SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

πŸ€£πŸ˜ƒπŸ˜‚

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Mume mgonjwa kazua mpya baada ya kuruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospitali alipokuwa kalazwa

John aliruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospital ya
Vichaa, akapakiwa ktk ambulance hadi karibu na
nyumbani kwake, akaulizwa kwako unapakumbuka?

akajibu ndio nyumba yangu ilee, mara wakatoka
watoto wawili wamevaa uniform akasema watoto
wangu walee wanakwenda shule..
Akatoka mwanamke akasema na mke wangu yulee,
Ghafla akatoka mwanaume john akasema mimi
yuleeeeeeee…. naenda kazini!! JE, NI KWELI
AMEPONA??

Faida za kuvaa saa ya Mkononi

leo tutajaribu kuongalia sababu kwanini tunatakiwa tuvae saa za mkoni yaani nini haswa kinatulazimisha kuvaa saa za mkononi , hebu kwa tujue saa za mkononi zilianza kuvaliwa mwaka gani.

Kabla ya vita ya kwanza ya dunia kulikuwa kuna saa za mfuko yaani pocket watch saa hizi zilipendwa sana enzi hizo. ila katika kipindi cha mapigano wanajeshi walihitaji saa ambayo itakuwa rahisi kuangalia sio mpaka watoe mfuko hivyo walianza kuvaaa saa mkononi na ikawa rahisi sana kuangalia wakati wa mapigano ..na vita ilivyoisha saa ikaonekana ni style sasa ikabidi watu waanze kuvaa kama fashion mitaani huko ulaya. sasa tuje sababu zinapelekea wewe au mimi kuvaaa saa japo simu zipo

SAA HUTUNZA MUDA VIZURI;

Japo kuna simu kuna computer hakuna kifaa kinachopita saa kwa utunzaji mzuri wa muda hasa saa za mabattery ya quartz za mwaka 1955 pia saa ya mkononi humpa mtu urahis wa kuangalia wakati muda wowote atakoa pia kuanza kufungua mfuko au bag

SAA ZINA NGUVU MBALIMBALI;

Saa mara nyingi huwa zina sifa mbalimbali kama uwezo wa kutoa ingia maji hivyo kufanya mtumiaji kuvaa popote atakapo hata kwenye maji kuna zingine ni ngumu kupasuka yaani shock resistant hasa kwa saa za company ya gshocK au skmei

SAA HAZIITAJI KUCHARGE’;

Kama tulipo sema saa ni simple sana hautaji wewe kuichaji maana kuna saa ambazo battery hukaa hata miaka mitano bila kuisha hasa saa kijapani pia kuna saa ambazo huwa hazitumii kabisa battery hizi huenda na mawimbi ya mkono wako

SAA NI FASHION;

Saa za mkononi pia ni fashion huongeza umaridadi na urembo wa mtumiaji au mmiliki wa saa husika. katika vitu wataalam wa fashion huwa wanashauri ni kuvaa saa mkononi ukitaka upendeze zaidi na mavazi yako wewe vaa saa ya mkononi muonekano wako utaongeza na utang’ara zaidi pia wanawake na wanapenda wanaume wanaovaa saa nzuri hahahahah natania sina uhakika ila well wanaume tuvaa saa ili tupendeze kitaa au maofisin wakuu

SAA HUTENGENEZA UHUSIANO KATI YA WEWE;

Asikwambie mtu watu wanao vaa saa mara nyingi huwa ni matime keeper wazur pia hujali muda wao tena ngoja nikukumbushe ndugu yangu we umeshahau kipindi tunasoma matime keeper wote walichagulia kisa anamiliki saa tu tena saa nzuri.. hivyo mara nyingi ukimiliki saa automatic utautunza muda wako sahihi ndugu yangu kuvaa saa.

Angalia binadamu walivyo

Angalia Binadamu walivyo!,

“Ukitafuta sana anakuita MCHAWI,”

Ukifanikiwa sio BURE,

“Ukitulia MVIVU,”,

Usipovaa vizuri MCHAFU,

Ukidili sana na masomo unajifanya MSOMI,

Usipodili nayo MJINGA,

Ukisema sana MBEA,

Ukiwa mkimya JEURI,

Ukiwasaidia watu UNATAKA SIFA,

Usipowasaidia ROHO MBAYA,

Ukiwa na kazi UNAJISIKIA,

Usipokua nayo MZEMBE.

Hivyo BINADAMU ndivyo walivyo wewe jali MAISHA YAKO TU NA MAENDELEO YAKO.

MUNGU akulinde na shari zao.

FURSA HAIJI MARA MBILI: Jinsi unavyoweza kupata faida au hasara ukitumia Nafasi au fursa uliyonayo

Kwenye maisha fursa moja tu inatosha kabisa
kubadilisha hali yako ya sasa na kukuweka kwenye
kiwango kingine kabisa cha mafanikio.Kuna watu
wengi sana ambao waliwahi kufikiria kuwa maisha
yao yatachukua miaka mingi sana kabla
hayajabadilika na kwa mshangao wao walipoanza
kufanya vitu sahihi wakakutana na mabadiliko
makubwa sana katika maisha yao kwa kupitia
fursa moja tu.

Kufanikiwa kwenye maisha ni matokeo ya kujua
mambo sahihi ya kuyafanya.Ni kama ilivyo wakati
unapotaka kufungua mlango
uliofungwa,unachohitaji ni ufunguo sahihi wa
kutumia na sio vinginevyo.
Ili ufanikiwe lazima uwe mtu mwenye bidii na
ambaye unawathamini watu bila kujali hali zao za
sasa.Ili kutoka hapo ulipo na kwenda kule
unakotaka unahitaji watu wa kukuunganisha na
fursa mpya,kukuonyesha njia nzuri ya kufanya
mambo,wa kukurekebisha na watu ambao
unaweza kujifunza kwao.

Mwaka 2012 mmiliki wa kampuni kubwa ya vifaa
vya michezo ya Modell nchini marekani,bwana
Mitchell Modell alifanya tukio la ajabu sana lililotoa
funzo kubwa la mafanikio katika maisha yetu ya
kila siku.Aliamua kujibadilisha mwonekano wake
kwa kunyoa nywele zake zote na kuweka ndevu
nyingi sana za bandia na pia kuvaa hereni sikio
moja.Kisha baada ya hapo alienda kuomba kazi
kwenye kampuni yake na akaanza kufanya kazi ya
daraja la chini kabisa.
Akiwa ameajiriwa bila watu kujua kuwa ndiye
mmiliki alikutana na wafanyakazi wengi sana wa
aina mbalimbali.Kati ya wafanyakazi katika tawi lile
alikuwepo dada mmoja anayeitwa Angel ambaye
alikuwa ana watoto 3 ila hakuwa anakaa na mume
wake na kwa muda wa miaka 2.Lakini pia,Angel na
watoto wake wamekuwa wanaishi kwenye vibanda
kwani hakuweza kulipia pango kwenye nyumba
nzuri ya kuishi.Gharama zote za
chakula,ada,matibabu na mavazi ya watoto yote
ilikuwa juu yake.
Pamoja na hali yake hiyo,Angel alikuwa ni
mfanyakazi anayewahi kazini kila siku na alikuwa
anafanya kazi kwa bidii sana.Hata wakati wengine
walikuwa wanalamika juu ya mshahara,yeye kazi
yake ilikuwa ni kuwatia moyo na kuwahamasisha
wafanye kazi kwa bidii sana akiamini ipo siku
mambo yatakuwa mazuri.Kila wakati Bwana
Mitchell alipokuwa anamkuta Angel,alikuta
anafanya kazi zake kwa umakini na hata akikuta
anaongea na wenzake basi itakuwa ni kuwatia
moyo na kuwapa hamasa na kuwataka waaache
kulalamika.
Wakati Bwana Mitchell akiwa kama mfanyakazi
mpya alihitaji sana msaada wa kufundishwa jinsi
mfumo unavyofanya kazi na mambo mengine.Kila
mmoja alikuwa hayuko tayari kumfundisha,ila
Angel alikuwa tayari kumfundisha na kumsaidia
hata na kazi ambazo alikuwa hawezi kuzifanya
kutokana na ugeni wake.Na kwa sababu ya ukaribu
wake ndipo alipoweza kumfahamu Angel na
kuyajua maisha yake kwa undani.
Baada ya siku kadhaa za kufanya kazi bila mtu
yoyote kujua kuwa ndiye mmiliki,ndipo alipoamua
kufanya kitu kikubwa kwa Angel.Kwanza
alimpandisha cheo na kumfanya kuwa meneja
msaidizi na kisha alimpa zawadi ya dola laki mbili
na hamsini(Takribani shilingi milioni 500 za
kitanzania) ili aweze kupata nyumba nzuri ya
kuishi.
Baada ya tukio hili kutokea wafanyakazi wengi
sana walijilaumu na walitamani sana kupata fursa
upya kama wangejua kuwa yule alikuwa ni mmiliki.
Ndivyo maisha yalivyo na ndivyo safari ya
mafanikio ilivyo.mara zote huwezi kujua ni wakati
gani fursa kubwa inayohusu maisha yako
itakutokea.Kilichomfanya Angel kufanikiwa ni ile
hali ya kuwa ni mtu ambaye hakuruhusu jambo
lolote limzuie kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi
kila wakati hata kipindi ambacho maisha yake
yalikuwa magumu.
Mara nyingi unaweza kujikuta katika hali ambazo
zinakatisha tamaa na zinakupa uhalali wa kila
namna wa wewe kuwa mtu wa kulalamika na
kukata tamaa.Hebu fikiria mama wa watoto
watatu,analipwa mshahara mdogo lakini bado
anawahi ofisini na huwa halalamiki.Kuna fursa
nyingi kwenye maisha unazikosa kwa sababu ya
malalamiko juu ya hali inayokuzunguka.Kitu cha
msingi unachotakiwa kujua ni kuwa kulalamikia
kitu au mtu hakuwezi kubadilisha hali yako ya sasa
lakini kufanya kwa bidii kunaweza kufungua fursa
nyingi kubwa katika maisha yako.
Inawezekana kazi unayoifanya ni ndogo
ukilinganisha na ndoto kubwa
uliyonayo,inawezekana mshahara unaolipwa sio
mkubwa kama unavyotaka,inawezekana biashara
yako bado haifanyi vizuri kama mipango yako
ilivyo ama hauna mtaji kiwango
unachotaka.Katikati ya hali hii unachotakiwa
kufanya sio kuanza kulalamika na kukata
tamaa,unatakiwa kuwa kama Angel,weka kiwango
kikubwa cha bidii kwani kwa kufanya hivyo
utakuwa unajifungulia milango mikubwa zaidi
katika maisha yako.
Kuanzia leo fanya maazimio katika maisha yako
kuwa utakuwa mtu wa kufanya kwa bidii kile
ambacho unakifanya hata kama itakuwa kwenye
mazingira magumu,kwani kwa kufanya hivyo
utakuwa unajitengenezea fursa kubwa sana mbele
yako.Ukiamua kuishi kwa mtazamo huu,muda
mfupi sana ujao utafanikiwa.
Kitu kingine cha msingi cha kukizingatia hapa ni
kuwa usidharau watu katika maisha yako.Kati ya
mafumbo makubwa ambayo Mungu ameyafumba
ni kuhusu hatima za watu ambao tunakutana nao
kila siku katika maisha yetu.Hakuna kitu kibaya
kama kumdharau mtu eti kwa sababu anaonekana
kwa wakati huo hawezi kukusaidia
chochote.Jifunze kumuheshimu na kumthamini
kila mtu.
Ilil ufanikiwe katika maisha yako jifunze kuishi
kama Angel,jifunze kuwa na bidii ya kazi hata
katika mazingira magumu lakini pia jifunze
kuthamini kila mtu ambaye unakutana naye-
Kuanzia mdada wa kazi
nyumbani,mlinzi,mfagizi,kondakta wa daladala
hadi dereva wako.Kila mtu ni muhimu na ana
mchango katika maisha yako.Kanuni ya maisha
inasema-β€œHusiana na watu kama wewe unavyotaka
watu wengine wahusiane na wewe pia”. Kuanzia leo
ishi na kila mtu kama β€œMitshell wako” wa
kukuunganisha na fursa kubwa uliyokuwa
unaisubiria.
Sina shaka kuwa fursa yako kubwa iko njiani
inakuja,usikate tamaa.
Kumbuka kuwa ndoto Yako Inawezekana,
See You AT The Top.
Β©Joel Nanauka

Safari ni safari

FUNDISHO : SAFARI NI SAFARI

Maisha ni ya ajabu sana, wakati mwingine maisha ni mazuri na mwingine ni mabaya, katika maisha yetu tumeshapitia safari nyingi sana na za aina mbalimbali kwa nyakati mbalimbali. Lakin kiukweli kila safari ni safari tuu.

Japokua kila safari ina changamoto zake lakini mwisho wake ni ule ule , kila safari ina uzuri na upekee wake.

Vile vile kila safari ina ubaya wake, kwa mfano kila safari ina gharama yake kulingana na upekee wake.

Usiwe na wasiwasi na mashaka na aina ya safari ulionayo, jipe moyo utaimaliza na kupata ulichokitarajia. Haya ndio maisha na wote tunatakiwa tuyafurahie.

Ingawa kila mtu ana safari yake bado wote tunatakiwa tufurahie pamoja kwa safari tuliyo nayo. Hata Uwe Na safar ya aina gani wewe furahi tuu. Hii ni kwa sababu safari mwisho wake ni mmoja kwa wote burudani ni ile ile

Safari🍺 ni safari 🍺hata kama ni ya chupa au ya kopo mwisho wake πŸ’€πŸ’€

πŸ˜‹πŸ˜œπŸ˜œπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Ulijua ni nn??

AMINI UNA AKILI YENYE UWEZO MKUBWA WA KUBUNI WAZO LA KUWEZA KUKUSAIDIA KUFANIKIWA KIMAISHA

AMINI UNA AKILI YENYE UWEZO MKUBWA WA KUBUNI WAZO LA KUWEZA KUKUSAIDIA KUFANIKIWA KIMAISHA.

Huwa nikikaa na kufikiri ni namna gani binadamu aliweza kubuni ndege, meli kubwa hasa za mizigo, gari na vitu vinginevyo na badae kuja kuwa msaada mkubwa katika dunia yetu ya siku leo hata kurahisisha maisha katika eneo fulani lililokuwa na ugumu kwetu, basi nauona uwezo wa Mungu aliouweka ndani ya binadamu huyu ingawa yeye binafsi kama binadamu wakati mwingine hatulitambui hilo na kama tunalitambua basi ni wachache na wakati mwingine hatujakaa vizuri kuitumia hii fursa ya uwezo huo tuliopewa. Hii inaonyesha ni jinsi gani binadamu alivyo na uwezo mkubwa wa kufanya ubunifu kwa kupitia akili aliyonayo na kuleta mageuzi na mshangao mkubwa katika ulimwengu tunaoishi.

Hebu tazama wengi wa wabunifu waliojitoa kwa kuumiza akili na kubuni vitu vipya katika ulimwengu huu tunaoishi leo hii, ndio tunaowaona matajiri katika dunia hii ya leo kuliko watu wengine waliokataa kutumia uwezo na akili zao walizopewa na Mwenyezi Mungu na zaidi sana kubakia kulalamikia watu wengine wanaofanikiwa. Nataka nikuambie unauwezo mkubwa sana ndani yako unaoweza kuutumia ili kubuni jambo kubwa litakaloleta matokeo chanya na kuwa msaada mkubwa katika jamii yako unayoishi na kwako pia.

Ndio. Una uwezo mkubwa sana tena sana unaoweza kuleta matokeo chanya na makubwa katika ulimwengu wako na ukasahau hata habari ya kuajiriwa na kuanza kujiajiri binafsi kupitia jambo ulilobuni. Tatizo ni kwamba hupendi kutumia akili yako kufikiri kwa upana na kwa kiwango cha juu kwa hofu ya kupoteza muda, kuumiza akili, kutokutaka matatizo (stress), nakadhalika. Kila siku umekuwa ni mtu wa kusema β€œmimi sitaki kuumiza akili yangu” mara unasema β€œmimi masuala yanayochosha akili yangu siyataki” unataka kufanya mambo marahisi marahisi ili utoke kimaisha, ni gumu sana kwa namna hiyo rafiki.

β€œIf you do what is easy your life will be hard, but if you do what is hard your life will be easy.” – Les Brown

Nataka nikuambie akili yako inauwezo mkubwa sana, narudia β€œinauwezo mkubwa sana” tena sana wa kubuni biashara ya kukutoa kimaisha, kutatua matatizo yaliyo magumu kwa jamii iliyokuzunguka, kuleta mbinu na mikakati mipya kwenye kazi au ofisini ili kusaidia kampuni kusimama, nakadhalika. Tatizo unajitetea na kujenga hofu kubwa ndani yako ya kujitoa na kufikiri ili kuhakikisha unaleta matokeo mapya na makubwa mahali ulipo muda huu. Hebu fikiri kama binadamu huyu huyu unayemjua na aliye kama wewe alibuni balbu za umeme anaitwa Thomas Edison kutoka nchini Marekani; na zaidi sana binadamu huyu huyu kama wewe aliweza kugeuza historia ya muonekano wa magari na kuja na kitu kipya zaidi anaitwa Henry Ford, na binadamu huyu huyu aliweza kubuni biashara ya kuuza kuku walioandaliwa kama chakula na hatimaye kuwa na mgahawa mkubwa wa KFC uliosambaa karibu nchi 123 duniani kote anaitwa Harland Sanders. Na wengine wengi sana ambao sitaweza kuwamaliza kwa kuwataja wote mahali hapa siku ya leo.

Naamini wapo watu wanaoweza kujitetea na kusema kwa kuwa hao ni watu weupe yaani wazungu na sijaona mtu mweusi hata mmoja hapo. Hebu fikiri ni watu wangapi wanabiashara ambayo leo hii inawaingizia mabilioni ya pesa na wakati mwingine biashara wanazozifanya ni za kawaida na zilizokuwa zikidharaulika na watu kwenye jamii zao na wapo hapa afrika. Angalia mtu kama Aliko Dangote kwa sasa zaidi ya kujishughulisha na uzalishaji wa cement na bidhaa nyingine za ujenzi na hata biashara zake kubwa nyingine kwa sasa ameenza kuzalisha nyanya na kuuza kwenye nchi yake huko nchini Nigeria. Ulitegemea mtu kama huyu ambaye ni tajiri wa kwanza afrika kuwaza kufanya biashara kama hiyo ya nyaya kwa sasa? Yawezekana wewe ulipoambiwa kuuza nyanya uliona ni biashara kichaa na haina maana ya kuifanya. Ukweli ni kuwa usipende kuanzia pakubwa bali anza na madogo ili kukupeleka kwenye kilele chako cha mafanikio na kutimiliza ndoto yako uliyonayo.

Hivyo hivyo kwa Bakhresa, Mengi, Dewji, Sheria Ngowi na wengine wengi tunaowaona nchini mwetu Tanzania wamefanikiwa kiuchumi, hii yote ni kutokana na kuamua kubuni kitu kipya kilichoweza kuwa msaada mkubwa kwenye jamii yao na kuweza kuwaletea wao mafanikio makubwa katika maisha yao. Sheria Ngowi pamoja na kusomea masuala ya Sheria nchini India lakini alijua bado ana kitu cha ziada ndani yake kinachoweza kumlipa na kumfanya awe na uhuru wa kifedha na maisha mazuri sawa na anavyotaka. Leo hii ni mbunifu wa mavazi Africa nzima inamjua na kumtazama. Jiulize kama asingetumia akili yake kwa kufikiri zaidi na kufuata ndoto yake aliyokuwanayo leo hii ingekuwaje kwake na kwenye jamii yake iliyohitaji mchango wake?

Nataka nikuambie huwezi kutoka kwa siku moja ni lazima uumize kichwa na akili yako leo hii na kujua ni nini cha kufanya kinachoweza kukupa uhuru unaoutaka kesho. Na suala la kuumiza kichwa chako na akili ni sasa na si kesho, narudia tena suala la kuumiza akili yako kwa ajili ya kubuni wazo la kukutoa kimaisha β€œni sasa na si kesho” kama unavyofikiri. Usiridhike na maisha yako unayoishi leo, usiridhike na kipato unachokipata huku sema ukweli ndani ya moyo wako na kwa uhalisia hakikutoshelezi kabisa kufikia kwenye kilele cha mafanikio makubwa unayoyataka. Usikubali kuwa mvivu wa kuumiza kichwa na kutumia akili yako kwa ajili ya kuja na kitu kipya kinachoweza kuleta manufaa kwako na kwa jamii yako iliyokuzunguka, anza kuwa mbunifu ili uweze kufikia ndoto yako ya maisha.

Umiza kichwa kuanzia sasa na amini katika wazo (idea) utakayoipata ndani ya moyo na akili yako ili kukusaidia na wewe kuwa miongoni mwa watatuzi wa matatizo katika ulimwengu huu. Unaweza kutumia matatizo yaliyopo kwenye jamii yako kama sehemu ya kukupatia wazo jipya na baada ya hapo kubuni njia na mkakati wa kulitatua tatizo ili kuleta matokeo chanya katikati ya watu waliokuzunguka na kwako pia. Mwombe Mungu akupe mwongozo wa kukusaidia kulitimiza na kulifanya hilo wazo (idea) kuwa wazi katika ulimwengu wa nje ili usibaki na wazo lililo kwenye akili na kichwa tu pasipo kuleta matokeo na mchango wowote makubwa kwa watu wako.

Nakusihi usisubiri kesho. Usione una siku nyingi za kuwaza au kuleta matokeo (ku_implement) ya hilo wazo lako (idea) uliyonayo au ndoto ya siku nyingi unayotembea nayo kila kukicha pasipo kuweka vitendo vya kuifanya izae faida na matunda kwako. Anza leo kuhidhilishia dunia kuwa nawe unauwezo mkubwa aliouweka Mungu ndani yako. Usijikatae wala usiogope kukataliwa na wengine pale utakapofanya uamuzi wa kuja na kitu chako kipya kwenye jamii yako, kumbuka kukataliwa ni sehemu ya kukupeleka katika mafanikio. Kadri unavyoongeza kukataliwa ndio unavyoongeza kufanikiwa.

Kama unahitaji kuwa mbunifu wa mavazi kama sheria ngowi anza kubuni leo hii au ikibidi mtafute na uwe chini yake na afanyike kuwa msaada na mshauri wako (mentor) wa hicho kitu unachotaka kukifanya. Amini inawezekana kwani watu waliofanikiwa si wachoyo unapojishusha na kuonesha uhitaji wa kujifunza kutoka kwao. Kama unataka kuwa mfanyabiashara mkubwa kama Dangote lakini bado huna wazo la biashara. Basi elewa una uwezo mkubwa wa kuumiza kichwa na akili kuanzia sasa na ukapata wazo linaloweza kuishangaza dunia yote hapo badae.

Lakini kumbuka si lazima ukaja na kitu kipya kabisa kwani tambua unauwezo pia wa β€œkuboresha wazo” au kitu fulani kinachofanyika na watu wengine ila wewe ukaleta ubunifu mpya kwenye hicho kitu na kuleta utofauti mkubwa kwenye eneo (industries) hiyo. Na hii ndio njia inayofanyika kwenye makampuni ya simu, magari, televisheni, nakadhalika. Leo hii samsung akileta simu yenye kamera yenye uwezo wa mega pixel 16 kesho yake utasikia Iphone ametoa simu yake mpya yenye kamera yenye uwezo wa mega pixel 20. Huu ni ubunifu tu ili kuzidi kutawala soko na kuteka wateja wa soko la simu ulimwenguni kote. Nataka nikuambie nawe unauwezo wa kufanya ubunifu mkubwa kwenye jambo lolote lile ili kukuletea mafanikio makubwa na hatimaye ukafanikiwa kufikia katika ndoto yako.

Nataka nikuambie una mawazo milioni na zaidi ndani yako ambayo hadi sasa dunia inayasubiri ili yaweze kuwa msaada kwa watu wengi na kufanyika kuwa faraja kubwa hata kwa watu waliokata tamaa. Ndio. usishangae wala sijakosea kusema ni mawazo β€œmilioni na zaidi” uliyonayo ndani yako. Ni wewe tu umejidharau, ni wewe unajiona huwezi kuwaza na kutoka na kitu kipya au kilichojaa ubunifu, ni wewe tu unajaa hofu ya kukataliwa kisa unaona utaonekana unaiga, huigi kwani hata waandishi wanaoandika kama mimi wanaandika kutokana na walichokipitia kwenye maisha na kujifunza kwa wengine, ni wewe tu unajiona huna lolote na si chochote katika ulimwengu huu hivyo huwezi kufanya mambo makubwa. Unajikosea heshima kwa kujiwiza mawazo hayo ya chini na kumkosea Mwenyezi Mungu yeye aliyekuumba na kukupa akili zote timamu ili uzitumie kwa ajili ya kuwaza na kubuni mambo mapya yanayoweza kuwa msaada mkubwa kwako na kwa jamii yako iliyokuzunguka. Anza kuwaza na kuumiza akili na kichwa chako leo hii, na amini kesho utafanikiwa.

JIAMINI NA AMINI UNAWEZA. ISHI NDOTO YAKO.

Kichekesho cha mwalimu na wanafunzi

Mtoto: Mwalimu mimi nataka nisome darasa la nne kwani hili la3 halinifai.

Mwalimu: Kwa nini unasema hivyo?

Mtoto: Nina akili…

Basi mwalimu akamueleza mkuu wa shule na mkuu kaitisha interview kwa dogo. Maswali ni haya….

Mwalimu: Kwenye ndege kuna matofali 20 tukitoa moja tukalidondosha chini yatabaki mangapi?

Dogo: Yatabaki 19.

Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka tembo kwenye friji.

Dogo: Unafungua friji unamuweka tembo kisha unafunga.

Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka nyani kwenye friji.

Dogo: Unafungua friji unamtoa tembo ulemuweka..unamueka nyani kisha unafunga friji.

Mwalimu: Kuna sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa simba, wanyama wote wameenda kasoro mmoja. Ni nani na kwa nini?

Dogo: Ni nyani kwa sababu tumemuweka kwenye friji.

Mwalimu: Bibi kizee amevuka mto unaokuwaga na mamba na viboko wakali, aliwezaje?

Dogo: Aliweza kwani mamba na viboko nao walienda kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa simba.

Mwalimu: Ingawa bibi kizee alivuka mto, baadae alikufa. Unadhani ni kwanini alikufa?

Dogo: Alidondokewa na lile tofali tulotoa kwenye ndege na kutupa chini.

Mwalimu mkuu: Huyu dogo akasome chuo kikuu….
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†

Ifahamu Saratani ya Tezi Dume, chanzo, Dalili, Uchunguzi na Tiba

Tezi Dume ni nini?

Tezi dume (prostate), ni tezi iliyo kwenye kizazi cha mwanaume inayozalisha maji maji yanayobeba manii/shahawa. InaizungukaΒ urethra, mrija unaotoa mkojo kwenye kibofu kwenda nje. Tezi dume ya kila mwanaume huongezeka ukubwa kadri umri unavyoongezeka. Kadri tezi inapokua na kuongezeka ukubwa,inaweza kukandamizaΒ urethraΒ na kusababisha matatizo ya kibofu na matatizo ya kukojoa. Tezi dume inapoongezeka ukubwa huitwa ”benign prostatic hyperplasia” kwa kifupi ”BPH”. Hii sio saratani, na haiongezi hatari ya kupata saratani ya tezi dume.

Saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vinavyotokana na kansa kwa wanaume duniani. Pia ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wenye umri wa miaka 70 na kuendelea. Hata hivyo, satarani ya tezi dume kwa sasa inawapata sana wanaume kuanzia miaka 25. Lakini kabla ya kuendelea mbele hebu kwanza tujue tezi dume ni zipi.

Kama tulivyosema neno saratani ni jina la gonjwa ambalo hutokea wakati chembe chembe za uhai au seli katika sehemu fulani ya mwili zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili na kutengeneza vijiuvimbe vidogo vidogo. Kwa kawaida seli huwa zinajigawa, kupevuka na baadaye kufa kwa kufuata taratibu za mfumo wa mwili. Lakini seli za saratani hazifuati mfumo huo. Badala ya kufa, zenyewe huishi muda mrefu kuliko chembe chembe za kawaida na wakati huo huo huendelea kutengeneza seli nyingine na kuwa uvimbe wa saratani au tumour.
Tezi dume linapatikana katika mwili wa mamalia dume tu na pale seli katika kiungo hicho zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili hapo ndipo mtu hupata saratani ya tezi dume. Ugonjwa huu pia hujulikana kama saratani ya kibofu cha mkojo. Saratani ya tezi dume huwapata wanaume tu na hasa wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea. Kutokana na tafiti mbali mbali, saratani hii imethibitika kushika nafasi ya pili, ukiachia mbali saratani ya mapafu kwa kusababisha vifo vya wanaume wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea.
Tafiti za Chama cha Saratani cha Marekani (ACS) na cha Afrika Kusini (CANSA) zimebaini kuwa, mwanaume mmoja kati ya sita hupata saratani ya tezi dume katika uhai wake. Kutokana na takwimu za mwaka 2010 za dunia nzima, malaria iliua watu laki tano, kifua kikuu watu milioni 2.1, Ukimwi watu milioni 1.8 na saratani watu milioni 9.9. Kwa mujibu wa takwimu hizo, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani ni kubwa ikilinganishwa na ya magonjwa mengine. Dk Emmanuel Kandusi ambaye ni miongoni mwa waathirika wa saratani hiyo, na mwanzilishi wa kampeni ya kuangamiza saratani ya tezi dume nchini Tanzania ya ’50 Plus Campaign’ anasema kuwa, ugonjwa huu ukitambuliwa mapema huweza kutibika kwa urahisi. Ameongeza kuwa, kutokana na ugonjwa huo kuwa hatari nchini, ifikapo mwaka 2020 unatarajiwa kuua watu milioni 20.

VIHATARISHI VYA TEZI DUME

Kuna vihatarishi vingi vinavyochangia mwanamume kupata saratani ya tezi dume. Vifuatavyo ni baadhi yake:-

πŸ‘‰πŸΏKwanza kabisa ni umri. Nafasi ya kupata saratani ya tezi dume huongezeka sana hasa ukifikia umri wa karibu miaka 50 na kuendelea.

πŸ‘‰πŸΏNasaba ni kihatarishi kingine ambapo wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu huwa katika hatarini ya kupata kansa hiyo kutokana na kurithi jeni za ugonjwa huo.

πŸ‘‰πŸΏSuala jingine ni lishe ambapo wanaume wanaopenda kula nyama au (red meat) na walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama huwa katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume.

Vilevile wataalamu wanatumbia kuwa, wanaume wasiopenda kufanya mazoezi, wanene na wenye upungufu wa virutubisho vya Vitamin E pia wako kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya kibofu cha mkojo.
Wanaume wengine walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni pamoja na wale wenye asili ya Afrika (Weusi) ikilinganishwa na wazungu, wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali, wanaofanya kazi katika viwanda vya kutengeneza matairi na wachimbaji madini, hususan aina ya cadmium.

DALILI ZA TEZI DUME

Hayo yote yakiwa ni tisa, kumi ni je, dalili za saratani ya tezi dume ni zipi?Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dume hazitofautiani na zile za kuvimba kwa tezi dume au BPH.
Dalili hizo ni pamoja na,

1) Kupata shida wakati wa kuanza kukojoa.

2) Kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa.

3) Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu.

4) Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku.

5) Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote

6) kutoa mkojo uliochanganyika na damu.
Pamoja na kueleza dalili hizo watu wanapashwa kutambua kuwa, mwanaume anapoanza kuona na kuhisi baadhi ya dalili hizo, anapaswa kujua kuwa, seli za saratani katika tezi dume lake huwa zina umri wa takribani miaka saba na kuendelea.
Iwapo saratani imesambaa mwilini kiasi cha kuhusisha sehemu nyigine za mwili, mgonjwa anaweza kuwa na maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni.
Aidha mgonjwa huwa na dalili nyingine zinazoweza kumpata mgonjwa mwingine yeyote wa saratani kama vile kupungua uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu na kadhalika.

UCHUNGUZI WA TEZI DUME

Wanaume wanashauriwa kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya kibofu cha mkojo au prostate cancer kwa kuwa imegundulika kuwa wanaume wengi wakiziona na kuzihisi dalili hizo huona soni kwenda kumwona daktari na kufanyiwa uchunguzi.
Baadhi ya watu huzihusisha na magonjwa ya zinaa au na dhana potofu za kishirikina. Wapo wanaokwenda mbali zaidi hata kuuita ugonjwa huo kuwa ni wa walawiti huku wengine wakiurahisisha kwa kuuita kuwa ni ugonjwa wa utu uzima kana kwamba saratani ya tezi dume ni jambo la kawaida kwa watu wazee.
Mambo kama hayo hupelekea wanaume wengi kujinyanyapaa wenyewe na hata wengine kujitibu kwa uficho au kwa kutumia waganga wababaishaji mpaka pale mambo yanapokuwa yamewazidi ndipo hupelekwa mahospitalini na mara nyingine huwa wamechelewa na kupoteza maisha yao bure kwa ugonjwa ambao ungeweza kutibiwa mapema.
Kwa ajili hiyo tunatoa wito kwa wanaume kutoona soni na kuwa na tabia ya kufanyiwa uchunguzi wa afya kwa ujumla, na hasa tezi dume angalau mara moja kwa mwaka.
Kuna vipimo viwili ambavyo daktari anaweza kumpima mwanaume ikiwa ni hatua ya kwanza ya kugundua ugonjwa huo. Vipimo hivyo vya kwanza ni “Digital Rectal Exam (DRE)” na cha pili ni “Prostate Specific Antigen (PSA)”. DRE pamoja na PSA huonesha uwepo wa tatizo kwenye tezi dume, lakini vipimo hivi havina uwezo wa kutofautisha iwapo tatizo hilo linamaanisha saratani au uvimbe katika tezi dume. Hivyo basi, ili kuweza kutofautisha kati ya magonjwa hayo mawili, kipimo kiitwacho Prostate biopsy hufanywa. Baada ya vipimo hivyo kama vitaashiria saratani ya tezi dume basi daktari anaweza kuamuru vipimo vingine ili kuthibitisha uwepo wa ugonjwa huo kama vile transrectal ultrasound au prostate needle biopsy.

MATIBABU YA TEZI DUME

Kuna njia kadhaa za matibabu ya saratani ya tezi dume. Hata hivyo uamuzi wa njia gani itumike unategemea ushauri na maoni ya daktari kulingana na hatua ya ugonjwa ulipofikia na umri wa mgonjwa husika. Katika hatua za awali za ugonjwa, daktari anaweza kushauri mgonjwa atibiwe kwa kufanyiwa upasuaji na tiba ya mionzi.
Hii ni katika hali ambayo kwa wagonjwa wazee, daktari anaweza kushauri mgonjwa kuwa chini ya uangalizi tu bila kufanyiwa upasuaji au bila kupatiwa tiba ya mionzi.

Matumizi ya dawa

Alpha 1-blockersΒ kama vileΒ doxazosin, prazosin, tamsulosin, terazosin, na alfuzosinΒ ni dawa zilizo kwenye kundi la dawa zinazotumika kutibuΒ shinikizo la juu la damu. Dawa hizi hulegeza misuli ya shingo ya kibofu na tezi dume. Hii huruhusu mkojo kutoka kwa urahisi. Watu wengi wanatumia dawa yaΒ Alpha 1-blockers,Β na husaidia sana kupunguza dalili zao.

FinasterideΒ naΒ dutasterideΒ Β ni dawa zinazopunguza kiwango cha homoni zinazotengenezwa na tezi dume,hupunguza ukubwa wa Β tezi dume, huongeza kiwango cha mtiririko wa mkojo, na kupunguza dalili zinazotokana na ukubwa wa tezi dume kuongezeka. Inaweza kuchukua miezi 3 hadi 6 kabla ya kuona mabadiliko makubwa katika dalili zako. KutumiaΒ finasterideΒ naΒ dutasterideΒ kunaweza kuwa na athari kama vile, kupungua kwa nguvu za kiume na hata kuwa hanithi.

Daktari anaweza kuagiza upewe dawa za antibiotikiΒ ili kutibu kuvimba kwa tezi dume (prostatitis), mara nyingiΒ prostatitisΒ huambatana na kuongezeka kwa ukubwa wa tezi dume.

Upasuaji

Upasuaji wa tezi dume unaweza kupendekezwa Β iwapo :

  • Unajikojolea/ unashindwa kuzuia mkojo
  • Unakojoa mkojo wenye damu mara kwa mara
  • Unashindwa kukojoa mkojo wote,(Mkojo unabaki kwenye kibofu hata baada ya kukojoa)
  • Maambukizi ya mara kwa mara kwenye njia ya mkojo
  • Kushindwa kwa figo kufanya kazi
  • Mawe kwenye kibofu

Uchaguzi wa aina maalum ya upasuaji, mara nyingi hutegemea ukali wa dalili ,ukubwa na umbo la tezi dume.

  • Transurethral resection of the prostate (TURP): Hii ni aina ya upasuaji inayopendelewa zaidi kutibu ugonjwa wa tezi dume.Β TURPΒ hufanyika kwa kuingiza kifaa chenye kamera kupitia kwenye uume na kisha kukata na kuondoa tezi dume kipande baada ya kipande.
  • Transurethral incision of the prostate (TUIP): Upasuaji huu unafanana kidogo naΒ TURP, na hufanyika kwa wanaume walio na tezi dume isiyo kubwa sana. Kwa kawaida upasuaji hufanyika na kisha mgonjwa huruhusiwa kwenda nyumbani (hakuna kulazwa). Kama ilivyo kwaΒ TURP, kifaa chenye kamera huungizwa kupitia kwenye uume mpaka kuifikia tezi dume. Kisha, badala ya Β kukatakata na kuiondoa, daktari hufanya mkato mdogo kupanuaΒ urethraΒ ili kuruhusu mkojo kupita.
  • SimpleΒ ProstatectomyΒ : Mgonjwa hupewa dawa ya nusu kaputi na kisha daktari hupasua tumbo (chini ya kitovu) ili kuifikia tezi dume. Sehemu ya ndani ya tezi dume huondolewa . sehemu ya nje huachwa . Huu ni utaratibu unaochukua muda mrefu, mgonjwa huhitajika kulazwa hospitalini kwa siku 5 hadi 10.


Iwapo saratani imesambaa na kuathiri sehemu nyingine za mwili, matibabu yake yanaweza kujumuisha upasuaji wa kuondoa korodani, matumizi ya dawa za kupunguza kiwango cha homoni ya testosterone katika damu au hormonal therapy, au matumizi ya kemikali za kuua seli za saratani (chemotherapy).

Tukumbuke kuwa, saratani ya tezi dume ni ugonjwa wa kawaida kama yalivyo magonjwa mengine na uchunguzi na matibabu ya mapema huweza kuokoa maisha ya waathirika wengi wa ugonjwa huo.

Mambo 10 unayofanya kimakosa wakati wa kujipodoa

Kama kote duniani, wanawake wengi Tanzania wanatumia vipodozi kama nyongeza ya urembo wao ya kiasili. Ila, kuna makosa maalum zinazofanyiwa kwenye kutumia vipodozi Tanzania. Kuwasaidia dada zetu, Yafuatayo ni makosa 10 ya kuweka vipodozi na jinsi ya kuzirekebisha.

1. Nyusi

Kuna tabia ya wanawake kunyoa nyusi zao sana, na wengine kuzitoa kabisa. Alafu, wanaishia kuzichora na rangi nyeusi.
Hii inamfanya mwanamke kuonekana kama kikatuni.
Sasa:

  • Badala ya kunyoa nywele zote, zipunguze kwa kiasi kidogo
  • Usituimie rangi nyeusi kuzijaza. Tumia rangi ya brauni
  • Kwa muonekano wa kiasili zaidi, tumia nyusi, poda ya nyusi au gel badala ya penseli.

2. Tumia faundesheni inayofanana na rangi ya ngozi yako

Ingawa kupata faundesheni inayofanana na ngozi yako ni ngumu, hasa kwa wanawake weusi zaidi, wanawake wengi wanapata shida na kukubali rangi ya kiasili na wanajaribu kutumia vipodozi kubadilisa rangi yao.
Suluhisho:

  1. Kubali rangi yako ya kiasili
  2. Rangi yetu inaweza ikawa mweusi au mweupe zaidi kutegemea na msimu. Kwa hiyo ni bora kuwa na faundesheni inayoendana na mabadiliko hayo

3. Usitumie poda asana

Wanawake wengi wanfikiri kwamba kutumia poda nying ndio kupendeza zaidi. Matokeo yake, wanaishia kufanana na jinni.
Suluhisho:

  1. Tumia poda inayofanana na ngozi yako
  2. Usiweke poda nyingi. Kiasi kidogo kitakutosha

4. Tumia blush kwa usahihi

Kutumia kwa usahihi ni tatizo duniani.
Suluhisho:

  1. Tumia blush kwenye mifupa ya mashavu, sio kwenye mashavu yenyewe.
  2. Kama una ngozi yeneye uweusi zaidi, tumia blush ya rangi ya dhahabu au zambarau.

5. Burashi za vipodozi ni muhimu

Badala ya kutumia vidole vyako, utahitaji burashi zifuatayo:

  1. Burashi ya faundesheni
  2. Burashi ya poda
  3. Burashi ya blush
  4. Burashi ya nyusi
  5. Burahi ya eyeshadow

6. Tumia kope bandia kwa usahihi

Wanawake wengi wanatumia kope bandia zisizo na ubora. Matokeo yake wanafanana na dolli ya mtoto.
Suluhisho:

  1. Badala ya kutumia kope bandia, nunua wanja nzuri inayonyoosha na kunenepesha kope zako
  2. Nunua kope bandia zenye ubora (zilizotengenezwa na nywele za binadamu au yalisanidiwa)
  3. Jifunze jinsi ya kuweka kope bandia kwa usahihi.

7. Jifunze kuweka jicho la paka kwa usahihi

Jicho la paka ni njia moja ya kuongeza umaridadi kwa sura yako na kuvutia zaidi. Ila, wanawake wengi wanakosea kuiweka.
Suluhisho:

  1. Ni bora kutumia liner ya maji au mafuta kuliko kutumia penseli kama huna ujuzi wa kutosha
  2. Jifunze kuchora jicho la paka

8. Matatizo ya nyusi…tena

Wanawake wengi wanatumia konsila kwa nje ya nyusi zao. Tatizo linakuja pale ambapo konsila iliyotumiwa haiendani na ngozi yao. Hii inafanya konsila hiyo kuonekana sana, kwenye picha haswa!
Suluhisho:

  1. Tumia konsila inayoendana na ngozi yako
  2. Hakikisha una changanya konsila kwa kutumia burashi, ili ijichangaye vizure na ngozi/faundesheni yako

9. Eyeshadows

Wanawake wanatumia eyeshadow zinazo ng’aa au za rangi kali. Zaidi ya hapo, hawazichanganyi vizuri.
Suluhisho:

  1. Tumia eyeshadow za rangi ya dhahabu, brauni au zambarau
  2. Jifunze jinzi ya kuweka eye shadow vizuri, zikiwemo
  • Rangi ya highlighter yakuweka chini ya nyusi zako
  • Rangi ya msingi ya kuweka
  • Rangi ya mpito
  • Rangi kuu ya eye shadow

10, Mdomo

Kabla ya kuweka lipstick, hakikisha mdomo yako inaunyevu. Hii ni muhimu sana kwa lipstick yako kuseti vizuri.

Usiweke vipodozi kwa fujo
Kwenye swala la vipodozi, kutumia kidogo ni bora kuliko kutumia nyingi. Unataka urembo wako wa kiasili kuboreshwa, sio kubadalika kabisa.
Kwa kifupi, ukitumia vipodozi lakini unaonekana kama vile hujatumia vipodozi, basi hapo ndio utakuwa umepatia.

Ujumbe wa kuasa kudumu katika upendo na mapenzi

Hii ni mbegu bora inaitwa UPENDO ipande kwa ndg zako,na pale utakapokuta imeota imwagilie maji ya FURAHA,iwekee kivuli cha USHIRIKIANO, ipalilie kwa jembe la KUSAMEHE, iwekee mbolea ya AMANI, ipige dawa ya NENO LA MUNGU, itakayoua wadudu wote waharibifu kama ubinafsi, chuki, wivu, dharau, unafki, kiburi, choyo, tamaa na fitna kwenye mmea huu, MMEA HUU (UPENDO) UENDELEE KUWA MCHE BORA KULIKO YOTE KTK MAISHA YAKO SIKU ZOTE.

Shopping Cart
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About