Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya

Jinsi ya kutengeneza juisi ya nyanya

Viamba upishi

Nyanya 1 kg
Maji Iita ½
Chumvi kijiko kidogo 1
Sukari

Hatua

• Osha nyanya, katakata na chemsha na maji mpaka zilainike.
• Chuja juisi.
• Pima juisi – vikombe 2 vya juisi kwa kikombe 1 cha sukari, weka
kwenya sufuria safi .
• Ongeza chumvi, chemsha ukikoroga mpaka ichemke.
• Mara ikichemka epua, pozesha na weak kwenya chombo safi kwa
kunywa.

Jinsi ya kutengeneza Biskuti Ya Keki Kavu (Shortcake)

VIAMBAUPISHI

Unga – 2 Magi (vikombe vya chai)

Sukari iliyosagwa – 2/3 Magi (kikombe cha chai)

Siagi – 220 g

Unga wa mchele – ½ Magi

Yai -1

Vanilla – 1 kijiko cha chai

MAANDALIZI

Changanya vitu vyote hivyo kwenye bakuli mpaka unga ushikamane.
Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30 cm au (8 in kwa 12 in)
Choma kwenye moto 325˚C kwa muda wa saa nzima au mpaka ibadilike kuwa rangi ya dhahabu.
Epua acha ipoe kisha kata vipande kama mstatili, weak kwenye sahani tayari kunywewa na chai.

NYONGEZA

Kwa unga huo huo unaweza kutengeneza vibiskuti vya duara duara.

Jinsi ya kuandaa Pilau ya sosi ya soya, nyama na mboga

Mahitaji

Nyama isiyokuwa na mifupa – 1 ½ Lb(ratili)
Mchele wa Basmati (rowanisha) – 3 Magi
Vitunguu maji – 2
Mchanganyiko wa mboga za barafu – 1 Magi
(karoti, mahindi, njegere)
Pilipili Mbichi – 3
Pilipili mboga kijani na nyekundu – 1
Pilipili manga – ½ kijiko cha chai
Chumvi – Kiasi
Sosi ya soya (soy sauce) – 5 Vijiko vya supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa – 1 Kijiko cha supu
Mchanganyiko wa bizari (garam masala) – 1 Kijiko cha supu
Kotmiri iliyokatwa – ½ Kikombe
Mafuta ya kukaangia – Kiasi

Namna Ya Kutaarisha

Ndani ya sufuria, tia mafuta yakipata moto kaanga vitunguu mpaka ziwe rangi ya hudhurungi.
Kisha tia nyama iliyokatwa vipande vidogo vidogo pamoja na maji ya kiasi na viungo vyote isipokuwa mchele, mboga zote na kotmiri. chemsha mpaka nyama iwive na maji yakauke.
Halafu changanya na mboga na iwache kwa muda wa dakika kumi kisha tia kotmiri na umimine kwenye bakuli au treya ya oveni na uweke kando.
Chemsha mchele na chumvi uwive kama kawaida ya kupika wali wa kuchuja, kisha umwagie juu ya ile treya ya nyama.
Nyunyizia mafuta na sosi ya soya na ipike katika oveni moto wa 350° kwa muda wa dakika 20 hivi.
Ukishawiva, uchanganye ukiwa tayari kwa kuliwa

Jinsi ya kutengeneza Muhogo Wa Nazi Na Samaki Wa Kukaanga

Mahitaji

Muhogo – 3

Tui La Nazi – 2 vikombe

Chumvi – kiasi

Pilipili mbichi – 2

Mafuta – 1 kijiko moja

Kitunguu maji – 1 kidogo

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Chambua muhogo ukatekate au tumia iliyo tayari.
Chemsha muhogo katika sufuria kwa maji kidogo na chumvi, funika uive muhogo.
Karibu na kukauka maji tia tui, kitunguu maji ulichokatakata na pilipili mbichi.
Unaupika moto mdogo mdogo hadi ukauke tayari kuliwa na samaki au kitoweo chochote kingine

Mapishi – Saladi ya Matunda

Matunda ni mojawapo wa kundi la vyakula, ni muhimu sana kwa afya bora. Matunda yakitengenezwa vizuri yanavutia sana na yanakuwa ni chakula kizuri sana.

Mahitaji

Embe iliyoiva kiasi
Nanasi
Tango
Tikiti maji
Zabibu
Papai

Matayarisho

1. Ondoa maganda kwenye embe, nanasi, tango, papai na tikiti maji kisha kata kata vipande vidogo vidogo vya mraba

2. Changanya vipande vya matunda kwenye bakuli safikisha weka na zabibu zilizotolewa kwenye kikonyo chake.

3. Weka kwenye friji yapate ubaridi kidogo

4. Saladi yako tayari kwa kuliwa

Waweza kula saladi hii kama mlo wa kati au kama mlo kamili wa usiku.

Mapishi ya Maharage

Mahitaji

Maharage (beans 2 vikombe vya chai)
Nazi (coconut milk kiasi)
Vitunguu maji (onion 1kikubwa)
Nyanya (fresh tomato 1)
Kitunguu swaum (garlic paste 1/4 kijiko cha chai)
Chumvi (salt kiasi)
Curry powder 1 kijiko cha chai
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Chemsha maharage mpaka yaive kisha yaweke pembeni. Kaanga vitunguu maji na mafuta mpaka vianze kuwa vya brown kisha weka kitunguu swaum,nyanya na curry powder. kaanga mpaka nyanya iive kisha tia maharage na chumvi kiasi. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri. Baada ya hapo tia tui la nazi na ukoroge vizuri na uache lichemke mpaka liive. Baada ya hapo ipua na maharage yatakuwa tayari kwa kuliwa

Jinsi ya kupika vizuri Wali Wa Karoti Na Nyama

MAHITAJI YA WALI

Mchele – 3 Magi

Mafuta – 1/4 kikombe

Karoti unakata refu refu – 3

Vitunguu maji kata vikubwa vikubwa – 1 kikubwa

Pilipli manga – 1/2 kijicho chai

Hiliki – 1/2 kijiko chai

Karafuu ya unga – 1/4 kijiko cha chai

Mdalasini wa unga – 1/2 kijiko cha chai

Zaafarani (ukipenda) roweka katika maji – 1 kijiko cha chai

Zabibu kavu (ukipenda) – 1/4 kikombe

Chumvi kiasi

KUPIKA WALI

Kwenye sufuria tia mafuta na kaanga karoti kidogo.
Tia vitunguu kisha tia bizari zote.
Tia maji kiasi (kutegemea aina ya mchele) na chumvi
Tia mchele upike uwive.
Karibu na kuwvia tia zabibu ukipenda.
Funika endelea kuupika hadi uwive.

MAHITAJI KWA NYAMA

Nyama – 2 Ratili (LB)

Chumvi – Kiasi

Mafuta – 1/4 kikombe

Kitunguu (kata virefu virefu) – 1 Kikubwa

Pilipili mboga kubwa – 2 ukipenda moja nyekundu moja kijani unazikata vipande virefu virefu.

Figili mwitu (celery) kata vipande virefu virefu- Miche miwili.

KUPIKA NYAMA

Chemsha nyama hadi iwive
Ikaange kwa mafuta hadi iwe nyekundu
Weka vitunguu, pilipili mboga na figili mwitu
Kaanga kidogo tu kama dakika moja.
Tayari kuliwa na wali.

Mapishi – Kisamvu cha Karanga

Mapishi yetu leo ni kisamvu cha kuchanganya na karanga. Karibu.

Mahitaji

Majani ya kisamvu
Karanga nusu kikombe
kitunguu kimoja
nyanya mbili
karoti moja
mafuta na chumvi kiasi

Matayarisho

1. Osha kisamvu chako vizuri kisha katakata vipande vidogo vidogo

2. Unaweza kutwanga kwa kutumia kinu au kuchemsha kidogo na kisha kusaga kwa kutumia mashine. Ukitumia mashine uwe makini usije ukasaga sana ukaharibu.

3. Kaanga karanga kidogo na kisha zisage ziwe unga unga.

4. Chemsha kisamvu chako hadi kiive.

5. Katakata kitunguu, karoti na na nyanya

6. Anza kuunga kisamvu kwa kukaanga vitunguu, weka karoti na kisha nyanya na vikishaiva weka kisamvu na koroga pamoja kisha weka karanga. Acha vichemke kwa muda na unaweza pia weka na nazi tui la kwanza.

7. Baada ya muda mfupi epua na kitakiwa tayari. Waweza kula kwa ugali, wali, chapati, makande n.k

Mapishi ya Bokoboko La Kuku

Mahitaji

Ngano nzima (shayiri) – 3 Vikombe

Kuku – ½ (3 LB takriban)

Thomu na tangawizi iliyosagwa – 1 kijko cha supu

Pilipili manga ya unga – ½ kijiko cha chai

Jiyrah (cumin/bizari ya pilau) – ½ kijiko cha chai

Chumvi – kiasi

Kidonge cha supu – 1

Samli ya moto – ½ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Roweka ngano (shayiri) tokea usiku au muda wa masaa.
Katakata kuku mtie katika sufuria, tia maji kiasi viungo vyote. Mchemeshe awive na ibakie supu yake.
Toa kuku, toa mifupa na umchambue chambue vipande vidogo vidogo.
Chemisha ngano (shayiri) kwa kufunika sufuria hadi iwive na kukauka maji.
Tia supu ya kuku katika ngano (shayiri), na kuku uliyemechambua. Tia kidonge cha supu.
Tia samli nusu (bakisha nusu) kisha songa mchanganyiko uchanganye hadi ivurugike kuku na ngano (shayiri) vizuri.
Mimina katika sahani, mwagia samli imoto ilyobakia likiwa tayari.

Mapishi ya Biskuti Za Kastadi

VIAMBAUPISHI

Unga 6 Vikombe

Sukari ya kusaga 2 vikombe

Siagi 500 gm

Baking powder 1 Kijiko cha chai

Kastadi ½kikombe

MAPISHI

Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy).
Mimina mchanganyiko uliopiga kwa mashine kwenye bakuli.
Tia unga na baking powder na Kastadi.
Kata usanifu (design) unaopenda halafu panga kwenye sahani ya kupikia (baking tray).
Pika (bake) katika oven moto wa 350° F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.

Jinsi ya kutengeneza Rock-cakes Za Njugu Na Matunda Makavu

Mahitaji

Unga – 4 Vikombe

Sukari -10 Ounce

Siagi – 10 Ounce

Mdalasini ya unga – 2 vijiko vya chai

Matunda makavu/njugu (kama lozi, Zabibu, maganda ya chungwa, Cherries na kadhalika – 4 ounce

Maziwa ya maji – 4 Vijiko vya supu

Maandalizi

Chukua siagi na sukari koroga na mixer mpaka iwe kama cream.
Tia vanilla mdalasini, tia yai moja mix tena endelea kuongeza yai lingine mpaka umalize yote, changanya mpaka iwe laini kama sufi (fluffy)
Tia unga na baking powder na dried fruits, changanya na mwiko.
Chota mchanganyiko na kijiko cha soup weka kwenye treya ya kupikia tandaza na uma ili upate matundu juu ya biskuti.
Pika (bake) kwenye oven lenye moto wa 375 F. kwa muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.

Jinsi ya kupika Wali Wa Samaki Na Mboga

VIPIMO VYA SAMAKI

Samaki wa sea bass vipande – 1 1/2 LB (Ratili)
Kitunguu saumu(thomu/galic) -1 Kijiko cha supu
pilipili mbichi iliyosagwa – 1 Kijiko cha chai
Bizari ya manjano au ya pilau – 1/2 Kijiko cha chai
Paprika ya unga au pilipili ya unga – 1 kijiko cha chai
Chumvi – Kiasi
Ndimu
Mafuta – 3 Vijiko vya supu

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Roweka samaki kwa viungo hivyo vyote kwa muda wa robo saa hivi.

Washa oven moto wa 400F.
Kisha weka samaki katika trea na choma kwa muda wa dakika 15 na weka moto wa juu dakika za mwisho ili ipate rangi nzuri.
Ikishaiva epua na itakuwa tayari kuliwa.

VIPIMO VYA MBOGA

Gwaru (green beans) – 1 LB
Kitunguu saumu(thomu/galic) – 1 kijiko cha supu
Karoti – 4-5
Chumvi – Kiasi
Bizari ya manjano – 1/2 Kijiko cha chai
Pilipili manga – 1/4 kijiko cha chai
Mafuta ya zaituni – Kiasi

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Kata kata karoti na toa sehemu ya mwisho za binzi.
Weka mafuta katika sufuria kisha kaanga karoti na gwaru
Kisha weka moto mdogo na funika ili ziwive na sio kuvurujika.
Karibu na kuiiva tia thomu kaanga kidogo,tia bizari ,chumvi na pilipili manga.
Ikisha changanyikana vizuri epua na tayari kuliwa na wali na samaki.

Jinsi ya kupika Baklawa Za Pistachio Na Lozi

VIAMBAUPISHI

Philo (thin pastry) manda nyembamba – 1 paketi

Siagi – ¼ Kikombe cha chai

Baking powder – 2 Vijiko vya chai

Pistachio/ lozi – 2 vikombe vya chai

Mafuta – ½ Kikombe

VIAMBAUPISHI VYA SHIRA

Sukari – 2 Vikombe vya chai

Maji – 2 ½ Vikombe vya chai

ndimu – ½ kijiko cha chai

JINSI YA KUANDAA

Tafuta treya iliyokuwa sawa na ukubwa wa hizo manda nyembamba (philo) au zikate hizo manda kwa ukubwa wa treya (mraba au mstatili)
Kisha yeyusha siagi changanya na mafuta.
Kisha panga manda moja pakaza mafuta juu yake kisha weka manda nyingine juu yake kisha pakaza mafuta tena weka manda nyingine juu yake, endelea kufanya hivyo mpaka ziwe kama sita au saba kisha nyunyizia pistachio na lozi halafu panga tena manda na mafuta manda na mafuta tena sita au saba kisha nyunyizia tena pistachio na lozi.
Panga namna hivyo mpaka treya ijae inapofika manda ya mwisho kata vipande vya mraba vidogodogo humo humo kwenye treya kisha nyunyizia mafuta yaliyobaki.
Washa moto wa oven 350°F kwa muda wa dakika 20 au hadi rangi ibadilike kidogo (isikauke sana)
Chemsha syrup yako kama shira ya majimaji lakini isiwe nzito sana ikishakuwa tayari mwisho tia ndimu acha ipoe kidogo kisha miminia juu ya treya yote halafu malizia kunyunyizia pistachio na lozi zilizobaki.
Zikishakuwa tayari zipange kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

ANGALIZO

Ukishatoa treya kwenye oven wacha ipoe kidogo na syrup yako pia wacha ipoe kidogo kabla hujamimina, ukitia ya motomoto zitalainika.
Manda nyembamba za baklawa zinauzwa tiyari madukani kwenye pakiti.

Kujifunza Misingi ya Upishi Bora kwa Afya Yako

Kujifunza misingi ya upishi bora kwa afya yako ni hatua muhimu katika kuboresha maisha yako na kuhakikisha una lishe bora. Upishi bora unaweza kuboresha afya yako kwa kiasi kikubwa na kukufanya ujisikie vizuri kimwili na kiakili. Kwa hivyo, katika makala haya, nitakupa vidokezo kadhaa juu ya jinsi ya kujifunza misingi hii na kufurahia chakula chenye afya.

Kwanza kabisa, unahitaji kuelewa umuhimu wa vyakula vyenye afya katika maisha yako. As AckySHINE, naomba usisahau kwamba chakula ni kama mafuta ya injini ya gari. Ikiwa unaingiza mafuta mabaya, gari lako haliwezi kuendesha vizuri. Vivyo hivyo, kula chakula kisicho na afya kunaweza kuathiri afya yako. Kwa hivyo, kufahamu vyakula vyenye afya ni muhimu sana.

🥦 Chagua vyakula vyenye afya: Kula matunda na mboga mboga mbalimbali, kupunguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari, na kula protini zenye afya kama samaki, kuku, na maharage.

🍓 Ongeza matunda kwenye lishe yako: Matunda ni chanzo kizuri cha vitamini, madini, na nyuzi ambazo zinasaidia kuimarisha mwili wako na kulinda dhidi ya magonjwa. Kwa mfano, kula tunda moja la parachichi kila siku linaweza kuboresha afya yako ya moyo.

🥗 Jumuisha mboga mboga katika milo yako: Mboga mboga zina virutubishi muhimu kama vile vitamini, madini, na nyuzi. Kula mboga mboga kama vile spinach, karoti, au matango kila siku kunaweza kuimarisha kinga yako na kukuweka katika hali nzuri ya afya.

🍽️ Pima sehemu ya kula: Kula sehemu ndogo lakini za usawa ni muhimu sana. Kujaza sahani yako na vyakula vyenye afya kama protini, nafaka nzima, na mboga mboga, na kupunguza ulaji wa vyakula vinavyoongeza uzito kama vile vyakula vyenye mafuta mengi na sukari.

🥛 Unywaji wa maji: Kunywa maji mengi ni muhimu kwa afya ya mwili na akili. Inashauriwa kunywa angalau lita mbili za maji kwa siku ili kuhakikisha mwili wako unakuwa vizuri.

🍽️ Pika chakula chako mwenyewe: Badala ya kununua chakula kilichotengenezwa tayari au chakula cha haraka, jaribu kupika chakula chako mwenyewe. Hii itakupa udhibiti zaidi juu ya viungo na utengenezaji wa chakula chako na kukusaidia kudumisha lishe bora.

🥦 Jaribu mapishi mapya: Kujifunza misingi ya upishi haimaanishi unapaswa kuwa mpishi wa kitaalam. Jaribu mapishi mapya na ubunifu na ujifunze jinsi ya kutengeneza chakula kitamu na chenye afya. Kwa mfano, weka ndizi kwenye smoothie yako badala ya sukari ili kuongeza ladha na virutubishi.

🍗 Punguza ulaji wa chumvi na sukari: Chumvi na sukari nyingi katika lishe yako zinaweza kuwa hatari kwa afya yako. Kula kiasi kidogo cha chumvi na sukari inaweza kusaidia kupunguza hatari ya magonjwa kama vile shinikizo la damu na kisukari.

🍽️ Panga milo yako: Kuweka ratiba ya milo yako na kuhakikisha unakula mara kwa mara ni muhimu sana. Kula milo kubwa mara kwa mara inaweza kusababisha ongezeko la uzito na matatizo mengine ya kiafya. Jaribu kula milo midogo mara kwa mara ili kuweka viwango vya nishati yako sawa.

🥗 Toa kipaumbele lishe: Unapopanga chakula chako, hakikisha unatoa kipaumbele lishe. Jumuisha chakula chenye afya kwenye orodha yako ya ununuzi na epuka kununua vyakula visivyo na afya. Kwa mfano, chagua mkate wa nafaka nzima badala ya mkate wa ngano iliyosafishwa.

🍓 Tumia viungo vyenye afya: Kuna viungo vingi vyenye afya ambavyo unaweza kuingiza kwenye milo yako ili kuongeza ladha na virutubishi. Kwa mfano, unaweza kuongeza parachichi kwenye sandwich yako badala ya mayonnaise ili kupunguza ulaji wa mafuta.

🍽️ Fanya chakula kiwe raha: Kujifunza misingi ya upishi bora haimaanishi kuwa chakula chako lazima kiwe kisicho na ladha. Emba ubunifu na utafute njia za kufanya chakula chako kiwe raha na kitamu. Kwa mfano, unaweza kutumia viungo mbalimbali na vyakula vya kipekee ili kubadilisha ladha ya sahani yako.

🥗 Punguza matumizi ya vyakula vya haraka: Vyakula vya haraka mara nyingi huwa na mafuta mengi, sukari, na chumvi nyingi. Kula vyakula vyenye afya zaidi kama vile saladi, sandwiches za nyumbani, au supu mboga. Hii itakusaidia kudumisha afya njema na kuepuka magonjwa.

🍓 Kula kwa utaratibu: Epuka haraka haraka wakati wa kula na kula kwa utaratibu. Kupunguza kasi ya kula kunaweza kukusaidia kuhisi kamilifu haraka na kuzuia kula zaidi. Kwa mfano, chukua dakika 20 kuweka chakula kwenye sahani yako na kula taratibu.

Kujifunza misingi ya upishi bora kwa afya yako ni uwekezaji muhimu katika maisha yako. Kwa kufuata vidokezo hivi, unaweza kuboresha afya yako na kufurahia chakula chenye afya na kitamu. Kumbuka kula kwa usawa, kufurahia mlo wako, na kufanya chaguo sahihi kwa afya yako. Je, una mawazo yoyote au maoni? Nipendekeze kuongeza nini katika vidokezo hivi?

Mapishi ya wali wa mboga

Mahitaji

Wali uliopikwa (cooked rice) kiasi
Hoho la kijani (green pepper) 1/2
Hoho jekundu (red pepper) 1/2
Carrot 1
Kitunguu kikubwa (onion) 1
Njegere (pears) 1/2 kikombe cha chai
Mayai (eggs) 2
Uyoga (mushroom) 2 vikombe vya chai
Soy source 2 vijiko vya chakula
Chumvi (salt) kiasi
Mafuta (veg oil) 3 vijiko vya chakula

Matayarisho

Katakata hoho, kitunguu,na uyoga vipande vikubwa kiasi(chunks) kisha katakata carrot zisiwe nene au nyembamba sana. Baada ya hapo weka mafuta katika katika frying pan yako isiyoshika chini acha yapate moto kisha tia uyoga na ukaange mpaka uive.Baada ya hapo tia vegetable zote na uzikaange pamoja na uyoga kwa muda wa dakika 2, kisha katika hiyohiyo frying pan zisogeze vegetable zako pembeni (ili kupata nafasi ya kukaangia mayai).Yakaange mayai katika hiyo sehemu yakiisha iva yavuruge na kisha yachanganye pamoja na vegetable na kisha tia chumvi kidogo sana. Baada ya hapo malizia kwa kutia wali na soy source kisha koroga vizuri mpaka mchanganyiko wako wote uchanganyike vizuri (hakikisha wali unapata moto na vegetable haziivi sana) . Na baada ya hapo chakula chako kitakuwa tayari.

Mapishi ya Biriyani Ya Kuku

Vipimo

Mrowanishe kuku na viungo hivi kwa muda mdogo tu

Kuku (Mkate kate Vipande) – 4 LB

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi – 2 Vijiko vya supu

Chumvi – kiasi

Pilipili nyekundu ya unga – 1 Kijiko cha supu

Bizari ya manjano (Haldi au Tumeric) – 1 Kijiko cha chai

Bizari ya pilau ya powder (Jeera) – 1 Kijiko cha chai

Gilgilani powder (Dania) – 1 Kijiko cha chai

Ndimu – 1 Kijiko cha supu

Mchele na vitu vya Masala:

Mchele (Basmati mzuri) (rowanisha) – 7 cups

Mafuta ya kupikia – kiasi

Vitunguu Vilivyokatwa – 8

Nyanya iliyokatwa katwa – 3

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi – 1 Kijiko cha supu

Garam Masala -1 Kijiko cha supu

Hiliki powder – ½ Kijiko cha chai

Tomatoe paste – 1 Kijiko cha supu

Pilipili mbichi zipasue katikati – 4

Chumvi – kiasi

Mtindi – 4 Vijiko vya supu

Kotmiri iliokatwa (Chopped) – ½ Kikombe

Mafuta ya kunyunyuzia katika wali – 3 Vijiko vya supu

Zaafarani au rangi ya biriani – kiasi

Namna Ya Kutaarisha Na Kupika

Weka kuku aliyerowanishwa na viungo vyake katika Foil tray au chombo chocote utakachomwagia wali humo humo na kupikia biriani, kisha mchome (Bake) mpaka awive na awe mkavu kiasi.

Wakati kuku anapikika, kaanga vitunguu katika karai au sufuria mpaka viwe brown na epua nusu yake weka kando.

Punguza mafuta yabakie kiasi tu, ongeza Thomu na tangawizi, na viungo vyote vya hapo juu isipokuwa Mtindi na kotmiri, endelea kukaanga hadi tomatoe zilainike.

Ongeza chumvi, malizia mwisho kwa kutia mtindi, kotmiri na vile vitunguu ulivyoweka kando. Masala yako tayari.

Mwagia masala juu ya kuku uliyekwishmpika changanya vizuri.

Chemsha Mchele uwive nusu, chuja na mwagia juu ya masala.

Nyunyiza mafuta kidogo juu ya mchele na zaafarani au rangi ya biriani.

Bake katika moto wa 350 – 400 kwa muda wa 15 – 20 minutes. Biriyani imekuwa tayari kuliwa.

Mtindi wa kutolea Biriyani:

Mtindi – 1 kikombe

Pilipili mbichi – 1 ndogo

Kitunguu saumu(/galic) thomu – chembe mbili

Nanaa – kiasi

Chumvi – chembe tu

Weka kwenye Blender na uchanganye, kisha mimina katika bakuli

Jinsi ya kupika Cookies Za Jam Ya Peach Na Raspberry

MAHITAJI

Unga kikombe 1 ½

Siagi ½ kikombe

Sukari ½ kikombe

Yai 1

Vanilla 1 kijiko cha chai

Jam ya peach na raspberry

MAANDALIZI

Wash oven moto wa takriban 180 – 190 Deg F
Piga siagi na sukari katika mashine mpaka iwe laini na nyororo (creamy) kisha weka yai na vanilla.
Tia unga kidogo kidogo uchanganye kwa mwiko wa mbao (wooden spoon).
Pakaza mkononi unga uchukue vidonge ubonyeze kufanya vishimo vya kuwekea jam.
Panga katika treya uliyopakaza siagi.
Tia nusu yake jam ya peach na nusu jam ya raspberry
Bake katika oven kiasi robo saa mpaka ziwive na kugeuka rangi ya brown light.
Epua vikiwa tayari

Mapishi ya Wali Wa Mboga Na Mchuzi Wa Kuku wa Tanduri

Vipimo vya Wali:

Mchele basmati – 3 magi (kikombe kikubwa)

Mchanganyiko wa mboga za barafu

(Frozen vegetables) – 1 ½ mug

Chumvi – kiasi

Mafuta – 3 vijiko vya chakula

Kitungu maji (kilichokatwa) – 1

Bizari ya pilau (nzima) – 1 kijiko cha chakula

Namna Ya kutayarisha na kupika:

Osha mchele uroweke kwenye maji muda wa dakika 20.
Chemsha maji kwenye sufuria kama magi 6.
Tia chumvi.
Yakisha kuchemka unatia mchele, chemsha usiive sana, uive nusu kiini. Mwaga maji na kuchuja wali.
Unamimina Yale mafuta kwenye sufuria unakaanga bizari ya pilau kidogo na kitunguu kabla ya kugeuka rangi ya hudhurungi (brown).
Tia mchanganyiko wa mboga za barafu.,
Mimina wali, changanya vizuri, ufunike na uweke katika moto mdogo kwa dakika 20.
Pakua tayari kwa kuliwa.

Vipimo Vya Mchuzi

Kuku – 2 Ratili (LB)

Chumvi – Kiasi

Mafuta – ¼ Kikombe

Nyanya Kata vipande – 4

Nyanya kopo – 2 vijiko wa chakula

Tangawizi – 1 kijiko ya chakula

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 1 kijiko ya chakula

Tanduri masala – 1 kijiko cha chakula

Kotmiri liliyokatwa – 3 vijiko vya chakula

Pilipili mbichi – 2

Pili masala – 1 kijiko cha chakula

Garam masala – ½ kijiko cha chakula

Bizari manjano – ½ kijiko cha chakula

Mtindi – 3 vijiko vya chakula

Pilipili boga (kata vipande virefu) – 1

Ndimu – 2 vijiko vya chakula

Namna ya kutayarisha na kupika:

Kwenye bakuli tia kuku na changanya vitu vyote pamoja isipokua mafuta.
Tia mafuta kwenye sufuria yakisha kupata moto mimina kuku umpike kwa muda ½ saa kwa moto kiasi.
Pakua kuku kwenye bakuli au sahani na ukate vitunguu maji duara na umpambie. Tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Mitai

VIAMBAUPISHI

Unga wa ngano – magi 2 (vikombe vikubwa)

Hamira kijiko 1 cha chai

Sukari Vijiko 2 vya supu

Maziwa ¾ Magi

Siagi Vijiko 2 vya supu

Mafuta ya kukaangia kiasi

VIAMBAUPISHI:SHIRA

Sukari ¾ Kikombe

Maji ¾ Kikombe

Illiki ya unga kiasi

Zafarani kiasi

JINSI YA KUPIKA

Katika bakuli, changanya vipimo vyote pamoja na ukande unga usiwe mgumu wala laini sana uwe kiasi.
Kisha fanya donge moja na iache pahali penye joto mpaka iimuke.
Halafu weka mafuta ya kukaangia kwenye moto.
Sukuma donge hadi liwe duara sio nyembamba sana, kisha katakata kama maandazi.
Mafuta ya kisha pata moto choma mittai hukuunazigeuza hadi ziwive na kugeuka rangi.
Katika sufuria tia vipimo vya shira na iache ichemke isiwe nzito sana.
Mimina mitai kwenye shira na uzipepete, kisha weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Shopping Cart
2
    2
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About