Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Angalia huyu ticha wa Hesabu alichofanyiwa

Looku Looku* ๐Ÿ‘€๐Ÿ‘€

*Ama Kweli Mkuki Kwa Nguruwe kwa Binadamu Mchungu Skia Hiiโ€ฆ.!!*

*Ishawahi kutokea Pale nilipokutana njiani na mwalimu aliyekufundisha MATHS secondary afu akaniambia nimuelekeze njia ya kwenda sehemu fulani.*

*_Nenda mbele kama 2KM hivi kisha kata kushoto,ila hakikisha ANGLE inakuwa ni 30.5 KUSINI MASHARIKI.Kisha tumia PYTHAGORAS na hakikisha una FOUR FIGURE ili kupata thamani ya ANGLE._*

*Mwalimu alisonya na kuondoka.*๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜’๐Ÿ˜’

*Stakagi ujinga kabisa mimi, wakati ananichapa alifikiri sifa*๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

๐Ÿ˜…๐Ÿ™Œ๐Ÿฝ๐Ÿ™Œ๐Ÿฝ *Mniache Tuu Mimi Sio Kwa Bifu Ilo Aiseee*๐Ÿƒ๐Ÿพ

Hii ndio ngoma droo kwa wanaume kati ya wanawake

{ NGOMA DROO}
Sikuizi utawasikia wadada wakisema kuachwa na mwanaume asie na pesa nisawa na kuluhusiwa hospital

{Sasa na sisi} wanaume tunasema
Kuachwa na demu mpenda pesa nisawa na kumaliza mkopo benk ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Wanaume atutakagi ujinga!!!! Wanaume heeeeee๐Ÿƒ๐Ÿพโ€โ™‚๐Ÿƒ๐Ÿพโ€โ™‚๐Ÿƒ๐Ÿพโ€โ™‚๐Ÿƒ๐Ÿพโ€โ™‚

Mapishi ya Pilau Ya Nafaka Na Nyama Ya Kusaga

VIAMBAUPISHI

Mchele – 3 vikombe

Nyama ya kusaga – 1 LB

Mchanganyiko wa Nafaka upendazo; maharagwe, njegere, mbaazi n.k 1 mug

Vitunguu maji kata vipande vipande – 3 vya kiasi

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi – 2 vijiko vya supu

Mafuta – ยฝ Kikombe

Mchanganyiko wa bizari (Garam Masala) – 2 vijiko vya chai

Vipande vya supu (Maggi cubes) – 3

Maji (inategemea mchele) – 5

Chumvi – Kiasi

MAPISHI

Osha mchele na roweka.
Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitunguu mpaka viwe brown.
Tia Thomu na tangawizi, kaanga kidogo.
Weka nyama ya kusaga, chumvi na garam masala, endelea kukaanga mpaka nyama iwive.
Mwaga maji yaliomo katika kopo la nafaka na utie nafaka pekee humo.
Tia maji na vipande vya supu (Maggi cubes) huku unavivuruga, koroga kidogo.
Tia mchele, koroga kidogo.
Funika na pika kwa moto mdogo mpaka karibu na kukauka ukikorogoka kidogo. (kama unavyopika pilau ya kawaida)
*Epua uipike katika moto wa oven 350-400 Deg kwa muda wa dakika 15.
*Kama sufuria uliyotumia sio ya kupikia katika oven, mimina katika chombo chochote kinachotumika kwa oven kama bakuli la pyrex au treya za foil.
Pakua katika sahani na iko tayari kuliwa.

MALAIKA WA MUNGU

Hapo Mwanzo Mungu aliumba Malaika katika hali ya njema na Heri kubwa. Kisha aliumba mbingu na nchi, na viumbe vyote vinavyoonekana na visivyoonekena. (Kol, 1;16, Mwa, 1;31)
Malaika ni viumbe vilivyo Roho tuu vyenye akili na utashi. (Zab 91:11, Ebr 1:7, Uf, 12:7-9).
Malaika wengine walikosa kwa kumkaidi Mungu, wakatupwa motoni na ndio Mashetani ambao Mkubwa wao ni Lusiferi. (Yn, 8:44: Uf 12:7-9,).
Mungu aliumba Malaika ili Wamtukuze, Wafurahi nae Mbinguni na wawe Matarishi/wajumbe wake kwa Wanadamu. (Tob 12:12, Lk. 16:22).
Malaika wema kazi yao ni kutuombea, kutumwa na Mungu kwetu, na wanatulinda kama Malaika walinzi. (Ebr, 13:2). Ambapo kila Mwanadamu ana Malaika wake wa kumlinda na kumuongoza Roho na Mwili, ndie Malaika wake mlinzi, (Zab, 91:11, Mt. 18:10).
Malaika wote sio sawa, wapo Malaika Wakuu, Malaika wanaomtumikia Mungu Mbinguni kwa mfano Makerubi na Maserafi, na pia wapo Malaika walinzi.
Malaika wakuu ni Mikaeli, Gabrieli na Raphaeli (Dn, 10:13, Tobiti 12:15, Lk 1:26).
Mashetani kazi yao ni kuteswa Motoni na hutaka kudhuru Roho na Miili ya wanadamuna kutupoteza milele. (1 Petro, 5:8, Yoh, 8:44).

MAFUNDISHO KUHUSU NAFASI YA MAMA BIKIRA MARIA

Leo nimeamua kutoa makala kuhusu Bikira Maria Baada ya maswali mbalimbali kuibuka kuhusu nafasi yake kwetu sisi. Chanzo cha makala hii ni www.alfagems.com

MAFUNDISHO KUHUSU NAFASI YA MAMA B. MARIA

Sisi Wakatoliki nyakati hizi zilizojaa madhehebu mbalimbali ya Kikristo, yanayotumia Biblia na kuitafsiri kadiri ya
imani yao ama wenyewe wanavyojisikia kwa namna fulani, tunajikuta tukichanganyikiwa na pengine kuona aibu ya
kumheshimu Mama Bikira Maria. Tunapoanza kuchunguza nafasi yake katika fumbo la ukombozi wa mwanadamu,
tunakiri pamoja naye kuwa ni Mwenyezi Mungu aliyemtendea makuu (Lk 1:49). Halafu tunakiri kwa unyenyekevu
wote pamoja na Yohane Mbatizaji, โ€œMtu hawezi kuwa na kitu asipopewa na Munguโ€ (Yoh 3:27). Hivyo yale yote
tunayoyasadiki kuhusu Bikira Maria, hakujipatia mwenyewe bali amejaliwa na Mwenyezi Mungu na kuitikia kwa
hiari fumbo la mpango wake.

MAANDIKO YANASHUHUDIA UMUHIMU WA WATU UNAOTOFAUTIANA

Maandiko matakatifu yanawasifu watu mbalimbali kutokana na walivyomuamini Mungu na kutenda makuu kwa
ajili ya taifa lake. Abrahamu alimuamini na kuwa tayari kumtolea sadaka mwanae Isaka, tukio lililomfanya apate
baraka ya pekee ya kuwa baba wa waamini (Mwa 22:15-18). Yosefu, kipenzi wa Yakobo, alikuwa mwaminifu hata
akaliokoa taifa lisiangamie kwa njaa (Mwa 50:20). Musa ndiye mkombozi wa taifa la Mungu katika Agano la Kale:
aliongoza Israeli kutoka utumwani Misri akalipatia sheria kutoka kwa Mungu katika mlima Sinai. Maandiko ya
Agano la Kale yanakiri, โ€œWala hajainuka kiongozi kama alivyokuwa Musaโ€ (Kumb 34:10-12). Kwa kuwa watu hao ni
wengi mno tunaorodhesha wafuatao: Yoshua, Debora, Gideoni, Samsoni, Samweli, Ruthu, wafalme Daudi na
Solomoni, manabii Eliya, Yeremia na Ezekieli. Nabii Isaya ana sifa ya pekee katika kumchora Masiya. Mwishoni
Bwana Yesu mwenyewe anamsifu Yohane Mbatizaji akisema, โ€œNi mkuu kati ya uzao wa wanawakeโ€ (Lk 7:24-28).
Bikira Maria ana nafasi gani kati yao? Hao tuliowataja walitenda kweli mambo makuu kwa imani, lakini Bikira
Maria yuko juu sana kupita hao wote, tena kwa mbali: yeye ni malkia wa makundi yote ya mbinguni, sio ya watu
tu, bali hata ya malaika. Mapokeo ya mashariki humuita โ€œdaraja linalounganisha dunia na mbinguโ€, โ€œmfano
aliouona Yakoboโ€ (Mwa 28:12).

BIKIRA MARIA KATIKA BIBLIA

1. UTABIRI KUHUSU BIKIRA MARIA, EVA MPYA
Mapokeo yamtazama Bikira Maria kama Eva mpya atakayemshinda nyoka wa kale (Ibilisi). Kwa nini Eva mpya?
Kwa sababu Eva wa kale alidanganywa na kuangushwa na Shetani, hivyo alitenda dhambi. Kumbe Maandiko
matakatifu yanatupatia utabiri kuhusu Eva mpya atakayemshinda adui (Shetani) kwa kumponda kichwa: โ€œNitaweka
uadui kati yako na huyu mwanamke, kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa chakoโ€ (Mwa 3:15).
โ€œTazama Bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamuita jina lake Emanueli, yaani Mungu
pamoja nasiโ€ (Isa 7:14). Dondoo hilo lilinganishwe na Lk 1:34-35, โ€œMariamu akamwambia malaika, Litakuwaje
neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu akakujilia juu yako, na nguvu zake
Aliye juu zitakufunika kama kivuli. Kwa sababu hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Munguโ€.
Utabiri mwingine wasema, โ€œLitatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa
matunda. Na Roho wa Bwana atakaa juu yake, Roho ya hekima na ufahamu, Roho wa shauri na uwezo, Roho wa
maarifa na ya kumcha Bwanaโ€ (Isa 11:1-2). Je, shina hilo si yeye Mama Bikira Maria, na tawi alilochipusha si
Mwanae Bwana wetu Yesu Kristo?
โ€œUmebarikiwa wewe katika kila hema la Yuda na katika kila taifa, nao wanaposikia jina lako watafadhaika.
Imani yako haitatoka mioyoni mwa watu wanaoukumbuka uweza wa Mungu mileleโ€ (Yudithi 14:7; 15:9).
Linganisha dondoo hili na Lk 1:42, โ€œAkapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe kuliko wanawake wote,
na yeye utakayemzaa amebarikiwaโ€. Je, utasema Bikira Maria ni mtu wa ziada katika mpango wa Mungu?
Tena tunasoma, โ€œImba, ee binti Sion, piga kelele, ee Israeli, furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, ee binti
Yerusalemu. Mfalme wa Israeli, naam, yeye Bwana yu katikati yakoโ€ (Sef 3:14-15). Linganisha dondoo hilo na
Injili: โ€œMalaika akaingia nyumbani mwake akamwambia, Furahi Maria, umejaliwa neema kubwa, Bwana yu pamoja
naweโ€ (Lk 1:28).
2. BIKIRA MARIA KATIKA AGANO JIPYA
Mambo yaliyotabiriwa katika Agano la Kale yametimia katika Agano Jipya: ukombozi wetu ulianza pale Bikira
Maria alipokubali fumbo la umwilisho wa Mwana wa Mungu, akisema kwa hiari, โ€œMimi ni mtumishi wa Bwana, na
iwe kwangu kama ulivyonenaโ€ (Lk 1:38).
Je, Bikira Maria ni bahasha? Siku hizi kuna baadhi ya waheshimiwa ambao wanadhani kujua Maandiko kuliko
watu wengine, tena wanadai wanaye Roho Mtakatifu; kumbe wanadiriki kumuita Mama huyo mtakatifu, eti ni
โ€œbahashaโ€ ambayo ikileta barua haina kazi! Jambo hili linasikitisha sana na sio tu kumkosea heshima Mama yetu
mpendwa wa mbinguni, bali inaweza pia kuwa kufuru kwa Mwenyezi Mungu aliyemuumba kama msaidizi wa
Mkombozi aliyejaa neema.
Manabii mbalimbali kwa mwanga wa Roho Mtakatifu walimuagua kwa heshima; Mama Elizabeti alijiona hastahili
kutembelewa naye akamuita, โ€œMama wa Bwana wanguโ€; mzee Simeoni alimuagulia mateso yenye uchungu kama
upanga yatakayopenya moyowe. Bwana Yesu aliyefurika Roho Mtakatifu tangu nukta ya kuchukuliwa mimba,
wakati alipokaribia kufa pale msalabani alimuita, โ€œMamaโ€; jumuia ya Mitume na wafuasi wa kwanza walimtaja
kipekee ilivyo ishara ya heshima. Je, Roho Mtakatifu ndiye anayewaongoza hawa ndugu zetu wamuite bahasha? Je,
ni Roho yuleyule aliyewaongoza Mitume na manabii ama roho ya aina nyingine? โ€œWapenzi wangu, msisadiki kila
mtu asemaye kwamba ana Roho wa Mungu, bali chunguzeni kwa makini kama huyo mtu anaongozwa na Roho wa
Mungu au la, maana manabii wengi wa uongo wamezuka ulimwenguniโ€ (1Yoh 4:1).
Bikira Maria sio โ€œchomboโ€ tu, bali mshiriki wa kazi ya ukombozi ya Mwanae. Kadiri ya mtume Paulo kuteseka ni
kutimiliza yaliyopungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya Kanisa, โ€œNa sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu,
maana kwa mateso yangu hapa duniani nasaidia kukamilisha kile kilichopungua bado katika mateso ya Kristoโ€ (Kol
1:24). โ€œโ€ฆ maana tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia utukufu wakeโ€ (Rom 8:17b). Katika hilo la
kumfuata Mwanae katika mateso Bikira Maria alitabiriwa wazi na mzee Simeoni, โ€œTazama huyu amewekwa kwa
kuanguka na kuinuka wengi katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. Nawe mwenyewe uchungu ulio kama
upanga utauchoma moyo wakoโ€ (Lk 2:34-35).
Bikira Maria alishiriki mateso ya ukimbizi huko Misri kwa lengo la kumficha Mwanae asiteswe na Herode, โ€œHivyo
Yosefu aliamka akamchukua mtoto pamoja na Mama yake akaondoka usiku akaenda Misri akakaa huko mpaka
Herode alipokufaโ€ (Math 2:14-15).
3. BIKIRA MARIA MWOMBEZI KATIKA HARUSI YA KANA:
Mama Bikira Maria anaonekana mwenye kuonea
huruma wenye shida: kwa ombi lake huko Kana ya Galilaya Yesu aligeuza maji kuwa divai, na wanafunzi wake
wakamwamini (Yoh 2:1-12).
4. BIKIRA MARIA AFANYWA EVA MPYA:
Juu ya Eva wa zamani imesemwa ni Mama wa walio hai: โ€œAdamu
akamwita mkewe jina lake Hawa, kwa kuwa ndiye aliye Mama wa walio haiโ€ (Mwa 3:20). Hata hivyo Agano Jipya
linaonyesha Adamu na Eva wa zamani wametuletea kifo (Rom 5:12).
Yesu, aliye Adamu mpya, alipokuwa anakamilisha sadaka ya ukombozi pale msalabani alimfanya Bikira Maria
awe Eva mpya kwa kitendo cha kumkabidhi mwanafunzi, tena yule aliyempenda zaidi. โ€œBasi Yesu aipomwona
Mama yake na yule mwanafunzi aliyempenda amesiMama karibu akamwambia Mama yake, Mama, tazama
Mwanao. Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama Mama yakoโ€ (Yoh 19:26-27). Zaburi yasema, โ€œLakini juu
ya Sion itasemwa, Sion ni Mama yao wote; Mungu mkuu ameuthibitisha. Mwenyezi Mungu ataorodhesha mataifa
na kuandika juu ya kila moja, Huyu chanzo chake ni Sionโ€ (Zab 87:5-6).
Pale msalabani Bikira Maria:
โ€ข alifanywa Mama wa wote wanaompenda Mwanae;
โ€ข alifanywa malkia wa wafiadini;
โ€ข kisha kumzaa pasipo uchungu Bwana wa uzima, pale alituzaa sisi kwa uchungu wa kutisha uliotokana na
kumuona Mwanae akifa msalabani. Hata hivyo Bikira Maria aliendelea kumuamini Mwanae aliyeonekana
ameshindwa;
โ€ข katika kuteswa kwa Yesu Bikira Maria alishuhudia hatua kwa hatua; wanafunzi wa Yesu walipokimbia na
kumtazama kwa mbali, Bikira mtakatifu alikuwa karibu akaona vema kila teso lililompata. Tena
kutokana na fungamano la upendo wa ajabu lililokuwepo kati ya Yesu na Mamaye, aliposhuhudia mateso
ya Mwanae aliteseka sana katika moyo wake safi usio na doa, kiasi kwamba baadhi ya watakatifu
wanasema, Msalaba wa Yesu uliwasulubisha wote, Yesu mwilini na Mama yake moyoni. Uaguzi wa mzee
Simeoni ulitimia hivyo.

JE, BIKIRA MARIA ALIZAA WATOTO WENGINE?

Mapokeo kuhusu Bikira Maria yanaonyesha alikuwa binti pekee wa wazee watakatifu Yohakimu na Ana. Vilevile
Mt. Yosefu, ingawa kisheria alikuwa mume wake, hakutenda naye tendo la ndoa hata moja. Ndiyo maana kwenye
litania yake tunamuita mwenye usafi kamili. Alikufa kabla Yesu hajaanza utume kwa kubatizwa kwenye mto
Yordani. Sisi tunasadiki Maria ni โ€œBikira daimaโ€.
Ndugu wa Yesu wanaosemwa katika Injili ni kina nani? Wanaosemwa katika Injili โ€œndugu zake Yesuโ€ si watoto
wa Bikira Maria wala Yosefu mtakatifu, bali ndugu wa kiukoo waliokuwa jirani sana na familia hiyo takatifu. Kama
Bikira Maria angekuwa na watoto wengine, je, Yesu Bwana wetu asingekuwa amefanya kosa la kiudugu
kuwanyangโ€™anya Mama yao na kumfanya awe Mama wa mtume Yohane alipomkabidhi msalabani, โ€œโ€˜Mwana, tazama
Mama yakoโ€™. Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwakeโ€ (Yoh 19:27).
Katika Agano Jipya yupo Yakobo anayeitwa na mtume Paulo โ€œndugu yake Bwanaโ€ (Gal 1:19): Yakobo huyo
alikuwa maarufu katika Kanisa la Yerusalemu (Mdo 12:7; 15:13-21; 21:18-20; Gal 2:9). Yakobo huyo si mtume
Yakobo mwana wa Alfayo, wala mtume Yakobo kaka yake Yohane (Lk 6:12-16), bali ni Yakobo ndugu yake Yose na
mama yao kwenye Injili anaitwa โ€œMaria mwingineโ€, si Maria Mama wa Yesu. โ€œWalikuwepo pia wanawake
waliotazama kwa mbali. Miongoni mwao akiwa Maria Magdalena, Salome na Maria mama wa akina Yakobo mdogo
na Yoseโ€ (Mk 15:40). Maria lilikuwa jina la kawaida kwa Wayahudi: akina Maria wakiwa wengi hivyo, tujue
kuwatofautisha kwenye Injili. Bikira Maria Injili zinamtaja kama โ€œMama wa Yesuโ€.

JE, WAKATI WA KUFANYA UTUME YESU ALIMDHARAU MAMA YAKE?

Wengine husoma Maandiko matakatifu wakiishia ujuu bila ya kufikiria wala kulinganisha na mistari mingine.
Hivyo hukwazwa na semi kadhaa za Bwana Yesu ambazo kimsingi hazimpingi Mama yake, bali zinampongeza.
โ€œAlipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katika lile kundi la watu akasema, โ€˜Hongera kwa mwanamke
aliyekuzaa na kukunyonyeshaโ€™. Yesu akamjibu, โ€˜Barabara, lakini heri yake zaidi yule anayelisikia Neno la Mungu na
kulishikaโ€™โ€ (Mk 11:27-28).
Tena lingine lasema, โ€œBasi, mtu mmoja akamwambia, โ€˜Mama yako na ndugu zako wako nje, wataka kusema
naweโ€™. Lakini Yesu akamjibu huyo mtu aliyemwambia hivyo, โ€˜Mama yangu ni nani, na ndugu zangu ni akina nani?โ€™
Kisha akanyosha mkono wake juu y aweanafunzi wake akasema, โ€˜Hawa ndio Mama yangu na ndugu zangu, maana
yeyote anayefanya anavyotaka Baba yangu aliye mbinguni, huyo ndiye kaka yangu na dada yangu na Mama
yanguโ€™โ€ (Math 12:46-50).
Je, sehemu hizi za Maandiko zinampinga kweli Bikira Maria au zinampongeza? Sababu:
โ€ข Jamaa yake Elizabeti alimpongeza, tena akiongozwa na Roho Mtakatifu, โ€œHeri yako wewe uliyesadiki
kwamba yatatimia yale uliyoambiwa na Bwanaโ€ (Lk 1:45).
โ€ข Bikira mtakatifu alipopashwa habari na malaika hakukataa mpango wa Mungu, bali kwa hiari yake
alikubali fumbo la mpango wake. โ€œMaria akasema, โ€˜Mimi ni mtumishi wa Bwana, na iwe kwangu kama
ulivyonenaโ€™. Kisha malaika yule akaenda zakeโ€ (Lk 1:38).
โ€ข Bwana Yesu alitaka kuwainua wasikilizaji wake wafuate mambo ya Kiroho kuliko ya mwilini. Hivyo ni
kweli, Bikira Maria anasifiwa kwanza kwa imani yake, iliyokuwa ya juu zaidi kushinda hata ile ya
Abrahamu, kuliko kwa kumchukua Yesu tumboni tu. Hata hivyo tusisahau kuwa Yesu, kama mtu yeyote
mcha Mungu, aliwaheshimu wazazi wake, tena tunasikia aliwatii. โ€œBasi, akarudi pamoja nao Nazareti,
akawa anawatiiโ€ (Lk 2:51).
Naomba, kabla hujahukumu neno moja, angalia ujumla wake.
Yesu alizaliwa na Bikira mtakatifu, ndiye aliyemlea na kuhangaika naye huko na huko hata Misri ili kumuepusha
na kifo. Ishara ya kwanza kwenye maisha ya hadhara iliyongozwa na Bikira Maria huko Kana. Maria alikuwepo hata
wakati wa Yesu kuteswa, akiteseka pamoja naye. Pale msalabani alikabidhiwa Kanisa kwa njia ya Yohane mtume.
Bikira Maria alikuwepo hapo mwanzo wa Kanisa, na ndiye aliyelivutia zaidi Roho Mtakatifu kwa njia ya sala yake.
โ€œHao wote walikusanyika pamoja kusali, pamoja na wanawake kadha wa kadha, na Maria Mama yake Yesu na
ndugu zakeโ€ (Mdo 1:14).

DOGMA ZA KANISA KUHUSU BIKIRA MARIA

Kuna mafundisho makuu manne kumhusu Bikira Maria ambayo ni lazima kila Mkatoliki ayasadiki kutokana na
ufunuo wa Mungu:
1. B. Maria mkingiwa dhambi ya asili
2. B. Maria Mama wa Mungu
3. B. Maria Bikira daima
4. B. Maria kupalizwa mbinguni mwili na roho

MKINGIWA DHAMBI YA ASILI

Tunasadiki Bikira Maria tangu atungwe mimba Mungu alimkinga na kila doa la dhambi kwa kutazamia stahili za
Yesu Kristo aliye Mkombozi wa binadamu wote. Ndiye mwanakanisa aliyekombolewa kwa namna bora kushinda
viungo vyote vya Kanisa. Maisha yake yote hakutenda dhambi hata moja. Mapokeo ya mashariki yanamuita A
Panagia = Mtakatifu tu. Dogma hiyo ilitangazwa na papa Pius IX mwaka 1854, hata mwaka 1858 Bikira Maria
alijitambulisha huko Lurdi (Ufaransa) kwa Mt. Bernadetta Soubirous kama Mkingiwa. Tena pale Fatima (Ureno)
tumefunuliwa moyo wake safi usio na doa.

MAMA WA MUNGU

Injili ya Yohane inaanza kwa kishindo, โ€œHapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu,
naye Neno alikuwa Munguโ€ (Yoh 1:1). Huyo Mungu Mwana ndiye aliyetwaa ubinadamu katika Bikira Maria
akazaliwa mtoto, jina lake Yesu, maana yake Mungu Mwokozi. Huyo ni binadamu kama sisi isipokuwa hana
dhambi. Ubinadamu wa Yesu unategemea Nafsi yake ya Kimungu, hivyo akisema, โ€˜Mimiโ€™, anamaanisha Nafsi yake
ya Kimungu. Ndiyo maana aliwaambia Wayahudi, โ€œKweli nawaambia, kabla Abrahamu hajazaliwa, nalikuwepoโ€
(Yoh 8:50). โ€œKama vile Baba alivyo asili ya uhai, ndivyo alivyomjalia Mwanae kuwa asili ya uhaiโ€ (Yoh 5:26).
Je, Bikira Maria ni Mama wa Mungu tangu lini? Mtume Paulo anaeleza, โ€œWakati maalumu ulipotimia Mungu
alimtuma Mwanae aliyezaliwa na mwanamkeโ€ (Gal 4:4). Ni kwanzia wakati huo: sasa imepita miaka 2006 tangu
Bikira Maria ajiliwe na sifa hiyo ya kumchukua mimba, kumzaa, kumnyonyesha na kumlea mtu ambaye kwa asili ni
Mungu. Cheo hicho kimemuinua juu kuliko hata malaika, akawa malkia wao. โ€œMalaika alimwambia, โ€˜Hicho
kitakachozaliwa kitaitwa Kitakatifu, Mwana wa Munguโ€™โ€ (Lk 1:35). Dogma ilitolewa mwaka 431 kwenye Mtaguso wa
Efeso uliomuita โ€œMzazi wa Munguโ€.

BIKIRA NA MAMA

Fumbo la Bikira Maria hapa linagongana na akili ya kibinadamu. Wote wanakiri ya kuwa Yesu alimwilishwa bila
ya mchango wa mwanamume, kumbe la ajabu zaidi ni kwamba hata uzazi wenyewe haukuondoa ubikira wake, bali
uliutakasa. Ingawa akili yetu inakataa, sisi tunakiri na malaika, โ€œHakuna lisilowezekana kwa Munguโ€ (Lk 1:38).
Ndiyo maana tunamkiri ni Bikira daima.

KUPALIZWA MBINGUNI MWII NA ROHO

Baada ya maisha haya ya duniani Bikira Maria mwenye heri alipalizwa mbinguni mwili na roho, ishara ya
mwanamke mshindi. โ€œIshara kubwa ikaonekana mbinguni, ambapo mwanamke aliyevikwa jua, pia na mwezi chini
ya miguu yake, na taji la nyota kumi na mbili juu ya kichwa chakeโ€ (Ufu 12:1).

HESHIMA ZA LITURUJIA KWA MARIA

Kuna ibada za Mama Bikira Maria zinazoadhimishwa katika liturujia. Hapa tunazipanga kulingana na heshima
zinavyozidiana:

SHEREHE

8 Desemba โ€“ Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili
1 Januari โ€“ Bikira Maria Mama wa Mungu
25 Machi โ€“ Bikira Maria Kupashwa Habari
15 Agosti โ€“ Bikira Maria Kupalizwa Mbinguni

SIKUKUU

31 Mei โ€“ Maamkio ya Bikira Maria
8 Septemba โ€“ Kuzaliwa kwa Bikira Maria

KUMBUKUMBU

Juni โ€“ Moyo Safi wa Maria
15 Septemba โ€“ Mama Yetu wa Huzuni
22 Agosti โ€“ Bikira Maria Malkia
7 Oktoba โ€“ Bikira Maria wa Rozari
21 Novemba โ€“ Bikira Maria Kutolewa Hekaluni
KUMBUKUMBU YA HIARI
11 Februari โ€“ Mama Yetu wa Lurdi
16 Julai โ€“ Mama Yetu wa Mlima Karmeli
5 Agosti โ€“ Kutabaruku wa Kanisa la B. Maria
Tena kila Jumamosi isiyo na adhimisho maalumu, Kanisa huadhimisha kumbukumbu ya Mama wa Mungu.
Pia zipo heshima za binafsi kwa Bikira Maria mwenye heri: mashariki tenzi na nyimbo (k.mf. Akatistos, tenzi za
mt. Efrem shemasi, na nyingine); magharibi (Roma) tunamheshimu binafsi na hata kijumuia kwa kusali rozari
takatifu. Ndiyo ibada ya binafsi inayompendeza sana baada ya zile za liturujia hata akatokea sehemu mbalimbali
duniani akihimiza tusali rozari ili tupate amani binafsi, kitaifa na kimataifa. Mwezi wa tano ni mwezi wa Maria.
Mwezi wa kumi ni mwezi wa Rozari. Mtu aliyeonja matunda ya kumheshimu Maria mtakatifu, Mama wa Mungu,
anajua uwezo wa maombezi yake. Kanisa linakiri neema zote za Mungu zaja kwetu kwa njia ya Maria.
Je, tunamuabudu Bikira Maria? Hapana, Bikira Maria hatumuabudu hata kidogo, bali tunamtolea heshima ya juu
kuliko watakatifu wengine. Mungu tu tunampa heshima ya โ€˜latriaโ€™ (kuabudu), watakatifu tunawaheshimu (dulia) na
Bikira Maria tunampa heshima sana (yuper-dulia).
Kweli Mama Bikira Maria ni โ€œkina kisichochunguzika kwa macho ya malaikaโ€ (Akatistos). Ni fumbo la ajabu
alilolifanya Mungu katika mpango wa wokovu kwa ajili yake na kwa ajili yetu. Katika Injili ya Yohane Bwana Yesu
alisema, โ€œNinayo bado mengi ya kuwaambieni, ila kwa sasa hamwezi kuyastahimili, lakini atakapokuja huyo Roho
wa ukweli atawaongoza kwenye ukweli woteโ€ (Yoh 16:12-13). Kwa msaada wa Roho Mtakatifu heshima kwa Bikira
Maria ilienea katika Kanisa lote tangu zamani kabisa. Tena katika Injili ya Luka kuna utabiri wa kumheshimu Bikira
Maria vizazi vyote, โ€œKwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mdogo, hivyo tangu sasa vizazi vyote
wataniita mwenye heriโ€ (Lk 1:48).

Je, Bikira Maria ni Bikira Daima au alizaa watoto wengine?

Jibu fupi ni kwamba Bikira Maria hakuzaa watoto wengine na hakuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu
Hapo zamani hakuna mkristu au dehebu lolote lililokuwa linapinga kuwa Bikira Maria sio Bikira Daima hata Waprotestanti/walokole waliamini Bikira Maria ni Bikira Hata Baada ya Kumzaa Yesu. Kwenye Miaka ya 1400-1600 Watu wote wakwanza waliopinga Kanisa Katoliki walikubali kuwa Bikira Maria ni Bikira daima wakiwemo Martin Lutha aliyeanzisha kanisa la Lutheran, John Calvin aliyeanzisha Ulokole/Protestanti, Mchungaji Ulrich Zwingli, Heinrich Bullinger, and Thomas Cranmer. Kwa miaka zaidi ya 350 Waprotestant/walokole waliendelea kuamini kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.
Lakini baadae wakristo wengi walianza kupinga kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.

Tunaweza kuthibitisha kuwa Bikira Maria hakuzaa watoto wengine kwa kunukuu Biblia Kama ifuatavyo;

1. Bikira Maria Alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu

Biblia inatuambia wazi kwamba Bikira Maria alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu Kama tunavyosoma katika Luka 1:26-35
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe.” 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” 34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)

2. Biblia Haiwataji ndugu wa Yesu wakati Yosefu na Maria walipokimbilia Misri kumficha Yesu na wakati waliporudi

19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.” 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.” Matayo 2:19-23
Kama wangekuwepo wadogo zake Yesu Biblia ingetuambia kwamba walikuwa wapi wakati huo na walikuwa na Yesu au la.

3. Biblia haituambii kuwa Yesu alikua na wadogo zake alipokuwa na miaka 12

Wakati wa Maria, Yoseph na Yesu walipoenda Yerusalemu Yesu akiwa na miaka 12 Biblia haituambii kuwa Yesu alikuwa na wadogo zake na walikuwa wapi. Kumbuka walikuwa na Desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka kwa ajili ya Pasaka familia nzima kama familia. Je hao watoto wengine walikuwa wapi. Kwa nini walikuwa na Yesu Mwenyewe? Maana yake ni kwamba Yesu hakuwa na Wadogo zake.
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.” 49 Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
Kwa hiyo Biblia haionyeshi kuwa Yesu alikuwa na kaka na dada wakati akiwa na miaka 12. Kama wangekuwepo wangetajwa hapa kuwa walikuwa pamoja na Wazazi wao kama Yesu au walikuwa na Yesu wakati anapotea. Biblia haituambii chochote kwa hiyo wakati huo hapakuwa na wadogo zake Yesu.

4. Kukosekana kwa neneo “Binamu” kwenye lugha ya Yesu

Wakristu wa kwanza pamoja na Yesu aliongea Kiaramaiki au Kiebrania. Katika lugha zote hizo hakuna neno “Binamu” kwa hiyo mabinamu walijulikana kama dada na kaka wa mtu. Kwenye Agano jipya Neno kaka na Dada lilitumika pia kuwakilisha binamu.
Biblia inapotuambia kuwa Kaka na dada zake Yesu haimaanishi kaka wa kuzaliwa bali ndugu au Binamu
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kwa hiyo wanaotajwa hapa ni ndugu wa Yesu kwa maana maneno kama; ndugu, kaka au dada lilitumika badala ya Binamu yaani mtoto wa shangazi au mjomba. Hapa juu Yosefu ametajwa kama kaka yake Yesu lakini tunajua kuwa Yosefu ni Baba yake Yesu. Baba na mwana hawawezi kuwa na jina sawa.

5. Biblia haitumii neno Ndugu, kaka au dada ikimaanisha ndugu wa kuzaliwa mama mmoja na baba mmoja

Sio mara zote Biblia imetumia neno Ndugu kumaanisha ndugu (Dada na Kaka) wa kuzaliwa yaani kaka na dada kwa mfano
Kwa kuangalia lugha ya Kiswahili na Kiingereza 1 Wakorintho 15:6 tunaona tafsiri tofauti.
KISWAHILI 6 Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa.
ENGLISH 6 After that, he appeared to more than five hundred of the brothers and sisters at the same time, most of whom are still living, though some have fallen asleep.
Kwa hiyo hapa neno kaka dada na ndugu linaonekana wazi halikumaanisha ndugu au kaka wa damu.

6. Undugu wa Yakobo, Simoni, Yosefu na Yuda kwa Yesu Sio wa mtu na kaka zake

Wasemao kuwa Bikira maria alikuwa na wana zaidi ya Yesu wananukuu kifungu hiki;
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kumbuka kulikuwa na Yakobo wawili wakati wa Yesu, Vifungu vifuatavyo yunaweza kuona kuwa kulikuwa na yakobo wawili ambao walikuwa ndugu za Yesu lakini sio kaka wa kuzaliwa kwa mama.
35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)
Tunaweza kuona Undugu huu na Yesu kwa kusoma;
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. (Wagalatia 1:19)
Lakini Yuda anasema;
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. (Yuda 1:1)
Kwa hiyo Yakobo na Yohane walikuwa watoto wa Mama mwingine ambao baba yao ni Zebedayo. Na Yakobo na Yosefu walikuwa watoto wa Maria Mwingine. Kwa hiyo ni Yakobo wa wili wa Mama wengine Tofauti na Maria. Yuda alikuwa ni ndugu yake Yakobo. Yakobo vilevile alikuwa ndugu yake Yesu.
Kuthibitisha kuwa Hawa kina Mama ndio waliokuwa Mama zao kina Yakobo wote hao wawili na wengine tunaweza kusoma;
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. (Yohana 19:25)
Kwa hiyo kwenye (Yohana 19:25) tunaona Kuwa ni kwenye Msalaba wa Yesu alikuwepo Mama yake Yesu (Bikira Maria), Dada yake Bikira Maria, Mke wa Cleopa na Maria Magdalena. Na kwenye (Matayo 27:55-56) wamwtajwa ni Mama za kina nani kama inavyoonekana kwenye kifungu kifuatachi;.
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56).
Kwa hiyo hii ina maanisha kulikua na wanawake watatu wenye majina sawa ya Maria waliokuwa chini ya Msalaba. Yakobo na Yuda walikuwa watoto wa Maria Mke wa Cleofasi, na sio Mama wa Yesu, na hivyo sio kaka za Yesu.

7. Yesu alimwacha Mama yake kwa Yohane kwa kuwa hakuwa na Kaka na dada wakumwachia mamaye

26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: “Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.” 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
Ndiyo maana Bikira Maria tangu siku ile alihamia kwa Yohani kwa kuwa hakuwa na watoto wengine.

Siri ya Kuwa na Amani ya Moyoni au Rohoni

Utangulizi

Amani ya Moyoni au Rohoni ni hali ya kutokua na wasiwasi na hofu moyoni kuhusu Mambo ya Rohoni na ya kidunia.

Ili kuwa na Amani ya Moyoni unatakiwa uishi kwa kutimiza wajibu wako wa kiroho na kidunia kama inavyotakiwa na kwa uwezo wako wote, Huku ukiwa na Matumaini ya kua kile unachokifanya kitafanikiwa, ni sahihi na umekifanya vizuri.

Uwe na Matumaini na utaipata Amani.

Amani ya Moyoni au Rohoni

Amani ya Moyoni au Rohoni ni hali ya kutokua na wasiwasi na hofu moyoni kuhusu mambo ya kiroho na ya kidunia. Ni hali ya utulivu na furaha ambayo hutokana na kuishi kwa namna inayolingana na maadili na imani zako, pamoja na kujua kwamba unafanya kila uwezalo kutimiza wajibu wako.

Kutimiza Wajibu Wako wa Kiroho na Kidunia

Ili kuwa na Amani ya Moyoni, unatakiwa uishi kwa kutimiza wajibu wako wa kiroho na kidunia kama inavyotakiwa na kwa uwezo wako wote. Hii inamaanisha kuwa mkweli kwa nafsi yako, kufanya kazi kwa bidii, na kuwa na nia safi katika kila jambo unalolifanya. Huku ukifanya hivyo, unapaswa kuwa na matumaini kwamba kile unachokifanya kitafanikiwa, ni sahihi, na umekifanya vizuri.

“Na lolote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo wote, kama kwa Bwana wala si kwa wanadamu, mkijua ya kuwa mtapokea kutoka kwa Bwana urithi kama thawabu. Mnamtumikia Bwana Kristo.” (Wakolosai 3:23-24)

Matumaini na Amani

Uwe na Matumaini na utaipata Amani. Matumaini yana nafasi kubwa katika kufikia amani ya moyoni. Matumaini ni imani kwamba mambo yatakuwa sawa hata kama hali inaonekana ngumu kwa sasa. Matumaini yanakusaidia kuvumilia changamoto na kukupa nguvu ya kuendelea mbele bila kukata tamaa. Hivyo, unapokuwa na matumaini na unajua kuwa unafanya jitihada zako zote, utaweza kupata amani ya ndani.

“Kwa maana mimi najua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa tumaini katika siku zenu za mwisho.” (Yeremia 29:11)

Shukrani na Kuridhika

Zaidi ya hayo, ni muhimu kujenga tabia ya kushukuru kwa kile ulichonacho na kukubali hali halisi ya maisha yako. Shukrani husaidia kuondoa hofu na wasiwasi, na inakuza hali ya kuridhika. Unapokuwa na moyo wa shukrani, utaona mambo mazuri katika maisha yako, hata yale madogo, na utaweza kufurahia safari yako ya maisha.

“Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.” (1 Wathesalonike 5:18)

Afya ya Kiroho

Kujali afya yako ya kiroho pia ni muhimu. Tafakari, sala, na kufanya mazoezi ya kiroho kama vile kutafakari kwa kina, kujisomea vitabu vitakatifu au kuzungumza na washauri wa kiroho kunaweza kusaidia kuimarisha amani yako ya ndani. Pia, kujenga mahusiano mazuri na watu wengine na kusaidia jamii kunaweza kuongeza hisia za furaha na amani ndani yako.

“Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ambayo ndio mliyoitiwa katika mwili mmoja. Tena iweni watu wa shukrani.” (Wakolosai 3:15)

Hitimisho

Kwa kifupi, Amani ya Moyoni inakuja kwa kuishi maisha yenye uwiano kati ya mambo ya kidunia na ya kiroho, kuwa na matumaini, kushukuru, na kujali afya yako ya kiroho. Ni hali inayoweza kufikiwa kwa kufanya jitihada za dhati na kuwa na mtazamo mzuri juu ya maisha.

“Amani nakuachieni; amani yangu nawapa; si kama ulimwengu utoavyo, ndivyo mimi nivyo wapa ninyi. Mioyo yenu isifadhaike, wala isikate tamaa.” (Yohana 14:27)

Angalia nilichokifanya Jana kumkomoa x-wangu

Mwenzenu nilikatiwa umeme jana basi leo si nikaamua kwenda kununua luku ya 10,000. Kufika njiani nikatamani fursana nikaingia kijisupermarket mara sindo nakutana na ex wangu! Mshenzi yule kaniona mimi sijui alikua na mpango wa kununua vocha ya jero eti kabadili kanunua vocha ya buku tano ilimradi nione maisha yake safi tangu tuachane. Mambo ya kijinga spendi kudadeky nimetoa buku kumi nikanunua mipampers nami nijifanye nimeowa nina mtoto halafu huyoo nikashika njia yangu.

Sasa washkaji zangu tafadhalini mwenye mtoto au shida ya pampers naomba anunue kwangu maana leo nalala tena kiza ๐Ÿ™†โ€โ™‚

Ziara za kushtukiza zinachekesha sana

Mimi Nimecheka sana
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

ZIARA ZA KUSHTUKIZA๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€
Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti, na msikilizaji mzuri wa redio, huwa naangalia luninga mara chache sana kama nikibahatika kupita mahala kuna luninga. Sasa wiki hii nimesikia mengi kuhusu hizi ziara za kushtukiza za viongozi wetu, nikaona hili ni jambo zuri tena linafaa kuigwa na sisi wananchi wapenda maendeleo. Nikaona nijipange na mimi nifanye ziara kadhaa za kushtukiza katika sehemu mbalimbali zinazonihusu.

Nikaona nianze na ziara ya kushtukiza pale shuleni kwa huyu mwanangu, maana kila siku anakunywa chai na kuondoka na daftari zake na mie sijawahi kwenda shuleni kwao toka nilipomuandikisha shule mwezi Januari. Nilifika shuleni na kumuona mwalimu mkuu, ambae alianza kutetemeka nilipomuambia kuwa nimekuja pale kwa ziara ya kustukiza, sijui alidhani mi ni mmoja wa Mawaziri wapya, maana nilimuona jasho linamtiririka ghafla. Akanikaribisha ofisi yake iliyokuwa na vitabu kila kona, na kuita waalimu wote na kunitambulisha kuwa ni kiongozi nimekuja kwenye ziara ya kustukiza.

Nilipojitambulisha kuwa ni mzazi, waalimu wote nikawaona waanza kupumua kwa raha. Nikawaambia kuwa mimi nina mwanafunzi pale na nilikuja ziara ya kustukiza kujua maendeleo yake. Baada ya mwalimu mkuu kusaka jina la mwanangu nae akanambia, โ€œMzee huyu mtoto hajaja shule mwezi wa tatu sasa, tulijaribu kukutafuta ikashindikana, hatujui yu wapiโ€ Jasho likaanza kunitoka mimi, yule mtoto kila asubuhi nampa nauli anaenda shule, na mara nyingi ananiomba michango kumbe hata shule haji. Niliondoka bila kuaga presha ikiwa juu.

Nikaona niende kwenye genge la mke wangu nae nikamfanyie ziara ya ghafla nimhadithie mambo ya mwanae, nilipofika pale nikakuta kuna mdada mwingine anauza genge. Nikamsalimu, na kumuuliza mwenye genge ntampataje, jibu lake lingeniua kama ningekuwa si mkakamavu, โ€œMume wake kaja kumchukua na gari wameenda kununua shamba Bagamoyoโ€. Nikaondoka nimechanganyikiwa, nikajuwa hapa dawa yangu moja tu, nayo ni Sabrina, mtoto wa Kinyaturu pale ambapo nikipata maudhi huwa naenda kubembelezwa.

Nikatwanga mguu kwa Sabrina nae nikamfanyie ziara ya ghafla ili anipoze moyo. Nilipogonga mlango wa chumba chake akatoka mbaba wa miraba minne, akanisalimia kwa upole, โ€œSalama kaka unasemaje?โ€ Jibu likanitoka โ€œSamahani mie nilimkopesha huyu dada wa chumba hiki vitenge, nilikuja kuuliza kama ameshapata hela yanguโ€ Ziara za kushtukiza zinataka moyo wa chuma jamani

Jinsi ya kupika Biskuti Za Kopa Za Kunyunyuziwa Sukari Za Rangi

MAHITAJI

Unga vikombe 2 ยผ

Siagi 250g

Sukari kukaribia kikombe ยฝ (au takriban vijiko 10 vya kulia)

Baking powder ยฝ kijiko cha chai

Ute wa yai 1

Vanilla 1 kijiko cha chai

Sukari Ya Kunyunyizia na rangi mbali mbali.

MATAYARISHO

Kagawa sukari katika vibakuli utie rangi mbali mbali uweke kando.
Changanya siagi na sukari katika mashine ya kusagia keki upige mpaka ilainike iwe nyororo.
Tia ute wa yai vanilla uhanganye vizuri.
Tia unga na baking powder kidogo kidogo uchanganye upate donge.
Sukuma donge ukate kwa kibati cha shepu ya kopa.
Pakaza siagi katika treya ya kupikia kwenye oveni upange biskuti
Nyunyizia sukari za rangi rangi kisha pika katika oven moto mdogo wa baina 180 โ€“ 190 deg F kwa takriban robo saa.
Epua zikiwa tayari.

Mbinu 11 za kufuata ili uweze kuacha pombe

Pombe ni kinywaji kinachotumiwa na watu wengi pasipo hata kufahamu athari zake. Pombe ina athari mbalimbali kiafya na kisaikolojia. Wengi baada ya kuathiriwa na pombe hutamani kuacha matumizi ya pombe lakini ni wachache tu ndiyo hufanikiwa katika hili.

Mwingereza Matt Haig ambaye ameandika kitabu kilichouzika sana cha โ€˜Reasons to Stay Aliveโ€™ anasema yeye akinywa pombe humletea wasiwasi hofu na uoga anatoa ushauri wa namna ya kufanya ili asinywe pombe.

โ€œHata kama watu hawakulazimishi kunywa nafsi yako tu inajisuta ni kama vile watu wasiokula nyama halafu umekaa kati yao unakula unajiona kama unawakosea unaweza ukajiondoa hapo,โ€ anasema Haig.

Jinsi ya Kuacha Pombe Tumia Mbinu hizi

1. Epuka watu watakaokushawishi kunywa pombe

Mara nyingi kama wewe unapenda kunywa pombe utakuwa na marafiki wanaokunywa pombe pia.

Ni wazi kuwa marafiki wanaokunywa pombe watakuhimiza kunywa hata kwa kukununulia au hata pengine kukukebehi na kukubeza juu ya uamuzi wako wa kuacha pombe.

Hivyo ikiwa unataka kuacha kunywa pombe ni lazima uepuke marafiki au watu wanaoweza kukushawishi kunywa pombe. Unaweza kutafuta marafiki wengine au watu wengine ambao hawatakatisha lengo lako la kuacha pombe.

2. Epuka mazingira yatakayokusababisha kunywa pombe

Ikiwa kuna mazingira yanayoshawishi kunywa pombe basi yaepuke. Inawezekana ni nyumbani kwa rafiki zako, hotelini, baa n.k; ikiwa unataka kuacha kunywa pombe basi huna budi kuepuka mazingira haya ambayo yatakushawishi kunywa pombe.

Kwa mfano Unaweza kujizoeza kukaa kwenye migahawa au hoteli ambazo hazina pombe ili usije ukajikuta umeshashawishika kuendelea kutumia pombe.

3. Usiweke pombe nyumbani au sehemu unayokaa

Kama unatabia ya kuweka pombe nyumbani, sasa inakupasa kuacha mara moja. Hata kama kuna mtu huwa analeta pombe nyumbani unaweza kumwomba kuwa wewe umekusudia kuacha pombe hivyo asilete pombe nyumbani. Kwa kufanya hivi utapunguza hatari ya kushawishika kuendelea kunywa pombe.

4. Wajulishe watu unaacha pombe

Unapowajulisha watu kuwa unaacha pombe ni rahisi zaidi wao kukusaidia wewe kuacha kunywa pombe. Tafuta watu ambao unahisi wanaweza kukusaidia na kukutia moyo katika mkakati wako huu wa kuacha pombe. Kuwajulisha watu pia kutakuhimiza kuacha kwani utaona aibu kwani umeshawatangazia watu unaacha, hivyo kuendelea ni kujiaibisha wewe mwenyewe.

5. Tatua matatizo ya kihisia na kiakili.

Mara nyingi wanywaji wa pombe hasa wale waliopindukia, hunywa kutokana na matatizo ya kihisia au kiakili yanayowakabili. Wengi huwa na majeraha kwenye maswala ya kifamilia au mahusiano, kazi, au hata kiuchumi.

Unaweza kutafuta suluhisho la matatizo haya kwa kuomba ushauri na msaada wa utatuzi kwa washauri nasaha ili kuepuka kunywa pombe kwa kisingizio cha kupoteza mawazo.

Kumbuka pombe huwa haiondoi matatizo haya bali hukufanya kuyasahau kwa muda tu; ikumbukwe kuwa hata wakati mwingine pombe hukusababishia kuyaongeza zaidi.

6. Tafuta kitu mbadala cha kufanya

Ikiwa kuna muda fulani ambao huwa unautumia kwa ajili ya kunywa pombe, basi yakupasa kubadili matumizi ya muda huo. Unaweza kujipangia shughuli nyingine yenye tija kwenye maisha yako kama vile, mazoezi, utunzaji wa bustani, kusoma vitabu, kutazama filamu, kusikiliza mziki, kutunza mazingira n.k. Kwa kufanya hivi utaweza kubana muda wako unaoutumia kwenda kunywa pombe.

7. Weka malengo tekelevu ya kuacha

Wengi hushindwa kuacha pombe kwa sababu hawana malengo yanayotekelezeka ya kuacha pombe. Kwa mfano unaweza kujiwekea mpango huu:

Nitaanza kuacha kwa kunywa chupa mbili tu kwa wiki.
Kisha nitapunguza na kunywa chupa moja kwa wiki
Na hatimaye nitaacha kabisa kwa wiki
Tarehe fulani (00/00/0000) ni lazima niwe nimeacha kabisa.

Ukijiwekea malengo kama haya na ukahakikisha unafanya juu chini kuyatimiza, hakika utaweza kuacha pombe kabisa.

8. Jipongeze wewe mwenyewe kwa kipindi ulichoweza kuacha pombe

Kujipongeza wewe mwenyewe kunakupa hamasa ya kufanya jitihada zaidi katika mpango wako wa kuacha pombe. Kwa mfano ikiwa umeweza kukaa wiki moja bila kunywa basi jipongeze kwa hatua hii na ujitahidi sasa kukaa mwezi au hata mwaka bila kunywa.

9. Usikae na pesa za ziada

Mara nyingi watu wengi hununua pombe kwa sababu wana pesa mfukoni; wanapokuwa hawana pesa hawalewi kabisa. Jambo hili linaweza kuzuilika kwa kubadili mfumo wako wa kutunza pesa. Unaweza kufanya mambo yafuatayo:

Ikiwa unalipwa pesa kila siku, omba upokee malipo kwa mwezi badala ya kila siku. Ikiwa hili haliwezekani unaweza kumwomba mtu unayemwamini akutunzie pesa zako.
Tunza pesa zako kwenye mifumo ya kutunza pesa kama vile benki na simu za mkononi. Kwa kufanya hivi kutapunguza pesa ulizo nazo mkononi.
Kumbuka njia bora zaidi ni kumwomba mtu unayemwamini akutunzie pesa zako na akukabidhi tu pale unapokuwa na hitaji muhimu. Ikiwa una mwenzi mwaminifu anaweza kukusaidia sana kwa hili.

10. Jikumbushe na kutafakari madhara ya pombe

Unapotafakari madhara ya pombe kama vile matatizo ya kiafya, kisaikolojia, kijamii na hata kiuchumi ni wazi kuwa hili litakuhimiza zaidi kuacha pombe. Tafakari madhara ya pombe na uone kuwa unapokunywa pombe unayapata. Kwa kufanya hivi utajijengea fikra za kujitahidi kuacha pombe ili uepuke madhara hayo.

11. Tafuta usaidizi na ushauri wa kuacha pombe

Zipo taasisi na watu mbalimbali wanaowashauri watu walioathirika kwa matumizi ya pombe. Inawezekana ni asasi ya kiraia, kituo cha ushauri nasaha au hata taasisi au kiongozi wa kidini; hawa wote wanaweza kukushauri na kukutia moyo katika mkakati mzima wa kuacha kunywa pombe.

Usipite bila kusoma kisa hiki cha kusisimua

Siku moja jioni katika mji flani, kulikuwa na basi likisafiri kutoka mji huo kuelekea mji mwingine. Lilikuwa ni basi kubwa na limejaa abiria. Wakati wakiendelea na safari, ghafla, mvua kubwa iliyoambatana na radi ikaanza kunyesha. Dereva hakuogopa, wala abiria, wakaendelea na safari. Mara wakati wanaenda, radi ikaanza kufuatilia gari. Kila wakienda, radi inapiga karibu na basi kana kwamba inalifuata basi. Likisimama, radi inapiga pembezoni mwa basi.

Dereva kuona hivyo, akasimamisha gari mita 5 kutoka kwenye mtiโ€ฆ Akawaambia abiria, “Humu ndani ya basi, kuna mtu ambaye leo ni siku yake ya kufa, tena kufa kwa radi. Ili tusife wote, nataka kila abiria ashuke akaguse mti ili anayepigwa na radi, apigwe wengine wasife kwa ajili yake. “Abiria wakitetemeka, wakaanza kushuka mmoja mmoja. Unaenda unagusa mti , kisha unarudi kwenye basi. Abiria wote pamoja na dereva mmoja mmoja, wakaenda, wakagusa mti na kurudi bila dhara lolote! Akawa kabaki abiria mmoja tu, ambaye alikuwa hajagusa mti. Abiria wote kwa macho ya hasira wakamwambia akaguse mti. Akawa anaogopa kufa. Akagoma. Wakamlazimisha kwa nguvu sana na kumtoa njeโ€ฆโ€ฆ. โ€ฆโ€ฆ.. Yule abiria akiwa amefumba macho, akaenda akagusa mti. Hamadi bin Vuu! Radi kali sana ikalipiga basi, abiria na wote waliokuwamo, wakafa palepale. Kumbe uwepo wake ndio ulikuwa unazuia abiria wengine wasidhurike na radi.

MAFUNZO

1. Unapofanikiwa, huwezi jua uwepo wa nani umefanikisha mafanikio yako, usichukue sifa zote peke yako. Wapatie na wengine bila kumsahau MUNGU.
2. Unaweza kujiona huna thamani sehemu ulipo, iwe kwenye kundi la WhatsApp, darasani, kazini, kwenye basi, barabarani bila kujua kama uwepo wako ni wa muhimu sana kwa ustawi wa wengine.
3. Usimtenge wala kumnyanyasa mtu au jirani yako, huwezi jua uwepo wake ni kwa ajili gani.

Angalia alichokifanya huyu mtu baada ya kuokota wallet ya thamani

Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station “naitwa Juma nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki7, ATM card na karatasi yenye PIN ya ATM card na kijimfuko cha dhahabu” Mtangazaji akasema, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama anakusikiliza? Jamaa akajibu; hapana, ninaomba kumuombea dedication wimbo wa R.Kelly usemao “U SAVED ME” umfikie popote alipo!!

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About