Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Angalia nilivyoingizwa mjini na ujanja wangu wote

Ndio nilikuwa nimeshuka kwenye basi la SAI BABA pale Ubungo, nina Begi kubwa Mgongoni na begi Dogo la Lap Top mkononi, sura inatazama Mbele Very Serious kama nipo kwenye Gwaride la Uhuru!..Mabega juu yanafanya Cheers na Mawingu!, natembea kwa madoido…..leo nimetoka Likizo Moshi,

“Brother Simu ya ukweli hii..kitu cha Tecno C9 bei poa” hii ilikuwa sauti ya Teja mmoja hivi!

Yaani huyu Teja Bwege kweli,anataka kumuuzia nani sabuni? mimi sio wa kuja!…kamwe Siwezi kuibiwa hapa Town,hakuna wizi au utapeli nisioujua!, Mimi nimezaliwa Mwananyamala kwa Manjunju, nikalelewa Tandale kwa Mtogole, Shule ya msingi nimesoma Turiani Magomeni, Hivi Mbwa gani aniibie?…kwa Style ipi?

Sipendi kabisa Upuuzi!, Wajinga ndio wataibiwa, sio Mimi!…sasa Kwa mwendo wa haraka nikatoka nje kabisa ya Stendi ya Ubungo straight mpaka Stendi ya dala dala za Kariakoo, hapo ndipo nikakutana na Vijana wawili wadogo wakiwa na mzani wa kupimia uzito,…hakika napenda sana vijana wanaojituma kama hawa na sio ile Mijizi ya kule ndani Stendi!!,….hapa sasa nikapata wazo!

“Dogo mnapima uzito kwa shilingi ngapi?”

“Mia mbili tu Kaka!”

”Ok”

Kwa mwendo wa kikakamavu nikapanda juu ya mzani,lengo hapa ni kujua uzito wangu, Mtori niliokula mwezi mzima kule kwa Mshekuu sio mchezo, hapa nahisi nacheza kwenye kg za John Cena,

“Mama wee! Dogo mzani mzima huu kweli? Mbona nina kilo 134?” (Nilihamaki)

“Aaah! Brother huoni umepanda na Mabegi juu ya mzani?”’

Hahaha! kweli nimechanganyikiwa!…Sasa nikatoa mabegi yote mawili na kurudi juu ya Mzani, hapa ndipo Uzito ukashuka kutoka kg 134 mpaka kg 56!…My God kweli Body la “One Pack ” haliongopi! thats means mabegi yaliniongezea kg 78! duh hii ni hatari!

“Yaani we Dogo kitambi chote hiki kg 56? huu Mzani Mzima kweli?”

Kimya…

“Dogo huu Mzani vipi?”

Kimya…

Dogo ana dharau huyu!…Sasa ndio nikabandua macho yangu toka kwenye kioo cha mzani ili nimtazame huyu dogo asiyejibu!….ndipo macho yangu yakakutana na Kigoda tupu kilichochongwa Mvomero!…Dogo hakuwepo!….na Mabegi pia hayapo!…lap top haipo!….NIMEPIGWA!

Ni dhahiri watoto wa Mjini walikuwa wameniacha juu ya Mzani, wamechukua Lap top ya Milioni na wameniachia Mzani chakavu wa elfu 40, what a stress!….sasa nilirudisha macho kwenye kioo cha uzito na sasa kilisoma KG 38!…yaani dakika hii hii nimepungua kilo zingine 18, Hakiyamama nahisi hata utumbo wangu wamebeba!…niitieni Ambulance!

🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼

Jinsi ya kufanya ili upate mtoto wa kike au wa kiume

Katika urutubishaji yai la mwanamke linabeba chromosome X yani XX. Na mbegu ya mwanaume inabeba chromosome XY. Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na Y kutoka kwa mwanaume mtoto wa kiume hupatikana. Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na X kutoka kwa mwanaume mtoto wa kike hupatikana

Fahamu sifa za chromosomes X na Y za mwanaume.

Ili uweze kufanikiwa kuchagua mtoto wa kiume au wa kike lazima ujue sifa za chromosomes hizi zinazoamua jinsia ya mtoto.

Sifa za chromosomes Y

• Zina spidi kubwa sana kwahiyo kama yai lipo tayari zenyewe zitawahi kwenda kurutubisha
• Zina maisha mafupi sana kulinganisha na X

Sifa za chromosomes X

• Zina spidi ndogo sana

• Zina maisha marefu kulinganisha na Y

Baada ya kujua sifa za chromosome ambazo ndo zinatusaidia kuamua jinsia twende moja kwa moja kwenye jinsi ya kupata mtoto wa jinsia unayotaka

Mambo ya kuzingatia katika suala la kuamua jinsia ya mtoto amtakaye:

• Lazima mwanamke ajue mzunguko wake (menstrual cycle)siku ya 1-28

• Lazima mzunguko wako uwe na mpangilio sahihi(unaweza ukachunguza mzunguko wako kwa miezi minne mfululizo)

• PH ya uke lazima iwe kiwango sahihi 4-5.5(Tumia neplily pad kwa kuwa na PH sahihi

• Ushirikiano kati ya mwanamke na mwanaume

Jinsi ya kumpata mtoto wa kiume

Ili uweze kupata mtoto wa kiume kisayansi unashauriwa kushiriki tendo la ndoa siku ambayo yai litakuwa limetoka kama mzunguko wako uko sahihi ni siku ya 14

Njia nyingine ya kujua yai limetoka baba anaingiza vidole viwili ukeni wakati wa asubuhi na ukikuta uteute ujue yai limetoka kwahiyo jioni mnashiriki tendo la ndoa kwa ajili ya kupata mtoto wa kiume

KWANINI USHIRIKI TENDO LA NDOA WAKATI YAI LIMETOKA ILI KUPATA MTOTO WA KIUME?

Kisayansi chromosome Y ambayo inahusika katika kutunga mimba ya mtoto wa kiume ina spidi kubwa sana ni nyepesi na haiwezi kisihi mda mrefu kwahiyo ukishiriki tendo la ndoa wakati yai limetoka maana ake unaongeza nafasi ya kupata mtoto wa kiume

Jinsi ya kuapata mtoto wa kike.

Ili ufanikiwe kupata mtoto wa kike utatakiwa ushiriki tendo la ndoa siku tatu kabla ya yai kupevuka yani hapa ni baada ya kujua mzunguko

KWANINI USHIRIKI TENDO LA NDOA SIKU TATU KABLA

Hii ni kwasababu chromosome X ambazo ndo zinaunda mtoto wa kike huwa zina sifa ya kuwa na maisha marefu na kutembea taratibu hivyo yai likitolewa litakuta chromosome X ziko hai

MAMBO YANAYOWEZA ATHIRI KUPATA MTOTO UNAYEMTAKA

• Kushindwa kuhesabu siku( tumia chart niliyokuwekea)
• Mzunguko mbovu wa hedhi(Tumia neplily pad)
• KUtokuwa na PH sahihi ukeni tumia Neplily

Ujumbe kwa leo

Kuna baadhi ya LEVEL huwezi kufika…Kuna MAFANIKIO huwezi kuyafikia…Kuna HELA huwezi kuzipata…Kama umezungukwa na watu BASIC…
Kuanzia asubuhi mpaka jioni wanaongelea WATU TU..Fulani kamegwa na yule..halafu yule naniliu saivi anatembea na yule ex wa nanii…Asubuhi mpaka jioni DISCUSSING PEOPLE…Hawa ndio watu BASIC…Hata siku 1 hawatakupa Ushauri kuhusu HOW TO REACH SOMEWHERE…NEVER

Na ukionekana unaanza kufanya vitu EPIC watakugeuka kwamba UNARINGA.. UNAJISIKIA.. UMEWATENGA…UNAJIDAI UNA HELA…and lots of bullshit…
Pengine ulipaswa kuwa mbaaalii kibiashara lakini HUWEZI coz umezungukwa n Mbaazi tupu…BASIC PEOPLE…Ukiwaambia umesikia Kiwanja kinauzwa Kigamboni wanakwambia Kigamboni watu wanatapeliwa kuna mradi wa Joji Bushi…Ukiwambia unataka kujiunga Forever Living wanakwambia UNALIWA HELA…Ukiwaambia kuna SACCOSS wanatoa mikopo unataka uchukue ujenge wanakwambia INTEREST ZAKE UTASHINDWA na kujenga sio mchezo shosti..Unaamini unaacha!…Nataka kufanya Kitu flani WANAKUKATISHA TAMAA
Unahitaji kuzungukwa na watu wenye POSITIVE ENERGY ambao ukiwambia unataka kwenda Mbinguni kwa kupitia Mkuranga wanakuchangia Nauli…Niliposema naacha kazi watu ohh utakula nini..utaishije…Mji Mgumu huu..Wenzio wanatafuta kazi we unaacha utalosti…WHO SAID??Nadunda kama kawa..NEGATIVE PEOPLE WILL BRING U DOWN….Ukitaka Kupaa kaa karibu na ndege…We unataka kupaa unakuwa rafiki wa Nyangumi…UNAZAMISHWA SASA HIVI!!
Tangu nianze kukaa na watu Positive I have changed a lot…Nikiwaza jambo wanauliza HOW DO WE ACHIEVE THIS na sio FULANI ALIWAHIFANYA HII AKAFELI..
Ikikusaidia Chukua..
KILL ALL NEGATIVE PEOPLE AROUND YOU kama unataka kufikia Malengo Makubwa, I will be ur Lawyer at the Court na mwambie Hakimu nilikutuma mimi!
TIME TO DELETE ALL BASIC PEOPLE who wait of option😜😜😉😉

Mapishi ya Biriani la nyama ya ng’ombe

Mahitaji

Nyama ya ng’ombe (beef 1/2 kilo)
Mchele (rice 1/2 kilo)
Vitunguu (onion 2)
Viazi (potato 2)
Vitunguu swaum (garlic 3 cloves)
Tangawizi (ginger)
Nyanya ya kopo (tomato 1/2 ya tin)
Curry powder (1/2 kijiko cha chai)
Binzari nyembamba ya kusaga (cumin 1/2 kijiko cha chai)
Binzari manjano (tarmaric 1/2 kijiko cha chai)
Mafuta (vegetable oil)
Chumvi (salt)
Rangi ya chakula (food colour)
Giligilani (fresh coriander)
Maziwa ya mgando (yogurt kikombe 1 cha chai)
Hiliki nzima (cardamon 3cloves)
Karafuu (clove 3)
Pilipili mtama nzima (black pepper 5)
Amdalasini (cinamon stick 1)

Matayarisho

Katakata nyama kisha ioshe na uiweke kwenye sufuria kisha tia kitunguu swaum, tangawizi, nyanya, curry powder, binzari zote, chumvi na maziwa ya mgando kisha bandika jikoni ichemke mpaka nyama iive na mchuzi ubakie kidogo.Baada ya hapo kaanga viazi na uweke pembeni, kisha kaanga vitunguu na mafuta mpaka viwe ya brown na kisha uvitie viazi vitunguu, na mafuta yake katika nyama. Koroga na uache uchemke kidogo kisha ipua na utie fresh coriander iliyokatwa na hapo mchuzi wako utakuwa tayari.
Baada ya hapo loweka mchele wako kwa muda wa dakika 10, kisha chemsha maji yatie chumvi, hiliki, karafuu, pilipili mtama na abdalasin na mafuta. Yakisha chemka tia mchele na uache uchemke mpaka ukauke maji yakisha kauka tia rangi ya chakula na uanze kugeuza ili ichanganyike na wali wote. Baada ya hapo ufunike na uache mpaka uive. Na baada ya hapo biriani litakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Pilau Ya Bilingani Na Kuku

Viambaupishi

Mchele wa basmati – 3 vikombe

Kuku – ½

Bilingani – 2 ya kiasi

Viazi – 4

Vitunguu – 2

Kitunguu (thomu/galic) iliyosagwa – 2 vijiko vya supu

Pilipili mbichi iliyosagwa – 2

Chumvi – kiasi

Garama masala (mchanganyiko wa bizari) – 1 kijiko cha chai

Hiliki ya unga – ¼ kijiko cha chai

Mafuta ya kupikia wali – ¼ kikombe

Mafuta ya kukaangia viazi na bilingani – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:

Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele.
Kata kuku vipande upendavyo safisha
Kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu, na bizari mchanganyiko (garama masala).
Akiwiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria.
Menya na kata viazi kaanga weka kando.
Kata kata bilingani slesi nene kaanga, chuja mafuta weka kando.
Katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangu ya hudhurungi. Tia vipande vya kuku, ukaange kidogo.
Tia supu ya kuku, mchele, tia hiliki, ufunike hadi karibu na kuwiva kabisa.
Tia viazi na bilingani uchanganye kidogo, kisha tia katika oven imalizike kupikika pilau humo au unaweza kuendelea kufunika juu ya jiko hadi pilau iwive.
Pakua katika sahani ikiwa tayari kuliwa kwa saladi ya mtindi.

Mume alichomjibu mchepuko wa mke wake

😎 Jamaa kamuaga mkewe anaenda semina Songea kwa wiki nzima kumbe kahamia kwa demu nyumba ya pili toka kwake. Siku ya 1 kalala asubuhi alipoamka kachungulia kwake kukoje,

Si kamuona jamaa yuko nje ya nyumba yake kavaa taulo lake anapiga mswaki. Akapiga kelele, ‘We nani?’, Jamaa akajibu, ‘Mshikaji mambo ya mjini, mume wa huyu demu kasafiri kaenda Songea mi ndo najivinjari hapa’. Mume kajibu kwa uchungu, Shenzi mkubwa, ngoja nirudi toka Songea nakuua.😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆

*Mniache mimi sipendi Ujinga Ujinga 🏃�🏃�🏃�🏃

Alichofanya maasai baada ya kupanda Tax

Baada ya kupanda daladala aina ya DSM kutoka Mbagala chalambe mpaka Mwenge na kulipa sh 500.Masai akachukua tax wakati wa kurudi.walipofika sasa shughuli ilikuwa hivi.

Masai: we dureva? Naulisa Ng’ombe na mbusi ipi ngali?
Dereva: Ni ng’ombe ghali Masai.
Masai: kwanini Ng’ombe ngali?
Dereva: kwa sababu ni mkubwa zaidi ya mbuzi
Masai: umepata..na mbusi na kuku ipi ngali
Dereva: ni mbuzi kwa sababu nae ni mkubwa kuliko kuku.
Masai: Umepata..
Masai: sasa me nimekwenda kule mwenge kwa ngali kubwa nikalitoa sh. 500 hii yko ndogo unasema nikupe 40,000 wewe acha wizi.. Nitakupa 250 Tu..wee acha lbia morani…!!!

Mapishi ya Koshari Na Sosi Ya Kuku

Vipimo Vya Koshari

Mchele – 2 vikombe

Makaroni – 1 kikombe

Dengu za brown – 1 kikombe

Vitunguu vilokatwakatwa (chopped) – 2

Nyanya ziilokatwakatwa (chopped) – 4

Nyanya ya kopo – 1 kijiko cha supu

Kitunguu saumu(thomu/galic) ilosagwa – 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi ilosagwa – 1 kijiko cha chai

Pilipili manga ya unga – 1 kijiko cha chai

Mdalisini kijiti – 1

Bizari ya pilau (cumin seeds) – 1 kijiko cha supu

Hiliki – 2 chembe

Mafuta – 3 vijiko vya supu

Chumvi – kiasi

Vipimo Vya Kuku

Kuku – 3 LB

Kitunguu saumu(thomugalic) na tangawizi – 1 kijiko cha supu

Mtindi (yoghurt) – 1 kijiko cha supu

Pilipili ya masala nyekundu – 1 kijiko cha chai

Bizari upendazo – 1 kijiko cha chai

Ndimu – 1

Vitunguu slesi vilokaangwa – 3

Namna Kutayarisha Kuku

Kata kuku vipande vikubwa kiasi, osha, weka kando achuje maji.
Changanya vipimo vya kuku pamoja katika kibakuli.
Changanya pamoja na kuku, roweka muda wa kiasi nusu saa au zaidi.
Mchome (grill) kuku hadi aive weka kando.

Namna ya Kutayarisha Koshari

Tia mafuta katika sufuria, kaanga vitunguu hadi viive kuwa rangi hudhurungi.
Tia thomu ,mdalisini, bizari ya pilau na hiliki kaanga tena kidogo.
Tia nyanya, pilipili zote, nyanya kopo, chumvi changanya vizuri ukaange kidogo.
Epua sosi acha kando.
Chemsha dengu pamoja na kidonge cha supu ziive nusu kiini na ibakie supu yake. Muda wa kuchemsha dengu inategemea aina yake.
Tia mchele uchanganyike, funika, pika hadi uive vizuri pamoja na dengu
Chemsha makaroni hadi yaive , epua chuja maji.
Changanya pamoja wali wa dengu na macaroni.
Pakua katika sahani, kisha weka juu yake kuku aliyechomwa, mwagia vitunguu vilokaangwa, kisha mwagia sosi.

Kilichompata huyu jamaa mroho wa nyama, Hata kaa arudie tena

Jamaa kaenda kumtembelea rafiki yake Levi, kule sehemu za kwetu, akakaribishwa bonge ya ugali na nyama nyingi tu, wakati anakula akagundua kuwa shemeji yake, mke wa rafiki yake hali nyama;

JAMAA: Aise hili ni bonge ya lanchi hii, lakini Levi mbona sisi tu tunakula nyama shemeji Gulo hagusi kabisa anaishia mchicha tu? Tabia gani hii?
LEVI: Hapana sijamkataza, ila shemeji yako Mngoni halagi nyama ya FISI kama sisi

Vyakula vya Kukuza nywele na kuzifanya ziwe na Afya

Kuwa na nywele zenye afya nzuri ni muhimu kwa wote bila kujali jinsi, hali hii husababisha wengi kutumia madawa ya aina mbalimbali ya kuhakikisha nywele zao zinastawi na kuwa na muonekano mzuri.
Kwa bahati mbaya, wengi waliotumia madawa yanayotengenezwa kwa kemikali hujikuta katika wakati mgumu siku za usoni wakikabiliwa na matatizo ya nywele kukatika na hata kupata madhara katika ngozi ya kichwa.

Njia bora na salama zaidi ya kustawisha nywele, kuzifanya ziwe na mvuto wa aina yake bila kujali wewe ni mtu wa asili ya bara Asia, Afrika au Marekani, ni kula vyakula vyenye virutubisho muhimu kwa afya ya nywele.

Vifuatavyo ni sehemu ya vyakula ambavyo hupatikana kirahisi barani Afrika na kwa bei nafuu, ambavyo vitakupa afya bora zaidi ya nywele zako.

1. Yai

Nywele za binadamu zina protini ambayo zimeumbiwa. Hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa zina protini ya kutosha, na hilo hufanyika kupitia vyakula. Protini ni nguzo kuu ya nywele za binadamu, na yai ni moja kati ya vyakula vyenye utajiri mkubwa wa protini. Hakikisha unakula yai angalau mara tatu kwa wiki.

2. Spinachi

Nywele zinahitaji madini ya chuma ili ziweze kuwa katika hali nzuri ya afya. Kukosekana kwa madini ya chuma husababisha nywele kunyonyoka. Mwili unapokosa madini ya chuma, hewa ya oxygen na virutubisho hushindwa kufika vizuri kwenye mizizi ya nywele hivyo hufanya nywele kuwa dhaifu na zisizo na muonekano mzuri.

Mboga za majani aina ya spinachi ni suluhisho, kwakuwa zina madini ya chuma kwa wingi ambayo seli za nywele huhitaji.

3. Jamii ya Machungwa, Limao

Mwili wa binadamu huhitaji vitamini C ambayo husaidia kuhuisha utendaji wa madini ya chuma. Hivyo, unapaswa kuongeza matunda ya jamii ya ‘citrus’, kama vile machungwa, chenza, balungi na limao. Pia, unaweza kutumia na asali pamoja.

Vitamini C husaidia katika ukuaji wa nywele kusaidia usambaaji wa virutubisho na ukuaji wa haraka wa nywele.

4. Karoti

Ni muhimu sana kuhakikisha unakunywa juice ya karoti kila siku, kama unataka nywele zako zikue haraka zikiwa na mwonekano mzuri wenye afya. Vitamini A inayopatikana kwenye karoti ni muhimu sana kwa ukuaji wa seli za nywele. Kumbuka nywele zina tishu ambazo hukua haraka zaidi katika mwili.

Karoti ina mafuta asili yanayofahamika kama ‘sebum’ na mizizi ambayo husaidia kukuza nywele kwa haraka.

5. Parachichi

Tunda aina ya parachichi lina kazi nyingi sana mwilini kama matunda mengine, lakini hili ni tunda la kipekee amnbalo lina utajiri wa vitamini E ambayo husaidia mzunguko wa damu na katika hilo husaidia mfumo wa ukuaji wa nywele kwa haraka.

Tunda hili husaidia kuhuisha na kurekebisha mafuta na kiwango cha PH (inayosafisha kemikalii mwilini) ambavyo kama vitazidi kwenye mwili vinaweza kusababisha kusimama kwa ukuaji wa nywele, yaani nywele hudumaa.

Kwa faida zaidi, vitamin E inayopatikana kwenye parachichi kwa wingi husaidia zaidi afya ya moyo wa binadamu na zaidi ngozi. Hakikisha unapata tunda hili kadiri iwezekanavyo.

Hivi ni baadhi tu ya vyakula na matunda kwa ukuaji mzuri wa nywele zako. Kama unatumia vizuri mlo wako, utakuwa adimu sana kutumia mafuta yenye kemikali ambayo yanaweza kukuletea madhara mabaya.

Jinsi ya kutumia maziwa ya mtindi kufanya ngozi yako kuwa laini na soft

Ulisha wahi kukaa ukajiuliza mbona kuna baadhi ya watu wana ngozi nzuri laini na soft? lakini kwako ni tofauti?

Ukawaza labda wanatumia vitu vya bei ghali ambavyo wewe huwezi ku – afford, au umesha hangaika na ma – cosmetics lakini bado ngozi yako haikubali kukaa vizuri?

Jaribu hii Home made Yogurt Cleansing, Tumia mtindi ambao hauna mafuta mengi au hauna kabisa (low fat),

Paka mtindi wako usoni fanya kama una sugua kwa muda mchache halafu uache kwa dakika 15, fanya hivi mara mbili kila siku na utapata matokeo kwa muda mchache.

Hii husaidia kuondoa cell za ngozi zilizo kufa (dead skin cells) na protein tighten the pore.

Ufalme wa simu wa sasa

➡ Asubuhi saa 12 : 00 mtu anaamka, kabla hata HAJAMUSHUKURU MUNGU, kabla hata hajatoka kitandani, kabla hata hajajifunua shuka,

👉ATARIPOTI KWA SIMU KWANZA KABLA YA KURIPOTI KWA YEYOTE, NDIO HAPO UNAONA MTU AKIAMKA KABLA HATA HAJASALI KWA MUNGU ANAAMKIA SIMU KWANZA KUIKAGUA,
– Nani alinitafuta?
-Nani alini-text?
-WhatsApp nani kanitumia msg?
– kwenye magroup kuna mpya gani?
– Fb kuna post gani kali?
– nani kaweka picha kali leo?
Nk.
Akimaliza KURIPOTI KWA Simu, faster faster, anapiga kaombi ka kidesturi, sekunde 20 basi.
Biblia ipo hapo kando tu ya kitanda, lkn anaona hana muda wa kuisoma.
✴BADALA YA KUANZA SIKU NA BWANA, MTU ANAANZA SIKU NA SIMU.
Pamoja na kazi za kuutwa, za mtu huyo, lkn atafanyq juu chini, apate muda wa KURIPOTI kwa SIMU.
Lakini mtu huyo huyo, hawez kbsa kupata muda wa kujitenga angalau kwa dk 3 tu, kw kutwa nzima ARIPOTI KWA MUNGU KWA NJIA YA MAOMBI.
Ana muda wa kusoma status kwenye social media kutwa nzima,
Lkn hana muda kbsa wa kupitia angalau sura moja tu, ya Biblia kwa siku.
Ana bundle la dk, sms, WhatsApp kila siku, lkn hana sadaka ya kumtolea Mungu.
Umeme ukikatika kutwa moja tu, akakosa kuwa na simu sababu ya chaji, anajisikia mpwekee, siku anaiona ndefuu, anajiona amepungukiwa saana!
Lakini huyo huyo, siku nzima inaisha, na ya pili, ya tatu , hajawahi kuwa na muda na Mungu wake hata kidogo, na anaona ni sawa tu.
Hata ktk siku ya ibada, yale masaa machache tu ya ibada, ambapo inatakiwa iwe ni mtu na Mungu wake tu, bila kuingiliwa na chochote, 👉mtu bado hawezi kukaa bila KURIPOTI kwa simu, ibada inaendelea huku mtu kawasha data, na anasoma na kujibu msg zake km kawaida.
👉 au kama ana kaustaraabu kidogo, atatoka nje, huko anaenda kukagua msg, kuangalia updates nk.
SIMU UNAYO KUTWA, KUCHWA, KIIILA SIKU, YANI HUKUWEZA KUVUMILIA KUIWEKA PEMBENI KWA MASAA TU?
➡ Swali nauliza, Mtu wa aina hiyo Mungu wake ni nani?
” Usiwe na miungu mingine ila mimi”.
KUTOKA 20 : 3
Kumuabudu Mungu peke yake, ni kumfanya Mungu awe wa KWANZA MOYONI NA MAWAZONI MWAKO.
Kumfanya awe kipaumbele kwenye kiila ulitendalo.
➡WENGI WAMEZIFANYA SIMU ZAO, ZICHUKUE NAFASI YA MUNGU KATIKA MIOYO, FIKRA NA MAISHA YAO KWA UJUMLA.
➡Wamekuwa tayari kupoteza karibu kiila kitu kwa ajili ya simu
– kupoteza marafiki > hawana muda na marafiki zao, wanajifungia ndani, wakichati.
– hawana muda na wazazi wao, hata kama wanaishi nyumba moja. > kijana akifika nyumbani, anapitiliza chumbani, ni yeye na simu, ataonekana muda wa kula tu, tena sometimes hata mezani anakuwa na simu, pale mezani wako wazazi wake kbsa, ndugu zake nk, lkn hajali uwepo wao, anaendelea na simu tu.
– Hawana muda na Mungu > Anahakikisha vyovyote itakavyokuwa, muda wa kuwa na simu unapatikana, HATA KAMA HILO LITAMAANISHA KUUPORA MUDA WA MUNGU (muda wa ibada).
Atakosa fedha za kusaidia wahitaji, fedha za zaka na sadaka, lkn fedha ya SIMU, (bundles) , lzm inakuwepo.
➡Mtu wa aina hiyo, anaiabudu simu bila kujua.
➡KITU CHOCHOTE KINACHOUVUTA MOYO KUTOKA KWA MUNGU, KUKIELEKEA CHENYEWE, KITU HICHO KINAJARIBU KUCHUKUA NAFASI YA MUNGU MOYONI.
NB: Sio lengo langu kupinga matumizi ya simu, lkn nilitaka tuwe na kiasi.

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About