EMBU SOMA HII KWA MAKINI SJUI NI KWELI? USIMAINDI LAKINI MAANA ITAKUGUSA TUU. MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI
βπ½Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa.
ππΎKatika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa “darasa la sabaβ au wale ambao hawakuingia darasani kabisa
ππ½π Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi π‘ na π πmagari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!)
ππΎWapo ππ½πwasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana
ππΎLakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga
Hii inachangiwa na mambo mawili:-
ππ½
I. Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli
ππΎHata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio
ππΎKadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa!
ππ½πWasomi wengi kwa sababu ya “mentality” ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika
ππΎ
II. Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!
ππΎKatika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha.
βπΎHuwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na “mentality” ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!
οΏ½Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninakwambia: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani
π£Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti
πUkitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze
πππ½ Hii habari haitaki hasira, vumilia tu na jiongeze
β¦.hata mimi sijawa tajiri badoππππππΏβ¦ But nakaza mwendo Bila kuangalia vipingamizi au ugumu wa safariβ¦
Recent Comments