitume wake,
“Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma” (Lk 10:16).
“Sisi nasi twamsukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kwelikweli, litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini” (1Thes 2:13).

Neno “BIBLIA” maana yake ni nini?
Neno “BIBLIA” ni neno linalotokana na neno la Kigiriki “Biblion” lenye maana ya vitabu.
Biblia ni Mkusanyiko wa vitabu mbalimbali vya dini vilivyochaguliwa na kuidhinishwa kua vyafaa kutumika.

Biblia ni nini? Asili, Historia, waandishi na mipaka yake
Biblia ni mkusanyiko wa vitabu mbalimbali vinavyohusu kazi ya Mungu ya kuwakomboa mwanadamu kuanzia enzi za Mababu na manabii Wa Waisraeli, Enzi za Yesu na za Mitume wa Yesu.
Je, Biblia ilipatikanaje? Nini chanzo na asili ya Biblia.
Biblia iliundwa kwa kukusanya vitabu vya dini vya wakristo hapo awali na kuunda kitabu kimoja. Kwa maana hii, Biblia ni vitabu teule vya dini vilivyoonekana vinafaa kutumika kwa waumini Wakristo ili kusaidia Imani yao. Hivyo basi, kama Biblia ni vitabu teule tuu vipo vitabu vingine vya dini ambavyo havikuwekwa Kwenye Biblia.
Wakristo wa kwanza walichagua vitabu kadhaa na kuviweka pamoja na kisha kuvita Biblia. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu muhimu tuu vya dini mpaka kufikia Enzi za Mitume.
Je, Biblia ndicho kitabu pekee cha neno la Mungu?
Hapana, Biblia sio kitabu pekee cha neno la Mungu isipokua Biblia ni kitabu kilichoidhinishwa rasmi kutumika Kama kitabu kikuu cha Wakristo. Hii ni kwa sababu Biblia imeundwa na vitabu muhimu tuu vilivyochaguliwa na wakristo wa kwanza vilivyoonekana vinafaa kwa kufundishia, Ibada na kukuza Imani. Kwa hiyo basi vipo vitabu vingine ambavyo haikuwekwa Kwenye Biblia ambavyo ni Maneno ya Mungu.
Hii ndiyo sababu kwa nini Wakatoliki wana vitabu vingi kuliko madhehebu Mengine. Yaani sababu ni kwamba madhehebu Mengine walivitoa vitabu vingine vilivyounda Biblia. Na Wakatoliki waliweka vitabu vingine vya dini Kwenye Biblia walivyoona vinafaa pia kutumika.
Je nje ya Biblia hakuna Neno la Mungu au Maandiko matakatifu?
Nje ya Biblia kuna Neno la Mungu na Maandiko Matakatifu. Hii Inamaanisha kuwa Biblia sio kitabu pekee cha neno la Mungu. Zipo nyaraka na Vipo vitabu vingine vingi ambavyo viliandikwa na Manabii na Mitume ambavyo havikuwekwa kwenye Biblia lakini ni mafundisho ya Mungu. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vikuu vya Mungu.
Kumbuka kuwa sio nyaraka zote za Mitume ziliandikwa Kwenye Biblia. Vile vile manabii walikuwa ni wengi kuliko waliowekwa Kwenye Biblia.
Je Biblia ndiyo mafundisho ya Mungu pekee?
Hapana, Biblia sio mafundisho pekee ya Mungu. Hii ni kwa sababu sio mambo yote aliyofanya na kusema Mungu yaliandikwa na vilevile Mitume hawakua watu wa Mwisho kupokea Roho mtakatifu na kupokea neno la Mungu.
Biblia inatuthibitishia yenyewe kuwa haijakamilika na Si mambo yote yameandikwa Kwenye Biblia
Biblia inatuthibitishia kuwa haijakamilika tunaposoma (Yohane 21:25)
Biblia inatuambia hivi…”Kuna mambo Mengine mengi aliyofanya Yesu, ambayo Kama yangeandikwa yote, moja baada ya jingine, nadhani hata ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.”…Kwa mstari huu Biblia inatuthibitishia kuwa haikuandikwa vitu vyote.
Je Biblia ni mwisho wa Maandiko ya Mungu?
Biblia sio mwisho wa Maandiko ya Kimungu.
Biblia ni sehemu ya maneno ya Mungu mpaka miaka ya Mitume
Hata sasa Mungu anafanya kazi na watu wake kupitia Roho Mtakatifu na kwa kwa sababu hii Biblia sio mwisho wa kazi ya Mungu ya kusema na watu wake.
Mungu yu hai na anafanya kazi na watu wake mpaka sasa kwa kutumia vinywa vya watu Kama aliyofanya hapo awali.
Hata maneno unayohubiriwa sasa yanaweza kuwa ni kutoka kwa Mungu kwa maana hata waandishi wa Biblia walitumiwa na Mungu Kama wahubiri wa sasa. Mungu ni yule yule, Roho Mtakatifu ni yuleyule na Neno ni lile lile.
Kwa hiyo Biblia ni maneno yaliyochaguliwa mpaka enzi za Mitume. Vitabu vilivyofwata Baada ya Mitume japokuwa viliandikwa kwa Roho Mtakatifu havikuwekwa Kwenye Biblia.
Sababu ya Kanisa katoliki kutumia mapokeo na Maandiko ya Watakatifu
Kanisa katoliki linatumia mapokeo na Makala za watakatifu kwa Imani kuwa Mungu yule yule aliyefanya kazi tangu zamani anafanya kazi na watu wake mpaka sasa na hivyo Maandiko ya watu wa Mungu yanafaa kutumika kama yalivyotumika ya watu wa kale.
Yesu alituambia nini kuhusu Neno la Mungu na Mwendelezo wa kazi ya Mungu ya kusema na watu?
Yesu alituambia hivi katika (Yohane 16:12-15)..”Ninayo mengi ya kuwaambieni Ila kwa sasa hamuwezi kuyastahimili. Lakini atakapokuja huyo Roho wa Ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote. Maana hatasema kwa Mamlaka yake mwenyewe bali atasema atakayoyasikia na kuwajulisheni yatakayokuja. Yeye atanitukuza Mimi kwa kuwa atawajulisheni Yale atakayoyapata kutoka kwangu “…
Sasa basi,kama Roho Mtakatifu ni yuleyule na kazi zake ni Zile Zile za tangu Mitume, kwa nini hatukubali kuwa Anafanya kazi mpaka sasa kupitia watu wa Mungu? Kwa nini tunakataa mafundisho yao? Kwa nini tunashindwa kuelewa kuwa Biblia haikuwa mwisho wa Neno la Mungu? Kwa nini tunakana Mapokeo ya Watakatifu? Kwa nini hatuwaamini watumishi wake wa sasa?

Biblia ina sehemu kuu ngapi?
Biblia ina sehemu kuu 2 (mbili) ambazo ni
1. Agano la Kale (A.K)
2. Agano Jipya (A.J)

Agano la Kale lina vitabu vingapi?
Agano la Kale lina vitabu 46

Agano Jipya lina vitabu vingapi?
Agano Jipya lina vitabu 27

Biblia nzima ina vitabu vingapi?
Biblia nzima ina vitabu 73

Vitabu vya Agano la Kale vimegawanywa katika sehemu ngapi?
Vitabu vya Agano la Kale vimegawanywa katika sehemu 4 nazo ni
1. Vitabu vya Musa (5)
2. Vitabu vya Historia (16)
3. Vitabu vya Hekima (7)
4. Vitabu vya Manabii (18)

Vitabu vya Agano Jipya Vimegawanywa katika sehemu ngapi?
Vitabu vya Agano Jipya Vimegawanywa katika sehemu 4 nazo ni
1. Injili (4)
2. Kitabu cha Matendo ya Mitume
3. Nyaraka mbalimbali (21)
4. Kitabu cha Ufunuo

Vitabu vya Musa ni vipi?
Vitabu vya Musa ni
1. Mwanzo
2. Kutoka
3. Walawi
4. Hesabu
5. Kumbukumbu la Torati

Wainjili wanne Katika Agano Jipya ni wakina nani?
Wainjili wanne Katika Agano Jipya ni
1. Mathayo
2. Marko
3. Luka
4. Yohane

Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano la Kale ni vipi?
Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano la Kale ni
1. Cha kwanza ni Kitabu cha Mwanzo
2. Cha mwisho ni Kitabu cha Malaki

Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano Jipya ni vipi?
Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano Jipya ni
1. Kitabu cha kwanza ni Injili ya Mathayo
2. Kitabu cha mwisho ni Kitabu cha Ufunuo

Injili ni nini?
Injili ni Habari njema ya wokovu iliyoletwa na Yesu Kristo

Watoto wawili wa Adamu na Eva walkikuwa wepi?
Walikuwa ni Kaini na Abeli

Watoto wa Nuhu ni wepi?
Watoto wa Nuhu ni Shemu, Hamu na Nefteli

Mababu watatu wa Imani Katika Biblia ni wakina nani?
Mababu wa Imani ni Ibrahimu, Isaka na Yakobo

Watoto wa Yakobo ni Wepi?
Watoto wa Yakobo ni
1. Reubeni
2. Simeoni
3. Lawi
4.Yuda
5. Dani
6. Naftali
7. Gadi
8. Asheri
9. Isakari
10. Zabuloni
11. Yosefu
12. Benjamini

Nani aliwatoa Waisraeli MIsri na Kuwaongoza Katika nchi ya Ahadi?
Musa ndiye aliwatoa Waisraeli MIsri na Kuwaongoza Katika nchi ya Ahadi

Mungu alimpa Musa Amri Kumi wapi?
Mungu alimpa Musa Amri Kumi katika mlima wa Sinai

Vitabu vya Historia katika Biblia ni vipi?
Vitabu vya Historia katika Biblia ni
1. Yoshua
2. Waamuzi
3. Ruthu
4. 1 Samweli
5. 2 Samweli
6. 1 Wafalme
7. 2 Wafalme
8. 1 Mambo ya Nyakati
9. 2 Mambo ya Nyakati
10. Nehemia
11. Ezra
12. Tobiti
13. Yudith
14. Esta
15. 1 Wamakabayo
16. 2 Wamakabayo

Vitabu vya manabii katika Biblia ni vipi?
Vitabu vya Manabii ni
1. Isaya
2. Yeremia
3. Maombolezo
4. Baruku
5. Eekieli
6. Danieli
7. Hosea
8. Yoeli
9. Amosi
10. Obadia
11. Yona
12. Mika
13. Nahumu
14. Habakuki
15. Sefania
16. Hagai
17. Zekaria
18. Malaki

Vitabu vya Hekima Katika Biblia ni Vipi?
Vitabu vya Hekima ni
1. Yobu
2. Zaburi
3. Mithali
4. Mhubiri
5. Wimbo ulio Bora
6. Hekima ya Solomoni
7. Yoshua Bin Sira

Nyaraka za Mitume katika Biblia ni zipi?
Nyaraka za Mitume ni;
1. Waroma
2. 1 Wakorinto
3. 2 Wakorinto
4. Wagalatia
5. Waefeso
6. Wafilipi
7. Wakolosai
8. 1 Wathesalonike
9. 2 Wathesalonike
10. 1 Timotheo
11. 2 Timotheo
12. Tito
13. Filemoni
14. Waebrania
15. Yakobo
16. 1 Petro
17. 2 Petro
18. 1 Yohane
19. 2 Yohane
20. 3 Yohane
21. Yuda

Je, Bikira Maria alikua na watoto wengine Mbali na Yesu?
Je, Bikira Maria ni Bikira Daima au alizaa watoto wengine?
Jibu fupi ni kwamba Bikira Maria hakuzaa watoto wengine na hakuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu
Hapo zamani hakuna mkristu au dehebu lolote lililokuwa linapinga kuwa Bikira Maria sio Bikira Daima hata Waprotestanti/walokole waliamini Bikira Maria ni Bikira Hata Baada ya Kumzaa Yesu. Kwenye Miaka ya 1400-1600 Watu wote wakwanza waliopinga Kanisa Katoliki walikubali kuwa Bikira Maria ni Bikira daima wakiwemo Martin Lutha aliyeanzisha kanisa la Lutheran, John Calvin aliyeanzisha Ulokole/Protestanti, Mchungaji Ulrich Zwingli, Heinrich Bullinger, and Thomas Cranmer. Kwa miaka zaidi ya 350 Waprotestant/walokole waliendelea kuamini kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.
Lakini baadae wakristo wengi walianza kupinga kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.
Tunaweza kuthibitisha kuwa Bikira Maria hakuzaa watoto wengine kwa kunukuu Biblia Kama ifuatavyo;
1. Bikira Maria Alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu
Biblia inatuambia wazi kwamba Bikira Maria alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu Kama tunavyosoma katika Luka 1:26-35
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe.” 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” 34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)
2. Biblia Haiwataji ndugu wa Yesu wakati Yosefu na Maria walipokimbilia Misri kumficha Yesu na wakati waliporudi
19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.” 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.” Matayo 2:19-23
Kama wangekuwepo wadogo zake Yesu Biblia ingetuambia kwamba walikuwa wapi wakati huo na walikuwa na Yesu au la.
3. Biblia haituambii kuwa Yesu alikua na wadogo zake alipokuwa na miaka 12
Wakati wa Maria, Yoseph na Yesu walipoenda Yerusalemu Yesu akiwa na miaka 12 Biblia haituambii kuwa Yesu alikuwa na wadogo zake na walikuwa wapi. Kumbuka walikuwa na Desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka kwa ajili ya Pasaka familia nzima kama familia. Je hao watoto wengine walikuwa wapi. Kwa nini walikuwa na Yesu Mwenyewe? Maana yake ni kwamba Yesu hakuwa na Wadogo zake.
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.” 49 Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
Kwa hiyo Biblia haionyeshi kuwa Yesu alikuwa na kaka na dada wakati akiwa na miaka 12. Kama wangekuwepo wangetajwa hapa kuwa walikuwa pamoja na Wazazi wao kama Yesu au walikuwa na Yesu wakati anapotea. Biblia haituambii chochote kwa hiyo wakati huo hapakuwa na wadogo zake Yesu.
4. Kukosekana kwa neneo “Binamu” kwenye lugha ya Yesu
Wakristu wa kwanza pamoja na Yesu aliongea Kiaramaiki au Kiebrania. Katika lugha zote hizo hakuna neno “Binamu” kwa hiyo mabinamu walijulikana kama dada na kaka wa mtu. Kwenye Agano jipya Neno kaka na Dada lilitumika pia kuwakilisha binamu.
Biblia inapotuambia kuwa Kaka na dada zake Yesu haimaanishi kaka wa kuzaliwa bali ndugu au Binamu
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kwa hiyo wanaotajwa hapa ni ndugu wa Yesu kwa maana maneno kama; ndugu, kaka au dada lilitumika badala ya Binamu yaani mtoto wa shangazi au mjomba. Hapa juu Yosefu ametajwa kama kaka yake Yesu lakini tunajua kuwa Yosefu ni Baba yake Yesu. Baba na mwana hawawezi kuwa na jina sawa.
5. Biblia haitumii neno Ndugu, kaka au dada ikimaanisha ndugu wa kuzaliwa mama mmoja na baba mmoja
Sio mara zote Biblia imetumia neno Ndugu kumaanisha ndugu (Dada na Kaka) wa kuzaliwa yaani kaka na dada kwa mfano
Kwa kuangalia lugha ya Kiswahili na Kiingereza 1 Wakorintho 15:6 tunaona tafsiri tofauti.
KISWAHILI 6 Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa.
ENGLISH 6 After that, he appeared to more than five hundred of the brothers and sisters at the same time, most of whom are still living, though some have fallen asleep.
Kwa hiyo hapa neno kaka dada na ndugu linaonekana wazi halikumaanisha ndugu au kaka wa damu.
6. Undugu wa Yakobo, Simoni, Yosefu na Yuda kwa Yesu Sio wa mtu na kaka zake
Wasemao kuwa Bikira maria alikuwa na wana zaidi ya Yesu wananukuu kifungu hiki;
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kumbuka kulikuwa na Yakobo wawili wakati wa Yesu, Vifungu vifuatavyo yunaweza kuona kuwa kulikuwa na yakobo wawili ambao walikuwa ndugu za Yesu lakini sio kaka wa kuzaliwa kwa mama.
35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)
Tunaweza kuona Undugu huu na Yesu kwa kusoma;
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. (Wagalatia 1:19)
Lakini Yuda anasema;
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. (Yuda 1:1)
Kwa hiyo Yakobo na Yohane walikuwa watoto wa Mama mwingine ambao baba yao ni Zebedayo. Na Yakobo na Yosefu walikuwa watoto wa Maria Mwingine. Kwa hiyo ni Yakobo wa wili wa Mama wengine Tofauti na Maria. Yuda alikuwa ni ndugu yake Yakobo. Yakobo vilevile alikuwa ndugu yake Yesu.
Kuthibitisha kuwa Hawa kina Mama ndio waliokuwa Mama zao kina Yakobo wote hao wawili na wengine tunaweza kusoma;
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. (Yohana 19:25)
Kwa hiyo kwenye (Yohana 19:25) tunaona Kuwa ni kwenye Msalaba wa Yesu alikuwepo Mama yake Yesu (Bikira Maria), Dada yake Bikira Maria, Mke wa Cleopa na Maria Magdalena. Na kwenye (Matayo 27:55-56) wamwtajwa ni Mama za kina nani kama inavyoonekana kwenye kifungu kifuatachi;.
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56).
Kwa hiyo hii ina maanisha kulikua na wanawake watatu wenye majina sawa ya Maria waliokuwa chini ya Msalaba. Yakobo na Yuda walikuwa watoto wa Maria Mke wa Cleofasi, na sio Mama wa Yesu, na hivyo sio kaka za Yesu.
7. Yesu alimwacha Mama yake kwa Yohane kwa kuwa hakuwa na Kaka na dada wakumwachia mamaye
26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: “Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.” 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
Ndiyo maana Bikira Maria tangu siku ile alihamia kwa Yohani kwa kuwa hakuwa na watoto wengine.

Baba wa Yesu Kristo ni nani?
Baba wa Yesu Kristo ni Mungu Mwenyewe

Baba Mlishi wa Yesu Kristu ni nani?
Baba mlishi wa Yesu Kristo ni Yosefu Mtakatifu (Mt 1:18-20)

Yesu Kristu alizaliwa wapi?
Yesu Kristu alizaliwa Bethlehemu pangoni (Lk 2:4-7)

Nini maana ya Jina Bethlehemu?
Bethlehemu maana yake ni
Nyumba ya mkate

Yesu Kristu aliishi wapi kabala ya kuanza kazi yake?
Yesu Kristu Aliishi Nazareti kabla ya kuanza kazi yake

Mtangulizi wa Yesu Kristu ni nan?
Mtangulizi wa Yesu Kristu ni Yohani Mbatizaji

Wazazi wa Yohani Mbatizaji ni nani?
Wazazi wa Yohani Mbatizaji ni Zakaria na Eizabeti

Wazazi wa Bikira Maria ni nani?
Wazazi wa Bikira Maria ni Yoakimu na Anna

Mitume kumi na wawili wa Yesu Kristu ni wapi?
Mitume wa yesu ni;
1. Simoni/Petro
2. Yakobo
3. Yohane
4. Andrea
5. Filipo
6. Barttholomayo
7. Mathayo
8. Thomaso
9. Yakobo wa ALfayo
10. Thadayo (Yuda Thadey)
11. Simoni Mkanaani
13. Yuda Iskarioti – Aliyemsaliti

Baba Mtakatifu wa kwanza ni nani?
Baba Mtakatifu wa Kwanza ni Mt. Petro

Nani ni Mitume wa Mataifa?
Mitume wa mataifa ni Paulo na Barnaba

Nani ni shahidi wa kwanza katika Agano Jipya?
Shahidi wa Kwanza ni Mt Stefano

Yesu Alianza kuhubiri injili kwa maneno gani?
“Wakati umetimia na ufalme wa Mungu umekaribia, tubuni na kuiamini Injili” (Mk 1:15)

Yesu alitukomboa kwa hatua zipi?
Yesu alitukomboa kwa Hatua Mbili (2) ambazo ni;
1. Mafundisho yake
2. Mateso, Kifo na Ufufuko wake

Sentesi saba za Yesu msalabani ni zipi?
Sentesi saba za Yesu Msalabani ni;
1. Baba uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya (Lk 23:34)
2. Nakuambia Hakika leo utakuwa pamojanami Mbinguni (Lk 23:43)
3. Mama huyu ndiye mwanao (Yoh 19:26)
4. Tazama huyu ndiye Mama yako (Yoh 19:27)
5. Eloi, Eloi, lema Sabakthani (Mk. 15:34) Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?
6. Naona kiu (Yoh 19:28)
7. Yametimia (Yoh 19:30)

Kwa hiki kilichonikuta sitadanganya tena kuanzia leo

Juzi nikitoka church nilipanda kihiace na kulikuwa na mrembo mkali hujawahi kuona,kila kijana alikuwa akimtupia macho,so me nilikuwa na wepesi wa kuongea naye kirahisi coz nilikuwa kando yake,,, Sasa kama unavyojuwa wanaume kwa kujikosha Nikaimigine mtto ananiangalia so nikaamuwa kupiga fake phone
“Hello Mr. Supervisor,nitachalewa kidogo coz kuna mahali nitapitia, so nipelekee tu hyo Ferrari yangu nyumbani”

Nikaona mrembo ameniangalia kwa macho ya husda apo nkajua nimeuwa ndege kwa jiwe moja, nkaamua kujikosha mtt wa kiume , “niaje mrembo”, akanikazia macho kisha akaniambia,
“Shika battery yako uliangusha ukitoa simu”

Icho kicheko watu walicheka hujawahi ona jooo adi ikabidi dereva aegeshe gari watu wacheke kwanza 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Nikaona isiwe tabu nikashukia pale pale🚶🏿🚶🏿🚶🏿

Tujifunze kusema ukweli kwani uongo sio mzuri hata kwa Mungu… 🙏🙏🙏🙏🙏

Utani wa wachaga

Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja. Kuna:-

1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”. Wanawake wa Rombo ni mama Huruma, wanaachia tu.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji.

2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu.

3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchinja… wengi wanamiliki mabucha. Wana hasira sana na ni wakatili.. Akikuchoma kisu, siku ya mazishi anakuja kudai kisu chake.

4. WAMACHAME; hawa ni wezi sana, ukifanya nae dili umeliwa. Ni wasiri sana lakini wako makini mno hasa kwenye pesa. Wakiwa na hasira hawaoneshi waziwazi, so Mmachame anaweza kukuua huku akitabasamu. Sio waaminifu sana lakini wanaenda kanisani mara nyingi zaidi kuliko Wachaga wote. Wanawake wa machame wanaitwa ‘Wapalestina’.. Mume ukitajirika mkeo anakuua ili arithi mali.

5. WAURU; hawa hupenda kusoma sana lakini hawapendi maendeleo kabisa. Hadi leo eneo lao la Kishumundu linatumika ku-identify wachagga washamba. Wanawake wakifikisha umri wa miaka 40 hua wehu na wanaume huwa vichaa mapema zaidi. Wanaume ni wavivu, lakini wanawake ni wachapakazi hodari. Wanazurura mjini na mabeseni wakiuza ndizi mbivu.. Ukioa Uru jiandae kulea kichaa.

6. WASIHA; Kwanza hawapendi kuitwa Wachagga. Wanajiita watu wa West-Kilimanjaro. Ni mchanganyiko wa Wachagga na WaMeru. Hawapendi shule ila wanapenda zaidi kazi za ufundi na kilimo. Viazi vingi vya Chips Arusha na Moshi vinatoka kwao. Wanawake zao wana “vigimbi” mguuni sababu ya kulima mno.!

7. WAKIRUA; wanapenda sifa kama Wahaya. Wanawake wa Kirua ni wachawi kupindukia.. Wanaloga hata jiwe ili tu alikomoe.. Wanaume wa Kirua hawapendi kuoa kwao.. Hawapendi kuishi mjini maana wanaogopa gharama.. lakini siku wakija mjini wawili tu utadhani wako mia.

8. WA OLD-MOSHI; Hawa ni mafundi stadi wa ujenzi wa nyumba, japo hawajengi kwao. Mpaka leo hamna daladala ya kwenda Old-Moshi inayoanzia Moshi mjini, maana ni wabishi kulipa nauli na pesa inaishia kwenye mbege njiani. Wanaume wamezoea kutoka nyumbani saa kumi na moja alfajiri na kurudi saa sita ya usiku kwa miguu.!

Wachaga mnisamehe!
🏃🏃🏃🏃✋✋

Jinsi ya kupika Biryani ya mbogamboga

Biriani ni miongoni mwa vyakula ambavyo ni nadra sana kupikwa katika familia nyingi tofauti na vyakula vingine. Inawezekana ni kutokana na watu wengi kutoelewa namna ya kuoika chakula hiki kutokana na kuhitaji viungo vingi ambavyo huwapa usumbufu wapishi.
Kuna aina mbalimbali za upishi wa biriani ambapo mara nyingi hutofautiana kutokana na viungo vinavyotumika katika upishi.
Biriani la mbogamboga ni miongoni mwa aina hizo za upishi. Chakula hiki kinaweza kuliwa na kila mtu hususan wale wasiotumia nyama wala samaki.

Mahitaji:

½ kg mchele wa basmati
Kitunguu maji kikubwa 1
Nyanya 1 kubwa
Karoti 1 kubwa
Njegere robo kikombe
Kiazi ulaya 1 kikubwa
Tangawizi za kusaga kijiko 1
Kitunguu swaumu cha kusaga kijiko 1
Karafuu kijiko 1
Majani ya kotimili fungu 1
Maziwa ya mtingi ¼ kikombe
Chumvi na pilipili kiasi
Unga wa dhani kijiko 1 cha mezani
Juisi ya limao kijiko 1 cha mezani
Mafua ¼ lita

Maandalizi:

Chemsha mchele na kisha weka pembeni
Osha mbogamboga zote isipokuwa vitunguu na nyanya
Changanya mtindi na tangawizi pamoja na kitunguu swaumu viache vikae kwa muda wa saa moja
Chukua sufuria weka mafuta na kisha kaanga vitunguu maji, weka nyanya, chumvi, kotimili na limao halafu weka karafuu na kanga hadi vichanganyike vizuri
Miminia mchanganyiko wa mtindi na baadaye weka pilipili na baadaye weka unga wa dhania
Chukua mchele uliochemshwa changanya na mchanganyiko huo
Palia moto juu ya chakula chako na acha kwa muda wa dakika 30
Baada ya hapo chakula chako cha biriani kitakuwa tayari kwa kuliwa

Mapishi ya Maini ya ng’ombe

Mahitaji

Maini (Cow liver) 1/4 kilo
Vitunguu (chopped onion) 2
Nyanya (chopped tomato) 1
Kitunguu swaum/tangawizi (ginger /garlic paste) 1 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia
Chumvi
Coriander
Curry powder 1 kijiko cha chai
Limao (lemon) 1/4
Pilipili (scotch bonnet ) 1

Matayarisho

Safisha maini na ukate vipande vidogovidogo na uweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu kidogo(visiwe vya brown) kisha tia ginger/ garlic paste,carry powder kaanga kidogo kisha tia nyanya. Kaanga nyanya mpaka zitoe mafuta kisha tia chumvi, pilipili na vimaji kidogo. Acha vichemke kidogo kisha tia maini na uyapike mpaka yaive. Malizia kwa kukamulia limao na kutia coriander kisha ipua na hapo yatakuwa tayari kwa kuliwa.

Vyakula vinavyosaidia macho kuongeza uwezo wa kuona

Je unakula chakula bora ambacho ni bora pia kwa ajili ya macho yako? Kula vizuri kuna manufaa mengi kwa ajili ya miili yetu; macho nayo yakiwemo. Kuna virutubisho mbalimbali vinavyohitajika kwenye macho kuliko tu vile vinavyofahamika na wengi vilivyoko kwenye karoti.

Jifunze ni vyakula gani vitayapa macho yako na kuyawezesha kupata virutubisho ambavyo vitayalinda dhidi ya kupungua kwa uwezo wa kuona.

Mboga za majani

Watu wengi hufikiri kuwa kula mboga za majani ni umaskini; lakini ukweli ni kuwa mboga za majani zina manufaa makubwa kwenye miili yetu. Mboga za majani zina kemikali ya luteini na zeaxanthini ambazo ni muhimu katika kulinda na kujenga uwezo wa macho kuona vizuri.

Mayai

Mayai yana manufaa kwa ajili ya afya ya macho na miili yetu kwani yamejaa vitamini. Vitamini A inayopatikana kwenye mayai hulinda macho dhidi ya kutokuona usiku pamoja na kukauka kwa macho (macho angavu).

Samaki

Samaki ni chakula bora kwa afya ya macho hasa wale wa maji baridi, kwani wamejaa asidi ya mafuta ya omega-3 ambayo ni muhimu kwa ajili ya kuzuia macho angavu (kunyauka kwa macho), kudhoofu kwa misuli ya macho na hata mtoto wa jicho. Kama umeshindwa kula vyakula hivi vya baharini unaweza kula matunda kama vile matunda damu ili kupata asidi ya mafuta ya omega-3.

Matunda jamii ya mchungwa na zabibu

Matunda kama vile malimao, machenza, machungwa na zabibu yamesheheni vitamini C. Hivyo yatakuwezesha macho yako kujikinga na magonjwa kama vile mtoto wa jicho pamoja na kudhoofu kwa misuli ya macho.

Karanga na jamii zake

Vyakula hivi vimejaa mafuta ya omega-3 na vitamini E ambavyo ni muhimu kwa ajili ya afya ya macho.

Vyakula vya jamii ya kunde

Vyakula vya jamii ya kunde vina kemikali kama vile Bioflavonoidi na Zinki ambavo ni muhimu kwa ajili ya ulinzi wa retina na kuzuia kudhoofu kwa misuli ya jicho.

Alizeti

Ulaji wa mbegu za alizeti utakuwezesha kupata madini ya zinki pamoja na vitamini E ambayo ni muhimu kwa ajili ya macho yako.

Matunda ya rangirangi

Chakula kama karoti, nyanya, pilipili hoho, boga na mahindi ni vyanzo bora vya vitamini A na C. Inaaminika kuwa kemikali ya carotenoids inayoyapa matunda haya rangi zake ni muhimu kwa afya ya macho. Ikumbukwe pia vitamini C na A zina manufaa kadha wa kadha kama tulivyoona kwenye hoja zilizopita.

Nyama ya ng’ombe

Nyama imejaa madini ya zinki ambayo huuwezesha mwili kufyonza vitamini A ambayo ni muhimu kwa macho pia. Ikumbukwe kuwa vitamini A huuwezesha mwili kukabiliana na matatizo yatokanayo na umri au uzee.

Kwa hakika maradhi mengi humpata mwanadamu kutokana na kuharibu au kuacha mfumo wa ulaji wa asili. Ni kweli kuwa matunda na mboga vina manufaa makubwa kwa ajili ya macho yetu pamoja na mwili mzima kwa ujumla. Jitahidi kufanya angalau nusu ya mlo wako uwe ni matunda na mboga. Usisahau pia kumwona daktari mara kwa mara ili kupima afya ya macho yako pamoja na kupata ushauri wa kitabibu.

Faida ya kunywa maji yenye limao au ndimu kila siku

Watalam mbalimbali wa afya wanasema ya kwamba kwa kila siku ni vyema unywe maji ya ndimu ili uweze kujitibu magonjwa yafuatayo;

Unachotakiwa kufanya ni;
Weka maji yenye joto kidogo (vuguvugu) katika glasi au kikombe , kata limao au ndimu vipande viwili na kamua kipande kimoja tu ndani ya glasi yenye maji.

Kunywa na uanze siku mpya. Ni vizuri ukafanya hivi dakika 30 kabla ya kula chochote kingine kwa faida zaidi.

Anza leo kwa kunywa maji yenye ndimu kila siku asubuhi na uone mabadiliko ndani ya mwili wako. Mshirikishe mwenzio ili naye afaidike.

1. Huchochea Mmeng’enyo wa Chakula Tumboni

Maji yenye ndimu husaidia chakula kusagika vizuri na haraka katika mfumo wa chakula. Japo limao lina asidi(acid) lakini likiwa tumboni huwa alkali (alkaline) na kufanya mazingira mazuri kwa usagaji wa chakula.

Pia maji ya uvuguvugu husaidia kusawazisha utumbo uliojikunja na kutoa mawimbi tumboni na kufanya chakula kusukumwa vizuri.

2. Huboresha Kinga za Mwili

Vitamini C na potasiumu iliyomo kwa wingi katika limao inasaidia katika utengenezaji wa seli za kinga katika mwili.

3. Husaidia Kinga Dhidi ya Saratani

Vitamini C ni antioksidant (antioxidant) ambayo inasaidia kuondoa free radicalsmwilini ambazo zimetambulika kusababisha saratani (cancer).

Usafishaji wa Mwili na DamuLimao husaidia kusafisha damu kwa kuondoa uchafu. Limao pia husafisha figo ,ini na mfumo wa chakula.

4. Kurekebisha Sukari katika Mwili

Limao husaidia kuweka kiasi cha sukari tumboni na katika mwili kuwa katika kiasi stahili.
Hii inawasaidia sana wagonjwa wa kisukari katika ulaji wao.

5. Dawa ya Kikohozi na Mafua

Limao ikitiwa katika maji ya uvuguvugu na asali husaidia sana katika kutibu mafua na kikohozi kwa njia ya asili.

6. Inasaidia Urekebishaji wa Ngozi na Kupona Makovu

Limao inasaidia kufanya ngozi isizeeke. Kama unataka kubaki kijana basi limao litakusaidia. Tabia za vitamin C za kusafisha uchafu zinasababisha kufanya ngozi kuwa na afya na kutozeeka haraka.

7. Husaidia Kupungua Uzito

Limao hupunguza hamu ya kula. Na inajulikana kuwa sababu kubwa ya watu kuwa na uzito mkubwa ni kula chakula kingi au kula mara kwa mara. Limao litakufanya ujisikie kushiba muda mrefu hivyo kusaidia wale amabao wanataka kupungua uzito.

8. Kuondoa Harufu ya Mdomo

Limao husaidia kuua bakteria wabaya mdomoni ambao husababisha harufu mbaya.


Madhara ya kunywa pombe wakati wa ujauzito

Kuacha Matumizi ya pombe wakati wa ujauzito ni moja ya njia ya kuzuia kupata matatizo ya kuzaliwa nayo na udhaifu kwa mtoto. Pia kuna matatizo kadhaa yanaweza kutokea kwa kichaga kutokana na matumizi ya pombe wakati wa ujauzito.

Madhara haya ya pombe huweza kuwa ya kujitambua tabia na madhara madhara ya mkusanyiko wa dalili na viashiria kwa mtoto vinavyoitwa fetal alcohol syndrome-FAS. Kutokana na shirika madhara ya pombe yanayoambatana na dalili na viashiria fulani yanaongezeka sana. Pombe imekuwa ikituiwa vibaya sana wakati wa ujauzito ukilinganisha na madawa mengine.

Dalili za mtoto ambaye mama alikuwa akitumia pombe kwa kiasi kikubwa;

  1. Kutokuwa vema kabla na baada ya kuzaliwa
  2. Mtindio wa ubongo
  3. Udhaifu wa kuzaliwa wa kichwa na uso
  4. Magonjwa ya moyo
  5. Tabia zisizoeleweka
  6. Matatizo ya mfumo wa fahamu

Kiasi gani cha pombe ni salama kwenye ujauzito?

Hakuna kiwango salama cha matumizi ya pombe kwenye ujauzito kilichotambuliwa. Kwa usalama ni kutofikiri kutumia pombe wakati wa ujauzito.

Je kuna uhusiano wa kiwango cha pombe na matokea mabaya ya ujauzito?

Hakuna. Miongozi mwa wanawake waliokunywa ounce 5 ya pombe kwa kila siku, 1/3 ya watoto walikuwa na FAS, 1/3 walionesha madhara sumu kabla ya kujifungua, na 1/3 waliobaki walikuwa kawaida. Kundi jingine lililotumia ounce 1-2 kila siku asilimia 10 ya watoto walikuwa na dalili za FAS. Hata kiwango kidogo cha pombe kimekuwa kikisababisha FAS!. Matumizi ya pombe kwa kiasi kidogo bado yamekuwa yakihusika kusababisha mtoto kuwa na IQ kidogo na matatizo ya kujifunza kwa watoto wenye anatomia ya kawaida.

Je pombe husafilishwa kwenye kondo la mtoto?

Kemikali ya ethyl iliyo kwenye Pombe hupita kwenye kondo na kuingia kwa kwenye mzunguko wa damu wa mtoto. Kiwango cha pombe kwenye damu ya mama huwa sawa na kile kwenye damu ya kichanga tumboni.

Je mama aliyekuwa teja wa pombe anatakiwa aache kunywa pombe?

Mama aliyekuwa teja wa pombe anatakiwa apewe msaada wa wataalamu ili kusaidiwa kuacha pombe, madhara a kujifungua kabla ya mda huongezeka kwa watumiaji wa pombe

Dalili za kuacha pombe ghafla zinaonekana wakati gani wa ujauzito?

Dalili za kukatisha kutumia pombe huanza kuonekana upesi pale mtu anapoacha kutumia pombe, Mara nyingi ndani ya masaa 4 hadi 12. Hata hivyo inawezekana dalili za kukatika kutumia pombe kuonekana siku chache baadae. Mtu asipopata tiba hufikia kilele cha dalili ndani ya masaa 48 na huweza kuendelea kufikia miezi 3 hadi 6 na huwa na dalili kiasi kuliko awali. Dalili na viashiria ni kutetemeka, wasiwasi, mapigo ya moyo kwenda kasi, shinikizo la damu la juu, kutokwa jasho, kichefuchefu, kukosa usingizi na hutegemea utegemezi wa pombe na hali ya mgonjwa.

Mara ujauzito unapotambuliwa kuacha kutumia ama kupunguza husaidia kuondoa madhara kwa mtoto?

Kemikali ya ethyl na ethanol iliyo kwenye pombe hupitaka kwenye kondo la nyuma na kuingia kwenye damu na ubongo wa mtoto. Inafikilika kwamba madhara hutokana na sumu iliyo kwenye pombe na mazao ya uchakataji wa pombe mwilini. Kuacha au kupunguza kutumia pombe mara ujauzito unapotambuliwa huweza kupunguza matatizo ya kuzaliwa kwa mtoto hata hivyo kuna uwezekano kwamba inaweza hili lisitokee. Hivyo tafiti zaidi zinatakiwa kufanyika ili kuonyesha usahihi wa jambo hili.

Maswali na Majibu kuhusu Kifo

Motoni ni nini?

Motoni ni makao mabaya kwa Shetani walaaniwa wakaapo mbali na Mungu wakiteswa milele. (Mt 25:41, Mik 9:42-43, 1Yoh 14:15)


Uzima wa milele ni nini?

Uzima wa milele ni maisha ya kukaa mbinguni na Mungu yasiyokua na mwisho.


Mambo makuu manne ya mwisho ni yapi?

Mambo hayo ni;
1. Kifo
2. Hukumu
3. Jehanamu (Motoni)
4. Paradiso. (Toharani/Mbinguni)


Je, ni muhimu tujiandae kufa?

Ndiyo, ni muhimu tujiandae kufa wakati wowote na namna yoyote kwa kuishi kitakatifu sasa na kwa kujiombea neema tutakazohitaji saa ya kufa kwetu, tukijua tumewekewa “kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu” (Eb 9:27).
“Katika mambo yako yote uukumbuke mwisho wako, hivyo hutakosa kamwe hata hatima” (YbS 7:36).
“Hamjui yatakayokuwako kesho! Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka” (Yak 4:14).
“Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni” (Math 26:41).


Je, ina thamani machoni pa Bwana mauti ya mtu aliyemcha?

Ndiyo, “ina thamani machoni pa Bwana mauti ya wacha Mungu wake” (Zab 116:15).
Hasa utiifu wa Yesu msalabani umegeuza laana ya kifo iwe baraka kwa waamini wake.
“Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao” (Ufu 14:13).


Tutakapofariki dunia itatutokea nini?

Tutakapofariki dunia roho yetu isiyokufa, mbali na mwili unaooza, itapewa tuzo au adhabu tuliyostahili kwa maisha yetu. “Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake” (Lk 16:22-23). “Kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida… ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo, maana ni vizuri zaidi sana” (Fil 1:21,23). “Nasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana” (2Kor 5:8). Kwa kuwa kifo ni “mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa” (Mhu 12:7). Siku ya ufufuo roho na mwili vitaungana tena kwa ajili ya uzima au moto wa milele. “Pumzi iliwaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno” (Ez 37:10).

Je baada ya kufa ni hapo hapo roho inaenda motoni au mbinguni, Au ni mpaka Siku ya hukumu Yesu Atakaporudi?

Ni siku ile ile Roho ya mtu aliyekufa inaenda Mbinguni, toharani au Motoni. Yesu alimwahidi yule mtu waliyesulubiwa pamoja kuwa watakuwa peponi pamoja siku hiyo hiyo na sio siku ya hukumu.
“Kisha akasema, “Ee Yesu! Unikumbuke wakati utakapoingia katika ufalme wako.” 43 Yesu akamwambia, “Nakwambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja nami peponi.” (Luka 23:42-43)
Sauli aliweza kuongea na Samweli hata baada ya kufa na Samweli alimbashiria mambo yatakayotokea kwa Sauli maanake ni kwamba Japokuwa alikuwa amekufa bado anayomuungano na Mungu ndio maana aliweza kumwambia Sauli mambo yatakayompata,
“7Basi Sauli akawaambia watumishi wake, “Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi ili nimwendee nipate kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, “Yuko mwanamke mmoja huko Endori.” 8Hivyo Sauli akajigeuza kwa kuvaa mavazi mengine, naye usiku akiwa amefuatana na watu wawili wakaenda kwa huyo mwanamke. Akamwambia, “Nibashirie na unipandishie huyo nitakayekutajia,” 9Huyo mwanamke akamwambia, “Wewe unajua lile alilofanya mfalme Sauli. Amewakatilia mbali wapunga pepo, wapiga ramli wote na wachawi katika nchi. Mbona umenitegea maisha yangu ili wapate kuniua?” 10Sauli akamwapia huyo mwananmke kwa Jina la BWANA, akasema, “Kwa hakika kama BWANA aishivyo, hutaadhibiwa kwa ajili ya jambo hili.” 11Ndipo yule mwanamke akauliza, “Je unataka nikupandishie nani? Sauli akasema, “Nipandishie Samweli.” 12Yule mwanamke alipomwona Samweli alipiga yowe kwa sauti kuu, naye akamwuliza Sauli, “Mbona umenidanganya? Wewe ndiwe Sauli.” 13Mfalme akamwambia, “Usiogope. Unaona nini? Yule mwanamke akasema, “Naona Mungu anapanda kutoka ardhini.” 14Sauli akamwuliza, “Ni mfano wa nini?” Yule mwanamke akasema, “Ni mwanaume mzee amevaa joho anayepanda.” Ndipo Sauli akatambua kwamba ni Samweli. Sauli akasujudu kifudifudi uso wake hadi ardhini. 15Samweli akamwuliza Sauli, Kwa nini unanitaabisha, kunipandisha juu?” Sauli akasema, “Mimi ninasumbuka sana, kwa maana Wafilisti wanapigana vita dhidi yangu, naye Mungu ameniacha. Hanijibu tena wala kwa njia ya manabii wala kwa ndoto. Kwa hiyo nimekuita wewe ili unijulishe lakufanya.” 16Samweli akamwuliza, “Kwa nini uniulize mimi, maadam BWANA amekuacha na kuwa adui yako? 17BWANA ametenda lile alilotangulia kusema kwa kupitia kwangu. BWANA ameurarua ufalme kutoka mikononi mwako, naye amempa mmoja wa jirani zako, yaani, Daudi. 18Kwa sababu wewe hukumtii BWANA, wala hukumtimizia ghadhabu yake kali juu ya Waamaleki, BWANA amekutendea mambo haya leo. 19Zaidi ya hayo, BWANA atawatia Israeli pamoja na wewe mkononi mwa Wafilisti na kesho wewe na wanao mtakuwa pamoja nami. BWANA pia atalitia jeshi la Israeli mkononi mwa Wafilisti.
Mfano Wa Tajiri Na Maskini Lazaro Yesu alisimulia hivi
19 Akasema, “Palikuwa na tajiri mmoja aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, nguo za gharama kubwa, kila siku. 20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, mwenye vidonda mwili mzima, alikuwa akiletwa mlangoni kwa huyo tajiri kila siku. 21 Lazaro alikuwa akitamani kula makombo yaliyodondoka mezani kwa tajiri. Hata mbwa walikuwa wakiramba vidonda vyake. 22 “Hatimaye, yule maskini alikufa. Malaika wakamchukua akakae pamoja na Ibrahimu mbinguni. Yule tajiri naye pia akafa, akazikwa. 23 Alipokuwa kuzimuni ambapo alikuwa akiteseka, alita zama juu, akamwona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro karibu yake. 24 Akaita, ‘Baba Ibrahimu, nionee huruma umtume Lazaro achovye japo ncha ya kidole chake katika maji aupoze ulimi wangu maana ninateseka kwenye moto huu.’ 25 Lakini Ibrahimu akamjibu, ‘Mwa nangu, kumbuka kwamba ulipokuwa hai ulipata kila kitu kizuri uli chotaka, ambapo Lazaro alipokea mabaya. Lakini sasa anafarijika hapa na wewe unateseka. 26 Isitoshe, kati yetu na ninyi huko, kumewekwa bonde kubwa lisilopitika ili wale wanaotaka kutoka huku kuja huko au kutoka huko kuja huku wasiweze.’ 27 Akasema, ‘Basi, baba, tafadhali umtume Lazaro aende nyumbani kwa baba yangu, 28 awaonye ndugu zangu, wasije wao pia wakaletwa mahali hapa pa mateso watakapokufa.’ 29 Ibrahimu akamjibu, ‘Ndugu zako wanazo sheria za Musa na maandiko ya Manabii. Itawapasa watii hayo.’ Lakini yule tajiri akazidi kumsihi, 30 ‘Hapana baba Ibrahimu, ndugu zangu hawatashawishiwa na hayo. Lakini mtu kutoka kuzimu akitumwa kwao watatubu na kuziacha dhambi zao.’ 31 “Ibrahimu akamwambia, ‘Wasiposikiliza na kutii sheria za Musa na Maandiko ya manabii, hawatashawishika kutubu hata kama mtu akifufuka kutoka kuzimu.”’ (Luka 16:19-31)
Wakati Yesu anabadilika Sura walitokea Musa na Eliya.
“Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane nduguye, akaenda nao peke yao juu ya mlima mrefu. 2 Huko, wakiwa wanamtazama, akageuka sura, uso wake ukang’aa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama nuru. 3 Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza naye. 4 Hapo Petro akamwambia Yesu, “Bwana, ni vizuri sana kwamba tupo hapa! Ukipenda nitajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Eliya.” (Mathayo 17:1-5)
Yesu alituambia kuwa Mungu sio wa wafu bali wa walio hai ndio maana akaitwa Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo kwa kuwa Wote wako hai kwake.
37Hata Mose alidhihirisha kuwa wafu wanafufuka, kwa habari ya kile kichaka kilichokuwa kikiwaka moto bila keteketea, alipomwita Bwana ‘Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki na Mungu wa Yakobo.’ 38Yeye Mungu si Mungu wa wafu bali wa walio hai, kwa kuwa Kwake wote ni hai.” (Luka 20:37-38)
Yesu alimwahidi yule mtu waliyesulubiwa pamoja kuwa watakuwa peponi pamoja siku hiyo hiyo na sio siku ya hukumu.
“Kisha akasema, “Ee Yesu! Unikumbuke wakati utakapoingia katika ufalme wako.” 43 Yesu akamwambia, “Nakwambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja nami peponi.” (Luka 23:42-43)
Angalia pia wakati Stefano akipigwa Mawe aliikabidhi roho yake kwa Mungu baada ya kuona mbingu zimefunguka hii ni kama Yesu alivyokuwa pale msalabani aliikabidhi Roho yake kwa Baba yake.
55Lakini yeye Stefano akiwa amejazwa Roho Mtakatifu, alikaza macho mbinguni, akaona utukufu wa Mungu, naye Yesu akiwa amesimama mkono wa kuume wa Mungu. 56Akasema, “Tazameni! Naona mbingu zimefunguka na Mwana wa Adamu amesimama upande wa kuume wa Mungu.’’ 57Lakini wao wakapiga kelele kwa sauti kubwa, wakaziba masikio yao, wakamrukia kwa nia moja. 58Wakamtupa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi wakaweka nguo zao miguuni mwa kijana mmoja aitwae Sauli. 59Walipokuwa wakimpiga mawe, Stefano aliomba, “Bwana Yesu, pokea roho yangu” 60Kisha akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa akasema, “Bwana usiwahesabie dhambi hii.’’ Baada ya kusema haya, akalala. (Mdo 7:55-60)
Kwenye Ufunuo tunasoma (Ufunuo 6:9-10) “Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao.”
Kwa hiyo mtu akifa anaenda mbinguni au motoni kulingana na alivyoishi.
“Nasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana” (2Kor 5:8). Kwa kuwa kifo ni “mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa” (Mhu 12:7).
Siku ya ufufuo roho na mwili vitaungana tena kwa ajili ya uzima au moto wa milele.
“Kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida… ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo, maana ni vizuri zaidi sana” (Fil 1:21,23).
Mtume Petro ameandika hivi…
“18 Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa,19 ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri; 20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.” (1Petro 3:18-20)


Je, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu?

Ndiyo, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu: hapa duniani katika mwanga hafifu wa imani, na kisha kufa katika uangavu wa utukufu usiofifia kamwe. Kwa kuwa lengo la Baba ni kwamba tuungane na Yesu Mwanae kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ili tuwe na utukufu wake.
“Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yoh 17:3).
“Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa” (2Pet 1:3-4).
Sisi tuliobatizwa tunaitwa “wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo!” (1Yoh. 3:1).
Kwa sababu tumesadiki kwamba “Mungu ni upendo” (1Yoh 4:8) na kwamba “hakuna lisilowezekana kwa Bwana” (Lk 1:37).
“Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, ‘Aba!’ yaani, ‘Baba!’ Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu” (Gal 4:6-7).


Aliyezungumzia moto wa milele ni nani?

Aliyezungumzia moto wa milele ni hasa Yesu: akitufunulia ukuu wa upendo wa Mungu, aliye heri yetu pekee, alituangalisha juu ya hatari ya kutengana naye milele kwa dhambi. Mwenyewe atatoa hukumu hiyo:
“Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake” (Math 25:41).
“Humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki” (Mk 9:48).
“Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku” (Ufu 14:11).


Toharani maana yake nini?

Toharani maana yake kuna hali ya muda ambayo huruma ya Mungu inawatakasa marehemu waliofariki dunia katika urafiki naye lakini bila ya usafi kamili unaotakiwa kwa kuingia mbinguni. Sisi tunaweza kuharakisha utakaso wao kwa kumtolea Mungu sala na sadaka, hasa ekaristi. Yuda Mmakabayo “alichanga fedha kwa kila mtu jumla drakma elfu mbili, akazipeleka Yerusalemu kutoa sadaka ya dhambi.
Kwa kufanya hivi alitenda vema na kwa haki, kwa kuwa aliukumbuka ufufuo wa wafu. Maana kama asingalitumaini ya kuwa wale waliokufa watafufuka, ingalikuwa kazi bure isiyo na maana kuwaombea wafu. Lakini kwa kuwa aliufikiri utukufu wa thawabu waliowekewa wale wafao katika utauwa, wazo lake lilikuwa takatifu na la kicho. Ndiyo sababu alifanya upatanisho kwa wafu ili wafunguliwe dhambi zao” (2Mak 12:43-46). Imani hiyohiyo iliongoza Wakristo wa kwanza kuwafanyia marehemu ibada ambayo haieleweki vizuri, lakini hailaumiwi na Mtume Paulo: “Kama wafu hawafufuliwi kamwe, kwa nini kubatizwa kwa ajili yao?” (1Kor 15:29).


Je, mwili utakaofufuliwa ni huuhuu tulionao sasa?

Ndiyo, mwili utakaofufuliwa ni huuhuu tulionao sasa, lakini katika hali tofauti: > “hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika” (1Kor 15:42).
Siku ya ufufuo “ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi” (Lk 21:27).
“Saa yaja ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuko wa uzima, na waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu” (Yoh 5:28-29).
“Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele” (Math 25:46).


Siku ya ufufuo Kristo mfalme atatuhukumu vipi?

Siku ya ufufuo Kristo mfalme atatuhukumu kwa kudhihirisha misimamo ya watu wote ambao, kwa kupokea au kukataa upendo wa Mungu moyoni mwao, wametenda mema au la.
“Imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyopenda, kwamba ni mema au mabaya” (2Kor 5:10).
“Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu” (1Kor 4:5).
“Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake. Na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, ‘Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia… Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi’” (Math 25:31-36,40).
“Heri wenye rehema, maana hao watapata rehema” (Math 5:7).


Baada ya hukumu ya mwisho itakuwaje?

Baada ya hukumu ya mwisho, waadilifu watatukuzwa mwili na roho pamoja na Yesu, na ulimwengu pia utageuzwa.
“Kama ilivyo ahadi yake, tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake” (2Pet 3:13).
“Na Roho na Bibi arusi wasema, ‘Njoo!’ naye asikiaye na aseme, ‘Njoo!’… Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, ‘Naam, naja upesi’. Amina. Na uje, Bwana Yesu! Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi nyote. Amina” (Ufu 22:17,20-21).

Uzinzi na Uasherati ndio mtego wa kizazi hiki

Uzinzi na uasherati wakati huu umekuwa ndio sumaku kuu ya kuwanasa watu ili waende jehanamu.

Sumaki hii imewanasa hata ambao hawakutegemewa wala kutarajiwa.

Uzinzi uzinzi uzinzi umekuwa kama perfume ya kujipulizia kila Mara mtu akipenda.

Uasherati umekuwa kama heshima ya kibinadamu kwa vijana wengi.

Mbingu zimenyamaza kwa sababu iko jehanamu inawangoja wazinzi na waasherati.

Dhambi hii imekuwa sumaku kubwa ya shetani ya kukamata wanadamu ili waende jehanamu.

Wanadamu wa Leo ukimwambia kwamba aache uzinifu maana wazinzi na waasherati hawataenda uzima wa milele, mtu huyo anakuambia unamhukumu.

Ni Neno la MUNGU ndile limesema katika maandiko mengi tu kwamba wazinzi na waasherati sehemu yako itakuwa katika ziwa la moto.

Hata makanisani baadhi ya watu wamenasa kwenye sumaku hii.

Dada mmoja ambaye kila wiki anasimama na kushika mic kanisani kwao siku moja aliniambia kwamba hawezi kumaliza wiki bila kufanya ngono, na hajaolewa. Niliumia sana rohoni nikamwambia aache kutumika madhabahuni, yeye akasema itakuaje maana yeye ndiye tegemeo.

Mama mmoja alisema yeye ana mume mema sana na mume wake ni mwaminifu sana katika ndoa yao lakini yeye huyo mama ndio hutoka nje ya ndoa Mara kwa Mara, ni hatari inayohitaji neema ya MUNGU tu ili kutubu na kuacha.

Mama mmoja yeye ana watoto zaidi ya wawili na yuko katika ndoa lakini hana uhakika kama watoto wale ni wa mume wake wa ndoa, ni hatari sana.

Baba mmoja akiwa ndani ya ndoa amezaa watoto zaidi ya watatu nje ya ndoa tena wanawake zaidi ya wanne(4) tofauti tofauti.

Mwanaume moja ambaye husimama madhabahuni yeye kila Mara humdanganya mkewe kwamba anaenda safari kumbe ana mahawara karibia kila mkoa, ni hatari sana.

Watu wengi sasa wanaona uzinzi na uasherati ndio fashion nzuri ya wakati kuu.

Kila kijana ana girlfriend kwa lengo la ngono tu na sio vinginevyo.

Kila binti ana boyfriend kwa ajili ya uasherati.

Ukitaka watu wakuchukie basi kemea uzinzi na uasherati.

Watu wengi wamekuwa vipofu wa kiroho kwa sababu ya uzinzi na uasherati.

Lakini upo mwisho mmoja kwa watenda dhambi wote ambayo ni jehanamu.

Ndugu unahitaji kutubu Leo na kuacha dhambi.

Ndugu mmoja akasema yeye anaishi maisha matakatifu ila dhambi moja tu yaani uzinifu ndio imemshinda, hiyo ni hatari.

Leo hata ndoa takatifu zimeadimika maana wahusika huanza kwanza uzinzi na uasherati ndio baadae ndoa, ndugu mnahitaji kutubu.

Ndugu yangu unayenisikiliza kwa njia ya ujumbe huu nakuomba tubu na acha dhambi hiyo.

Amua kuiacha.

Mwisho wa uzinzi na uasherati ni kifo(Mauti) na baada ya kifo ni hukumu(Waebrania 10:27)

Nimekuonya wewe Leo ili ukishupasa shingo usije ukalaumu siku ile ukiwa katikati ya bahari ya moto huku kifo kimezuiliwa ili uteseke milele.

Mimi naamini utatengeneza ndugu baada ya kuusoma ujumbe huu.

Mimi naamini utaachana na mahawara na kuanza kuiheshimu ndoa yako.

Mimi naamini hutamsaliti tena mkeo/Mumeo.

Mimi naamini utaachana na huyo girlfriend/Boyfriend, wengine wanao zaidi ya mmoja, nakuomba ndugu achana nao.

Kijana au binti kaa tulia hadi wakati wako wa ndoa.

Uliyenisikia na utatubu na kuacha dhambi hiyo, MUNGU akubariki sana.“`

ALIYE NA AKILI AWEKE MOYONI MANENO HAYA. AMINA

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About