Vituko Vya Wikiendi

Madhara ya kubeba nauli kamili tuu. Cheki kilichonipata

Kubeba nauli kamili nayo ni shida
Yani nimepanda daladala
Kondakta mmoja akaingia kwenye Gari amevaa suti za blue za daladala na miwani Kisha akakusanya pesa Gari Zima alafu akakaa siti ya nyuma baade Kondakta mwingine akaanza kukusanya pesa watu wakalalamika na kusema tayari tumelipa na kumuonyesha tuliemlipa Kondakta akacheka na kusema huyo tuliemlipa ni kipofu na alikuwa anaomba msaada..!!

Cheki jamaa alivyoumbuka baada ya kuhudhuria semina isiyomuhusu

Jamaa kavamia semina ya wasomi iliyokua inafanyika maeneo ya ubungo plaza bas wakaanza kujitambulisha
1. Naitwa Anna niko SUA mwaka3 nasoma agriculture
2. Naitwa Stella niko UDSM mwaka2 nasoma public relation

3. Naitwa Emmanuel niko UDOM mwaka3 nasoma computer science
bas jamaa nae akainuka kwa kusuasua huku akijishtukia akasema”Naitwa Elisha niko Tanesco mwaka wa 7 nasoma mita”

Kweli tamaa ni mbaya, mke wa mtu kaponzwa na tamaa, ndio basi tena

Jamaa kaenda kwa mke wa rafiki yake:
JAMAA: Shem nakupenda!
MKE: Hebu toka hapa! Je rafiki
yako akijua? tena koma!
JAMAA: Ntakupa milioni 1!
MKE: Basi njoo kesho mchana
mume wangu akiwa kazini!

Kesho yake Jamaa kaja
na milioni 1 wakamalizana na mke wa rafki yake,
jioni ilipofika
Mume akarudi home na
kumuuliza Mkewe, “Rafki yangu SAM kaleta hela yangu milioni 1?”
MKE akajibu kwa unyonge, “Ndio!”
MUME: Yes! Ndio maana nampenda SAM kanikopa asubuhi jioni karejesha!!!!
Mke hoi……

Unakumbuka hizi enzi za utoto?

Kitambo tukiwa watoto ulikuwa unaitwa uje ule kwa lugha tofauti kulingana na chakula kilichopikwa siku na muda husika

1. UGALI NA KUNDE
Mwitaji : 🗣Joniiiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Uje ukule

2. UGALI NA SAMAKI
Mwitaji: 🗣 we Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Unaitwa na Mama

3. WALI NA NYAMA/KUKU
Mwitaji: 🗣 Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Shauri yako!
😂😂😂😂😂😂

Cheki tabia za kuandika vimaneno vya ajabuajabu kwenye pikipiki na bodaboda ilivyomponza huyu

Jamaa mmoja dereva wa bajaji alianguka, sasa bajaji ikawa imem’bana akawa anafurukuta bila mafanikio Cha ajabu watu wakawa wanampita bila kumsaidia, Kumbe Nyuma ya Bajaji yake alikua Kaandika “NIACHENI KAMA NILIVYO, HII NDIO STYLE YANGU” 😂😂😂 Mpaka sasa nimemwacha bado yuko hapo *Sipendagi Ujinga mimi* 🚶🏽🚶🏽🚶🏽🚶🏽🚶🏽

Huyu mchungaji ni noma, cheki alichomwambia pedeshe

Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa
kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki;
MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za
kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa
mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu
atakubariki zaidi

PEDESHE: Samahani Mchungaji haitakuwa vizuri
mimi kuchangia kanisa, fedha zangu ni haramu,
huwa nazipata kwa utapeli na kuuza madawa ya
kulevya.
MCHUNGAJI: Yote ni heri, pesa yako tutatumia
kwa kujenga eneo la choo we toa tu!!!

Angalia ndoto nyingine zilivyo na Majanga

Ndoto zingine bwana usiombe zikupate

Mimi usiku wa kuamkia Leo nikiwa nimelala nimeota naendesha gari Yangu aina ya BMW mpya Mara gafla ikakwama kwenye tope .hivyo ikabidi nishuke ili kuisukuma loh! Yani kudadeki ile kuamka nikakuta nimesukuma kitanda hadi sebleni Daaa ilinisikitisha sana jiangalie sana sese hivi ndio narudisha kitanda chumbani .angalizo angalia ndoto unazo ota unaweza kuota upo baharini ukaamka unajikukuta unaogelea kwenye Jaba la Maji shauri yako.

Shopping Cart
21
    21
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About