Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Askari na yeye kumbe muoga, cheki anachomjibu afande

Askari wametumwa nyumba iliyokuwa kuna ugomvi wakafika wakatakiwa kuripoti kwa njia ya simu juu ya walichokikuta
ASKARI: Mkuu tumekuta mama mwenye nyumba kampiga mumewe chuma cha kichwa na kumuumiza vibaya sanaa

AFANDE: Kha! kisa mkasa mpk akafanya hivyo
ASKARI: Mama mwenye nyumba alikua anapiga deki mumewe akaingia ndani viatu kabla sakafu haijakauka
AFANDE: Sasa mmesha mkamata huyo mwanamke
ASKARI: Bado mkuu
AFANDE: Kha! sasa mnangoja nini
ASKARI: Si tunangoja sakafu ikauke

Dondoo muhimu kwa Afya yako unapostuka usiku

Kumekuwepo na tatizo la vifo vya ghafla sana tena kwa watu ambao wana afya njema na hii inatokana na kuamka ghafla usiku ambapo ubongo hukisa damu ya kutosha.

Unapoamka katikati ya usiku kwenda kujisaidia haja ndogo mfumo wa damu unakuwa umebadilika. Kwa sababu kuamka ghafla,kinakuwa hakuna mzunguko wa kutisha wa damu kwenye ubongo unaosababisha moyo kushindwa kufanya kazi kutokana na ukosefu wa damu.

Ushauri:tumia dakika 3 na nusu kufanya yafuatayo”:

1. Unapoamka usingizini lala kitandani kwa nusu dakika ;
2. Kaa kitandani kwa takribani nusu dakika;
3. Shusha miguu,kaa pembeni ya kitanda takribani nusu dakika.

Baada ya dakika 3 na nusu hutakuwa na tatizo la ukosedu wa damu kwenye ubongo na moyo kushindwa kufanya kazi inapunguza uwezekano wa vifo vya ghafla na kuanguka ghafla.

Shirikisha marafiki na jamaa.

Inatokea bila kujali umri.

Kushare ni kujali.Kama tayari ulikuwa unajua hili lichukulie kama kumbukumbu.

Mungu ni zaidi ya Mzazi na upendo wake ni zaidi ya wa Wazazi

Wakati wazazi waliweza kuaamua kuzaa mtoto tuu, Mungu yeye alikuchagua wewe utungwe mimba na kukulinda ungali tumboni mwa mama yako….Wakati wazazi wanasubiri kwa shauku kuona muonekano wako wewe, Mungu anawaweka wajukuu wa wazazi wako/ watoto wako ndani mwako…. Wakati wazazi wakitafuta chakula kwa ajili yako, Mungu yeye aliwawezesha kukipata…. Wakati wazazi wakingoja kuona unavyoendelea kukua huku wakiwaza hatima ya maisha yako Mungu anakuendeleza na alishapanga maisha yako tangu alipokuchagua uwe mtu ukiwa tumboni mwa mama yako…. Wazazi wanaweza kukuombea kwa Mungu lakini Mungu ndiye anayeamua akufanyie nini maana Wewe ni wa kwake….Wewe na wazazi wako ni watoto wa Baba mmoja ambaye ndiye Mungu.

Hizi hapa, Aina 10 za ndoa usizozijua

Karibuni tuangalie aina hizi 10 za ndoa.

1. NDOA YA MKEKA

Inatokana na kufumaniwa na Binti wa watu.
Ndoa hii huwa Haina mahari. Hii huvunjika
mwaka mmoja tu,baada ya wanandoa kugundua
hawakuwa wakipendana!

2. NDOA YA MIHEMKO (NYEGE)

Hufungwa na vijana wenye umri wa miaka kati
mume18 mke 16.Huvunjika baada ya miaka 3 au
4 ya ndoa.

4. NDOA YA MAONYESHO

Wenye ndoa Hii hupenda kujionyesha
barabarani.Ila ndani hazina utii.Hupigana kila
wanaporudi kutoka kwenye mizunguko. Cha
kushangaza huwa hazivunjiki lakini ndiyo ndoa
zinazoongoza kwa kuchepuka!

5. NDOA YA UHAMISHO.

Hufungwa na watumishi wa vijijini na mjini. Ili wa
kijijini ahamie mjini.Mahari utoa anaetaka
kuhamia mjini. Hata kama mahari atatoa mume
lakini hii ndiyo ndoa yenye ukakasi
zaidi.Huvunjika mara tu wanapoanza kuishi wote
mjini. Salama ya hii ndoa ni kuhama kutoka mjini
kwenda kijijini.

6. NDOA YA MIMBA.

Hufungwa kwa sababu wanaoowana hawataki
kuonekana makwao kuwa wamezaa nje. Au
muolewaji alikuwa hampendi muoaji kwa
dhati.Muoaji hutumia mimba kama mtego wa
kuingia ndoani. Hii huvunjika mtoto akizaliwa na
kufikisha mwaka 1.

7. NDOA YA MALI (UTAJIRI)

Muolewaji miaka 18 au 28 Muoaji 65 au 70.Ndoa
hii pia huitwa ndoa ya babu na mjuukuu. Ndoa ya
aina hii hudumu, kwasababu mwenye kauli ni
mwenye mali. Asilimia kubwa ya waume wa ndoa
hizi hulea watoto wasio wao.

8. NDOA YA KWASABABU.

Hufungwa ili mradi muoaji au muolewaji
aonekane tu kwa jamii kuwa naye kaoa au
kaolewa.Huwa hazina utii wala upendo dhati.
Ndoa ya aina hii ikifikisha miaka 4 huwa
hazivunjiki wahusika huishi kwa mazoea.

9. NDOA YA UPENDO.

Ndoa hizi ziliishia mwaka 1978 kabla ya vita vya
kagera.Muoaji na muolewaji hawakuangalia vitu
ila utu tu ambao uliwaunganisha na kutengeneza
upendo wa kudumu. Hii ilidumu miaka yote.

10. NDOA KUCHUMA

Ndoa hii ufungwa ili mradi muoaji au muolewaji
akapate kitu au vitu fulani kutoka kwa upande
mmoja wapo. Hii hudumu miaka kadhaa
kutegemea na malengo ya mhusika. Wengine
husubiri mpaka mhusika afe,lkn hujikuta
wanakufa wao kwanza.
Kuwa mwangalifu!

Faida za kutumia mafuta ya Nazi

Mafuta ya nazi hung’arisha ngozi:

Siyo sehemu za ndani tu ya mwili zinazofaidika na mafuta haya ya nazi kama yanavyofanya mafuta mengine ya asili, kama unataka kuwa na ngozi nzuri yenye mng’aro na yenye afya na yenye muonekano wa asili basi paka mafuta ya nazi kila siku kwenye ngozi yako, mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa katika kuua bakteria, virusi, na vijidudu vya aina yeyote vinavyoweza kuidhuru ngozi, haya ni mafuta kwa mwili mzima yaani pakaa kwenye ngozi yote usoni, mwilini, kwenye nywele na kwenye kucha. Pia unaruhusiwa kuyatumia mafuta haya wakati wa masaji.

Huongeza nguvu mwilini:

Mafuta ya nazi ni chanzo kizuri cha nguvu ya mwili kwani yana sifa ya kuelea kwa kiasi kidogo kwenye damu ‘medium chain triglycerides – MCT’ ambapo sifa hii huyafanya kusafirishwa moja kwa moja hadi kwenye ini ambako hutumika kama chanzo cha haraka cha nguvu au hubadililishwa kuwa ‘ketones’ ambacho ni chakula cha ubongo. Kwahiyo ikiwa unatafuta lift ya kuinua nguvu yako basi chukua kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya nazi weka kwenye kikombe chako cha juisi au uji na utaona maajabu.

Hutumika kulainisha uke mkavu:

Mafuta ya nazi yana matumizi mengi sana mwilini zaidi ya 100, kuna wanawake wana tatizo la kuwa na uke mkavu muda wote hata wakisisimuliwa vipi bado huwa wakavu, kuondokana na tatizo hilo pakaa mafuta ya nazi katika uke wako na utaona faida yake tena bila madhara yeyote hasi.

Husaidia katika ugonjwa wa mzio/aleji:

Tukisema tuelezee faida zote za mafuta ya nazi kwa hakika hatutaweza, moja ya faida zake zinazoshangaza wengi ni uwezo wa kudhibiti dalili za ugonjwa wa aleji, kila siku pakaa mafuta ya nazi ndani ya pua zako na uone kama utapiga chafya unapokuwa karibu na kile kinachokuletea aleji/mzio.

Ni mafuta mubadala ya kupikia yenye afya:

Tofauti na mafuta ya alizeti au hata mafuta ya zeituni, kupika chakula kwa mafuta ya nazi ni zaidi ya afya. Mafuta haya yana uwezo mkubwa wa kuungua na bado yakabaki na viinilishe vyake kama kawaida hata baada ya kuunguzwa au kuchomwa katika moto, hii ni kwamba mafuta kama ya zeituni ambayo huweza kuliwa hata yakiwa mabichi lakini yanapochomwa katika moto basi ubora wake hupungua au kwa maneno mengine huzalisha taka sumu kama ilivyo kwa vitu vingi vinapounguzwa lakini hili halitokei kwa mafuta ya nazi!

Ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama:

Siyo kupika tu na mafuta ya nazi ndiko huleta afya, bali pia ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama kama mubadala kwa siagi au vitu vingine mnavyopaka juu ya mikate mnapokula. Hii nikwa sababu mafuta ya nazi hubaki kuwa magumu hata katika joto la kawaida la chumba tofauti na mafuta mengine.

Huzuia maradhi mengi hatari mwilini:

Kama ilivyo katika kuipunguza kolesteroli, mafuta ya nazi yanao uwezo mkubwa katika kuzuia na kutibu magonjwa mengine sababu ya kuwa na kiasi kingi cha asidi iitwayo lauric acid. Utafiti mwingi umeendelea kuthibitisha kuwa hii lauric asidi hubadilishwa kuwa asidi mafuta nyingine ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘monolaurin’ ambayo inayo sifa ya kudhibit na kuvizuia baadhi ya virusi ikiwemo vile vya ukimwi kuziingia na kuzidhuru seli za mwili na kusababisha maradhi mwilini. Ili kutibu virusi vya ukimwi inashauriwa kunywa glasi 4 za tui la nazi kila siku kwa muda wa miezi mitatu mine na utaona maajabu.

Hutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu:

Hii inaweza ikakushangaza kidogo unapoisikia kwa mara ya kwanza lakini tafiti nyingi zimeonyesha kuwa mafuta ya nazi yanao uwezo kuziamusha seli na shughuli za ubongo na katika kufanya hivyo kutasaidia kuzuia matatizo ya uwendawazimu au ukichaa (dementia) na kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Mafuta ya nazi kwa afya ya Moyo:

Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo ‘lauric acid’ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla. Lauric acid huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalamu kama High Density Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalamu wa lishe wa Lifesum.

Mafuta ya nazi huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula:

Hii ndiyo moja ya faida ya mafuta ya nazi niipendayo zaidi. Ndiyo mafuta ya nazi yanayo uwezo kusaidia kudhibiti uzito uliozidi kwa sababu mafuta haya ni mepesi kumeng’enywa na hayagandi kama yalivyo mafuta mengine mazito (fatty acids) jambo linalosaidia kuuondoa uzito uliozidi mwilini. Kutokana na kitendo hiki cha kuongeza uwezo wa mwili kukimeng’enya chakula, watu wanaoyatumia mafuta haya kupikia vyakula vyao kila siku kwa kawaida huwa na uzito wa kawaida. Anasema Geeta Sidhu Robb, mtaalamu wa lishe na mwanzilishi wa Nosh Detox.

MHIMU: Hakikisha unapata mafuta ya nazi ambayo ni ya asili kwa asilimia 100, ikiwa utanunua dukani kuna uwezekano mkubwa yakawa yamechanganywa na kemikali zingine au haidrogeni kitu kinachoyapunguzia thamani ile ya asili. Kama unapikia kwenye chakula najuwa wengi mnapenda wali wa nazi au hata tui lake likiwekwa kwenye samaki au hata mboga yoyote lazima utajing’ata ulimi, basi nakushauri usichanganye na mafuta mengine kwenye hicho chakula.

Namna ya kufanya Ukaguzi wa mara kwa mara wa banda la kuku kuzuia magonjwa

Ukaguzi wa Kila siku
• Hakikisha unasafisha vyombo vya kulishia na kunyweshea pamoja na viota.
• Ondoa kinyesi kwa kuku.
• Waangalie kuku wako kwa makini ili kujua afya na maendeleo yao. Yaani ili kutambua kama kuna mwenye ugonjwa

Ukaguzi Kwa wiki
• Ondoa matandazo machafu na kuweka mapya ili kuzuia kuzaliana kwa vijidudu vya magonjwa.

Ukaguzi kwaKwa mwezi
• Angalia uwepo wa wadudu na chawa, kisha utibu kama kuna ulazima.

FUNZO: Maisha ni kuchagua

Siku hizi kuna tangazo moja la kampuni ya simu za mikononi, Tigo, likimuonesha mama akiwa _busy_ na pembeni yupo mwanae mdogo apo akijisemesha na akatamka maneno ambapo mama akaona ni kama ameanza kuongea. Kwa furaha anampigia simu mumewe akimtaka amsikilize mwanae akiongea. Hapo mama anamtaka mwanae aseme “mama” na baba naye anavutia kwake akimtaka aseme “baba”. Kwa maajabu kabisa mtoto anawapotezea wote na kutamka “ni Tigo peesa”. Wazazi wakashikwa na butwaa lakini huku wakitabasamu.

Ukiitazama vizuri kazi ya ubunifu iliyotumika katika tangazo hili unaweza kupata funzo, pamoja na mengine, kwamba mtoto alikua na chaguzi lake ambalo ni tofauti na yale ambayo wazazi walikua wamempa. Lakini zaidi, pamoja na kuwa amekuwa na chaguzi lake binafsi, pasipo kufuata alichoagizwa na baba au mama, bado wazazi wanatabasamu kwani wanaona mwanao kafanya jambo jema.

👉Unaona unavyofanya kazi bila furaha kwa kua ulifanya chaguo la kazi hiyo kwa kusikiliza ndugu au marafiki.

👉Unaona unavyo _struggle_ katika biashara kwani halikua chaguo lako bali ni la ndugu au marafiki

👉Unakumbuka ulivyoshindwa kusomea kile unachopenda kwa kusikiliza ndugu au marafiki
9
👉Unakumbuka ulivyoshindwa kuishi na yule mwenzi uliyempenda na mkapendana naye kwa kusikiliza ndugu na marafiki

Unaweza kushauriwa, na ushauri ukawa ni mzuri kabisaa na ukaona ni vyema uufuate kwa kua hata wewe umeambiwa na ukachanganya na akili yako ukaona inafaa.

Jana nilitoa semina kwa wanafunzi wote wa Shule ya Sekondari Chang’ombe, pamoja na mambo mengine nikawataka kupima sana marafiki walio nao na kuona kama ni washauri wazuri na kama sivyo waachane nao na kuwa na marafiki wapya wenye mawazo chanya ya kuwasaidia kutimiza ndoto zao.

Kuna hii daladala imeandikwa nyuma *_Marafiki wengi mjini hasara_*. 😃. Mie nakuambia sio marafiki tu, hata ndugu pia. Kikubwa ni kuwapima wale ulio nao karibu na kuona kama bado ni wa msaada kwako. Wapime na chukua hatua. Kumbuka Mheshimiwa JK aliwahi kutuasa ” _Akili za kuambiwa, changanya na za kwako_ “.

Alichokifanya jamaa baada ya kuokota wallet yenye pesa za kumwaga

Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station

“Naitwa John nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki 7, ATM Card na kikaratasi chenye PIN ya ATM Card na kijimkufu cha dhahabu kinene hivi…”

Mtangazaji akasema:- Akhasante sana John, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama ana kusikiliza akutafute kwa No. Gani!?

John: Hapana, mi nilikuwa namshukuru tu maana amenitoa kwenye matatizo na ninapenda kumuombea Dedication wimbo wa Snura “MAJANGA” umfikie popote pale alipo…!!!

Majibu ya mkato ya kuchekesha Kutoka Kenya

Njeri: Roysambu ni ngapi?
Makanga: Roysambu ni moja tu. Pengine kama Chinese wamejenga ingine.

Odhis: Hii gari haina watu bana.
Makanga: Kwani hao wawili wenye wamekaa hapo ndani ni ng’ombe?

Man: Wekeni nyimbo za Yesu tafadhali.
Makanga: Yesu bado hajatoa album. Akitoa tutaeka.

Mwikali: Excuse me conda…gari za Mwingi zinapandiwa wapi?
Makanga: Ziliacha kupandwa juu hazimei.

Man: Kwani mwisho wa gari ni wapi?
Makanga: Mwisho ni hapo penye number plate iko.

Karis: Ruaka ni how much?
Makanga: Sijaskia Ruaka ikiuzwa. But nikiskia nitakwambia.

Passenger: Shukisha dere.
Makanga: Tukishukisha dere utaendesha gari?

Johnny: Maze, hii gari iko na joto sana.
Makanga: Basi shuka upande fridge

Umeshawahi kufanya hili jaribio?

Figisu ya Leo. UMESHAWAHI KUFANYA HILI JARIBIO.?

kadri temperature inavyo ongezeka chura nae huwa ana increase temperature ya mwili wake..

pindi inapokaribia kufika boiling point yaani nyuzi 100 chura atashindwa kuongeza temperature ktk mwili wake na hapo ndipo atataka kutoka ktk maji hayo ya moto na yanayo endelea kuchemka..
kutokana na kutumia nguvu nyingi sana ktk kuongeza temperature ktk mwili wake,pindi anapotaka kuruka atashindwa na atakufa humo ndani ya chombo cha maji yanayochemka..
SWALI; NINI KIMEMUUA CHURA.!??
Najua utaniambia ni maji ya moto…
La hashaa.!
kilichomuua chura ni kushindwa kufanya maamuzi mapema ya kutoka katika chombo cha maji yanayochemka hali ya kuwa bado nguvu anazo..
FUNZO
Fanya maamuzi sahihi sasa kabla nguvu za kutaka kufanya changes hazijakuishia kama yaliyomkuta chura..
NOTE; Kuvumilia jambo usiloliweza ni sifa ya punda.
BADILIKA.

Mambo muhimu kujua Kuhusu Uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke

Naamini umeshawahi kusikia kuhusu changamoto ya uvimbe kwenye kizazi kwa Wanawake yaani Fibroids. Uchunguzi unaonesha kuwa kati ya asilimia 30 mpaka 70 ya wanawake wapo kwenye hatari ya kupata tatizohili au wengine Tayari wameshalipata. Mpaka hivi sasa hakuna Sababu ya moja kwa moja ambayo inaelezwa kama chanzo cha tatizo hili.

JE NI NANI YUPO HATARINI ZAIDI KULIPATA UVIMBE KWENYE KIZAZI?

Ni Wanawake ambao wanakaribia kukoma hedhi (Menopause) hasa wa kati ya miaka ya 38-45.
Pia Wanawake wanene au wenye Matumbo makubwa (Obesity)
Pia wanawake wasiokuwa na watoto wapo kwenye hatari zaidi ukifananisha na wale wenye Watoto.

DALILI ZA UVIMBE KWENYE KIZAZI NI ZIPI

Tatizo hili linaweza kuwa na Dalili au Kutokuwa na Dalili kabisa. Lakini kwa mara nyingi Dalili zake ni hizi…

👉🏿Kutoka kwa Hedhi nzito pia kwa muda zaidi ya kawaida.
👉🏿Damu kutoka kipindi ambacho sio cha siku zake.
👉🏿Maumivu ya Sehemu za Kiuno.
👉🏿Maumivu ya Chini ya Mgongo.
👉🏿Kwenda haja ndogo mara nyingikwa hali isiyo ya kawaida.
👉🏿Maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Sio lazima uwe na Dalili zote na mara nyingi hazitokei zote hasa ni moja au mbili.

Hivyo Kujikinga au kuepukana na Tatizo hili ni vyema kwa Mwanamke ukapungua Uzito hasa Kitambi au Tumbo kubwa.

Kilichotokea baada ya mzungu na mbongo kukaa siti moja, bongo wasanii wengi

Mzungu akamdharau sana Mbongo nakujiona anajua kila kitu duniani!,
Akamwambia Mbongo waulizane maswali na Mbongo akishindwa anatoa sh.500 na endapo yeye atashindwa atatoa 100,000/=.
Mzungu akauliza ni nchi ipi ilishindwa kwenye vita kuu ya kwanza ya Dunia?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hajui.

Na yeye akamuuliza Mzungu ni kitu gani kikienda juu kina miguu minne na kikirudi chini kina miguu mitatu?

Mzungu akafikiria akakosa jibu akatoa 100,000/= kuashiria hajui ila akataka kujua, akauliza ni nini hicho?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hata yeye hajui!.

SHARE na marafiki kama umemkubali Mbongo kwa ujanja. Lakini unafikiri Mbongo huyu kwa akili hizi atakuwa ametokea mkoa gani!?.

Mapishi ya Ugali Kwa Mchuzi Wa Nyama, Mchicha, Maharage Na Chatini Ya Pilipili Mbichi

Vipimo Vya Mchuzi Wa Nyama

Nyama ya ng’ombe vipande vidogo – 2lb

Nyanya – 1

Kitunguu Kilichoktwa katwa – 1

Mafuta – 2 vijiko vya supu

Paprika (bizari ya masala ya rangi) – ½ kijiko cha chai

Kidonge cha supu – 1

Chumvi – Kiasi

Ndimu – Kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha nyama kwa chungio ili itoke maji. Kwenye sufuria, weka mafuta na ukaange vitunguu mpaka viwerangi ya hudhurungi.
Kisha tia nyama na kidonge cha supu uwachie moto mdogo mpaka iwive.
Halafu tia nyanya na paprika ufunike sufuria na uiwache motoni mpaka ikauke, kamulia ndimu na itakuwa tayari.

Vipimo Vya Mboga

Mchicha ulio katwa katwa 400 gm

Nyanya 1

Kitunguu kilicho katwa 1

Nazi ya unga kiasi

Pilipili mbichi 2

Mafuta ½ kijiko cha supu

Chumvi kiasi

Namna Ya Kutayarisha na Kupika

Osha mboga vizuri mpaka iwe haina mchanga.
Katika sufuria, kaanga vitungu hadi viwe laini.
Tia nyanya, mboga, pilipili na chumvi ikisha toa maji
Tia nazi na utaiwacha motoni mpaka ikauke kiasi na itakuwa
tayari kuliwa

Vipimo Vya Maharage

Maharage – 1 kopo

Kitunguu – 1

Nazi – 1 mug

Nyanya (itowe maganda) – 1 kiasi

Pilipili mbichi – 2

Mafuta – 1 kijiko cha supu

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na kupika

Tia mafuta katika sufuria na ukaanga vitungu mpaka vilainike.
kisha tia nyanya na pilipili na ukaange kidogo.
Tia chumvi, maharage na nazi uwachie
moto mdogo mpaka iwe nzito kiasi na itakuwa tayari.

Vipimo Vya chatini Ya Pilipili mbichi

Pilipili mbichi – 4/5

Kotmiri – 1 Kijiko cha supu

Ndimu – kiasi

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 1 chembe

Mafuta ya zaituni – 2 vijiko Vya supu

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha

Kwenye blender, tia vipimo vyote na sage isipokuwa chumvi tia mwisho kwa juu kwenye bakuli na itakuwa tayari kwa kuliwa.

Vipimo Vya ugali

Maji – 4 Vikombe kiasi inategemea na unga

Unga wa sembe – 2 vikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Tia maji kiasi katika sufuria, weka motoni, yakipata moto korogea unga wa sembe kiasi na ufanye uji mzito uache uchemke vizuri huku ukikoroga.
Chota kibakuli kimoja cha uji huo weka pembeni kisha mimina unga wote uliobaki upigepige uchanganyike vizuri kwenye uji huo mpaka ushikamane
Punguza moto anza kuusonga taratibu huku ukiongeza ule uji ulioweka pembeni kidogo kidogo mpaka uone sasa umeshikamana vizuri.
Endelea kusonga mpaka ulainike kisha mimina kwenye bakuli au sahani na itakuwa tayari kwa kuliwa na mchuzi wa nyama, maharage, mboga na chatini.

Nini kinachokufanya udhani utashindwa sasa?

Kwa mujibu wa Biologia, baada ya tendo la kukutana kimwili takribani mbegu milioni 200 hadi 300 hutolewa na mwanaume…halafu zote huanza kupiga mbizi kuogelea kwenye njia safarini kukutana na yai la kike.

Ajabu ya kwanza ni kwamba sio zote 200 – 300 ambazo hufanikiwa kulifikia yai( nyingi huchoka na kufia njiani maana si mashindano ya mchezo mchezo).
Ajabu ya pili ni kwamba kati ya hizi 300 zinazofanikiwa kufikia yai, ni moja tu..moja tu itakayoshinda nakufanikiwa kupenya na kurutubisha yai, na kwa mantiki hii ILIYOSHINDA NI WEWE HAPO.

Umewahi kuwaza kuhusu hili vizuri?
Yaani ulishindana mbio hizo ukiwa huna macho na ulishinda, ulishindana bila elimu na ukashinda,ulishindana bila hata cheti chochote wala msaada wa yeyote ….na UKASHINDA.

Nini kinachokufanya udhani utashindwa sasa?
Tena sasa uko na macho yote, miguu, sasa Unamjua Mungu, sasa ukiwa na mipango,ndoto na maono.
Kumbuka ULISHASHINDA toka tumboni huna sababu ya kuwa na hofu yeyote, PAMBANA

Maswali na Majibu kuhusu Sala

Sala ni nini?

Sala ni kuinua mioyo yetu kwa Mungu na kuongea nae. Kuongea maana yake ni kusema na Kusikiliza. Sala sio kuongea tuu, sala ni kuongea na kusikiliza. Mungu anatualika tuongee nae kwa kusema na kusikiliza. Kwenye Biblia tunasoma Hivi;
“Niite, nami nitakujibu na kukuambia mambo makubwa yaliyofichika ambayo hujapata kuyajua”.(Yeremia 33:3)
Vile tunavyokuwa na juhudi ya kusali kwa kusema mbele ya Mungu ndivyo hivyo hivyo tunatakiwa tuwe na juhudi ya kumsikiliza Mungu kile anachotuambia.
Tunaweza kumsikiliza Mungu ndani kabisa ya Mioyo yetu, mara nyingine kwa kupitia dhamira zetu, kupitia watu wengine na kupitia neno lake (Biblia). Tuombe neema ya kutambua sauti yake anaposema nasi ili tuweze kumsikiliza na kutengeneza mahusiano mazuri kati yetu na yeye.
Mungu ni Baba yetu, anatupenda sana na yupo tayari kutusikiliza wakati wote ndio maana Mungu anatualika kwa kutuambia;
“Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu”. (Isaya 1:18)
Tudumu katika sala daima kwa sababu njia ya sala ndipo tunaweza kusema yale tunayotaka mbele ya Mungu na kusikia yale anayotaka Mungu.


Kwa nini tunasali?

Tunasali ili kudumisha mahusiano yetu na Mungu na ili kutimiza wajibu wetu Mbele ya Mungu. Sababu kuu za kusali ni;
  1. Kumwabudu Mungu,
  2. Kumshukuru Mungu,
  3. Kuomba neema na baraka kwa ajili yetu na wenzetu,
  4. Kuomba msamaha,
  5. Kumsifu na kumtukuza Mungu

1. Kumwabudu Mungu

Tunasali ili kumwabudu Mungu, yaani kumpa heshima ya mwisho juu ya kila kitu. Kuonyesha kuwa ni mkuu na wa kipekee kuliko mtu au kitu chochote.

2. Kumshukuru Mungu

Tunasali ili kumshukuru Mungu kwa yale yote aliyokwisha kuyatenda, anayoyatenda na yale atakayoyatenda. Tunamshukuru Mungu kwa yote kwa kuwa yote anayoyafanya anayafanya kwa Mapenzi/ Matakwa yake Matakatifu. Nia ya Mungu ni njema daima ndio maana tunapoona ameruhusu mambo ambayo kwa akili zetu tunayaona ni magumu na sio mema tunapaswa kushukuru kwa sababu ameyafanya kwa makusudi mema.
Biblia inatuambia hivi;
16 Furahini siku zote; 17ombeni bila kukoma; 18shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. (1 Wathesalonike 5:16-18)
Tunatakiwa kumshukuru Mungu kwa Kila jambo na kumshukuru huku ni kwa njia ya sala.

3. Kuomba neema na baraka kwa ajili yetu na wenzetu

Tunasali kwa kuomaba neema na baraka kwa ajili yetu sisi wenyewe na kwa ajili ya wenzetu. Tunamuomba Mungu baraka na Mkono wake katika yale tunayoyafanya na kwa yale wanayoyafanya wengine.
Maombi yetu ili ykubalike mbele ya Mungu ni lazima yawe katika mapenzi yake na yawe na nia njema. Tunafundishwa hivi katika biblia;
3Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu. (Yakobo 4:3)
Tunatakiwa tusali kwa kuomba mema na kwa nia njema ili tuweze kupata yale tunayoyaomba kwa Mungu.

4. Kuomba Msamaha

Tunasali ili kuomba msamaha mbele ya Mungu kwa yote mabaya tuliyoyafanya. Mungu ni mwaminifu hasa kwenye kutusamehe na kutuondolea dhambi zetu.
9Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. (1 Yohana 1:9)
Vilevile Tunatakiwa kusali katika mapungufu yetu na kuwa na matumaini.
9Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. (2 Wakorinto 12:9)

6. Kumsifu na kumtukuza Mungu

Tunasali ili kusifu na kumtukuza Mungu. Mungu anapenda kusifiwa na kutukuzwa. Kwa njia ya sifa tunapokea neema na baraka hata ambazo hatujaziomba.
1Mfanyieni BWANA shangwe, dunia yote;
2Mtumikieni BWANA kwa furaha;
Njoni mbele zake kwa kuimba;
3 Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu;
Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake;
Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
4Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru;
Nyuani mwake kwa kusifu;
Mshukuruni, lihimidini jina lake;
5 Kwa kuwa BWANA ndiye mwema;
Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake vizazi na vizazi. (Zaburi 100:1-4)


Nani anapaswa kusali?

Watu wote wanapaswa kusali, wema na wabaya. Sala ndiyo njia pekee ya kumuunganisha Mwanadamu na Mungu. Tunapaswa kusali Katika hali yoyote. Tunapokuwa katika hali ya neema tunapaswa kusali vivyo hivyo tunapokuwa katika hali ya dhambi tunapaswa kusali.
Tunapokuwa katika hali ya neema tunapaswa kusali. Tunasali ili tuweze kudumu katika hali ya neema. Hatupaswi kuacha kusali kama tunajiona hali yetu ya kiroho ipo vizuri. Hatupaswi kuacha kusali kama tumepata neema ya kusimama vyema mbele ya Mungu.
Tunapokuwa katika hali ya dhambi tunapaswa kusali. Tunasali ili tuweze kurudi katika hali ya neema. Hatupaswi kuacha kusali kama tunajiona tupo katika hali ya dhambi. Kwa njia ya sala ndipo tutakapoweza kutoka katika hali ya dhambi.
Mungu yupo tayari kusikiliza ukiwa katika hali ya neema au kama ukiwa katika hali ya dhambi. Ndio maana tunapaswa kumwelekea Mungu katika hali yoyote tulio nayo.
14Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. 15Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba. (1 Yohane 5:15)
Tena Mungu anasubiri tumuombe ili furaha yetu itimilike.
24Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. (Yohane 16:24)
Hata kama tuna dhambi Mungu yupo tayari kutupokea na kutusikiliza.
“Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu”. (Isaya 1:18)
Mungu yupo tayari kutusikiliza hata tunapokuwa wadhambi kwa kuwa haziweki dhambi zetu na makosa yetu mbele yetu. Huruma yake ni kubwa kushinda dhambi zetu.
12 Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,
Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.
13 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake,
Ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao. (Zaburi 103:12-13)
Mungu anatuwazia mema daima ndio maana tunapaswa kusali kwake
11Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. 12Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. 13Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. (Yeremia 29:11-13)


Yatupasa kusali lini?

Yatupasa kusali kila siku bila kukata tamaa (Lk 18:1) Sala ndiyo njia pekee ya kutuunganisha na Mungu.
Tunatakiwa tusali daima Kama Yesu alivyotuhimiza kwa mfano huu;
1 Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.
2 Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu.
3 Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu.
4 Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu,
5 lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima.
6 Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu.
7 Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?
8 Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani? 
(Lk 18:1-8)
Kwa hiyo basi, Tusali daima kila siku, kila saa na katika hali yoyote. Tusichoke kusali hata kama maombi Yetu hayajajibiwa. Mungu ni mwenye Hekima na anajua lini hasa akujibu kile unachokiomba kwa manufaa yako wewe. Usipopewa Leo kile ukiombacho unaweza kukipata kwa wakati ufaao tena bila ya Kukiomba.

Sala ni Hazina

Sala ni hazina. Kusali ni kujiwekea hazina. Sala unayosali leo inaweza kukunufaisha wakati usioutarajia.

Maana ya Sala kwa Mkristo Mkatoliki

Maana ya sala kwa Mristu Mkatoliki sio kuomba tuu. Sala kwa Mkatoliki ni zaidi ya kuomba. Kwa Mkatoliki sala inamaanisha kufanya haya;
  1. Tunasali kushukuru,
  2. Tunasali kuomba,
  3. Tunasali kusifu na Kutukuza,
  4. Tunasali kumshirikisha Mungu Furaha zetu na huzuni zetu,
  5. Tunasali kuomba Toba na Msamaha,
  6. Tunasali kumshirikisha Mungu Juhudi zetu na Mipango yetu,
  7. Tunasali kumshirikisha Mungu changamoto zetu.
Tuna kila sababu ya Kusali kila Siku na Kila saa. Maisha yetu yote yanatakiwa yawe Maisha ya Sala. Usifikiri kwamba Wakati wote unaposali lazima utamke maneno Mengi sana ili uwe umesali, Sala haipimwi kwa Maneno. Sala inapimwa kwa nia yake na Kujiweka wazi mbele ya Mungu.
Kila Usalipo Jijengee Tabia ya kunuia, kuwa wazi na kusali kwa ukweli wa Moyo wako. Hata kama ni sentesi Moja fupi Kabisa itamke kwa Upendo na Imani. Kwa Mfano, kuna wakati inatosha kabisa kusema Ee Mungu wangu ninakushukuru kwa hili, hii inaweza kuwa sala Yenye nguvu Kama imetamkwa kwa Imani, Shukrani na Mapendo ya Kweli. Maneno machache yanayotamkwa kwa Imani na Mapendo yanaweza kuzidi Mkesha wa Kusali Usiku Mzima huku unasinzia.
Pamoja na kwamba sala fupi ni nzuri na inafaa sana, kuna haja pia ya kujitengea Muda wa Kutosha Kusali na Kutafakari Huku tukiungana na Mungu. Kila siku tunanye mambo yote mengine lakini tusisahau kuwa Tunahitaji kuwa na Muda wa Kusali.
Tusali daima, Kila wakati na Maisha yetu yawe ni Maisha ya Sala.
Mungu Akubariki sana, Azijibu sala zako na Akujalie Neema ya Kuwa Mtu wa Sala.


Yatupasa kusali namna gani?

Yatupasa kusali kwa Unyenyekevu, Ibada, Matumaini na kwa Saburi. Yesu alitufundisha kuhusu kusali kwa kutumia mfano huu;
9 Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote.
10 Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.
11 Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.
12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote.
13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
14 Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa. 
Luka 18:9-14
Tunatakiwa tusali kwa nia njema na kwa kufuata Mapenzi ya Mungu ili sala zetu zipate kibali mbele za Mungu. Tunapoomba kwa nia mbaya ya tamaa na majivuno hatuwezi kupata kile tukiombacho.
3Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu. Yakobo 4:3
Mungu anajibu sala zetu kulingana na nia ya kile tunachokiomba. Watu wote waliofanikiwa Katika sala zao walifanikiwa kwa sababu ya nia ya kile walichokiomba.
Sala sio kutamka manano tuu, sala ni kutamka maneno kwa kunuia. Tena tusalipo yatupasa kujua kuwa tunaongea na Mungu na sio tuu kwamba tunatamka maneno. Tusisahau nia kuu ya kusali ambayo ni mawasiliano Yetu na Mungu.
Tunaposali Tunapaswa Kukumbuka na kuzingatia haya;
  1. Nia na Imani (Kuamini na Kuwa na Uhakika na Unachokifanya)
  2. Unyenyekevu wa Kweli
  3. Ibada na Uchaji
  4. Upendo na Uwazi (Honest)
  5. Matumaini na Saburi (Subira)
Kila unaposali jiulize unasali kwa kwa sababu gani? Kila ubapoomba, jiulize unamuomba Mungu ili nini? Sababu yako ndio kibali cha sala yako.
Mungu Akubariki kwa Kukujalia Imani, Unyenyekevu, Ibada, Uwazi na Matumaini Usalipo. Uwe na Amani.


Sala zipo za namna ngapi?

Sala zipo za namna tatu,
1. Sala ya sauti
2. Sala ya fikara
3. Sala ya taamuli


Sala ya Taamuli ni nini?

Sala ya taamuli ni sala ya kumtazama tuu Mungu kwa upendo mkubwa moyoni


Sala ya sauti ni nini?

Sala ya sauti ni sala asaliyo mtu au kundi kwa kutamka maneno


Sala ya fikara ni nini?

Sala ya fikra ni sala asaliyo mtu peke yake au akiwa na wengine kimya kimya akimuwaza Mungu


Sala ya kanisa ni nini?

Sala ya kanisa ni sala maalumu wasaliyo Maklero, Watawa, na Walei kwa ajili ya Kanisa zima


Ni nyakati gani zafaa kwa sala?

Nyakati zote zafaa kwa sala hasa:
1. Asubuhi na jioni
2. Kabla na baada ya kula
3. Kila Dominika
4. Sikukuu za amri
5. Kabla na baada ya kazi
6. Katika kishawishi


Yesu alitufundisha sala gani?

Yesu alitufundisha sala ya Baba Yetu (Mt. 6:9-13)


Je, yatupasa kuombea wengine?

Ndiyo. Yatupasa kuwaombea watu wote hasa wenye shida, wakosefu na hata maadui zetu.


Vyanzo vya sala za Kikristo

Vyanzo vya sala za kikristo ni;
1. Neno la Mungu
2. Litrujia ya kanisa
3. Fadhila za Kimungu
4. Matukio ya kila siku


Je, ni sahihi kusali sala kwa kurudia rudia mfano Novena?

Ndiyo, Hii ni kwa sababu sala nyingi za kurudia ni za Ahadi na zinasaliwa ili kutimiza ahadi ile. Mfano Novena husaliwa kwa siku 7 au 9 kwa nia ya kupata kile kilichoahidiwa au kinachodhamiriwa. Mungu alishawahi kuwaagiza Waisraeli wafanye Ibada maalumu kwa kurudiarudia mfano wakati walipoangusha kuta za Yeriko walifanya Ibada maalumu kwa siku 7 (Saba).
“Waisraeli walipopita waliagizwa na Mungu kuzunguka Mji wa Yeriko 2Kisha BWANA akamwambia Yoshua,“Tazama, nimeitia Yeriko mikononi mwako, pamoja na mfalme wake na watu wake wa vita. 3Zunguka mji mara moja pamoja na watu wako wote wa vita. Fanya hivi kwa siku sita. 4Uwe na makuhani saba wakibeba mabaragumu ya pembe za kondoo waume mbele ya sanduku. Siku ya saba, mzunguke mji mara saba, nao makuhani wakipiga baragumu hizo. 5Utakaposikia makuhani wamepaliza sauti kubwa ya baragumu, watu wote wapige kelele kwa sauti kuu, kisha ukuta wa mji utaanguka na watu watakwea, kila mtu aingie ndani moja kwa moja kutokea pale alipo.’’ (Yoshua 6:2-5).
Naamani aliambiwa na Nabii Elisha aoge mara saba kwenye mto Yordani ili apone.
14Hivyo akashuka na kujizamisha ndani ya mto Yordani mara saba, kama vile huyo mtu wa Mungu alivyokuwa amemwambia, nayo nyama ya mwili wake ikapona na kutakasika kama ya mwili wa mvulana mdogo. (2 Wafalme 5:14)
Yesu alisali sala ya kurdia rudia kama tunavyosoma,
39Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akaomba, akisema, “Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniepuke, lakini si kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo Wewe.’’ 40Kisha akarudi kwa wanafunzi wake na kuwakuta wamelala. Akamwuliza Petro, “Je, hamkuweza kukesha pamoja nami kwa saa moja? 41‘‘Kesheni na mwombe, msije mkaanguka majaribuni. Hakika roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.’’ 42Akaenda tena mara ya pili na kuomba, “Baba yangu, kama ikiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, mapenzi yako yafanyike.’’ 43Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. 44Hivyo akawaacha akaenda zake tena mara ya tatu na kuomba akisema maneno yale yale. (Mathayo 26:39-44)

Je ni makosa kurudia sala maneno yale yale kwa Mfano Rozari?

Hapana sio Makosa. Kwa Mfano Biblia inatuambia kuwa Malaika humtukuza Mungu kwa maneno ya kurudia rudia.
“8Kila mmoja wa hawa viumbe wenye uhai wanne, alikuwa na mabawa sita na kujawa na macho pande zote, hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawakuacha kusema: ‘‘Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.’’ (Ufunuo 4:8).
Vile vile tunasoma katika kitabu cha Isaya kuwa malaika walikua wakimsifu na kumtukuza Mungu kwa sala/ maneno ya kurudiarudia. “Katika mwaka ule mfalme Uzia alipokufa, nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu na kilichotukuzwa sana, nalo pindo la joho lake likajaza hekalu. 2Juu yake walikuwepo maserafi, kila mmoja alikuwa na mabawa sita: Kwa mabawa mawili walifunika nyuso zao, kwa menngine mawili walifunika miguu yao na kwa mawili walikuwa wakiruka. 3Nao walikuwa wakiitana kila mmoja na mwenzake: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni BWANA Mwenye Nguvu, Dunia yote imejaa utukufu wake.”
Kama Malaika humtukuza Mungu kwa maneno ya kurudia rudia kwa nini sisi tukifanya hivyo tuwe tunakosea? Na sisi tunaweza kumuomba, kumsifu na kumtukuza Mungu kwa sala au maneno ya kurudiarudia kama walivyofanya malaika. Kwa hiyo sala za kurudia rudia sio makosa.
Tukiangalia Zaburi ya 136 inarudia maneno “kwa maana fadhili zake zadumu milele” mara 26 yaani kwenye mistari yake yote. (Zaburi 136:1-26)
Yesu pia allimuomba Mungu Baba kwa kurudia maneno yale yale kama tunavyosoma,
39Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akaomba, akisema, “Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniepuke, lakini si kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo Wewe.’’ 40Kisha akarudi kwa wanafunzi wake na kuwakuta wamelala. Akamwuliza Petro, “Je, hamkuweza kukesha pamoja nami kwa saa moja? 41‘‘Kesheni na mwombe, msije mkaanguka majaribuni. Hakika roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.’’ 42Akaenda tena mara ya pili na kuomba, “Baba yangu, kama ikiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, mapenzi yako yafanyike.’’ 43Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. 44Hivyo akawaacha akaenda zake tena mara ya tatu na kuomba akisema maneno yale yale. (Mathayo 26:39-44)

Sala kwa Mkatoliki ni nini hasa? Tunaposema sala tunamaanisha nini hasa?

Sala ni kuongea na Mungu. Sala kwa Mkatoliki inajumuisha maombi, tafakari, ibada, taamuli, shukrani na sifa. Maana ya sala kwa Mkristo Mkatoliki sio kuomba tuu kama wanavyotafsiri watu wasio wakatoliki. Wengi wa wasio Wakatoliki wanaposema Sala wanamaanisha Maombi.
Kwa hiyo kwa Mkatoliki, Sala ni zaidi ya Maombi. Ndiyo maana kwa mkatoliki kuna sala za namna mbalimbali kama vile za Tafakari, za Maombi za Sifa na za kushukuru. Mfano sala ya Atukuzwe Baba sio maombi bali ni sala ya kumtukuza Mungu kwa maana hiyo sio Maombi, ndiyo maana husaliwa baada ya sala au matukio fulani kama ishara ya kumtukuza Mungu na kutambua ukuu wa Mungu

Yesu alifundisha tusali vipi?

Kisha Yesu akawapa wanafunzi Wake mfano ili kuwaonyesha kuwa yawapasa kuomba pasipo kukata tamaa.
2Akawaambia, “Katika mji mmoja alikuwapo hakimu ambaye hakumwogopa Mungu wala kumjali mtu. 3Katika mji huo alikuwako mjane mmoja ambaye alikuwa akija kwake mara kwa mara akimwomba, ‘Tafadhali nipatie haki kati yangu na adui yangu.’ Wa Mjane Asiyekata Tamaa 4“Kwa muda mrefu yule hakimu alikataa. Lakini hatimaye akasema moyoni mwake, ‘Japokuwa simwogopi Mungu wala simjali mwanadamu, 5lakini kwa kuwa huyu mjane ananisumbuasumbua, nitahakikisha amepata haki yake ili asiendelee kunichosha kwa kunijia mara kwa mara!’ ” 6Bwana akasema, “Sikilizeni asemavyo huyu hakimu dhalimu. 7Je, Mungu hatawatendea haki wateule Wake wanaomlilia mchana na usiku? Je, atakawia kuwasaidia? 8Ninawaambia, atawapatia haki upesi. Lakini je, Mwana wa Adamu atakapokuja ataikuta imani duniani?” (Luka 18:1-8)


Roho Mtakatifu ana nafasi gani katika sala?

Roho Mtakatifu ndiye Mlezi wa ndani wa sala ya Kikristo


Ni ipi sala kubwa ya Kanisa?

Sala kubwa ya Kanisa ni Misa Takatifu


Ni ipi sala bora kwa Bikira Maria? Kwa nini Tunasali kwa Bikira Maria?

Sala bora kwa Bikira Maria ni Rozari Takatifu

Kwa nini watu wengi wanaomba kwa Bikira Maria?

Watu wengi wanaomba kupitia Bikira Maria kwa sababu wanashuhudia sala zao kujibiwa kirahisi zaidi wanaposali kupitia Bikira Maria kwani Bikira Maria anatuombea kile tunacho mwomba. Bikira Maria anasimama Kama mwombezi wetu mbele ya Mungu hasa pale tunaposhindwa kusali Inavyotakiwa.

Bikira Maria anatuombea kwa jina na mamlaka ya nani?

Bikira Maria anatuombea kwa jina la Yesu Kristu na kwa mamlaka ya Yesu Kristu aliye mwanaye. Hakuna Sala yoyote inayotolewa kwa Bikira Maria moja kwa moja kwani Sala zote kwa Bikira Maria zinatolewa kwa kusema utuombee ikimaanisha kuwa utupelekee Maombi yetu kwa Mungu. Bikira Maria hatusaidii sisi moja kwa moja bali anatusaidia kwa kutuombea msaada kutoka kwa Mungu.

Je ni halali au ni sawa kwa Bikira Maria kutuombea kwa Jina la Yesu? Na Je tunajuaje kuwa Bikira Maria anaushirika na Yesu?

Ni halali na nisawa kabisa Bikira Maria kutuombea. Tunajua kuwa Bikira Maria anaushirika na Yesu kwa kuwa Yesu mwenyewe alituambia kuwa “asiyepingana na sisi yupo upande wetu”. Biblia iintuambia…
“Yohane akadakia na kusema “Umemwona Mtu mmoja akifukuza pepo kwa kutumia jina lako, nasi tukajaribu kumkataza kwa kuwa si mmoja wetu.” Lakini Yesu akawaambia, “Msimkataze kwani asiyepingana nanyi yupo upande wenu” (Luka 9:49-50).
Kwa hiyo Bikira Maria anapolitumia jina la Yesu bila kupingana na sisi wala Yesu ni ishara tosha kuwa ni mshirika wa Mungu (Yesu)

Je ni kweli kwamba Bikira Maria ni Malkia wa Kipepo?

Sio kweli kwamba Bikira Maria ni Malkia wa Kipepo/Kishetani
Sababu hizi zifuatazo zinadhihirisha kuwa Bikira Maria sio Malkia wa kipepo;
1) Kuomba kwa jina la Yesu: Angekua ni Malkia wa Kipepo asingeomba kwa Jina la Yesu. Kama ilivyoelezwa hapo juu. Biblia iintuambia linapotamkwa Jina la Yesu mapepo hukimbia. Sasa iweje yeye alitumie Jina hilo kutuombea Kama yeye ni pepo? (Luka 10:17)
2) Hafundishi uovu/dhambi: Mbali na kuomba kwa jina la Yesu, vilevile Yesu alituambia tuzichunguze roho na tutazitambua roho hizo kwa matendo yake. Kwa lengo hili tukichunguza kuhusu Bikira Maria tutaona kuwa Bikira Maria ni Mtakatifu aliye upande wa Mungu kwa sababu Mara zote alipowatokea watu amekuwa akifundisha na kuelekeza watu kuishi maisha ya utakatifu na kumfuata Mungu kweli kwa kutii amri zake na kufuata mafundisho ya mwanae ambayo ni yakuelekea katika utakatifu. Hakuna hata Mara moja mafundisho ya Bikira Maria yalihusishwa na vitendo viovu au vya kuvunja Amri za Mungu.
3) Mafundisho yake yanaendana na Neno la Mungu (Biblia): Bikira Maria hajawaji hata mara moja kufundisha na kuelekeza vitu vilivyo nje ya Mafundisho ya neno la Mungu (Biblia). Hakuna hata Mara moja mafundisho ya Bikira Maria yalikinzana na Mafundisho ya Neno la Mungu.
4) Anahubiri Wema, Unyenyekevu, Upole na Utii: mambo ambayo ni alama ya kudhihirisha Utakatifu.
5) Anasisitiza Upendo kwa Binadamu wenzetu na kwa Mungu: Anahubiri Upendo hasa kwa Maadui zetu na wale wanaoipinga Imani ya Kikristu na wanaomkataa Yesu Kristu. Anasisitiza mara zote Tumpende Mungu na kumtii.
6) Anahubiri Amani: Anahubiri Injili ya Amani na Mara zote anasisitiza tuombe amani ambapo amani ndio Ishara ya Utakatifu.
7) Hajitukuzi mbele ya Mungu bali anajinyenyekesha: Hajawahi kufundisha kwamba tumtukuze yeye au tumuheshimu yeye. Mara zote anahubiri tumheshimu Mungu pekee na kumtukuza Mungu. Amekua akijishusha kwa unyenyekevu huku akituelekeza tuige mfano wake wa unyenyekevu wa kumuelekea Mungu aliye Baba wa huruma na upendo.
8) Anaongeza imani kwa Mungu: Kwa sala na Ibada za Bikira Maria waumini wanapata kuongezewa Imani na Uchaji wao kwa Mungu. Wengi wanabadili maisha yao ya dhambi na kuelekea Maisha mema ya utakatifu ya Kumtumikia Mungu.
9) Sala Ibada yake inachanganyika na Ibada nyingine za Kikristu: Hakuna mgongano/ushindani wa Ibada kwa Bikira Maria na Ibada nyingine za Kikristu. Kama angekua ni pepo kamwe Ibada yake isingechanganyika na Ibada Takatifu.
10) Ibada kwa Bikira Maria Imedumu: Haikufifia wala kupotea bali ilizidi kuendelea vizazi hata vizazi. Hii inadhihirisha kwamba kuna Neema ya Mungu.
Kwa sababu hizi unaweza ukaona kwamba Bikira Maria anaushirika na Mungu na ni Mtakatifu.


Ni zipi sala Muhimu kwa Mkristo?

Sala muhimu kwa Mkristo ni;
1. Misa Takatifu
2. Baraka ya Sakramenti Kuu
3. Litania Takatifu
4. Njia ya Msalaba
5. Rozari Takatifu
6.Novena


Ipi ni shule ya kwanza ya sala?

Familia ni shule ya kwanza ya sala


Mahali gani panafaa kwa sala?

Mtu anaweza kusali mahali popote lakini Kanisani ndipo mahali Rasmi pa sala


Mwenye kusali anakutana na majaribu gani?

Anakutana na Majaribu haya;
1. Mtawanyiko wa Mawazo
2.Ukavu wa moyo
3. Uvivu na Uregevu
Ndiyo maana kwa Wakatoliki sala nyingi zimeandikwa ili kutuongoza hasa tunapokuwa majaribuni katika sala.


Neno “Amina” katika sala lina maana gani?

Neno “Amina” katika sala lina maanisha “Na iwe Hivyo” (Hesabu 5:22)


“Aleluya” katika sala, hasa zaburi ina maana gani?

“Aleluya” katika sala, hasa zaburi ina maanisha “Msifuni Mungu”


Ishara ya msalaba ni nini?

Ishara ya Msalaba ni tendo la mtu kugusa panda la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na kutamka “Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”


Kwa kugusa paji la uso tuna maana gani?

Kwa kugusa paji la uso tuna maana ya kukubali kwa akili


Kwa kugusa kifua tuna maana gani?

Kwa kugusa kifua maana yake ni kuupokea na kuukubali msalaba moyoni.


Kwa kugusa mabega tuna maana gani?

Kwa kugusa mabega maana yake ni kuwa tayari kuubeba msalaba kwa nguvu zetu zote


Kwa nini tunafanya Ishara ya Msalaba?

Tunafanya Ishara ya Msalaba kwa nia ya kumkiri Mungu mmoja katika Nafsi Tatu. Pia msalaba ni Ishara ya Ukombozi wetu


Ishara ndogo ya Msalaba juu ya panda la uso, mdomo, na kifua kabla ya Injili ina maana gani?

Maana yake ni kama Ahadi kuwa, Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu kwa akili yangu, Nitalitangaza kishujaa kwa Midomo yangu, Nitalipenda na kulishika kwa Moyo wangu wote.


Sala zina faida gani? Kwa nini watu tunasali?

Sala zina faida hizi;
1. Zinaleta neema nyingi
2. Zinatuimarisha ili kushinda vishawishi na dhambi
3. Zinatuunganisha na Mungu
4. Zinatudumisha katika kutenda mema


Mazinguo ndiyo nini?

Mazinguo ni sala za kupungia mashetani ili kuepusha watu na balaa au madhara, hasa kama wamepagawa nao.
“Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu” (Mk 5:8).
“Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena!” (Mk 9:25).
Yesu ameliachia Kanisa mamlaka yake juu yao.
“Aliwaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu” (Mk 6:7).
“Paulo alisikitika, akageuka akamwambia yule pepo, ‘Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu’. Akamtoka saa ileile” (Mdo 16:18).


Ikiwa sala ni maongezi ya Mungu na mtu, kwanza tufanye nini?

Ikiwa sala ni maongezi ya Mungu na mtu, kwanza tumsikilize kwa makini na kutafakari alichosema ili tukifanyie kazi. Tukisema peke yetu si sala, kwa kuwa ukisema upande mmoja tu si maongezi.
“Nena, Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikia” (1Sam 3:10).
“Nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku” (Zab 63:6).
“Sheria yako naipenda mno ajabu, ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa” (Zab 119:97).
“Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu” (Yer 15:16).


Kielelezo cha sala yetu ni nani?

Kielelezo cha sala yetu ni Yesu Kristo.
“Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, ‘Bwana, tufundishe sisi kusali” (Lk 11:1).
Yeye kama binadamu alichota humo uaminifu kwa wito wake wa pekee.
“Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe” (Yoh 17:1).
“Aba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe” (Mk 14:36).


Kama binadamu Yesu alijifunza kusali kwa nani?

Kama binadamu Yesu alijifunza kusali kwa Mama yake na kwa mapokeo yote ya Israeli, yaliyojitokeza hasa katika Zaburi.
“Wazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka. Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuu” (Lk 2:41-42).
“Saa tisa Yesu alipaza sauti yake kwa nguvu, ‘Eloi, Eloi, lama sabakthani?’” (Mk 15:34).
“Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu” (Lk 23:46).


Je, sala ya Yesu inatokana na utu wake tu?

Hapana, sala ya Yesu haitokani na utu wake tu, bali katika huo Mwana wa milele ndiye anayemuelekezea Baba yake sala kamili ya kitoto.
“Saa ileile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, ‘Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili, umewafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza” (Lk 10:21).
“Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote” (Yoh 11:41- 42).
“Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo” (Lk 23:34).


Yesu alisali vipi?

Yesu alisali kila mahali na kila wakati, akidumisha ushirika wa upendo kati yake na Baba katika Roho Mtakatifu.
“Saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu” (Yoh 4:23).
Pamoja na kushiriki kiaminifu ibada za taifa lake, mara nyingi alijitafutia mahali pa faragha.
“Aliongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani” (Lk 4:1).
“Alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba” (Lk 5:16).
“Aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu” (Lk 6:12).
Ndiyo sababu ametuambia,
“Wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini” (Math 6:6).
Tusipojua kuongea na Baba moyo kwa moyo, tutawezaje kuongea naye kati ya umati?


Yesu ametufundisha kusali vipi?

Yesu ametufundisha kusali akitueleza misimamo ambayo tuwe nayo.
“Upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako… Waombeeni wanaowaudhi… Msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu” (Math 5:24,44; 6:5).
“Mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipigapiga kifua akisema, ‘Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi’. Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki” (Lk 18:13-14).
Hasa ametutia Roho Mtakatifu atuongoze kama alivyomfanyia yeye.


Je, Yesu ametufundisha maneno ya sala pia?

Ndiyo, Yesu ametufundisha maneno ya sala ya ‘Baba Yetu’, kamili kuliko zote. Maombi yake saba yanategemea utangulizi ambao tunamuendea Mungu kwa ujasiri na furaha kama watoto wake, ndugu kati yetu.
Maombi matatu ya kwanza yanalenga atukuzwe, atawale, apate ushirikiano wetu. Maombi manne ya mwisho yanalenga tupate chakula cha roho na cha mwili, msamaha wa dhambi, ushindi katika vishawishi, usalama dhidi ya yule Mwovu.
“Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. Basi ninyi salini hivi…” (Math 6:8-9).


Je, sala inategemea maneno?

Hapana, sala haitegemei maneno mengi mazuri, bali kujijenga
“juu ya imani… na kuomba katika Roho Mtakatifu” (Yud 20).
“Mkiwa katika kusali, msipayukepayuke, kama watu wa mataifa; maana hao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi” (Math 6:7).
Hii haituzuii tusirudie maneno yetu kwa dhati zaidi na zaidi.
Yesu “alikwenda, akaomba mara ya tatu, akisema maneno yaleyale” (Math 26:44).
Tunaweza kusali kimoyomoyo pia.
“Hana alikuwa akinena moyoni mwake, midomo yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe… ‘Nimeimimina roho yangu mbele za Bwana’” (1Sam 1:13,15).
“Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee Bwana” (Zab 19:14).


Je, sala yetu inasikilizwa daima?

Ndiyo, sala yetu inasikilizwa daima kwa kuwa imeunganika kwa imani na ile ya Yesu, njia pekee ya kumuendea Baba.
“Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata, furaha yenu iwe timilifu” (Yoh 16:24).
Lakini Baba, kwa ujuzi na upendo usio na mipaka, anaweza akatupatia mambo tofauti na yale tuliyomuomba.
“Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, ‘Nipe maji ninywe’, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai” (Yoh 4:10).
“Ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je, Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?” (Lk 11:13).
Imani yetu ikubali kwamba aliyotupatia ni bora zaidi.


Je, sala inaweza kumuendea Yesu?

Ndiyo, sala inaweza kumuendea Yesu, Bwana wetu na kaka yetu, aliye hai mbinguni, kama ilivyomuendea na kusikilizwa alipokuwa duniani.
Mhalifu alisema,
“‘Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako’. Yesu akamwambia, ‘Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi” (Lk 23:42-43).
Stefano aliomba,
“‘Bwana Yesu, pokea roho yangu’. Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, ‘Bwana, usiwahesabie dhambi hii’” (Mdo 7:59-60).
“Roho na Bibi arusi wasema, ‘Njoo!’. Naye asikiaye na aseme, ‘Njoo!’… Na uje, Bwana Yesu!” (Ufu 22:17,20).


Roho Mtakatifu anatusaidiaje kusali?

Roho Mtakatifu anatusaidia tusali kama Yesu, akiwa mlezi wa ndani na kutumia vipaji vyake saba.
“Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, ‘Aba!’ yaani, ‘Baba!’” (Gal 4:6).
“Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo; lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa… huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu” (Rom 8:26-27).
Ndiyo sababu Kanisa linatuhimiza tumtamani na kumualika kila mara, ‘Njoo, Roho Mtakatifu!’ yaani kumuomba Baba kwa njia ya Mwana amtume zaidi na zaidi ndani mwetu.


Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha hadi wapi?

Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha hadi muungano wa dhati na Mungu.
“Yeye awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake, katika utu wa ndani. Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu” (Ef 3:16-19).
“Huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote” (Yoh 16:13).
Safari hiyo inategemea sana sala isiyoishia katika maneno bali inalenga kupenya mafumbo kwa imani na upendo.


Je, sala inaweza kuwaendea Mama na marafiki wa Yesu (Watakatifu)?

Ndiyo, sala inaweza kuwaendea Mama na marafiki wa Yesu, walioungana naye kuwa mwili mmoja, wasiweze kutenganishwa na chochote.
“Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine chochote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Rom 8:38-39).
“Kwangu mimi kuishi na Kristo, na kufa ni faida… Ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo” (Fil 1:21,23)
.
Kwa kuwa hao wako na Kristo mbinguni, wanatuombea mfululizo pamoja naye.
“Niliona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, ‘Ee Mwenyezi, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini…’” (Ufu 6:9-10).
Tunawaomba wazidi kutuombea kwa Mungu, kama tunavyowaomba wenzetu waliopo duniani.
“Mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; pia na kwa ajili yangu mimi” (Ef 6:18-19).


Je, Yatupasa kumwomba Roho Mtakatifu?

Ndiyo, kwani twataka kwake maonyo na msaada. Tusipokuwa na neema yake hatuwezi kutenda jambo jema la kufaa kutuokoa. (Yoh 16:13)

Faida na namna ya kutumia mafuta ya Zaituni Olive Oil kwenye nywele

Faida ya Mafuta Ya Zaituni Olive Oil kwenye nywele.

1. Yanasaidia kufanya mzunguko wa damu kufanya kazi vizuri kwenye ngozi ya kichwa na kupenyeza hadi kwenye shina ya nywele kisha kuifanya nywele inayoota kuwa imara

2. Yanasaidia kupambana na mba kwenye ngozi ya kichwa

3. Yanasaidia uzalishwaji wa mzizi au shina ya nywele

4. Yanasaidia uzalishwaji wa melanin ambayo inafanya kazi ya kutoa rangi ya nywele inayotakiwa.

5. Yanasaidia kuifanya nywele isiwe kavu sana.

NAMNA YA KUZIHUDUMIA NYWELE:

Unaweza kuchanganya na Mdalasini pamoja na Asali.

1. Olive oil vijiko 2 vya chakula

2. Asali kijiko 1 cha chakula

3. Mdalasini kijiko 1 cha chai

Pasha moto olive oil kisha changanya vyote kwa pamoja pakaa kwenye nywele acha kwa muda wa dakika 20 kisha osha nywele zako na upakae mafuta zikishakauka.

Ninashauri utumie mafuta haya kwenye nywele na ngozi ni mazuri sana. Ukiwa na mba pakaa kwenye ngozi mba itaisha na muwasho utaondoka.

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About