Vituko Vya Kujienjoy Leo
Nilichokifanya kwa rafiki yangu
Nimekuja kwa Rafiki angu kumtembelea kaacha maji jikon yeye kaenda kununua unga. Huku mm nikaongeza maji pale jikon. Kumbe yy aliweka maji saiz ya unga wake peke yke… Sasa hiv TUNAKUNYWA UJI hata hatuongeleshani. Kimbelembele changu kimeniponza.. 😂😂😂😂
Hawa Machizi wamezidi sasa
Chizi kakaa ukingoni mwa bahari analia kwa masikitiko na huku kakamata kijiko cha chai. Mwezake akamuuliza mbona unalia mwenzangu. Chizi akajibu nimetia vijiko vitatu vya sukari baharini, kila nikionja bado ina chumvi. Mwenzake akacheka sanaaaaaa akamwambia. Hujakoroga!!!!😂😂😂😂😂😂
Hii ndiyo sababu ya kumfanya huyu jamaa kujiita fara
MZEE:”sasa huyu mgeni sijui alale wap?”
MKE:”saa hizi ni usiku akalale na Bebi.”
jamaa akaona huyo Bebi pengne mtoto anakojoa kitandani au akalia asije msumbua usiku
JAMAA:”msipate tabu mi ntalala hapa kwenye kochi” akalala
asubh wanakunywa chai akaibuka mrembo,jamaa akapigwa bumbuwazi almanusra ajimwagie chai.
BINTI:”Naitwa BEBI,we unaitwa nani?”
Jamaa akasema mimi naitwa Fara…..!
Kilichompata huyu jamaa mroho wa nyama, Hata kaa arudie tena
Jamaa kaenda kumtembelea rafiki yake Levi, kule sehemu za kwetu, akakaribishwa bonge ya ugali na nyama nyingi tu, wakati anakula akagundua kuwa shemeji yake, mke wa rafiki yake hali nyama;
JAMAA: Aise hili ni bonge ya lanchi hii, lakini Levi mbona sisi tu tunakula nyama shemeji Gulo hagusi kabisa anaishia mchicha tu? Tabia gani hii?
LEVI: Hapana sijamkataza, ila shemeji yako Mngoni halagi nyama ya FISI kama sisi
Huyu mchungaji ni noma, cheki alichomwambia pedeshe
Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa
kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki;
MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za
kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa
mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu
atakubariki zaidi
PEDESHE: Samahani Mchungaji haitakuwa vizuri
mimi kuchangia kanisa, fedha zangu ni haramu,
huwa nazipata kwa utapeli na kuuza madawa ya
kulevya.
MCHUNGAJI: Yote ni heri, pesa yako tutatumia
kwa kujenga eneo la choo we toa tu!!!
Kilichotokea baada ya babu mzee kuibiwa nauli kwenye daladala
Mzee mmoja alipanda Gari Stend;
Wakati wa kugombania Siti,
Akaibiwa Nauli.
Akasimama katikati ya Gari-Akasema; “Jamani Naomba Aliyeniibia Pesa yangu Arudishe Haraka,
Tena Fasta kabla Sijafanya Tukio kama Nililofanya 1977″
Abiria kuskia hivyo wakaogopa.
Ikabidi Mwizi Ajitokeze,
Akarudisha Pesa na Kuomba Msamaha! Mtu Mmoja akauliza,
Mzee,
Kwani 1977 Ulifanya nn?
Si nilienda kwa Miguu mpaka Nyumbani!
Uscheke Peke Yako, wa2mie na wengine ili nao wacheke!
Cha kufanya msichana akikukimbia halafu atake kukurudia
……… Kama msichana atakutupa kwa sababu huna pesa, na baadaye unapopata pesa akarudi tena kuomba msamaha… Ndugu yangu….. Msamehe…. Mpe ahadi ya ndoa, mwambie utamuoa…. iambie familia yake unataka kufanya ukarabati wa nyumba yao…… Ondoa paa lote la nyumba yao halafu TOWEKA…..
😂……… 😂…….. 😂
SOMA HII: Kama wewe ndo baba au mama hapa ungefanyaje!???
Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue. Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika. Ilikua ni bahati tu alimvizia na kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua anamtetea Bakari, ili kumthibitishia mkewe kuwa Bakari ndo culprit,
boss alianza kwa kumuuliza Bakari maswali. Siku hiyo Bakari alikua jikoni,boss na mkewe walikua sebuleni.
Boss:- Bakariiii!
Bakari:- Naam baba!
Boss:- Nani anakunywa wine yangu?
Bakari:- Kimyaaaa hajibu kitu! Boss:- Bakariiiii !
Bakari:- naam baba! Boss:- nauliza nani anakunywa wine yangu halafu anajazia majiii!
Bakari:- kimyaaaaa!
Boss akaamua amfuate hukohuko jikoni.
Boss: Kwanini nikikuita unaitikia, nikikuuliza unanyamaza?
Bakari: Baba huku jikoni ndo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa lakini maneno menginehusikii, na kama huamini baki jikoni mi niende sebuleni.
Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita.
Bakari:Babaa!
Boss: Naam Bakari!
Bakari: Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?
Boss:- kimyaaaa!
Bakari:- Baba babaa!
Boss:- Ndio Bakari!
Bakari:- Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini?
Boss:- kimyaaaaaaa!
Boss akatoka nje: Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina!.
Mama akasema msinizingue nyie…Mbona siwaelewi..
Bakar: mama kama uamini na ww nenda uone.
Mama akaenda jikoni..
Bakari: akaita mamaa
Mama : bee bakari
Bakari: eti hiyo mimba niya baba au yangu.?
Mama kimya
Bakari; mama nakauliza tena hiyo mimba niyababa au yangu.
Mama akatoka aisee kweli humu unasikia jina tu…..😄😄😄😄😄
Hapo sasa akili itakuja
Pale unapo gundua kuwa yule ulie mtukana kwenye bajaji ndio boss anaeenda kukufanyia interview😥😥😥😭
My freand apo ndo utagundua kwaanini wimbo wa Taifa tokea 1961 ni audio aujatolewa video
😆😆😆😆😆😆😆😆
Duh! Huyu kazidi sasa
Kuna jamaa kapita hapa kaniuliza et mbona umekunja sura nikamjibu nataka niweke kwenye begi😂😂😂
Cheki wanachokisema vichaa baada ya kuona ndege inapita angani
Vichaa wawili walikuwa wamekaa sehemu ghafla ikapita ndege angani kichaa mmoja akasema ndege ile hitakua imembeba rais kichaa mwenzake akajibu hapana ile imebeba wazungu kama ingekuwa imembeba rais ungeona mapikipiki mbele
Misemo 10 bora ya kuchekesha itakayokuacha mdomo wazi
1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.
2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.
3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?
4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.
5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.
6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.
7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.
8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.
9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.
10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi
kufunika sufuria.
Watu wana vimaneno
Eti linalo jamba ni tumbo makalio ni spika tu
Dah!!
Nimecheka hadi basi leo
😸😸😹😹
Angalia haya maswali ya huyu mtoto yalivyomagumu, ndio maana wazee wetu walikua wanatudanganya
Mtoto: Mama, hivi kabla hujanizaa uliniona!?
Mama: Hapana mwanangu sijakuona.
Mtoto: Kwahiyo ulivyonizaa ulijuaje kwamba ni mimi…!??
Hii ndio maana ya Matatizo, usiombee hili likukute
Matatizo ni nini???
`Matatizo ni pale unapokuwa umefika ukweni usiku na haja kubwa ikakubana na hukuwa unajua choo kilipo, ukatoka nje na kujisaidia kwenye majani kumbe ni mboga asubuhi ukasikia mama mkwe anasema kuna mjinga kajisaidia kwenye mboga na kaangusha pochi yake hapohapo haa! Vile unajisachi pochi hamna na kulikuwa na passport,vitambulisho, kadi ya benki, pesa zaidi ya laki 2 na nusu, funguo za nyumba yako, `
🤒🤒🤒🤒🤒🤒🤒🤒🤒
Walahi haya ndo matatizo😅😅😅😅😅😅
Angalia nilivyoingizwa mjini na ujanja wangu wote
Ndio nilikuwa nimeshuka kwenye basi la SAI BABA pale Ubungo, nina Begi kubwa Mgongoni na begi Dogo la Lap Top mkononi, sura inatazama Mbele Very Serious kama nipo kwenye Gwaride la Uhuru!..Mabega juu yanafanya Cheers na Mawingu!, natembea kwa madoido…..leo nimetoka Likizo Moshi,
“Brother Simu ya ukweli hii..kitu cha Tecno C9 bei poa” hii ilikuwa sauti ya Teja mmoja hivi!
Yaani huyu Teja Bwege kweli,anataka kumuuzia nani sabuni? mimi sio wa kuja!…kamwe Siwezi kuibiwa hapa Town,hakuna wizi au utapeli nisioujua!, Mimi nimezaliwa Mwananyamala kwa Manjunju, nikalelewa Tandale kwa Mtogole, Shule ya msingi nimesoma Turiani Magomeni, Hivi Mbwa gani aniibie?…kwa Style ipi?
Sipendi kabisa Upuuzi!, Wajinga ndio wataibiwa, sio Mimi!…sasa Kwa mwendo wa haraka nikatoka nje kabisa ya Stendi ya Ubungo straight mpaka Stendi ya dala dala za Kariakoo, hapo ndipo nikakutana na Vijana wawili wadogo wakiwa na mzani wa kupimia uzito,…hakika napenda sana vijana wanaojituma kama hawa na sio ile Mijizi ya kule ndani Stendi!!,….hapa sasa nikapata wazo!
“Dogo mnapima uzito kwa shilingi ngapi?”
“Mia mbili tu Kaka!”
”Ok”
Kwa mwendo wa kikakamavu nikapanda juu ya mzani,lengo hapa ni kujua uzito wangu, Mtori niliokula mwezi mzima kule kwa Mshekuu sio mchezo, hapa nahisi nacheza kwenye kg za John Cena,
“Mama wee! Dogo mzani mzima huu kweli? Mbona nina kilo 134?” (Nilihamaki)
“Aaah! Brother huoni umepanda na Mabegi juu ya mzani?”’
Hahaha! kweli nimechanganyikiwa!…Sasa nikatoa mabegi yote mawili na kurudi juu ya Mzani, hapa ndipo Uzito ukashuka kutoka kg 134 mpaka kg 56!…My God kweli Body la “One Pack ” haliongopi! thats means mabegi yaliniongezea kg 78! duh hii ni hatari!
“Yaani we Dogo kitambi chote hiki kg 56? huu Mzani Mzima kweli?”
Kimya…
“Dogo huu Mzani vipi?”
Kimya…
Dogo ana dharau huyu!…Sasa ndio nikabandua macho yangu toka kwenye kioo cha mzani ili nimtazame huyu dogo asiyejibu!….ndipo macho yangu yakakutana na Kigoda tupu kilichochongwa Mvomero!…Dogo hakuwepo!….na Mabegi pia hayapo!…lap top haipo!….NIMEPIGWA!
Ni dhahiri watoto wa Mjini walikuwa wameniacha juu ya Mzani, wamechukua Lap top ya Milioni na wameniachia Mzani chakavu wa elfu 40, what a stress!….sasa nilirudisha macho kwenye kioo cha uzito na sasa kilisoma KG 38!…yaani dakika hii hii nimepungua kilo zingine 18, Hakiyamama nahisi hata utumbo wangu wamebeba!…niitieni Ambulance!
🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼
Wazo la jioni hii
📢WAZO LA JIONI HII 📢
KAMA MWAKA JANA ULIPIGA HATUA NA HUJAFIKIA MALENGO MWAKA HUU PIGA MSAMBA😝
Soma alichokisema mlevi baada ya kukuta watu wakimpiga mwizi
Mlevi mmoja aliona wananchi wakipiga mwizi akawaambia “mwacheni msimpige, hii tabia yenu ya kupiga wezi mtakuja shtukia mnampiga Yesu, maana imeandikwa atakuja kama mwizi!”
Huyu mwanamke kazidi sasa
Jamaa: Mambo honey, upo ok?
Mrembo: Sipo ok my dear
Jamaa: Una tatizo gani baby?
Mrembo: Nimetoka hospitali kupima, nna mimba.
Jamaa: Weeh usiniletee balaa hiyo mimba imeingiaje wakati huwa tunatumia kinga?
Mrembo Kwani nani kakwambia mimba ni yako, hebu tuliza mshono huo.
😆😆😆😆😆😆😆
MTATUUA
Recent Comments