Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

MAANA YA MANENO YANAYOTUMIKA KATIKA MASUALA YA LISHE

1. Chakula

ni kitu chochote kinacholiwa au kunywewa na kuupatia mwili virutubishi mbalimbali Chakula huupatia mwili nguvu, kuulinda na kuukinga dhidi ya maradhi mbalimbali .Mfano wa chakula ni ugali, wali, maharagwe, ndizi, viazi, mchicha, nyama, samaki.

2. Lishe

ni mchakato unaohusisha hatua mbalimbali za jinsi mwili unavyokitumia chakula kilicholiwa, hatua hizi ni kuanzia chakula kinapoliwa, jinsi mwili unavyokisaga na kukiyeyusha, umetaboli, na hatimaye virutubishi kufyonzwa na kutumika mwilini.

3. Virutubishi

ni viini vilivyoko kwenye chakula ambavyo vinauwezesha mwili kufanya kazi zake, karibu vyakula vyote huwa na kirutubishi zaidi ya kimoja ila hutofautiana kwa kasi na ubora. Kila kirutubishi kina kazi yake mwilini na mara nyingi hutegemeana ili viweze kufanya kazi yake kwa ufanisi. Hakuna chakula kimoja chenye virutubishi vya aina zote isipokuwa maziwa ya mama kwa miezi sita ya mwanzo ya maisha ya mtoto, ni mhimu kula vyakula vya aina mbalimbali ili kuwezesha mwili kupata virutubishi mchanganyiko vinavyohitajika.

4. Mlo kamili

ni ule ambao hutokana na chakula mchanganyiko kutoka katika makundi yote ya chakula na una virutubishi vyote muhimu kwa ajili ya lishe na afya bora. Mlo huu unapoliwa kwa kiasi cha kutosha kulingana na mahitaji ya mwili angalau mara tatu kwa siku huupatia mwili virutubisho vyote muhimu.

5. Ulaji unaofaa

hutokana na kula chakula mchanganyiko na cha kutosha (mlo kamili) ili kukidhi mahitaji ya mwili. Ulaji unaofaa pia huzingatia matumizi ya kiasi kidogo cha chumvi, mafuta, sukari, ulaji wa nyama nyekundu kwa kiasi kidogo. Ni muhimu kuzingatia ulaji wa mboga mboga, matunda, na vyakula vya jamii ya kunde kwa wingi ili kudumisha uzito wa mwili unaotakiwa na kupunguza magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

6. Nishati- lishe

ni nguvu inayopatikana baada ya virutubishi (kabohaidreti, mafuta) kuvunjwa vunjwa mwilini. Mwili huitumia nguvu hiyo kufanya kazi mbalimbali Kama kulima, kutembea, kupumua, kuziweka seli za mwili katika hali inayotakiwa n.k.

7. Kalori au kilo kalori

ni kipimo kinachotumika kupima nishati -lishe

8. Makapi mlo

ni sehemu ya chakula ambayo mwili hauwezi kuyeyusha lakini ni muhimu katika uyeyushwaji wa chakula. Mfano wa vyakula venye makapi mlo kwa wingi ni mboga za majani, matunda( maembe, machungwa, mapera, machenza, mafenesi, unga usiokobolewa( dona) na vyakula vya jamii ya kunde.

9. Lehemu

ni aina ya mafuta yanayopatikana hasa kwenye vyakula vya asili ya wanyama na pia hutengenezwa mwilini. Lehemu inayotokana na vyakula ikizidi mwilini huleta madhara ya kiafya. Vyakula venye lehemu kwa kiasi kikubwa ni pamoja na maini, figo, mayai, nyama iliyonona kama nundu, nyama ya nguruwe yenye mafuta, mkia wa kondoo, samli, siagi, ngozi ya kuku n.k.

10. Utapiamlo

ni hali ya kupungua au kuzidi kwa baadhi ya virutubishi mwilini ambapo husababisha lishe duni au unene uliozidi.

11. Antioxidants

ni viini ambavyo vina uwezo wa kukinga seli za mwili zisiharibiwe na chembe chembe haribifu (free radicals) ambazo huweza kusababisha saratani. Viini hivyo huungana na chembechembe hizo haribifu na kuzidhibiti ili zisisababishe madhara. Mifano ya antioxidants ni pamoja na beta-carotene, lycopene, vitamin C, E, na A.

Eti wanadamu walikuja vipi duniani

Mtoto wa miaka sita alimuuliza babake:
MTOTO: Baa, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
BABA: Mungu alimuumba Nabii Adam na Hawa.
Kisha wao wakaanza kuzaa watoto na watoto
wakazaa mpaka tukazaliwa sisi. (Mtoto hakuridhika
akamfuta mamake)
MTOTO: Mma, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
MAMA: Wanasayansi wamesema sisi tulitokana na
manyani baadae tukawa binadamu. (Mtoto akarudi
kwa baba)
MTOTO: Baa mbona mama ansema sisi tulikuwa
manyani mwanzo?Au wanidanganya?
BABA: Mwanangu, mimi nimekuelezea kuhusu ukoo
wetu. Mamako amekuelezea kuhusu ukoo wao๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿšถ๐Ÿผ๐Ÿšถ๐Ÿผ๐Ÿšถ๐Ÿผ

Jinsi ya kupika Mkate

Mahitaji

Unga wa ngano ( self risen flour) kikombe 1 na 1/2
Hamira (yeast) 1 kijiko cha chai
Sukari (sugar) 1 kijiko cha chakula
Chumvi (salt) 1/2 kijiko cha chai
Siagi iliyoyeyushwa (melted butter) 1 kijiko cha chakula
Maji ya uvuguvugu ( warm water) kiasi

Matayarisho

Changanya vitu vyote katika bakuli kubwa kisha aanza kukanda mpaka upate donge laini.Baada ya hapo liweke hilo donge kwenye bakuli la plastic na weke katika sehemu yenye joto ili unga uumuke. Hakikisha unga unaumuka zaidi (yani unaji double size) unaweza kuchukua kama saa 1 na nusu hivi. Baada ya hapo ukande tena na uache uumuke tena kwa mara ya pili, Ukisha umuka pakaza butter katika baking tin (chombo cha kuokea) na upakaze mkate butter kwa juu,kisha uoke katika oven kwa muda wa dakika 30 (katika moto wa 200C) (hakikisha juu na chini unakuwa wa brown Na hapo mkate wako utakuwa tayari

Mapishi ya Kuku wa kukaanga

Mahitaji

Miguu ya kuku (chicken legs) 10
Kitunguu swaum na tangawizi (ginger & garlic paste) 1 kijiko cha chakula
Limao (lemon) 1
Pilipili iliyosagwa (ground scotch bonnet) 1/2
Giligilani iliyokatwakatwa (chopped coriander) kiasi
Chumvi (salt) kiasi
Mafuta ya kukaangia (veg oil)

Matayarisho

Safisha kuku kisha mtie kwenye sufuria na viungo vyote (kasoro mafuta na giligilani) kisha mchemshe mpaka aive na umkaushe supu yote. Baada ya hapo mkaange katika mafuta mpaka awe wa brown kisha mtoe na uweke katika kitchen towel ili kuchuja mafuta. Baada ya hapo weka katika sahani na umwagie giligilani kwa juu. Na hapo kuku wako atakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Kachori

Mahitaji

Viazi mbatata (potato 4 vya wastani)
Nyama ya kusaga (mince beef 1 kikombe cha chai)
Kitunguu (onion 1 cha wastani)
Carrot 1
Hoho (green pepper 1/2)
Kitunguu swaum (garlic)
Tangawizi (ginger )
Binzari nyembamba (ground cumin 1/2 kijiko cha chai)
Binzari manjano (turmeric 1/2 kijiko cha chai)
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Limao (lemon 1/2)
Pilipili ya unga (chilli powder 1/2 kijiko cha chai)
Giligilani (coriander kiasi)
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil)
Unga wa ngano kiasi

Matayarisho

Katakata vitunguu na hoho katika vipande vidogo vidogo na kisha kwangua carrot na uweke pembeni. Chemsha viazi na chumvi kidogo vikiiva viponde na uviweke pembeni, Baada ya hapo tia nyama limao, chumvi, kitunguu swaum na tangawizi ichemshe mpaka iive na uhakikishe maji yote yamekauka. Kisha Tia binzari zote, pilipili, curry powder, giligilani, vitunguu, hoho na carrot. Pika mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 3 na kisha ipua. Baada ya hapo changanya na viazi kisha tengeneza maduara ya kiasi na uyaweke pembeni. Chukua unga wa ngano kiasi na uchanganye na maji kupata uji usiokuwa mzito au mwepesi sana. baada ya hapo chovya madonge katika huo uji na uyachome katika mafuta. Hakikisha zinaiva na kuwa rangi ya brown na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.Unaweza ukazisevu na chatney yoyote unayopendelea.

Utaratibu wa Mkristo Mkatoliki Kanisani

Ninapoingia kanisani nachovya maji ya baraka na kusema;
“Unitakase Ee Bwana mimi na uovu wangu wote, ili nipate kustahili kushiriki ibada takatifu’ Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu” Amina!
Ninapiga goti huku nikisema
“Mungu wangu na Bwana wangu”
๐Ÿ™‹๐ŸฝNikiinuka nasema
“Nitakusifu na kukuabudu katika Ekaristi takatifu”
๐Ÿ™‹๐ŸฝNaenda mpaka kwenye bench, napiga magoti au nakaa nikiwa mimeinamisha kichwa (kama mabenchi yameisha nabaki nimejisimamia) huku nikitoa nia yangu ya kusali misa siku hiyo, mfano
“Ee Mungu, ninaungana nawe na jeshi lote la mbinguni, pamoja na Mama Bikira Maria, nikiwa na nia ya kumwombea mama yangu ambaye ni mgonjwa, jirani yangu ambaye mpaka sasa hatuelewani na pia familia yetu ambayo haina amani, Mungu kupitia misa hii rejesha hali ya mama yangu, rejesha uelewano na jirani yangu, na pia rejesha amani ya familia yetu pamoja na familia zote ambazo hazina amani”
๐Ÿ™‹๐ŸฝNinaendelea na misa na Kushiriki litrujia kikamilifu
๐Ÿ™‹๐ŸฝWakati wa komunyo nikikumbuka kuwa nina dhambi kubwa huwa nakominika kwa sala ya tamaa wala siendi mbele, huwa najikalia tu kwenye bench naangalia wenye moyo safi wanaenda mbele kumpokea Yesu (Kweli huwa najisikia wivu sana, itanibidi katikati ya wiki nifanye kitubio ili nisikae tena)”
๐Ÿ™‹๐ŸฝMwisho wakati wa kuondoka nachovya maji ya baraka nikisema
“Unilinde Ee Mwenyezi Mungu, nikapate kuwa mfano katika jamii yangu, na nikushuhudie katika matendo yangu”
(Hapo nachovya maji ya baraka na kufanya ishara ya msalaba) “Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, amina”
Usiku mwema wapendwa. Malaika awalinde

Mme amemfuma fundi wa kitanda na mke wake, cheki walichokua wanafanya

Kuna mama mmoja ameolewa na wanapendana sana na mmeo. siku moja mme wake alisafiri kikazi (safari ya zaidi ya mwezi) nje ya mkoa. Siku mmeo anarudi, yule mama alimtafuta fundi seremala amrekebishie chaga za kitanda zilikuwa zimeharibika, kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya above +18.

Wakati fundi anaendelea na kazi kumbe mmeo huyu dada alishafika. hakutaka kumjulisha mkeo, kwa nia nzuri tu ya kumfanyia suprise, kwani alikuja na mazaga zaga kibao. Hiyo aliingia kwa kunyatia hadi kwenye mlango wa chumbani kwao. Ghafla akasikia mazungumzo ya mkeo na fundi ndani. Mazungumzo yalikuwaje? fuatilia hapa chini

Mama X: Fanya haraka mme wangu amekaribia
Fundi: Nakaribia kumaliza, nisaidie kuchomeka vizuri upande wako (akikusudia chaga)
Mama X: Mbona haiingii
Fundi: Ingiza kwa upande upande
Mama X: Sukuma kwa nguvu
Fundi: Angalia usiumie
Mama X: Hamna shida imeingia

Wakati jamaa akiendelea kusikiliza mlangoni, fundi akaweza godoro juu ya kitanda na mama x akajitupa kitandani kujaribu kama kimetengamaa. mara chaga akachomoka na kuanguaka chini. Nini kilifuata

Mama x: Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii iiiii(miguno) “my God, mbona hivi”
Fundi : Pole sana
Mama X: sasa?
Fundi: Ngoja nichomeke tena
Mama X: Yaan wewe, utaacha mme wangu afike hatujamaliza
Fundi: Usijali namaliza sasa hivi

Baada ya dakika chache, fundi akamuaga mama na kumwambia tayari, sasa naona umefurahi. Kutoka tu mlangoni akakutana uso kwa uso na jamaa amekunja ndita kama matuta ya viatu. Gues what happened?

Kitu gani kitatokea kisia toa maoni yako kama ni ww ungefanyaje?

Jinsi wigo wa mimea kwenye shamba unavyoweza kukinga mazao yako na wadudu waharibifu

Jinsi wigo wa mimea kwenye shamba unavyoweza kukinga mazao yako na wadudu waharibifu

Wigo wa mimea ni kinga nzuri ya mazao shambani. Mimea ya wigo inaweza kutumika kama kizuizi cha wadudu kuhama hama.

Wigo hutatiza vidukari kuhama na kuingia bustanini. Kwa mfano, mimea kama tithonia ni kizuizi kwa aina nyingi sana za wadudu.

Safu za mbaazi zimekuwa zikitumika kulinda nyanya, viazi, kabichi dhidi ya buibui wekundu.

Maharage yanaweza kupandwa kati ya mistari ya kabichi yakiwa kama mitego kwani yanasaidia kulinda kabichi dhidi ya buibui wekundu.

Maharagwe yanapandwa kama mtego kwenye kabichi lakini yanafanya kazi ya kudhibiti wadudu (mtego), kuboresha udongo, chakula cha mifugo, matandazo au kutengenezea mbolea.

Vile vile wigo wa mimea ni makazi ya wanyama/wadudu wanaowinda.

Maana halisi ya kuolewa au ya kuwa mke

NDOA sio kichaka cha kujificha kukimbia matatizo. NDOA sio mahali pa kutolea mkosi. Wala sio mahali pa kupunguzia shida. Ndoa sio mbadala wa elimu na michakato ya kimaisha. Huolewi ili kupunguza adha za maisha. NDOA ni jukumu zito kuliko hata kusoma masters degree ya Neuro-surgeon. Wengi hamjaweza kumudu maisha yenu binafsi na bado mnalilia Mungu kuwaongezea jukumu la kumeneji maisha ya mtu mwingine.

Kama huwezi hata kujitafutia hela ya kusuka nywele zako utawezaje kuendesha maisha ya familia. Maana unaweza kuolewa na mwanaume mwenye pesa lakini akapitia mithihani pesa zikatoweka utafanyaje kama huna akili ya kujiongeza? Ndio maana wengi mnawakataa watu wenye Ndoto lakini hawanapesa kwa sasa kwa sababu ya akili ya utegemezi. Unataka mwanaume mwenye kila kitu, sababu kubwa ni uvivu na uzembe. Hutaki kujitafutia vya kwako.
Ukisoma MITHALI 31 inaeleza habari za MKE MWEMA.

Hapo ndio pa kujipima je unakidhi hivyo viwango? Mke mwema sio tegemezi ila ni mwanamke mwenye uhuru wa kifedha (Financial Freedom). JIULIZE TU KAMA IKITOKEA HUJAOLEWA MIAKA MITANO IJAYO UTAKUWAJE? MAISHA YAKO YATAKUWAJE? UTAKUWA NA HALI GANI? Maswali kama haya yatakusaidia kujiongeza. Tafuta kitu cha kufanya hata kama Ndoa isipotokea leo isiwe mwisho wa maisha, Ndoto na maono yako. Siku hizi wanaume hawaulizi ukoo wanauliza UNAFANYA NINI?

Mtu anapiga hesabu akikuoa mkaunganisha nguvu mtafanya nini kwenye maisha. Sasa wewe kalia kubandika kope na kuchora kucha kutwa nzima huna shughuli ya kufanya huku ukingoja kuombewa upate Mume. Watu hawaoi mapambo wanataka Wake watakao tengeneza nao hatma zao. Pambo ni kwaajili ya Starehe lakini MKE ni kwaajili ya maisha. Sikupondi wala sio nia yangu kukuvunja moyo, nataka utoke hapo ulipo ujiongeze ili hata ukiingia kwenye Ndoa isijae visa na kuonewa. Pesa itakupa heshima, pesa inakupa sauti, hata Wakwe zako hawawezi kukunyanyasa ukiwa na pesa kwani wanajua watakosa vitenge.

Nataka nikwambie kweli, ukiwa na hela utachagua mwanaume wa kukuoa kwani wapo wengi ila kama umefulia, tegemezi kweli utaona wanaume ni wachache. Pata kitu cha kufanya, tengeneza milango ya kipato. Badala ya kukesha unaomba Mungu akupe Mume anza kuomba Mungu akupe uhuru wa kifedha, kama itakubidi kurudi shule rudi tu. Jiongeze usibaki hapo ulipo. Ni Yesu peke yake asiyebadilika (Hebrania 13) Lakini wanadamu wote lazima tubadilike kila kukicha tukihama hatua moja kwenda nyingine.

Mungu akufungue macho kuona kiini cha ujumbe huu na lengoF lake na wala usichukuliwe na upepo wa adui upindishao maana katika jumbe zenye kubadilisha maisha kama hii.

Kuolewa sio mwisho wa maisha, Mungu kwanza achukue nafasi kwenye maisha yako na akupe utoshelevu katika moyo wako kiasi kwamba uone hata bila Mume unaweza kuishi.

Mambo ya msingi kufahamu kuhusu Lishe

Nini maana ya lishe?

โ€ข Lishe yahusu mafunzo ya chakula na jinsi miili yetu inavyotumia chakula kamakichocheo cha ukuaji, kuzaana na utunzaji wa afya.
โ€ข Lishe inajumuisha mchakato wa utoaji virutubishi vinavyohitajika kwa afya, ukuaji, kuendelea na kuishi.

Umuhimu wa lishe bora

Lishe bora ni muhimu katika mambo yafuatayo

โ€ข Utoaji nishati ili kuishi, uwepo wa mwendo, utendaji kazi, na joto.
โ€ข Ukuaji, uendeleaji, ujengaji mwli, urejeshaji na utengenezaji wa seli na mikusanyika ya seli hizo (tishu)
โ€ข Ufanyaji michakato ya kikemia kama vile uyeyushaji chakula, umetaboli na utunzaji mwili.
โ€ข Kinga dhidi ya magonjwa, upigaji vita maambukizi na uponaji magonjwa.
โ€ข Ili afya njema iweze kudumishwa, mlo wa kila siku lazima ukamilishe shughuli nne zilizotajwa hapo awali. Vyakula vinavyokamilisha moja au zaidi ya shughuli tatu huitwa virutubishi.

Virutubishi

Aina za irutubishi vikuu tunavyohitaji kwa wingi. Hivi ni:

โ€ข kabohaidreti (vyakula vya wanga, sukari na vyakula vya ufumwele):
โ€ข mafuta yatokanayo na wanyama – haya yapo ya aina kadhaa
โ€ข Protini- kuna mamia ya aina mbalimbali za protini.
โ€ข Maji.

Virutubishi vidogovidogo tunavyohitaji kwa kiwango kidogo. Kuna aina nyingi ya hivi bali vile vinavyoelekea kukosekana kwenye mlo ni:

โ€ข madini โ€“ madini ya chuma (angalia Kisanduku cha 6, ukurasa 16), madini ya joto na zinki.
โ€ข vitamnini โ€“ vitamini A, vitamini za kundi B (ikiwemo folate) na vitamini C. Kama chakula chaweza kuwa chanzo bora cha kirutubishi au la hutegemea:
โ€ข Kiwango cha kirutubishi katika chakula. Vyakula vyenye viwango vingi vya virutubishi vidogovidogo kulinganisha na viwango vyake vya nguvu huitwa vyakula โ€˜vilivyosheheni virutubishiโ€™ (nutrient-rich) au wakati mwingine huitwa vyakula vyenye โ€˜ujanzo mwingiโ€™ wa virutubishi (nutrient dense). Vyakula hivi hupendwa kwa kuwa hutoa virutubishi vyote vinavyohitajika. Kiambatisho hiki kinaorodhesha vyakula vinavyotoa viwango muhimu vya virutubishi mbalimbali.
โ€ข Kiwango cha chakula kinachotumika mara kwa mara.

Sababu ya meno kubadilika rangi

Wapo baadhi ya watu wanashindwa hata kuachia kicheko chenye bashasha hii ni kwa sababu meno yao yamekuwa na rangi, hivyo kuwafanya watu hao kuona aiabu. Pia watu wengi wakiona meno yana rangi ya njano hudhani ni machafu, meusi yanahitaji kusafishwa ili yawe meupe.

Meno kubadilika rangi huweza kuwa ni sababu moja au muunganiko wa sababu mbalimbali kama ifuatavyo;

Matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye kaboni, sigara na mvinyo (wine) kwa muda mrefu husababisha kubadilika kwa rangi ya meno kwa juu (extrinsic staining).

Utumiaji wa maji yenye madini mengi ya fluoride katika kipindi cha utoto (dental fluorosis).

Matumizi ya dawa aina ya tetracycline kwa mama mjamzito ambaye tayari meno ya mtoto aliye tumboni yameanza kuumbwa lakini hayapata madini ya kutosha.

Maumbile yasiyo sahihi ya sehemu ya juu ya jino (amelogenesis imperfecta). Iwapo sehemu hii imeumbwa ikiwa laini kuliko inavyotakiwa huwa rahisi kufyonza rangi na jino huota likiwa limebadilika rangi au hubadilika baada ya muda.

Kufa kwa sehemu hai ya jino hasa kutokana na kuumia kwa jino au ajali (pulp necrosis), hali hii huweza huchukua miaka mingi mpaka kutokea kubalika rangi ya jino..

Jino liliozibwa kwa kutumia material aina ya amalgam huweza kubadilika rangi na kuwa nyeusi.

Mara nyingne jino lililotibiwa kwenye mzizi wa jino (root canal treatment ) huweza kubadilika rangi baada ya miaka mingi.

Kuna njia mbalimbali ambazo hutumika kuyafanya meno yaliyo na rangi isiyo ya kawaida kuwa meupe.

Njia hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu kutokana na jinsi alivyoathirika. Kuna njia nyingi ambazo huweza kuyangโ€™arisha kwa ndani (internal bleaching) au kuyangarisha kwa nje (external bleaching).

Endapo una tatizo la meno yaliyobadilika rangi, muone daktari wa kinywa na meno kwaajili ya ushauri na matibabu kwani kinywa kizuri na chenye afya huongeza kujiamini.

Mapishi ya Wali Wa Karoti Na Kuku Wa Kukaanga

Vipimo Vya Wali

Mchele wa Basmati/Pishori – 1 kilo moja

Vitunguu maji – 3

Karoti – 2

Siagi – 3 vijiko vya supu

Kidonge cha supu (stock) – 1 kimoja

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

ร“sha mchele uroweke kama saa moja au mbili
Katakata vitunguu vipande vidogodogo (chopped) weka kando.
Kwaruza karoti (grate) weka kando.
Tia siagi katika sufuria ya kupikia wali, weka katika moto iyayuke
Kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi kiasi tu.
Tia maji kiasi ya kupikia wali, changanya na kidonge cha supu.
Yakichemka tia mchele, koroga, funika uweke moto mdogo mdogo.
Kabla ya maji kukauka tia karoti changanya wali kisha funika uive kama unavyopika pilau.

Vipimo Vya Kuku Wa Kukaanga

Kuku alokatwakatwa – 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa – 2 vijiko vya supu

Bizari ya mchanganyiko/garam masala – kijiko cha supu

Mtindi/Yoghurt – 1 kijiko cha supu

Ndimu – 1

Chumvi – kiasi

Mafuta ya kukaangia – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Ukishamuosha kuku, mchuje atoke maji yote.
Changanya viungo vyote katika kibakuli kidogo.
Changanya pamoja na kuku kisha acha akolee viungo (marinate) kwa muda wa masaa mawili takriban.
Weka mafuta katika karai na kaanga kuku, akiwiva yu tayari kuliwa na wali.

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About