SMS Nzuri: Meseji za Vituko Vya Weekend

Madenge hakosi visa. Soma hii

MADENGE
HAKOSI
VISA

baada ya kumaliza form four baba akamwambia achague zawadi yoyote aipendayo
MADENGE: naomba pesa nikamuoe bibi maana siku nyingi amekuwa akiniita mchumba wake.
BABA: Shenzi, yule ni mama yangu mzazi huwezi kumuoa.
MADENGE: Mbona wewe umemuoa mama yangu mzazi sijasema kitu ww inakuuma? lazima nilipize kisasi ikikuuma muache mama yangu kila mtu akae na mamayake. ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Tofauti ya ukopaji wa mzungu na mswahili

MZUNGU: Hi, I need $100, will pay back on Monday

MSWAHILI: Kaka vipi, shwari? Dah.. hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini? Juzi nimekuona kwa mbaaaliโ€ฆ mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, afu misiba mingi tu, wife nae kajifungua ghafla. Sasa, kuna cheque naisubiri haijatoka hadi leo, wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata ‘Laki Moja’ ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mweziโ€ฆ?๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Faida 3 za uvutaji wa sigara

Ni hizi

1. Mvuta sigara hazeeki
2. Mvuta sigara haumwi na mbwa
3. Mvuta sigara nyumbani kwake haingii mwizi

UFAFANUZI

1. Hazeeki kwa sababu hufa mapema kwa kifua kikuu

2. Haumwi na mbwa kwa vile kifua na mapafu yanapooza na hulazimika kutembea na bakora

3. Nyumbani kwake haingii mwizi kwa kuwa inafika wakati ambapo halali:
atakohoa usiku kucha hivyo mwizi anajua yupo macho
kumbe kikohozi tu!

Angalia kilichotokea baada ya dogo kupewa ada na kuitumia kubeti

Dogo kampigia simu baba yake;
DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa
nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti
BABA : Unasema nini we mpumbavu mshenzi
mkubwa? Nimekukanya mara ngapi kuhusu kubeti?
DOGO : Lakini baba
BABA : Lakini baba nini ngoja urudi utaona
ntakachofanya.
DOGO : Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda
shilingi milioni 3
BABA : Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu
sana kwanini hukutumia laki nzima kubeti? Si
ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi niwataarifu
ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua
haraka mwanangu mpenziโ€ฆ

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Mkalimani alivyoharibu ibada ya leo

Leo nikaamua niingie misa ya asubuhi kwenye kanisa moja la kilokole kulikua na ugeni wa mchungaji kutoka Bulgaria, Mahubiri yameanza saa 1 asubuhi hali ikawa kama hivi:

MCHUNGAJI: My name is Pastor Livingstone
MKALIMANi: Kwa jina naitwa mchungaji Jiwe linaloishi
MCHUNGAJI: We thank God for All goals we set by our hands
MKALIMANI: Tunamshukuru Mungu kwa Magoli yote tuliyoweka kwa Mkono

Hivi navyoongea kanisa halina viti waumini wote tumekimbia nje naona Mkalimani amebaki na kiatu cha kushoto tu.
Sunday joke

Angalia pombe ilichomfanya huyu jamaa, kweli pombe haimuachi mtu salama

Leo nimeiogopa pombe.

Nimetokea kuiogopa pombe baada ya kumwona jirani yangu akicheza muziki kwa sauti ya jenereta langu, akidhani yuko clubโ€ฆ..nkamsikia anasema “wee dj noomaaaa”

Baada ya kuzima jenereta akaniuliza uo mziki kaimba nan?

Nlivyokuwa na roho mbaya Nikamwambia iyo ni collabo ya Yamaha na Petrol
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Kwa nini vitu vunavyoanza na “K” ni vitamu sana?

Zuzu kaniuliza, “Anko, unajua vitu vinavyoanzia na K ni vitamu sana.”
Nikashtuka, “Astaghafilulah we mtoto! Niondolee wehu wako hapa!”

Zuzu akatabasamu. Akaendelea kuongea kabla sijafanikiwa kumzuia. “Kweli kabisa anko. Vitu vinavyoanza na K ni vitamu sana kwa mfano kuku, kalimati, keki, kabab, katleti, kashata, kisheti na karoti.”
Nikashusha pumzi. “Ahaa! Kumbe ndo hivyo, ni kweli!”

Zuzu akanitupia swali. “Kwani we anko ulidhani nini?”

Cheki masifa yalivyomponza huyu, Sifa nyingine ni mbaya jamani

Mbongo, Mganda, na Mkenya walikamatwa na makosa Uchina.

Wakaambiwa adhabu ni ama kifo cha moja kwa moja au adhabu nyingine ambayo atakayeifaulu atakuwa huru, atakayeshindwa atauawa.

Basi wao wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao.

Wakapelekwa msituni wakaambiwa kila mmoja aende kwa njia yake halafu arudi na matunda kumi ya kufanana.

Wakaingia msituni kila mtu njia yake.

โ€ฆ Mganda akarudi wa kwanza na machungwa kumi. Akaambiwa adhabu yake ni kumeza moja moja likiwa zima bila kufumba macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa mpaka yote kumi yaishe. Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili, akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi akafa.

Mkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogo kama pili vilaini. Akasomewa masharti. Akaanza kumeza bila kufumba macho wala kulia, wala niniโ€ฆ alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa.

Wakiwa kuzimu Mganda akamwuliza Mkenya, โ€œVipi, mbona ulishindwa kuvumilia wakati kilibaki kitunda kimoja tu?โ€

Mkenya akamjibu: โ€œMkuu, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mbongo anakuja na matikiti maji!โ€

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About