Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Suluhisho rahisi la nguvu za kiume hili hapa

NI muujiza! Pengine hivyo ndivyo yeyote anaweza kusema pindi akisikia kwa mara ya kwanza juu ya namna mihogo mibichi na nazi kavu maarufu kama mbata vinavyoweza kuwasaidia watu kiafya, na hasa wanaume.

Uchunguzi uliofanywa kwa siku kadhaa ukihusisha mahojiano na baadhi ya madaktari na pia maandiko yatokanayo na tafiti mbalimbali, umebaini kuwa mihogo na nazi mbata ambavyo huuzwa kwa wingi na kina mama jijini Dar es Salaam, vina uwezo mkubwa wa kurejesha heshima kwa kina baba mbele ya wenzi wao kwa kuimarisha uwezo wa kushiriki tendo la ndoa.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, imebainika kuwa uwezo wa mihogo na nazi mbata katika kuwasaidia wanaume kwenye ushiriki wa tendo la ndoa hutokana na wingi wa virutubisho vilivyomo, hasa madini ya Zinc na Potassium (kwenye mihogo mibichi) na kiambata cha selenium kinachopatikana kwenye nazi mbata.

“Vyakula hivi vina maajabu makubwa kwa afya ya kina baba… vinapoliwa kila mara na tena kwa kuzingatia usafi, huwasaidia wengi katika kuimarisha nguvu zao za tendo la ndoa na hivyo kuwapa heshima kwa wenzi wao,” mtaalamu mmoja wa masuala ya lishe jijini Dar es Salam aliiambia Nipashe.

Ofisa Utafiti wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Walbert Mgeni, alisema mihogo mibichi na nazi kavu (mbata) ni vyakula ambavyo vimethibitika kitaalamu kuwa husaidia kuiamrisha nguvu za tendo la ndoa kutokana na madini mbalimbali yanayopatikana, na hasa Zinc.

Alisema ni kwa sababu hiyo, anaamini ndiyo maana kuna kina baba wengi hutumia bidhaa hizo jijini Dar es Salaam na kwingineko nchini huku wauzaji wake wakubwa wakiwa ni kina mama.

“Kuna uvumi mwingi kuhusu faida za mihogo mibichi na nazi kavu kwa wanaume. Wengi huhusisha na masuala ya tendo la ndoa…ukweli ni kwamba wanaozungumzia suala hilo wako sahihi ingawa wanaweza kuwa siyo wataalamu.

Vitu hivyo vina madini mengi yakiwamo ya Zinki ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume na kuongeza nguvu za kiume kwa mtu anayekula kwa usahihi na kwa muda mrefu,” alisema Mgeni.

Alisema zaidi ya kuimarisha mfumo wa uzazi kwa wanaume, mihogo mibichi na mbata vina faida nyingine nyingi mwilini mwa walaji ikiwa ni pamoja na kuimarisha milango ya fahamu, kusaidia uponaji wa vidonda vya ndani na nje ya mwili, kutunza ngozi na kuilinda, nywele na pia kusaidia uponaji wa matatizo mengi ya macho.

MUUJIZA ZAIDI
Dokta John Kimai wa Kituo cha Afya cha Arafa kilichopo Kimara jijini Dar es Salaam alisema ni kweli mihogo mibichi na nazi mbata husaidia kuiamrisha afya za walaji katika maeneo mengi ikiwamo via vya uzazi.

Aidha, alisema faida nyingine kiafya, hasa kwenye nazi mbata ni kuepusha matatizo ya moyo yatokanayo na wingi wa lehemu kwa kuwa nazi aina hiyo huwa na kiwango kikubwa cha kiambata kiitwacho ‘lauric acid’.

Alisema faida nyingine ya nazi mbata ni kusaidia mlaji kuepukana na athari za kuvimbiwa, kuongeza nguvu za mwili kutokana na mafuta yake kuelea kwa kiasi kidogo kwenye damu (medium chain triglycerides – MCT) na hivyo huyafanya kusafirishwa moja kwa moja hadi kwenye ini ambako hutumika kama chanzo cha haraka cha nguvu.

Aidha, kwa mujibu wa Dk. Kimai, mbata husaidia pia kuimarisha kinga dhidi ya maradhi mbalimbali kutokana na uthibitisho wa tafiti mbalimbali kuthibitisha kuwa ‘lauric acid’ hubadilishwa kuwa acid inayojulikana kama ‘monolaurin’. Aidha, nazi kavu husaidia pia kuzisisimua seli na shughuli za ubongo na kwa kufanya hivyo husaidia kuzuia matatizo ya akili (dementia) na upotezaji wa kumbukumbu (Alzheimer).

Akielezea kuhusu faida za mihogo mibichi, daktari mwingine alisema kuwa ina madini mengi pia yakiwamo ya calcium, phosphorus, chuma na potassium ambayo kwa pamoja husaidia ukuaji wa tishu za mwili wa binadamu.

“Kwa mfano, calcium ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha mifupa na meno kwa mwanadamu na hivyo mtu anayekula kwa wingi mihogo mibichi huimarisha meno yake na kuyafanya kuwa na nguvu,”alisema.

Katika mbata, baadhi ya virutubisho vingine vilivyomo ni Folates, Niacin, Pantothenic acid,
Pyridoxine, Riboflavin, Thiamin, Sodium na Copper

Mvua zazua kasheshe! Soma hii..

Baba- : Halloo mke wangu.. yaani ni shida sitaweza kurudi nyumban, daraja limevunjika na kutoka morogoro kurudi dar haiwezekani
MAMA:- Mme wangu morogoro ulienda bila kuniaga! ?
BABA:- Ilikuwa ni ghafla sana mke wangu sikuweza kukwambia
MAMA:- kha! Sasa watoto nani atawaangalia
BABA:- Unasemaje! We uko wapi kwan
MAMA:- Niko bagamoyo na daraja limeondolewa na maji sitaweza kurudi.
BABA:- Unasemaje we mwanamke.. nakwambia nikukute nyumban ndani ya dk 15
Baada ya dk 15 Baba kafika nyumban.
MAMA:- Haya umefkaje kutoka morogoro?
BABA:- Nimepewa lift na helkopta ya Mbowe..

Kama umeipenda shea na rfiki zakooo…..

Mahaba kwa wanawake wa siku hizi

Wanawake wengi siku hizi hawajui au hawataki kuonesha mahaba
Nimefanya kautafiti kangu kadogo nimegundua wanawake wengi siku hizi hawaonyeshi mahaba yani kwa ujumla hawako “Romantic”. Wanawake wengi siku hizi akipata mwanaume anaona amepata mtu wa kumsaidia shida zake kwa hiyo hata akiwa ndani ya mahusiano anafikiria zaidi kutatuliwa shida zake kuliko mahusiano yenyewe.

💞
Wanawake wa siku hizi wengi, kwa mfano umemtoa out kidogo mkapate walau msosi sehemu nzuri, mkianza kula mpaka mnamaliza hakumbuki hata kukulisha kidogo kimahaba. Unakuta anakula msosi kimpango wake utafikiri anakula na kaka yake. Mnatoka kidogo mnatembea unakuta anatembea na wewe utafikiri anatembea na kaka yake; yani unaweza ukamuacha nyuma kidogo au akawa mbele yako anashindwa kujiongeza kupitisha mkono wake kwenye kikwapa chako na kukushika kimahaba.
💞
Wakati mwingine anakuona jasho linakutoka usoni anashindwa hata kukufuta kimahaba anakutazama tu utafikiri wewe ni kinyago cha mpapure. Wakati anakuaga anaondoka utafikiri anamuaga kaka yake hakupigi hata busu. Mwanamke unazungumza nae hakushiki hata ndevu zako kimahaba, mwanamke unakuwa nae hakufunyii massage wala hakukati mara moja moja kucha zako kimahaba.
💞
Wakati mwingine unakuta umekaa nae mwaka mzima kwenye mahusiano lakini hajawahi kukwambia neno “Nakupenda”mpaka wewe uanze kumwambia kwanza.
💞
Wanawake wengi wa siku hizi wanapenda kudekezwa, kubembelezwa na kupewa pesa ndio maana wengi utasikia wakisema “nataka mwanaume Romantic na mwenye pesa” lakini hawajiulizi je, wao ni Romantic? Au sisi wanaume hatuhitaji hayo mahaba ya wanawake?
💞
Asili ya mwanamke ni mfariji mkuu wa mwanaume lakini siku hizi wanawake wengi wamekuwa stress kwa wanaume.
💞
Note: Hakuna mwanaume mbahili kwa mwanamke Romantic.

Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke

Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

Mume alichomjibu mchepuko wa mke wake

😎 Jamaa kamuaga mkewe anaenda semina Songea kwa wiki nzima kumbe kahamia kwa demu nyumba ya pili toka kwake. Siku ya 1 kalala asubuhi alipoamka kachungulia kwake kukoje,

Si kamuona jamaa yuko nje ya nyumba yake kavaa taulo lake anapiga mswaki. Akapiga kelele, ‘We nani?’, Jamaa akajibu, ‘Mshikaji mambo ya mjini, mume wa huyu demu kasafiri kaenda Songea mi ndo najivinjari hapa’. Mume kajibu kwa uchungu, Shenzi mkubwa, ngoja nirudi toka Songea nakuua.😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆

*Mniache mimi sipendi Ujinga Ujinga 🏃�🏃�🏃�🏃

Kuna watu makauzu ila huyu kazidi.. Soma hii!

Kakubaliana vizuri na msichana fulani hivi kuwa aibuke gheto, mchizi kajipanga vizuri kabisa…. mara saa nne hivi mdada kasema hana nauli.
Mshkaji kajikunja kamtumia Elfu tano maana mwenye shida alikuwa ni yeye……
Baada ya nusu saa yule dada akamtumia meseji.
“Jamani mpenzi, kumbe baba hatoki nilijua atatoka… sorry bae sitaweza kuja kwa leo… sooo sorry!”
Mshkaji jiii! hajajibu kitu…..

Baada ya muda kidogo meseji ikaingia katika simu ya binti, akajua mchizi kajibu. Mh! kutazama ni meseji kutoka Mpesa.

“CA90F0511 IMETHIBITISHWA Tshs 5000 ILIYOTUMWA KIMAKOSA KATIKA ACCOUNT YAKO IMETOLEWA SALIO LAKO NI Tshs 5”

Halafu ndo ikaingia meseji ya mshkaji.
“BASI POA SIKU NYINGINE KAMA VIPI”

#dada wa watu mashavu yakamshuka… hakuamini kilichotokea…. yaani jamaa keshawapigia Voda na pesa fasta imezuiliwa……

Faida za kuoga maji ya Baridi

Watu wengi hupenda kuogea maji ya moto, hii ni kutokana na kuogopa baridi au sababu za kimazoea tu. Ingawa mara nyingi umekuwa ukisisitiziwa kuwa maji moto yana manufaa mengi, lakini hata maji ya baridi nayo yana manufaa yake.

Je uko tayari kuongeza maarifa au hata kubadili mtazamo wako? Karibu nikushirikishe faida za kuogea maji ya baridi.

Huongeza utayari katika mwili.

Maji ya baridi hukufanya uchangamke, hili ni tofauti na maji ya moto. Mara nyingi mtu anapoogea maji ya baridi hasa baada ya kuamka humfanya awe katika hali nzuri ya kuwa tayari kuendelea na majukumu yake.

Kumbuka hata wakati wa kuogea maji baridi kasi ya upumuaji hubadilika na kukufanya kuongeza kiasi cha oksijeni kinachoingia mwilini.

Hulainisha ngozi na nywele

Maji moto huchubua ngozi na nywele, hasa kwa kuondoa mafuta laini yanayolinda ngozi na nywele na kuvifanya viwe vikavu sana.

Kwa kuogea maji ya baridi, ngozi na nywele zako havitapaushwa bali vitasafiwa na kuachwa katika hali nzuri ya kupendeza.

Huboresha kinga mwili

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Thrombosis Research Institute, ulibainisha kuwa watu wanaoogea maji ya baridi wanaongeza uzalishaji wa seli nyeupe za damu.

Utafiti huu unaeleza kuwa kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha metaboli mwili unapojaribu kujipasha moto, ndipo seli hizi nyeupe ambazo hupambana na maradhi zinapozalishwa.

Huhamasisha kupunguza uzito

Kupunguza uzito? Ndiyo kupunguza uzito. Baada ya binadamu kula vyakula, kiasi fulani huhifadhiwa mwilini kama mafuta. Baadhi ya mafuta haya huyeyushwa na kutumiwa kuupasha mwili joto.

Hivyo kuogea maji ya baridi kutawezesha aina fulani ya mafuta kuyeyushwa ili kuzalisha joto mwilini, jambo ambalo litapelekea kupungua kwa uzito.

Huchangia katika afya ya misuli

Wanamichezo wanafahamu kuwa kuogea maji baridi baada ya michezo au mazoezi huwafanya wajisikie vizuri mapema. Hili ni kutokana na maji baridi kuhamasisha mzunguko wa damu ambao huiwezesha misuli kujijenga tena upya vyema.

Huondoa msongo wa mawazo

Utafiti uliofanyika kwenye chuo cha tiba Virginia, ulibaini kuwa kuogea maji baridi huzalisha kemikali ya noradrenaline ambayo husaidia kukabili msongo wa mawazo.

Hukusaidia kulala vyema

Je umeshawahi kuogea maji baridi ukiwa umechoka sana au umefanya kazi ngumu? Kama umeshawahi kuogea maji baridi ni wazi kuwa ulijisikia vizuri na ukalala vizuri pia.

Hili ni tofauti na maji ya moto kwani badala ya kukupooza na kukufanya ulale vyema yatakufanya uchemke na kuchoka zaidi.

Naamini umepata maarifa juu ya faida za kuogea maji baridi. Naamini sasa hakuna haja ya kuongeza foleni za maji jikoni wakati unaweza kuogea maji ya baridi na ukapata manufaa yaliyoelezwa hapa.

Matumizi ya kahawa kutibu presha ya kushuka au shinikizo la chini la damu

Kahawa husaidia kuongeza presha au shinikizo la damu. Unashauriwa Kunywa kikombe kimoja cha kahawa kunaweza pia kusaidia kupandisha shinikizo lako la damu kwa muda.

Kama unapatwa na kushuka kwa shinikizo la damu mara kwa mara basi kunywa kikombe cha kahawa asubuhi au unywe wakati unakula cha mchana na cha jioni.

Usizidishe matumizi ya kahawa kwakuwa kahawa ina madhara mabaya kwa afya ya mwili kwa ujumla.

Maana ya siku ya Jumatano ya Majivu

Utangulizi

Wakati umetimia na ufalme wa Mungu umekaribia, tubuni na kuiamini Injili, (Mk 1:15), haya ndiyo maneno ya kwanza ya Yesu ambayo kadri ya Mwinjili Marko yanafungua kazi ya hadhara ya Yesu, kwa maana hiyo kazi ya Yesu inaanza kwa kuwaandaa watu katika toba ili hatimaye, wapate kuukaribia au kuingia katika ufalme wa Mungu.
Na wakati ndiyo sasa. Wakati ni sasa, Yesu anatuhubiria na Kwaresima imewadia, na ndiyo maana siku ya Jumatano ya majivu, kwa kuitikia mwito wa maneno ya Yesu kanisa linatualika kuingia katika kipindi cha Kwaresma, ambacho ni kipindi cha kujikusanya, kujitayarisha, kijitengeneza na kujikarabati hasa kwa toba, kufunga, kusali na kujitoa sadaka zaidi mambo yanayorutubishwa kwa tafakari ya kina ya Neno la Mungu.

Nini maana ya Jumatano ya majivu?

Jumatano ya majivu ni mwanzo wa kipindi cha kwaresima katika kanisa, Ni mwanzo wa siku arobaini za kutafakari kwa undani fumbo kuu la upendo wa Mungu linalofunuliwa kwa kujitoa kwake na kufa msalabani, kifo cha aibu cha Msalaba ili kuichukua aibu yetu au dhambi zetu.

Kwaresma ni nini?

Kwaresma ni kipindi cha siku 40 cha kujiandaa kuadhimisha Sherehe kuu ya PASAKA yaani kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Tunajiandaa kwa Kufunga Kusali, Kutubu, na Matendo mema.
Mama kanisa anatupatia kipindi hiki ili tuweze kutafakari njia na mienendo yetu na kubadilika kama haimpendezi Mungu
Tunapofunga tunatakiwa kuzuia vilema vyetu na kuviacha kabisa, tunaomba kujaliwa moyo wa toba, tunainua mioyo yetu na tunaomba Mungu atujalie nguvu na tuzo. Haitoshi tu kukiri makosa yetu bali tunahimizwa kuungama na kutubu hayo makosa na kuwa tayari kuanza upya. Kipindi cha Kwaresima huanza tangu Jumatano ya majivu. Mwanzoni mwa kazi yake ya kuhubiri Habari njema Yesu anaanza kwa kusema tubuni na kuiamini Injili – Mk 1,15. Maneno haya haya tunayasikia/tumeyasikia kila tunapopakwa majivu. Mwaliko huu wa Yesu unatuingiza katika kipindi cha toba – tubuni na kuiamini Injili. Huu ni mwaliko wa uzima. Ni mwaliko ili tuongoke, tuanze maisha mapya, maisha ya sala, kufunga na kutoa sadaka.

Kwa nini ikaitwa Jumatano ya majivu?

Jina linatokana na desturi ya kumpaka mtu majivu kichwani pamoja na kumtamkia maneno ya kumhimiza afanye toba inavyotakiwa na kipindi hicho cha liturujia kinachoandaa Pasaka.
Kwa kawaida siku ya Jumatano ya majivu unaanza mfungo unaofuata kielelezo cha Yesu kufunga chakula siku arubaini jangwani baada ya kubatizwa na Yohane Mbatizaji na kabla ya kuanza utume wake mwenyewe.

Nini maana ya majivu tunayopaka?

Majivu ni ishara ya majuto, nayo hufanywa visakramenti kwa kubarikiwa na kanisa. Tunapopakwa majivu katika paji la uso hutusaidia kutafakari na kutukumbusha kuwa wanadamu sisi tu mavumbi na mavumbini tutarudi. Hutukumbusha zaidi kuwa maisha ya hapa duniani tunapita na safari yetu itakamilika pale tutakapoungana na Bwana na mwokozi wetu katika ufalme wako.
Angalia; Isaya 61:3, Ester 4:1-3, Yeremia 6:26, Ezekieli 27:30, Mathayo 11:21 na Luka 10:13.

Kwa nini majivu yanapakwa kwenye paji la uso na si vinginevyo?

Ishara yoyote iwekwayo katika paji la uso huonesha umiliki (soma Ufunuo 7:3, Ufunuo 9:4, Ufunuo 14:1, Ezekieli 9:4-6, ). Tunapochorwa ishara ya msalaba katika paji la uso ni ishara kwamba sisi tupo chini yake yeye aliyekufa msalabani kwa ajili yetu.
Hali kadhalika hutukumbusha ishara ya msalaba tuliyochorwa na mafuta matakatifu siku ya ubatizo wetu, hutukumbusha ahadi tuliyoiweka siku hiyo ya ubatizo na kutuita tuishi maisha ya utakatifu

Padri hutamka maneno gani wakati anapaka majivu?

Tunapopakwa majivu Padre husema; Mwanadamu kumbuka u mavumbi na mavumbini utarudi AU Tubuni na kuiamini Injili.

Maneno anayosema padre yana maana gani?

Maneno haya kwa upande mmoja hutukumbusha tunapoelekea, tusisikitike kwamba siku moja tutarudi mavumbini bali tuwe na furaha kwani wakati miili yetu unarudi mavumbini roho zetu zitakwenda kuungana na Mungu Baba mbinguni.
Hivyo maandalizi tunayoalikwa kuyafanaya si maandalizi ya kuelekea mavumbini bali maandalizi ya kuelekeza roho zetu mbinguni. Ndio maana pia twaambiwa tubuni na kuiamini Injili.

Majivu tunayopakwa yanatoka wapi?

Majivu tunayopakwa hutoka katika matawi yaliyotumika katika jumapili ya matawi ya mwaka jana. Majivu haya hubarikiwa na kuwa visakramenti. Hivyo majivu yanapoashiria toba na majuto pia hutukumbusha wema wa Mungu na utayari wake wa kutusamehe.

Kwa nini unatumia matawi ya Jumapili ya Matawi?

Matawi haya yalimkaribisha Yesu Yerusalemu akiwa tayari kufa kwa ajili ya dhambi zetu, yalimpokea mfalme kwa furaha na shangwe kuu. Matawi haya yanapochomwa na sisi kupakwa majivu yetu yanatukumbusha kuwa ni kwa ajili ya dhambi zetu Mungu alimtoa mwanae wa pekee kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu sisi wanaadamu. Hivyo hututafakarisha kuacha dhambi.

Kanisa limekataza nini siku ya Jumatano ya majivu?

Tumekatazwa kula chakula siku ya Jumatano ya Majivu na kula nyama siku ya Ijumaa Kuu katika Amri ya Pili ya Kanisa.

Nani analazima kufunga siku ya Jumatano ya majivu na Kwaresma?

Kila Mkristo aliyetimiza miaka 14 na zaidi anapaswa kufunga kula nyama (Ijumaa kuu) na mwenye miaka zaidi ya 21 kufunga chakula Jumatano ya Majivu

Tunaposema kujinyima wakati wa Kwaresma tunamaana gani?

Kujinyima ni kujikatalia kitu ukipendacho mfano nyama, pombe, sigara, muziki, safari, maongezi n.k.

Mwisho

Wakati wa Kwaresma Waamini wanapaswa kujitakasa zaidi kwa kusali, kufunga, toba na matendo mema
Kipindi cha Kwaresima ni fursa makini ya kumkimbilia Mwenyezi Mungu, kwani kwa njia ya dhambi wamejikuta wakiwa mbali na Uso wa huruma ya Mungu, kiasi hata cha kupoteza imani na matumaini kwa Mwenyezi Mungu. Hii ni changamoto ya kumpenda Mungu na jirani badala ya kukumbatia malimwengu yanayoendelea kuwatumbukiza katika utupu wa maisha ya kiroho. Kwaresima ni kipindi cha waamini kukimbilia na kuambata huruma ya Mungu inayoganga na kuponya dhambi. Ni wakati wa sala, upendo na kufunga.

Jinsi ya kupika Eggchop

Mahitaji

Mayai yaliochemshwa 4
Nyama ya kusaga robo kilo
Kitunguu swaum
Tangawizi
Limao
Chumvi
Pilipili
Breadcrambs
Carry powder
Binzari nyembamba ya unga
Yai moja bichi
Mafuta

Matayarisho

Marinate nyama na pilipili, kitunguu swaum, tangawizi, limao, chumvi, carry powder, binzari nyembamba na breadcrambs pamoja. Kisha vunja yai moja bichi kwenye kibakuli na ulikoroge kisha tia kwenye mchanganyiko wa nyama.Gawanisha matonge manne kwa ajili ya kuzungushia kwenye mayai .Chemsha mayai kwa muda wa dakika 20. Yakisha iva acha yapoe na kisha yamenye maganda na uyaweke pembeni. Baada ya hapo chukua yai moja lililochemshwa na ulizungushie donge moja la mchanganyiko wa nyama. fanya hivyo kwa mayai yote yaliobakia. Baada ya hapo paka mafuta kwa nje ya hizo eggchop na kisha paka mafuta kwenye sinia la kuokea na uziokee kwenye oven kwa moto wa kawaida, kwa muda wa dakika 20.Na eggchop zako zitakuwa tayari kwa kuliwa

Namna nzuri ya kuhudumia nywele zako za asili kirahisi

Kwa wale ambao tuna nywele asilia (natural hair), tayari tunafahamu changamoto kadhaa tunazokumbana nazo. Kwa wale mnaofikiria kuanza kuwa na nywele asilia, karibuni sana tuendelee kujuzana namna ya kutunza nywele zetu kama tulivyopewa na Mungu.

Katika mada ya leo, nitakwenda kuzungumzia vitu vya kuzingatia ili kuikuza nywele yako asilia kwa haraka zaidi. Je,unazifahamu nywele zako vizuri?Una nywele za aina gani? Zina tabia gani? Zinataka nini?

Zifuatazo ndizo njia ya kuzihudumia nywele zako;

1. Kuzikubali kama zilivyo na kuzipenda.

Utasikia ..hiki kipilipili changu ni steelwire ya kimataifa, ..hakitikisiki hata upepo wa dunia yote ungevumia pande hizi. Mwingine oh..nywele zangu kama miti ya mibuyu kichwani…hazishikiki.T atizo ni kwamba hamjafahamiana vizuri yani wewe na nywele zako. Hata mimi niligombana nazo sana huko nyuma kabla ya kuzielewa vizuri. Jenga mahusiano mazuri tu na nywele zako,zielewe,ukifikia hapo utaanza kuzipatia hata hazitakusumbua.

2. Usafi wa ngozi ya nywele na nywele zenyewe.

Nywele zenye afya huanzia kwenye ngozi safi ya nywele.Nafahamu unataka nywele zako zisidumae kwa hiyo zioshe vizuri.Wakati uliopita nilizungumzia kuziosha kwa product zilizo rafiki( ‘friendly’) .Ngozi safi ya nywele itasababisha nywele kupata njia ya kujitokeza nje kwa urahisi.Unapoziacha chafu,ule uchafu unaziba matundu ya nywele zako na kuzuia njia,kama ambavyo matundu ya uso yakiziba unapata machunusi maana uchafu unajaa basi kwa nywele hazitakua vizuri.

3. Linda unyevu wa nywele zako

Kila mtu akisikia kiu hunywa maji.Nywele zako zinahitaji kulindwa zisisikie kiu.Unapoziosha,yale mafuta asilia ya kuzilinda huondoka na uchafu.Nywele inabaki ikiwa na udhaifu fulani maana haiwezi hata kushikilia hayo maji yaliyopo vizuri,na zikikauka zinakua kavu sana.Ni vizuri kabla hazijakauka vizuri,ukazi-’condition’.Kwa nywele ambazo ni nyepesi na chache,pia kuna product za kuzisaidia ziweze kutunza vizuri unyevu na hivyo kuwa na afya nzuri.

4. Zifahamu nywele zako

Yani hapa ndo shule ilipolalia kabisaa maana ukizijua tu basi utazihudumia kwa usahihi. Unatakiwa kuangalia namna gani nywele zako zinanyonya unyevu .Unajuaje?

Chukua kikombe,kijaze maji safi.Ukipata glass itakuwa vizuri zaidi.

Chomoa unywele mmoja kichwani,hakikisha unatoka na kale kamzizi kake keupe keupe hivi.

Tumbukiza unywele wako kwenye glass yako ya maji hakikisha imeingia yote.Kama ikizama hapo hapo na hainyanyuki tena,basi nywele zako zinanyonya unyevu kwa haraka kabisa.Kama inachukua muda kuzama,au haizami kabisa,nywele zako zinanyonya unyevu taratibu au zinanyonya kwa shida.

(Wala usihofu,zipo namna ya kuzifanya zinyonye unyevu kwa haraka,tutajuzana.)Ni kwamba ‘cuticle’ zake zimefunga haswa,ndio maana unyevu au maji haviingii kwa haraka.

Kwa hiyo ukifanya ‘deep conditioner’ kwa kutumia joto kama la drier lakini uwe moto mdogo sana au ufanye ‘hot oil treatment’ itakusaidia ‘cuticle’kufunguka na unyevu kupita.

Mbadala,unaweza baada ya kuosha suuza na maji ya vuguvugu halafu weka mafuta ya kimiminika.Inasaidia sana.

Mimi nina aina gani?..Nina nywele zinazonyonya unyevu haraka.

5. Mafuta ya Kupaka kichwani.

Ni ya muhimu mnoo!.Nimefanya utafiti wa kina nimeona mafuta ya nazi yanaweka afya nzuri kwa nywele aina nyingi hivyo na mimi nikaanza kuyatumia. Kwangu mimi,mafuta ya nazi ya kutengeneza mwenyewe yamenikubali sana. Japo huwa nanunua pia mafuta kama ya olive(extra virgin) na ya tea tree.

6. Kuzichambua vizuri kabla ya kuchana.

Uwe mkarimu na mwenye subira kwa nywele zako. Mimi zikijifunga huwa nazichambua kwa mikono taratibu wakati mwingine nazilowesha na maji kwa mbali halafu nachana kwa chanuo lenye mapana sio ambalo reli zake zimebanana. sio kitana. Chanuo kubwa(wide toothed comb).

7. Usizisumbue mara kwa mara na usuke mitindo ya kuzitunza zikue.

Kama unataka zikue haraka, usizisumbue sana. Unaweza ukasuka mitindo mizuri tu ukakaa nazo wiki nzima au kadri zitakavyodumu. Au upunguze kuzichana mara kwa mara lakini utafute siku kama wikiendi ukae uzichambue taratibu na vidole kuondoa mafundo. Kuchana mara kwa mara zinapukutika,zinaanguka. Zitakua lakini sio kwa kasi ya kama ukizisuka ukaziacha kwa muda.

8. Punguza matumizi ya vitu vya moto kwenye nywele zako kama pasi ya nywele na vingine vya hivyo.

Mimi dryer la nywele situmii zaidi ya mara mbili kwa mwezi. Mara nyingi naziacha zikauke na hewa hata kama nimezifunga rollers natoa kesho baada ya masaa 24

Jinsi ya kutengeneza Rock-cakes Za Njugu Na Matunda Makavu

Mahitaji

Unga – 4 Vikombe

Sukari -10 Ounce

Siagi – 10 Ounce

Mdalasini ya unga – 2 vijiko vya chai

Matunda makavu/njugu (kama lozi, Zabibu, maganda ya chungwa, Cherries na kadhalika – 4 ounce

Maziwa ya maji – 4 Vijiko vya supu

Maandalizi

Chukua siagi na sukari koroga na mixer mpaka iwe kama cream.
Tia vanilla mdalasini, tia yai moja mix tena endelea kuongeza yai lingine mpaka umalize yote, changanya mpaka iwe laini kama sufi (fluffy)
Tia unga na baking powder na dried fruits, changanya na mwiko.
Chota mchanganyiko na kijiko cha soup weka kwenye treya ya kupikia tandaza na uma ili upate matundu juu ya biskuti.
Pika (bake) kwenye oven lenye moto wa 375 F. kwa muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.

Chanzo, dalili, aina na matibabu ya ugonjwa wa kifafa

Huu ni ugonjwa ambao unasabababishwa na seli zilizopo katika mishipa ya fahamu zilizopo kwenye ubongo kutoa umeme[impulses] mwingi kuliko kawaida kwenda kwenye misuli na sehemu zingine za mwili, na kusababisha mtu kupata dalili kama vile kuishiwa nguvu, kichwa kuuma, kuchanganyikiwa, mwili kukakamaa na hata kupoteza fahamu. Hali hii hujirudia mara kwa mara.

Ifahamike kuwa, aina ya kifafa inayojulikana sana mitaani ni ile ambayo mtu anakakamaa na kupoteza fahamu, japokuwa kuna aina za kifafa ambazo mtu hakakamai wala kupoteza fahamu, kama tutakavyoona hapo baadae.

Mwaka 2013 ugonjwa huu uliua zaidi ya watu laki moja duniani, 80% wakiwa waafrika.

Mgonjwa huyu huweza kuanguka mara kadhaa kwa mwezi lakini anaweza asianguke kabisa kama anafuata masharti na utaratibu mzuri wa matibabu…

Chanzo cha ugonjwa wa kifafa ni nini?

Chanzo kikuu cha ugonjwa huu kwa watu wengi hua hakifahamiki lakini baadhi ya hiz ni moja ya sababu za kuugua kifafa.

Kurithi; familia na koo zingine zinakua na ugonjwa huu hivyo watoto na wajukuu huzaliwa tayari na ugonjwa huu.

Kuumia kichwa: ajali zinazohusisha kuumia kwa kichwa huweza kusababisha kuumia kwa mishipa ya fahamu na mtu kuugua kifafa.

Magonjwa mengine; kuna magonjwa mtu akiugua maishani mwake baadae huweza kupata kifafa kwasababu magonjwa hayo yanavyoharibu mfumo wa ubongo.. mfano homa ya uti wa mgongo kitaalamu kama meningitis.

Uvimbe kwenye ubongo: matatizo ya uvimbe kwenye ubongo kama kansa huweza kusababisha mtu kuugua kifafa.

Kiharusi; huu ni ugonjwa ambao husababishwa na damu kushindwa kupita vizuri kwenye ubongo au kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo hali hii husababisha mtu kupooza nusu ya mwili wake na huweza kuugua kifafa baadae.

Matatizo wakati wa kuzaliwa: wakati mwingine mtoto huzaliwa kwa shida sana kwa njia ya kawaida kiasi kwamba kichwa chake hubanwa sana wakati wa kupita na hali hii huweza kumsababishia kifafa kwanzia utotoni.

Matatizo ya utengenezaji wa mtoto tumboni; wakati mwingine ile miezi mitatu ya kwanza ambayo mtoto ndio anapata viungo tumboni huweza kutokea kasoro kwenye mfumo wa fahamu za kwenye ubongo na kumfanya apate kifafa akizaliwa.

Magonjwa ya uzee yanayoathiri ubongo; kuna magonjwa huharibu ubongo wakati wa uzee na magonjwa haya huweza kusababisha kifafa kipindi hicho.

Aina za kifafa

Kuna aina mbili kubwa za kifafa:

1)Primary marygeneralized seizures

Hii ndio aina ya kifafa ambayo inafahamika sana mitaani; na inahusisha mgonjwa kukamaa, na kupoteza fahamu, pamoja na dalili zingine kama vile kutoa povu mdomoni, na kujisaidia haja kubwa na/au ndogo bila kujitambua akishikwa na hali hiyo.

Pia wengine hupatwa kama na wazimu au kuchanganyikiwa kwa muda kabla au baada ya kushikwa na hali hiyo.

2)Partial seizures

Aina hii ya kifafa ni ile ambayo haihusishi muhusika kupoteza fahamu na kukakamaa!! Bali hushikwa na hali fulani kama ya bumbuwazi kwa dakika kadhaa; Wengine huwa na dalili zisizoeleweka za mara kwa mara kama vile kusihiwa nguvu, kizungu zungu, kichwa kuuma sana (bila sababu ya kiafya inayojulikana), na kadhalika. Aina hizi za kifafa ziko nyingi, na dalili hutofautiana kwa kadri ya aina ya kifafa!!

Vipimo vinavyofanyika kugundua kifafa

Ugonjwa huu unaweza kutambulika kwa daktari kuchukua historia ya dalili zinazomkabili muhusika tu(hakuna kipimo ambacho kinaweza kutambua kifafa kwa asilimia 100); Kuna kipimo kinachopima jinsi ubongo unavyotoa taarifa za umeme (ELECTROENCEPHALOGRAM-EEG), ambacho kinaweza kutambua kifafa, lakini kipimo hiki kinaweza kikaonekana kuwa hakina shida, na bado mtu akawa na tatizo hilo la kifafa. Hivyo basi, kifafa ni moja kati ya magonjwa machache ambayo kutambulika kwake kunategemea sana ujuzi na utaalamu wa daktari katika kuunganisha dalili za mgonjwa kuliko vipimo!!

Hata hivyo, mara nyingi nyingi mgonjwa hupimwa vipimo tofauti ili kuweza kujua chanzo cha ugonjwa… mfano

• Uwezo wa kufanya kazi figo

• Uwezo wa kufanya kazi maini

• Kupima maji ya uti wa mgongo

• Kupima Kaswende

• Picha ya ubongo mfano CT SCAN.

Mambo yanayofanya kupata degedege za kifafa mara kwa mara..

• Kukosa usingizi kwa muda mrefu

• Mianga na miale ya disko

• Unywaji wa pombe

• Kuishiwa sukari mwilini wakati wa akisikia njaa kali.

• Kutomeza dawa kama ilivyoelekezwa

Huduma

Matibabu yasiyo ya dawa wakati mgonjwa amekamatwa na kifafa:{non pharmacological treatment}yaani HUDUMA YA KWANZA

• Mzuie mgonjwa asijiumize kwa kuweka kitu laini chini ya kichwa chake, ondoa vitu vikali karibu yake kama kisu, sindano au vyuma.

• Usilazimishe kitu chochote kwenye mdomo wa mgonjwa.

• Usimshike kuzuia mizunguko yake

• Weka kichwa alale anaangalia upande mmoja ili kutoa mate mdomoni.

• Kaa na mgonjwa mpaka degedege ziishe

• Usiweke chochote mdomoni kwa mgonjwa kama dawa au chakula mpaka apate fahamu zake.

Mtu mwenye kifafa hali hii ya kukamatwa na degedege za kifafa sio ya ajabu sana ila ukiona dalili hizi mkimbize hospitali..

• Degedege za kifafa zaidi ya dakika kumi

• Kutapika sana

• Kushindwa kuona vizuri

• Kupoteza fahamu

• Kichwa kuuma sana.

MATIBABU YA UGONJWA

Kama kawaida chanzo cha ugonjwa kikipatikana mgonjwa huanzishiwa matibabu lakini kama mgonjwa alikua tayari ameshapata madhara kwenye ubongo kulingana na chanzo husika ataendelea kua na kifafa.

Ugonjwa wa kifafa hauponi kabisa kwa 100% hospitali, ukishaambiwa una kifafa au mgonjwa wako ana kifafa basi utapewa utaratibu wa matibabu yaani kumeza dawa siku zote za maisha yako na kufuata baadhi ya masharti na utaishi maisha ya kawaida kabisa.

Mkalimani alivyoharibu ibada ya leo

Leo nikaamua niingie misa ya asubuhi kwenye kanisa moja la kilokole kulikua na ugeni wa mchungaji kutoka Bulgaria, Mahubiri yameanza saa 1 asubuhi hali ikawa kama hivi:

MCHUNGAJI: My name is Pastor Livingstone
MKALIMANi: Kwa jina naitwa mchungaji Jiwe linaloishi
MCHUNGAJI: We thank God for All goals we set by our hands
MKALIMANI: Tunamshukuru Mungu kwa Magoli yote tuliyoweka kwa Mkono

Hivi navyoongea kanisa halina viti waumini wote tumekimbia nje naona Mkalimani amebaki na kiatu cha kushoto tu.
Sunday joke

Mapishi ya Wali, mchicha wa nazi na nyama ya kukaanga

Mahitaji

Mchele (rice 1/2 kilo)
Mchicha uliokatwakatwa (spinach mafungu 2)
Nyama (beef 1/2 ya kilo)
Nyanya (tin tomato 1/2 ya tin)
Nyanya chungu ( garden egg 3)
Kitunguu swaum (garlic cloves 3)
Tangawizi (ginger)
Curry powder
Vitunguu (onion 2)
Limao (lemon 1)
Chumvi
Pilipili (scotch bonnet pepper )
Tui la nazi (coconut milk 1 kikombe cha chai)

Matayarisho

Kaanga kitunguu kikishaiva tia nyanya na chumvi. kaanga mpaka nyanya ziive kisha tia nyanya chungu,curry powder na pilipili 1 nzima, baada ya hapo tia mchicha na uuchanganye vizuri kwa kuugeuzageuza. Mchicha ukishanywea tia tui la nazi na uache lichemke mpaka liive na hapo mchicha utakuwa tayari.
Safisha nyama kisha iweke kwenye sufuria na utie chumvi, tangawizi, limao na kitunguu swaum. Ichemshe mpaka itakapoiva na kuwa laini. Baada ya hapo weka sufuria jikoni na mafuta kidogo yakisha pata moto tia vitunguu na nyama na uvikaange pamoja, kisha tia curry powder na ukaange mpaka nyama na viunguu vya brown. na hapo nyama itakuwa imeiva. Malizia kwa kupika wali kwa kuchemsha maji kisha tia mafuta, chumvi na mchele na upike mpaka uive. Baada ya hapo chakula kitakuwa tayari kwa kuseviwa.

Maswali na Majibu kuhusu Biblia

Neno Bwana lina maana gani katika Biblia?
Neno Bwana Katika Biblia linamaanisha “Mungu Mtawala”

Mapokeo ya Mitume ndiyo nini?
Mapokeo ya Mitume ndiyo yale yote ambayo Yesu aliwakabidhi Mitume wake, na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu yatadumu hata mwisho wa dunia katika mafundisho, liturujia na maisha ya Kanisa.
“Nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vilevile kama nilivyowatolea… Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe” (1Kor 11:2; 15:3).
“Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu… Mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine” (2Tim 1:14; 2:2).
Tukikata huo mnyororo wa mapokeo, hata kama ni kwa kisingizio cha kushikilia Biblia, tunaachana na asili ya Kanisa.
“Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu… Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu” (2Thes 2:15; 3:6).

Maandiko Matakatifu ndiyo nini?
Maandiko Matakatifu ndiyo vitabu vyote 73 ambavyo viliandikwa na watu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu vikakusanywa na Kanisa kwa jina la “Biblia”, yaani “Vitabu”.
Hao “wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu” (2Pet 1:21).

Je, Biblia zote ni sawa?
Hapana, Biblia zote si sawa. Tujihadhari na matoleo mapungufu ambamo vimenyofolewa vitabu 7 vizima na sehemu kadhaa za vitabu vingine vilivyotumiwa na Wakristo wa kwanza.
“Amin, nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie” (Math 5:18). “Na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki” (Ufu 22:19).
Je wakristo Wakatoliki wanasoma Biblia kwenye Ibada ya Misa? Biblia inanukuliwa mara ngapi Kwenye Ibada ya misa ya Wakatoliki?
Ndiyo, Wakatoliki wanasoma Biblia kila siku wanapoadhimisha Ibada ya Misa wakati wa Liturujia ya Neno.
Wakatoliki wananukuu Biblia mara Tano kwenye Ibada ya Misa. Wananukuu wanaposoma somo la Kwanzaa, Somo la pili, wimbo wa katikati, Shangilio na Injili.

Tunatambuaje Maandiko Matakatifu kati ya maandishi yote ya binadamu?
Tunatambua Maandiko Matakatifu kati ya maandishi yote ya binadamu kwa njia ya Mapokeo, yaani kwa sababu yametumiwa na Kanisa tangu mwanzo kwa kulisha kwa hakika imani yake.
Tunahitaji Mapokeo kwa kuwa Maandiko yenyewe hayataji orodha ya vitabu vyake vyote, Sanasana Yesu alividokeza baadhi akisema yanamzungumzia na kutimia ndani yake,
“Ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii, na Zaburi” (Lk 24:44).
Halafu Barua ya Pili ya Mtume Petro ikalinganisha “na Maandiko mengine” nyaraka zote ambazo Paulo aliziandika “kwa hekima aliyopewa” (2Pet 3:15-16).

Sababu nyingine za Biblia kutojitosheleza ni zipi?
Sababu nyingine za Biblia kutojitosheleza ni kwamba mambo mengi muhimu hayakuandikwa,
“Kuna mambo mengine mengi aliyoyafanya Yesu, ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa” (Yoh 21:25).
Tena barua ni nusu tu ya kuonana; hivyo Yesu hakuandika lolote, nao Mitume hawakupenda kuandika yote.
“Kwa kuwa ninayo mambo mengi, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini nataraji kuja kwenu, na kusema nanyi mdomo kwa mdomo, ili furaha yetu iwe imetimizwa” (2Yoh 12).
“Nalikuwa na mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa wino na kalamu. Lakini nataraji kukuona karibu, nasi tutasema mdomo kwa mdomo” (3Yoh 13-14).
Hasa ibada haziwezi kufanyika kwa barua; k.mf. kuwekea mikono ili kumshirikisha Roho Mtakatifu. Paji la namna hiyo halipitii Maandiko, bali Mapokeo tu. Hatimaye Biblia ikipotoshwa haipingi, kwa kuwa si mtu hai anayeweza kujitetea.

Biblia iliandikwa kwa kusudi gani?
Biblia iliandikwa kusudi tupate “kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini” tuwe “na uzima wa milele” (Yoh 20:31).
“Tangu utoto umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. Kila Andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki” (2Tim 3:15-16).
Si lengo lake kutufundisha historia, jiografia wala sayansi: kuhusu elimu hizo na kuhusu ufasaha wa lugha Biblia ilitegemea ujuzi na vipawa vya watu walioiandika.

Je, vitabu vya Biblia vinatofautiana?
Ndiyo, vitabu vya Biblia vinatofautiana kwa kuwa Mungu alijifunua hatua kwa hatua; hivyo vitabu 46 vilivyoandikwa kabla ya Yesu vinaitwa Agano la Kale na 27 vilivyomfuata vinaitwa Agano Jipya.
“Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka” (Eb 8:13).
Mungu “ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha” (2Kor 3:6).

Je, vitabu vyote vya Biblia vinahusiana?
Ndiyo, vitabu vyote vya Biblia vinahusiana kwa kuwa vinaangaziana na kuunda kitabu kimoja ambacho ni Neno la Mungu yuleyule, ingawa katika hatua tofauti: Agano la Kale ndiyo maandalizi na Agano Jipya ndio utimilifu wake.
Yesu alisema, “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua Torati au Manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza” (Math 5:17).
Tunahitaji Agano la Kale ili tuelewe vizuri Agano Jipya katika maandalizi yake, na tunahitaji Agano Jipya ili tuelewe Agano la Kale lilivyotimilizwa na Yesu.

Je, inafaa tushike neno lolote la Agano la Kale kama Wayahudi?
Hapana, haifai tushike neno lolote la Agano la Kale kama Wayahudi wasiozingatia jinsi Yesu alivyolitimiliza kwa maneno na matendo hata wakamshutumu kutenda kinyume:
“Mtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato” (Yoh 9:16).
Alipofafanua amri 10 za Mungu alikariri:
“Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa… lakini mimi nawaambieni…” (Math 5:21,27,31,33,38,43).
Alipouliziwa unajisi wa vyakula kadhaa, alisisitiza,
“’Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi; kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni?’ Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote” (Mk 7:18- 19).
“Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo” (Kol 2:16-17).
Hakika, mwili ni mzito kuliko kivuli chake.
Vile vile katika Warumi 4:16. Tunasoma “Kwa sababu hiyo, jambo hili lategemea imani, hivyo kwamba ahadi hiyo yatokana na neema ya Mungu, na kwamba ni hakika kuwa ahadi hiyo ni kwa ajili ya wote:si kwa wale tu wanaoishika sheria, bali kwa wale waishio kwa Imani kama Abrahamu. Yeye ni Baba yetu sote.”
Wakristo wengine wanachanganywa na wale wasioyajua maandiko na kuwataka washike sheria na Torati,basi tukisema ni lazima kushika sheria tutakua tunakataa kua Abrahamu hakuwa mtu wa Mungu maana kwa Abrahamu hatukuwa na Sheria wala Torati na alipata kibali machoni Pa Mungu tuu kwa Imani. Kumbuka pia Abrahamu alitahiriwa baada ya Kuwa tayari mtu wa Mungu kwa Imani yake na sio kwamba Kutahiriwa ndio kulifanya mtu wa Mungu.
Tumekombolewa kwa Imani na sio kwa Sheria. Wagalatia 5:18 “Lakini Mkiongozwa na Roho hampo chini ya sheria”
Hatumtumikii Mungu ili tuwe watu wa Mungu bali tukishakua watu wa Mungu ndio tunamtumikia Mungu.

Yesu alitimiliza Agano la Kale kwa namna isiyotarajiwa hasa lini?
Yesu alitimiliza Agano la Kale kwa namna isiyotarajiwa hasa aliposulubiwa, akionekana na Wayahudi wenzake kama kwamba amelaaniwa:
“Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa: ‘Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti’; ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani” (Gal 3:13-14).

Kati ya vitabu vya Biblia, vilivyo bora ni vipi?
Kati ya vitabu vya Biblia, vilivyo bora ni Injili 4 zilizoandikwa na Mathayo, Marko, Luka na Yohane.
Ndio moyo wa Maandiko Matakatifu yote, kwa kuwa ndizo shuhuda kuu juu ya maisha na mafundisho ya Yesu.
Yeye “amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora. Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili” (Eb 8:6-7).

Tueleweje Maandiko Matakatifu?
Tuelewe Maandiko Matakatifu kwa kuzingatia hasa Mungu alitaka kusema nini kuhusu wokovu wetu kupitia waandishi wengi aliowaongoza kuyatunga kwa lugha na mitindo mbalimbali.
Lakini ebu, “Yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na Maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe” (2Pet 3:16).
Utitiri wa madhehebu yanayoshindana yakidai kushikilia Biblia tu unathibitisha uwekezano mkubwa wa kuipotosha kwa namna moja au nyingine.
“Utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia walimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo” (2Tim 4:3-4).
Njia pekee ya kukwepa fujo hiyo ni kuelewa Maandiko ndani ya Kanisa, kadiri ya Mapokeo yake hai.
“Lakini mtu yeyote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu” (1Kor 11:16).
Biblia nje ya Kanisa ni kama samaki nje ya maji.

Tupokeeje ufunuo wa Mungu?
Tupokee ufunuo wa Mungu kwa kusadiki mafundisho ya Kanisa lake, ili tuzidi kumjua na kuambatana naye bila ya kudanganyika. Yesu aliwaambia Mitume wake,
“Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma” (Lk 10:16).
“Sisi nasi twamsukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kwelikweli, litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini” (1Thes 2:13).

Neno “BIBLIA” maana yake ni nini?
Neno “BIBLIA” ni neno linalotokana na neno la Kigiriki “Biblion” lenye maana ya vitabu.
Biblia ni Mkusanyiko wa vitabu mbalimbali vya dini vilivyochaguliwa na kuidhinishwa kua vyafaa kutumika.

Biblia ni nini? Asili, Historia, waandishi na mipaka yake
Biblia ni mkusanyiko wa vitabu mbalimbali vinavyohusu kazi ya Mungu ya kuwakomboa mwanadamu kuanzia enzi za Mababu na manabii Wa Waisraeli, Enzi za Yesu na za Mitume wa Yesu.
Je, Biblia ilipatikanaje? Nini chanzo na asili ya Biblia.
Biblia iliundwa kwa kukusanya vitabu vya dini vya wakristo hapo awali na kuunda kitabu kimoja. Kwa maana hii, Biblia ni vitabu teule vya dini vilivyoonekana vinafaa kutumika kwa waumini Wakristo ili kusaidia Imani yao. Hivyo basi, kama Biblia ni vitabu teule tuu vipo vitabu vingine vya dini ambavyo havikuwekwa Kwenye Biblia.
Wakristo wa kwanza walichagua vitabu kadhaa na kuviweka pamoja na kisha kuvita Biblia. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu muhimu tuu vya dini mpaka kufikia Enzi za Mitume.
Je, Biblia ndicho kitabu pekee cha neno la Mungu?
Hapana, Biblia sio kitabu pekee cha neno la Mungu isipokua Biblia ni kitabu kilichoidhinishwa rasmi kutumika Kama kitabu kikuu cha Wakristo. Hii ni kwa sababu Biblia imeundwa na vitabu muhimu tuu vilivyochaguliwa na wakristo wa kwanza vilivyoonekana vinafaa kwa kufundishia, Ibada na kukuza Imani. Kwa hiyo basi vipo vitabu vingine ambavyo haikuwekwa Kwenye Biblia ambavyo ni Maneno ya Mungu.
Hii ndiyo sababu kwa nini Wakatoliki wana vitabu vingi kuliko madhehebu Mengine. Yaani sababu ni kwamba madhehebu Mengine walivitoa vitabu vingine vilivyounda Biblia. Na Wakatoliki waliweka vitabu vingine vya dini Kwenye Biblia walivyoona vinafaa pia kutumika.
Je nje ya Biblia hakuna Neno la Mungu au Maandiko matakatifu?
Nje ya Biblia kuna Neno la Mungu na Maandiko Matakatifu. Hii Inamaanisha kuwa Biblia sio kitabu pekee cha neno la Mungu. Zipo nyaraka na Vipo vitabu vingine vingi ambavyo viliandikwa na Manabii na Mitume ambavyo havikuwekwa kwenye Biblia lakini ni mafundisho ya Mungu. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vikuu vya Mungu.
Kumbuka kuwa sio nyaraka zote za Mitume ziliandikwa Kwenye Biblia. Vile vile manabii walikuwa ni wengi kuliko waliowekwa Kwenye Biblia.
Je Biblia ndiyo mafundisho ya Mungu pekee?
Hapana, Biblia sio mafundisho pekee ya Mungu. Hii ni kwa sababu sio mambo yote aliyofanya na kusema Mungu yaliandikwa na vilevile Mitume hawakua watu wa Mwisho kupokea Roho mtakatifu na kupokea neno la Mungu.
Biblia inatuthibitishia yenyewe kuwa haijakamilika na Si mambo yote yameandikwa Kwenye Biblia
Biblia inatuthibitishia kuwa haijakamilika tunaposoma (Yohane 21:25)
Biblia inatuambia hivi…”Kuna mambo Mengine mengi aliyofanya Yesu, ambayo Kama yangeandikwa yote, moja baada ya jingine, nadhani hata ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.”…Kwa mstari huu Biblia inatuthibitishia kuwa haikuandikwa vitu vyote.
Je Biblia ni mwisho wa Maandiko ya Mungu?
Biblia sio mwisho wa Maandiko ya Kimungu.
Biblia ni sehemu ya maneno ya Mungu mpaka miaka ya Mitume
Hata sasa Mungu anafanya kazi na watu wake kupitia Roho Mtakatifu na kwa kwa sababu hii Biblia sio mwisho wa kazi ya Mungu ya kusema na watu wake.
Mungu yu hai na anafanya kazi na watu wake mpaka sasa kwa kutumia vinywa vya watu Kama aliyofanya hapo awali.
Hata maneno unayohubiriwa sasa yanaweza kuwa ni kutoka kwa Mungu kwa maana hata waandishi wa Biblia walitumiwa na Mungu Kama wahubiri wa sasa. Mungu ni yule yule, Roho Mtakatifu ni yuleyule na Neno ni lile lile.
Kwa hiyo Biblia ni maneno yaliyochaguliwa mpaka enzi za Mitume. Vitabu vilivyofwata Baada ya Mitume japokuwa viliandikwa kwa Roho Mtakatifu havikuwekwa Kwenye Biblia.
Sababu ya Kanisa katoliki kutumia mapokeo na Maandiko ya Watakatifu
Kanisa katoliki linatumia mapokeo na Makala za watakatifu kwa Imani kuwa Mungu yule yule aliyefanya kazi tangu zamani anafanya kazi na watu wake mpaka sasa na hivyo Maandiko ya watu wa Mungu yanafaa kutumika kama yalivyotumika ya watu wa kale.
Yesu alituambia nini kuhusu Neno la Mungu na Mwendelezo wa kazi ya Mungu ya kusema na watu?
Yesu alituambia hivi katika (Yohane 16:12-15)..”Ninayo mengi ya kuwaambieni Ila kwa sasa hamuwezi kuyastahimili. Lakini atakapokuja huyo Roho wa Ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote. Maana hatasema kwa Mamlaka yake mwenyewe bali atasema atakayoyasikia na kuwajulisheni yatakayokuja. Yeye atanitukuza Mimi kwa kuwa atawajulisheni Yale atakayoyapata kutoka kwangu “…
Sasa basi,kama Roho Mtakatifu ni yuleyule na kazi zake ni Zile Zile za tangu Mitume, kwa nini hatukubali kuwa Anafanya kazi mpaka sasa kupitia watu wa Mungu? Kwa nini tunakataa mafundisho yao? Kwa nini tunashindwa kuelewa kuwa Biblia haikuwa mwisho wa Neno la Mungu? Kwa nini tunakana Mapokeo ya Watakatifu? Kwa nini hatuwaamini watumishi wake wa sasa?

Biblia ina sehemu kuu ngapi?
Biblia ina sehemu kuu 2 (mbili) ambazo ni
1. Agano la Kale (A.K)
2. Agano Jipya (A.J)

Agano la Kale lina vitabu vingapi?
Agano la Kale lina vitabu 46

Agano Jipya lina vitabu vingapi?
Agano Jipya lina vitabu 27

Biblia nzima ina vitabu vingapi?
Biblia nzima ina vitabu 73

Vitabu vya Agano la Kale vimegawanywa katika sehemu ngapi?
Vitabu vya Agano la Kale vimegawanywa katika sehemu 4 nazo ni
1. Vitabu vya Musa (5)
2. Vitabu vya Historia (16)
3. Vitabu vya Hekima (7)
4. Vitabu vya Manabii (18)

Vitabu vya Agano Jipya Vimegawanywa katika sehemu ngapi?
Vitabu vya Agano Jipya Vimegawanywa katika sehemu 4 nazo ni
1. Injili (4)
2. Kitabu cha Matendo ya Mitume
3. Nyaraka mbalimbali (21)
4. Kitabu cha Ufunuo

Vitabu vya Musa ni vipi?
Vitabu vya Musa ni
1. Mwanzo
2. Kutoka
3. Walawi
4. Hesabu
5. Kumbukumbu la Torati

Wainjili wanne Katika Agano Jipya ni wakina nani?
Wainjili wanne Katika Agano Jipya ni
1. Mathayo
2. Marko
3. Luka
4. Yohane

Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano la Kale ni vipi?
Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano la Kale ni
1. Cha kwanza ni Kitabu cha Mwanzo
2. Cha mwisho ni Kitabu cha Malaki

Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano Jipya ni vipi?
Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano Jipya ni
1. Kitabu cha kwanza ni Injili ya Mathayo
2. Kitabu cha mwisho ni Kitabu cha Ufunuo

Injili ni nini?
Injili ni Habari njema ya wokovu iliyoletwa na Yesu Kristo

Watoto wawili wa Adamu na Eva walkikuwa wepi?
Walikuwa ni Kaini na Abeli

Watoto wa Nuhu ni wepi?
Watoto wa Nuhu ni Shemu, Hamu na Nefteli

Mababu watatu wa Imani Katika Biblia ni wakina nani?
Mababu wa Imani ni Ibrahimu, Isaka na Yakobo

Watoto wa Yakobo ni Wepi?
Watoto wa Yakobo ni
1. Reubeni
2. Simeoni
3. Lawi
4.Yuda
5. Dani
6. Naftali
7. Gadi
8. Asheri
9. Isakari
10. Zabuloni
11. Yosefu
12. Benjamini

Nani aliwatoa Waisraeli MIsri na Kuwaongoza Katika nchi ya Ahadi?
Musa ndiye aliwatoa Waisraeli MIsri na Kuwaongoza Katika nchi ya Ahadi

Mungu alimpa Musa Amri Kumi wapi?
Mungu alimpa Musa Amri Kumi katika mlima wa Sinai

Vitabu vya Historia katika Biblia ni vipi?
Vitabu vya Historia katika Biblia ni
1. Yoshua
2. Waamuzi
3. Ruthu
4. 1 Samweli
5. 2 Samweli
6. 1 Wafalme
7. 2 Wafalme
8. 1 Mambo ya Nyakati
9. 2 Mambo ya Nyakati
10. Nehemia
11. Ezra
12. Tobiti
13. Yudith
14. Esta
15. 1 Wamakabayo
16. 2 Wamakabayo

Vitabu vya manabii katika Biblia ni vipi?
Vitabu vya Manabii ni
1. Isaya
2. Yeremia
3. Maombolezo
4. Baruku
5. Eekieli
6. Danieli
7. Hosea
8. Yoeli
9. Amosi
10. Obadia
11. Yona
12. Mika
13. Nahumu
14. Habakuki
15. Sefania
16. Hagai
17. Zekaria
18. Malaki

Vitabu vya Hekima Katika Biblia ni Vipi?
Vitabu vya Hekima ni
1. Yobu
2. Zaburi
3. Mithali
4. Mhubiri
5. Wimbo ulio Bora
6. Hekima ya Solomoni
7. Yoshua Bin Sira

Nyaraka za Mitume katika Biblia ni zipi?
Nyaraka za Mitume ni;
1. Waroma
2. 1 Wakorinto
3. 2 Wakorinto
4. Wagalatia
5. Waefeso
6. Wafilipi
7. Wakolosai
8. 1 Wathesalonike
9. 2 Wathesalonike
10. 1 Timotheo
11. 2 Timotheo
12. Tito
13. Filemoni
14. Waebrania
15. Yakobo
16. 1 Petro
17. 2 Petro
18. 1 Yohane
19. 2 Yohane
20. 3 Yohane
21. Yuda

Je, Bikira Maria alikua na watoto wengine Mbali na Yesu?
Je, Bikira Maria ni Bikira Daima au alizaa watoto wengine?
Jibu fupi ni kwamba Bikira Maria hakuzaa watoto wengine na hakuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu
Hapo zamani hakuna mkristu au dehebu lolote lililokuwa linapinga kuwa Bikira Maria sio Bikira Daima hata Waprotestanti/walokole waliamini Bikira Maria ni Bikira Hata Baada ya Kumzaa Yesu. Kwenye Miaka ya 1400-1600 Watu wote wakwanza waliopinga Kanisa Katoliki walikubali kuwa Bikira Maria ni Bikira daima wakiwemo Martin Lutha aliyeanzisha kanisa la Lutheran, John Calvin aliyeanzisha Ulokole/Protestanti, Mchungaji Ulrich Zwingli, Heinrich Bullinger, and Thomas Cranmer. Kwa miaka zaidi ya 350 Waprotestant/walokole waliendelea kuamini kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.
Lakini baadae wakristo wengi walianza kupinga kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.
Tunaweza kuthibitisha kuwa Bikira Maria hakuzaa watoto wengine kwa kunukuu Biblia Kama ifuatavyo;
1. Bikira Maria Alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu
Biblia inatuambia wazi kwamba Bikira Maria alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu Kama tunavyosoma katika Luka 1:26-35
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe.” 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” 34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)
2. Biblia Haiwataji ndugu wa Yesu wakati Yosefu na Maria walipokimbilia Misri kumficha Yesu na wakati waliporudi
19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.” 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.” Matayo 2:19-23
Kama wangekuwepo wadogo zake Yesu Biblia ingetuambia kwamba walikuwa wapi wakati huo na walikuwa na Yesu au la.
3. Biblia haituambii kuwa Yesu alikua na wadogo zake alipokuwa na miaka 12
Wakati wa Maria, Yoseph na Yesu walipoenda Yerusalemu Yesu akiwa na miaka 12 Biblia haituambii kuwa Yesu alikuwa na wadogo zake na walikuwa wapi. Kumbuka walikuwa na Desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka kwa ajili ya Pasaka familia nzima kama familia. Je hao watoto wengine walikuwa wapi. Kwa nini walikuwa na Yesu Mwenyewe? Maana yake ni kwamba Yesu hakuwa na Wadogo zake.
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.” 49 Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
Kwa hiyo Biblia haionyeshi kuwa Yesu alikuwa na kaka na dada wakati akiwa na miaka 12. Kama wangekuwepo wangetajwa hapa kuwa walikuwa pamoja na Wazazi wao kama Yesu au walikuwa na Yesu wakati anapotea. Biblia haituambii chochote kwa hiyo wakati huo hapakuwa na wadogo zake Yesu.
4. Kukosekana kwa neneo “Binamu” kwenye lugha ya Yesu
Wakristu wa kwanza pamoja na Yesu aliongea Kiaramaiki au Kiebrania. Katika lugha zote hizo hakuna neno “Binamu” kwa hiyo mabinamu walijulikana kama dada na kaka wa mtu. Kwenye Agano jipya Neno kaka na Dada lilitumika pia kuwakilisha binamu.
Biblia inapotuambia kuwa Kaka na dada zake Yesu haimaanishi kaka wa kuzaliwa bali ndugu au Binamu
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kwa hiyo wanaotajwa hapa ni ndugu wa Yesu kwa maana maneno kama; ndugu, kaka au dada lilitumika badala ya Binamu yaani mtoto wa shangazi au mjomba. Hapa juu Yosefu ametajwa kama kaka yake Yesu lakini tunajua kuwa Yosefu ni Baba yake Yesu. Baba na mwana hawawezi kuwa na jina sawa.
5. Biblia haitumii neno Ndugu, kaka au dada ikimaanisha ndugu wa kuzaliwa mama mmoja na baba mmoja
Sio mara zote Biblia imetumia neno Ndugu kumaanisha ndugu (Dada na Kaka) wa kuzaliwa yaani kaka na dada kwa mfano
Kwa kuangalia lugha ya Kiswahili na Kiingereza 1 Wakorintho 15:6 tunaona tafsiri tofauti.
KISWAHILI 6 Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa.
ENGLISH 6 After that, he appeared to more than five hundred of the brothers and sisters at the same time, most of whom are still living, though some have fallen asleep.
Kwa hiyo hapa neno kaka dada na ndugu linaonekana wazi halikumaanisha ndugu au kaka wa damu.
6. Undugu wa Yakobo, Simoni, Yosefu na Yuda kwa Yesu Sio wa mtu na kaka zake
Wasemao kuwa Bikira maria alikuwa na wana zaidi ya Yesu wananukuu kifungu hiki;
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kumbuka kulikuwa na Yakobo wawili wakati wa Yesu, Vifungu vifuatavyo yunaweza kuona kuwa kulikuwa na yakobo wawili ambao walikuwa ndugu za Yesu lakini sio kaka wa kuzaliwa kwa mama.
35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)
Tunaweza kuona Undugu huu na Yesu kwa kusoma;
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. (Wagalatia 1:19)
Lakini Yuda anasema;
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. (Yuda 1:1)
Kwa hiyo Yakobo na Yohane walikuwa watoto wa Mama mwingine ambao baba yao ni Zebedayo. Na Yakobo na Yosefu walikuwa watoto wa Maria Mwingine. Kwa hiyo ni Yakobo wa wili wa Mama wengine Tofauti na Maria. Yuda alikuwa ni ndugu yake Yakobo. Yakobo vilevile alikuwa ndugu yake Yesu.
Kuthibitisha kuwa Hawa kina Mama ndio waliokuwa Mama zao kina Yakobo wote hao wawili na wengine tunaweza kusoma;
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. (Yohana 19:25)
Kwa hiyo kwenye (Yohana 19:25) tunaona Kuwa ni kwenye Msalaba wa Yesu alikuwepo Mama yake Yesu (Bikira Maria), Dada yake Bikira Maria, Mke wa Cleopa na Maria Magdalena. Na kwenye (Matayo 27:55-56) wamwtajwa ni Mama za kina nani kama inavyoonekana kwenye kifungu kifuatachi;.
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56).
Kwa hiyo hii ina maanisha kulikua na wanawake watatu wenye majina sawa ya Maria waliokuwa chini ya Msalaba. Yakobo na Yuda walikuwa watoto wa Maria Mke wa Cleofasi, na sio Mama wa Yesu, na hivyo sio kaka za Yesu.
7. Yesu alimwacha Mama yake kwa Yohane kwa kuwa hakuwa na Kaka na dada wakumwachia mamaye
26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: “Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.” 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
Ndiyo maana Bikira Maria tangu siku ile alihamia kwa Yohani kwa kuwa hakuwa na watoto wengine.

Baba wa Yesu Kristo ni nani?
Baba wa Yesu Kristo ni Mungu Mwenyewe

Baba Mlishi wa Yesu Kristu ni nani?
Baba mlishi wa Yesu Kristo ni Yosefu Mtakatifu (Mt 1:18-20)

Yesu Kristu alizaliwa wapi?
Yesu Kristu alizaliwa Bethlehemu pangoni (Lk 2:4-7)

Nini maana ya Jina Bethlehemu?
Bethlehemu maana yake ni
Nyumba ya mkate

Yesu Kristu aliishi wapi kabala ya kuanza kazi yake?
Yesu Kristu Aliishi Nazareti kabla ya kuanza kazi yake

Mtangulizi wa Yesu Kristu ni nan?
Mtangulizi wa Yesu Kristu ni Yohani Mbatizaji

Wazazi wa Yohani Mbatizaji ni nani?
Wazazi wa Yohani Mbatizaji ni Zakaria na Eizabeti

Wazazi wa Bikira Maria ni nani?
Wazazi wa Bikira Maria ni Yoakimu na Anna

Mitume kumi na wawili wa Yesu Kristu ni wapi?
Mitume wa yesu ni;
1. Simoni/Petro
2. Yakobo
3. Yohane
4. Andrea
5. Filipo
6. Barttholomayo
7. Mathayo
8. Thomaso
9. Yakobo wa ALfayo
10. Thadayo (Yuda Thadey)
11. Simoni Mkanaani
13. Yuda Iskarioti – Aliyemsaliti

Baba Mtakatifu wa kwanza ni nani?
Baba Mtakatifu wa Kwanza ni Mt. Petro

Nani ni Mitume wa Mataifa?
Mitume wa mataifa ni Paulo na Barnaba

Nani ni shahidi wa kwanza katika Agano Jipya?
Shahidi wa Kwanza ni Mt Stefano

Yesu Alianza kuhubiri injili kwa maneno gani?
“Wakati umetimia na ufalme wa Mungu umekaribia, tubuni na kuiamini Injili” (Mk 1:15)

Yesu alitukomboa kwa hatua zipi?
Yesu alitukomboa kwa Hatua Mbili (2) ambazo ni;
1. Mafundisho yake
2. Mateso, Kifo na Ufufuko wake

Sentesi saba za Yesu msalabani ni zipi?
Sentesi saba za Yesu Msalabani ni;
1. Baba uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya (Lk 23:34)
2. Nakuambia Hakika leo utakuwa pamojanami Mbinguni (Lk 23:43)
3. Mama huyu ndiye mwanao (Yoh 19:26)
4. Tazama huyu ndiye Mama yako (Yoh 19:27)
5. Eloi, Eloi, lema Sabakthani (Mk. 15:34) Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?
6. Naona kiu (Yoh 19:28)
7. Yametimia (Yoh 19:30)
Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About