Januari kweli ngumu, soma hii
Januari kweli kiboko
Hii january sabuni za kuogea ni zile za kuoshea vyombo, yani unakutana mjini na mtu ana mchicha shingoniโฆ๐
Januari kweli kiboko
Hii january sabuni za kuogea ni zile za kuoshea vyombo, yani unakutana mjini na mtu ana mchicha shingoniโฆ๐
Kama yalivyo maisha ya kimwili, maisha ya kiroho pia yanahitaji mipango. Kila siku panga utafanya nini kiroho, mfano unaweza kupanga sala, kusaidia masikini, kuwa mpole au mwema. Vivyo hivyo kila wiki, kila mwezi na kila mwaka mpya panga cha kufanya kiroho naye Mungu atakubariki na kukupangia zaidi. Huwezi kufanikiwa kiroho kama hujui unafanya nini kiroho.
Mbangi mwitu au kwa kisayansi ni African marigold / (Tagetes erecta) Unazuia Bakteria, fungusi na wadudu kama vile Siafu, bungo pamoja na aina nyingine za wadudu.
CHEKA KIDOGO
MVUVI MASKINI NA MKEWE MALAYA.
Mvuvi mmoja alikua akiishi na mke wake huku
akiwa hajui kama mkewe malaya,
Leo hii kamuaga mkewe baada ya kuondka
mkewe akaanza kuingiza wanaume kama
kawaida
Hawara 1;nakupenda
Mke Wa Mvuvi;oke, Nipe Penz Haraka Kabla
Mume wngu hajarudi.
Hawara 1;oke!
Basi picha likaanza wakati wanaendelea mara
mlango ukagongwa, akamwambia hawara mume
wangu huyo jifiche darini jamaa akafanya,, mke
wa mvuvi akaelekea mlangon kumbe alikua
hawara 2.
mke wa mvuvi; aaahaa kumbe ni wewe nilijua
mume wangu bas njo haraka kabla mume wangu
hajarudi..
picha likaendelea huku wa darini akiona vyote,
mlangon kukagongwa
mke wa mvuvi; mume wangu hyo jifiche uvungun
jamaa akafanya kisha mke akajikoki kumpokea
mumewe,
mke wa mvvi; oooh! mume wngu pole umechoka
eeh leo umepata samaki mkubwa nashukuru sana
tulikua hatuna mboga
mvuvi;usinishukuru mimi mshukuru aliye juu.
hawara 1; sipo mwenyewe mwingine yupo
uvunguniโฆย
Amri za kanisa ni;
1. Hudhuria Misa Takatifu Dominika na sikukuu zilizoamriwa.
2. Funga siku ya Jumatano ya Majivu; usile nyama siku ya Ijumaa Kuu
3.Ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka.
4. Pokea Ekaristi Takatifu hasa wakati wa Pasaka
5. Saidia Kanisa Katoliki kwa zaka
6. Shika sheria Katoliki za ndoa.
Tumeamriwa tusikilize Misa kila siku ya Mungu na Sikukuu zilizoamriwa.
Ndizo:
1. Kuzaliwa kwa Yesu – Noeli tarehe 25/12 Ufufuko wa Bwana Yesu
2. Pasaka –
3. Kupaa Yesu โ- Siku 40 baada ya Pasaka.
4. Kupalizwa Mbinguni Bikira Maria 15/8
5. Sikukuu ya Watakatifu Wote 1/11
Tumekatazwa;
1. Kukosa Misa
2. Kufanya kazi nzito siku hizo
Kujinyima ni kujikatalia kitu ukipendacho mfano nyama, pombe, sigara, muziki, safari, maongezi n.k.
Kila Mkristo aliyetimiza miaka 14 na zaidi anapaswa kufunga kula nyama (Ijumaa kuu) na mwenye miaka zaidi ya 21 kufunga chakula. (Jumatano ya Majivu)
Siku za kufunga ni Jumatano ya majivu, siku za Kwaresima isipokuwa Dominika zake, na siku iliyokatazwa kula nyama ni siku ya Ijumaa kuu.
Katika Amri ya Tatu ya Kanisa tumeamriwa kuungama mara kwa mara walau mara moja kila mwaka
Katika Amri ya Nne ya Kanisa tumeamriwa tupokee Ekaristi Takatifu walau mara moja kwa mwaka wakati wa pasaka.
Katika Amri ya Tano ya Kanisa tumeamriwa kufahamu kuwa gharama za dini na za mapadre zatupasa. Yaanai wakristo walitegemeze Kanisa na wahudumu wake na hasa katika kazi ya kueneza injili.
Zaka ni asilimia kumi (10%) ya pato la mtu kwa mwaka ambalo anapaswa kulitoa kwa Kanisa.
Atenda dhambi kubwa: Yampasa kulipa na kuungama.
Inadai kushika Sheria Takatifu Za ndoa
ni viini vilivyoko kwenye chakula ambavyo vinauwezesha mwili kufanya kazi zake, karibu vyakula vyote huwa na kirutubishi zaidi ya kimoja ila hutofautiana kwa kasi na ubora. Kila kirutubishi kina kazi yake mwilini na mara nyingi hutegemeana ili viweze kufanya kazi yake kwa ufanisi. Hakuna chakula kimoja chenye virutubishi vya aina zote isipokuwa maziwa ya mama kwa miezi sita ya mwanzo ya maisha ya mtoto, ni mhimu kula vyakula vya aina mbalimbali ili kuwezesha mwili kupata virutubishi mchanganyiko vinavyohitajika.
Kabohaidreti / vyakula vya wanga huvipa mwili nguvu inayoihitajika kujiendesha. Vyakula
hivi vyaweza kuwa sahili au changamani. Hii inahusu jinsi ambavyo chakula chaweza
kubadilisha sukari katika mwili. Vyakula vya wanga na sukari huvipa mwili nguvu
inayohitajika kuufanya upumue na kuendelea kuishi, kuwa na mwendo na utoaji joto, na kwa
ukuaji na utengenezaji wa mkusanyiko wa seli (tishu). Baadhi ya wanga na sukari
hubadilishwa kuwa mafuta mwilini.
Ufumwele utokanao na kabohaidreti hufanya kinyesi kiwe laini na kingi na huondoa kemikali
za sumu, na hivyo hufanya matumbo yawe na afya njema. Hupunguza uyeyushaji na
ufyonzaji wa virutubishi katika vyakula, na husaidia kupunguza unene.
Vyanzo vikuu vya kabohaidreti ni:
– Mahindi/ugali
– Serena
– Mtama
– Mchele
– Unga wa ngano
– Viazi vitamu
– jimbi
– Viazi mviringo
– Muhogo mbichi
– Unga wa muhogo
– Ndizi
– Mahitaji hutofautiana kutegemea na umri, jinsi, jinsia, shughuli, hali ya kiafya
– Kula mara tatu au zaidi kwa siku.
Mafuta ya wanyama na mimea kwenye chakula na tishu ya shahamu kwenye miili yetu huwa
na shughuli nyingi
โขย Virutubishi:ย mafuta ya wanyama hutoa tindikali za mafuta muhimu, ambazo
huhitajika katika ukuaji wa kawaida kwa watoto wachanga na watoto wengine na
kwa uzalishaj wa michanganyiko ya aina ya kihomoni inayorekebisha upeo mpana
wa shughuli za kimwili na kukufanya uwe mwenye afya njema.
โขย Usafirishaji:ย mafuta ya wanyama hubeba mafuta ya miyeyusho ya vitamini (A, D,
E, na K) na kurahisisha ufyonzaji wake.
โขย Ufahamu:ย mafuta ya wanyama huchangia kwenye harufu nzuri na ladha ya
chakula.
โขย Umbile la asili:ย mafuta ya wanyama hufanya chakula (hususan nyama na vyakula
vya kukaushwa) kuwa nyororo.
โขย Ukinaishaji:ย mafuta ya wanyama hukipa chakula ukinaishaji, hivyo hujikuta
umeshiba na kutosheka kwa muda mrefu baada ya chakula.
โขย Mafuta ya wanyama ni chanzo cha utoaji wa mkusanyiko wa kalori.ย Hili ni jambo
jema unapokuwa kwenye safari ndefu, itumiayo nguvu nyingi, ukiwa umebeba
chakula chako.
โข Mafuta ni muundo mkuu wa mwili wa kuhifadhi nishati (ambazo ni muhimu wakati wa
ugonjwa au kupungua kwa ulaji chakula)
โข Mafuta hutoa sehemu kubwa ya nishati inayotumika kwenye kufanyiza kazi misuli.
โข Mafuta hukinga viungo vya ndani na kuhami miili yetu dhidi ya hali za joto
zinazopitiliza mipaka.
โข Mafuta huunda malighafi kuu ya utando wa seli (hususan seli za ubongo na za
mishipa ya fahamu)
โข Mafuta hugeuzwa kuwa aina nyingi za homoni (ikiwemo homoni za mambo yahusuyo
mapenzi)
Mafuta ki kitu kizuri! Isipokuwa tu pale uzuri unapozidi kiwango ndipo kunapokua na tatizo.
mafuta yaliyokolea dhidi ya yale yasiyokolea
Kama ambavyo kuna aina kuu mbili za kabohaidreti, kuna aina kuu mbili za mafuta
kutegemea na mfumo wake wa kikemia; mafuta yaliyokolea na yale ambayo hayajakolea.
Aina hizi za mafuta zina athali tofauti kabisa kwa afya yako.
โข Huwa na kawaida ya kuongeza lehemu โmbayaโ kwenye damu na kuongeza
uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo.
โข Mafuta yaliyokolea huwa na kawaida ya kuganda kwenye hali ya joto la kawaida.
โข Hupatikana kwa wingi kutokana na vyanzo vya mafuta ya wanyama.
Vyanzo vya mafuta yaliyokolea
โข Siagi, malai, mafuta ya nyama ya ngรณmbe, ngozi ya kuku, mafuta ya maziwa yenye
malai, jibini, aisikirimu, siagi, samli, mafuta ya nguruwe/ya kupikia, mafuta
yatokanayo na nyama, mawese mekundu, na nazi.
โข Yaliyopo nje ya utaratibu: mafuta ya nchi za joto (ikiwemo ya nazi na mawese) yana
kiwango kikubwa cha mafuta yaliyokolea.
โข Mafuta yasiyokolea ni aina ya mafuta ambayo kwa ujumla yanahusishwa na afya bora.
โข Yana kwaida ya kushusha viwango vya lehemu na kupunguza hatari za magojwa ya
moyo.
โข Mafuta yasiyokolea huwa na kawaida ya kuwa ya mmiminiko katika joto la kawaida.
โข Hupatikana kwa wingi kutokana na mimea.
Vyanzo vya mafuta yasiyokolea
โข Mafuta yatokanayo na mboga za majani, mizeituni, miparachichi, njugu, mafuta ya
karanga, maharagwe meupe, mbegu za alizeti, mbegu za ufuta na aina nyingine za
mbegu, mafuta ya samaki na soya.
โข siagi, samli, mafuta ya nguruwe/ya kupikia, maziwa yenye malai, jibini, mafuta
yatokanayo na nyama, mawese mekundu, na nazi.
Kuna mafuta yatokanayo na kuchujwa kwa mafuta ya mbogamboga na kugandishwa. Mafuta
haya huishia kuwa na tabia za mafuta yaliyokolea. Mafuta haya pia hayapashwi kutumiwa
kwa wingi.
โข majarini, mafuta ya nguruwe, vyakula vya kukaangwa, donati, keki, biskuti, aiskrimu.
Mahitaji ya mafuta huelezewa kama โni asilimia ya mahitaji yote ya nishatiโ. Kiwango chote
cha asilimia ya nishati kinachopashwa kitokane na mafuta katika mlo bora uliokamilika ni
kama ifuatvyo:
โข Asilimia 30-40 kwa watoto hadi kufikia miaka miwili kwenye milo ya nyongeza
โข Asilimia 15-30 kwa watoto wakubwa na wengi wa watu wazima; kwa watu wazimu
wenye afya – hadi asilimia 35 inakubalika.
โข Angalau asilimia 20 hadi 30 kwa akina mama wenye umri wa kuweza kuzaa (15-45).
Protini ni zana za ujenzi wa misuli yetu, viungo na baadhi ya vitu vingi vinavyotengeneza
miili yetu. Hutoa tindikali muhimu za amino zitumiwazo na mwili kutengeneza misuli ya tishu.
Mwili unahitaji protini na kalori kila siku.
Unapokosa kupata kalori na protini za kutosha kila siku, mwili wako hutumia akiba yake
kufidia pengo la ukosefu wa nishati. Hali hii huinyima mwili wako kalori unazohitaji kuufanya
uwe na afya bora na hivyo kusababisha kupungua kwa uzito.
Protini yaweza kupatikana kwenye vyakula vya wanyama na mimea.
โข Nyama, kuku/mabata n.k., samaki, mayai, jibini, maziwa na mtindi.
โข Vyakula hivi vinachukuliwa kuwa kama โkamiliโ au โvyenye kiwango cha juuโcha
protini kwa kuwa vina aina zote za โtindikali muhimu za aminoโ. โMuhimuโinamaanisha
lazima vitumiwe kwenye milo yetu; miili yetu haiwezi kuzitengeneza.
โข Bidhaa zitokanazo na soya, (tofu, tempeh), maziwa ya soya na mazao mengine
yatengenezwayo na soya), maharagwe, mbegu na njugu.
โข Viwango vidogo vya protini vinapatikana vilevile kwenye mikate, mahindi /ngano, na
aina nyinge ya nafaka, na mbogamboga pia.
โข Vyanzo hivi vya protini vinachukuliwa kama โsi kamiliโkwa kuwa vinakosa moja au
zaidi ya tindikali muhimu za amino.
โข Protini ya maharagwe meupe ndiyo ya kipekee. Haya yanachukuliwa kuwa ni kamili.
Mahitaji hutofautiana kulingana na umri, jinsi, jinsia, na shughuli.
โข Vitamini husaidia mwili kugeuza chakula kuwa nishati na tishu.
โข Kuna aina 13 za vitamini kwa ujumla: Vitamini A; vitamini B; vitamini B mchanganyiko
unayojumuisha vitamini B1, Vitamini B2, Viamnini B3 vitamin, B6, Vitamini C, Vitamin
B12 tindikali ya pantotheniki (pantothenic acid), na biotini (biotin); na vitamini C, D, E,
na K.
โข Madini yanahitajika katika ukuaji na utunzaji wa miundo ya mwili. Yanahitajika pia
katika kutunza juisi za uyeyushaji chakula na mimiminiko iliyopo ndani na
kandokando mwa seli.
โข Madini hayatokani na mimea wala wanyama. Mimea hupata madini kutokana na maji
au udongo, na wanyama hupata madini kwa kula mimea au wanyama wanaokula
mimea.
โข Vitamini na madini hujulikana pia kama vyakula vya ujenzi na ulinzi wa mwili.
โข Vijirutubishi ambavyo havipatikani kwa wingi na ambavyo husababisha matatizo
mengi yatokanayo na utapiamlo wa ukosefu wa vijirutubish duniani ni kama
vifuatavyo; madini ya joto, zinki, vitamini A, chuma na folate.
โข Mboga jamii ya machungwa, kama vile viazi vitamu vya njano na karoti, matunda jamii
ya machungwa kama vile, embe, papai, na mawese mekundu ni vyanzo vizuri sana
vya vitamini A.
โข Matunda mengi yatokanayo na jamii ya michungwa na mboga zisizoivishwa sana
huwa na vitamini C.
โข Mboga za kijani kibichi hutupatia folate na kiasi cha vitamini A.
โข Mbogamboga nyingi (mf. nyanya, vitunguu) hutoa vijirutubishi muhimu vya nyongeza
viwezavyo kukinga mwili dhidi ya magonjwa sugu kama ya mioyo.
โข Njia bora ya kuhakikisha tunapata vijirutubishi na ufumwele wa kutosha ni kula aina
mbalimbali za mbogamboga, matunda na nafaka zisizokobolewa kila siku.
โข Nyama, viungo vya ndani vya wanyama na maini ya aina zote ni chanzo kizuri sana
cha vitamini A.
โข Vitamini na madini vinahitajika kwa viwango vidogo vidogo.
โข Mahitaji hutegemea umri, jinsi na kiwango cha shughuli, na ulaji wa aina mbalimbali
za matunda, mbogamboga na nafaka zisizokobolewa.
Maji ni kirutubishi muhimu sana. Hakika, zaidi ya nusu ya mwili ni maji. Unaweza kuishi bila
ya chakula kwa wiki kadhaa, bali hauwezi kuishi zaidi ya wiki moja bila ya maji.
Mwili unahitaji maji ili kufanya kazi.
โข Kuhifadhi joto la mwili;
โข Kusafirisha virutubishi mwilini;
โข Kuvifanya viungo viwe na unyevunyevu;
โข Kuyeyusha chakula;
โข Kuondoa uchafu mwilini;
โข Kupoza mwili.
(Fikiria matumizi ya maji unapojenga nyumba; bila ya maji: saruji, mchanga na zege
havitakuwa na matumizi yeyote).
โข Maji yenyewe
โข Juisi za matunda
โข Supu
โข Maziwa
โข Uji
โข Vinywaji visivyo na kafeini (vinywaji vyenye kafeini na kileo vina madawa ya
kuongeza mkojo (diuretics) inayosababisha upotevu wa maji mwilini)
Lita 1.5 au glasi 8 kwa siku.
Wakati wazazi waliweza kuaamua kuzaa mtoto tuu, Mungu yeye alikuchagua wewe utungwe mimba na kukulinda ungali tumboni mwa mama yakoโฆ.Wakati wazazi wanasubiri kwa shauku kuona muonekano wako wewe, Mungu anawaweka wajukuu wa wazazi wako/ watoto wako ndani mwakoโฆ. Wakati wazazi wakitafuta chakula kwa ajili yako, Mungu yeye aliwawezesha kukipataโฆ. Wakati wazazi wakingoja kuona unavyoendelea kukua huku wakiwaza hatima ya maisha yako Mungu anakuendeleza na alishapanga maisha yako tangu alipokuchagua uwe mtu ukiwa tumboni mwa mama yakoโฆ. Wazazi wanaweza kukuombea kwa Mungu lakini Mungu ndiye anayeamua akufanyie nini maana Wewe ni wa kwakeโฆ.Wewe na wazazi wako ni watoto wa Baba mmoja ambaye ndiye Mungu.
KILA mtu duniani ana ndoto ingawa haijalishi ni ndoto gani uliyonayo.
Ndoto uliyonayo ina thamani kubwa kuliko fedha wala kitu chochote kile. Ndoto uliyonayo ina nguvu kubwa ya kubadilisha maisha yako na kukufikisha sehemu ambayo ulitaka ufike ama zaidi ya pale ulipotarajia kufika.
Ndoto yako inaweza kukupeleka sehemu mbalimbali duniani ukazunguka kufanya mambo yako si kwa sababu una fedha sana, bali ni kwa sababu una ndoto. Ni vyema utambue nguvu ya ndoto uliyonayo ni kubwa kuliko fedha.
Ndoto inaweza kuzaa fedha kwa maana matunda yake yanaweza kuwa fedha, lakini katu fedha haiwezi kuzaa ndoto. Kwa hiyo bais, ndoto ni kubwa kuliko fedha.
Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa, mtu maskini kuliko wote duniani ni yule asiyekuwa na ndoto!
Hivyo utakubaliana naye kuwa kila mwenye ndoto ni tajiri na si maskini, maana ana kitu cha thamani, cha pekee na cha tofauti ambacho hakuna mwenye nacho isipokua wewe mwenyewe.
Tatizo kubwa ni kwamba, watu wengi wameua ndoto zao kwa kisingizio cha kukosa fedha lakini wanashindwa kutambua kwamba hakuna fedha inayozidi ndoto isipokuwa ndoto inazidi fedha.
Tatizo lingine ni kwamba, watu wengi hawajui kuwa ndoto zao zina nguvu kubwa kufanikisha maisha yao kijamii, kiuchumi, kisiasa na kila nyanja.
Ndani ya ndoto zako kuna kila kitu unachokitaka ama unachokihitaji โ iwe fedha, utajiri, umaarufu, familia nzuri, mume mzuri, mke mzuri, watoto wazuri, kazi nzuri, afya nzuri โ hivyo ukiacha kutafuta fedha ukatafuta kutimiza ndoto zako utapata kila kitu ikiwemo utoshelevu na amani ya moyo.
Lakini tatizo lipo kwenye kufanya ndoto zako zitimie na zikuzalie mafanikio. Haijalishi una ndoto kubwa kiasi gani, kama hutaitimiza ikaja kwenye uhalisia tambua kwamba utakufa maskini ukiwa na utajiri wa ndoto, jambo ambalo linaumiza na linatesa maisha ya watu wengi wanaoishi maisha ya chini tofauti na walivyopaswa wawe.
Ndoto yako ndiyo imebeba kusudi la maisha yako. Kama hutaishi katika ndoto yako maana yake utakuwa hujaishi maisha yako ambayo kwa kiasi kikubwa yapo kwenye ndoto zako.
Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa, watu wengi duniani hawaishi, bali wapo tu. Kuna tofauti kati ya kuishi na kuwepo. Kuishi ni kutimiza ndoto zako na ndani ya kusudi la maisha yako, lakini kama hutimizi ndoto hizo uko nje ya kusudi la maisha yako. Wewe utakuwa hauishi bali upo upo tu.
Anaamka asubuhi kwa sababu watu wanaamka. Ukimuuliza kwanini umeamka anasema ni kwa sababu watu wameamka! Hana sababu za msingi. Kataa kuishi bila agenda, bila kuwa na ndoto ambayo kila siku unapiga hatua kuifikia ama uko ndani yake sasa katika kuitimiza na kuifanikisha kwa kiwango cha juu.
Kila kitu kipo kwenye ndoto zako, tafuta kutimiza ndoto zako kuliko kutafuta fedha kwa sababu fedha ni moja kati ya bidhaa iliyomo ndani ya ndoto zako.
Sisemi watu wasitafute fedha, la hasha. Wazitafute, tena kwa bidi, ila wasisahau kutafuta kutimiza ndoto zao na kutumia fedha kama moja kati ya nyenzo za kuwawezesha kutimiza ndoto zao.
Ukweli ni kwamba, fedha daima huwa hazitoshi, hata kama ni nyingi kiasi gani. Kama unabisha waulize matajiri kama wamewahi kuridhika. Lakini katika kutimiza ndoto zako kuna utoshelevu kiasi na kuridhika kiasi fulani (satisfaction) hata kama si kwa asilimia 100.
Mwandishi mashuhuri wa vitabu, Myles Munroe, aliwahi kusema kuwa โWatu wenye kusumbuliwa na msongo mkubwa wa mawazo ni wale ambao ndoto zao hazijatokea kwenye uhalisia, zinawasumbua.โ
Inawezekana unasumbuka sana kwenye maisha yako kwa sababu hujatimiza ndoto zako, maana ndoto huwa haimwachi mtu akatulia, inampa mahangaiko, mfadhaiko wa kutaifuta.
Kila mtu anapaswa azae, ndoto yako izae, uwezo ulionao uzae. Unaweza kukuzalia mafanikio makubwa, hivyo usikubali kufa na kitu cha thamani kilichoko ndani yako.
Hakuna ndoto kubwa wala ndogo. Fikiria mtu aliyegundua lipstick, leo hii wanawake dunia nzima wanapaka lipstick, si jambo dogo tena.
Hukuja duniani kuwa mtu wa kuhangaikia fedha, inatakiwa fedha ikuhangaikie wewe, ikupende na ikutamani na si wewe utamani fedha.
Tengeneza miundombinu ya fedha na hiyo miundombinu iko kwenye ndoto zako, maono yako, kipaji
FUNDISHO : SAFARI NI SAFARI
Maisha ni ya ajabu sana, wakati mwingine maisha ni mazuri na mwingine ni mabaya, katika maisha yetu tumeshapitia safari nyingi sana na za aina mbalimbali kwa nyakati mbalimbali. Lakin kiukweli kila safari ni safari tuu.
Japokua kila safari ina changamoto zake lakini mwisho wake ni ule ule , kila safari ina uzuri na upekee wake.
Vile vile kila safari ina ubaya wake, kwa mfano kila safari ina gharama yake kulingana na upekee wake.
Usiwe na wasiwasi na mashaka na aina ya safari ulionayo, jipe moyo utaimaliza na kupata ulichokitarajia. Haya ndio maisha na wote tunatakiwa tuyafurahie.
Ingawa kila mtu ana safari yake bado wote tunatakiwa tufurahie pamoja kwa safari tuliyo nayo. Hata Uwe Na safar ya aina gani wewe furahi tuu. Hii ni kwa sababu safari mwisho wake ni mmoja kwa wote burudani ni ile ile
Safari๐บ ni safari ๐บhata kama ni ya chupa au ya kopo mwisho wake ๐ค๐ค
๐๐๐๐๐๐
Ulijua ni nn??
Uti wa mgongo ulio wazi( Spinal bifida) ni hali ambayo mtoto anazaliwa nayo huku uti wa mgongo (mishipa ya fahamu mkubwa unaotoka kwenye ubongo) ukiwa wazi kutokana na mifupa (vipingili vya uti wa mgongo) kutokufunga vizuri.
Mgongo wazi(spinal bifida) inaweza pata watoto 3 kati ya watoto 10000 wanaozaliwa.
Uti wa mgongo hutengenezwa mara tu baada ya mimba kutungwa, ikiwa kuna kasoro katika utengenezaji wa uti huu basi sehemu fulani ya uti wa mgongo itabaki bila kuzibwa.
Kuna sababu mbalimbali zinapelekea uti wa mgongo kutoziba, ambazo zinaweza zuhilika, nazo ni Upungufu wa folic acid(vit B9) na vitamin B12 katika kipindi cha ujauzito, katika kipindi cha miezi ya awali.
Mama mjamzito kupiga X-ray, mattumizi ya dawa za kifafa katika kipindi cha ujauzito .
Pamoja na maambukizi ya baadhi ya virusi kwa mama mjamzito.
Zipo aina mbiliza tatizo la tundu katika mgongo ama mgongo wazi
Aina ya kwanza ni occultaย ambapo huwa na aina mbili pia, aina ya kwanza ni ile ambapo panakuwa na vinyweleo tu vinavyoonekana nyuma chini ya mgongo bila kuwa na dalili zozote zile, ama kunaweza kujitokeza kwa kuta zinazofunika mishipa ya fahamu tu.
Aina ya pili ni ni cysticaย ambapo panakuwa na vifuko vinavyofunika mishipa ya fahamu pamoja na mishipa ya kuchomoza katika tundu la mgongoni.
Aina hii ni mbaya zaidi kwani linaweza kusababisha mtoto asitembee ama asiweze kuzuia haja kubwa na ndogo.
Dalili huwa kama zifuatazo
Kuwa na uvimbe nyuma chini ya mgongo.
Kuwa na vinyweleo sehemu za chini za mgongo bila kuwa na tatizo la mishipa ya fahamu
Kushindwa kutembea ama kukosa hisia katika miguu
Mtoto anaweza kushindwa kuzuia haja kubwa ama ndogo endapo mishipa yote ya fahamu imepita katika tundu hilo.
Na dalili zingine zinazoambatana kuharibika kwa mishipa.
Upasuaji
Upasuaji ni tiba pekee ya uti wa mgongo ulio wazi(spinal bifida) inayofanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu(neurosurgeons) wanachofanya ni kuziba lile tundu lililowazi.
Wanawake wengi walio katika kipindi cha kuzaa na wajawazito hawatumii vyakula vyenye vitamin B na folic acid inavyopaswa, vyakula hivyo ni matunda,mboga za majani, mbaazi na choroko.
Mwanamke mjamzito akipata lishe yenye virutubisho hivyo pamoja na kunywa vidonge vya folic acid, kwa asilimia 30% inaweza kupunguza hatarishi ya kupata watoto wenye uti wa mgongo ulio wazi.
Pia kwa wanawake wajawazito katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo, wanashauriwa kutokupiga X-ray.Inawezekana mwanamke akawa hatambui kama ni mjamzito,kipimo cha mkojo cha ujauzito(UPT-urinary pregnancy test) kifanyike kwa haraka kama mwanamke haelewi vizuri mzunguko wake wa hedhi kabla hajapiga X-ray ikiwa ana tatizo lingine la kiafya,
Mwanamke mwenye kifafa akiwa mjamzoto pia yupo kwenye matibabu, awahi haraka kwa daktari kushauriana ni nini zaidi cha kufanya ili kumsaidia.
Wanawake wajawazito wanashauriwa kuhudhulia kliniki mapema zaidi ili wapate elimu ya lishe na kuweza kuanza mapema kutumia folic acid kama kinga ya Mgongo wazi.
Jamii inapaswa kujua kuwa Mgongo wazi(Spinal bifida) haitokani na mambo ya kishirikina bali ni hali ambayo inaweza kuzuilika. Mzazi yeyote mwenye mtoto mwenye Mgongo wazi anashauriwa ampeleke mtoto wake hospitali ili apate maelekezo ni wapi mtoto anaweza kupata matibabu ya upasuaji.)
Choroko kikombe 1 na nusu
Nazi kopo 1
Kitunguu kikubwa 1
Nyanya 1/2 kopo
Swaum 1 kijiko cha chai
Curry powder 1 kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Olive oil
Pilipili nzima
Loweka choroko usiku mzima kisha zichemshe mpaka ziive na ziweke pembeni. Baada ya hapo saga pamoja nyanya, kitunguu, na swaum kisha vipike mpaka maji yote, baada ya hapo tia mafuta na curry powder, pika mpaka nyanya zitoe mafuta kisha tia choroko,tui la nazi, maji nusu kikombe,pilipili na chumvi, kisha koroga vizuri na uache ichemke. Pika mpaka tui la nazi litakapoiva na rojo ibakie kidogo sana, kisha ipua na mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Mi huwa napenda kuila na wali ila hata na ugali au chapati inaenda pia.
Unga – 1 Kikombe
Sukari ya kusaga – 3/4 Kikombe
Siagi – 125 gms
Yai – 1
Baking powder – 1/2 kijiko cha chai
Zabibu kavu – 1/2 kikombe
Cornflakes iliyovunjwa (crushed) – 2 Vikombe
Vanilla – 1 kijiko cha chai
Tia kwenye mashine ya kusaga (blender) au mashine ya keki, siagi, yai na vanilla uchanganye hadi ichanganyike vizuri.
Tia baking powder, zabibu na unga na changanya vizuri.
Paka siagi sinia ya kupikia ya oveni.
Tengeneza viduara vidogo vidogo.
Weka cornflakes katika sahani ya chali (flat) na zungusha viduara humo kisha upange katika sinia ya oveni.
Pika katika moto wa 350ยบF kwa muda wa dakika 20-25 hadi vigeuke rangi na viwive.
Siku moja jioni katika mji flani, kulikuwa na basi likisafiri kutoka mji huo kuelekea mji mwingine. Lilikuwa ni basi kubwa na limejaa abiria. Wakati wakiendelea na safari, ghafla, mvua kubwa iliyoambatana na radi ikaanza kunyesha. Dereva hakuogopa, wala abiria, wakaendelea na safari. Mara wakati wanaenda, radi ikaanza kufuatilia gari. Kila wakienda, radi inapiga karibu na basi kana kwamba inalifuata basi. Likisimama, radi inapiga pembezoni mwa basi.
Dereva kuona hivyo, akasimamisha gari mita 5 kutoka kwenye mtiโฆ Akawaambia abiria, “Humu ndani ya basi, kuna mtu ambaye leo ni siku yake ya kufa, tena kufa kwa radi. Ili tusife wote, nataka kila abiria ashuke akaguse mti ili anayepigwa na radi, apigwe wengine wasife kwa ajili yake. “Abiria wakitetemeka, wakaanza kushuka mmoja mmoja. Unaenda unagusa mti , kisha unarudi kwenye basi. Abiria wote pamoja na dereva mmoja mmoja, wakaenda, wakagusa mti na kurudi bila dhara lolote! Akawa kabaki abiria mmoja tu, ambaye alikuwa hajagusa mti. Abiria wote kwa macho ya hasira wakamwambia akaguse mti. Akawa anaogopa kufa. Akagoma. Wakamlazimisha kwa nguvu sana na kumtoa njeโฆโฆ. โฆโฆ.. Yule abiria akiwa amefumba macho, akaenda akagusa mti. Hamadi bin Vuu! Radi kali sana ikalipiga basi, abiria na wote waliokuwamo, wakafa palepale. Kumbe uwepo wake ndio ulikuwa unazuia abiria wengine wasidhurike na radi.
MAFUNZO
1. Unapofanikiwa, huwezi jua uwepo wa nani umefanikisha mafanikio yako, usichukue sifa zote peke yako. Wapatie na wengine bila kumsahau MUNGU.
2. Unaweza kujiona huna thamani sehemu ulipo, iwe kwenye kundi la WhatsApp, darasani, kazini, kwenye basi, barabarani bila kujua kama uwepo wako ni wa muhimu sana kwa ustawi wa wengine.
3. Usimtenge wala kumnyanyasa mtu au jirani yako, huwezi jua uwepo wake ni kwa ajili gani.
โฆUpo kazini umeacha familia yako nyumbani mara ghafla unapigiwa simu kutazama unakutana na no ngeni na kuamua kuipokea ndipo unakutana na Sauti ya msichana ya kuvutia lakin kabla hajasema shida yake anaamua kukata simu. Unashikwa na hamu ya kujua ni nani. Tamaa ya mchepuko inakujia ghafla na kuamua kuipiga ile no tena kwa mara nyingine inakuwa haipatikani.
Siku hiyo hiyo usiku ukiwa umelala chumba kimoja na mkeo meseji inaingia tena kwenye cm yako kwa ile namba iliyokupigia mchana ikikuomba umpigie kwa mida ule na kusisitiza kuwa ana hamu ya kukufahamu. kila ukimtumia meseji ya kumdanganya upo sehemu mbaya hasikii anakubipu mara nyingi. Uzalendo unakushinda, unamuangalia pembeni mkeo kalala fofofo kajifunika shuka hadi usoni. Unaamua kuondoka kwa kunyata mpaka sebuleni kwenda kuipiga Ile namba kwa lengo la Kumwambia kesho mkutane. Ile unafika sebuleni na kuanza kuipiga ile cm ndipo unakutana na sauti hii:-ย MUME WANGU ACHA MCHEPUKO, NILIKUWA NAKUPIMA TU RUDI TU CHUMBANI TULALEย ๐๐๐๐๐๐๐๐ Hapo ndo utajua kwann bata hata ale kokoto anaharisha ๐๐๐๐๐๐๐๐
Unga – 6 vikombe
Samli – ยฝkikombe
Baking Powder – ยฝkijiko cha chai
Maziwa- 1 kikombe
Maji -Kisia kiasi kama unga bado mzito
VIAMBAUPISHI VYA SHIRA
Sukari – 5 vikombe
Maji – 2ย 1/2 vikombe
Vanilla – 2 vijiko vya chai
Rangi ya orange – 1 kijiko cha chai
Iliki ya unga – 1 Kijiko cha chai
Changanya unga wa dengu, samli, baking powder pamoja na maziwa katika mashine ya keki (cake mixer).
Ukisha changanya angalia kama mchanganyiko wako umekua mwepesi kidogo kuliko wa keki, kama bado mzito basi ongeza maji kiasi.
Kisha weka mafuta kiasi kwenye karai,weka na samli kikombe kimoja, weka kwenye moto wa kiasi.
Mafuta yakisha pata moto, chukua kijiko kikubwa cha matundu chota mchanganyiko wako na kijiko cha kawaida tia kwenye kijiko cha matundu. Hakikisha kijiko cha matundu kiwe juu ya karai ili mchanganyiko wako uchuruzike ndani ya mafuta yalio pata moto.
Pika ndani ya mafuta mpaka iwive, ila usiache ikawa brown.
Toa mchanganyiko ulowiva tia ndani ya shira uliyo pika. Hakikisha shira iwe imepoa kabla ya kutia mchanganyiko huo.
Endelea kupika mchanganyiko wako mpaka uishe, kila ukitoa katika mafuta hakikisha unatia ndani ya shira.
Ukishamaliza wote kanda huo mchanganyiko ulokua ndani ya shira mpaka uone shira yote imekauka (yaani iwe imeingia ndani ya mchanganyiko).
Tupia zabibu kavu na lozi zilizo katwa, changanya na mkono.
Wacha mchanganyiko katika bakuli, funika na foil mpaka siku ya pili.
Siku ya pili chukua mchanganyiko kiasi katika mkono tengeneza mviringo (round).
Katika sufuria, tia sukari, maji, iliki, vanilla na rangi.
weka kwenye moto wacha ichemke mpaka itowe povu (bubbles) juu.
Kisha toa povu, wacha shira kwenye moto kama dakika 3.
Hakikisha shira yako iwe inanata kiasi kwenye vidole, lakini iwe nyepesi kidogo kuliko shira ya kaimati.
Et jana usiku mwiz kavunja mlango kwangu akaanza kutafuta kitu kila kona ikabid na mie niamke namuuliza unatafuta nini ananijibu hela ndipo nilipoanza na mie kutafuta nae maana hta hela ya kula Jana sikua nayo alichoka zaid nilipomuliza una uhakika uliweka humu? sipendagi ujinga๐ถ๐ป na kitu hela mm!
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe.” 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” 34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)
19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.” 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.” Matayo 2:19-23
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.” 49 Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. (Wagalatia 1:19)
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. (Yuda 1:1)
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. (Yohana 19:25)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56).
26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: “Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.” 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
Recent Comments