Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya

Jinsi ya kutengeneza Fagi Ya Kumumunyuka Mdomoni

VIAMBAUPISHI

Maziwa mazito matamu (condensed milk) – 2 vibati

Sukari – 1 kikombe

Samli 1 ยฝ kikombe

Vanilla 2 kifuniko cha chupa yake

Hiliki ilosagwa – 2 vijiko vya chai

Sinia kubwa ya bati Paka samli

MAANDALIZI

Changanya maziwa, sukari na samli katika sufuria isiyogandisha chakula (non-stick) uweke katika moto.
Koroga huku ikipikika hadi ianze kugeuka rangi na kuanza kuachana. Usiache mkono kuroga isije kufanya madonge.
Tia hiliki na vanilla, endelea kuipika.
Itakapogeuka rangi vizuri mimina katika sinia na haraka uitandaze kwa mwiko huku ukiuchovya katika maji na kuendelea kuitandaza hadi ikae sawa kote.
Pitisha kisu kuikataka ili ikipoa iwe wepesi kuitoa vipande.

Kila inapozidi kupoa na kukaa ndipo fagi inakauka na kumumunyuka.

Jinsi ya kupika Biskuti Za Njugu/Matunda Makavu (Rock Cakes)

Viambaupishi

Unga 4 Vikombe

Sukari 10 Ounce

Siagi 10 Ounce

Mdalasini ya unga 2 vijiko vya chai

Matunda makavu/njugu (kama lozi,
Zabibu, maganda ya chungwa,
Cherries na kadhalika 4 ounce

Maziwa ya maji 4 Vijiko vya supu

Jinsi ya kuandaa na kupika

1) Chukua siagi na sukari koroga na mixer mpaka iwe kama cream.

2) Tia vanilla mdalasini, tia yai moja mix tena endelea kuongeza yai lingine mpaka umalize yote, changanya mpaka iwe laini kama sufi (fluffy)

3) Tia unga na baking powder na dried fruits, changanya na mwiko.

4) Chota mchanganyiko na kijiko cha soup weka kwenye treya ya kupikia tandaza na uma ili upate matundu juu ya biskuti.

5) Pika (bake) kwenye oven lenye moto wa 375ย F. kwa muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.

Mapishi ya wali Wa Nazi Kwa Mchuzi Wa Nyama Ngโ€™ombe Na Mchicha

Wali Wa Mpunga

Mchele wa mpunga – 4 Vikombe

Tui la nazi – 6 vikombe

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mchele kisha

Bandika tui jikoni likichemka tia mchele na chumvi.

Funika uchemke, tui likikauka wacha moto mdogomdogo hadi wali uive ukiwa tayari. Ikiwa unatumia mkaa unapalia juu yake.

Mchuzi wa nyama Ngโ€™ombe

Nyama – 1 kilo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa -2 viijiko vya supu

Viazi/mbatata – 2

Kitunguu maji kilokatwakawa (slice ndogo) – 2

Nyanya/tungule – 4

Nyanya kopo – 3 vijiko vya supu

Majani ya mchuzi/mvu – 3 msongo (bunches)

Bizari ya mchuzi (simba 2) – I kijiko cha chai

Ndimu – 1 kamua

Mafuta – ยผ kikombe

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Weka nyama katika sufuri, tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi, ndimu na chemsha nyama hadi iwive na ibakie supu yake kidogo.
Weka mafuta katika sufuri nyingine, kaanga kitunguu. Vinapogeuka rangi tia majani ya mchuzi endelea kukaanga hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (golden brown)
Tia nyanya/tungule, viazi/mbatata, endelea kukaanga mpaka nyanya ziive.
Tia nyama na supu yake kisha tia nyanya ya kopo, kotmiri, bizari ya mchuzi, chumvi uache mchuzi kidogo katika moto hadi viazi viive vikiwa tayari.

Mboga Mchicha

Mchicha – 4 michano/vifungu

Kitunguu – 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 3

Nyanya/tungule – 2

Tui la nazi zito – 1 kikombe cha chai

Chumvi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mboga iache ichuje maji.
Ikatekate kisha weka katika sufuria.
Katika kitunguu maji, kitunguu thomu kisage au kikatekate kidogodogo (chopped), nyanya.
Weka jikoni ipikike kwa maji yake na mvuke.
Tia tui endelea kuweka katika moto mdogomdogo hadi ikaribie kukauka ikiwa tayari.

Mawazo Rahisi na yenye Afya ya Kujiandaa kwa Chakula cha Kazi

Mawazo Rahisi na yenye Afya ya Kujiandaa kwa Chakula cha Kazi

Kwa mara nyingine tena, hapa ni AckySHINE nikikuletea mawazo bora na yenye afya ya kujiandaa kwa chakula cha kazi. Kama unavyojua, chakula ni nishati muhimu katika kuwezesha utendaji wetu wa kazi. Kwa hiyo, ni muhimu sana kuwa na chakula bora na kilicho na lishe ili kuboresha ubora wa kazi zetu. Hapa kuna orodha ya mawazo 15 rahisi na yenye afya ya kujiandaa kwa chakula cha kazi:

  1. ๐ŸŽ Kula matunda na mboga safi kama tunda la kifungua kinywa. Matunda na mboga ni chanzo kikubwa cha vitamini na madini muhimu kwa afya yetu.

  2. ๐Ÿ— Chagua protini nzuri kama kuku, samaki au maharagwe kama sehemu ya chakula cha mchana. Protini ni muhimu kwa ukuaji na ukarabati wa misuli yetu.

  3. ๐Ÿฅฆ Ongeza mboga za majani kama spinach na kale kwenye sahani yako. Mboga hizi zina virutubisho muhimu kama chuma na vitamini C.

  4. ๐Ÿฅช Jenga sandwishi zenye afya kwa kutumia mkate wa ngano nzima, mboga mbalimbali na protini kama turkey au tofu. Hii itakupa nishati ya kutosha na kukusaidia kuhimili mawasiliano ya kazi yako.

  5. ๐Ÿ“ Tumia matunda kama vitafunio vya asili. Matunda yana virutubisho na sukari asili ambayo ni bora kuliko pipi au vitafunio vya sukari.

  6. ๐Ÿ… Ongeza nyanya kwenye sahani zako. Nyanya zina lycophene, antioxidant ambayo inasaidia kulinda mwili dhidi ya magonjwa.

  7. ๐Ÿš Chagua mchele wa kahawia badala ya mchele mweupe. Mchele wa kahawia una nyuzi nyingi na unaweza kukusaidia kusimamia uzito wako na kuboresha digestion yako.

  8. ๐Ÿฅ› Kunywa maziwa ya jamii ya skim au maziwa ya mbuzi badala ya maziwa ya ng’ombe ya kawaida. Maziwa ya mbuzi na maziwa ya jamii ya skim yana mafuta kidogo na yanaweza kusaidia kudumisha uzito wako.

  9. ๐ŸŒฝ Tumia nafaka nzima kama mkate wa ngano nzima, mchele wa kahawia au quinoa badala ya nafaka zilizopakuliwa. Nafaka hizi ni tajiri katika nyuzi na hutoa hisia ya kujazia kwa muda mrefu.

  10. ๐Ÿฅ• Ongeza karoti kwenye saladi yako. Karoti ni chanzo kikubwa cha vitamini A, ambayo inasaidia kuimarisha mfumo wetu wa kinga.

  11. ๐ŸŒ Kula ndizi kama chakula cha baada ya mazoezi. Ndimu zina wanga na potasiamu, ambayo inasaidia kuimarisha misuli na kurejesha nishati baada ya mazoezi.

  12. ๐Ÿš Pika vyakula vyenye mafuta kidogo kama vile kukaanga kwa kutumia mafuta ya mizeituni. Mafuta ya mizeituni ni bora kwa afya ya moyo na yanaweza kusaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo.

  13. ๐Ÿฅค Kunywa maji ya kutosha. Maji ni muhimu kwa afya na ustawi wetu. Unapaswa kunywa angalau glasi 8 za maji kwa siku.

  14. ๐Ÿฅฆ Jaribu kuchemsha mboga zako badala ya kuzipika kwa muda mrefu. Kuchemsha mboga zitahifadhi virutubisho vyao na kuboresha ladha yao.

  15. ๐Ÿฅ— Jitahidi kula chakula kilichoandaliwa nyumbani na kuwa na udhibiti mkubwa juu ya viungo vyote unavyotumia. Hii inaweza kusaidia kuepuka vyakula vya haraka na kuongeza lishe kwenye chakula chako.

Hizi ni baadhi tu ya mawazo rahisi na yenye afya ambayo unaweza kuzingatia kujipatia chakula bora na kilicho na lishe wakati wa kukabiliana na changamoto za kazi. Kumbuka, chakula ni mafuta yetu ya ajabu ambayo inatuwezesha kufanya kazi vizuri na kwa ufanisi. Kwa hiyo, kula vizuri na ujaze nishati yako! Je, una mawazo mengine yoyote kwa chakula cha kazi? Tafadhali shiriki nasi katika sehemu ya maoni hapa chini!

Mapishi ya Maini ya kuku

Mahitaji

Maini ya kuku 1/2 kilo
Vitunguu vikubwa 2
Hoho 1
Pilipil 1
Limao 1/2
Swaum/tangawizi 1 kijiko cha chai
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia

Matayarisho

Safisha maini weka pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu,swaum na tangawizi pamoja (hakikisha vitunguu visiwe vya brown), kisha tia maini, curry powder, pilipili, chumvi ,hoho na limao kisha changanya vizuri na ufunike. Pika mpaka maini yaive na hakikisha yanakuwa na rojo kidogo. Baada ya hapo ipua na yatakuwa tayari kwa kuliwa na chochote upendacho kama vile chapati, chips, ugali, wali.

Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ya Ng’ombe Na Nyanya

Vipimo

Mchele (Basmati) – 3 vikombe

Nyama ya ngoโ€™mbe – 1ย kg

Pilipili boga – 1 kubwa

Nyanya – 2 kubwa

Vitunguu maji – 2 vikubwa

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa – 1 kijiko cha supu

Tangawizi – 1 kijiko cha chai

Ndimu – 1

Mafuta ya kupikia – ยฝ kikombe

Mdalasini – ยฝ kijiko cha chai

Binzari nyembamba – 1 kijiko cha chai

Pilipili manga – ยฝ Kijiko cha chai

Hiliki – ยฝ Kijiko cha chai

Namna ya kutayarisha na Kupika

Roweka mchele wako katika chombo

Chukuwa nyama na ioshe vizuri na itie thomu, tangawizi, ndimu, pilipili manga na chumvi kiasi

Iweke jikoni hadi ikauke maji na kuwa imewiva huku ukiikaanga kaanga kwa hayo hayo mafuta yake hadi kuwa rangi ya hudhurungi

Katakata Vitunguu na nyanya weka pembeni

Chukua pilipili boga, thomu, tangawizi na visage katika mashine ya kusagia

Weka sufuria pembeni na utie mafuta, subiri yapate moto

Kisha tia vitunguu na vikaange hadi kuwa hudhurungi na tia nyanya

Kisha mimina mchanganyiko wako ulio usaga wa pilipili boga, thomu na tangawizi

Koroga kwa dakika kadhaa Kisha mininia nyama uliyokuwa tayari, maji kiasi na chumvi wastani na subiri maji hayo yachemke

Weka mchele humo na koroga kiasi na onja chumvi kama ipo sawa au kama ndogo unaweza kuongeza

Funika na punguza moto na uache uive taratibu

Baada ya kukauka maji kabisa basi ugeuze na subiri tena kwa dakika kama mbili na tayari kuliwa.

Mapishi ya Ugali na dagaa

Mahitaji

Dagaa (dried anchovies packet 1)
Unga wa ugali (corn meal flour 1/4 kilo) (unaweza kutumia unga wa choice uipendayo)
Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2)
Kitunguu maji (onion 1)
Limao (lemon 1/4)
Pilipili mbuzi nzima bila kukata (scotch bonnet pepper1, do not chop)
Chumvi (salt 1/4 ya kijiko cha chai)
Mafuta (vegetable oil)
Hoho (green pepper)

Matayarisho

Chambua dagaa kwa kutoa vichwa vyao na utumbo, baada ya hapo waloeke katkika maji ya moto kwa muda wa dakika 5 na uaoshe tena katika maji ya baridi na uwakaushe uwaweke pembeni. Ukishamaliza katakata kitunguu na uandae nyanya tayari kwa upishi. Bandika sufuria ya kupikia dagaa jikoni na utie mafuta, yakishapata moto tia vitunguu pamoja na dagaa. Kaanga mpaka dagaa wawe light brown kisha tia nyanya, chumvi na pilipili. Pika nyanya mpaka ziive (ukitaka kujua kama nyanya zimeiva utaona zinatengana na mafuta) Baada ya hapo kamulia limao kidogo sana na tia pilipili hoho na zipike kama dakika mbili. kisha ipua.
Ukisha maliza kupika dagaa andaa chungu cha ugali. Kwanza unatakiwa kuchemsha maji ya moto, kisha koroga pembeni unga kiasi katika maji ya baridi na utie kwenye maji yanayochemka, Fanya kama unatengeneza uji, uji wa ugali ukishachemka tia unga na uanze kuusonga mpaka ugali uive. Ukisha iva pakua na usevu na mboga tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kupika Mchuzi Wa Ngogwe Na Bamia

Viamba upishi

Ngogwe ยฝ kg
Kitunguu 2
Bamia ยผ kg
Karoti 2
Mafuta vijiko vikubwa 8
Maji vikombe 3 Mayai 2
Nyanya 2
Chumvi

Hatua

โ€ข Osha, menya na katakata nyanya na vitunguu.
โ€ข Osha, menya na kata karoti virefu virefu.
โ€ข Osha, kata ncha za bamia pande zote na kama ndefu sana kata
vipande viwili.
โ€ข Osha, kata vikonyo vya ngongwe, kama ni kubwa kata vipande viwili.
โ€ข Kaanga vitunguu, ongeza nyanya, korogoa mpaka zilainike.
โ€ข Ongeza ngogwe, karoti, bamia na chumvi, koroga mpaka
zionekane kukolea rojo.
โ€ข Ongeza maji vikombe 2 koroga na funikia kwa dakika 10-15 au
mpaka ziive. Punguza moto.
โ€ข Koroga mayai kwenye maji mpaka iwe kama maziwa, ongeza
kwenye mboga na koroga polepole usiponde ngogwe wala bamia
kwa dakika 5.
โ€ข Onya chumvi, pakua za moto kama kitoweo.

Mapishi ya Viazi vitamu na kachumbari

Mahitaji

Viazi utamu 3
Nyanya 2 kubwa
Kitunguu
Tango
Limao
Chumvi
Pilipili
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Menya viazi na kisha vikate katika vipande. Tia mafuta kwenye chuma cha kukaangia, yakisha pata moto tia viazi nauviache vikaangike mpaka upande mmoja uwe wa brown na kisha geuza upande wa pili na upike mpaka uwe wa brown. Vikisha iva ipua na uweke kwenye kitchen towel ili vikauke mafuta.
Kachumbali: Katakata vitunguu katika bakuli na kisha tia chumvi kwa ajili ya kuondoa ukali wa vitunguu. Baada ya hapo vioshe mpaka chumvi yote iishe. osha nyanya, Pilipili tango na kisha katakata slice nyembamba na uchanganye na vitunguu. Baada ya hapo tia chumvi, kamulia limao na uchanganye zote pamoja .Baada ya hapo viazi na kachumbali vitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Supu ya makongoro

Mahitaji

Makongoro (miguu ya ng’ombe) kiasi
Limao 1 kubwa
Kitunguu swaum
Tangawizi
Chumvi
Pilipili

Matayarisho

Safisha makongoro kisha yatie kwenye pressure cooker. Kisha tia kitunguu swaum, tangawizi, chumvi,limao na maji kiasi. Baada ya hapo yachemshe mpake yaive na yawe malaini na pia ubakize supu kiasi inaweza kuchukua kama dk 45 au saa 1 hivi. Baada ya hapo yaipue na upakue supu yako kwenye bakuli katia pilipili kiasi kisha itakuwa tayari kwa kuliwa.

Note:
Ukiwa unanunua makongoro hakikisha unachukuwa yale yasiyokuwa na manyoya na pia
hakikisha usiyachemshe kupitiliza kwani yakiwa malaini sana utashindwa kuyaenjoy.

Jinsi ya kutengeneza Biriani Ya Nyama Ya Ng’ombe

Mahitaji

Nyama – 2 Ratili (LB)

Chumvi – kiasi

Mafuta – 1 Kikombe

Samli – ยฝ Kikombe

Kitungu (Kata virefu virefu) – 3 Vikubwa

Nyanya (kata vipande) – 2

Nyanya kopo – 1 Kijiko cha chakula

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 1 Kijiko cha chakula

Tangawazi – 1 Kijiko cha chakula

Pilipili mbichi iliyosagwa – 1 Kijiko cha chai

Pilipili ya unga nyekundu – ยฝ Kijiko cha chai

Kotmiri iliyokatwa – 2 Vijiko vya chakula

Viazi – 6

Gram masala – 1 Kijiko cha chai

Mtindi – ยผ Kikombe cha chai

Namna Ya kutaarisha Na Kupika

1. Kwenya karai au (sufuria) mimina mafuta na samli. Yakishapata moto mimina vitunguu vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi. Vitowe viweke pembeni.
2. Kaanga viazi na viweke pembeni.
3. Chukua sufuria tia nyama, thomu, tangawizi, pilipili, nyanya, nyanya ya kopo, mtindi, na pilipili ya unga. Chemsha mpaka iive.
4. Tia vile vitungu ulioyovikaanga, tia viazi, gram masala, kotmiri na yale mafuta uliokaangia vitunguu kama ยผ kikombe, acha moto mdogo mdogo kama ยผ saa, epua weka pembeni.

Vipimo Vya Wali

Mchele – 5 Magi (Kikombe kikubwa)
Hiliki nzima – 4
Mdalasini mzima – 1
Zafarani – ยฝ kijiko cha chai
Rangi ya biriani – ยผ Kijiko cha
Mafuta yaliyokaangiwa vitunguu – ยฝ Kikombe
Chumvi – kiasi
Roweka zafarani na rangi kwenye kikombe na ยผ kikombe cha maji. Roweka kabla ya robo saa.

Namna Ya Kutaarisha

Osha mchele uroweke kwenye maji muda wa dakika 20.
Chemsha maji kwenye sufuria kama magi 10.
Tia hiliki na mdalasini.
Yakishachemka unatia mchele,chemsha usiive sana, unamwaga maji.
Unamimina tena ule mchele ยฝ yake kwenye sufuria, unatia rangi na zafrani kidogo, halafu unamimina
mchele uliyobakia unatia rangi iliyobakia.
Mafuta yake unayachemsha mpaka yachemke unamimina juu ya mchele, unarudisha motoni unaweka
moto mdogo ukisha kuiva, tayari kupakuliwa.
Unapakuwa wali unaweka chini kwenye sahani na juu yake sosi ya nyama

Mapishi ya Wali Wa Nyanya Wa Kukaanga

Vipimo

Mchele basmati, pishori – 3 vikombe

Vitunguu katakata – 2

Nyanya/tungule katakata – 5 takriban

Viazi/mbatata menya katakata – 3 kiasi

Thomu (saumu/garlic) ilosagwa – 1 kijiko cha supu

Bizari mchanganyiko – 1 kijiko cha kulia

Hiliki ya unga – ยฝ kijiko cha chai

Kidonge cha supu – 2

Chumvi – kisia

Mafuta – ยฝ kikombe

Maji ya moto au supu – 5 takriban

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha na roweka mchele
Katika sufuria weka mafuta yashike moto, tia viazi, vitunguu ukaange.
Vikianza tu kugeuka rangi tia thomu na bizari, hiliki, endelea kukaanga kidogo.
Tia nyanya kaanga lakini usiache zikavurugika sana.
Tia mchele ukaange chini ya dakika moja.
Tia maji ya moto, na kidonge cha supu au supu yoyote kiasi cha kufunika mchele yazidi kidogo.
Koroga vichanganyike vitu, kisha funika upike kama pilau.
Pakua ikiwa tayari, tolea kwa samaki wa kukaanga au kitoweo chochote kile

Mapishi ya Ndizi na Nyama Ya Ngโ€™ombe

Mahitaji

Ndizi mbichi – 10-12

Nyama ngโ€™ombe – 1 kilo moja

Kitunguu maji – 2

Nyanya/tungule – 2

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 7

Tangawizi mbichi – 1 kipande

Ndimu – 2 kamua

Chumvi – kiasi

Mafuta – 3 vijiko vya supu

Tui la nazi – 3 vikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Saga kitunguu thomu na tangawiz mbichi.
Weka nyama katika sufuria tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi na ndimu kisha chemsha hadi iive.
Menya ndizi ukatekate
Weka mafuta katika sufuria tia kitunguu maji kilokatwakatwa ukaange kidogo tu kisha tia nyanya/tungule uendelea kukaanga.
Tia tangawizi na thomu ilobakia.
Tia ndizi, kaanga kidogo kisha tia supu ya nyama na nyama yake.
Ziache ndizi ziive zikiwa tayari tia tui la nazi zikiwa tayari.

Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Ufuta Na Jam

VIAMBAUPISHI

Unga vikombe 2

Sukari ya kusaga 1/4 Kikombe

Siagi 250 gms

Jam kisia

Ufuta kisia

Vanilla 1 kijiko cha chai

MAPISHI

Tia kwenye mashine ya kusaga (blender) au mashine ya keki, siagi, yai, sukari na vanilla uchanganye hadi ichanganyike vizuri.
Tia baking powder, na unga na changanya kwa mkono vizuri.
Paka siagi sinia ya kupikia ya oveni.
Tengeneza viduara vidogo vidogo.
Bonyeza kila kiduara katikati kwa kidole, kisha weka jam, halafu juu yake paka mayai na unynyuzie ufuta.
Pika katika moto wa chini 350ยบF kwa muda wa dakika 20-25.
Tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Samaki wa kuokwa

Mahitaji

Mackerel 2
Kitunguu swaum na tangawizi (ginger and garlic paste) 1 kijiko cha cha kula
Pilipili iliyo katwakatwa (chopped scotch bonnet ) 1/2
Limao (lemon) 1/2
Chumvi (salt) kiasi
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Coriander powder 1/2 kijiko cha chai
Mafuta 1 kijiko cha chai

Matayarisho

Safisha samaki kisha wakaushe maji ( ukipenda unaweza kuwakata kati au ukawapika wazima) Baada ya hapo wakate mistari kila upande ( ili spaces ziweze kuingia ndani) kisha waweke kwenye bakuli na utie spice zote. Wachanganye vizuri kisha waweke frijini na uwaache wamarinate kwa muda wa masaa 3. Baada ya hapo washa oven kisha wapakaze mafuta na uwafunge kwenye foil na uwatie kwenye oven kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo fungua foil na uwaache kwenye oven kwa muda wa dakika 10 ili wapate kukauka kidogo. Na hapo watakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuwala kwa kitu chochote upendacho.

Jinsi ya kutengeneza saladi

Mahitaji

Tango 1/2
Kitunguu 1/2
Cherry tomato 8
Lettice kiasi
Green olives kidogo
Black olives kidogo
Hoho jekundu 1
Carrot
Giligilani kidogo

Salad dressing
Yogurt 1/2 kikombe
Swaum 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/2
Pilipili ya unga 1/4 kijiko cha chai
Chumvi kidogo
Olive oil kiasi

Matayarisho

Osha vitu vyote kisha vikaushe maji. Baada ya hapo ktk bakuli kubwa katakata, lettice, tango,hoho, kitunguu,giligilani na kisha ikwangue carrot na utie bila kusahau nyanya zote pamoja na olives.Baada ya hapo ichanganye vizuri, kisha tengeneza salad dressing kwa kuchanganya vitu vyote vilivyo (kwenye list ya salad dressing) kisha koroga vizuri.Baada ya hapo ichanganye na salad.Na hapo salad yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila na chochote upendacho kama vile chips, nyama choma au au chakula kikuu.

Jinsi ya kupika vitumbua inavyotakiwa

Mahitaji

Unga wa mchele ( Vikombe 2 vikubwa)
Sukari (Nusu ya kikombe kikubwa)
Hamira ( Nusu ya kijiko cha chai)
Hiliki (Nusu ya kijiko cha chai)
Tui la nazi ( Kikombe kimoja kikubwa)
Unga wa ngano (Vijiko viwili vya chakula)
Mafuta ya kuchomea (Vegetable oil)

Matayarisho

Unachanga unga, sukari, hamira, hiliki, unga wa ngano na tui la nazi pamoja katika bakuli la plastiki. Kisha unaukoroga mpaka mchanganyiko unakuwa kama uji mzito. Kava bakuli lililokuwa na mchanganyiko kisha hifadhi katika sehemu yenye joto kwa muda wa masaa matatu.

Jinsi ya kupika

Weka chuma cha kuchomea vitumbua katika moto wa wastani, kisha weka mafuta kwenye chuma cha kuchomea ( Kijiko kimoja cha chai) mafuta yakisha pata moto tia uji wako (upawa mmoja) katika kila shimo la chuma cha kuchomea. Acha mpaka kitumbua kikauke kisha geuza na tia mafuta. Acha upande wa pili wa kitumbua mpaka uwe rangi ya kahawia na hapo kitumbua kitakuwa kimeiva utakitoa. Rudia hatua hizo kwa vitumbua vyote vilivyobaki.

Jinsi ya kutengeneza Rock-cakes Za Njugu Na Matunda Makavu

Mahitaji

Unga – 4 Vikombe

Sukari -10 Ounce

Siagi – 10 Ounce

Mdalasini ya unga – 2 vijiko vya chai

Matunda makavu/njugu (kama lozi, Zabibu, maganda ya chungwa, Cherries na kadhalika – 4 ounce

Maziwa ya maji – 4 Vijiko vya supu

Maandalizi

Chukua siagi na sukari koroga na mixer mpaka iwe kama cream.
Tia vanilla mdalasini, tia yai moja mix tena endelea kuongeza yai lingine mpaka umalize yote, changanya mpaka iwe laini kama sufi (fluffy)
Tia unga na baking powder na dried fruits, changanya na mwiko.
Chota mchanganyiko na kijiko cha soup weka kwenye treya ya kupikia tandaza na uma ili upate matundu juu ya biskuti.
Pika (bake) kwenye oven lenye moto wa 375ย F. kwa muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.

Mapishi ya Bokoboko La Kuku

Mahitaji

Ngano nzima (shayiri) – 3 Vikombe

Kuku – ยฝ (3 LB takriban)

Thomu na tangawizi iliyosagwa – 1 kijko cha supu

Pilipili manga ya unga – ยฝ kijiko cha chai

Jiyrah (cumin/bizari ya pilau) – ยฝ kijiko cha chai

Chumvi – kiasi

Kidonge cha supu – 1

Samli ya moto – ยฝ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Roweka ngano (shayiri) tokea usiku au muda wa masaa.
Katakata kuku mtie katika sufuria, tia maji kiasi viungo vyote. Mchemeshe awive na ibakie supu yake.
Toa kuku, toa mifupa na umchambue chambue vipande vidogo vidogo.
Chemisha ngano (shayiri) kwa kufunika sufuria hadi iwive na kukauka maji.
Tia supu ya kuku katika ngano (shayiri), na kuku uliyemechambua. Tia kidonge cha supu.
Tia samli nusu (bakisha nusu) kisha songa mchanganyiko uchanganye hadi ivurugike kuku na ngano (shayiri) vizuri.
Mimina katika sahani, mwagia samli imoto ilyobakia likiwa tayari.

Mapishi ya samaki aina ya salmon

Mahitaji

Salmon fillet 2
Potatao wedge kiasi
Lettice kiasi
Cherry tomato
Limao 1
Swaum
Chumvi
Olive oil

Matayarisho

Mmarinate samaki na chumvi, swaum na nusu ya limao kisha muweke pembeni, baada ya hapo washa oven kisha tia potato wedge zikisha karibia kuiva anza kumpika samaki, tia mafuta kidogo sana kama kijiko kimoja cha chai hivi katika frypan isiyoshika chini yakisha pata moto kiasi muweke samaki wako (upande wenye ngozi chini kwanza) Mpike mpaka uone rangi ya kahawia kwa chini kisha mgeuze upande wa pili, uku samaki wako akiwa anaendelea kuiva, tayarisha salad yako kwa kusafisha lettice na nyanya kisha zichanganye pamoja kisha tengeneza salad dressing pembeni , kamua limao kisha tia olive oil na chumvi kidogo, Baada ya hapo samaki na potato wedge vitakuwa vimeiva, andaa mlo wako na utakuwa tayari kwa kuliwa.

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About