Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Padri Akimbia wakati wa kuungamisha, chanzo ni hiki

Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
“Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sana.”
Padri, “Endeleaโ€ฆ”

“Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia
amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema
nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa
kufungwa.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu,nikatoa bastola nikamuuaโ€ฆ.. Yesu atanisamehe?”

Padri: “Utasamehewa.”
“Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango
unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona
kilichotokea akasema anapiga polisi simu.
Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuua na yeye piaโ€ฆ Yesu atanisamehe hilo?”
Padri: “Utasamehewa.”

Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi
akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa
bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuuaโ€ฆ.. Yesu atanisamehe?”
Padri:”Utasamehewa.”

“Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda
nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi
akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi
nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya
babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye
wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua?
Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.

Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke
yetu, nikamuuaโ€ฆ.. Yesu atanisamehe na hilo?”

Kimyaaโ€ฆ.
“Padri yesu atanisamehe?”
kimyaโ€ฆ.

Jamaa akatazama kwenye confession booth padri
hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo
za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.

Jamaa, “Sasa baba mbona umekimbia?”
Padri kwa taabu akajibu, “Nilitazama huku na huku
nikagundua tuko wawili peke yetuโ€ฆโ€ฆ.”

Mlevi kazua tafrani, angalia alichokifanya hapa

MLEVI mmoja aliingia baa akavuta kiti na kukaa mhudumu akatokea kumsikiliza.
MHUDUMU: Nikusaidie nini?
MLEVI: Eeh! nipe bia ya baridi kisaha wasikilize wote waliokaa hapa, wape bia na wao maana sipendi kunywa pombe wengine wananiangalia
Akaja mhudumu wa jikoni “nikusaidie nini?”

MLEVI: Niletee supu kisha wasikilize wote waliokaa hapa na wao wape supu sipendi kunywa supu watu wananiangalia
Safari hii watu wakapiga makofi
Baadae akamuita mhudumu
MLEVI: Niandikie bili zangu kisha waandikie wote bili zao sipendi kulipa huku watu wananiangalia

Wale wateja wakamvaa na kumshushia kichapoโ€ฆ teh teh teh teh teh hii kali hakuna cha bure mjini hahahaha na jasho la mtu haliliwi wandugu

Nifunge nini Kwaresma? Mambo ya kufunga kipindi cha Kwaresima

NIFUNGE NINI?
Fungaย huzuniย upateย furaha,
Fungaย ulabuย upateย siha,
Fungaย majivunoย upataย utukufu,
Fungaย uzinziย upateย wongofu,
Fungaย kisiraniย upateย utakatifu,
Fungaย umbeaย upateย fanaka,
Fungaย wivuย upataย baraka,
Fungaย unafikiย upateย uchaji,
Fungaย kinyongoย upateย faraja,
Fungaย kwaresimaย wakati ni huu
Fungaย kiburiย ujazweย hekima,
Fungaย jeuriย ujaweย rehema,
Fungaย hofuย ujazweย imani,
Fungaย kinywaniย ujazweย moyoni,
Fungaย kisiraniย ujazweย rohoni,
Fungaย dharauย ujazweย heshima,
Fungaย majungu,ย ujazweย neema,
Fungaย usiriย ujaweย wafuasi,
Fungaย tamaaย ujazweย kiasi,
Fungaย kwaresima wakati ni huu.

Matumizi ya Papai Katika Urembo

Tunda la kitropiki la papai lina vitamini C na E likiwa na siri kubwa ya urembo na hutumika kutengeneza facial za aina mbalimbali.
Papai limekuwa likitumiwa kama njoia boya ya kutunza uso wako na kumfanya mtu kuwa na ngozi ya asili.

Bidhaa ambazo zimekuwa zikitengenezwa kwa kutumia tunda la papai ni pamoja na sabuni, lotion, tona, moisturiza, facial peels na nyingine nyingi.

Ukitumia facial mask ya papai utakuwa na sura nzuri ya asili na kukupa uonekanaji mzuri wa uso wako. Facial mask hii huweza hutumika kwa watu wa umri na aina yoyote ya ngozi.

Facial mask ya papai ina nguvu ya kungโ€™arisha uso wako.
Pia inasaidia ngozi ambayo imeshaanza kupatwa na makunyanzi kutokana na umri kuonekana ya kuvutia kwani pia imekuwa ikiondoa chunusi na makunyanzi pia.

Ni rahisi kutengeneza facial mask ya papai na ukitumia itakusaidia katika kukabiliana na ngozi iliyoanza kuchoka, kungโ€™arisha ngozi.

Kuna na njia nzuri za kuhakikisha kuwa, tunakuwa na nyuso nzuri zenye kupendeza na kuvutia ikiwemo kutumia vitu vya asili pamoja na matunda ya aina mbalim ambayo husaidia zaidi katika kuimarisha ngozi.

Mask ya mchanganyiko wa papai yai na yai ni nzuri katika kuhakikisha kuwa unakuwa na ngozi nzuri na nyororo.

Njia hii pia husaidia hata wale wenye nyuso za mafuta ambao wamekuwa wakisumbuliwa na chunusi mara kwa mara kwa kufanya ngozi kuwa kavu.

Unaweza kutengeneza aina hii ya mask kwa kufanya yafuatayo:-
Chukua papai likate kasha toa mbegu na kasha lisage kwa kutumia blenda ya kuondaponda kwenye kibakuli kwa kutumia kitukama mchi mdogo wa kinu.

Kisha weka mchanganyiko huo kwenye chombo ulichokichagua kama kikombe au bakuli.
Vunja yai na koroga kuhakikisha kuwa mchanganyiko huo umechanganyika vizuri.
Safisha uso wako kwa kutumia cleanser au maji ya vuguvugu na uondoeuchafu wote ulioganda usoni.

  • Kisha paka mask kuzunguka uso wako, na unapopaka hakikisha kuwa,
  • mchanganyiko huo haugusi macho yako.
  • Osha uso wako baada ya dakika 15 kwa kutumia maji ya vuguvugu.
  • Jifute kwa kutumia taulo safi
  • Unaweza kupaka losheni, tona au moisturiza.

Husaidia kutunza ngozi na kuondoa vipele na uchafu ulioganda usoni.
Hii ni njia rahisi ya kutengeneza uso isiyo na gharama.

Jinsi ya kupika Biskuti Za Kuchoveya Chokoleti

Viambaupishi

Unga 300gm

Siagi 225gm

Icing Sugar 60gm

Chokoleti iliyokoza (Dark Chocolate) 225gm

Vanilla 2 kijiko cha chai

Yai 1

Baking Powder ยฝ kijiko cha chai

Njugu za vipande ยฝ kikombe cha chai

Njugu zilizosagwa ยผ kikombe cha chai

Jinsi ya kuandaa na kupika

1. Piga sukari na siagi katika mashine ya keki mpaka iwe laini

2. Kisha mimina yai na vanilla koroga vizuri

3. Mwisho mimina unga na baking powder polepole mpaka ichanganyike.

4. Kata kata umbo (shape) lolote unavyopenda (kama nyota, pembetatu,duara, kopa n.k)

5. Panga kwenye treya na choma kwa moto wa 350ยฐC , vikibadilika rangi kidogo tu vitoe

6. Yayusha chokoleti tia kwenye bakuli ndogo.

7. kisha paka kwa kijiko au chovyea upande mmoja mmoja wa biskuti kisha nyunyizia njugu za kipande na njugu ya unga.

8. Panga kwenye sahani tiyari kunywewa na chai ya maziwa au kahawa.

Cheki huyu jamaa alivyoumbuka kwenye harusi

Jamaa mmoja alialikwa ktk harusi. Akafika mlango Wa 1 umeandikwa kulia ni ndugu Wa maharusi, kushoto ni wageni waalikwa, akaenda kushoto maana yy alialikwa. Akakuta mlango wa2 umeandikwa kulia wenye zawadi kushoto wasionazawadi yy hakuwa na zawadi. Mlango Wa 3 umeandikwa kulia wanawake kushoto waume akapita kushoto akajikuta ametokea mtaani

๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„. Tujifunze kutoa wandugu

*hatupendagi ujinga sisi*
๐Ÿšถ๐Ÿฟ๐Ÿšถ๐Ÿฟ๐Ÿšถ๐Ÿฟ๐Ÿšถ๐Ÿฟ๐Ÿšถ๐Ÿฟ๐Ÿšถ๐Ÿฟ๐Ÿšถ๐Ÿฟ

Uhusiano uliopo kati ya pesa na muda

Bila shaka upo uhusiano mkubwa kati ya pesa na muda..

-Ndio maana nauli ya ndege ni kubwa kuliko ya basi, why..?

Kwa sababu ndege hutumia mda mchache (mf. Ukitoka dar kwenda moshi ni dk45 tu kwa ndege bt kwa gari ni takriban masaa 7-8)

Linapokuja suala la MUDA NA PESA, duniani kuna makundi manne ya watuโ€ฆ!

1. wapo wenye muda wa kutosha Lkn hawana pesa mf watu wasio na kazi maalum au wa kijiweni(ukimwambia akusindikize mahali yuko tayari muda wowote)

2. wapo wenye pesa lakini hawana muda. Unaweza kumualika ktk harusi akaacha kuja lakini akakuchangia hela ya maana tu.. hili ni kundi la madirector na mameneja wa vitengo muhimu ktk makampuni (ndio hawa JPM amewataka walipwe sio zaidi ya 15mil kwa sasa)

3. wapo wasio na PESA wala MUDA.. takwimu zinaonyesha kuwa hawa ni 95% ya watu wote ulimwenguni. Hili ni kundi la wafanyakazi na vibarua ( unaweza ukamualika ktk shughuli yako na akakosa nafasi lakini pia hana hela ya kukuchangia)
Yaani mtu yuko busy 24/7 bt ukimwomba hata elfu 50,000/= hana..Why..?

Mtu huyo unakuta ana mshahara mdogo halafu ana mikopo mingi mf kakopa nyumba, gari, mtaji wa biashara ambapo kutokana na kukosa usimamizi makini napo hakuna pesa, hivyo neno MAREJESHO ndio msamiati mkuu kwao.

4 wapo watu wana PESA na MUDA wakutosha..

Ndio matajiri au watu waliofanikiwa sana. Why..?
Hawa wameandaa mfumo ambao hata wasipokuwepo pesa inaingia (mf Mengi au Bakhresa akienda likizo hata miezi mitatu bado akirudi biashara znaendelea vizuri)

Hapa unakuta yeye ndio CEO na pengine asbh yuko anawaandaa na anawapeleka wanae shule huku mm na ww ndio tunakomaa na mafoleni tukielekea kufanya kazi za kujenga ndoto za hao watu kwa masaa mengi na tunalipwa kidogo..

-Wapo watu wanasema, usipoitengeneza FUTURE yako mtu mwingine atakutengenezea kadiri atakavyoona inakufaa
AU
usipojenga ndoto zako kuna mtu atakuchukua(kukuajiri) ukajenge ndoto zakeโ€ฆ!

JE WEWE UPO KUNDI GANI?

WASWAHILI HUSEMA, USIPOJIPANGA UTAPANGWA..๐Ÿ™ˆ

Amka na Tafakari sana. MCHANA MWEMAโ€ฆโ€ฆ.

Jinsi ya kupika Roast ya biringanya na mayai

Mara nyingi biringanya hutumika kama kiungo cha nyongeza katika mchuzi. Hata hivyo, kiungo hiki kinaweza kupikwa chenyewe na kutoa mchuzi wenye ladha ya kipekee.

Baadhi ya wapishi wameweza kubuni aina hii ya upishi ambayo huweza kupikwa kwa dakika tano tu na kukupa chakula kitamu chenye ladha ya kuvutia.

Uzuri wa chakula hi ni kwamba kinaweza kuliwa wakati wowote na kwa chakula chochote kulingana na matakwa ya mlaji.

Kwa mujibu wa wataalamu wa maswala ya mapishi, biringanya ni miongoni mwa vyakula vyenye mapishi mengi kama ilivyo kwa mchele.
Hapa tutaenda kuona jinsi ya kupika roast ya biringanya na mayai.

Mahitaji:

Biringanya 2 kubwa
Nyanya 4 kubwa
Kitunguu maji kilichosagwa kijiko 1 cha mezani
Mayai 2
Mafuta ya mzeituni vijiko vitatu vya mezani
Chumvi kiasi
Pilipili 1 (kama unatumia)
Hoho 1
Karoti 1
Kitunguu swaumu kilichosagwa 1
Kotimili fungu 1

Maadalizi:

Chukua biringanya ioshe vizuri na kasha katakata vipande vidogo vidogo.
Osha na menya nyanya hapafu katakata. Fanya hivyo kw akaroti na hoho pia.
Weka mafuta kwenye sufuria na weka jikoni kwenye moto kiasi
Yakishachemka maji na kasha weka kitunguu maji na kasha swaumu huku ukikaanga taratibu.
Weka hoho na karoti huku ukiendelea kukaanga. Baada ya hapo weka nyanya na baadae chumvi. Funika hadi ziive kabisa na kasha weka majani ya kotimili.
Weka biringanya. Acha vichemke hadi viive. Koroga ili kuruhusu mchanganyiko wako uchanganyike vizuri.
Kwa kuwa biringanya ina majimaji huhitaji kuweka maji ya ziada, weka pilipili.
Acha kwa muda wa dakika tatu hadi dakika tano. Pasua mayai na kisha miminia huku ukikoroga taratibu. Fanya hivyo hadi yaive kabisa na kuwa mchuzi mzito. Roast yako ya biringanya iko tayari kwa kuliwa
Unaweza kula aina hii ya mboga na mikate, maandazi na hata ugali

Angalia binadamu walivyo

Angalia Binadamu walivyo!,

“Ukitafuta sana anakuita MCHAWI,”

Ukifanikiwa sio BURE,

“Ukitulia MVIVU,”,

Usipovaa vizuri MCHAFU,

Ukidili sana na masomo unajifanya MSOMI,

Usipodili nayo MJINGA,

Ukisema sana MBEA,

Ukiwa mkimya JEURI,

Ukiwasaidia watu UNATAKA SIFA,

Usipowasaidia ROHO MBAYA,

Ukiwa na kazi UNAJISIKIA,

Usipokua nayo MZEMBE.

Hivyo BINADAMU ndivyo walivyo wewe jali MAISHA YAKO TU NA MAENDELEO YAKO.

MUNGU akulinde na shari zao.

Raha ya kuoa mke ambaye hajasoma

Ukioa mke asiyesoma hata hili unaweza kufanya

KUOA MKE AMBAE HAJASOMA RAHA SANA LEO NIMEMUAMBIA MWEZI HUU HATUTOLIPWA MSHAHARA KWAKUA HAUNA TR 30 KAENDA KUNGALIA KARENDA KARUDI ANANIAMBIA HAMNA SHIDA MME WANGU TUTAVUMILIA TU

๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ

๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚

Mambo ya Muhimu kufahamu kuhusu Mungu

Je, Yatupasa kumtolea Mungu shukrani?

Ndiyo, Yatupasa kumtolea Mungu shukrani kila wakati hasa kwa kuadhimisha Ekaristi Takatifu

Nani ameumba vitu vyote?

Mungu ameumba vitu vyote

Mungu ni nani?

Mungu ndiye muumba wa kila kitu katika uwingu na nchi, Mkubwa wa ulimwengu mwenye kuwatuza watu wema na kuwaadhibu watu wabaya.
“8Msiwe kama wao, kwa sababu Baba yenu anajua kile mnachohitaji kabla hamjamwomba.โ€™โ€™ 9โ€˜โ€˜Hivi basi, ndivyo iwapasavyo kuomba : โ€œBaba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe.(Mt. 6:8-9).
17Yesu akamwambia, โ€˜โ€˜Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, โ€˜Ninapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu ambaye ni Mungu wenu.โ€™ โ€™โ€™ย (Yoh 20:17)

Mungu ni Muumba vyote maana yake ni nini?

Mungu ni Muumba vyote Maana yake amefanya vitu vyote kwa kutaka tu pasipo kutumia chochote. (2Wamakabayo 7:28, Yoh 1:3)

Mungu ni nini?

Mungu ni Roho kamili na ukamilifu wake hauna mipaka. (Yoh. 4:24, Kut.3:13-15, Zb. 144:3)

Mungu ni Roho maana yake ni nini?

Mungu ni Roho maana yake haonekani wala hashikiki. (Lk: 24:39)

Mungu ni mweza wa yote maana yake ni nini?

Mungu ni mweza wa yote maana yake kila atakalo hufanya. (Zab 135:6)

Mungu ni wa Milele maana yake ni nini?

Mungu ni wa Milele maana yake hana mwanzo wala mwisho, amekuwapo kabla ya nyakati, yupo na atakuwapo baada ya nyakati, yupo daima. (1Tim, 1:17)

Mungu ni mwema maana yake ni nini?

Mungu ni mwema maana yake apenda na kuvitunza viumbe vyake vyote hasa wanadamu na anawatakia mema tu. (Zab, 25:8-10)

Mungu ni Mwenye haki maana yake ni nini?

Mungu ni Mwenye haki maana yake kila mtu hupata kwa Mungu haki yake kadiri anavyostahili

Mungu aenea pote maaana yake ni nini?

Mungu aenea pote maaana yake yupo kila mahali mbinguni na duniani wala hakuna mahali asipokuwepo?. (Zab, 139:7-12)

Mungu ajua yote maana yake nini?

Mungu ajua yote maana yake ajua ya sasa, ya zamani na ya wakati ujao hata mawazo yetu

Mungu ni mwenye huruma maana yake nini?

Mungu ni mwenye huruma maana yake anawasamehe watu dhambi zao wakitubu.

Mungu ni mwenye subira maana yake ni nini?

Mungu ni mwenye subira maana yake mara nyingi akawia kuwaadhibu wakosefu maana ataka kuwapa nafasi ya kuongoka. (Eze, 33:11, Zb, 102;1-5)

Mungu wako wangapi?

Mungu yupo mmoja tuu Mkubwa wa wote na Baba wa wote. (Is: 44:6)

Katika Mungu mmoja kuna nafsi ngapi?

Katika Mungu mmoja kuna nafsi tatu nazo ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; nafsi zote ni sawa.

Neno hili kuwa nafsi tatu kwa Mungu mmoja laitwaje?

Laitwa fumbo la Utatu Mtakatifu. (Lk, 3:21-22)

Kwa ajili gani Mwana wa Mungu (Yesu) alijifanya mtu?

Mwana wa Mungu (Yesu) alijifanya mtu kwa ajili yetu wanadamu na wokovu wetu ili atupatanishe na Mungu na kutushirikisha tabia ya umungu. (2Pet, 1:4)

Nafasi ya Heshima kwa Bikira Maria ni ipi?

Nafasi ya Heshima kwa Bikira Maria inafuata baada ya Heshima kwa Utatu Mtakatifu

Tunaanzaje kumjua Mungu?

Tunaanza kumjua Mungu kwa kuzingatia viumbe vyake, hasa dhamiri yetu.
โ€œKwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wakeโ€ (Rom 1:20).

Je, tunaweza kusema juu ya Mungu?

Ndiyo, tunaweza kusema juu ya Mungu kuanzia wema, ukweli na uzuri wa viumbe vyake na kumsifu kiasi chetu kwamba ndiye wema, ukweli na uzuri wenyewe.
Lakini tukiri pia kuwa maneno yetu duni hayawezi kutosha kamwe kufafanua fumbo lake.
โ€œKwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajuaโ€ (Ayu 42:3).
Tungemuelewa, asingekuwa Mungu.

Mwenyezi Mungu yukoje basi?

Mwenyezi Mungu ni ukamilifu mtupu usio na mipaka kwa milele yote.
โ€œTazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui; hesabu ya miaka yake haitafutikiโ€ (Ayu 36:26).
โ€œMungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweliโ€ (Yoh 4:24).

Mungu akiwa Roho, viungo ambavyo pengine anapewa vina maana gani?

Mungu akiwa Roho, viungo ambavyo pengine anapewa vinamaanisha tu sifa fulani: k.mf. macho ujuzi wake, mikono uwezo wake, mabawa ulinzi wake, n.k. โ€œRoho haina mwili na mifupaโ€ (Lk 24:39).

Je, Mungu amewasiliana nasi?

Ndiyo, Mungu amewasiliana nasi, akijitambulisha na kujitoa kwetu, tuweze kuishi katika urafiki naye na hatimaye tushiriki heri yake.
โ€œNikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota ulizoziratibisha; mtu ni kitu gani hata umkumbuke, na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; umemvika taji ya utukufu na heshimaโ€ (Zab 8:3-5).
โ€œSiwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki, kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifuโ€ (Yoh 15:15).

Hasa Mungu amejifunua kuwa nani?

Hasa Mungu amejifunua kuwa upendo wenyewe.
โ€œBwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweliโ€ (Kut 34:6).
โ€œMungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yakeโ€ (1Yoh 4:16).
โ€œYeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendoโ€ (1Yoh 4:8).

Je, Mungu amejitambulisha pia kwa jina?

Ndiyo, Mungu amejitambulisha pia kwa majina mbalimbali. Katika Agano la Kale jina muhimu kuliko yote liliandikwa โ€œYHWHโ€ yaani, โ€œMimi Ndimiโ€. Tangu zamani Wayahudi hawalitamki, hivyo wakilifikia wanasoma kwa kutafsiri, โ€œBwanaโ€.
Ndiyo sababu katika Agano Jipya halitumiki kamwe, isipokuwa Yesu alifunua Umungu wake kwa kujisemea, โ€œMimi Ndimiโ€ na kwa kukubali kuitwa, โ€œBwanaโ€. Pamoja na hayo, alisali na kufundisha kusali kwa kumuelekea โ€œABAโ€ yaani, โ€œBabaโ€. Ndilo jina ambalo linampendeza zaidi na kutuingiza katika fumbo lake kama wana ndani ya Mwana pekee ambaye โ€œMungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Babaโ€ (Fil 2:9-11).
โ€œMsalipo, semeni, โ€˜Baba, jina lako litakasweโ€™โ€ (Lk 11:2).
โ€œMlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, โ€˜Aba!โ€™ yaani, โ€˜Baba!โ€™โ€ (Rom 8:15).

Mungu ametufunulia nini?

Mungu ametufunulia pia ukweli juu yetu wenyewe akijibu kabisa maswali yanayotusumbua kuhusu maana na lengo la maisha yetu.
Amefanya hivyo kwa maneno na matendo yanayoshikamana sana kwa kuwa maneno yanafafanua matendo, nayo matendo yanathibitisha maneno.
โ€œMungu hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweliโ€ (1Tim 2:4).
โ€œMungu si mtu, aseme uongoโ€ (Hes 23:19).
Yeye hadanganyiki wala hadanganyi.

Mungu akiwa wema mkuu na mwenye uwezo wote, mbona katika viumbe vyake kuna ubaya? Kwa nini Mungu anaruhusu mabaya na maovu?

Kwa nini dhambi zipo?

Mungu akiwa wema mkuu na mwenye uwezo wote, hakuumba ubaya wowote. Tena kila anapovumilia ule uliosababishwa na viumbe vyenye hiari anaufanya uzae mema makubwa zaidi kwa njia tusizoweza kuzifahamu vizuri hapa duniani.
โ€œMimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri. Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watuโ€ฆ Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leoโ€ (Mwa 45:4-5; 50:20).

Mungu aliwahi kujifunua kwa watu gani?

Mungu aliwahi kujifunua kwa wazazi wetu wa kwanza, akaendelea hasa kwa taifa la Israeli, hadi alipomtuma Mwanae ajifanye mtu wa taifa hilo teule.
โ€œMungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwanaโ€ (Eb 1:1-2).

Je, ufunuo wa Mungu unaendelea hata leo?

Hapana, ufunuo wa Mungu hauendelei, kwa sababu alikwisha kuukamilisha kwa kumtuma duniani Neno wake wa milele.
โ€œKwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunuaโ€ (Yoh 1:17-18).
Baada yake hauwezekani ufunuo mpya. Hatutakiwi kumuamini yeyote akidai eti, ametumwa kukamilisha kazi ya Yesu; kwa kuwa mwenyewe alisema,
โ€œMbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamweโ€ (Math 24:35).
โ€œIjapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe! Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe!โ€ (Gal 1:8-9).

Ufunuo wa Mungu unatufikiaje miaka elfu mbili baada ya Kristo?

Ufunuo wa Mungu unatufikia kupitia Kanisa lake, lililokabidhiwa Mapokeo ya Mitume na linaloongozwa na Roho Mtakatifu hadi ukweli wote.
Yesu aliahidi kwamba,
โ€œYeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yakeโ€ (Yoh 16:13).
โ€œMaana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Munguโ€ (1Kor 2:10).

Je, Mungu amegawanyika sehemu tatu?

Hapana, Mungu hagawanyiki hata kidogo, bali daima ni Umoja kamili.
โ€œBwana Mungu wetu ni Bwana mmojaโ€ (Mk 12:29).
Tumuabudu yeye peke yake katika nafsi tatu, na Utatu wa nafsi katika Umoja wa hali yake, tusichanganye nafsi wala kugawa Umungu. Baba si Mwana wala Roho Mtakatifu. Mwana si Baba wala Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu si Baba wala Mwana. Lakini milele yote nafsi hizo tatu ni Mungu yuleyule pasipo tofauti ya kuzitenganisha: kila moja imo ndani ya nyingine.
โ€œMimi na Baba tu umojaโ€ (Yoh 10:30).

Tumejuaje kuwa Mungu ni Umoja wa nafsi tatu?

Tumejua kuwa Mungu ni Umoja wa nafsi tatu kwa sababu Baba aliwatuma kwetu Mwanae na Roho Mtakatifu.
โ€œYesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake. Na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, โ€˜Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa nayeโ€™โ€ (Math 3:16-17).
Naye akaagiza, โ€œBasi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifuโ€ (Math 28:19).
Ni nafsi tatu zenye jina moja, yaani Umungu mmoja tu.

Umoja wa Mungu unategemea nini?

Umoja wa Mungu unategemea hasa kwamba Mwana na Roho Mtakatifu wanachanga Umungu wa Baba, ambaye wanatokana naye pasipo utengano wowote. Baba anajifahamu na kujipenda: wazo analojifahamu ndiye Mwana, upendo anaojipenda katika wazo hilo ndiye Roho Mtakatifu.
โ€œBaba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwenguโ€ (Yoh 17:24).

Je, nafsi tatu za Mungu zina Umoja hata katika utendaji?

Ndiyo, nafsi tatu za Mungu zina Umoja hata katika utendaji, kila nafsi akiuchangia kulingana na sifa yake maalumu ndani ya Utatu. Baba Mwenyezi sifa yake ni Uwezo. Mwana kama Neno la Baba sifa yake ni Hekima. Roho kama Pumzi ya uhai ya Baba sifa yake ni Upendo.
Katika Uwezo wake Baba anafanya yote kwa Hekima na Upendo, hasa katika utume wa Mwana aliyefanyika mtu na katika utume wa Roho kama paji.
โ€œAmin, amin, nawaambia: Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vilevileโ€ (Yoh 5:19).

Mungu angeweza kuzuia watu wasitende dhambi?

Ndiyo, Mungu angeweza kuzuia watu wasitende dhambi, lakini aliwaacha watende kwa hiari yao awaonyeshe ukuu wa huruma yake.
โ€œMaana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu woteโ€ (Rom 11:32).

Yesu ni Mungu au mtu?

Yesu ni Mungu na mtu kwa pamoja, ndiyo sababu ni mshenga pekee kati ya Mungu na watu. โ€œKwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, mwanadamu Kristo Yesuโ€ (1Tim 2:5). โ€œKatika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwiliโ€ (Kol 2:9). Hivyo ni Mungu kweli na mtu kweli.

1 Hapo mwanzo, kabla ya kuwapo kitu kingine cho chote, aliku wapo Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo Neno amekuwa na Mungu. 3 Vitu vyote viliumbwa na yeye, wala hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho hakukiumba. 4 Uzima ulikuwa ndani yake na uzima huo ndio ulikuwa nuru ya watu. 5 Nuru hiyo huangaza gizani na giza haliwezi kamwe kuizima.
6 Mtu mmoja aitwaye Yohana alitumwa na Mungu 7 awaambie watu kuhusu hiyo nuru, ili kwa ushuhuda wake wapate kuamini. 8 Yohana mwenyewe hakuwa ile nuru. Yeye alitumwa kuishuhudia hiyo nuru. 9 Nuru halisi ambayo inawaangazia watu wote ilikuwa inakuja ulim wenguni. 10 Neno alikuwepo ulimwenguni, lakini japokuwa aliumba ulimwengu, watu wa ulimwengu hawakumtambua! 11 Alikuja nyumbani kwake, lakini watu wake hawakumpokea! 12 Bali wote waliompokea na kumwamini aliwapa haki ya kufanywa watoto wa Mungu. 13 Hawa hawakuwa watoto wa Mungu kwa kuzaliwa kwa njia ya asili, wala kwa mapenzi au mipango ya watu bali wamezaliwa na Mungu mwenyewe.
14 Neno akawa mwanadamu akaishi kati yetu akiwa amejaa utu kufu na kweli. Tuliona utukufu wake, utukufu wa Mwana pekee wa Baba. 15 Yohana alishuhudia habari zake, akatangaza: โ€œHuyu ndiye yule niliyewaambia kuwa, โ€˜Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi kwa kuwa alikuwapo kabla sijazaliwa.โ€โ€™ 16 Na kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema tele. 17 Musa alitule tea sheria kutoka kwa Mungu, lakini Yesu Kristo ametuletea neema na kweli. 18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Lakini Mwanae pekee, ambaye ana uhusiano wa karibu sana na Baba yake, amemdhihirisha Mungu kwetu. Yohana 1:1-6:37

5 Tomaso akamwuliza, โ€œBwana, hatujui unakokwenda; tutaijuaje njia?โ€ 6 Yesu akawaam bia, โ€œMimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu. 7 Kama mngekuwa mnajua mimi ni nani, mngemfahamu na Baba yangu. Tangu sasa mnamfahamu Baba yangu na mmemwona.โ€
8 Filipo akamwambia Yesu, โ€œBwana, tuonyeshe Baba yako nasi tutaridhika.โ€ 9 Yesu akamjibu, โ€œFilipo, imekuwaje hunifahamu baada ya mimi kuwa pamoja nanyi muda wote huu? Mtu ye yote ambaye ameniona mimi, amemwona Baba. Sasa inakuwaje unasema, โ€˜Tuonyeshe Babaโ€™? 10 Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba yangu, na Baba yangu yuko ndani yangu? Mambo ninayowaambia siyasemi kwa mamlaka yangu mwenyewe, bali yanatoka kwa Baba yangu ambaye anaishi ndani yangu, na ndiye anayetenda haya yote. Yohane 14:5-10

29 Baba yangu ambaye amenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwatoa hawa kutoka katika mikono yake. 30 Mimi na Baba yangu tu mmoja.โ€
31 Kwa mara nyingine wale Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo. 32 Yesu akawauliza, โ€œNimewaonyesha mambo mengi mazuri kutoka kwa Baba yangu. Kati ya hayo ni lipi linalosababisha mtake kunipiga mawe?โ€ 33 Wao wakamjibu, โ€œTunataka kukupiga mawe si kwa sababu ya mambo mema uliyotenda bali ni kwa kuwa umekufuru. Wewe ni mtu tu lakini unajiita Mungu.โ€ Yohane 10: 29-33

Yesu anapatikana wapi? Yesu anakaa wapi? Yesu Yupo wapi kwa sasa?

Yesu kama Mungu yupo kila mahali, hakuna mahali asipokuwepo. Yesu kama mwanadamu yupo Mbinguni kwa Baba na anakaa nasi duniani katika Maumbo ya Mkate na Divai Katika Ekaristi.


Je, Umungu na utu wa Yesu vinachanganyikana?

Hapana, Umungu na utu wa Yesu vimeunganika katika nafsi moja visichanganyikane, kwa kuwa ndani yake hali hizo mbili zinatenda kila moja ya kwake.
โ€œBasi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, โ€˜Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Munguโ€™โ€ (Mk 15:39).

Je, Mwana wa Mungu tangu atwae mwili ni mtu kamili mwenye akili na utashi wa kibinadamu?

Ndiyo, Mwana wa Mungu tangu atwae mwili ni mtu kamili mwenye akili na utashi wa kibinadamu. Katika umoja wa nafsi yake vipawa hivyo vinatenda kulingana na Umungu anaouchanga na Baba na Roho Mtakatifu milele.
โ€œHayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zakeโ€ (Yoh 14:10).

Kwa nini Maria anastahili kuitwa โ€œMama wa Munguโ€?

Maria anastahili kuitwa โ€œMama wa Munguโ€ kwa sababu Mwana wa milele wa Mungu, ambaye ni Mungu sawa na Baba, alifanyika mtu toka kwake. Akiwa mja mzito alishangiliwa:ย โ€œUmebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa.ย Limenitokeaje neno hili, hataย mama wa Bwanaย wangu anijilie mimi?
โ€ (Lk 1:42-43).

Je, Bikira Maria ni kama Bahasha au chombo cha kumleta Yesu tuu Duniani au anayo thamani zaidi?

Bikira Maria sio kama bahasha au chombo cha kumleta Yesu tuu duniani. Yesu ametokana na Bikira Maria katika ubinadamu wake. Mwili wa Yesu wa kiubinadamu ni sehemu au uzao wa Bikira Maria. Bikira Maria anayo uhusiano wa damu na Yesu Kristu. Ndiyo maana Mungu alimtakasa Bikira Maria Ili atakayezaliwa kutoka kwake awe na yeye mtakatifu.
Mungu alimtakasa Bikira Maria kabla ya Kuamua kuzaliwa kupitia yeye kwa kuwa Mungu ni Mtakatifu. Ubinadamu wa Yesu (MWILI – Nyama na Damu) asili yake ni Bikira Maria.

Kwa nini Yesu alishawishiwa/alijaribiwa na Shetani?

Yesu alishawishiwa na Shetani kwa kuwa ni mtu kweli, akamshinda kwa niaba ya watu wote, akituonyesha namna ya kumtii Mungu moja kwa moja, โ€œhata mauti, naam, mauti ya msalabaโ€ (Fil 2:8).
โ€œKwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye hakiโ€ (Rom 5:19).

Je, Mungu Baba alihusika na sadaka ya Mwanae?

Ndiyo, Mungu Baba alihusika sana na sadaka ya Mwanae, kwa sababu;
โ€œMungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yakeโ€ฆ Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeyeโ€ (2Kor 5:19,21).

Roho Mtakatifu ni nani?

Roho Mtakatifu ni upendo wa Mungu, nafsi ya tatu ya Utatu Mtakatifu, mwenye Umungu mmoja na Baba na Mwana.
โ€œPendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisiโ€ (Rom 5:5).
Ametumwa kwetu atufanyie kazi pasipo kuonekana.
โ€œUpepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Rohoโ€ (Yoh 3:8).
โ€œWote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Munguโ€ (Rom 8:14).

Je, tumuadhimishe Mungu katika Nafsi zake tatu pia?

Ndiyo, tumuadhimishe Mungu katika Nafsi zake tatu pia: Baba kama asili ya umungu na ya uhai wote, Mwana kama Neno wake aliyejifanya mtu atukomboe, tena Roho Mtakatifu kama Upendo wao ambao unawaunganisha na kututakasa.
Pamoja na viumbe vyote tuwaimbie usiku na mchana,ย โ€œMtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja!โ€ (Ufu 4:8).
โ€œMungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweliโ€ (Yoh 4:24).

Hamu kuu ya binadamu ni ipi?

Hamu kuu ya binadamu ni kumwona Mungu

Je, Yatupasa kumwomba Roho Mtakatifu?

Ndiyo, kwani twataka kwake maonyo na msaada. Tusipokuwa na neema yake hatuwezi kutenda jambo jema la kufaa kutuokoa. (Yoh 16:13)

Wazo mbadala kuhusu ajira au kupata kazi

Katika mambo ambayo nadhani nimeshawahi kujidanganya ni kufikiri kwamba nikipata kazi ndiyo utakuwa mwisho wa matatizo yangu na kuwa huru kufanya kila kitu ninacho kitaka.
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
Sasaa baada ya kuipata iyo kazi nimekuja kupata ukweli kwamba kumbe kazi ya kuajiriwa siyo Mwarobaini wa Yale niliyo Nayo kumbe ndiyo safari inaanza na siyo mwisho kama nilivyo dhani.

Kazi Mara nyingi napenda kuifananisha na Ndoa, watu wengi walio nje ya kazi wanataka sana kazi na wakidhani ndiyo itakuwa mwanzo wa mafanikio yao.

Vijana waliopo nje ya mfumo rasmi wa ajira wanatamani waingie huko, lakini kutokana na ukweli kwamba kuna vitu hawavijui katika kazi ya kuajiriwa na ndio maana wanajihisi Wanyonge kwa kuto kuajiriwa.

USHAURI
kwanza tambua kukosa ajira siyo mkosi, wala siyo kwamba huna bahati. Yawezekana kwakukosa kwako ajira ni mlango wa kuwa muajiri. Unachotakiwa usilalamike tafuta fursa hapo ulipo, ndipo pana utajiri.

1. Kama hujaariwa acha kutamani maisha ya watu walio ajiriwa, ikiwezekana sitisha hata kupiga misele kwenye ofisi, zao kugongea maji ya dispenser

Badala yake anza kutafiti kwakina ni kwa namna gani watu ambao hawajaariwa wanaishi mtaani. Kuwa na marafiki wengi zaidi wanao pambana mtaani ili ujue wao wamewezaje.
Tafuta ndege unao fanana nao

2. Usidanganye kwamba ajira ndiyo itajibu matatizo yako yote unajidanganya

Badala yake kama utafanikiwa kupata iyo ajira, hakikisha unaifanya mbegu. Anza kwakuwekeza kwenye miradi ya uzalishaji maana mshahara hauto kutosha kuishi maisha uliyo nayo kwenye akili yako.

Mwisho kabisa Nguvu na imani uliyoweka kwenye ajira iweke hivyo hivyo kwenye shughuli zako binafsi

Maana ya siku ya Jumatano ya Majivu

Utangulizi

Wakati umetimia na ufalme wa Mungu umekaribia, tubuni na kuiamini Injili, (Mk 1:15), haya ndiyo maneno ya kwanza ya Yesu ambayo kadri ya Mwinjili Marko yanafungua kazi ya hadhara ya Yesu, kwa maana hiyo kazi ya Yesu inaanza kwa kuwaandaa watu katika toba ili hatimaye, wapate kuukaribia au kuingia katika ufalme wa Mungu.
Na wakati ndiyo sasa. Wakati ni sasa, Yesu anatuhubiria na Kwaresima imewadia, na ndiyo maana siku ya Jumatano ya majivu, kwa kuitikia mwito wa maneno ya Yesu kanisa linatualika kuingia katika kipindi cha Kwaresma, ambacho ni kipindi cha kujikusanya, kujitayarisha, kijitengeneza na kujikarabati hasa kwa toba, kufunga, kusali na kujitoa sadaka zaidi mambo yanayorutubishwa kwa tafakari ya kina ya Neno la Mungu.

Nini maana ya Jumatano ya majivu?

Jumatano ya majivu ni mwanzo wa kipindi cha kwaresima katika kanisa, Ni mwanzo wa siku arobaini za kutafakari kwa undani fumbo kuu la upendo wa Mungu linalofunuliwa kwa kujitoa kwake na kufa msalabani, kifo cha aibu cha Msalaba ili kuichukua aibu yetu au dhambi zetu.

Kwaresma ni nini?

Kwaresma ni kipindi cha siku 40 cha kujiandaa kuadhimisha Sherehe kuu ya PASAKA yaani kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Tunajiandaa kwa Kufunga Kusali, Kutubu, na Matendo mema.
Mama kanisa anatupatia kipindi hiki ili tuweze kutafakari njia na mienendo yetu na kubadilika kama haimpendezi Mungu
Tunapofunga tunatakiwa kuzuia vilema vyetu na kuviacha kabisa, tunaomba kujaliwa moyo wa toba, tunainua mioyo yetu na tunaomba Mungu atujalie nguvu na tuzo. Haitoshi tu kukiri makosa yetu bali tunahimizwa kuungama na kutubu hayo makosa na kuwa tayari kuanza upya. Kipindi cha Kwaresima huanza tangu Jumatano ya majivu. Mwanzoni mwa kazi yake ya kuhubiri Habari njema Yesu anaanza kwa kusema tubuni na kuiamini Injili โ€“ Mk 1,15. Maneno haya haya tunayasikia/tumeyasikia kila tunapopakwa majivu. Mwaliko huu wa Yesu unatuingiza katika kipindi cha toba โ€“ tubuni na kuiamini Injili. Huu ni mwaliko wa uzima. Ni mwaliko ili tuongoke, tuanze maisha mapya, maisha ya sala, kufunga na kutoa sadaka.

Kwa nini ikaitwa Jumatano ya majivu?

Jina linatokana na desturi ya kumpaka mtu majivu kichwani pamoja na kumtamkia maneno ya kumhimiza afanye toba inavyotakiwa na kipindi hicho cha liturujia kinachoandaa Pasaka.
Kwa kawaida siku ya Jumatano ya majivu unaanza mfungo unaofuata kielelezo cha Yesu kufunga chakula siku arubaini jangwani baada ya kubatizwa na Yohane Mbatizaji na kabla ya kuanza utume wake mwenyewe.

Nini maana ya majivu tunayopaka?

Majivu ni ishara ya majuto, nayo hufanywa visakramenti kwa kubarikiwa na kanisa. Tunapopakwa majivu katika paji la uso hutusaidia kutafakari na kutukumbusha kuwa wanadamu sisi tu mavumbi na mavumbini tutarudi. Hutukumbusha zaidi kuwa maisha ya hapa duniani tunapita na safari yetu itakamilika pale tutakapoungana na Bwana na mwokozi wetu katika ufalme wako.
Angalia; Isaya 61:3, Ester 4:1-3, Yeremia 6:26, Ezekieli 27:30, Mathayo 11:21 na Luka 10:13.

Kwa nini majivu yanapakwa kwenye paji la uso na si vinginevyo?

Ishara yoyote iwekwayo katika paji la uso huonesha umiliki (soma Ufunuo 7:3, Ufunuo 9:4, Ufunuo 14:1, Ezekieli 9:4-6, ). Tunapochorwa ishara ya msalaba katika paji la uso ni ishara kwamba sisi tupo chini yake yeye aliyekufa msalabani kwa ajili yetu.
Hali kadhalika hutukumbusha ishara ya msalaba tuliyochorwa na mafuta matakatifu siku ya ubatizo wetu, hutukumbusha ahadi tuliyoiweka siku hiyo ya ubatizo na kutuita tuishi maisha ya utakatifu

Padri hutamka maneno gani wakati anapaka majivu?

Tunapopakwa majivu Padre husema; Mwanadamu kumbuka u mavumbi na mavumbini utarudi AU Tubuni na kuiamini Injili.

Maneno anayosema padre yana maana gani?

Maneno haya kwa upande mmoja hutukumbusha tunapoelekea, tusisikitike kwamba siku moja tutarudi mavumbini bali tuwe na furaha kwani wakati miili yetu unarudi mavumbini roho zetu zitakwenda kuungana na Mungu Baba mbinguni.
Hivyo maandalizi tunayoalikwa kuyafanaya si maandalizi ya kuelekea mavumbini bali maandalizi ya kuelekeza roho zetu mbinguni. Ndio maana pia twaambiwa tubuni na kuiamini Injili.

Majivu tunayopakwa yanatoka wapi?

Majivu tunayopakwa hutoka katika matawi yaliyotumika katika jumapili ya matawi ya mwaka jana. Majivu haya hubarikiwa na kuwa visakramenti. Hivyo majivu yanapoashiria toba na majuto pia hutukumbusha wema wa Mungu na utayari wake wa kutusamehe.

Kwa nini unatumia matawi ya Jumapili ya Matawi?

Matawi haya yalimkaribisha Yesu Yerusalemu akiwa tayari kufa kwa ajili ya dhambi zetu, yalimpokea mfalme kwa furaha na shangwe kuu. Matawi haya yanapochomwa na sisi kupakwa majivu yetu yanatukumbusha kuwa ni kwa ajili ya dhambi zetu Mungu alimtoa mwanae wa pekee kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu sisi wanaadamu. Hivyo hututafakarisha kuacha dhambi.

Kanisa limekataza nini siku ya Jumatano ya majivu?

Tumekatazwa kula chakula siku ya Jumatano ya Majivu na kula nyama siku ya Ijumaa Kuu katika Amri ya Pili ya Kanisa.

Nani analazima kufunga siku ya Jumatano ya majivu na Kwaresma?

Kila Mkristo aliyetimiza miaka 14 na zaidi anapaswa kufunga kula nyama (Ijumaa kuu) na mwenye miaka zaidi ya 21 kufunga chakula Jumatano ya Majivu

Tunaposema kujinyima wakati wa Kwaresma tunamaana gani?

Kujinyima ni kujikatalia kitu ukipendacho mfano nyama, pombe, sigara, muziki, safari, maongezi n.k.

Mwisho

Wakati wa Kwaresma Waamini wanapaswa kujitakasa zaidi kwa kusali, kufunga, toba na matendo mema
Kipindi cha Kwaresima ni fursa makini ya kumkimbilia Mwenyezi Mungu, kwani kwa njia ya dhambi wamejikuta wakiwa mbali na Uso wa huruma ya Mungu, kiasi hata cha kupoteza imani na matumaini kwa Mwenyezi Mungu. Hii ni changamoto ya kumpenda Mungu na jirani badala ya kukumbatia malimwengu yanayoendelea kuwatumbukiza katika utupu wa maisha ya kiroho. Kwaresima ni kipindi cha waamini kukimbilia na kuambata huruma ya Mungu inayoganga na kuponya dhambi. Ni wakati wa sala, upendo na kufunga.
Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About