Vituko Vya Wikiendi
Wavuta bangi wa Colombia watoa mpya
Asubuhi ya leo huko nchini Colombia baada ya serikali kuidhinisha matumizi ya bangi kuwa halali +++ Wavutaji bangi wamepanda basi la gorofa wengine juu wengine chini….
Waliopanda chini wanawauliza wa juu huko speed ni ngapi maana huku ni 80.
Wajuu wakajibu huku mpaka sasa hatujui dereva bado hajaja…. 😂😂😂
Ungekua wewe ndio boss wa huyu jamaa ungempa kazi? Ungemjibu nini?
*Boss*:-kijana unataka nini ndani ya ofisi zangu?
*Jamaa*:-Samahani naomba kazi ya ulinzi ndugu.
*Boss*:-umesoma mpaka wapi?
*Jamaa*:-mpaka form four.
*Boss*:-unajua kingereza?
*Jamaa*:-kwani hao wezi wanakuja na wazungu???.
😅😅😅😅😅😅
Angalia huyu Jamaa alichomfanyia mke wake jana
Jana niligombana na mke wng, Akaniambia nibebe kila kitu changu niondoke, Bas kiustaarabu tu nikachukua nguo zangu,mwishoni nikambeba na yeye nikamuweka begani nikaanza kuondoka nae
hua sipendagi ujinga, amesahau na yeye pia ni wangu
Huyu bibi kweli kiboko, cheki alichofanya akiwa na babu
Bibi na Babu walisafiri wakielekea kwa mtoto wao ambae hawajamuona zamani.
Walipofika njiani wakawa wamechoka Sanaa. Wakaamua kutafuta hotel ili walale.
Wakakubaliana walale kwa masaa 4. Wakalala, Walipoamka, mfanyakazi wa Hotel akawatoza Tsh. 500,000/=
Wale wazee wakashangaa hata kama ni hotel ya kisasa lakini sio laki tano kwa masaa 4.
Babu akagoma kulipa akasema aitiwe meneja.
Meneja akaja kuwasikiliza
Babu: ” Kwanini bili ni kubwa hata kama ni hotel ya kisasa?”
Manager;“kuna maswiming puli, ya kisasa “
Babu; “Lakini hatukuyatumia”
Manager; “Ah ah ah. Lakini mungeweza kama mngetaka”
Babu: “Hata hivo bado haithamini kuwa laki 5”
meneja: “Pia Kuna waimbaji kutoka sauzi, Uganda , Congo”
Babu: “Lakini sisi hatukuwasikiliza”
Meneja: “Ndiooo. Lakini mngeweza kama mngetaka”
Babu; aka give up na kumwambia mkewe andika cheki uwape,,
Bibi akaandika akampa meneja.
Meneja anaangalia anaona sh. 50,000
Akashangaa na kusema. “VP mbona hamsini'”
Bibi akajibu “450,000 ya kulala na mimi”
Meneja akajibu; “Lakini sijalala”
Bibi :“ungeweza kama ungetaka”
Angalia huyu jamaa alivyomuweza huyu binti wa chuo
😁😁😁😁 .. TABU KUDATE NA MADEMU WA CHUO
Demu ; Baby Safari Hii Nataka Pale Hostel Niwafunike Mashoga Zangu Wote.
Jamaa ; Poa Sweetie Ondoa Shaka Nitakununulia #Turubai Utawafunika Wote…!!!
Demu: Mxiuuuuuuuu Lione Sura Kama Goti La mbuzi Na Namba yangu futa Nakublock Mpaka Sanduku la posta…!!!
😂😂😂😂nmecheka adi nmelazwa
Safari ni safari
FUNDISHO : SAFARI NI SAFARI
Maisha ni ya ajabu sana, wakati mwingine maisha ni mazuri na mwingine ni mabaya, katika maisha yetu tumeshapitia safari nyingi sana na za aina mbalimbali kwa nyakati mbalimbali. Lakin kiukweli kila safari ni safari tuu.
Japokua kila safari ina changamoto zake lakini mwisho wake ni ule ule , kila safari ina uzuri na upekee wake.
Vile vile kila safari ina ubaya wake, kwa mfano kila safari ina gharama yake kulingana na upekee wake.
Usiwe na wasiwasi na mashaka na aina ya safari ulionayo, jipe moyo utaimaliza na kupata ulichokitarajia. Haya ndio maisha na wote tunatakiwa tuyafurahie.
Ingawa kila mtu ana safari yake bado wote tunatakiwa tufurahie pamoja kwa safari tuliyo nayo. Hata Uwe Na safar ya aina gani wewe furahi tuu. Hii ni kwa sababu safari mwisho wake ni mmoja kwa wote burudani ni ile ile
Safari🍺 ni safari 🍺hata kama ni ya chupa au ya kopo mwisho wake 💤💤
😋😜😜😂😂😂
Ulijua ni nn??
Njia 3 rahisi za kuondoa kitambi
JE, una KITAMBI na unataka kukiondoa?
FANYA HAYA;
1. Kopa mkopo mkubwa benki
2. Nunua gari bovu la biashara
3.Oana na mke mwenye kelele.
Ukiona miezi mitatu hakijaisha basi ujue umevimba BANDAMA sio kitambi..
Cheki huyu mtoto anachomjibu mwalimu wake, kufundisha watoto ni kazi kweli kweli
Mwanafunzi wa darasa la 2 kaulizwa na mwalimu wake
Hivi:je ukipewa maandazi 5 ukiambiwa kula 3 tu yatabaki mangapi?
Akamjibu hivi:nikipewa na chai hakibaki kitu mwalimu.
Kilichotokea baada ya bibi na babu kukumbukia mahaba ya ujanani
Mzee wa miaka 60 alimwambia mkewe, leo nataka tukumbukie enzi zetu kutongozana, mke akajibu sawa, inabidi unisubiri mwembeni saa 1 usiku nitapita, mzee akafika saa 1 alikaa hadi saa 5 usiku, aliporudi nyumbani akamuuliza mkewe kwa hasira; sasa tumepanga nin halafu haujatokea ?
Mke; leo mama alinikataza nictoke nyumbani usiku nijisomee ! Babu hoii…
Baada ya kunitumia SMS usiku ikawa hivi….
Jana usiku kuna Jirani yangu..kanitumia text “mambo vipi?”…halafu tunakaa nae mtaa mmoja nikaona nikimjibu ni uharibifu wa hela nikaenda kumgongea mlango saa 7 usiku. Alipofungua nikamjibu “shwari”halafu nikarudi nyumbani kulala zangu..
Sipendagi kuchezea salio..
😂😂😂😂😂
Ufugaji wa nguruwe kazi, Cheki jamaa hawa wake walivyompa mtihani
MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalishanini?
.
MFUGAJI: Nawalisha mabaki ya chakula toka migahawa mbalimbali
.
MWANAHARAKATI: Hayo ni makosa unawatesawanyama kwa kuwalisha chakula kichafu. Akapigwa faini… Baada ya siku chache wakaja wanaharakati toka Umoja wa Mataifa
.
MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalisha nini?
.
MFUGAJI: Huwa nawaanzia siku na uji wa ulezi, halafu mikate, mchana ugali kwa kabeji na usiku viazi
.
MWANAHARAKATI: Loh watu wanakufa kwa njaa wewe unalisha nguruwe, akapigwa faini….siku chache baadae wakaja wanaharakati wa Mazingira
.
MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalisha nini?
.
MFUGAJI: (Kwanza akasita kidogo) Hawa huwa nawapa shilingi alfu tano kila mmoja kila siku halafu wao wenyewe wanaenda kununua chakula wanachokitaka.. .
Angalia huyu jamaa alivyowafanyia watu uhuni bar
Jamaa kaingia Bar;
Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji. Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,
Jamaa: Muhudumu nipe supu na kila mtu humu ndani mpe supu maana ninapokunywa supu kila mtu lazima anywe supu. Watu wakapewa supu tena safari hii wakapiga makofi.
Jamaa: Muhudumu nipe bili, na kila mtu humu ndani mpe bili maana wakati nalipa bili yangu kila mtu lazima alipe yake. Zogo lilianzia hapo…….
Cheki huyu jamaa anachomfanyia huyu mrembo kanisani
Jamaa kaenda kanisani akakaa karibu na mrembo.
Wakati mahubiri yakiendlea jamaa akaanza kuingiza vocal:
Jamaa: dada mi nakupenda saana
Dem: Kaka naomba umsikilize mchungaji
Jamaa: nipe nafasi uwe msimamizi wa serikali ya moyo wangu…
Dem: niache…
Jamaa: kweli nakupenda mpnz
Dem: (kwa sauti kubwa) nmesema NIACHEEEE!!
Watu wote kanisani wakageuka… Jamaa kaona noma na ili atulize msala
Jamaa: sikuachi hadi ukiri YESU kuwa Bwana na mwokozi wa Maisha yako.
Angalia pombe ilichomfanya huyu jamaa, kweli pombe haimuachi mtu salama
Leo nimeiogopa pombe.
Nimetokea kuiogopa pombe baada ya kumwona jirani yangu akicheza muziki kwa sauti ya jenereta langu, akidhani yuko club…..nkamsikia anasema “wee dj noomaaaa”
Baada ya kuzima jenereta akaniuliza uo mziki kaimba nan?
Nlivyokuwa na roho mbaya Nikamwambia iyo ni collabo ya Yamaha na Petrol
😂😂😂😂😂
Cheka kidogo, angalia anachosema huyu mchaga
Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?
MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee.
MALAIKA: Kwa nini?
MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni.
Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?
Baadhi ya misemo mikali ya leo
1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.
2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.
3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?
4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.
5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.
6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.
7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.
8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.
9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.
10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi kufunika sufuria.
Recent Comments