Karibu AckySHINE
Karibu AckySHINE
Chagua Unachotaka Kusoma Hapa
Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.
Hichi ndicho unatakiwa uwe nacho kulingana na umri wako
20 – 25 =Iwe kama ni kielimu hujafikia malengo yako,sitisha mara moja tafuta kazi/biashara ya kufanya,pigana kufa na kupona ili kama vipi urudi shule kwa pesa yako.
25 – 30 = Hakikisha uwe na angalau na SHUGHULI RASMI kama umeajiliwa au umejiajili.
30 – 35 = Uwe na angalau kama sio nyumba basi kiwanja,tena ujitahidi uwe umeoa/umeolewa kama sio kuishi nae,tena si mbaya ukawa umeshatengeneza familia,kwa maana ya kuwa na watoto kama mungu kakuwezesha.
35 – 40 = Ni umri wa kama kiwanja kiwe kimejengwa, na kama ni tayari basi nenda step nyingine ya kumiliki kama ni Gari au kuongeza nyumba na hakikisha vinaenda sambamba na ongezeko la familia.
40 – 45 = Ni umri wa masahihisho, kama hukuwahi kununua kiwanja au kujenga basi hapa pambana afe kipa afe beki,kama umegundua mkeo hazai fanya mchakato kwingine kama ni mwanaume na kama mwanamke umegundua mumeo ndio mwenye shida basi tafuta nje umletee mtoto. Kifupi ni umri wa masahihisho.Ila kwa wale ambao wameenda vizuri huko nyuma basi hapa kama ni wale watoto wapo kwenye level tofauti za elimu,kwahiyo ni muda wa kuwawekea malengo ya kimasomo watoto wao.
45 -50 = Kwa yule ambaye hakukosea huko nyuma,basi umri huu ni wa kuanza kuwatengenezea mazingira watoto wako,kama ni shuguli zako ni kuanza kuwahusisha,huku wewe ukijiweka pembeni taratibu na kuangalia fulsa za umri wako. Lakini kwa wale waliokosea hapa ni kupitia zile hatua za 35 -40.
50 – 60 = Ni kujiandaa na maisha mapya ya kustaafu au kujiweka mbali na shughuli za shulba.Na kama ulijitenga na msikiti/kanisa huu ndio muda wako.
60 – 70 = kula matunda yako huku ukiangalia misingi ya wanao inaendaje.
70 – 80 = kula matunda.
80 – n.k= unamsikilizia Mungu anasemaje
Mapishi ya Pilau Ya Bilingani Na Kuku
Viambaupishi
Mchele wa basmati – 3 vikombe
Kuku – ½
Bilingani – 2 ya kiasi
Viazi – 4
Vitunguu – 2
Kitunguu (thomu/galic) iliyosagwa – 2 vijiko vya supu
Pilipili mbichi iliyosagwa – 2
Chumvi – kiasi
Garama masala (mchanganyiko wa bizari) – 1 kijiko cha chai
Hiliki ya unga – ¼ kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia wali – ¼ kikombe
Mafuta ya kukaangia viazi na bilingani – kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele.
Kata kuku vipande upendavyo safisha
Kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu, na bizari mchanganyiko (garama masala).
Akiwiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria.
Menya na kata viazi kaanga weka kando.
Kata kata bilingani slesi nene kaanga, chuja mafuta weka kando.
Katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangu ya hudhurungi. Tia vipande vya kuku, ukaange kidogo.
Tia supu ya kuku, mchele, tia hiliki, ufunike hadi karibu na kuwiva kabisa.
Tia viazi na bilingani uchanganye kidogo, kisha tia katika oven imalizike kupikika pilau humo au unaweza kuendelea kufunika juu ya jiko hadi pilau iwive.
Pakua katika sahani ikiwa tayari kuliwa kwa saladi ya mtindi.
Kali ya mwaka iliyotokea Benki Baada ya wezi kuiba
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuni…unaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuni…😂😂😂😂
Faida za kula Karoti kiafya
Asilimia kubwa tunapenda kutumia karoti katika kuunga katika mboga ya nyama na si kuila karoti kama karoti. wataalamu wanashauri ili uwe na afya bora unatakiwa ule karoti sita kwa wiki au moja kwa siku. Unaweza kula karoti ya kuchemshaa,juisi au mbichi.
Zifuatazo ndizo faida za kutumia karoti;
·Karoti ina element ijulikanayo kama beta-carotene ambayo husaidia kupambana na kansa.
·Pia ni chanzo kizuri cha vitamin na husaidia kuongeza kinga ya mwili,
·Karoti ina vitamin A ambayo ina patikana kwa wingi husaidia kuongeza uwezo wa kuona na mawasiliano ya seli.
· Pia ina madini kama sodiam,sulphur,chlorine na iodine.
·Juisi ya caroti husaidia sana katika kutibu ngozi iliyo kauka na ulaji wa mara kwa mara hupunguza uwezo wa kupata vidonda vya tumbo pamoja na madhara mengine kwenye mfumo wa chakula.
Mapishi ya Chicken Curry
Leo wapendwa nitaenda kuzungumzia mapishi ya mchuzi wa kuku (chicken curry).
Mahitaji
Kuku mzima
Nyanya kubwa 3
Karoti mbili
Pilipili hoho
Kotmiri
Tangawizi
Kitunguu maji
Kitunguu saumu kidogo
Ndimu
Mafuta ya kupikia
Chumvi (pilipili ukipenda)
Matayarisho
1. Menya vitunguu saumu na tangawizi na uvitwange pamoja.
2. Katakata kuku vipande vidogo kisha ukamulie ndimu na kupaka mchanganyiko wa tangawizi na vitunguu saumu (kiasi tu).
3. Katakata vitunguu maji na pilipili hoho uweke pembeni.
4. Grind (Kwangua) kwenye grater nyanya na karoti pia uweke pembeni.
5.Katakata kotmiri vipande vidogo uweke pembeni.
6. Andaa kikaango na jiko.
Mapishi
1. Bandika kikaango jikoni na mafuta kiasi, yakishachemka weka vitunguu maji na kaanga hadi vimelainika na kuiva (hakikisha haviungui).
2. Weka pilipili hoho na karoti na endelea kukoroga hadi vyote viive na kulainika, Kisha weka chumvi.
3. Sasa weka vipande vya nyama koroga na funikia kwa dakika 3, kisha weka nyanya zako ulizo grind na koroga ili zichanganyike vizuri, vikishachanganyika weka kotmiri na pilipili kama utapenda. Acha vichemke kwa dakika 5. Hakikisha moto sio mkali sana.
4. Angalia kama nyama zimeiva vizuri kisha epua mchuzi wako.
5. Pakua kwenye bakuli na katakata kotmiri uweke kwa juu.
Unaweza kula kwa ugali, wali, ndizi rost au chipsi.
Hii sasa kali kweli kweli!!
MCHUNGAJI alitangaza kila mwanaume aliye na mke atoe sadaka kulingana na uzuri wa mke wake…bac watu wakaanza kutoa 50,000/= 30,000/= na 20,000/=.
Kuna jamaa akatoa 500/=.
MCHUNGAJI akamuita ofisin akamuuliza.
MCHUNGAJI:Ina maana mkeo siyo mzuri?. Jamaa akajibu: Ukimuona utanirudishia na chenji.
😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆
Mambo ya Kuzingatia ili uwe na ngozi laini
Takribani kila mtu angependa kuwa na ngozi laini, au hata laini zaidi. Watu wengi wamekuwa wakiitafuta ngozi nzuri au kujitahidi kuitunza ili isiharibike. Lakini je, wamefanikiwa?
Wachache hufanikiwa na wengi hushindwa. Na hata hao waliofanikiwa wengi wao hutumia vipodozi vikali ambavyo vingi huchubua na kuharibu ngozi zao na kuwaletea madhara makubwa sana baadae.
Vipi wewe, ungependa kuwa na ngozi nzuri bila kuidhuru afya yako? Karibu somo la leo ili uweze kuwa na ngozi nzuri bila kuidhuru afya yako.
Ngozi laini ni nzuri na inaongeza mvuto wa mwili. Ulaini wa ngozi hupotezwa na mambo mbalimbali kama vile seli za ngozi kupungukiwa na maji na kuanza kusinyaa na kunyauka, seli za ngozi kujeruhiwa, na seli za ngozi kufa. Matokeo yake ni michirizi, makunyanzi, makovu, chunusi, madoa, ngozi kufubaa na kuzeeka.
Kuifanya ngozi kuwa laini unahitaji kuupatia mwili virutubisho vyote vya kujenga mwili vizuri na kunywa maji ya kutosha ili seli zisikauke, kusinyaa wala kunyauka. Kula mlo kamili, matunda mengi na kunywa maji ya kutosha.
Pia unahitaji kuepuka jua kali ambalo litaunguza ngozi, kuikausha na kuifanya iwe na makunyanzi na vitu vingine vinavyoota kwenye ngozi kutokana na jua.
Tumia vipodozi vizuri vinavyosaidia ngozi kuwa laini bila kuidhuru. Hapa kuna vipodozi vya aina mbali mbali na vinavyofanya kazi kwa njia mbali mbali. Vipodozi vya muhimu ni
- Vipodozi vya kuongeza unyevu au maji kwenye (seli za) ngozi
- Kwa kiingereza vinaitwa “Moisturizers”. Hivi hufanya kazi ya kufunika ngozi na kuzuia maji yasipotee kutoka kwenye ngozi, na pia husaidia kuongea maji kuingia kwenye seli za ngozi. Vipo katika mtindo wa sabuni, mafuta na losheni.
- Vipodozi vya kusaidia kuongeza kasi ya kuzalishwa kwa seli mpya za ngozi
- Hivi husaidia kuzalisha seli mpya za ngozi ambazo zitaleta ngozi mpya na nzuri na kuondoa ile ya zamani iliyochoka na kuzeeka. Mifano ni losheni na krimu zenye Vitamini A na Vitamini E.
- Vipodozi vya kusaidia kuondoa uchafu na seli (ngozi) zilizozeeka au kufa
Tumia sabuni zenye uwezo mkubwa wa kuondoa uchafu kutoka kwenye ngozi, na ukiweza tumia “face wash” au “facial cleansers”. Hivi husaidia kusafisha kabisa ngozi na kuondoa uchafu.
Kwa upande wa seli zilizokufa na kubaki juu ya ngozi tumia “scrub”. Scrub hufanya kazi kwa kuondoa seli zilizoharibika na zilizokufa na kuacha seli changa na ngozi nzuri.
USHAURI:
- Pata ushauri wa kulainisha na kupendezesha ngozi yako kutoka kwa wataalam wanaojua vizuri afya, urembo na vipodozi. Utashauriwa vizuri jinsi ya kufanya, vipodozi vya kutumia na jinsi ya kuvitumia vizuri kwa matokeo mazuri zaidi. Epuka wauza vipodozi wasio waaminifu au wasiovijua vizuri vipodozi, maana wanaweza kukupa vipodozi vya tofauti na mahitaji yako au vipodozi vinavyodhuru afya yako.
- Safisha ngozi yako vizuri, kila siku. Hakikisha unaondoa uchafu na vijidudu vyote vinavyotua na kukaa juu ya ngozi yako. Ondoa vumbi, seli zilizokufa, mafuta ya ziada, jasho nk Lala na pumzisha ngozi yako kiasi cha kutosha ili iweze kujitengeneza na kuwa nzuri. Ipumzishe kila siku kwa matokeo mazuri zaidi. Pata usingizi wa kutosha na ulio bora
- Tumia vipodozi vizuri vyenye uwezo wa kukupa matokeo mazuri unayoyataka na visivyodhuru afya yako. Pata ushauri mzuri kutoka kwa wataalam ili uweze kufanikisha hili vizuri. Tumia vipodozi vinavyoendana na ngozi yako. Kama ngozi yako ni kavu tumia vipodozi ambavyo ni maalum kwa ajili ya ngozi kavu, na kama ngozi yako ni ya mafuta basi tumia vipodozi ambavyo ni mahususi kwa ajili ya ngozi ya mafuta.
- Usitumie vipodozi vinavyoharibu ngozi na kuihatarisha ngozi yako. Epuka vipodozi vyote visivyo salama na vile visivyoendana na ngozi yako.
- Jihadhari na michubuko au majeraha mengine yoyote yatakayoweza kuharibu ngozi yako. Hii ni kwa sababu michubuko na majeraha hayo yatakuharibia uzuri wa ngozi yako na pia yatakuachia makovu baada ya kupona
- Kuwa na furaha, amani na tabasamu itakusaidia pia kuwa na ngozi nzuri, hususan ngozi ya usoni.
Madhara ya kunywa soda
Tafiti zinasema kwamba mtu mmoja anayekunywa soda moja kwa siku, anakunywa zaidi ya galoni au dumu 56 za soda kwa
mwaka.
Japokua kuna watu wamekiri kunywa hata zaidi ya soda moja kwa siku ambayo huenda wanakunywa zaidi ya hicho kipimo.
Biashara ya soda inalipa sana duniani kwani ni kinywaji cha pili
kinachoongoza kunywewa duniani baada ya maji.
Sasa ukiangalia mahusiano ya unywaji mdogo wa soda kila siku kiafya una madhara makubwa kuliko unywaji mdogo wa pombe kila
siku.
Yaani ni bora unywe chupa moja ya bia kila siku kuliko chupa moja ya soda kila siku.
Yafuatayo ni madhara ya soda ambayo yatakufanya ufikirie mara mbili kunywa soda tena.
1.Ugonjwa wa kisukari;
Kunywa soda moja ni sawa na kunywa vijiko 10 vya sukari, baada ya kunywa sukari hupanda sana mwilini na kongosho hutoa homoni ya insulini nyingi ili kushusha sukari.
Muda unavyozidi kwenda insulini huendelea kuishiwa nguvu[insulin resisitance] na hali hii husababisha kisukari.
2. Unene na kitambi;
Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Havard umegundua kwamba watu wanaokunywa soda hunenepa mara mbili zaidi ya wale ambao hawanywi hivyo kama uko busy unapunguza uzito na pia mnywaji wa soda basi unapoteza muda.
3. Upungufu wa madini muhimu mwilini;
Soda ina kemikali inayoitwa phosporic acid ambayo huzuia mwili kuchukua madini ya calcium kwenye chakula ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya mifupa na misuli yenye afya kweye mwili wa binadamu.
4. Ugonjwa wa kansa;
Soda ina kemikali inayoitwa caffeine ambayo imehusishwa na cancer mbalimbali za mwili mfano kansa ya kongosho, kansa ya utumbo na magonjwa mengine kama presha ya damu na kansa ya matiti.
5. Huongeza sumu mwilini;
Soda haina lishe wala faida yeyote ile kwenye mwili wa binadamu hivyo huongeza kiasi kikubwa cha sumu mwilini ambacho ni hatari sana kwa afya mtumiaji.
Sumu hizo huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa presha, na kuua figo.
6. Hubadilisha rangi ya meno;
Kila mtu anataka kuwa na meno masafi na meupe lakini baadhi ya soda zina kiasi kikubwa cha tindikali ambacho hushambulia na kuharibu meno kwa muda mfupi hivyo kama unasumbuliwa na meno basi huu ni muda mzuri wa kuachana nayo.
7. Addiction;
Soda nyingi zina tabia ya kumfanya mtu apate ulevi wa soda husika yaani kuna watu unakuta anapenda sana soda fulani na asipoinywa kwa siku atahisi kama amepungukiwa kabisa na kitu fulani mwilini.
Hii itakufanya uwe mtumwa wa mwili wako mwenyewe.
8. Huongeza kasi ya uzee;
Sumu ambazo unazipokea kwenye soda zinazeesha mtu mapema sana yani kijana mdogo wa miaka 20 hujikuta anaonekana kama miaka 35.
9. Hupunguza sana maji mwilini ;
Soda ina kiwango kikubwa cha madini ya sodium ambayo humfanya mtu abaki na maji kidogo na kwa muda mrefu atapata matatizo mengine ya kiafya kama mawe ya kwenye figo[kidney stone] na mawe kwenye nyongo ya binadamu.
10.Mwisho;
Ni vizuri kubadili mfumo wako wa maisha na kuanza kunywa vitu ambavyo haviharibu mwili yaani badala ya kunywa soda basi tumia juice (unayoitengeneza mwenyewe) ambayo ni mbadala mkubwa wa soda, lakini pia unaweza kunywa maziwa na kadhalika.
Ujumbe wa salamu kwa mpenzi kumjulia hali
Furaha ni kawaida yangu, kununa si busara kwangu, kuishi nawewe vizuri ni sehemu ya Maisha yangu, kukusalimia ni hulka ya Moyo wangu, Uhali gani mpenzi?
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Sababu za magonjwa ya figo na jinsi ya kuondokana na janga la magonjwa ya Figo
1.Usichelewe kwenda HAJA. Kutunza mkojo kweye kibofu chako kwa muda mrefu ni wazo baya. Kibofu kikijaa kinaweza kusababisha uharibifu. Mkojo ambao unakaa kwenye kibofu huzidisha bakteria haraka.
Mara mkojo unaporudi nyuma ya njia na Figo, sumu dutu husababisha maambukizi ya figo, pia njia ya mkojo na “nephritis”, pamoja na “uremia”. Wakati wito asili (unahisi mkojo) fanya hivyo haraka iwezekanavyo.
2. Kula Chumvi kupita kiasi.
Inatupasa kula Chumvi isiyozidi 5.8 gramu kwa siku.
3. Kula nyama kupita kiasi.
Protini ikizidi sana katika mlo wako inadhuru figo zako. Mmeng’enyo wa Protini unazalisha amonia- sumu dutu ambayo ina uharibifu mkubwa kwa figo zako. Nyama nyingi inaleta uharibifu zaidi wa figo.
4. Unywaji mwingi wa “Caffeins”.
Caffein hutokana na vinywaji vya Soda na vinywaji vingine laini kama Kahawa, Redblue n.k. Hupandisha shinikizo la damu na figo zako kuanza mateso. Unapaswa kupunguza kiwango cha Coke, Pepsi, Red Bull, nk ambavyo hunywa kila siku.
5. Kutokunywa maji.
Figo zetu lazima zichakatwe vizuri kutekeleza majukumu yake vizuri. Endapo hatunywi ya kutosha, sumu dutu inaweza kuanza kukusanyika katika damu, kama hakuna kimiminika cha kutosha kutoa kwa njia ya figo. * Kunywa zaidi ya bilauri 10 za maji kila siku.
Kuna njia rahisi ya kuangalia kama unakunywa maji ya kutosha: Angalia rangi ya mkojo wako; Wepesi wa rangi, ndiyo vzuri.
6. Kuchelewa matibabu.
Tibu matatizo yako yote ya kiafya kwa uhakika na uwe unachunguza afya yako mara kwa mara. Wapendwa na wapenzi wangu, hebu tujisaidie wenyewe… Shirikisha wengine, kama unajali. —-
Pia epuka vidonge hivi, ni hatari sana:
D- baridi*
Vicks Action- 500*
Actified*
Coldarin*
Cosome*
Nice*
Nimulid*
Cetrizet- D
Hivi vidonge vina Phenyl propanol- amide PPA ambayo husababisha stroke na ni marufuku Marekani.
MWISHO… Tafadhali, kabla ya kufuta, msaidie rafiki yako kwa kumpitishia hii..!
Inaweza kumsaidia mtu!**
Wasambazie wengi kwa kadiri uwezavyo.
Shirikisha ujumbe huu kwa mpendwa wako.
Maonyo muhimu ya Afya
1. Jibu (pokea) simu wito na sikio la kushoto.
2. Usinywe dawa zako kwa maji baridi….
3. Usile milo mizito baada ya saa 11 jioni.
4. Kunywa maji vuguvugu mengi asubuhi na kiasi usiku. Usinywe maji baridi kamwe.
5. Muda bora wa kulala ni kutoka saa 4 usiku hadi saa 10 Alfajiri.
6. Usilale mapema baada ya kumeza dawa au baada ya mlo. Usiku, Kula chakula laini.
7. Usipokee simu yako ikiwa haina chaji. Wakati huo mionzi huwa ina nguvu mara 1000 .
Je, unaweza kuwasambazia watu unao wajali?
Mimi nimeshafanya kwako….!!.
Mzee wa kichaga na hela zake. Angalia anachofanya
Mzee moja alikuwa kila usiku anapita mbele ya bank anasimama,kisha anapiga honi,akitoka askari mlinzi,anaondoka.Hilo jambo likamkera sana askari mlinzi, askari akawa na mvizia yule mzee wa kichaga ,siku alipokuja tena akamkamata, akamuuliza kwa nini unakuja unapiga honi kisha unakimbia? Mzee akasema: Haki ya mungu babaangu , Nina pesa zangu ktk account hapa bank naogopa usilale usingizi ndo maana kila siku usiku napita kukuangalia kama umelala!!
😂😂😂😂😂😂
Jinsi ya kutengeneza biskuti za Matunda Makavu Na Cornflakes
VIAMBAUPISHI
Unga – 4 Vikombe
Sukari – 1 Kikombe
Baking powder 1 kijiko cha chai mfuto
Siagi – 454 gms
Mayai – 2
Matunda makavu (tende, zabibu, lozi) – 1 Kikombe
Vanilla – 2 Vijiko vya chai
Cornflakes – ½ kikombe
JINSI YA KUANDAA
Changanya sukari na siagi katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy)
Tia yai moja moja huku unachanganya mpaka iwe laini kama sufi. (fluffy)
Tia unga, baking powder, matunda makavu, changanya na mwiko.
Chota mchanganyiko wa biskuti kwa mkono kama (kiasi cha kijiko kimoja cha supu) fanya duara na uchovye katika cornflakes iliyopondwa kwa mkono (crushed)
Zipange katika treya ya kupikia na zipike (bake) katika moto wa 375°F kwa muda wa kiasi dakika 15 huku unazitazama tazama.
Magonjwa hatari 10 yanayotibika kwa kutumia mbegu za Maboga
Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya mhimu zaidi mwilini kama madini ya zinki, kopa, maginizia, manganizi na chuma, mbegu za maboga ni tamu na zinaweza kutafunwa nyakati zozote na mahali popote hasa kwa wapenda kutafuna-tafuna kama mimi. Tafiti mbalimbali zimethibitisha pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida nyingi kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10 yafuatayo:
1. UGONJWA WA MOYO:
Kiasi kingi cha madini ya magnesium katika mbegu za maboga yanazifanya mbegu hizi kuwa mhimu sana kwa watu wenye magonjwa mbalimabli ya moyo. Madini ya magnesium ni mhimu kwa ajili ya kuimarisha msukumo wa damu kwenye moyo na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hatimaye kutibu na kuzuia magonjwa ya moyo. Mbegu hizi pia zina mafuta mengine mhimu zaidi kwa watu wenye ugonjwa wa moyo yenye OMEGA 3.
2. HUIMARISHA KINGA YA MWILI:
Mbegu za maboga zimebarikiwa kuwa na kiasi cha kutosha cha madini ya zinki (zinc). Kazi kubwa ya madini ya zink ni kuimarisha kinga ya mwili. Upungufu wa madini ya zink unaweza kupelekea matatizo kadhaa mwilini ikiwemo kuzaa watoto njiti, kuishiwa nguvu za kiume, matatizo ya homoni, chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo shuleni kimasomo na matatizo mengine kadhaa ya kimwili na kiakili.
3. HUONGEZA UWEZO WA MACHO KUONA
Mbegu za maboga zina Vitamini E, vitamini A, lutein, beta-carotene na zeaxanthin, vitu hivi vinavyopatikana katika mbegu za maboga ni mhimu kwa ajili ya nuru ya macho. Vitamini A na madini ya zinki ni mhimu kwa ajili ya uzalishaji wa ‘melanin’ kimeng’enya mhimu ambacho hutengenezwa kwa asili na miili yetu kwa ajili ya ulinzi wa afya ya macho.
4. KINGA YA KISUKARI
Kisukari ni moja ya ugonjwa unaoendelea kwa kasi kuwasumbua watu wengi kila pembe ya dunia. Mbegu za maboga zina vitu vitatu mhimu zaidi ambavyo ni ‘Nicotinic acid’, ‘Trigonelline’ na ‘D-chiro-inositol’ ambavyo husaidia kushusha damu sukari mwilini na kudhibiti kazi za insulini hivyo kuwa kinga na kuleta ahueni kubwa kwa watu wenye kisukari.
Kama unasumbuliwa na kisukari fanya mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na unipe mrejesho hapa.
5. DAWA BORA YA USINGIZI
Mbegu hizi zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha homoni za usingizi. Kwenye mbegu za maboga kuna vimeng’enya viwili mhimu zaidi ambavyo huhusika na usingizi na afya ya akili moja kwa moja navyo ni ‘L-tryptophan’ na ‘tryptophan’. Gramu 100 tu za mbegu za maboga zina kiasi cha kutosha cha ‘tryptophan’ mpaka mg 576. Tryptophan ndiyo inahusika kuleta usingizi wenye utulivu pia huondoa msongo wa mawazo au stress mwilini. Kwa kuongezea mbegu za maboga zina kiasi kingi cha vitamini za kundi B. Muda mchache kabla ya kwenda kulala tafuna mbegu za maboga na utapata usingizi mtulivu kabisa mpaka asubuhi.
Kwahiyo kama una tatizo la kukosa usingizi jaribu kutumia mbegu za maboga na uniletee majibu hapa. Kumbuka kukosa usingizi mara nyingi huwa ni matokeo ya msongo wa mawazo na kama ulivyoona mbegu hizi zinaondoa pia stress! Kazi ni kwako ndugu.
6. DAWA BORA YA UVIMBE
Mbegu za maboga zinao uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini sambamba na uvimbe (inflammation). Kama ujuavyo sehemu kubwa ya vivimbe mwilini ni matokeo ya sumu kadhaa mwilini. Mbegu za maboga zitakuondolea uvimbe mwilini bila kukuachia madhara yoyote mabaya hapo baadaye. Kama unasumbuliwa na uvimbe popote jaribu kutumia mbegu za maboga na utuletee majibu. Mbegu za maboga pia ni dawa nzuri kwa aina nyingi za kansa mwilini.
7. HUONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAYENYONYESHA
Mbegu za maboga zina protini nyingi bora itokanayo na mimea isiyo na madhara kama ile ya kwenye wanyama. Pia zina OMEGA 3. Mama mjamzito hata unayenyonyesha tumia mbegu za maboga na utakuwa na uhakika wa kutoa maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto.
8. DAWA NZURI KWA MATATIZO YA TEZI DUME
Wataalamu wengi wa lishe wanapendekeza mbegu za maboga zitumike kwa wanaume wa rika zote yaani vijana hadi wazee kwani zimethibitika kuwa msaada mkubwa kwa afya ya tezi dume. Tafiti nyingi zinasema mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya Zinki madini ambayo ni mhimu SANA kwa afya ya tezi dume na husaidia uponyaji wa tatizo la tezi dume moja kuwa kubwa kuliko nyingine tatizo lijukanalo kwa kitaalamu kama ‘benign prostatic hyperplasia’. Wanaume kazi ni kwenu.
9. ZINAONGEZA NGUVU ZA KIUME
Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo ulikuwa huyajuwi bado.
Utaniuliza kivipi zinaondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume? Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo/stress kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), zinashusha kisukari, zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya zaidi ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili. Bado huelewi? Zina madini ya chuma pia
Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina uchungu wowote, ni tamu kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ukiwa ofisini unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi zako. Sambamba na hilo kama tulivyoona pale juu kwamba zinaongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha kwa upande wa wanaume zinaongeza pia uwingi wa mbegu za kiume (sperm count) ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utaona ukimwaga bao linatoka la kutosha na zito kweli kweli basi ujuwe ni mbegu za maboga hizo.
10. ZINAONDOA PIA MSONGO WA MAWAZO (STRESS)
Msongo wa mawazo au stress kama mlivyozoea wengi ni tatizo linaloendelea kuwasumbua watu wengi miaka ya sasa. Mbaya zaidi wengi huwa hawaelewi nini madhara ya hizo stress wanazojipa. Yaani stress au msongo wa mawazo unaweza kukuletea magonjwa mengine mwilini zaidi ya 50, hivyo utaona ni jinsi gani ilivyo mhimu kwako kuweka chini stress zako na uendelee na maisha kwani kuendelea kuwa na stress ni hatari zaidi kwa afya yako.
Moja ya sababu kuu ya watu wengi kuwa na stress ni usawa usio sawa wa homoni zao (hormonal imbalance). Hivyo kama una tatizo la homoni kwenye mwili hebu weka mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na hutakawia kuona tofauti. Mbegu za maboga zina kimeng’enya mhimu sana kwa kutuliza mawazo kiitwacho ‘tryptophan’ na asidi amino zingine mhimu zinazohusika kutengenezwa kwa homoni nyingine ijulikanayo kama ‘serotonin’. Kama ulikuwa hujuwi ni kuwa serotonin ni homoni inayohusika na kazi mhimu sana ya kurekebisha matendo ya kitabia na kutoa matokeo chanya kwa mambo yanayohusu usingizi, hali ya mawazo kwa ujumla na mambo yanayohusu njaa.
Mbegu za maboga ni msaada mkubwa kwa kina mama waliofikia ukomo wa siku zao na huondoa matatizo ya kiafya yatokanayo na kukoma kwa hedhi. Ni msaada kwa watu wenye saratani mbalimbali, huimarisha ukuaji na ustawi wa mifupa na meno, huondoa harufu mbaya ya kinywa na husaidia pia wenye tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara.
NAMNA NZURI YA KULA MBEGU ZA MABOGA:
Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo kama dakika 15 hivi na huwa nazichanganya na maji ya chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha.
Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga kwa siku ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi kwa siku.
Njia za kutibu shinikizo la chini la damu au presha ya kushuka
👉Kutibu shinikizo la chini la damu kwa kutumia maji chumvi
Kunywa Maji yenye chumvi husaidia kutibu shinikizo la chini la damu sababu sodiamu iliyomo kwenye chumvi hupandisha juu shinikizo la damu. Usizidishe dawa hii kwa sababu chumvi nyingi kuzidi ina madhara kiafya.
Matumizi:
Changanya nusu kijiko cha chai cha chumvi ndani ya maji glasi moja (robo lita) na unywe mchanganyiko huu mara 1 au 2 kwa siku
👉Matumizi ya kahawa kutibu presha ya kushuka au shinikizo la chini la damu
Kahawa husaidia kuongeza presha au shinikizo la damu. Unashauriwa Kunywa kikombe kimoja cha kahawa kunaweza pia kusaidia kupandisha shinikizo lako la damu kwa muda.
Kama unapatwa na kushuka kwa shinikizo la damu mara kwa mara basi kunywa kikombe cha kahawa asubuhi au unywe wakati unakula cha mchana na cha jioni.
Usizidishe matumizi ya kahawa kwakuwa kahawa ina madhara mabaya kwa afya ya mwili kwa ujumla.
👉Matumizi ya zabibu kavu kutibu shinikizo la chini la damu
Zabibu huweza kutumika kama tiba ya shinikizo la chini la damu kama ifuatavyo
1. Chukua zabibu kavu Loweka zabibu 30 mpaka 40 ndani ya kikombe cha maji kwa usiku mzima.
2. Asubuhi kabla ya kula wala kunywa chochote kula zabibu moja baada ya nyingine na unywe pia maji yake
3. Rudia zoezi hili kila siku kwa majuma kadhaa hata mwezi.
👉Matumizi ya Tangawizi kutibu shinikizo la chini la damu
Hatua za kufuata
- Chukua Kijiko kikubwa kikubwa cha tangawizi mbichi iliyoparuzwa
- Changanya na Kikombe kimoja cha maji ya moto
- Chemsha katika moto kwa dakika 12 hivi
- Kisha ipua na uchuje
- Ikipoa kidogo kunywa yote,
- fanya hivi mara 2 kwa siku kila siku
👉Matumizi ya Mrehani (basil) kutibu presha ya kushuka
Hii ni dawa nzuri ya kutibu shinikizo la chini la damu sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C, magnesiamu na potasiamu, vilevile dawa hii husaidia kuweka sawa akili na kuondoa msongo wa mawazo (stress).
Matumizi
- Chukua majani 10 mpaka 15 ya mrehani mbichi
- Saga au twanga kupata maji maji yake (juisi).
- Weka asali kijiko kidogo kimoja ndani yake.
- Kunywa mchanganyiko huu kila siku asubuhi ukiamka tu tumbo likiwa tupu.
Vile vile unaweza kutafuna tu moja kwa moja majani kadhaa ya mrehani kila siku asubuhi.
👉Matumizi ya karoti na asali kutibu presha ya kushuka
Hatua za kufuata
1. Tengeneza glasi moja ya juisi ya karoti
2. Weka vijiko vikubwa viwili vya asali ndani yake na kisha changanya vizuri
3. Kunywa yote asubuhi tumbo likiwa tupu na jioni glasi nyingine kwa majuma kadhaa
👉Matumizi ya maji kutibu shinikizo la chini la damu
Matumizi ya maji ya kunywa ni moja ya dawa rahisi kabisa ya shinikizo la chini la damu.
Hii ni kwa sababu Maji ni mhimu kwa kila ogani ndani ya mwili iweze kufanya kazi zake sawa.
Kwa hiyo sababu kuu ya mtu kuwa na shinikizo la chini au hata la juu ni matokeo ya mishipa ya damu kutokuwa na vimiminika vya kutosha.
Mishipa ya damu imeundwa kwa maji maji ya damu (serum) na seli za damu.
Maji yanapopungua kwenye mwili hata vipenyo vya mishipa yako navyo hupungua ukubwa wake jambo linaloleta kushuka kwa shinikizo la damu.
Matatizo yote haya ni matokeo ya kutokunywa maji ya kutosha kila siku.
Kwa sababu hii, ili kupandisha juu shinikizo la damu unahitaji kunywa zaidi maji sambamba na juisi nyingine za matunda au za mboga mboga kila siku.
Hii inasaidia kuongeza vimiminika katika mishipa ya damu.
👉Matumizi ya juisi ya limao kutibu shinikizo la chini la damu
Juisi hii ni nzuri sana katika kutibu shinikizo la juu la damu.
Lakini inaweza pia kutumika kutibu shinikizo la chini la damu hasa ikiwa hili shinikizo la chini la damu limesababishwa na upungufu wa maji mwilini (dehydration).
Kutibu shinikizo la chini la damu unaweza kuchanganya juisi ya limau na chumvi kidogo na sukari au unaweza kutumia maji maji ya miwa.
👉Ulaji mzuri hupunguza uwezekano wa kupata shinikizo la chini la damu
Ni mhimu kula mlo kamili kila siku. Kula lishe duni kunaweza kupelekea kuzalishwa kwa damu isiyo na afya inayoleta shinikizo la damu.
Kula zaidi vyakula vyenye protini, vyenye vitamini B na C kwa wingi. Kula milo midogo midogo hata mitano kuliko kula miwili au mitatu lakini ya nguvu sana.
Unaweza kutumia kitunguu swaumu hasa kibichi ukitafuna punje 2 kila unapoenda kulala kadharika glasi moja ya juisi ya ubuyu kutwa mara 1.
Acha vilevi vyovyote mara tu unapogundulika na shinikizo la chini la damu. Epuka pia vyakula vyenye wanga sana kama tambi, mikate, viazi, wali nk
Upungufu wa baadhi ya vitamini hasa vitamini za kundi B na madini kunaweza pia kuleta shinikizo la chini la damu. Hivyo ili kudhibiti shinikizo la chini la damu unahitaji kula mlo sahihi kila siku.
👉Matumizi ya Lozi na maziwa kutibu shinikizo la chini la damu
Unaweza kutumia Lozi na maziwa kutibu shinikizo la chini la damu kama ifuatavyo;
- Loweka lozi 5 mpaka 6 kwenye kikombe cha maji kwa usiku mmoja
- Asubuhi menya hizo lozi na uzisage
- Chukua hizo lozi ulizosaga na uweke ndani ya kikombe cha maziwa
- Chemsha mchanganyiko huu kwa dakika kadhaa
- Kunywa kinywaji hiki kila siku asubuhi
Sifa mbaya: Cheki kilichompata huyu mwanaume mpenda sifa
SIFA MBAYA…
Jamaa alikuwa ndani ya daladala Mara simu ikaita alikuwa ni mkewe kwa sifa jamaa akaweka loud speaker ili watu wasikie wanavyopendana.
JAMAA;wife Mara hii umenimiss jaman
WIFE; kwa nini umekunywa uji wa mtoto?!!!
😂😂😂😂😂
Njia 3 rahisi za kuondoa kitambi
JE, una KITAMBI na unataka kukiondoa?
FANYA HAYA;
1. Kopa mkopo mkubwa benki
2. Nunua gari bovu la biashara
3.Oana na mke mwenye kelele.
Ukiona miezi mitatu hakijaisha basi ujue umevimba BANDAMA sio kitambi..
Meseji ya kumtumia mpenzi wako kumwambia kuwa yeye ndiye chaguo lako
Nafsi yangu inafurahia ya kwamba
wewe ndio chaguo langu, ubavu wangu
tabasamu usoni mwangu ndio siri ya
pendo lako kwangu
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Jinsi ya kutengeneza Nangatai
MAHITAJI
Unga wa ngano – 2 – 2 ¼ Vikombe
Siagi – 1 ½ Kikombe
Sukari – 1 Kikombe
Yai – 1
Vanilla -Tone moja
Baking Powder -kijiko 1 cha chai
Chumvi – Kiasi kidogo (pinch)
Unga wa Kastadi – 2 Vijiko vya supu
MATAYARISHO
Changanya vitu vyote isipokuwa unga.
Tia unga kidogo kidogo mpaka mchanganyiko uwe sawa.
Kisha fanya duara ndogo ndogo uzipange kwenye treya na utie rangi katikati.
Halafu zichome katika moto wa 300°F kwa muda wa dakika 20 – 25 na zisiwe browni .
Kisha panga kwenye sahani tayari kuliwa na chai.
Ushauri wangu kwa leo
Kuna watu wengi sana huwa wanani-challenge ninaposema kwamba ni muhimu sana mtu kuishi katika kusudi la maisha yake. Na moja kati ya hoja zao ni kwamba haya maisha ya sasa mtu akisema aanze kutafuta kusudi la maisha yake atakufa maskini. Hivyo wanaonelea ni bora kufanya chochote kitakachotokea mbele yake ilimradi mwisho wa siku anapata pesa. Yaani anachagua kuwa mtumwa wa Pesa
Kusudi la maisha ya mtu huwa halina ukomo na halibadiliki, kinachobadilika au kufikia ukomo ni malengo ya kuli-ishi kusudi hilo. Kwa hiyo unapopanga malengo yako au unapokuwa na ndoto zako ni lazima uweze kupambanua mwisho wa siku hizo ndoto au hayo malengo yanakwenda kukidhi kiu ya aina gani inayofukuta ndani yako.
Ukifanikiwa kulitambua kusudi la maisha yako na ukafanikiwa kuli-ishi kwa vitendo, ni dhahiri utakuwa maarufu kwenye mazingira yanayohusiana na maisha yako. Mazingira yanayohusiana na maisha yako yapo ndani ya kusudi la maisha yako.
Ni wakati gani mtu anaweza kusema amefanikiwa katika maisha yake? Ni pale ambapo tu mtu anapoweza kutatua tatizo fulani katika jamii; Kugundua uhitaji wa kutimizwa au kukamilishwa kwa jambo fulani katika jamii. Ukiweza kuziba pengo fulani. Ukiweza kupata ufumbuzi wa kukamilishwa kwa hilo jambo kwa faida ya jamii fulani au niseme ukiweza kutatua tatizo hilo hapo unaweza kusema umefanikiwa. Huwezi kutatua tatizo lolote katika jamii kama hujawekeza ndani yako.
Haijalishi ni jambo gani unafanya katika jamii na liko kwenye kiwango kipi ilimradi liko ndani ya mstari wa maisha yako. Kwa mfano, una kamtaji kadogo na unaamua kuanzisha genge la kuuza mahitaji madogo madogo ya nyumbani (hasa jikoni) naamini unakuwa umeanzisha kwa sababu umeona eneo hilo kuna uhitaji wa aina hiyo ya huduma. Wewe unaweza kuwa unafanya tu labda kwa sababu ya shida fulani za maisha lakini wakati huo huo moyo wako unafurahia kile unachokifanya na unajikuta kila siku unabuni mbinu mpya na mikakati wa kuboresha genge lako. Kidogo kidogo unafungua genge lingine sehemu nyingine, na lingine na lingine, nk. Mwishowe unajikuta unatamani kuwa na duka kubwa la vyakula na mahitaji mengine ya kila siku au supermarket. Ukijiona unang’ang’ana kwenye “line” moja ya shughuli (Biashara) basi tambua hilo ndio kusudi lako na ndani yako una zawadi kubwa sana ya kutoka kwa Mungu ya kuhudumia jamii kupitia uuzaji wa mahitaji ya nyumbani.
Lakini ukijiona unatanga tanga leo umefanya shughuli hii kesho umefanya shughuli ile ambazo mwisho wa siku hakuna mahali zinakutana kwa namna yoyote ile japo unapata pesa, basi wewe hujatambua kusudi la maisha yako na usipokuwa makini utakuwa mhangaikaji hadi mwisho.
Ukifanya jambo nje ya kusudi ya maisha yako hutakaa ulifurahie kamwe, litageuka kuwa mateso hata kama linakuingizia pesa nyingi. Unaweza ukawa unafanya kitu nje ya mstari wako wa maisha hata kama kinakulipa mabilioni yaani bado utakuwa kama SAMAKI ALIYETUPWA NJE YA MAJI. Samaki akiwa nje ya maji, zile dakika chache kabla hajafa huwa anahangaika sana na ukimmiminia tone moja la maji kwenye mkia utaona anavyojaribu kutaka kuogelea. Kale katone ka maji kwenye mkia wa samaki akiwa nchi kavu ni sawa na wewe unapokuwa unafanya shughuli nje ya kusudi la maisha yako inyokupa hela nyingi lakini ikatokea katika kuhangaika ukafanya ka-kitu kadogo ambako kako ndani ya kusudi la maisha yako – moyo waku unakuwa na amani sana na unafurahi sana. Lakini unajikuta huendelei kufanya hilo jambo kwa sababu halikuingizii hela nyingi kwa wakati huo ukilinganisha na lile lingine hivyo unaamua kuendelea kuishi nje ya kusudi la maisha yako ili upate mali za nje na kuunyanyasa moyo wako. Maana yake ni kwamba, kama unafanya shughuli inayokuingizia kipato iliyo nje ya kusudi la maisha yako, hutokaa uache kuhangaika kujaribisha vitu vya aina mbalimbali. Kwa sababu moyo wako hautotosheka wa kuridhika – HUWEZI KUKATA KIU YA MAJI KWA KUNYWA SODA AU JUISI JAPOKUWA VYOTE NI VIMIMINIKA. . Ndio sababu huwa napenda kusisitiza sana kupata muda kwa ajili ya maisha yako binafsi, hii inakusaidia kujitambua.
Tatizo wengi hatutaki kuanzia chini, tunapadharau huku chini lakini matajiri wakubwa duniani kama unafuatilia historia za maisha yao na jinsi walivyoanza utagundua kwamba walianza wengine wakiwa hawana kitu kabisa. Ukiwa na nidhamu ya maisha hasa kwa kufuata kanuni za maisha, kanuni za biashara/shughuli unayofanya na kanuni za maisha yako binafsi huwezi kuacha kufanikiwa. Mafanikio ni safari. Umaarufu hauji bila kuwa umefanikiwa kwenye jambo fulani hata kama ni ujinga utapata umaarufu kwa wajinga wenzako.
Mafanikio yanaanza kwa wewe kuweza kujitofautisha na maisha yako ya nyuma. Usiruhusu maisha yako ya nyuma kukuwinda na hivyo kuwa kikwazo cha maisha yako unayoyaendea. Usiishi kwa mazoea ya nyuma. Mafanikio ni pale unapoweza kujitambua na kusimama imara katika kanuni za maisha ulizojiwekea na kujitofautisha na watu wengine wote kwa sababu wewe ni wa tofauti, kila binadamu ni wa tofauti ndio mana kila mtu ana nafsi yake mwenyewe hata mkiwa mapacha mmeunganika viungo vya mwili.
MAFANIKIO YANAANZA NAWEWE
Recent Comments