Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Maswali na Majibu kuhusu Biblia

Neno Bwana lina maana gani katika Biblia?
Neno Bwana Katika Biblia linamaanisha “Mungu Mtawala”

Mapokeo ya Mitume ndiyo nini?
Mapokeo ya Mitume ndiyo yale yote ambayo Yesu aliwakabidhi Mitume wake, na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu yatadumu hata mwisho wa dunia katika mafundisho, liturujia na maisha ya Kanisa.
“Nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vilevile kama nilivyowatolea… Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe” (1Kor 11:2; 15:3).
“Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu… Mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine” (2Tim 1:14; 2:2).
Tukikata huo mnyororo wa mapokeo, hata kama ni kwa kisingizio cha kushikilia Biblia, tunaachana na asili ya Kanisa.
“Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu… Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu” (2Thes 2:15; 3:6).

Maandiko Matakatifu ndiyo nini?
Maandiko Matakatifu ndiyo vitabu vyote 73 ambavyo viliandikwa na watu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu vikakusanywa na Kanisa kwa jina la “Biblia”, yaani “Vitabu”.
Hao “wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu” (2Pet 1:21).

Je, Biblia zote ni sawa?
Hapana, Biblia zote si sawa. Tujihadhari na matoleo mapungufu ambamo vimenyofolewa vitabu 7 vizima na sehemu kadhaa za vitabu vingine vilivyotumiwa na Wakristo wa kwanza.
“Amin, nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie” (Math 5:18). “Na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki” (Ufu 22:19).
Je wakristo Wakatoliki wanasoma Biblia kwenye Ibada ya Misa? Biblia inanukuliwa mara ngapi Kwenye Ibada ya misa ya Wakatoliki?
Ndiyo, Wakatoliki wanasoma Biblia kila siku wanapoadhimisha Ibada ya Misa wakati wa Liturujia ya Neno.
Wakatoliki wananukuu Biblia mara Tano kwenye Ibada ya Misa. Wananukuu wanaposoma somo la Kwanzaa, Somo la pili, wimbo wa katikati, Shangilio na Injili.

Tunatambuaje Maandiko Matakatifu kati ya maandishi yote ya binadamu?
Tunatambua Maandiko Matakatifu kati ya maandishi yote ya binadamu kwa njia ya Mapokeo, yaani kwa sababu yametumiwa na Kanisa tangu mwanzo kwa kulisha kwa hakika imani yake.
Tunahitaji Mapokeo kwa kuwa Maandiko yenyewe hayataji orodha ya vitabu vyake vyote, Sanasana Yesu alividokeza baadhi akisema yanamzungumzia na kutimia ndani yake,
“Ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii, na Zaburi” (Lk 24:44).
Halafu Barua ya Pili ya Mtume Petro ikalinganisha “na Maandiko mengine” nyaraka zote ambazo Paulo aliziandika “kwa hekima aliyopewa” (2Pet 3:15-16).

Sababu nyingine za Biblia kutojitosheleza ni zipi?
Sababu nyingine za Biblia kutojitosheleza ni kwamba mambo mengi muhimu hayakuandikwa,
“Kuna mambo mengine mengi aliyoyafanya Yesu, ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa” (Yoh 21:25).
Tena barua ni nusu tu ya kuonana; hivyo Yesu hakuandika lolote, nao Mitume hawakupenda kuandika yote.
“Kwa kuwa ninayo mambo mengi, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini nataraji kuja kwenu, na kusema nanyi mdomo kwa mdomo, ili furaha yetu iwe imetimizwa” (2Yoh 12).
“Nalikuwa na mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa wino na kalamu. Lakini nataraji kukuona karibu, nasi tutasema mdomo kwa mdomo” (3Yoh 13-14).
Hasa ibada haziwezi kufanyika kwa barua; k.mf. kuwekea mikono ili kumshirikisha Roho Mtakatifu. Paji la namna hiyo halipitii Maandiko, bali Mapokeo tu. Hatimaye Biblia ikipotoshwa haipingi, kwa kuwa si mtu hai anayeweza kujitetea.

Biblia iliandikwa kwa kusudi gani?
Biblia iliandikwa kusudi tupate “kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini” tuwe “na uzima wa milele” (Yoh 20:31).
“Tangu utoto umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. Kila Andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki” (2Tim 3:15-16).
Si lengo lake kutufundisha historia, jiografia wala sayansi: kuhusu elimu hizo na kuhusu ufasaha wa lugha Biblia ilitegemea ujuzi na vipawa vya watu walioiandika.

Je, vitabu vya Biblia vinatofautiana?
Ndiyo, vitabu vya Biblia vinatofautiana kwa kuwa Mungu alijifunua hatua kwa hatua; hivyo vitabu 46 vilivyoandikwa kabla ya Yesu vinaitwa Agano la Kale na 27 vilivyomfuata vinaitwa Agano Jipya.
“Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka” (Eb 8:13).
Mungu “ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha” (2Kor 3:6).

Je, vitabu vyote vya Biblia vinahusiana?
Ndiyo, vitabu vyote vya Biblia vinahusiana kwa kuwa vinaangaziana na kuunda kitabu kimoja ambacho ni Neno la Mungu yuleyule, ingawa katika hatua tofauti: Agano la Kale ndiyo maandalizi na Agano Jipya ndio utimilifu wake.
Yesu alisema, “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua Torati au Manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza” (Math 5:17).
Tunahitaji Agano la Kale ili tuelewe vizuri Agano Jipya katika maandalizi yake, na tunahitaji Agano Jipya ili tuelewe Agano la Kale lilivyotimilizwa na Yesu.

Je, inafaa tushike neno lolote la Agano la Kale kama Wayahudi?
Hapana, haifai tushike neno lolote la Agano la Kale kama Wayahudi wasiozingatia jinsi Yesu alivyolitimiliza kwa maneno na matendo hata wakamshutumu kutenda kinyume:
“Mtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato” (Yoh 9:16).
Alipofafanua amri 10 za Mungu alikariri:
“Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa… lakini mimi nawaambieni…” (Math 5:21,27,31,33,38,43).
Alipouliziwa unajisi wa vyakula kadhaa, alisisitiza,
“’Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi; kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni?’ Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote” (Mk 7:18- 19).
“Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo” (Kol 2:16-17).
Hakika, mwili ni mzito kuliko kivuli chake.
Vile vile katika Warumi 4:16. Tunasoma “Kwa sababu hiyo, jambo hili lategemea imani, hivyo kwamba ahadi hiyo yatokana na neema ya Mungu, na kwamba ni hakika kuwa ahadi hiyo ni kwa ajili ya wote:si kwa wale tu wanaoishika sheria, bali kwa wale waishio kwa Imani kama Abrahamu. Yeye ni Baba yetu sote.”
Wakristo wengine wanachanganywa na wale wasioyajua maandiko na kuwataka washike sheria na Torati,basi tukisema ni lazima kushika sheria tutakua tunakataa kua Abrahamu hakuwa mtu wa Mungu maana kwa Abrahamu hatukuwa na Sheria wala Torati na alipata kibali machoni Pa Mungu tuu kwa Imani. Kumbuka pia Abrahamu alitahiriwa baada ya Kuwa tayari mtu wa Mungu kwa Imani yake na sio kwamba Kutahiriwa ndio kulifanya mtu wa Mungu.
Tumekombolewa kwa Imani na sio kwa Sheria. Wagalatia 5:18 “Lakini Mkiongozwa na Roho hampo chini ya sheria”
Hatumtumikii Mungu ili tuwe watu wa Mungu bali tukishakua watu wa Mungu ndio tunamtumikia Mungu.

Yesu alitimiliza Agano la Kale kwa namna isiyotarajiwa hasa lini?
Yesu alitimiliza Agano la Kale kwa namna isiyotarajiwa hasa aliposulubiwa, akionekana na Wayahudi wenzake kama kwamba amelaaniwa:
“Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa: ‘Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti’; ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani” (Gal 3:13-14).

Kati ya vitabu vya Biblia, vilivyo bora ni vipi?
Kati ya vitabu vya Biblia, vilivyo bora ni Injili 4 zilizoandikwa na Mathayo, Marko, Luka na Yohane.
Ndio moyo wa Maandiko Matakatifu yote, kwa kuwa ndizo shuhuda kuu juu ya maisha na mafundisho ya Yesu.
Yeye “amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora. Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili” (Eb 8:6-7).

Tueleweje Maandiko Matakatifu?
Tuelewe Maandiko Matakatifu kwa kuzingatia hasa Mungu alitaka kusema nini kuhusu wokovu wetu kupitia waandishi wengi aliowaongoza kuyatunga kwa lugha na mitindo mbalimbali.
Lakini ebu, “Yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na Maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe” (2Pet 3:16).
Utitiri wa madhehebu yanayoshindana yakidai kushikilia Biblia tu unathibitisha uwekezano mkubwa wa kuipotosha kwa namna moja au nyingine.
“Utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia walimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo” (2Tim 4:3-4).
Njia pekee ya kukwepa fujo hiyo ni kuelewa Maandiko ndani ya Kanisa, kadiri ya Mapokeo yake hai.
“Lakini mtu yeyote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu” (1Kor 11:16).
Biblia nje ya Kanisa ni kama samaki nje ya maji.

Tupokeeje ufunuo wa Mungu?
Tupokee ufunuo wa Mungu kwa kusadiki mafundisho ya Kanisa lake, ili tuzidi kumjua na kuambatana naye bila ya kudanganyika. Yesu aliwaambia Mitume wake,
“Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma” (Lk 10:16).
“Sisi nasi twamsukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kwelikweli, litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini” (1Thes 2:13).

Neno “BIBLIA” maana yake ni nini?
Neno “BIBLIA” ni neno linalotokana na neno la Kigiriki “Biblion” lenye maana ya vitabu.
Biblia ni Mkusanyiko wa vitabu mbalimbali vya dini vilivyochaguliwa na kuidhinishwa kua vyafaa kutumika.

Biblia ni nini? Asili, Historia, waandishi na mipaka yake
Biblia ni mkusanyiko wa vitabu mbalimbali vinavyohusu kazi ya Mungu ya kuwakomboa mwanadamu kuanzia enzi za Mababu na manabii Wa Waisraeli, Enzi za Yesu na za Mitume wa Yesu.
Je, Biblia ilipatikanaje? Nini chanzo na asili ya Biblia.
Biblia iliundwa kwa kukusanya vitabu vya dini vya wakristo hapo awali na kuunda kitabu kimoja. Kwa maana hii, Biblia ni vitabu teule vya dini vilivyoonekana vinafaa kutumika kwa waumini Wakristo ili kusaidia Imani yao. Hivyo basi, kama Biblia ni vitabu teule tuu vipo vitabu vingine vya dini ambavyo havikuwekwa Kwenye Biblia.
Wakristo wa kwanza walichagua vitabu kadhaa na kuviweka pamoja na kisha kuvita Biblia. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu muhimu tuu vya dini mpaka kufikia Enzi za Mitume.
Je, Biblia ndicho kitabu pekee cha neno la Mungu?
Hapana, Biblia sio kitabu pekee cha neno la Mungu isipokua Biblia ni kitabu kilichoidhinishwa rasmi kutumika Kama kitabu kikuu cha Wakristo. Hii ni kwa sababu Biblia imeundwa na vitabu muhimu tuu vilivyochaguliwa na wakristo wa kwanza vilivyoonekana vinafaa kwa kufundishia, Ibada na kukuza Imani. Kwa hiyo basi vipo vitabu vingine ambavyo haikuwekwa Kwenye Biblia ambavyo ni Maneno ya Mungu.
Hii ndiyo sababu kwa nini Wakatoliki wana vitabu vingi kuliko madhehebu Mengine. Yaani sababu ni kwamba madhehebu Mengine walivitoa vitabu vingine vilivyounda Biblia. Na Wakatoliki waliweka vitabu vingine vya dini Kwenye Biblia walivyoona vinafaa pia kutumika.
Je nje ya Biblia hakuna Neno la Mungu au Maandiko matakatifu?
Nje ya Biblia kuna Neno la Mungu na Maandiko Matakatifu. Hii Inamaanisha kuwa Biblia sio kitabu pekee cha neno la Mungu. Zipo nyaraka na Vipo vitabu vingine vingi ambavyo viliandikwa na Manabii na Mitume ambavyo havikuwekwa kwenye Biblia lakini ni mafundisho ya Mungu. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vikuu vya Mungu.
Kumbuka kuwa sio nyaraka zote za Mitume ziliandikwa Kwenye Biblia. Vile vile manabii walikuwa ni wengi kuliko waliowekwa Kwenye Biblia.
Je Biblia ndiyo mafundisho ya Mungu pekee?
Hapana, Biblia sio mafundisho pekee ya Mungu. Hii ni kwa sababu sio mambo yote aliyofanya na kusema Mungu yaliandikwa na vilevile Mitume hawakua watu wa Mwisho kupokea Roho mtakatifu na kupokea neno la Mungu.
Biblia inatuthibitishia yenyewe kuwa haijakamilika na Si mambo yote yameandikwa Kwenye Biblia
Biblia inatuthibitishia kuwa haijakamilika tunaposoma (Yohane 21:25)
Biblia inatuambia hivi…”Kuna mambo Mengine mengi aliyofanya Yesu, ambayo Kama yangeandikwa yote, moja baada ya jingine, nadhani hata ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.”…Kwa mstari huu Biblia inatuthibitishia kuwa haikuandikwa vitu vyote.
Je Biblia ni mwisho wa Maandiko ya Mungu?
Biblia sio mwisho wa Maandiko ya Kimungu.
Biblia ni sehemu ya maneno ya Mungu mpaka miaka ya Mitume
Hata sasa Mungu anafanya kazi na watu wake kupitia Roho Mtakatifu na kwa kwa sababu hii Biblia sio mwisho wa kazi ya Mungu ya kusema na watu wake.
Mungu yu hai na anafanya kazi na watu wake mpaka sasa kwa kutumia vinywa vya watu Kama aliyofanya hapo awali.
Hata maneno unayohubiriwa sasa yanaweza kuwa ni kutoka kwa Mungu kwa maana hata waandishi wa Biblia walitumiwa na Mungu Kama wahubiri wa sasa. Mungu ni yule yule, Roho Mtakatifu ni yuleyule na Neno ni lile lile.
Kwa hiyo Biblia ni maneno yaliyochaguliwa mpaka enzi za Mitume. Vitabu vilivyofwata Baada ya Mitume japokuwa viliandikwa kwa Roho Mtakatifu havikuwekwa Kwenye Biblia.
Sababu ya Kanisa katoliki kutumia mapokeo na Maandiko ya Watakatifu
Kanisa katoliki linatumia mapokeo na Makala za watakatifu kwa Imani kuwa Mungu yule yule aliyefanya kazi tangu zamani anafanya kazi na watu wake mpaka sasa na hivyo Maandiko ya watu wa Mungu yanafaa kutumika kama yalivyotumika ya watu wa kale.
Yesu alituambia nini kuhusu Neno la Mungu na Mwendelezo wa kazi ya Mungu ya kusema na watu?
Yesu alituambia hivi katika (Yohane 16:12-15)..”Ninayo mengi ya kuwaambieni Ila kwa sasa hamuwezi kuyastahimili. Lakini atakapokuja huyo Roho wa Ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote. Maana hatasema kwa Mamlaka yake mwenyewe bali atasema atakayoyasikia na kuwajulisheni yatakayokuja. Yeye atanitukuza Mimi kwa kuwa atawajulisheni Yale atakayoyapata kutoka kwangu “…
Sasa basi,kama Roho Mtakatifu ni yuleyule na kazi zake ni Zile Zile za tangu Mitume, kwa nini hatukubali kuwa Anafanya kazi mpaka sasa kupitia watu wa Mungu? Kwa nini tunakataa mafundisho yao? Kwa nini tunashindwa kuelewa kuwa Biblia haikuwa mwisho wa Neno la Mungu? Kwa nini tunakana Mapokeo ya Watakatifu? Kwa nini hatuwaamini watumishi wake wa sasa?

Biblia ina sehemu kuu ngapi?
Biblia ina sehemu kuu 2 (mbili) ambazo ni
1. Agano la Kale (A.K)
2. Agano Jipya (A.J)

Agano la Kale lina vitabu vingapi?
Agano la Kale lina vitabu 46

Agano Jipya lina vitabu vingapi?
Agano Jipya lina vitabu 27

Biblia nzima ina vitabu vingapi?
Biblia nzima ina vitabu 73

Vitabu vya Agano la Kale vimegawanywa katika sehemu ngapi?
Vitabu vya Agano la Kale vimegawanywa katika sehemu 4 nazo ni
1. Vitabu vya Musa (5)
2. Vitabu vya Historia (16)
3. Vitabu vya Hekima (7)
4. Vitabu vya Manabii (18)

Vitabu vya Agano Jipya Vimegawanywa katika sehemu ngapi?
Vitabu vya Agano Jipya Vimegawanywa katika sehemu 4 nazo ni
1. Injili (4)
2. Kitabu cha Matendo ya Mitume
3. Nyaraka mbalimbali (21)
4. Kitabu cha Ufunuo

Vitabu vya Musa ni vipi?
Vitabu vya Musa ni
1. Mwanzo
2. Kutoka
3. Walawi
4. Hesabu
5. Kumbukumbu la Torati

Wainjili wanne Katika Agano Jipya ni wakina nani?
Wainjili wanne Katika Agano Jipya ni
1. Mathayo
2. Marko
3. Luka
4. Yohane

Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano la Kale ni vipi?
Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano la Kale ni
1. Cha kwanza ni Kitabu cha Mwanzo
2. Cha mwisho ni Kitabu cha Malaki

Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano Jipya ni vipi?
Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano Jipya ni
1. Kitabu cha kwanza ni Injili ya Mathayo
2. Kitabu cha mwisho ni Kitabu cha Ufunuo

Injili ni nini?
Injili ni Habari njema ya wokovu iliyoletwa na Yesu Kristo

Watoto wawili wa Adamu na Eva walkikuwa wepi?
Walikuwa ni Kaini na Abeli

Watoto wa Nuhu ni wepi?
Watoto wa Nuhu ni Shemu, Hamu na Nefteli

Mababu watatu wa Imani Katika Biblia ni wakina nani?
Mababu wa Imani ni Ibrahimu, Isaka na Yakobo

Watoto wa Yakobo ni Wepi?
Watoto wa Yakobo ni
1. Reubeni
2. Simeoni
3. Lawi
4.Yuda
5. Dani
6. Naftali
7. Gadi
8. Asheri
9. Isakari
10. Zabuloni
11. Yosefu
12. Benjamini

Nani aliwatoa Waisraeli MIsri na Kuwaongoza Katika nchi ya Ahadi?
Musa ndiye aliwatoa Waisraeli MIsri na Kuwaongoza Katika nchi ya Ahadi

Mungu alimpa Musa Amri Kumi wapi?
Mungu alimpa Musa Amri Kumi katika mlima wa Sinai

Vitabu vya Historia katika Biblia ni vipi?
Vitabu vya Historia katika Biblia ni
1. Yoshua
2. Waamuzi
3. Ruthu
4. 1 Samweli
5. 2 Samweli
6. 1 Wafalme
7. 2 Wafalme
8. 1 Mambo ya Nyakati
9. 2 Mambo ya Nyakati
10. Nehemia
11. Ezra
12. Tobiti
13. Yudith
14. Esta
15. 1 Wamakabayo
16. 2 Wamakabayo

Vitabu vya manabii katika Biblia ni vipi?
Vitabu vya Manabii ni
1. Isaya
2. Yeremia
3. Maombolezo
4. Baruku
5. Eekieli
6. Danieli
7. Hosea
8. Yoeli
9. Amosi
10. Obadia
11. Yona
12. Mika
13. Nahumu
14. Habakuki
15. Sefania
16. Hagai
17. Zekaria
18. Malaki

Vitabu vya Hekima Katika Biblia ni Vipi?
Vitabu vya Hekima ni
1. Yobu
2. Zaburi
3. Mithali
4. Mhubiri
5. Wimbo ulio Bora
6. Hekima ya Solomoni
7. Yoshua Bin Sira

Nyaraka za Mitume katika Biblia ni zipi?
Nyaraka za Mitume ni;
1. Waroma
2. 1 Wakorinto
3. 2 Wakorinto
4. Wagalatia
5. Waefeso
6. Wafilipi
7. Wakolosai
8. 1 Wathesalonike
9. 2 Wathesalonike
10. 1 Timotheo
11. 2 Timotheo
12. Tito
13. Filemoni
14. Waebrania
15. Yakobo
16. 1 Petro
17. 2 Petro
18. 1 Yohane
19. 2 Yohane
20. 3 Yohane
21. Yuda

Je, Bikira Maria alikua na watoto wengine Mbali na Yesu?
Je, Bikira Maria ni Bikira Daima au alizaa watoto wengine?
Jibu fupi ni kwamba Bikira Maria hakuzaa watoto wengine na hakuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu
Hapo zamani hakuna mkristu au dehebu lolote lililokuwa linapinga kuwa Bikira Maria sio Bikira Daima hata Waprotestanti/walokole waliamini Bikira Maria ni Bikira Hata Baada ya Kumzaa Yesu. Kwenye Miaka ya 1400-1600 Watu wote wakwanza waliopinga Kanisa Katoliki walikubali kuwa Bikira Maria ni Bikira daima wakiwemo Martin Lutha aliyeanzisha kanisa la Lutheran, John Calvin aliyeanzisha Ulokole/Protestanti, Mchungaji Ulrich Zwingli, Heinrich Bullinger, and Thomas Cranmer. Kwa miaka zaidi ya 350 Waprotestant/walokole waliendelea kuamini kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.
Lakini baadae wakristo wengi walianza kupinga kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.
Tunaweza kuthibitisha kuwa Bikira Maria hakuzaa watoto wengine kwa kunukuu Biblia Kama ifuatavyo;
1. Bikira Maria Alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu
Biblia inatuambia wazi kwamba Bikira Maria alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu Kama tunavyosoma katika Luka 1:26-35
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe.” 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” 34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)
2. Biblia Haiwataji ndugu wa Yesu wakati Yosefu na Maria walipokimbilia Misri kumficha Yesu na wakati waliporudi
19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.” 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.” Matayo 2:19-23
Kama wangekuwepo wadogo zake Yesu Biblia ingetuambia kwamba walikuwa wapi wakati huo na walikuwa na Yesu au la.
3. Biblia haituambii kuwa Yesu alikua na wadogo zake alipokuwa na miaka 12
Wakati wa Maria, Yoseph na Yesu walipoenda Yerusalemu Yesu akiwa na miaka 12 Biblia haituambii kuwa Yesu alikuwa na wadogo zake na walikuwa wapi. Kumbuka walikuwa na Desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka kwa ajili ya Pasaka familia nzima kama familia. Je hao watoto wengine walikuwa wapi. Kwa nini walikuwa na Yesu Mwenyewe? Maana yake ni kwamba Yesu hakuwa na Wadogo zake.
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.” 49 Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
Kwa hiyo Biblia haionyeshi kuwa Yesu alikuwa na kaka na dada wakati akiwa na miaka 12. Kama wangekuwepo wangetajwa hapa kuwa walikuwa pamoja na Wazazi wao kama Yesu au walikuwa na Yesu wakati anapotea. Biblia haituambii chochote kwa hiyo wakati huo hapakuwa na wadogo zake Yesu.
4. Kukosekana kwa neneo “Binamu” kwenye lugha ya Yesu
Wakristu wa kwanza pamoja na Yesu aliongea Kiaramaiki au Kiebrania. Katika lugha zote hizo hakuna neno “Binamu” kwa hiyo mabinamu walijulikana kama dada na kaka wa mtu. Kwenye Agano jipya Neno kaka na Dada lilitumika pia kuwakilisha binamu.
Biblia inapotuambia kuwa Kaka na dada zake Yesu haimaanishi kaka wa kuzaliwa bali ndugu au Binamu
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kwa hiyo wanaotajwa hapa ni ndugu wa Yesu kwa maana maneno kama; ndugu, kaka au dada lilitumika badala ya Binamu yaani mtoto wa shangazi au mjomba. Hapa juu Yosefu ametajwa kama kaka yake Yesu lakini tunajua kuwa Yosefu ni Baba yake Yesu. Baba na mwana hawawezi kuwa na jina sawa.
5. Biblia haitumii neno Ndugu, kaka au dada ikimaanisha ndugu wa kuzaliwa mama mmoja na baba mmoja
Sio mara zote Biblia imetumia neno Ndugu kumaanisha ndugu (Dada na Kaka) wa kuzaliwa yaani kaka na dada kwa mfano
Kwa kuangalia lugha ya Kiswahili na Kiingereza 1 Wakorintho 15:6 tunaona tafsiri tofauti.
KISWAHILI 6 Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa.
ENGLISH 6 After that, he appeared to more than five hundred of the brothers and sisters at the same time, most of whom are still living, though some have fallen asleep.
Kwa hiyo hapa neno kaka dada na ndugu linaonekana wazi halikumaanisha ndugu au kaka wa damu.
6. Undugu wa Yakobo, Simoni, Yosefu na Yuda kwa Yesu Sio wa mtu na kaka zake
Wasemao kuwa Bikira maria alikuwa na wana zaidi ya Yesu wananukuu kifungu hiki;
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kumbuka kulikuwa na Yakobo wawili wakati wa Yesu, Vifungu vifuatavyo yunaweza kuona kuwa kulikuwa na yakobo wawili ambao walikuwa ndugu za Yesu lakini sio kaka wa kuzaliwa kwa mama.
35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)
Tunaweza kuona Undugu huu na Yesu kwa kusoma;
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. (Wagalatia 1:19)
Lakini Yuda anasema;
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. (Yuda 1:1)
Kwa hiyo Yakobo na Yohane walikuwa watoto wa Mama mwingine ambao baba yao ni Zebedayo. Na Yakobo na Yosefu walikuwa watoto wa Maria Mwingine. Kwa hiyo ni Yakobo wa wili wa Mama wengine Tofauti na Maria. Yuda alikuwa ni ndugu yake Yakobo. Yakobo vilevile alikuwa ndugu yake Yesu.
Kuthibitisha kuwa Hawa kina Mama ndio waliokuwa Mama zao kina Yakobo wote hao wawili na wengine tunaweza kusoma;
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. (Yohana 19:25)
Kwa hiyo kwenye (Yohana 19:25) tunaona Kuwa ni kwenye Msalaba wa Yesu alikuwepo Mama yake Yesu (Bikira Maria), Dada yake Bikira Maria, Mke wa Cleopa na Maria Magdalena. Na kwenye (Matayo 27:55-56) wamwtajwa ni Mama za kina nani kama inavyoonekana kwenye kifungu kifuatachi;.
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56).
Kwa hiyo hii ina maanisha kulikua na wanawake watatu wenye majina sawa ya Maria waliokuwa chini ya Msalaba. Yakobo na Yuda walikuwa watoto wa Maria Mke wa Cleofasi, na sio Mama wa Yesu, na hivyo sio kaka za Yesu.
7. Yesu alimwacha Mama yake kwa Yohane kwa kuwa hakuwa na Kaka na dada wakumwachia mamaye
26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: “Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.” 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
Ndiyo maana Bikira Maria tangu siku ile alihamia kwa Yohani kwa kuwa hakuwa na watoto wengine.

Baba wa Yesu Kristo ni nani?
Baba wa Yesu Kristo ni Mungu Mwenyewe

Baba Mlishi wa Yesu Kristu ni nani?
Baba mlishi wa Yesu Kristo ni Yosefu Mtakatifu (Mt 1:18-20)

Yesu Kristu alizaliwa wapi?
Yesu Kristu alizaliwa Bethlehemu pangoni (Lk 2:4-7)

Nini maana ya Jina Bethlehemu?
Bethlehemu maana yake ni
Nyumba ya mkate

Yesu Kristu aliishi wapi kabala ya kuanza kazi yake?
Yesu Kristu Aliishi Nazareti kabla ya kuanza kazi yake

Mtangulizi wa Yesu Kristu ni nan?
Mtangulizi wa Yesu Kristu ni Yohani Mbatizaji

Wazazi wa Yohani Mbatizaji ni nani?
Wazazi wa Yohani Mbatizaji ni Zakaria na Eizabeti

Wazazi wa Bikira Maria ni nani?
Wazazi wa Bikira Maria ni Yoakimu na Anna

Mitume kumi na wawili wa Yesu Kristu ni wapi?
Mitume wa yesu ni;
1. Simoni/Petro
2. Yakobo
3. Yohane
4. Andrea
5. Filipo
6. Barttholomayo
7. Mathayo
8. Thomaso
9. Yakobo wa ALfayo
10. Thadayo (Yuda Thadey)
11. Simoni Mkanaani
13. Yuda Iskarioti – Aliyemsaliti

Baba Mtakatifu wa kwanza ni nani?
Baba Mtakatifu wa Kwanza ni Mt. Petro

Nani ni Mitume wa Mataifa?
Mitume wa mataifa ni Paulo na Barnaba

Nani ni shahidi wa kwanza katika Agano Jipya?
Shahidi wa Kwanza ni Mt Stefano

Yesu Alianza kuhubiri injili kwa maneno gani?
“Wakati umetimia na ufalme wa Mungu umekaribia, tubuni na kuiamini Injili” (Mk 1:15)

Yesu alitukomboa kwa hatua zipi?
Yesu alitukomboa kwa Hatua Mbili (2) ambazo ni;
1. Mafundisho yake
2. Mateso, Kifo na Ufufuko wake

Sentesi saba za Yesu msalabani ni zipi?
Sentesi saba za Yesu Msalabani ni;
1. Baba uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya (Lk 23:34)
2. Nakuambia Hakika leo utakuwa pamojanami Mbinguni (Lk 23:43)
3. Mama huyu ndiye mwanao (Yoh 19:26)
4. Tazama huyu ndiye Mama yako (Yoh 19:27)
5. Eloi, Eloi, lema Sabakthani (Mk. 15:34) Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?
6. Naona kiu (Yoh 19:28)
7. Yametimia (Yoh 19:30)

Huyu bibi kweli kiboko, cheki alichofanya akiwa na babu

Bibi na Babu walisafiri wakielekea kwa mtoto wao ambae hawajamuona zamani.

Walipofika njiani wakawa wamechoka Sanaa. Wakaamua kutafuta hotel ili walale.

Wakakubaliana walale kwa masaa 4. Wakalala, Walipoamka, mfanyakazi wa Hotel akawatoza Tsh. 500,000/=

Wale wazee wakashangaa hata kama ni hotel ya kisasa lakini sio laki tano kwa masaa 4.

Babu akagoma kulipa akasema aitiwe meneja.

Meneja akaja kuwasikiliza

Babu: ” Kwanini bili ni kubwa hata kama ni hotel ya kisasa?”

Manager;“kuna maswiming puli, ya kisasa “

Babu; “Lakini hatukuyatumia”

Manager; “Ah ah ah. Lakini mungeweza kama mngetaka”

Babu: “Hata hivo bado haithamini kuwa laki 5”

meneja: “Pia Kuna waimbaji kutoka sauzi, Uganda , Congo”

Babu: “Lakini sisi hatukuwasikiliza”

Meneja: “Ndiooo. Lakini mngeweza kama mngetaka”

Babu; aka give up na kumwambia mkewe andika cheki uwape,,

Bibi akaandika akampa meneja.

Meneja anaangalia anaona sh. 50,000

Akashangaa na kusema. “VP mbona hamsini'”

Bibi akajibu “450,000 ya kulala na mimi”

Meneja akajibu; “Lakini sijalala”

Bibi :“ungeweza kama ungetaka”

Umeshawahi kufanya hili jaribio?

Figisu ya Leo. UMESHAWAHI KUFANYA HILI JARIBIO.?

kadri temperature inavyo ongezeka chura nae huwa ana increase temperature ya mwili wake..

pindi inapokaribia kufika boiling point yaani nyuzi 100 chura atashindwa kuongeza temperature ktk mwili wake na hapo ndipo atataka kutoka ktk maji hayo ya moto na yanayo endelea kuchemka..
kutokana na kutumia nguvu nyingi sana ktk kuongeza temperature ktk mwili wake,pindi anapotaka kuruka atashindwa na atakufa humo ndani ya chombo cha maji yanayochemka..
SWALI; NINI KIMEMUUA CHURA.!??
Najua utaniambia ni maji ya moto…
La hashaa.!
kilichomuua chura ni kushindwa kufanya maamuzi mapema ya kutoka katika chombo cha maji yanayochemka hali ya kuwa bado nguvu anazo..
FUNZO
Fanya maamuzi sahihi sasa kabla nguvu za kutaka kufanya changes hazijakuishia kama yaliyomkuta chura..
NOTE; Kuvumilia jambo usiloliweza ni sifa ya punda.
BADILIKA.

Jinsi ya kufanya kupunguza mwili kwa kupanga ulaji wa chakula

Ulaji wa vyakula vingi vya wanga na mafuta ni chanzo kikubwa cha unene na uzito kuongezeka. Vyakula kama ugali,wali,mkate mweupe,bia na pombe za kienyeji zinazotokana na wanga (kimea) huchangia kuongezeka kwa uzito. Matumizi ya aina hii ya chakula ni muhimu kupunguzwa katika mlo wako.

Yafuatayo ndiyo mambo ya msingi ya kuzingatia katika ualaji wa chakula ili kupunguza mwili

Acha kula vyakula vya Sukari

Sukari inayozidi mwilini toka katika vyakula hubadilishwa na kuwa mafuta. Vyakula kama chokuleti,biskuti,keki na vinyaji kama soda vina kiwango kikubwa cha sukari. Pia usitumie sukari nyingi katika chai na juisi.

Kula mboga mboga na matunda kwa wingi

Mboga mboga ni nzuri kwa afya kwa ujumla lakini pia haina mafuta hivyo itakufanya kuingiza mafuta kidogo mwilini.

Tumia Chai ya kijani

Umesikia kuhusu chai ya kijani (Green Tea), ni chai ambayo ni ya kijani na inasaidia kuondoa sumu za mwili (antioxadation). Hii inasaidia katika kusaidia mwili kuunguza mafuta katika njia inayoitwa thermogenesis.

Tumia chai ya Tangawizi

Tangawizi kama ilivyo chai ya kijani inafahamika kuongeza mmeng’enyo wa chakula tumboni hivyo kupunguza mrundikano wa mafuta yasiyotumika

Kunywa Maji mengi

Maji yanachangia kuharakisha mfumo wa uvunjaji chakula tumboni na hivyo kupunguza mafuta yanayohifadhiwa.

Matunda halikadharika hayapunguzi uzito moja kwa moja bali yatakufanya ushibe na usitamani kula kila mara kwani yanakata hamu ya chakula. Hivyo utaokoka na tabia ya kula kila mara ambayo huchangia sana kuongezeka uzito.

Acha kula kula ovyo nje ya milo maalumu

Uzito na kula kula hovyo ni marafiki wakubwa. Ukiona mtu ni mnene ujue anapenda kula. Ile kweli anakulakula ikimaanisha anakula kila mara na kila wakati chakula kinapokuwepo.

Anza leo kujenga tabia ya kula kidogo na katika milo muhimu mitatu.

Punguza matumizi ya Chumvi

Ndiyo,chumvi inaongeza uzito. Sodiamu iliyomo katika chumvi inachangia katika mchakato wa kikemikali unaopelekea kuongezeka uzito. Tumia chumvi katika kiwango kidogo.

Umakini katika kuwaza

Kuwa makini sana na mawazo yako, Yanaweza kukupeleka Mbinguni au motoni.


Kumbuka vile unavyowaza ndivyo utakavyovitenda.


Amua kuwaza mema kutoka ndani ya moyo wako kisha utatenda mema katika maisha yako


Kumbuka Mungu humhukumu mtu kwa mawazo yake maana mawazo ya mtu ndiyo mtu mwenyewe


Tuwaze mema wapenzi ili tuwe wema

Kuwa Makini na Mawazo Yako

Kuwa makini sana na mawazo yako, yanaweza kukupeleka Mbinguni au motoni. Mawazo ni nguvu inayoweza kuelekeza maisha yako kwa njia ya heri au shari, na ni muhimu kuyadhibiti na kuyatumia kwa njia inayofaa.

“Ndivyo aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.” (Mithali 23:7)
“Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema; na mtu mwovu katika hazina mbaya hutoa yaliyo mabaya; kwa kuwa wingi wa moyo huongea kinywa chake.” (Luka 6:45)
“Tena mkiwaza hayo, yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya staha, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema, ikiwepo wema wowote, ikiwa na sifa njema yoyote, mawazeni hayo.” (Wafilipi 4:8)

Mawazo Yanaelekeza Matendo

Kumbuka vile unavyowaza ndivyo utakavyovitenda. Mawazo yako yanaathiri moja kwa moja matendo yako. Unapowaza mema, utatenda mema; unapowaza mabaya, utatenda mabaya. Hivyo, ni muhimu kuzingatia na kuimarisha mawazo yako kuwa chanya na yenye kujenga.

“Kwa maana nimemwita Bwana siku zote; heshima na utukufu una mpata.” (Zaburi 19:14) “Mkishika maagizo yangu, mtapata uzima; tena msifanye mfano wa matendo ya nchi ya Misri mliyokaa, wala msifanye mfano wa matendo ya nchi ya Kanaani niliyowaleta; wala msizifuate sheria zao.”_ (Mambo ya Walawi 18:3-4)
“Jishughulisheni na mawazo yaliyo juu, wala siyo ya chini.” (Wakolosai 3:2)

Amua Kuwaza Mema

Amua kuwaza mema kutoka ndani ya moyo wako kisha utatenda mema katika maisha yako. Uamuzi wa kuwaza mema unatokana na kujitolea kuwa na moyo safi na mwenye nia njema. Jenga tabia ya kusoma na kutafakari Neno la Mungu ili moyo wako uweze kujazwa na mawazo mema yanayokuza tabia njema.

“Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu.” (Zaburi 119:105)
“Nitalificha neno lako moyoni mwangu, nisije nikakutenda dhambi.” (Zaburi 119:11)
“Mwenye hekima ana moyo wa busara, neno la Mungu ni ngao kwake.” (Mithali 14:33)

Hukumu ya Mungu kwa Mawazo

Kumbuka Mungu humhukumu mtu kwa mawazo yake maana mawazo ya mtu ndiyo mtu mwenyewe. Mungu anaangalia moyo wa mtu na mawazo yanayotoka ndani yake. Ni muhimu kujitahidi kuwa na mawazo yanayoendana na mapenzi ya Mungu ili tuweze kumpendeza.

“Kwa maana neno la Mungu ni hai, tena lina nguvu, tena lina makali kuliko upanga wowote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake, tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.” (Waebrania 4:12)
“Kila njia ya mtu ni safi machoni pake mwenyewe, lakini Bwana huzipima roho.” (Mithali 16:2)
“Kwa maana mimi, Bwana, nachunguza mioyo, nakijaribu viuno, nimpe kila mtu kwa kadiri ya njia zake, kwa kadiri ya matunda ya matendo yake.” (Yeremia 17:10)

Mawazo Mema Yanaweza Kutupeleka Kwa Wema

Tuwaze mema wapenzi ili tuwe wema. Mawazo mema hujenga tabia nzuri na matendo mema. Ni jukumu letu kujitahidi kuwaza na kutenda mema kila wakati, kwani kwa kufanya hivyo, tunakuwa vyombo vya amani na upendo wa Mungu duniani.

“Wenye amani hawatafutwa kwa bure, bali watapata furaha ya Bwana.” (Isaya 32:17)
“Kwa hiyo, wote mnaoamini, muwe na nia moja, wenye huruma, wenye kupendana kama ndugu, wenye huruma nyingi, wanyenyekevu.” (1 Petro 3:8)
“Na Bwana mwenyewe awafanye ninyi mzidi sana na kuongezeka katika upendo ninyi kwa ninyi na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu.” (1 Wathesalonike 3:12)

Kwa hivyo, tuwe makini na mawazo yetu, tuwe na nia ya kuwaza mema, na tuishi kwa kutenda matendo mema yanayotokana na mawazo hayo. Mungu anapenda watu wenye moyo safi na wenye nia njema, na atawabariki kwa wingi wa rehema na neema zake.

Mizigo tuliyoibeba ambayo haina faida

1.💥Umejipa jukumu la kuwa “mpelelezi” wa maisha ya wengine na umesahau maisha yako.

2.💥Umebeba vinyongo na visasi moyoni vinavyokufanya uwafikirie waliokuumiza zaidi kuliko kufikiria furaha na maendeleo yako.

3.💥 Una marafiki wengi ambao ni kama kupe, wapo kukutumia tu na hawachangii lolote katika maendeleo zaidi ya kujifanya ndio watu wako karibu lakini kumbe wapo kwa maslahi yao!

4.💥Umeweka mbele zaidi “watu watanichukuliaje” kuliko kuangalia maisha yako.Watu ndio wanakuchagulia aina ya maisha unayoishi na unajilazimisha kuishi kama wao hata kama huna uwezo huo.

5.💥Unaongea zaidi ya kasuku lakini vitendo hakuna. Unatamani mafanikio tu moyoni lakini huna mipango ya kuyafikia.
6.💥Maisha yako yote umeyaweka kwenye mitandao ya kijamii. Huna siri hata moja! Hivyo unalazimika kuishi aina ya maisha ambayo yataendelea kufanana na yale uliyoyaweka kwenye mitandao ya jamii kwa sababu ukibadilika tu watasema “umefulia”

7.💥Kila aliefanikiwa ni rafiki yako au utasema ni mtu wako wa karibu na unaishia kuwasifia tu na kupiga nao picha lakini hujifunzi kutokana na mafanikio yao na wala hutumii fursa hiyo ya kujuana nao.

8.💥Upo sahihi kila siku(you are always right). Huambiliki, hushauriki na kila wazo atakalotoa mwenzako basi si zuri ila la kwako ndio sahihi na utataka litekelezwe hilo hilo. Mwisho wa siku kila mtu anakukimbia hakuna wa kukuambia “hapa umekosea” kwa sababu ya ujuaji wako.

9.💥Hujifunzi maarifa mapya.Mara ya mwisho kusoma kitabu ilikuwa ni “Ngoswe, penzi kitovu cha uzembe” Tena ni kwa sababu ilikuwa ni kwa ajili ya kujibia mtihani. Hujifunzi “life skills” wala ujuzi mwingine.

10.💥Unazurura mno mitandaoni bila faida. Kwako wewe intaneti ni kwa ajili ya kuchati tu na kufuatilia habari za mjini ambazo tangu umeanza kuzifuatilia hujawahi kuingiza hata shilingi moja, zaidi unateketeza tu hela yako ya vocha.

ISHUSHE hiyo mizigo kama kweli inahitaji kusonga mbele!

Faida za matumizi ya Ukwaju kiafya

Faida kuu za ukwaju ni kama ifuatavyo:

Huondoa sumu Mwilini

Chanzo kizuri cha viua sumu mwilini ‘antioxidants’ ambavyo huzuia Saratani (cancer)

Una Vitamin B na C

Chanzo cha Vitamini B na C vile vile “carotentes”

Huondoa homa

Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo

Huzuia mafua

Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni

Husaidia mmengenyo wa chakula

Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa

Hutibu nyongo

Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)

Husaidia kurahisisha choo (laxative)

Hupunvuza Lehemu

Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo

Husaidia Ngozi

Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidonda

Huua minyoo

Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo

Ufalme wa simu wa sasa

➡ Asubuhi saa 12 : 00 mtu anaamka, kabla hata HAJAMUSHUKURU MUNGU, kabla hata hajatoka kitandani, kabla hata hajajifunua shuka,

👉ATARIPOTI KWA SIMU KWANZA KABLA YA KURIPOTI KWA YEYOTE, NDIO HAPO UNAONA MTU AKIAMKA KABLA HATA HAJASALI KWA MUNGU ANAAMKIA SIMU KWANZA KUIKAGUA,
– Nani alinitafuta?
-Nani alini-text?
-WhatsApp nani kanitumia msg?
– kwenye magroup kuna mpya gani?
– Fb kuna post gani kali?
– nani kaweka picha kali leo?
Nk.
Akimaliza KURIPOTI KWA Simu, faster faster, anapiga kaombi ka kidesturi, sekunde 20 basi.
Biblia ipo hapo kando tu ya kitanda, lkn anaona hana muda wa kuisoma.
✴BADALA YA KUANZA SIKU NA BWANA, MTU ANAANZA SIKU NA SIMU.
Pamoja na kazi za kuutwa, za mtu huyo, lkn atafanyq juu chini, apate muda wa KURIPOTI kwa SIMU.
Lakini mtu huyo huyo, hawez kbsa kupata muda wa kujitenga angalau kwa dk 3 tu, kw kutwa nzima ARIPOTI KWA MUNGU KWA NJIA YA MAOMBI.
Ana muda wa kusoma status kwenye social media kutwa nzima,
Lkn hana muda kbsa wa kupitia angalau sura moja tu, ya Biblia kwa siku.
Ana bundle la dk, sms, WhatsApp kila siku, lkn hana sadaka ya kumtolea Mungu.
Umeme ukikatika kutwa moja tu, akakosa kuwa na simu sababu ya chaji, anajisikia mpwekee, siku anaiona ndefuu, anajiona amepungukiwa saana!
Lakini huyo huyo, siku nzima inaisha, na ya pili, ya tatu , hajawahi kuwa na muda na Mungu wake hata kidogo, na anaona ni sawa tu.
Hata ktk siku ya ibada, yale masaa machache tu ya ibada, ambapo inatakiwa iwe ni mtu na Mungu wake tu, bila kuingiliwa na chochote, 👉mtu bado hawezi kukaa bila KURIPOTI kwa simu, ibada inaendelea huku mtu kawasha data, na anasoma na kujibu msg zake km kawaida.
👉 au kama ana kaustaraabu kidogo, atatoka nje, huko anaenda kukagua msg, kuangalia updates nk.
SIMU UNAYO KUTWA, KUCHWA, KIIILA SIKU, YANI HUKUWEZA KUVUMILIA KUIWEKA PEMBENI KWA MASAA TU?
➡ Swali nauliza, Mtu wa aina hiyo Mungu wake ni nani?
” Usiwe na miungu mingine ila mimi”.
KUTOKA 20 : 3
Kumuabudu Mungu peke yake, ni kumfanya Mungu awe wa KWANZA MOYONI NA MAWAZONI MWAKO.
Kumfanya awe kipaumbele kwenye kiila ulitendalo.
➡WENGI WAMEZIFANYA SIMU ZAO, ZICHUKUE NAFASI YA MUNGU KATIKA MIOYO, FIKRA NA MAISHA YAO KWA UJUMLA.
➡Wamekuwa tayari kupoteza karibu kiila kitu kwa ajili ya simu
– kupoteza marafiki > hawana muda na marafiki zao, wanajifungia ndani, wakichati.
– hawana muda na wazazi wao, hata kama wanaishi nyumba moja. > kijana akifika nyumbani, anapitiliza chumbani, ni yeye na simu, ataonekana muda wa kula tu, tena sometimes hata mezani anakuwa na simu, pale mezani wako wazazi wake kbsa, ndugu zake nk, lkn hajali uwepo wao, anaendelea na simu tu.
– Hawana muda na Mungu > Anahakikisha vyovyote itakavyokuwa, muda wa kuwa na simu unapatikana, HATA KAMA HILO LITAMAANISHA KUUPORA MUDA WA MUNGU (muda wa ibada).
Atakosa fedha za kusaidia wahitaji, fedha za zaka na sadaka, lkn fedha ya SIMU, (bundles) , lzm inakuwepo.
➡Mtu wa aina hiyo, anaiabudu simu bila kujua.
➡KITU CHOCHOTE KINACHOUVUTA MOYO KUTOKA KWA MUNGU, KUKIELEKEA CHENYEWE, KITU HICHO KINAJARIBU KUCHUKUA NAFASI YA MUNGU MOYONI.
NB: Sio lengo langu kupinga matumizi ya simu, lkn nilitaka tuwe na kiasi.

Mambao ya saluni ni shida, cheki kilichotokea kwa huyu

DADA alienda Salon wakati anasukwa akaingia
MKAKA mtanashati,
DADA akaamua kujaribu bahati yake.
DADA:Mambo? KAKA:Poa.
DADA:Mimi na wewe tunaweza kuongea baade?
KAKA:Kuhusu nini?
DADA:Nimekupenda nataka nikutoe out.
KAKA:Sawa ila nitamwambia nini
MKE wangu?
DADA:Aah ilo sio tatizo mdanganye tu,mwambie unakwenda kumtembelea rafiki yako hospitalini.
KAKA:Mwambie mwenyewe huyo hapo anayekusuka.

 

Unajua nn kiliendelea?

Jaribu kufikiria haya

1. Uelekeo ni muhimu kuliko kasi. Ni heri kwenda taratibu katika Uelekeo sahihi, kuliko kwenda kwa kasi katika Uelekeo usio sahihi.

2. Kulalamika mambo hayaendi wakati wewe mwenyewe hujui unakokwenda ni kuwa na matatizo ya akili.

3. Kasi yako inaamuliwa sana na umbali unaoweza kuona. Kama huoni chochote mbele ya maisha yako, basi huna chochote.

4. Sayansi inadai kuwa kazi ni nguvu inayotumika kusukuma kitu kwa umbali fulani kwenye Uelekeo maalumu. Kwa hiyo kama unatumia nguvu kusukuma mambo, lakini hayana Uelekeo maalumu jua kwamba hufanyi kazi yoyote, unapoteza nguvu tu.

5. Masaa yanaenda, siku zinapita, miaka inaongezeka, umri wako ndio unaenda hivyo, unafanya nini katika maisha?

Mzee wa kichaga na hela zake. Angalia anachofanya

Mzee moja alikuwa kila usiku anapita mbele ya bank anasimama,kisha anapiga honi,akitoka askari mlinzi,anaondoka.Hilo jambo likamkera sana askari mlinzi, askari akawa na mvizia yule mzee wa kichaga ,siku alipokuja tena akamkamata, akamuuliza kwa nini unakuja unapiga honi kisha unakimbia? Mzee akasema: Haki ya mungu babaangu , Nina pesa zangu ktk account hapa bank naogopa usilale usingizi ndo maana kila siku usiku napita kukuangalia kama umelala!!
😂😂😂😂😂😂

Jinsi ya kupika Wali Wa Samaki Na Mboga

VIPIMO VYA SAMAKI

Samaki wa sea bass vipande – 1 1/2 LB (Ratili)
Kitunguu saumu(thomu/galic) -1 Kijiko cha supu
pilipili mbichi iliyosagwa – 1 Kijiko cha chai
Bizari ya manjano au ya pilau – 1/2 Kijiko cha chai
Paprika ya unga au pilipili ya unga – 1 kijiko cha chai
Chumvi – Kiasi
Ndimu
Mafuta – 3 Vijiko vya supu

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Roweka samaki kwa viungo hivyo vyote kwa muda wa robo saa hivi.

Washa oven moto wa 400F.
Kisha weka samaki katika trea na choma kwa muda wa dakika 15 na weka moto wa juu dakika za mwisho ili ipate rangi nzuri.
Ikishaiva epua na itakuwa tayari kuliwa.

VIPIMO VYA MBOGA

Gwaru (green beans) – 1 LB
Kitunguu saumu(thomu/galic) – 1 kijiko cha supu
Karoti – 4-5
Chumvi – Kiasi
Bizari ya manjano – 1/2 Kijiko cha chai
Pilipili manga – 1/4 kijiko cha chai
Mafuta ya zaituni – Kiasi

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Kata kata karoti na toa sehemu ya mwisho za binzi.
Weka mafuta katika sufuria kisha kaanga karoti na gwaru
Kisha weka moto mdogo na funika ili ziwive na sio kuvurujika.
Karibu na kuiiva tia thomu kaanga kidogo,tia bizari ,chumvi na pilipili manga.
Ikisha changanyikana vizuri epua na tayari kuliwa na wali na samaki.

Baada ya kumkuta mwanamme mwingine chumbani kwake na mke wake cheki huyu anachokifanya

NAKUA(BABA) karudi kazini mwanae mdogo akamuwahi,
DOGO: Baba usiingie ndani kina jini chumbani kwenu
NAKUA: Hakuna kitu kama hicho
DOGO: Kweli baba kuna jini liko kwenye kabati lenu la nguo….

NAKUA kaingia ndani kamkuta mkewe kalala kitandani kajifunika shuka gubigubi hadi kichwani. Kaenda kwenye kabati kufungua mlango , akamkuta rafiki yake wa miaka mingi yuko uchi ndani ya kabati
NAKUA: Aise unajua we fala sana, we rafiki yangu miaka yote hiyo halafu unamtisha mwanangu eti wewe jini, hebu toka huko nenda kwenu kacheze michezo hiyo na mwanao.

Mambo 9 ya kuzingatia kuepuka ugonjwa wa saratani au Kansa

Tafiti nyingi zilizolizofanywa zinaonesha kuwa sababu kuu zinazosababisha saratani ni mtindo wa maisha usiofaa kama ulaji usiofaa na kutofanya mazoezi ya mwili.
Ili kuepukana na ugonjwa wa saratani au kupunguza uwezekano wa kupata saratani ni muhimu kuzingatia yafuatayo:

1. Kula zaidi vyakula vya mimea na nafaka zisizokobolewa

Matokeo ya tafiti yanaonesha kuwa vyakula hivi vinapunguza uwezekano wa kupata saratani, Hakikisha unakula mboga mboga za kijani na rangi nyingine kama njano,zambara. Kula nafaka zisizokobolewa kama unga wa dona, mchele wa brauni,unga wa ngano usiokobolewa,mtama na ulezi.

2. Kuwa na Uzito Uliosahihi

Uzito mkubwa uliopitiliza ni hatari na husababisha saratani. Hakikisha uwiano wa urefu na uzito wako (BMI- Body -to-Mass Index) ni sahihi ambayo ni 18 -25 kwa mtu mzima na mwenye afya nzuri unashauriwa kuwa na uwiano wa 21-23.

Punguza vyakula vinavyonenepesha mwili kama vyenye mafuta na sukari kwa wingi. Vyakula vyenye mafuta kwa wingi kama chipsi na vitumbua mfano ni hatari kwa afya yako.Vyakula vyenye sukari ni kama soda,chokoleti,keki,barafu na iskrimu na juisi bandia.

3. Fanya mazoezi ya mwili

Fanya mazozi ya mwili kila siku. Dakika 15-30 tu zinatosha kufanya mazoezi kwa afya njema. Ukikosa muda fanya anagalau mara 3 kwa wiki kwa muda usiopungua dakika 30.
Kukimbia(jogging) ni njia rahisi ya kufanya mazoezi yanayohusisha mwili mzima. Ukiweza jiunge katika timu ya mpira au klabu za mazoezi ya ndani.

Tembea kwa miguu pale inapobidi. Rafiki yangu mmoja ambaye ana gari ameweka ratiba ya kutotumia gari wakati wa mwisho wa juma. Anapanda dalala na kutembea kwa sehemu kubwa. Unaweza ukafanya hivyo pia.

4. Punguza au Acha kula Nyama nyekundu.

Ukiachia mbali saratani, nyama nyekundu imetambulika kusababisha madhara mengi na makubwa kwa binadamu.

Amua sasa kuachana nayo. Hamia katika samaki na kuku kwa kuanzia na baadae huenda ukaachana na hizo nyingine pia.
Nyama ya nguruwe maarufu kam Kitimoto ni nyama nyekundu na ni hatari kwa afya yako . Heri wale ambao hata dini zao zilikataza nyama hii ya Nguruwe kwani wameepuka hatari.

5. Epukana na Nyama za kusindikwa.

Nyama za makopo na soseji zinasababisha saratani kutokana na kemikali za kutunzia zisioze na pia huwekwa chumvi nyingi sana ambayo ni hatari kwa afya.

6. Punguza Matumizi ya Chumvi

Chumvi ya kupita kiasi inaongeza uwezekano wa kupata saratani hivyo ni hatari. Tumia chumvi kwa kiasi kidogo kwa afya njema. Binadamu anahitaji gramu 5 tu kwa siku sawa na kijoko kidogo cha chai.

Usiongeze chumvi wakati wa kula,chumvi isiyoyeyuka nia hatari zaidi.

7. Acha kula Vyakula vyenye Ukungu

Acha kula nafaka na kundekunde zilizootesha ukungu hasa kwa kutohifadhiwa vyema. Vyakula hivi vinatoa sumu ya aflatoxin

8. Usivute Sigara

Uvutaji wa sigara ni hatari na huenda ukakusababishia saratani ya koo,kinywa na mapafu. Acha kuvuta sigara ili kuepukana na ugonjwa wa saratani. Fikiria kidogo,kwanini ufe kwa sababu ya moshi tu?.

9. Punguza au Acha Pombe Kabisa

Ukiacha pombe utapunguza uwezekano wa kupata saratani na hivyo kuwa salama zaidi.
Achana na pombe, kuna madhara mengi sana ya kunywa pombe ukiachia ya saratani.

Badilisha Mtindo wa Maisha na Uwe Salama na Saratani
Namna ya kuishi kunachangia kwa kiasi kikubwa kupata saratani au la. Chagua mtindo ulio bora na salama kama ilivyoshauriwa katika mada hii juu ya kuepukana na ugonjwa wa saratani.

Afya yako ni jukumu lako mwenyewe na kupanga ni kuchagua. Panga kuishi mtindo wa maisha ulio bora na salama chagua kuishi bila saratani.

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About