SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

๐Ÿคฃ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜‚

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Ushauri wangu kwa leo

Kuna watu wengi sana huwa wanani-challenge ninaposema kwamba ni muhimu sana mtu kuishi katika kusudi la maisha yake. Na moja kati ya hoja zao ni kwamba haya maisha ya sasa mtu akisema aanze kutafuta kusudi la maisha yake atakufa maskini. Hivyo wanaonelea ni bora kufanya chochote kitakachotokea mbele yake ilimradi mwisho wa siku anapata pesa. Yaani anachagua kuwa mtumwa wa Pesa

Kusudi la maisha ya mtu huwa halina ukomo na halibadiliki, kinachobadilika au kufikia ukomo ni malengo ya kuli-ishi kusudi hilo. Kwa hiyo unapopanga malengo yako au unapokuwa na ndoto zako ni lazima uweze kupambanua mwisho wa siku hizo ndoto au hayo malengo yanakwenda kukidhi kiu ya aina gani inayofukuta ndani yako.

Ukifanikiwa kulitambua kusudi la maisha yako na ukafanikiwa kuli-ishi kwa vitendo, ni dhahiri utakuwa maarufu kwenye mazingira yanayohusiana na maisha yako. Mazingira yanayohusiana na maisha yako yapo ndani ya kusudi la maisha yako.

Ni wakati gani mtu anaweza kusema amefanikiwa katika maisha yake? Ni pale ambapo tu mtu anapoweza kutatua tatizo fulani katika jamii; Kugundua uhitaji wa kutimizwa au kukamilishwa kwa jambo fulani katika jamii. Ukiweza kuziba pengo fulani. Ukiweza kupata ufumbuzi wa kukamilishwa kwa hilo jambo kwa faida ya jamii fulani au niseme ukiweza kutatua tatizo hilo hapo unaweza kusema umefanikiwa. Huwezi kutatua tatizo lolote katika jamii kama hujawekeza ndani yako.

Haijalishi ni jambo gani unafanya katika jamii na liko kwenye kiwango kipi ilimradi liko ndani ya mstari wa maisha yako. Kwa mfano, una kamtaji kadogo na unaamua kuanzisha genge la kuuza mahitaji madogo madogo ya nyumbani (hasa jikoni) naamini unakuwa umeanzisha kwa sababu umeona eneo hilo kuna uhitaji wa aina hiyo ya huduma. Wewe unaweza kuwa unafanya tu labda kwa sababu ya shida fulani za maisha lakini wakati huo huo moyo wako unafurahia kile unachokifanya na unajikuta kila siku unabuni mbinu mpya na mikakati wa kuboresha genge lako. Kidogo kidogo unafungua genge lingine sehemu nyingine, na lingine na lingine, nk. Mwishowe unajikuta unatamani kuwa na duka kubwa la vyakula na mahitaji mengine ya kila siku au supermarket. Ukijiona unangโ€™angโ€™ana kwenye โ€œlineโ€ moja ya shughuli (Biashara) basi tambua hilo ndio kusudi lako na ndani yako una zawadi kubwa sana ya kutoka kwa Mungu ya kuhudumia jamii kupitia uuzaji wa mahitaji ya nyumbani.

Lakini ukijiona unatanga tanga leo umefanya shughuli hii kesho umefanya shughuli ile ambazo mwisho wa siku hakuna mahali zinakutana kwa namna yoyote ile japo unapata pesa, basi wewe hujatambua kusudi la maisha yako na usipokuwa makini utakuwa mhangaikaji hadi mwisho.

Ukifanya jambo nje ya kusudi ya maisha yako hutakaa ulifurahie kamwe, litageuka kuwa mateso hata kama linakuingizia pesa nyingi. Unaweza ukawa unafanya kitu nje ya mstari wako wa maisha hata kama kinakulipa mabilioni yaani bado utakuwa kama SAMAKI ALIYETUPWA NJE YA MAJI. Samaki akiwa nje ya maji, zile dakika chache kabla hajafa huwa anahangaika sana na ukimmiminia tone moja la maji kwenye mkia utaona anavyojaribu kutaka kuogelea. Kale katone ka maji kwenye mkia wa samaki akiwa nchi kavu ni sawa na wewe unapokuwa unafanya shughuli nje ya kusudi la maisha yako inyokupa hela nyingi lakini ikatokea katika kuhangaika ukafanya ka-kitu kadogo ambako kako ndani ya kusudi la maisha yako โ€“ moyo waku unakuwa na amani sana na unafurahi sana. Lakini unajikuta huendelei kufanya hilo jambo kwa sababu halikuingizii hela nyingi kwa wakati huo ukilinganisha na lile lingine hivyo unaamua kuendelea kuishi nje ya kusudi la maisha yako ili upate mali za nje na kuunyanyasa moyo wako. Maana yake ni kwamba, kama unafanya shughuli inayokuingizia kipato iliyo nje ya kusudi la maisha yako, hutokaa uache kuhangaika kujaribisha vitu vya aina mbalimbali. Kwa sababu moyo wako hautotosheka wa kuridhika โ€“ HUWEZI KUKATA KIU YA MAJI KWA KUNYWA SODA AU JUISI JAPOKUWA VYOTE NI VIMIMINIKA. . Ndio sababu huwa napenda kusisitiza sana kupata muda kwa ajili ya maisha yako binafsi, hii inakusaidia kujitambua.

Tatizo wengi hatutaki kuanzia chini, tunapadharau huku chini lakini matajiri wakubwa duniani kama unafuatilia historia za maisha yao na jinsi walivyoanza utagundua kwamba walianza wengine wakiwa hawana kitu kabisa. Ukiwa na nidhamu ya maisha hasa kwa kufuata kanuni za maisha, kanuni za biashara/shughuli unayofanya na kanuni za maisha yako binafsi huwezi kuacha kufanikiwa. Mafanikio ni safari. Umaarufu hauji bila kuwa umefanikiwa kwenye jambo fulani hata kama ni ujinga utapata umaarufu kwa wajinga wenzako.

Mafanikio yanaanza kwa wewe kuweza kujitofautisha na maisha yako ya nyuma. Usiruhusu maisha yako ya nyuma kukuwinda na hivyo kuwa kikwazo cha maisha yako unayoyaendea. Usiishi kwa mazoea ya nyuma. Mafanikio ni pale unapoweza kujitambua na kusimama imara katika kanuni za maisha ulizojiwekea na kujitofautisha na watu wengine wote kwa sababu wewe ni wa tofauti, kila binadamu ni wa tofauti ndio mana kila mtu ana nafsi yake mwenyewe hata mkiwa mapacha mmeunganika viungo vya mwili.

MAFANIKIO YANAANZA NAWEWE

Dondoo kuhusu tezi dume

Tezi dume kila mwanaume anazaliwa nayo ambayo inasaidia kutoa maji maji ambayo yanaweza kusaidia kutengeneza mbegu za kiume.

Maji maji hayo yana alkaline ambayo husaidia Wakati Wa tendo la ndoa asidi (acid) iliyopo Kwa mwanamke isiue mbegu za kiume.

Kwahiyo alkaline ikichanganyika na asidi tunapata neutral na hivyo kusaidia mbegu za kiume zisife zinapoingia Kwa mwanamke.

Kwenye uke kuna asidi ambayo inaua kila bacteria wanaoingia.

Acid+base=salt+water

Tezi dume endapo itakuwa zaidi ndo huweza kuleta madhara ambayo ni kufunga mkojo usitoke kwani hubana mrija unaotoka kwenye kibofu kwenda nje.

Tatizo hilo huwakumba zaidi wanaume zaidi ya miaka 50,60,80 japo sio wote.

Kinga yake.
1. Kunywa maji ya kutosha.
2. Kupunguza kula nyama nyekundu.
3. Kupunguza ulaji wa mafuta.
4. Kula matunda na mbogamboga.
5. Kushiriki tendo la ndoa angalau Mara moja au mbili Kwa wiki ili kupunguza maji maji kwenye tezi dume.
6. Kufanya mazoezi ya viungo.

Kwahiyo tezi dume ni kiungo ambacho wanaume huzaliwa nacho isipokuwa kinaleta madhara endapo kitakuwa kupita kiasi na hutibiwa na kupona.

Matibabu yake ni kufanya upasuaji na kupunguza ukubwa pamoja na kudhibiti homoni za ukuaji wake.

Tiba nzuri ya tezi dume ni kufuata ushauri hapo juu na si vidole

Mambo ya msingi kufahamu kuhusu uotaji wa meno kwa mtoto

Mtoto wako atakapofikisha miezi sita, ataanza kuota meno. Watoto wengi wanapotaka kuota meno humwaga mate sana na hutaka kutafunatafuna vitu. Wakati mwingine watoto hutapika au kuhara wakiota meno.

Kwa kawaida kuota meno hakufanyi mtoto kupandwa na joto. Kama mtoto wako atapata joto, yaweza kuwa jambo lingine. Hakikisha umemwona daktari wa watoto.

Yafuatayo ni mambo ya msingi kujua kuhusu uotaji wa meno.

ยทWakati wa kulala, weka kitambaa safi chini ya kichwa cha mwanao ambapo ute utamwagika. Unaweza kibadilisha kitambaa hichi kitakapo loweka ute.

ยทMpatie mtoto kitu cha kutafuna ambacho hakitamdhuru. Usimpatie kitu kidogo sana kwani anaweza kukimeza. Unaweza kumpatia vidunde vya mpira visivyokuwa na majimaji ndani kwani vyaweza kupasuka.

ยทUsifungilie kidunde cha kutafuna kwa shingo ya mwanao. Kinaweza kushikwa na kummyonga.

ยทKuna dawa nyingi dukani za kupiunguza maumivu wakati mwanao anaota meno. Hata hivyo, mwone daktari wa watoto kabla jujampa mwanao dawa yoyote

ยทBaada ya mwanao kuota meno hakikisha unayatunza vizuri

Faida 3 za uvutaji wa sigara

Ni hizi

1. Mvuta sigara hazeeki
2. Mvuta sigara haumwi na mbwa
3. Mvuta sigara nyumbani kwake haingii mwizi

UFAFANUZI

1. Hazeeki kwa sababu hufa mapema kwa kifua kikuu

2. Haumwi na mbwa kwa vile kifua na mapafu yanapooza na hulazimika kutembea na bakora

3. Nyumbani kwake haingii mwizi kwa kuwa inafika wakati ambapo halali:
atakohoa usiku kucha hivyo mwizi anajua yupo macho
kumbe kikohozi tu!

Madhara ya Kujichubua

Katika baadhi ya sehemu duniani watu wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria uzuri, utajiri na uwezo(kifedha) alionao mtu.Katika baadhi ya sehemu watu wenye ngozi nyeusi huchukuliwa kuwa wapo chini ya kiwango, hii hupelekea watu hawa kutumia vingยดarisha ngozi kama krimu, vidonge au nyenzo zingine kubadilisha ngozi zao.

Tafiti zinaonyesha kwamba wavulana na wasichana hupendelea kutumia bidhaa zinazongยดarisha ngozi ili waweze kupata hadhi nzuri katika kundi la familia zao, na jamii. Kwa kweli,hata matangazo yanayoonyeshwa kwenye televisheni mbalimbali huonyesha kitu hiki. Mambo hayo yote huwa na athari kubwa juu ya mawazo ya vijana wa kiume na wakike ambayo hupelekea kuwafanya wachague chochote wanachomudu kati ya krimu au vidonge.

Madhara ya kujichubua ni yapi?
Mtu anaeyejichubua anaweza kupata kansa ya ngozi, chunusi, uvimbe katika ngozi, ngozi kuwa nyembamba,Kuongezeka kwa hamu ya kula na uzito,kutokwa na mabaka, pumu, kupata watoto wenye kasoro, kupata matatizo ya akili, kuharibika kwa ini, kuharibika kwa mishipa ya fahamu pamoja na figo kutokana na kiwango kikubwa cha zebaki(mercury) kilichomo katika krimu,Osteoporosis(kupungua kwa uzito wa mifupa ambapo huongeza hatari ya kuvunjika kwa mifupa)

Baadhi ya madhara haya huonekaa mara moja na mengine hujitokeza kadri mtu anavyotumia vingยดarisha ngozi.

Salamu za kuaga mwaka na kukaribisha mwaka mpya

KWAHERI MWAKA JANA. UMENIFUNZA MENGI.

Mwaka umefika mwisho, zimebaki siku tatu tu
kuingia mwaka mwingine lakini yapo mengi
niliyojifunza mwaka huu na pengine ningepesha
kushare:

1. Kwamba si lazima sana kuwa na rundo la
marafiki kama hawaleti positive effects kwenye
maisha yako. Urafiki wa maongezi yasiyoleta
maendeleo ni uzamani chakavu.
2. Matumizi madogomdogo yasiyo ya lazima
huchelewesha maendeleo makubwa yenye kiu na
mimi. Nmekuwa na matumizi yasiyo ya lazima na
ndio matundu hayo madogo yamezamisha meli.
3. Mungu ndio kila kitu. Anza na maliza siku na
Mungu. Ukikosacho hakukupangia, usiumie,
muombe akuletee atakacho.
4. Harusi zinaumiza. Usipojiwekea kiwango
maalum na idadi ya harusi za kuchangia kwa
mwaka na kwa umuhimu utakuja kujenga nyumba
kwenye harusi za wenzako.
5. Lawama ni muhimu sana ili maisha yaende,
usiogope hasa pale unapokuwa unasimamia lililo
la kimaendeleo kwako. Kumridhisha kila binadam
ni ngumu. Kuna muda ni kwa maendeleo yako
inabidi uwe mbinafsi.
6. Mapenzi ni mazuri ila yasikuzidi ‘kimo’, vipo
vyamaana vya kulilia sio mapenzi. Kikulizacho
ndicho ulichokipa kipaumbele. Mtu aamuapo
kukuliza na wewe ukalia basi umemtukuza.
Mapenzi yasiyosumbua na yaliyojaa mijadala ya
kimaendeleo ndiyo mapenzi yenye afya.
7. Watu waliowengi hasa kwenye mitandao ya
kijamii wana matatzo na ukichaa, usibishane nao
hasa kwenye mambo yasiyokuletea wewe
maendeleo. Usione hasara kuwafanya wajione
washindi.
8. Wazazi ni Muhimu sana, sala zao ni muhimu
kwako. Usipende kuhonga mpita njia akuachaye
siku yeyote ukawasahau wazazi wako. Wapo
watu sikukuu hizi wametumia maelfu ya shilingi
kuhudumia wanawake zao au wanaume zao
wapitaji wakasahau wazazi wao hata kwa pesa
ya dawa.
9. Kuahirisha mambo ni ugonjwa wa kuridhika na
dhiki. Uahirishapo atakaye uwe chini anafurahi.
Muaibishe shetani kwa mipango thabiti.
10. Panga kwaajili ya MWAKA kabla haUjafika,
kupanga kunakupa nafasi ya kujihakiki.
Mpya mwaka wa kucheza na ‘altenatives’.

SEASON GREETINGSโ€ฆ..HAPPY NEW YEAR.

Mwanamke kuamka mapema asubuhi kunapunguza uwezekano wa kupata saratani ya matiti

Kuamka asubuhi na mapema hupunguza uwezekano wa mwanamke kupata saratani ya matiti.

Kulingana na shirika la habari la BBC,wataalamu wa chuo kikuu cha Bristol nchini Uingereza wamewafanyia tathmini wanawake 400,000 na kutambua kuwa sio rahisi kwa mwanamke anaeamka asubuhi na mapema kupata saratani ya matiti.

Utafiti huo umeoneysha kuwa wanawake wanaoamka wamechelewa wana hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo ukilinganisha na wale wanaoamka wamechelewa.

Utafiti wa hapo awali ulionyesha kuwa kufanya kazi mpaka usiku wa manane kunaongeza hatari ya kupata saratani.

Matokeo ya utafiti huo yatawasilishwa kwenye Mkutano wa Taifa wa Taasisi ya Utafiti wa Saratani huko Glasgow.

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    ๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About