Karibu AckySHINE
Karibu AckySHINE
Chagua Unachotaka Kusoma Hapa
Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.
Mapishi ya Mandazi ya nazi
Mahitaji
Unga wa ngano (self risen flour) vikombe 2 na1/2
Sukari (sugar) 1/2 kikombe
Hamira (yeast) 1/2 kijiko cha chai
Hiliki (cardamon powder) 1/4 kijiko cha chai
Tui la nazi (coconut milk) kiasi
Baking powder 1/4 kijiko cha chai
Siagi (butter)1 kijiko cha chakula
Mafuta ya kukaagia
Matayarisho
Changanya unga na vitu vyote kasoro tui la nazi na mafuta ya kukaangia. Ukisha changanyika vizuri tia tui la nazi na uanze kuukanda mpaka uwe mlaini. Baada ya hapo usukume na ukate mandazi katika shape uipendayo, Kisha uyawe katika sehemu yenye joto (warm place) ili yapate kuumuka.
Yakisha uumuka yakaange katika mafuta mpaka yaive kisha ipua na uyaache yapoe tayari kwa kuliwa. (Mafuta ya kukaangia yasiwe yamoto sana kwani yatayababua mandazi na hivyo ndani hayataiva vizuri.
Wanaume ni noma, Angalia wanachokifanyaga wakimwona mwanamke
Wanaume ni viumbe WASTAARABU sana..Mdada anapokua kavaa BIKINI na BRA tu, 98% ya mwili wake unakuwa waziโฆSisi kwa USTAARABU huwa tunaangalia pale PALIPOFUNIKWA..Hatutaki Dhambi za Kijinga kabisa Sisiโฆ
๐๐๐๐๐๐
Jambo la kufanya kama binti alikuachaga zamani na sahizi anakutaka
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuniโฆunaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuniโฆ๐๐๐๐
Jinsi ya kuvaa viatu mbalimbali inavyotakiwa na ili upendeze
Viatu ni kinga kwa ajili ya kuhifadhi miguu. Vile vile viatu ni vazi ambalo linaongeza urembo na nakshi kwa mvaaji. Viatu vipo vya aina mbalimbali na vinavaliwa kulingana na mahali na mavazi yanayoambatana navyo. Tuangalie baadhi ya aina za viatu na wapi hasa na vipi vikitumika vinapendeza zaidi.
1.Viatu vya ngozi vya kufunika
Viatu vya kufunika vipo virefu sana, vyenye urefu wa wastani na vifupi kabisa. Mara nyingine haviwi vya ngozi kabisa bali ni kama vina plastiki na pia vingine huwa na uwazi mdogo kwa mbele.Viatu virefu zaidi mara hupendeza zaidi kuvaliwa kwenye sherehe na kanisani. Unaweza kuvaa kazini kama kazi yako haikulazimu kutembea tembea maana vitachosha miguu yako na kupunguza ufanisi.
Viatu vyenye urefu wa wastani unaweza kuvaa popote iwe kazini, kanisani, kwenye sherehe n.k. Viatu vya chini kabisa vinakuwa vyenye matumizi zaidi wakati unamatembezi mengi. Havifai sana kuvaa kwenye sherehe za usiku hasa kama unavaa nguo maalumu ya usiku. Vinafaa sana kwa mjamzito hasa katika miezi ya mwisho.
2.Viatu vya wazi virefu
Viatu hivi vipo vya aina mbili, vyenye rangi za mngโao na ambavyo ni mahususi kwa sherehe za usiku na vyenye rangi ngumu ambavyo waweza kuvaa kazini au kanisani. Viatu hivi vinapendeza kuvaliwa na nguo yoyote ila ikiwa ya urefu wa wastani ni nzuri zaidi maana huwezesha kuonekana urembo na uzuri wote wa kiatu. Viatu hivi vinakuja katika mitindo mbalimbali na unachagua ule ambao wewe unaupendelea zaidi mfano vyenye visigino vyembamba, visigino vinene au aina ya โwedgesโ.
3.Viatu vya wazi vifupi
Viatu hivi ni vizuri sababu vinawezesha miguu kupumua na kuโrelaxโ. Viatu hivi vipo vya aina tofauti tofauti na vinafaa sana kuvaliwa kwa matembezi ya jioni, wakati wa safari ndefu, wakati ukiwa na mizunguko mingi na pia hata kazini au kanisani pale unapokuwa umevaa nguo za kawaida (casual). Havivutii sana kuvaliwa na suti au nguo ya usiku. Pia mara nyingi viatu vya chini hupendezea kuvaliwa na nguo ndefu( hasa casual) na viatu virefu hupendeza zaidi kwa nguo yenye urefu wa wastani.
4.Viatu vya muda maalumu
Hivi ni viatu ambavyo vinavaliwa wakati wa kazi maalumu kama wakati wa kazi za mashambani, mgodini, wakati wa michezo au wakati wa baridi kali.
Ni vyema na inapendeza kama unauwezo uwe na viatu vya aina mbalimbali angalau aina tatu. Mfano viatu vyeusi vya urefu wa wastani, viatu vya usiku vya wazi, viatu vya chini vya kufunika na vya wazi.
Hakuna siku mbaya maishani kama hii
Hakuna siku mbaya maishan kuona mtu uliyesoma naye darasa moja, anakupita na private car,, afu we umeninginia kwenye daladala,,, tena ulikua unamzid akili ๐๐๐hapo Ndo utajua kwann gunia na dunia vinatofautiana neno moja
Mambo ya kutafakari unapokuwa katika shida kubwa, unapoelekea kukata tamaa
Tafakari Kuhusu Wakati wa Shida
Leo tunatafakari kuhusu wakati wa shida. Maisha ya mtu yanabadilika wakati wowote kwa namna yoyote. Yanaweza yakawa mazuri mpaka ukashangaa au yanaweza yasiwe mazuri kama unavyotarajia. Yote hayo ni sehemu ya maisha.
“Nimejifunza kuwa na kuridhika na hali yoyote niliyo nayo. Najua jinsi ya kuwa na hali duni, najua jinsi ya kuwa na hali ya wingi. Katika hali zote na mambo yote, nimefundishwa jinsi ya kushiba na jinsi ya kuwa na njaa, jinsi ya kuwa na wingi na jinsi ya kupungukiwa.” (Wafilipi 4:11-12)
Kumbuka Wakati wa Matatizo
Unapokua na matatizo makubwa katika maisha, kumbuka haya yafuatayo:
1. Mungu Yupo na Anakuona
Mungu yupo na anakuona. Mwambie matatizo yako, huo ndio wakati wake wa kuonyesha uwepo wake na nguvu zake. Wewe tu kusema na Mungu kwa utayari na uwazi, hivyo utakao kuwezesha kupata au kutatua tatizo lako.
“Naomba BWANA akujibu siku ya dhiki, jina la Mungu wa Yakobo likuinue.” (Zaburi 20:1)
“Mchungueni Bwana na nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote.” (1 Mambo ya Nyakati 16:11)
“Bwana ni ngome yao katika wakati wa shida.” (Zaburi 37:39)
2. Matendo na Maamuzi Yako
Maneno, vitendo, na maamuzi yako ndiyo yanaweza yakawa njia ya kutatua matatizo yako. Usiogope kuchukua hatua zinazohitajika. Tafuta hekima na uongozi kutoka kwa Mungu katika kila hatua unayochukua.
“Yehova atakuelekeza siku zote, na kukusibisha katika nchi yenye ukame, na kukuimarisha mifupa yako. Utakuwa kama bustani iliyomwagiliwa, na kama chemchemi ya maji ambayo maji yake hayatapungua.” (Isaya 58:11)
“Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe. Katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako.” (Mithali 3:5-6)
“Nawafundisha njia iliyo njema na adili; msiiachilie sheria yangu.” (Mithali 4:11-13)
3. Matatizo Hayako Sio Mwisho wa Maisha
Tatizo lako sio mwisho wa maisha yako, sio mwisho wa yote mazuri ya jana, leo, na kesho. Bado unayo mambo mengi mazuri yanakungojea. Mungu anapanga mambo mazuri kwa ajili ya wale wanaompenda na kumtumainia.
“Maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu, asema Bwana, ni mipango ya amani na si ya mabaya, ili niwape tumaini katika siku zenu za usoni.” (Yeremia 29:11)
“Na tusiache kutenda mema, kwa maana tutavuna kwa wakati wake tusipozimia roho.” (Wagalatia 6:9)
“Bwana atakamilisha mambo yangu; Ee Bwana, fadhili zako ni za milele; usiache kazi ya mikono yako.” (Zaburi 138:8)
4. Uangalizi wa Tatizo
Kumbuka tatizo lako linaweza likawa sio kubwa ila wewe ndio unaliona kubwa. Wewe sio wa kwanza kuwa na tatizo kama hilo, wengine hayo ndo maisha yao. Angalia kwa mtazamo wa matumaini na uombe hekima ya Mungu ili uweze kuona njia ya kutoka kwenye tatizo lako.
“Mkipungukiwa na hekima, na aombe kwa Mungu, naye atampa kwa ukarimu wala hachukii.” (Yakobo 1:5)
“Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.” (2 Wakorintho 4:16)
“Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” (Wafilipi 4:13)
Kwa hivyo, wakati wa shida, ni muhimu kujikumbusha kwamba Mungu yupo, anakusikiliza, na yupo tayari kukusaidia. Usiache matumaini, endelea kuamini na kutenda kwa hekima na imani, ukijua kwamba matatizo yako ni sehemu ya safari yako ya kiroho na Mungu anapanga mazuri mbele yako.
Utani kwa wadada wembamba
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Wadada wembamba hebu nenepeni basi mnatupa tabu kusoma maneno ya kwenye kanga jamanii โฆโฆโฆmnaviringisha kanga mwili mara 3 mpaka maandishii hayaonekanii
๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Mapishi ya Mihogo ya nazi na kuku
Mahitaji
Mihogo kilo 1
Kidali cha kuku 1 kikubwa
Nyanya 1 kubwa
Kitunguu maji 1 cha wastani
Swaum/tangawizi i kijiko cha chai
Nazi kopo 1
curry powder 1 kijiko cha chai
Binzari manjano 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/2
Pilipili 1
Chumvi kiasi
Matayarisho
Saga pamoja nyanya, kitunguu na swaum/ginger pamoja na vimaji kidogo. Kisha vitie kwenye sufuria isiyoshika chini na uvishemshe mpaka maji yote yakauke kisha tia mafuta na upike ktk moto mdogo mpaka viive.Baada ya hapo tia spice na uzipike kidogo kisha tia mihogo na kuku (kuku na mihogo vikatwe vipande vya wastani) vichanganye vizuri kisha tia nazi na vimaji kiasi,limao chumvi na pilipili na ufunike kisha punguza moto. Pika mpaka mihogo na kuku viive na ibaki rojo kidogo kisha ipua na mihogo yako itakuwa tayari kwa kuliwa
Mapishi ya Biskuti Za Mayai
VIAMBAUPISHI
Unga 3 Vikombe
Sukari ya unga (icing sugar) 1 Kikombe
Siagi 250 gm
Mayai 3
Vanilla 2 Vijiko vya chai
Baking powder 1 Kijiko cha chai
JINSI YA KUPIKA
Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy).
Tia mayai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini.
Tia unga na baking powder changanya na mwiko.
Tengeneza round upange kwenye tray utie nukta ya rangi.
Nyunyuzia sukari juu ya hizo round ulizotengeneza kabla huja choma.
Pika (bake) katika oven moto wa 350ยฐF kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.
Ujumbe kwa leo
Kuna baadhi ya LEVEL huwezi kufikaโฆKuna MAFANIKIO huwezi kuyafikiaโฆKuna HELA huwezi kuzipataโฆKama umezungukwa na watu BASICโฆ
Kuanzia asubuhi mpaka jioni wanaongelea WATU TU..Fulani kamegwa na yule..halafu yule naniliu saivi anatembea na yule ex wa naniiโฆAsubuhi mpaka jioni DISCUSSING PEOPLEโฆHawa ndio watu BASICโฆHata siku 1 hawatakupa Ushauri kuhusu HOW TO REACH SOMEWHEREโฆNEVER
Na ukionekana unaanza kufanya vitu EPIC watakugeuka kwamba UNARINGA.. UNAJISIKIA.. UMEWATENGAโฆUNAJIDAI UNA HELAโฆand lots of bullshitโฆ
Pengine ulipaswa kuwa mbaaalii kibiashara lakini HUWEZI coz umezungukwa n Mbaazi tupuโฆBASIC PEOPLEโฆUkiwaambia umesikia Kiwanja kinauzwa Kigamboni wanakwambia Kigamboni watu wanatapeliwa kuna mradi wa Joji BushiโฆUkiwambia unataka kujiunga Forever Living wanakwambia UNALIWA HELAโฆUkiwaambia kuna SACCOSS wanatoa mikopo unataka uchukue ujenge wanakwambia INTEREST ZAKE UTASHINDWA na kujenga sio mchezo shosti..Unaamini unaacha!โฆNataka kufanya Kitu flani WANAKUKATISHA TAMAA
Unahitaji kuzungukwa na watu wenye POSITIVE ENERGY ambao ukiwambia unataka kwenda Mbinguni kwa kupitia Mkuranga wanakuchangia NauliโฆNiliposema naacha kazi watu ohh utakula nini..utaishijeโฆMji Mgumu huu..Wenzio wanatafuta kazi we unaacha utalostiโฆWHO SAID??Nadunda kama kawa..NEGATIVE PEOPLE WILL BRING U DOWNโฆ.Ukitaka Kupaa kaa karibu na ndegeโฆWe unataka kupaa unakuwa rafiki wa NyangumiโฆUNAZAMISHWA SASA HIVI!!
Tangu nianze kukaa na watu Positive I have changed a lotโฆNikiwaza jambo wanauliza HOW DO WE ACHIEVE THIS na sio FULANI ALIWAHIFANYA HII AKAFELI..
Ikikusaidia Chukua..
KILL ALL NEGATIVE PEOPLE AROUND YOU kama unataka kufikia Malengo Makubwa, I will be ur Lawyer at the Court na mwambie Hakimu nilikutuma mimi!
TIME TO DELETE ALL BASIC PEOPLE who wait of option๐๐๐๐
JINSI YA KUANDAA VILEJA
MAHITAJI
Unga wa mchele – 500g
Samli – 250g
Sukari – 250g
Hiliki iliyosagwa – 1/2 kijiko cha chai
Arki (rose flavour) – 1/2 kijiko cha chai
Baking powder – 1 kijiko cha chai
Mayai – 4
Maji ya baridi – 1/2 kikombe cha chai
MAANDALIZI
Saga sukari iwe laini kiasi, changanya unga wa mchele, baking powder, hiliki na sukari.
Pasha moto samli mpaka iwe nyepesi kama maji mimina kwenye ule mchanganyiko wa unga wa mchele, kisha uchanganye pamoja na arki.
Ongeza mayai yaliopigwa endelea kuchanganya mpaka unga umeanza kuchanganyika vizuri.
Ongeza maji ya baridi sana kama nusu kikombe tu ili uchanganyike vizuri.
Kata kwa design unayotaka viwe vinene visiwe kama cookies za kawaida kama ilivyo kwenye picha na ukipenda utaweka kidoto kwa kutumia zaafarani katikati ya kileja kama inavyoonesha hapo juu.
Choma kwa moto wa baina ya 300F na 350F kwa dakika 15 mpaka 20 visiwe vyekundu toa na tayari kwa kuliwa.
Mbinu za kuzuia magonjwa kwa kuku
Mbinu hizo ni hizi zifuatazo;
Namna ya kufanya Ukaguzi wa mara kwa mara wa banda la kuku kuzuia magonjwa
Ukaguzi wa Kila siku
โข Hakikisha unasafisha vyombo vya kulishia na kunyweshea pamoja na viota.
โข Ondoa kinyesi kwa kuku.
โข Waangalie kuku wako kwa makini ili kujua afya na maendeleo yao. Yaani ili kutambua kama kuna mwenye ugonjwa
Ukaguzi Kwa wiki
โข Ondoa matandazo machafu na kuweka mapya ili kuzuia kuzaliana kwa vijidudu vya magonjwa.
Ukaguzi kwaKwa mwezi
โข Angalia uwepo wa wadudu na chawa, kisha utibu kama kuna ulazima.
Mambo 8 ya kuzingatia kabla ya kuleta mifugo (kuku, ng’ombe,mbuzi n.k) wapya bandani
Mambo hayo ni haya yafuatayo;
1. Hakikisha unaondoa matandazo yote ndani ya nyumba,
2. Ondoa vyombo vya kulishia na kunyweshea.
3. Ondoa uchafu wote unaoonekana bandani.
4. Safisha banda lote kwa kutumia maji na dawa.
5. Suuza na uache likauke.
6. Puliza dawa ya kuua wadudu.
7. Weka matandazo mapya,
8. Weka viombo vya kulishia na kunyweshea.
Jinsi ya kutunza nyumba ya kuku ili kuzuia magonjwa
1. Nyumba ya kuku iwe safi na kavu muda wote kuzuia ueneaji na kuzaliana kwa vijidudu vya magonjwa
2. Nyumba ya kuku iwe na nafasi za kupitisha hewa ya kutosha ili kuepuka joto na unyevunyevu ambao unachangia uwepo wa magonjwa kwa kuku
3. Hakikisha unaondoa matandazo na takataka zote kwenye banda wakati wote hasa yenye unyevu.
4. Fagia banda na kuhakikisha ni safi wakati wote. Weka matandazo mapya mara kwa mara.
5. Weka sehemu za kutosha kuku kupumzikia.
6. Weka viota vya kutosha.
7. Weka maji sehemu ambayo ni rahisi kusafisha.
8. Hakikisha unaondoa wanyama kama panya na wadudu nyemelezi kwenye sehemu ya malisho ya kuku kwani wao hubeba vimelea vya magonjwa.
Namna ya kutunza kuku na kuwakinga na magonjwa
1. Zingatia chanjo muhimu kwa kuku ili kuzuia magonjwa kama utakavyoshauriwa na mtaalamu wa mifugo.
Chanjo huanza katika wiki ya kwanza (mfano chanjo ya kuzuia sotoka) na inaweza kurudiwa baadaye.
2. Epuka kuweka kuku wengi mahali pamoja.
Ni rahisi magonjwa kuenea kwa haraka kuku wanaporundikana.
3. Kumbuka kutenganisha vifaranga na kuku wakubwa (isipokuwa kutoka kwa mama) kwa sababu vifaranga ni rahisi na wepesi sana kushambuliwa na magonjwa.
4. Hakikisha unaweka mipaka na madaraja ya sehemu za kuku kuzunguka/kucheza.
Namna ya kulisha kuku ili wasipatwe na magonjwa
Safisha vyombo vya kulishia na kunyweshea kila siku. Osha, sugua vizuri, kisha suuza kuondoa utando unaobeba bakteria.
Kuku wanahitaji wapewe chakula cha kutosha na chenye virutubisho vyote. Unaweza kuwaongezea majani, makombo, nafaka, mchanga laini, au maganda ya mayai.
Wapatie kuku maji safi muda wote. Wafugaji wengi wameripoti kuwa na matokeo mazuri baada ya kuchanganya dawa ya kuua vimelea kwenye maji ya kunywa.
Nunua chakula kwa wauzaji wazuri na wanaoaminika ili kuepuka minyoo na sumu hatarishi. Usiwape kuku chakula chochote kinachoonekana kuoza au kunuka uvundo.
Hifadhi chakula cha kuku katika sehemu kavu isiyo na joto na isiwe kwa zaidi ya miezi mitatu ili kuepuka kuharibiwa na fangasi.
Namna ya kukabiliana na Magonjwa ya kuku
Hakikisha unamuona mtaalamu wa mifugo mara uonapo dalili zozote za kuumwa kwa mifugo wako.
Tenga na wapatie tiba au kuwaua na kuteketeza kabisa kuku wagonjwa kuepuka kuenea kwa magonjwa.
Ondoa ndege waliokufa mara moja, uwafukie au kuchoma moto. Usile kuku aliekufa. Baadhi ya magonjwa ya ndege yanaweza kuambukizwa kwa binadamu.
Endapo kuna mlipuko wa ugonjwa katika eneo lako, usiruhusu watu kutembelea banda lako. Watu wanaweza kuleta maambukizi kwa miguu yao katika mabuti, nguo na mikono.
Pia magari yanaweza kuleta madhara kwa mabanda yako kupitia matairi na upakuaji wa mizigo.
Mbinu 11 za kufuata ili uweze kuacha pombe
Pombe ni kinywaji kinachotumiwa na watu wengi pasipo hata kufahamu athari zake. Pombe ina athari mbalimbali kiafya na kisaikolojia. Wengi baada ya kuathiriwa na pombe hutamani kuacha matumizi ya pombe lakini ni wachache tu ndiyo hufanikiwa katika hili.
Mwingereza Matt Haig ambaye ameandika kitabu kilichouzika sana cha โReasons to Stay Aliveโ anasema yeye akinywa pombe humletea wasiwasi hofu na uoga anatoa ushauri wa namna ya kufanya ili asinywe pombe.
โHata kama watu hawakulazimishi kunywa nafsi yako tu inajisuta ni kama vile watu wasiokula nyama halafu umekaa kati yao unakula unajiona kama unawakosea unaweza ukajiondoa hapo,โ anasema Haig.
Jinsi ya Kuacha Pombe Tumia Mbinu hizi
1. Epuka watu watakaokushawishi kunywa pombe
Mara nyingi kama wewe unapenda kunywa pombe utakuwa na marafiki wanaokunywa pombe pia.
Ni wazi kuwa marafiki wanaokunywa pombe watakuhimiza kunywa hata kwa kukununulia au hata pengine kukukebehi na kukubeza juu ya uamuzi wako wa kuacha pombe.
Hivyo ikiwa unataka kuacha kunywa pombe ni lazima uepuke marafiki au watu wanaoweza kukushawishi kunywa pombe. Unaweza kutafuta marafiki wengine au watu wengine ambao hawatakatisha lengo lako la kuacha pombe.
2. Epuka mazingira yatakayokusababisha kunywa pombe
Ikiwa kuna mazingira yanayoshawishi kunywa pombe basi yaepuke. Inawezekana ni nyumbani kwa rafiki zako, hotelini, baa n.k; ikiwa unataka kuacha kunywa pombe basi huna budi kuepuka mazingira haya ambayo yatakushawishi kunywa pombe.
Kwa mfano Unaweza kujizoeza kukaa kwenye migahawa au hoteli ambazo hazina pombe ili usije ukajikuta umeshashawishika kuendelea kutumia pombe.
3. Usiweke pombe nyumbani au sehemu unayokaa
Kama unatabia ya kuweka pombe nyumbani, sasa inakupasa kuacha mara moja. Hata kama kuna mtu huwa analeta pombe nyumbani unaweza kumwomba kuwa wewe umekusudia kuacha pombe hivyo asilete pombe nyumbani. Kwa kufanya hivi utapunguza hatari ya kushawishika kuendelea kunywa pombe.
4. Wajulishe watu unaacha pombe
Unapowajulisha watu kuwa unaacha pombe ni rahisi zaidi wao kukusaidia wewe kuacha kunywa pombe. Tafuta watu ambao unahisi wanaweza kukusaidia na kukutia moyo katika mkakati wako huu wa kuacha pombe. Kuwajulisha watu pia kutakuhimiza kuacha kwani utaona aibu kwani umeshawatangazia watu unaacha, hivyo kuendelea ni kujiaibisha wewe mwenyewe.
5. Tatua matatizo ya kihisia na kiakili.
Mara nyingi wanywaji wa pombe hasa wale waliopindukia, hunywa kutokana na matatizo ya kihisia au kiakili yanayowakabili. Wengi huwa na majeraha kwenye maswala ya kifamilia au mahusiano, kazi, au hata kiuchumi.
Unaweza kutafuta suluhisho la matatizo haya kwa kuomba ushauri na msaada wa utatuzi kwa washauri nasaha ili kuepuka kunywa pombe kwa kisingizio cha kupoteza mawazo.
Kumbuka pombe huwa haiondoi matatizo haya bali hukufanya kuyasahau kwa muda tu; ikumbukwe kuwa hata wakati mwingine pombe hukusababishia kuyaongeza zaidi.
6. Tafuta kitu mbadala cha kufanya
Ikiwa kuna muda fulani ambao huwa unautumia kwa ajili ya kunywa pombe, basi yakupasa kubadili matumizi ya muda huo. Unaweza kujipangia shughuli nyingine yenye tija kwenye maisha yako kama vile, mazoezi, utunzaji wa bustani, kusoma vitabu, kutazama filamu, kusikiliza mziki, kutunza mazingira n.k. Kwa kufanya hivi utaweza kubana muda wako unaoutumia kwenda kunywa pombe.
7. Weka malengo tekelevu ya kuacha
Wengi hushindwa kuacha pombe kwa sababu hawana malengo yanayotekelezeka ya kuacha pombe. Kwa mfano unaweza kujiwekea mpango huu:
Nitaanza kuacha kwa kunywa chupa mbili tu kwa wiki.
Kisha nitapunguza na kunywa chupa moja kwa wiki
Na hatimaye nitaacha kabisa kwa wiki
Tarehe fulani (00/00/0000) ni lazima niwe nimeacha kabisa.
Ukijiwekea malengo kama haya na ukahakikisha unafanya juu chini kuyatimiza, hakika utaweza kuacha pombe kabisa.
8. Jipongeze wewe mwenyewe kwa kipindi ulichoweza kuacha pombe
Kujipongeza wewe mwenyewe kunakupa hamasa ya kufanya jitihada zaidi katika mpango wako wa kuacha pombe. Kwa mfano ikiwa umeweza kukaa wiki moja bila kunywa basi jipongeze kwa hatua hii na ujitahidi sasa kukaa mwezi au hata mwaka bila kunywa.
9. Usikae na pesa za ziada
Mara nyingi watu wengi hununua pombe kwa sababu wana pesa mfukoni; wanapokuwa hawana pesa hawalewi kabisa. Jambo hili linaweza kuzuilika kwa kubadili mfumo wako wa kutunza pesa. Unaweza kufanya mambo yafuatayo:
Ikiwa unalipwa pesa kila siku, omba upokee malipo kwa mwezi badala ya kila siku. Ikiwa hili haliwezekani unaweza kumwomba mtu unayemwamini akutunzie pesa zako.
Tunza pesa zako kwenye mifumo ya kutunza pesa kama vile benki na simu za mkononi. Kwa kufanya hivi kutapunguza pesa ulizo nazo mkononi.
Kumbuka njia bora zaidi ni kumwomba mtu unayemwamini akutunzie pesa zako na akukabidhi tu pale unapokuwa na hitaji muhimu. Ikiwa una mwenzi mwaminifu anaweza kukusaidia sana kwa hili.
10. Jikumbushe na kutafakari madhara ya pombe
Unapotafakari madhara ya pombe kama vile matatizo ya kiafya, kisaikolojia, kijamii na hata kiuchumi ni wazi kuwa hili litakuhimiza zaidi kuacha pombe. Tafakari madhara ya pombe na uone kuwa unapokunywa pombe unayapata. Kwa kufanya hivi utajijengea fikra za kujitahidi kuacha pombe ili uepuke madhara hayo.
11. Tafuta usaidizi na ushauri wa kuacha pombe
Zipo taasisi na watu mbalimbali wanaowashauri watu walioathirika kwa matumizi ya pombe. Inawezekana ni asasi ya kiraia, kituo cha ushauri nasaha au hata taasisi au kiongozi wa kidini; hawa wote wanaweza kukushauri na kukutia moyo katika mkakati mzima wa kuacha kunywa pombe.
Jinsi ya kutengeneza Keki Ya Mbegu Za Mchicha
Viamba upishi
Unga ngano vikombc 3
Unga mbegu za mchicha kikombe 1
Baking powder vijiko vidogo
Maziwa kikombe 1
Sukari kikombe 1
Blue band kikombe ยฝ
Mayai 10-12
Hatua
โข Chagua, osha, kausha mbegu za mchicha mweupe, kisha saga zilainike.
โข Chekecha unga wa ngano, unga wa mbegu za mchicha na baking powder Kwenye bakuli kubwa.
โข Ongeza sukari na changanya.
โข Ongeza mayai kidogo, kidogo ukikoroga na mwiko kwenda njia moja mpaka ilainike.
โข Kama rojo ni zito ongeza mayai, au maziwa ili iwe laini, ongeza vanilla na koroga.
โข Paka mafuta kwenye chombo cha kuoka au sufuria na chekechea unga kidogo.
โข Mimina rojo ya keki na oka kwenye oveni au kama ni sufuria funika, weka moto mwingi juu, chini weka moto kidogo.
โข Ukinusia harufu nzuri ya vanilla, funua, choma kisu katikati ya keki, kama ni kavu epua, pozesha na pakua kama kitafunio.
Mapishi ya wali kuku wa Kisomali
Mahitaji ya wali
Mchele – 3 vikombe
Vitunguu (viliokatwa vidogo vidogo) – 2
Mafuta – 3 vijiko vya supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa – 1 kijiko cha chai
Bizari ya pilau – 1 kijiko cha supu
Mdalasini – 1 kijiti
Hiliki – 3 chembe
Pilipili manga nzima – chembe chache
Siagi – Vijiko 2 vya supu
Chumvi – kiasi
Mahitaji kwa kuku
Kuku kidari (Breast) kata vipande vipande – 2 LB
Mafuta – 3 vijiko vya supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa – 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi iliyosagwa – 1 kijiko cha supu
Kotmiri iliyokatwa ndogo ndogo – kiasi
Bizari ya pilau (cummin au jiyrah) – 1 kijiko cha chai
Pilipili kubwa tamu la kijani – 1
Pilipili kubwa tamu nyekundu – 1
(zikate vipande vipande)
Karoti iliyokunwa – 1 โ 2
Chumvi – Kiasi
Mapishi ya Wali:
Roweka mchele kwa muda fulani kutegemea mchele
Katika sufuria tia mafuta na kaanga vitunguu hadi vibadilike rangi kidogo.
Tia thomu iliyosagwa, mdalasini, bizari ya pilau, hiliki, pilipili manga na chumvi, kaanga kidogo.
Tia mchele kaanga kidogo, kisha tia maji ya moto kiasi kutegemea na aina ya mchele kama kawaida ya kupika wali kama pilau.
Tia sigai, funika upikike wali hadi uwive.
Mapishi ya Kuku:
Mchanganye kuku pamoja na thomu/tangawizi iliyosagwa, chumvi, pilipili mbichi.
Katika karai tia mafuta yapate moto vizuri.
Mtie kuku, bizari ya pilau (jiyrah) na ukaange, karibu na kuiva tia vitunguu.
Tia mapilipili makubwa, kotmiri, na kaanga kwa dakika moja tu uzime moto na epua weka kando.
Mbinu 4 anazotumia Shetani kuteka na kurubuni Watu
1. Kutushawishi tuache kusali maaana njia kuu ya mawasiliano kati yetu na MUNGU.Hivyo akifanikiwa hapo kwisha habari yako
2. Kufanya umwogope shetani na nguvu zake kuliko unavyompenda MUNGU. Wakristo wengi leo hii husali na kuomba kwa nguvu mno siyo sababu wanampenda MUNGU mno hapana ni sababu wanamwogopa shetani na majeshi yake na muda mwingine hata watumishi wa MUNGU wanamsaidia kwa kuhubiri mno na muda mwingine kuongeza jumvi juu ya nguvu za giza kuna wahubiri huambatanisha kila kitu na vifungo vya nguvu za giza na kusahau kuhubiri uzuri na wema wa MUNGU kwetu.
3.Kutufanya tusahau uwepo wake au kuupuzia. pale tunapokuwa hatupay attention existance ya shetani yeye ndio hupata wakati mzuri wa kutupiga ,sababu ni rahisi mno kutouutambua ubaya wa dhambi kama hatutaamini uwepo wa shetani ktk uovuโฆhii hutupelekea kutenda dhambi na kuziona siyo dhambi mfano kwa wasomi wengi hupuuzia baadhi ya mambo kama kujilinda na zinaa wakiamini ni kupitwa na wkt kama utakuwa hauna mahusiano ya kingono mpaka umefika chuo kikuu tena huchukulia wasiokuwa hivyo ni wagonjwa.hapo ni kuwa wengi wameignore uwepo wa shetani “no devil no evil” hivyo watu ndio hupotea.
4.KUTUTIA MOYO WAKATI WA KUTENDA DHAMBI NA KUTUKATISHA TAMAA YA KUSAMEHEWA. nitatoa mfano huu mtu ambaaye anataka kufanya uzinzi shetani humtia moyo kuwa MUNGU anajua kuwa sisi ni binadamu dhaifu na yeye husamehe dhambi zetu daima lakini ifikiapo wakati ukataka kutubu hafanya kila njia kukukatisha tamaa ya kusamehewa na hututia aibu hata kutsmka kwa padri kuwa nimedhini maana huanza kufikiria padre atanionaje mimi.
BASI NDUGU TUSISINZIE BALI TUWE MACHO DAIMA MSHITAKI WETU YU MACHO KUTUJARIBU.
Ulishawahi kupenda kwa namna hii??!!
Ushawai kumpenda dem na kumfia mazima kiasi kwmb anakwambia ye ana msela lkn we huelewi..unamkazia!!
Inabidi dem asisitize,”I HAVE ONLY ONE HEART,PLZ, I CANT LOVE TWO MEN”
Nawewe unaona haiwezekan,unamwambia ‘NIPENDE ATA NA KIDNEY’๐๐๐๐๐๐๐๐
Mambo ya msingi kwa mwanamke kuyajua unapojiremba
Kope nazo humpendezesha mwanamke kuna aina ya rangi za kupaka kwenye kope, lakini zinatofautiana. Ni vyema ukawasiliana na wataalamu wa mambo ya urembo kwa ushauri na siyo kukurupuka. Siyo umemuona fulani kapendeza na aina fulani ya rangi ya kwenye kope halafu na wewe ukakimbilia kupaka, utachekesha.
Rangi ya mdomo nayo ni eneo lingine linalompendezesha mwanamke. Ukweli ni kwamba tunatofautiana sana midomo wazungu wanaita โLipsโ Kila mwanamke ana tofautiana midomo na mwingine kwa hiyo hata rangi ya midomo nayo inakwenda sambambana aina ya lips na rangi ya ngozi ya mwili aliyo nayo mwanamke, siyo unajisiriba rangi ya mdomo halafu unaonekana kituko. Wasiliana na wataalamu wa urembo kwa ushauri zaidi.
Kucha kwa wanawake ni eneo lingine linolatakiwa kuwekwa katika unadhifu. Kuna baadhi ya wanawake unaweza kukutana nao kucha zao zimelika aidha kwa kung’atwa au kwa kuliwa na fangasi.
Ni vyema wanawake wenye tatizo hilo kumuona mtaalamu wa ngozi kwa msaada wa tiba. Unaweza kukutana na mwanamke kucha zake zimelika na zina sharp edges kiasi kwamba akikugusa utadhani umeguswa na msasa.
Au akishika Glasi ya Kinywaji ukiangalia kucha utadhani mkono ni wa mwanaume maana kwa jinsi kucha zake zilivyo hata hafanani nazo. Kuna kucha za bandia kama mwanamke ana matatizo ya kucha basi akazinunue kusitiri aibu.
Marashi, manukato au unyunyu kama wanavyoita vijana wa mjini ni muhimu kwa wanawake lakini ni vyema nikaweka angalizo. Haipendezi kwa mwanamke anayepulizia manukato yanayonukia sana mpaka yakawakera wengine ni vyema wanawake wakajipulizia marashi yenye staha na yasiyokera.
Ngozi ya mwanamke ni bora โsensitiveโ sana na inaakiwa ipakwe aina ya mafuta au lotion yenye virutubisho kulingana na aina ya Ngozi. Kuna wanawake wenye Ngozi ya mafuta โOil Skinโ kuna wenye Ngozi mchanganyiko na kuna wale wenye ngozi kavu (Dry Skin).
Ni vyema mwanamke kujua aina ya ngozi yake ili ajie aina ya product ya ngozi anayopaswa kutumia na siyo kwa sababu umemuona mwenzio anapaka aina fulani ya losheni na wewe unakimbilia kununua. Omba ushauri kwa wataalamu wa ngozi watakusaidia. Kuna baadhi ya maduka yanyouza vipodozi wanatoa msaada huo bure kabisa.
Kichekesho cha mtalii na mbongo
Duh! Sikubali bora mbavu zituume wote!
Watalii wana dharau sana bana, Mtalii alikodi boti akazunguka nayo kwenye mto Rufiji kuangalia mandhari, akamuuliza kijana anayeongoza boti, “Do you know Biology, Psychology and Anthropology?” Kijana akajibu “NO,” Mtalii akamwambia “nothing you know under the sun? You are useless, and u’ll die with your illiteracy!” baada ya muda boti ikaanza kuzama, kijana akamwambia mtalii “Do you know kuogelealogy and kusepalogy from mambalogy? Mtalii akajibu huku ametoa macho “No” kijana akamwambia “You will kufalogy and mambalogy wil eat your matakology because of your bad-mdomology..๐๐๐๐๐๐
Recent Comments