Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Madhara ya dawa za kuulia wadudu maarufu kama viwatilifu

Dawa za kuulia wadudu maarufu kama viwatilifu zimetengenezwa kwa lengo la kuangamiza wadudu wanaoharibu mazao au wanaomdhuru binadamu. Hata hivyo kutokana na sababu kuwa lengo la dawa hizi ni kuangamiza, huathiri pia viumbe hai vingine akiwemo binadamu.

Takwimu kutoka shirika la afya duniani WHO zinabainisha kuwa kuna zaidi ya vifo 220,000 vitokanavyo na athari za sumu zilizoko kwenye dawa za kuulia waduduโ€”viwatilifu.

Ikiwa unataka kuweka afya yako salama, basi karibu nikushirikishe athari 8 kiafya za dawa za kuulia wadudu โ€” viwatilifu.

1. Husababisha saratani.

Watafiti mbalimbali wa maradhi ya saratani wanaeleza kuwa dawa za kuulia wadudu zinachangia kwa kiasi kikubwa kusababisha seli za saratani mara zinapoingia kwenye mwili wa binadamu.

Hatari hii hutokea zaidi pale ambapo mtu anakula vyakula vilivyoathiriwa na sumu za dawa za kuulia wadudu.

2. Huvuruga mfumo wa homoni.

Mwili wa binadamu huzalisha homoni mbalimbali zinazowezesha viungo mbalimbali kufanya kazi vyema.

Dawa za kuulia wadudu zinapoingia mwilini huathiri mfumo wa homoni wa binadamu na kuufanya usifanye kazi vyema.

3. Huathiri mfumo wa uzazi.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa matatizo ya uzazi kati ya wanaume na wanawake huchangiwa kwa kiasi kikubwa na athari za dawa za kuulia wadudu.

Inaelezwa kuwa sumu hizi zinapoingia mwilini kupitia matunda au mbogamboga huharibu mfumo wa uzazi na kusababisha ugumba au utasa.

4. Huharibu ubongo.

Madawa ya kuulia wadudu โ€” viwatilifu huathiri pia mfumo wa ubongo hasa kwa watu wanaoyapulizia au kukaa nayo karibu kwa muda mrefu.

Maradhi kama vile Mild Cognitive Dysfunction (MCD) ambayo humfanya mtu ashindwe kutambua vyema maneno, rangi au namba huchangiwa kwa kiasi kikubwa na athari za dawa za kuulia wadudu.

5. Huathiri mama mjamzito na mtoto

Mama mjamzito anatakiwa kuchukua tahadhari nyingi sana wakati wa ujauzito ili kulinda afya yake na mtoto aliyeko tumboni.

Matumizi ya viwatilifu ndani ya nyumba au karibu na makazi kwa lengo la kuua wadudu kama vile mbu, chawa, kunguni, au utitiri kunaweza kumwathiri mama mjamzito na mtoto kwa kiasi kikubwa.

Inaelezwa kuwa sumu hizi zinaweza kusababisha mtoto kuzaliwa bila viungo vyote, kuzaliwa kabla ya wakati au hata kifo.

6. Huharibu viungo muhimu vya mwili

Kumekuwa na taarifa mbalimbali ulimwenguni zikieleza kuwa dawa za kuulia wadudu huharibu viungo muhimu vya mwili kama vile figo na ini.

Utafiti uliofanyika huko India ulibaini kuwa watu wengi waliokufa kutokana na maradhi ya figo waliishi katika mazingira yenye sumu za kuulia wadudu au kula vyakula vyenye mabaki ya sumu hizo.

7. Huathiri mfumo wa upumuaji

Kutokana na watu wengi kutumia dawa za kuulia wadudu bila kuvaa vifaa vya kujikinga, wengi huvuta sumu zilizoko kwenye dawa hizo na kusababisha kuathiri mfumo wa upumuaji hasa mapafu.

Hivyo ili kujikinga na athari hii inashauriwa kuvaa vifaa bora vya kuzuia kuvuta sumu zilizoko kwenye dawa za kuulia wadudu.

8. Huathiri ngozi

Kama ilivyo kwenye swala la kuathiri mfumo wa upumuaji, watumiaji wengi wa dawa za kuulia wadudu hawakingi ngozi zao kwa mavazi au vifaa maalumu vinavyoepusha athari za dawa hizo kwenye ngozi zao.

Ikumbukwe kuwa sumu zilizoko kwenye dawa za kuulia wadudu zinaweza kuingia mwilini kirahisi kupitia ngozi na kusababisha athari nyingi za kiafya.

Naamini umeona jinsi ambavyo dawa za kuulia wadudu โ€” viwatilifu zinavyoweza kuathiri afya ya binadamu ikiwa hazitatumiwa kwa uangalifu na kwa kufuata kanuni muhimu za matumizi yake.

Ikumbukwe kuwa vifo vingi na matatizo mbalimbali ya kiafya hutokana na mwili wa binadamu kukutana na sumu mbalimbali, hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari.

Kilichompata huyu jamaa mroho wa nyama, Hata kaa arudie tena

Jamaa kaenda kumtembelea rafiki yake Levi, kule sehemu za kwetu, akakaribishwa bonge ya ugali na nyama nyingi tu, wakati anakula akagundua kuwa shemeji yake, mke wa rafiki yake hali nyama;

JAMAA: Aise hili ni bonge ya lanchi hii, lakini Levi mbona sisi tu tunakula nyama shemeji Gulo hagusi kabisa anaishia mchicha tu? Tabia gani hii?
LEVI: Hapana sijamkataza, ila shemeji yako Mngoni halagi nyama ya FISI kama sisi

Cheki hawa wachungaji

CHEKA KIDOGO

Wachungaji watatu walikutana kwa siri na kuelezana matatizo yao ili waweze kuombeana.

MCHUNGAJI WA KWANZA: mimi tatizo langu ni wizi, kila nikimaliza ibada lazima niibe pesa za sadaka.

WA PILI: Mimi tatizo langu ni wanawake yani nimeshalala na wana kwaya wote pamoja na mke wa ASKOF.

WA TATU akaanza kulia badala ya kuongea.WENZAKE:

We vp unatatizo gani mbona unalia???

AKAJIBU: jamani mimi tatizo langu ni “umbea” haya yote tuliyoongea lazima nikaseme!

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ‘†๐Ÿป๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Maswali ya kijinga yakijibiwa vizuri

Haya ndiyo majibu mazuri๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Q: Umenyoa nywele?

A: *Hapana, nimebadilisha kichwa.*

Q: Hiyo simu umenunua?

A: *Hapana nimeitengeneza mwenyewe.*

Q: Utakula mboga na nini?

A: *Mdomo*

(Simu inaita usiku,then aliyepiga anauliza) Q: Nimekuamsha?

A: *Hapana nilikuwa naota jua hapa nje.*

Q: Gazeti la leo linasemaje?

A: *Sijaongea nalo.*

Q: Gari limejaa, nitakaa wapi?

A: *Usijali dereva anashuka kituo kinachofata utapata kiti.*

Q: Hiyo ni ajali?

A: *Hapana ni driver ameamua kupark gari upside down* .

Q: Umepause movie?

A: *Hapana wamechoka kuact wanarest.*
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚

Ujumbe kwa mabinti kuhusu uvaaji

Familia Kwanza: Wasichana wawili waliwasili kwenye Kikao huku wamevaa nguo ambazo zilikuwa zikionyesha miili yao.

Hiki ndo kitu ambacho Mwenyekiti wa kikao alichowaambia, aliwatazama kwa muonekano mzuri kisha akawataka wakae, kisha akawaambia jambo ambalo hawatoweza kusahau katika Maisha yao.

Aliwaangalia moja kwa moja katika macho yao, kisha akasema;

“Wasichana, kila kitu ambacho MUNGU amekiumba chenye thamani katika Dunia hii kimesitiriwa, na ni vigumu kukiona au kukipata.

1.Wapi unapoipata Almasi?
Ni chini kabisa ndani zaidi katika ardhi, na yamefunikwa na kuhifadhiwa humo

2. Wapi mnapoweza kuipata Lulu? Pia ni ndani zaidi kwenye kina kirefu zaidi katika Bahari, na yamehifadhiwa humo na kujificha ndani ya Sanamu zuri la Baharini

3. Wapi mnapoweza kuipata Dhahabu? napo pia ni ndani zaidi katika Migodi, na yamefunikwa juu na Ardhi za Miamba na ndio uyapate hapo. Yatupasa tufanye kazi ya ziada zaidi na tulime kwa undani zaidi ndipo tuyapate.

Kisha Mwenyekiti akawaangalia wale Mabinti kwa Jicho kali zaidi na kisha akawaambia;
“Miili yenu ni ya kuogopwa na ina thamani sana, na inazidi sana hata thamani ya Dhahabu, Almasi au Lulu. Na yawapasa muihifadhi zaidii.

Kama mtatunza Madini yenu kama ilivyotunzwa Almasi, Dhahabu na Lulu basi Makampuni yenye sifa nzur katika Jamii, Makampuni ya uhakika, Makampuni ya kuaminika yenye Mitambo mizuri yatatenga Muda wa miaka kadhaa katika kufanikisha kuyapata Madini hayo.

Kwanza itawapasa wawasiliane na Serikali (ambayo ndio familia yako) pia kusahihisha Mikatabata muhimu (ndoa) na mwisho ni Mgodi wenye dhana kubwa (ambayo ndiyo ndoa) lakini kama ukiacha madini yako yenye thamani nje hayajahifadhiwa katika uso wa Dunia basi utamvutia kila Mmoja (Mwanaume) na hasa wale ambao ni Wachimbaji haramu watakuja na kuchimba kiharamu (Zinaa), kwa hiyo kila mmoja atachukua kwa vifaa vilivyo na Makali na hivyo ndio watakavyokulima kirahisi.

Hivyo basi nawashauri hifadhini Miili yenu vizuri ili iwavutie wachimbaji wa halali (Waoaji) ndio wakukaribie upate kuheshimika

Jinsi ya kuishi maisha marefu (Mambo ya kuzingatia ili uishi maisha marefu)

Kuishi ukiwa na afya na kuishi maisha marefu kunawezekana kwa kubadili hali ya maisha unayoishi inayoharibu afya yako mfano uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe kupita kiasi,kutokufanya mazoezi na kutokula matunda na mbogamboga.

Mambo yanayoweza kukusaidia kuishi maisha marefu ni kama yafuatayo

  1. Kuuandaa mwili kwa maisha marefu kwa kufanya mazoezi
  2. Kuwa makini kutambua na kutibu matatizo ya kiafya
  3. Kuepuka mazingira na kufanya kazi kwa namna au kazi zinazoweza kudhuru maisha yako. Mfano kuendesha gari bila kufuata utaratibu, kutokuvaa vifaa vya kujikinga wakati wa kazi
  4. Epuka vitu vyenye sumu vinavyoweza kudhuru afya yako na kukuletea matatizo ya kiafya kama dawa za mimea na mifugo, zitumie kama inavyotakiwa
  5. Usinywe pombe, usivute sigara wala kutumia dawa za kulevya
  6. Kula mlo kamili
  7. Usile vyakula vyenye chumvi na mafuta mengi
  8. Kunywa maji mengi ili kusafisha mwili
  9. Epuka msongo wa mawazo

Sababu ya mwanaume kunya kitandani alipokuwa kalala na mke wake

Jamaa flani alikuwa amelala na mkewe. Mara akamuona mtu amesimama kitandani.

Jamaa akafoka, “Toka hapa, we ni nani mpaka unakuja kitandani mwangu?”

Yule mtu akajibu, “Mi ni malaika na hapa sio kitandani mwako uko mbinguni!”

Jamaa, “Huh! Inamaana nimekufa,mbona mi bado kijanaโ€ฆ naomba nirudishwe!”

Malaika, “Inawezekana lakini siwezi kukurudisha kama mtu labda urudi kama mbwa ama kuku.”

Jamaa akakumbuka mbwa wanavyopata taabu ya kulinda, akaonelea arudi kama kuku.

Malaika akamgeuza kuku, akamwambia ajifunze kutaga kabla hajapelekwa duniani.

Akachuchumaa na kuanza kujikamua; yai la kwanza likatoka. akajikamua tena, yai la pili likatoka. Akajikamua tena mara ya tatu.

Wakati yai la tatu linatokaโ€ฆ akashtukia amepigwa konde ikifuatwa na sauti ya hasira ya mkewe, “Pumbav*! Balaa gani hiiโ€ฆ. unakuny* kitandani!!”

Jinsi ya kuchagua rangi sahihi wakati wa Kujipodoa

YAPO mambo mabalimbali katika tasnia ya urembo hasa katika vipodozi yanayopaswa kuzingatiwa katika kuboresha muonekano wa mtu.
Moja ya mambo hayo ni ujuzi na uelewa wa kutumia rangi katika kujipodoa kwani ni wanawake wachache wenye ujuzi huu.
Katika makala hii, nitakuelezea namna ya kuchanganya na kutofautisha rangi za vipodozi, lengo likiwa ni kuboresha muonekano wako.

Uchanganyaji wa rangi za vipodozi ni muhimu sana kwani katika kujipodoa, rangi zote za vipodozi unavyopaka zinatakiwa zioane ili kuleta muonekano ulio sawa na wa kueleweka.

Kwanza kabisa unatakiwa uwe makini katika kuoanisha rangi za vipodozi pamoja na rangi ya ngozi yako, hivyo katika hili unatakiwa kuwa na ujuzi maalumu ili usije ukafanya makosa na kuharibu muonekano wako.

Pia inabidi ufahamu hatua za upakaji vipodozi ili usije ukafanya vipodozi vingine visionekane katika uso wako.

Namna ya kuoanisha na kutofautisha rangi

Siku zote vipodozi vyako lazima viendane na mavazi yako ili kuleta maana zaidi kwa mfano, mara nyingi rangi ya mdomo โ€˜lipstickโ€™ huendana na vazi lako wakati shedo โ€˜eye shadowโ€™ zinatofautiana.

Kwa nguo za pinki

Katika mavazi haya, unatakiwa kupaka rangi ya mdomo yenye rangi ya pinki ambayo itaendana sawasawa na mavazi yako huku ukichanganya na shedo โ€˜eyeshadowโ€™, inaweza kuwa ya rangi ya bluu ili kuitofautisha na mavazi yako, hapo utakuwa sawa katika kanuni za urembo.

Vazi la kijani

katika vazi hili unatakiwa kupaka rangi ya mdomo yenye rangi ya kahawia huku ukichanganya na shedo ya rangi ya kijani au kahawia iliyoingiliana na pinki au rangi ya machungwa.

Kwa vazi la njano au kahawia

Katika vazi hili unatakiwa kupaka โ€˜lipstickโ€™ ya rangi ya kahawia iliyokolea, kwa upande wa shedo waweza kupaka ya rangi ya dhahabu.

Kwa vazi la bluu

Katika vazi hili unatakiwa kupaka โ€˜lipstickโ€™ yenye rangi ya pinki huku ukipaka shedo ya rangi ya bluu kwa mtindo huu utakuwa mwenye kuvutia siku zote.

Staili nyingine za michepuko ni shida

Mtu na mkewe walikuwa bado wamelala asubuhi, mtu akapiga hodi mke akaenda kufungua mlango, si akakuta mchepuko wake,
MKE: Unataka nini we mpumbavu?

MUME: Nani huyo unamtukana?
MKE: Kuna mtu hapa anakichwa kama nenda urudi badae
MCHEPUKO:Nawewe pua kama poa
MKE:Miguu kama masaa mawili
MCHEPUKO:Masikio kama sichelewi
MKE: Ondoka hapa mjinga we. โ€ฆโ€ฆ Akafunga mlango
MUME: mwambie ana macho kama sitoki leo ng’oo
SIPENDI UJINGA MM nikiwa na my love pr

Njia nzuri ya kufanikiwa katika maisha

Kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu anayejengaย GHOROFAย na yule anayejengaย Nyumba ya KAWAIDA.

Anayejengaย Ghorofaย anatakiwa achimbe msingi Mrefu kwenda chini kabla hajaanza
kuinuaย Ghorofaย yake juu. Hivyo wakati huyu mwingine anapokuwa anajenga Nyumba ya kawaida atakapokuwa tayari anakaribia hata kuezeka, unaweza kukuta yule anayejengaย Ghorofaย bado yuko kwenye Msingi.
Ila siku akianza kuinuaย Ghorofaย lake, kila mtu atashangaa urefu wa juu atakaoenda nao.

Kwenye maisha ndivyo ilivyo-ย “If want to go so high, you need to go so deep” (Kama unataka kwenda juu sana ni lazima ukubali kwenda chini sana).ย Ni lazima ufanye kitu cha tofauti kitakochokujengeaย Future imara.

Ukweli ni kuwa Watu wengi wanaokuzunguka wanajenga maisha ambayo ni kamaย Nyumba ya kawaida.
Na wewe kama unataka kujenga maisha yanayofanana naย Ghorofa,
Ni lazima ukubali kuonekana unachelewa kwenye baadhi ya mambo.

Hii inamaanisha nini?โ€ฆ
Hii inamaanisha kuwa utalazimika kufanya vitu vyaย TOFAUTIย na kuwaย TAYARIย kusubiri.
Utatakiwaย Kuwekezaย wakati wengine wanaenda kununua nguo mpya waendane na Fashion,
Utatakiwaย Kusoma vitabuย wakati wengine wanaangalia movie na kupiga stories,
Utatakiwaย Uanzishe Biashara yakoย wakati wenzako wamesharidhika na mshahara wanaopata n.k

Unachofanya kuanzia unapoamka hadi unapoenda kulala kitajulisha kama unajengaย Maisha GHOROFAย amaย Maisha KAWAIDA.

Ukijiona unapoteza muda hovyo,
ukiingiaย Facebook/instagramย ni kusoma umbea tu,
Unalalamika unasema utafanya na hakuna unachofanya, ujue unajengaย Maisha ya KAWAIDAย tena ni kamaย Nyumba ya UDONGO.

Ukitaka kujenga maishaย GHOROFA;
1.ย _Jifunze kitu kipya leo._
2.ย _Chukua hatua kuelekea Ndoto yako._
3.ย _Usiwe mtu wa kulalamika bali tafuta suluhisho kwa kila changamoto._

Je, LEO utajiunga na wanaojengaย Maisha GHOROFAย ama wale wanaojengaย Maisha ya KAWAIDA?

Twende zetu tujengeย Maghorofa !!!

Jinsi ya kutibu chunusi za usoni kwa kutumia Parachichi na asali

Unahitaji:

a)Kijiko kimoja cha asali
b)Parachichi 1

Hatua kwa hatua namna ya kufanya tiba hii:

a)Safisha vizuri uso wako
b)Kausha na taulo uso wako
c)Chukua nyama ya ndani ya parachichi
d)Ongeza asali kijiko kimoja ndani ya parachichi
e)Changanya vizuri vitu hivyo viwili upate uji mzito.
f)Pakaa mchanganyiko huo kwenye sehemu yenye chunusi
g)Acha kwa dakika 15 mpaka 20 hivi
h)Mwisho jisafishe na maji ya uvuguvugu na ujifute vizuri

Jinsi ya Kupika skonzi

Mahitaji

Unga wa ngano (self risen flour 2 vikombe vya chai)
Sukari (sugar 1/2 kijiko cha chakula)
Chumvi (salt 1/2 kijiko cha chai)
Hamira (yeast 1/2 kijiko cha chakula)
Baking powder 1/2 kijiko cha chai
Siagi (butter 1/4 ya kikombe cha chai)
Maziwa (fresh milk 3/4 ya kikombe cha chai)(unaweza kutumia maji badala ya maziwa)

Matayarisho

Pasha maziwa yawe ya uvuguvugu kisha weka pembeni, pia yeyusha siagi na uweke pembeni.Baada ya hapo tia kila kitu kwenye bakuli la kukandia kasoro maziwa, na uchanganye vizuri kisha tia maziwa kidogo kidogo katika mchanganyiko huo kisha ukande. Ukimaliza uweke kwenye sehemu ya joto na uache uumuke. Ukisha umuka utawanyishe katika madonge saba Kisha .pakaza mafuta au siagi katika chombo cha kuokea kisha yapange hayo madonge katika hicho chombo na uyaache yaumuke tena (kwa mara ya pili). Baada ya hapo pakaza mafuta juu ya hayo madonge na uyaoke (bake) katika oven (moto 200ยฐC ) kwa muda wa dakika 25 na hapo scones au maskonzi yatakuwa tayari

Mapishi mazuri ya Wali Wa Kukaanga Kwa Kidari Cha Kuku

Vipimo vya Wali:

Mchele – 3 vikombe

*Maji ya kupikia – 5 vikombe

*Kidonge cha supu – 1

Samli – 2 vijiko vya supu

Chumvi kiasi

Hiliki – 3 chembe

Bay leaf – 1

Vipimo Vya Kuku

Kidari (chicken breast) – 1Kilo

Kitunguu – 1

Tangawizi mbichi – ยฝ kipande

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 7 chembe

Pilipili mbichi – 3

Ndimu – 2

Pilipilimanga – 1 kijiko cha chai

Mdalasini – ยฝ kijiko cha chai

Jira/Cummin ya unga – 1 kijiko cha chai

Maji – ยผ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Wali:

Osha na roweka mchele kisha weka sufuria katika moto tia samli ipashe moto.
Tia hiliki, bay leaf, kaanga, kisha tia mchele ukaange kidogo.
Tia maji, chumvi na kidonge cha supu, upike wali kama unavyopika pilau.
*Maji kisia kwa kutegemea mchele ulivyo.
*Unaweza kutumia supu yoyote badala ya kidonge.

Kuku:

Katakata kidari cha kuku vipande vya kiasi, weka katika sufuria, tia ndimu, bizari zote, chumvi.
Katakata kitunguu vipande vidogodogo, pilipili, na kitunguu thomu (chopped), tia katika kuku.
Chuna tangawizi mbichi tia katika kuku. Changanya vitu vyote vizuri.
Tia maji kiasi ยผ kikombe tu kiasi cha kumkaushia kuku. Weka katika moto mpike huku unageuzageuza. Anapokaribia kukauka epua akiwa tayari kuliwa na wali (na saladi upendayo)

Jinsi ya kutengeneza Keki Ya Mbegu Za Mchicha

Viamba upishi

Unga ngano vikombc 3
Unga mbegu za mchicha kikombe 1
Baking powder vijiko vidogo
Maziwa kikombe 1
Sukari kikombe 1
Blue band kikombe ยฝ
Mayai 10-12

Hatua

โ€ข Chagua, osha, kausha mbegu za mchicha mweupe, kisha saga zilainike.
โ€ข Chekecha unga wa ngano, unga wa mbegu za mchicha na baking powder Kwenye bakuli kubwa.
โ€ข Ongeza sukari na changanya.
โ€ข Ongeza mayai kidogo, kidogo ukikoroga na mwiko kwenda njia moja mpaka ilainike.
โ€ข Kama rojo ni zito ongeza mayai, au maziwa ili iwe laini, ongeza vanilla na koroga.
โ€ข Paka mafuta kwenye chombo cha kuoka au sufuria na chekechea unga kidogo.
โ€ข Mimina rojo ya keki na oka kwenye oveni au kama ni sufuria funika, weka moto mwingi juu, chini weka moto kidogo.
โ€ข Ukinusia harufu nzuri ya vanilla, funua, choma kisu katikati ya keki, kama ni kavu epua, pozesha na pakua kama kitafunio.

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About