SMS Nzuri: Meseji za Vihoja Vya Pasaka Hii

Utoto raha..! Angalia hawa watoto wanachokifanya sasa

Leo nimepulizia Air Fresh yenye Harufu ya Pilau nyumbani kwangu sasa watoto wa Jirani wamehamia Mlangoni kwangu ndio wanacheza hapo. Kila nikitoka wananisalimia. Mama yao ndio kanimaliza kabisa nimetoka akaniambia

“Kumbe wewe ni Mpishi mzuri, Hongera”

Imebidi nisirudi nyumbani maana wale watoto wanaweza kuingia ndani kabisa na pilau hakuna.

#UTOTO RAHA ๐Ÿ˜‚

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ‘†๐Ÿป๐Ÿ‘†๐Ÿป๐Ÿ‘†๐Ÿป

Baada ya mwanamke kukataa kufungua mlango angalia kilichomkuta

MUME: Fungua mlango!

MKE: Leo sifungui! Nimechoshwa na ulevi wako.

MUME: kama hufungui najitupa kwenye hili shimo nife kabisa.

MKE. Kufa huna faida yoyote duniani!

MUMEย kachukua jiwe kubwa kalitupa kwenye shimo chubwiiiiiii!

MKE kajifunga kanga, kafungua mlango. Ghafla mume kaingia ndani na kumfungia mke nje.

MKE: Nifungulie la sivyo nitapiga kelele majirani waje.

MUME: Piga kelele na wakija uwambie unakotoka usiku huu na khanga moja.

Mambao ya saluni ni shida, cheki kilichotokea kwa huyu

DADA alienda Salon wakati anasukwa akaingia
MKAKA mtanashati,
DADA akaamua kujaribu bahati yake.
DADA:Mambo? KAKA:Poa.
DADA:Mimi na wewe tunaweza kuongea baade?
KAKA:Kuhusu nini?
DADA:Nimekupenda nataka nikutoe out.
KAKA:Sawa ila nitamwambia nini
MKE wangu?
DADA:Aah ilo sio tatizo mdanganye tu,mwambie unakwenda kumtembelea rafiki yako hospitalini.
KAKA:Mwambie mwenyewe huyo hapo anayekusuka.

ย 

Unajua nn kiliendelea?

Cha kufanya msichana akikukimbia halafu atake kukurudia

โ€ฆโ€ฆโ€ฆ Kama msichana atakutupa kwa sababu huna pesa, na baadaye unapopata pesa akarudi tena kuomba msamahaโ€ฆ Ndugu yanguโ€ฆ.. Msameheโ€ฆ. Mpe ahadi ya ndoa, mwambie utamuoaโ€ฆ. iambie familia yake unataka kufanya ukarabati wa nyumba yaoโ€ฆโ€ฆ Ondoa paa lote la nyumba yao halafu TOWEKAโ€ฆ..

๐Ÿ˜‚โ€ฆโ€ฆโ€ฆ ๐Ÿ˜‚โ€ฆโ€ฆ.. ๐Ÿ˜‚

Ulevi noma! Angalia huyu mlevi alichomfanyia huyu jamaa usiku! Ungekua wewe ungefanyaje?

Jamaa alikuwa amelaa na mkewe saa tisa ya usiku akastuka baada ya kusikia mtu anabisha hodi kwenda kufungua mlango
Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao
JAMAA: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
MLEVI: Naomba uje unisukume.
Jamaa akiamini kuwa pengine kuna gari la huyu mlevi limezima jirani akamwambia subiri nikavae viatu. Baada ya kuvaa viatu akatoka na wakaanza kusindikizana na mlevi. Mlevi akaongoza njia
mpaka kwenye mabembea ya jirani akakaa kwenye bembea moja na kumgeukia jamaa na kumwambia.. Okay nisukume basi.

Huyu jamaa kawaweza wapenda vya bure

Jamaa kaingia mgahawani kwa fujo
JAMAA :ย Nipe soda moja na kila mtu mpe yake maana ninapokunywa soda napenda kila mtu anywe
WATU :ย Ha! Ha! Ha! Haaaa!
JAMAA :ย Nipe mchemsho na kila mtu mpe wa kwake maana ninapokula mchemsho napenda kila mtu ale wake
WATU:ย Watu weweeee! Tena safari hii Na makofi juu..
JAMAA :ย Mhudumu, nipe bili na kila mtu mpe yake maana ninapolipa bili napenda kuona kila mtu analipa yake
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Angalia nilivyoingizwa mjini na ujanja wangu wote

Ndio nilikuwa nimeshuka kwenye basi la SAI BABA pale Ubungo, nina Begi kubwa Mgongoni na begi Dogo la Lap Top mkononi, sura inatazama Mbele Very Serious kama nipo kwenye Gwaride la Uhuru!..Mabega juu yanafanya Cheers na Mawingu!, natembea kwa madoidoโ€ฆ..leo nimetoka Likizo Moshi,

“Brother Simu ya ukweli hii..kitu cha Tecno C9 bei poa” hii ilikuwa sauti ya Teja mmoja hivi!

Yaani huyu Teja Bwege kweli,anataka kumuuzia nani sabuni? mimi sio wa kuja!โ€ฆkamwe Siwezi kuibiwa hapa Town,hakuna wizi au utapeli nisioujua!, Mimi nimezaliwa Mwananyamala kwa Manjunju, nikalelewa Tandale kwa Mtogole, Shule ya msingi nimesoma Turiani Magomeni, Hivi Mbwa gani aniibie?โ€ฆkwa Style ipi?

Sipendi kabisa Upuuzi!, Wajinga ndio wataibiwa, sio Mimi!โ€ฆsasa Kwa mwendo wa haraka nikatoka nje kabisa ya Stendi ya Ubungo straight mpaka Stendi ya dala dala za Kariakoo, hapo ndipo nikakutana na Vijana wawili wadogo wakiwa na mzani wa kupimia uzito,โ€ฆhakika napenda sana vijana wanaojituma kama hawa na sio ile Mijizi ya kule ndani Stendi!!,โ€ฆ.hapa sasa nikapata wazo!

“Dogo mnapima uzito kwa shilingi ngapi?”

“Mia mbili tu Kaka!”

”Ok”

Kwa mwendo wa kikakamavu nikapanda juu ya mzani,lengo hapa ni kujua uzito wangu, Mtori niliokula mwezi mzima kule kwa Mshekuu sio mchezo, hapa nahisi nacheza kwenye kg za John Cena,

“Mama wee! Dogo mzani mzima huu kweli? Mbona nina kilo 134?” (Nilihamaki)

“Aaah! Brother huoni umepanda na Mabegi juu ya mzani?”’

Hahaha! kweli nimechanganyikiwa!โ€ฆSasa nikatoa mabegi yote mawili na kurudi juu ya Mzani, hapa ndipo Uzito ukashuka kutoka kg 134 mpaka kg 56!โ€ฆMy God kweli Body la “One Pack ” haliongopi! thats means mabegi yaliniongezea kg 78! duh hii ni hatari!

“Yaani we Dogo kitambi chote hiki kg 56? huu Mzani Mzima kweli?”

Kimyaโ€ฆ

“Dogo huu Mzani vipi?”

Kimyaโ€ฆ

Dogo ana dharau huyu!โ€ฆSasa ndio nikabandua macho yangu toka kwenye kioo cha mzani ili nimtazame huyu dogo asiyejibu!โ€ฆ.ndipo macho yangu yakakutana na Kigoda tupu kilichochongwa Mvomero!โ€ฆDogo hakuwepo!โ€ฆ.na Mabegi pia hayapo!โ€ฆlap top haipo!โ€ฆ.NIMEPIGWA!

Ni dhahiri watoto wa Mjini walikuwa wameniacha juu ya Mzani, wamechukua Lap top ya Milioni na wameniachia Mzani chakavu wa elfu 40, what a stress!โ€ฆ.sasa nilirudisha macho kwenye kioo cha uzito na sasa kilisoma KG 38!โ€ฆyaani dakika hii hii nimepungua kilo zingine 18, Hakiyamama nahisi hata utumbo wangu wamebeba!โ€ฆniitieni Ambulance!

๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ

Angalia Kiingereza kilivyoniponza

Shikamoo kingereza..!

Baada ya kufika Kempiski nikaona menu imeandikwa:

Sauteed white corn, rare lucy beans, garnished with rift potatoes & topped with organic unprocessed guacamole!

Price: TSH 44,000/=

Nikaagiza!

Nilipoletewa ndio nagundua kwamba:ย ni makande na parachichiย ..๐Ÿค”

hapo ndo unagundua mwalimu wa kiingereza alikuwa sio mtu wa mchezo mchezo๐Ÿค’๐Ÿ’จ

Tabia za Kimama kwa wanaume

1, mwanaume kuoga haraka haraka ili uwahi kuangalia igizo, huo ni UMAMA..๐Ÿ˜‚

2, mwanaume kupiga picha umeng’ata Lips na Unapiga na Camera Beauty Plus huo ni UMAMA..๐Ÿ˜‚

3, Mwanaume kuangalia tamthilia na Jamai Raja na Maigizo kwenye chanel ya sinema zetu wakati mechi za kombe la dunia zinaendelea, pia nawe ni MMAMAAโ€ฆ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

4, Mwanaume kuandika ‘Jomon’ badala ya Jamani, kuandika ‘Pw’ badala ya Poa, kuandika ‘Thatha’ badala ya Sasa, kumwandikia mwanaume mwenzio ‘Mambo my’ Huu ni UDADA, tena UDADA wa CHUO..๐Ÿ˜‚
.
5, Mwanaume kunywa soda au Juice na kubakisha, kununua chakula halafu unakibakisha, kubagua bagua chakula na kujamba hovyo hovyo baada ya kushiba, huo nao ni UMAMAA..๐Ÿ˜‚
.
6, Mwanaume kumuuliza mwanaume mwenzio anapata faida gani kuangalia Mpira, pia nawe ni MMAMAโ€ฆ
.
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Tofauti ya mke na mchepuko!!!

MKE NA MCHEPUKO.

Mke ni kama Tv na Mchepuko ni kama Simu.
Nyumbani unaangalia Tv lakini ukitoka unatoka na simu.

Mara chache unafurahia Tv lakini Muda mrefu unacheza na simu yako.

Tv ni bure kwa maisha yako yote, lakini Simu kama hujalipia hupati huduma.

Tv ni kubwa nzito na wakati wote ni ya zamani. Lakini simu ni nzuri, nyembamba, na ni rahisi kubeba.

Gharama za huduma za tv ni ndogo sana, Lakini gharama za huduma za Simu ni kubwa na pia ni lazima kuzitimiza.

Tv ina remote lakini Simu haina.

Kitu muhimu zaidi simu ina njia mbili za kuwasiliana unaongea na unasikiliza lakini Tv unalazimika kusikiliza hata kama hutaki au unataka.

Unaweza kununua Tv mara moja na ukatumia kwa kipindi kirefu lakini Simu mara zote unabadilisha inategemea na fasheni.

Ya mwisho na ya kuzingatia

Tv haina Virusi lakini Simu inayo.

KUWA MAKINI.

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About