Funga huzuni upate furaha,
Funga ulabu upate siha,
Funga majivuno upata utukufu,
Funga uzinzi upate wongofu,
Funga kisirani upate utakatifu,
Funga wivu upata baraka,
Funga unafiki upate uchaji,
Funga kinyongo upate faraja,
Funga kwaresima wakati ni huu
Funga jeuri ujawe rehema,
Funga hofu ujazwe imani,
Funga kinywani ujazwe moyoni,
Funga kisirani ujazwe rohoni,
Funga dharau ujazwe heshima,
Funga majungu, ujazwe neema,
Funga usiri ujawe wafuasi,
Funga tamaa ujazwe kiasi,
Funga kwaresima wakati ni huu.