Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

UJUE NA UFAHAMU MFUMO WA MOYO (CARDIOVASCULAR SYSTEM)

Mfumo huu wa moyo una kazi zifuatazo:-

👉kupampu damu Mwilini pia kusafirisha gas, taka na homoni mwilini.
👉kuongoza mfumo mzima Wa umeme mwilini.
👉mfumo Wa kujilisha wenyewe na kulisha mwili.

Lakini katika kuyafanya yote haya mambo mengi hutokea ambayo yanasababisha Moyo ushindwe kufanya kazi vizuri na mambo hayo ni kama:-
👉umri
👉mambo ya kurithi
👉aina halisi ya maisha.
👉jinsia
👉uvutaji Wa sigara.
👉kisukari
👉lishe

Pia Kwa mwili wa mwanadamu kuna kolestro (mafuta) nzuri na mbaya
Kolestro nzuri inahitajika sana mwilini na mbaya haihitajiki mwilini.
Hizi ni Bidhaa ambazo ukizitumia zitakusaidia kuimarisha vizuri afya yako ya Moyo na kukuweka katika nafasi nzuri ya kutoweza kupata madhara yoyote yatakayopelekea Moyo kushindwa kufanya kazi yake.

*Artic Sea*

*Inasaidia kupunguza kolestro mbaya Mwilini

  • Ina Omega 3 ambayo inashusha kolestro mbaya mwilini na Omega 9 ambayo ina mafuta ya mzeituni ambayo inaongeza kolestro nzuri mwilini

*Argi +*

  • ina L-Arginine inayobadilisha nitric Acid Kusaidia kutanua blood verse pia inaruhusu damu ipite vizuri pamoja na virutubisho vingine pia mishipa ikae vizuri

*Vitamin C*

  • Inasaidia kuta za mwili na nyuzi nyuzi

*ni Anti Oxidant

  • Forever Vitamin C inaongeza Oat Brand

*Garlic Thyme*

*Inasaidia mishipa kuwa madhubuti na imara pia inaipa mishipa relaxation

*Calcium*

*Ni muhimu kwa kusambaza ujumbe

  • Ni muhimu kwenye misuli ya moyo

*_Angalizo wenye magonjwa ya moyo atumie Calcium kwa ushauri wa daktari wake_*

Madhara ya kuwa mnene kupindukia

Unene(obesity), ni ugonjwa unaokua kwa kasi kipindi hiki ukiambatana na madhara makubwa kiafya hata vifo.

Unene hupimwa kwa kutumia kipimo kinachotambulika kitaalamu kama BMI (yaani uzito kwa Kilogram kugawa kwa urefu kwa mita mara mbili).

Tatizo la unene uliopindukia huweza kusababisha mhusika kutengwa katika jamii, kubaguliwa, kudhihakiwa hata kunyanyapaliwa hivyo kuleta madhara kisaikologia kwa mgonjwa.

Sababu za unene uliopindukia ni pamoja na kurithi. Mtoto aliyezaliwa na wazazi wanene, ana asilimia 80 ya kuwa mnene, aliyezaliwa na wazazi wembamba, ana asilimia 10 ya kuwa mnene.

Utamaduni na ukosefu wa nidhamu katika vyakula, pia unachangia unene uliopindukia.

Mfano; kuna ongezeko kubwa la watoto na vijana wanene kwa sasa mijini kuliko vijijini.

Madhara yaletwayo na unene uliopindukia ni mengi, lakini kwa uchache ni pamoja na kulika kwa jointi hasa za miguu, maumivu kiunoni na katika nyonga, shinikizo la damu, kisukari, pia kukosa usingizi kutokana na kubanwa kwa hewa.

Mengine ni athma, kiungulia, mafuta mengi mwilini, magonjwa ya moyo na moyo kushidwa kufanya kazi na mawe katika kibofu cha nyongo.

Wagonjwa hujikuta wakishindwa kufanyakazi vyema ili kujipatia kipato, hivyo kuwa tegemezi, kunyanyapaliwa pia huleta matatizo ya kisaikologia kama nilivyoeleza awali.

Matibabu ya ugonjwa huu ni pamoja na kubadili mfumo na aina ya maisha. Hii ni pamoja na kuwa na nidhamu katika chakula na kufanya mazoezi.

Ni wazi kwamba wazazi na watoto wanaoishi mjini, wanakabiliwa na tatizo hili, kutokana na maisha ya mfumo mgando ( kula kazi bila jasho-kulala, au kula-kusoma-kulala).

Matibabu ya muda mrefu ya tatizo hili na ambayo husaidia mgonjwa kwa kiwango kikubwa ni kufanyiwa upasuaji. Upasuaji katika tumbo ndiyo tiba mwafaka kwa unene uliopindukia.

Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ya Ng’ombe Na Nyanya

Vipimo

Mchele (Basmati) – 3 vikombe

Nyama ya ngo’mbe – 1 kg

Pilipili boga – 1 kubwa

Nyanya – 2 kubwa

Vitunguu maji – 2 vikubwa

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa – 1 kijiko cha supu

Tangawizi – 1 kijiko cha chai

Ndimu – 1

Mafuta ya kupikia – ½ kikombe

Mdalasini – ½ kijiko cha chai

Binzari nyembamba – 1 kijiko cha chai

Pilipili manga – ½ Kijiko cha chai

Hiliki – ½ Kijiko cha chai

Namna ya kutayarisha na Kupika

Roweka mchele wako katika chombo

Chukuwa nyama na ioshe vizuri na itie thomu, tangawizi, ndimu, pilipili manga na chumvi kiasi

Iweke jikoni hadi ikauke maji na kuwa imewiva huku ukiikaanga kaanga kwa hayo hayo mafuta yake hadi kuwa rangi ya hudhurungi

Katakata Vitunguu na nyanya weka pembeni

Chukua pilipili boga, thomu, tangawizi na visage katika mashine ya kusagia

Weka sufuria pembeni na utie mafuta, subiri yapate moto

Kisha tia vitunguu na vikaange hadi kuwa hudhurungi na tia nyanya

Kisha mimina mchanganyiko wako ulio usaga wa pilipili boga, thomu na tangawizi

Koroga kwa dakika kadhaa Kisha mininia nyama uliyokuwa tayari, maji kiasi na chumvi wastani na subiri maji hayo yachemke

Weka mchele humo na koroga kiasi na onja chumvi kama ipo sawa au kama ndogo unaweza kuongeza

Funika na punguza moto na uache uive taratibu

Baada ya kukauka maji kabisa basi ugeuze na subiri tena kwa dakika kama mbili na tayari kuliwa.

Maswali na Majibu kuhusu Malaika

Kwanza Mungu aliumba nini?

Kwanza Mungu aliumba Malaika (Kol 1:16)


Malaika ni viumbe gani?

Malaika ni viumbe vya Mungu vilivyo roho tu wenye akili na utashi. (Zab 91:11, Ebr 1:7, Ufu 12:7-9)


Mungu aliumba Malaika katika hali gani?

Mungu aliumba Malaika katika hali njema na heri kubwa.


Malaika wote walidumu katika hali njema na ya heri?

Siyo, Malaika wengine walikosa kwa kumkaidi Mungu, Wakatupwa Motoni.
Ndio Mashetani ambao Mkubwa wao ni Lusiferi. (Yoh 8:44, Uf 12:7-9)


Kwa nini Mungu ameumba Malaika?

Mungu ameumba Malaika ili wamtukuze, wafurahi naye Mbinguni, na wawe matarishi wake kwa wanadamu. (Tob 12:12, Lk 16:22)


Malaika wema kazi yao ni nini?

Malaika wema kazi yao ni kutuombea, kutumwa na Mungu kwetu, na wanatulinda kama Malaika wetu Walinzi. (Ebr 13:2)


Kila Mwanadamu anaye Malaika wake wa kumlinda?

Ndiyo, Kila Mwanadamu anaye Malaika wake wa kumlinda ndiye Malaika Mlinzi. (Mt. 18:10)


Malaika Walinzi wanatutendea nini?

Malaika walinzi hutupenda, hutuongoza, na kutulinda roho na mwilini (Zab 90:11)


Je Malaika wote ni sawa?

Hapana. Malaika wote sio sawa, maana kuna;
1. Malaika wakuu
2. Malaika wanaomtumikia Mungu Mbinguni yaani Makerubi na Maserafi
3. Malaika Walinzi


Malaika wakuu wako watatu ambao ni?

Malaika wakuu wako watatu: Mikaeli, Raphaeli na Gabrieli (Dn 10:13, Tobiti 12:15, Lk 1:26)


Makao ya shetani ni wapi na anatamani nini?

1. Mashetani kazi yao ni kuteswa Motoni
2. Hutaka kutudhuru roho na mwili na kutupoteza milele (1 Petro 5:8, Yoh 8:44)


Kisha kuumba Malaika Mungu aliumba nini?

Kisha kuumba Malaika Mungu aliumba Mbingu na dunia, na viumbe vingine vingi vyenye kuonekana mimea na watu. (Mwanzo 1;31)


Viumbe vyenye hiari ni vipi?

Malaika na watu ndio viumbe pekee vyenye hiari ya kuchagua wenyewe wachangie mpango wa Mungu au la.
“Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi, chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; kumpenda Bwana, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako” (Kumb 30:19-20).


Malaika na watu wanaweza kuchagua hata nini?

Malaika na watu wanaweza kuchagua hata wawe wema au wabaya milele.
“Kulikuwa na vita mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni” (Ufu 12:7-8).
Chaguo letu binadamu linafanyika siku kwa siku kwa kuchukua misimamo mizuri au mipotovu kuhusu dini na maadili.
“Mwayachunguza Maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima” (Yoh 5:39-40).


Malaika wakoje?

Malaika ni roho tupu walioumbwa na Mungu ili wamtukuze milele, wamlinde kila mtu na kumtumikia Bwana Yesu katika kutuokoa.
“Angalieni, msidharau mmojawapo wadogo hawa, kwa maana nawaambia ya kwamba malaika zao mbinguni sikuzote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni” (Math 18:10).


Je, toka mwanzo sisi watu tunaasi mpango wa Mungu peke yetu?

Hapana, toka mwanzo sisi watu tunaasi mpango wa Mungu kwa kuvutwa na mashetani, yaani malaika waliokataa moja kwa moja kumtumikia; baada ya dhambi ya asili hao wanatutumia sisi pia tuangushane na wenzetu.
Lakini Mungu aliwahi kumuambia Shetani:
“Nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako, na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino” (Mwa 3:15).
“Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke” (Gal 4:4).

Jinsi ya kumlisha n’gombe anayekamuliwa atoe maziwa mengi

Ng’ombe wa maziwa wanahitaji virutubisho zaidi ili kuweza kuzalisha maziwa kwa wingi hasa katika kipindi cha miezi 3-4 ya mwanzo baada ya kuzaa, wakati ambao uzalishaji wa maziwa unakuwa juu.

Malisho ya ng’ombe wa maziwa ni lazima yawe na uwiano sahihi wa viungo. Mifugo inahitaji chakula kitakachowapa nguvu, protini, madini, na vitamin ili kujenga miili yao, kuzalisha maziwa, na kuzaliana.

Kulisha ng’ombe wa maziwa kwa kutumia aina yoyote ya malisho haitoshi kukuhakikishia ng’ombe anakuwa na afya nzuri na kutoa maziwa ya kutosha. Kama ilivyo kwa mifugo mingine kama kuku na hata binadamu, ng’ombe anahitaji
mlo bora yaani kamili.

Vyakula vinavyohitajika kwa ng’ombe wa maziwa

Malisho ya kijani (Majani)

Huu ni mlo mkuu kwa ng’ombe wa maziwa. Mlo ni muhimu na wenye virutubisho. Lakini malisho bora ya kijani ni yale yanayoweza kumpatia ng’ombe wa maziwa virutubisho muhimu vinavyohitajika.

Malisho ya kijani yanatakiwa yawe ya kijani kibichi na machanga, hii ina maana kuwa, majani ya malisho ni lazima yakatwe na kuhifadhiwa yakiwa bado machanga na kabla ya kuchanua. Hii ina maana kuwa mimea ambayo imepoteza rangi yake halisi ya kijani inaweza tu kuwasaidia mifugo kuishi lakini haina virutubisho muhimu vya kuwapa mifugo nguvu, madini, protini na haiwezi kusaidia katika uzalishaji wa maziwa.

Malisho yenye viwango vya chini vya virutubisho yanatakiwa yaongezewe kwa chakula cha ziada chenye virutubisho vya kutosha kitakachoziba pengo la virutubisho vilivyokosekana.

Vyakula vya kutia nguvu

Kwa kawaida aina zote za majani ni chanzo kizuri cha vyakula vya kutia nguvu kwa mifugo, kama tuu tu yatalishwa yakiwa bado machanga.

Mfano wa Majani yaliyo maarufu kwa malisho ni matete, ukoka, majani ya tembo, seteria na Guatemala. Majani ya mahindi au mtama ni chakula kizuri sana kwa kuwapa nguvu mifugo.

Vyakula vingine vinaweza kutokana na aina zote za nafaka, punje za ngano, au molasesi.

Vyakula hivi vya kutia nguvu vinatakiwa vilishwe kwa kiasi kidogo.

Vyakula vya Protini

Mimea michanga ina kiasi kikubwa cha protini kuliko mimea iliyokomaa. Mahindi machanga pamoja na majani ya viazi vitamu ni mahususi kwa protini.

Mikunde ina protini nyingi zaidi kuliko nyasi. Mfano, mabaki ya majani ya maharage, njegere, desmodium na lusina. Majani yanayotokana na mimea kama lusina, calliandra au sesbania ina kiwango kikubwa cha protini pia.

Aina nyingine ya vyakula vyenye protini ni mashudu ya pamba, mashudu yaalizeti na soya.

Ng’ombe wa maziwa wasilishwe kwa kutumia aina zote za jamii ya mikunde kwa zaidi ya asilimia 30 ya uwiano wa mchanganyiko wa malisho ili kuepuka matatizo ya kiafya.

Madini

Ng’ombe wa maziwa wanahitaji madini ya ziada. Madini Ni lazima yapatikane muda wote, mfano kama jiwe la chumvi au kama chumvi ya unga ya kuweka kwenye (chakula) pumba.

Wanyama wanaokuwa, wenye mimba, na ng’ombe anaenyonyesha wanahitaji kiasi kikubwa cha madini, mfano calcium na phosphorous kwa kuwa madini mengi yanatoka kwenye maziwa.

Madini yanaweza kupatikana katika Mimea ya jamii ya mikunde na mengineyo isipokuwa nyasi. Mimea hii inatoa kiasi kikubwa cha calcium na madini mengineyo.

Chakula cha ziada (mf. Pumba)

Ng’ombe wa maziwa anapewa cha kula cha ziada mfano pumba. Pumba inahitajika kwa ng’ombe lakini kwa kiasi kidogo. Pumba aina ya Dairy meal ina kiwango kikubwa sana cha madini. Lakini ina madhara kwa mifugo endapo wanyama watalishwa kwa kiwango kikubwa.

Malisho yanayotokana na majani au nyasi kavu ni lazima yabakie kuwa chakula kikuu kwa mifugo. Haishauriwi kulisha zaidi ya kilo 6 za pumba kwa siku kwa ng’ombe mwenye kilo 450.

Ni lazima wapewe kwa kiwango kidogo sana, ambacho si zaidi ya Kilo 2 kwa mara moja na kichanganywe na majani. Kuongeza kiwango cha pumba kabla na wakati wa kunyonyesha/kukamuliwa, kisizidi kiasi cha kilo 2 kwa wiki ili tumbo la mnyama lizoee.

Ungekua wewe ni mwalimu ungemshauri nini huyu mwanafunzi?

Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.

MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?

JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.

MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?

ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.

MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.

MWAL: Na wewe James??

JAMES: mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiwe……”

Akameza mate kisha akaendelea….

“Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali.”

MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??

JENNY: Nataka kuwa mke wa James.!!

Angalia jinsi maamuzi yako ya jana na ya leo yanavyoweza kukuathiri

By Malisa GJ,
Nimeitoa kwa Comrade Markus Mpangala na kuitafsiri kwa Kiswahili (kisicho rasmi sana).
Mwaka 1998 “Google” walitaka kuiuza kampuni yao kwa “Yahoo” kwa dola Milioni 1 (sawa na Shilingi Bilioni 2) lakini Yahoo wakakataa. Yani Yahoo wakakataa kuinunua Google.

Mwaka 2002 Yahoo wakagundua kwamba walifanya makosa kuikataa Google kwahiyo wakarudi na kutaka kuinunua kwa dola Bilioni 3 (sawa na Trilioni 6). Lakini Google wakataka wapewe Dola Bilioni 5 (sawa na Trilioni 10). Yahoo wakagoma.

Mwaka 2008 kampuni ya Microsoft ikataka kuinunua Yahoo kwa Dola Bilioni 40 (sawa na Trilioni 80) lakini Yahoo wakakataa offer hiyo. Wakaona ni “ndogo”

Lakini Yahoo ikazidi kuporomoka kwenye soko na ilipofika mwaka 2016 hatimaye ikauzwa kwa dola Bilioni 4.6 (sawa na Trilioni 9) kwa kampuni ya Verizon.

#MyTake:

Unajifunza nini kupitia kisa hiki cha Yahoo? Binafsi nimejifunza mambo kadhaa:

#Mosi ni kuhusu fursa. Ukipata fursa leo itumie huwezi kujua kesho itakuaje. Yahoo wamechezea fursa nyingi sana. Kama wangekua makini huenda wao ndio wangekua wamiliki wa Google leo. Au wangeuzwa kwa bei kubwa (Trilioni 80) kwa Microsoft mwaka 2008. Lakini maringo yao yamewafanya kuja kuiishia kuuzwa bei ya “mbwa” (trilioni 9). Usifanye makosa ya Yahoo.!

#Pili ni kuhusu Thamani. Ukiwa kwenye nafasi leo usijione una thamani kuliko asiye na nafasi hiyo. Huwezi kujua kesho itakuaje. Maisha ni kupanda na kushuka. Unaweza kumnyanyasa mtu leo kwa sababu una nafasi fulani, kesho ukaenda kuomba kazi ukakuta ndio “boss” anayeajiri. Unayemuona leo yupo chini kesho aweza kuwa juu, na aliye juu akawa chini. Yahoo ilikua juu sana miaka ya 1990’s lakini kwa sasa imebaki “skrepa”. Hata sijui kama kuna watu wanaitumia siku hizi zaidi ya wale wabibi waliofungua email kipindi kile cha zama za kale za mawe.

Yahoo ilijiona juu kuliko wengine kwahiyo ikadharau kampuni zingine. Hata Google ilipotaka kuuzwa kwa Yahoo mwaka 1998, Yahoo iliona kama vile kuinunua Google ni kupoteza fedha. Leo inatamani kuwa hata “department” ya Google lakini haiwezekani. Usifanye makosa ya Yahoo.!

#Tatu nimejifunza majuto ni mjukuu. Wamiliki wa Yahoo huenda wanajuta sana kwa kupoteza fursa zote zilizokuja mbele yao. Vivyo hivyo katika maisha kuna maamuzi unaweza kufanya leo kesho ukayajutia. Mwanadada anaweza kukataa kuchumbiwa na kijana kwa sababu hana kazi, hana nyumba wala gari. Lakini baada ya miaka kadhaa anamuona yule kijana amefanikiwa kuliko alivyofikiri. Anatamani awe hata mchepuko wake lakini haiwezekani.
Usifanye makosa ya Yahoo.!

#Nne nimejifunza kuwa ukichagua sana nazi utapata koroma. Yahoo walijifanya kuchagua sana. Kila aliyekuja na “Offer” walikataa. Matokeo yake wakaja kuuzwa bei ya kuku za kienyeji kutoka Singida. Mwaka 2008 Microsoft walitaka kuinunua Yahoo kwa Dola bilioni 40 wakagoma. Lakini miaka 8 baadae (2016) wamekuja kuuzwa Dola bilioni 4.6 (yani 10% ya kile walichokua wapewe mwaka 2008).

Vivyo hivyo na binadamu ndivyo tulivyo. Ngoja nitumie mfano wa akina dada ili unielewe vzr. Kuna kina dada kuringa kwao ni fahari. Sisemi kina dada wasiringe. Ni vizuri kuringa lakini isiwe “too much”. Sasa wewe unaringa wanaume zaidi ya 10 waliokuja kukuposa, wote unawakataa unataka uolewe na nani?

Mwenye elimu umemkataa, mwenye gari umemkataa, mwenye nyumba umekataa, mwenye biashara umekataa. Umewakataa wote. Ukija kuhamaki umekuwa kama “Yahoo”… una miaka 35 na huna hata mchumba wa kusingiziwa. Unaanza kwenda kwenye mikesha ya maombi ili upate muujiza. Miaka mitatu inaisha hakuna muujiza wala mazingaombwe.

Unaamua kuweka tangazo gazetini “natafuta mchumba mwenye miaka 40 na kuendelea. Hata kama hana kazi mimi nina kazi tutasaidiana”. Miaka miwili inapita hupati. Unagundua ulikosea kama Yahoo. Hakuna mwanaumwe wa miaka 40 ambaye yupo single. Unarekebisha na kusema kuanzia miaka 25, wakati wewe una 40.

Unaamua kujilipua kama Jackline Wolper na Harmonizer. Au Zari na Diamond. Au Wema na Idris. Hujui wakati Wema anachukua taji la Miss Tanzania Idriss alikua form one?? Lakini leo wanamitana mababy?? Kwahiyo unaona miaka 25 kwa 40 sio issue. Na wewe unaamua kuingia kwenye kundi la “akina bibi wanaolea wajukuu zao”

Lakini hupati “husband material”. Unawapata “maplay boy” wa mjini. Wanakuja wanakuta ni bibi wa miaka 40 wanakuuliza “umemaliza eddah” wakidhani ni mjane umefiwa na mume unataka kuolewa tena. Kumbe hujawahi kutolewa mahari hata mara moja. Wanakuambia ngoja tufikirie, halafu haoooo wanapotea kama Microsoft ilivyopotea mbele ya uso wa Yahoo. Hawarudi ng’o.

Baadae baba yako anaamua kuondoa tangazo la “Jihadhari mbwa mkali” lililokuwa getini anaweka tangazo jipya “tunauza barafu” Na hapo ndipo utakapogundua kuwa vifusi vya mchanga wa mgodini vinaweza kutumika kupiga “plasta” nyumba yenu.

My dear Life is too short to be complicated. Live your life. Enjoy every moment of your life. Tumia fursa zote muhimu unazozipata. Usiringe. Usimdharau mtu. Heshimu kila mtu. Mche Mungu. Usifanye makosa ya “Yahoo”.!

Mapishi ya Supu ya makongoro

Mahitaji

Makongoro (miguu ya ng’ombe) kiasi
Limao 1 kubwa
Kitunguu swaum
Tangawizi
Chumvi
Pilipili

Matayarisho

Safisha makongoro kisha yatie kwenye pressure cooker. Kisha tia kitunguu swaum, tangawizi, chumvi,limao na maji kiasi. Baada ya hapo yachemshe mpake yaive na yawe malaini na pia ubakize supu kiasi inaweza kuchukua kama dk 45 au saa 1 hivi. Baada ya hapo yaipue na upakue supu yako kwenye bakuli katia pilipili kiasi kisha itakuwa tayari kwa kuliwa.

Note:
Ukiwa unanunua makongoro hakikisha unachukuwa yale yasiyokuwa na manyoya na pia
hakikisha usiyachemshe kupitiliza kwani yakiwa malaini sana utashindwa kuyaenjoy.

Kukataliwa ni mtaji

Hakuna mtu duniani ambaye hajawahi kukutana na hali ya kukataliwa. Yaani kukataliwa katika hali yoyote ile. Waweza kuwa umekataliwa katika kupata ajira, umekataliwa katika mahusiano, umekataliwa kupata nafasi ya kusoma, umekataliwa kupata mtaji wa biashara, umekataliwa tuu..umekataliwa.

—-= Unaweza kuwa umekataliwa katika ajira moja kumbe kuna ajira nyingine tena yenye maslahi zaidi inakusubiri.

—-= Umekataliwa na mteja mmoja na kumbe kuna wateja wengi wanakusubiri.

—-= Umekataliwa katika chuo kimoja mwaka huu kumbe mwakani kuna nafasi yako inakusubiri.

——= Umekataliwa na mpenzi ulioamini kabisa atakua wako wa maisha kumbe aliye wako haswaa anakusubiri ufike.

Watu wengi kinachowarudisha nyuma, “ni kuacha kuboresha fikra zao ili kuwa watatuzi wa matatizo_(problem solvers)_ ila wameamua kuwa walalamikaji tu kila siku, ili tuendelee ni lazima tujikite katika kutafuta majibu ya matatizo yanayotuzunguka.” Yaani, mara zote jiulize ” *sasa nifanye nini? Na sio kwa nini mimi?”*

Mtaalamu mmoja aliwahi kusema ” _Life is 10% of what happens to you and 90% of how you respond to it_”. Yaani _yale yanayokutokea maishani yanachangia asilimia kumi tu kuboresha au kuharibu maisha yako na asilimia 90 ya maisha yako ni jinsi wewe unavyoyachukulia maisha hayo_. Kwa nini ukate tamaa baada ya kukataliwa. Yape maisha yako maana sana thamani ya juu kabisa ili kukataliwa kwako iwe ni kukupa nguvu ya kufanya vizuri zaidi. Tambua utakacho na unachoweza kukifanya. Jifunze vizuri na ubobee ili kuuhakikishia ulimwengu kwamba wewe sio mzigo ila ni sehemu ya wenye majibu ya matatizo yanayotuzunguka.

Kukataliwa, ni mtaji. Kila jambo lina wakati wake.

Faida za ulaji wa Peasi

Peasi ni tunda ambalo limekuwa halithaminiwi licha ya kuwa na faida lukuki katika mwili wa binadamu. Tunda hilo ambalo kwa umbo linafanana na tufaa (apple), lina faida nyingi kwa binadamu iwapo atalitumia mara kwa mara.

Tunda hili limekuwa adimu kutokana na kutostawi katika maeneo mengi hivyo watu wengi hawalifahamu na hata walionapo hawalitilii maanani kama ilivyo kwa matunda mengine kama vile ndizi, embe, papai na mengine.
Tunda hili lina faida mbalimbali katika mwili wa binadamu kama vile kukausha jasho la kwapa kwa wale wenye kutokwa na jasho jingi endapo litaliwa mara kwa mara.
Pia tunda hilo ambalo hulimwa sana katika Mkoa wa Tanga husaidia kupunguza mwasho wa koo na juisi yake ni nzuri skwa kuua mba, hutibu kibofu cha mkojo na uti wa mgongo.
Vilevile tunda hili lina Vitamin A na B ambazo husaidia kuepukana na upofu, pia husaidia kuongeza hamu ya kula na kuboresha mfumo wa fahamu.
Wakati mwingine tunda la peasi husafisha mishipa ya moyo na kutibu mafua ya ndege na husaidia mmeng’enyo wa chakula ufanyike vizuri.
Tunda la Peasi husaidia kuongeza kinga za mwili, kuupa mwili nguvu, hupunguza shinikizo la damu, kuzuia mafuta kuganda mwilini (cholestrol), huzuia magonjwa ya saratani, kiungulia pamoja kupunguza homa.
Pia tunda hili likitumika baada ya chakula cha usiku au baada ya kupata kifungua kinywa huweza kuleta matokeo mazuri.

Hizi ndizo sababu kwa nini ule Tende kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Kitaalamu chakula unachokula leo ndio kinaamua hali ya afya yako kwa siku za usoni. Na ni muhimu sana kuzingatia ulaji bora wa chakula na si kula ilimradi umekula. Wataalamu wa lishe wanatuambia kuwa ulaji unaofaa hutokana na kula chakula mchanganyiko kulingana na wakati.

Lakini hata ulaji huo, unatakiwa kutazamwa ni ulaji gani unaofaa kulingana na mchanganyiko kulingana na mahitaji ya mwili. Na pia, wanasema mlo kamili unaofaa ni ule ulio na virutubisho vyote muhimu kwa ajili ya lishe na afya bora.

Leo katika makala haya, yataangazia ulaji wa tende, na kwa kuzingatia kuwa huu ni Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, tende ndiyo tunda pekee linaloliwa kwa wingi, pengine kuliko tunda lingine lolote.

Inaelezwa kuwa kisayansi, tunda hilo limethibitika kusheheni madini na vitamini nyingi kiasi cha kulifanya liwe na faida nyingi kiafya.

Ulaji wa tende kwa waliofunga

Mtaalamu wa Lishe, Juliana Majaliwa anasema mtu aliyekwenye mfungo, mara zote huwa kiwango chake cha sukari mwilini hupungua na kutakiwa airejeshe tena kwa kula vyakaula vitakavyosaidia kufanya mara tu anapotakiwa kufuturu.

Majaliwa anasema aina ya kwanza ya sukari itumikayo mwilini ni ya glukosi. Lakini sukari inayoshuka kwa watu ambao hawajala wala kula kwa muda mrefu, inaweza kuwasababishia kupatwa na kizunguzungu au kulegea.

Hivyo, anasema ulaji wa tende mara mtu anapotakiwa kufuturu, humfanya aliyefunga asijihisi kuchoka sana na huwa na nuru zaidi ya macho. Pia tende zitamsaidia kuimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji wa chakula tumboni, hivyo ataondokana na matatizo ya ukosefu wa choo au matatizo ya kupata choo kigumu kinachosababisha maumivu wakati wa kujisaidia.

Hivyo, mfungaji akila tende zitamsaidia kupata virutubisho vya ‘amino acids’ ambavyo ni muhimu mwilini, pia mwili wake utapata aina mbalimbali za madini na vitamin za kutosha, ambazo zinapatikana kwenye tunda hili maarufu ambalo lina kiasi kidogo cha mafuta yasiyo na lehemu. Majaliwa anasema sukari inapoliwa kwa njia ya chakula au kinywaji, mara zote viwango vya glukosi ya mwili hujisawazisha yenyewe na kumfanya mlaji aliyefunga asijihisi.

Ingawaje tende mara nyingi si chakula kinachopendelewa sana na watu wenye njaa, lakini ndicho chakula kisicho na mafuta na ni chanzo madhubuti cha sukari.

Wataalamu wa lishe wanasema mfungaji akila tende, atajipatia kiasi cha kutosha cha protini na vitamin B1, B2, B3, B5, A1, na C, virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ustawi wa afya ya mwili kwa ujumla.

Faida zaidi za tende

Wale walio kwenye mfungo, muda wa kufuturu ukiwadia, wanashauriwa pia kuchanganya tende na maziwa halisi kisha wale. Na kama wanajisikia uchovu, badala ya kunywa vinywaji baridi vinavyodaiwa kuongeza nguvu, wale tende hata punje tatu tu zinatosha.

Wataalamu wa lishe wanawashauri kuanza kufungua kwa kula tende ili kuurejeshea mwili nguvu iliyopotea kwa siku nzima.

Kwa sababu tende pia ina madini aina ya potasium na kiasi kidogo cha chumvi.

Madini haya husaidia uimarishaji wa mishipa ya fahamu. Watafiti wamegundua kwamba ulaji kiasi wa madini ya potasium husaidia kumwepusha mtu na maradhi ya kiharusi. Pia tende husaidia kupunguza lehemu mwilini.

Wenye matatizo ya kukauka damu

Wataalamu wanasema kwa mfungaji mwenye tatizo la kukauka damu mwilini (anemia), anaweza kupata ahueni kwa kula tende kwa wingi ambayo ina kiwango cha kutosha cha madini ya chuma ambayo huhitajika katika utengenezaji wa damu mwilini. Wakati vitu vingine vitamu vinadaiwa kuwa huozesha meno, lakini wataalamu wa tiba lishe wanasema utamu wa tende huzuia uozaji wa meno.

Faida zingine za tende

Kwa mtu aliye na tatizo sugu la kukosa choo, anatakiwa kuloweka tende za kutosha kwenye maji kiasi cha lita moja kwa muda ili kupata juisi nzito, muathirika anywe na atapata choo laini.

Kwa matatizo ya ukosefu wa nguvu za kiume, mchanganyiko maalum wa tende, maziwa, asali na unga wa hiriki vinaweza kuondoa tatizo hilo. Chukua kiasi cha kiganja kimoja cha tende, loweka kwenye maziwa ya mbuzi kiasi cha lita moja, ziache zilowane kisha zisage kwenye maziwa hadi zichangayike, weka vijiko vitatu au vinne vikubwavya asali pamoja na nusu kijiko cha chai cha hiriki, kisha kunywa mchangayiko huo kila siku hadi utakapoona mabadiliko ya kuridhisha.

Tende ni dawa

Tunaelezwa kuwa tende ni dawa ya unene na kwa wale wenye matatizo ya wembamba wa kupindukia na wanataka kuongeza uzito, ulaji wa tende kila siku unaweza kuwasaidia. Lakini hii ina maana wale wanaohitaji kupunguza uzito, ulaji wa tende kwa wingi hauwezi kuwafaa.

Mtaalamu wa tiba ya mimea, Japhet Lyatuu, anasema tende hutibu pia saratani ya tumbo na husaidia pia kuondoa hali ya ulevi kwa wale wanaokunywa pombe.

Anasema tende tiba ni na haina madhara yoyote kwa sababu ni dawa ya asili na inafanyakazi vizuri kuliko dawa za ‘kizungu’.

Laytuu anasema tunda hilo husaidia pia kuimarisha nuru ya macho na tatizo la kutokuona usiku. Anasema faida za tende ni nyingi na mtu anaweza kuila kwa namna mbalimbali.

Sababu za kumuacha mke kama umemchoka

Ukimchoka mkeo, waweza kumtaftia sababu za kumuacha kama hizi

_
1. Missed calls 16? Umeua betri la simu yangu. Kwa hiyo hata mimi unaweza kuniua… It’s Over!!!
_
2. Hata hunieshimu. Mi naongea na wewe lakini we upo bize unavuta pumzi? It’s over!
_
3. Nimekupigia umepokea simu hapohapo. Huna subira. It’s over!!
_

4. Nilikwambia huwa napenda chakula cha moto lakini hujanipashia ice cream. Hunijali. It’s over!
_
5. Nimekupa mayai mawili, moja uchemshe jingine ukaange. We umekaanga ambalo ulitakiwa kuchemsha na umechemsha ulilotakiwa kukaanga. Huniheshimu, It’s over!
_
6. Nimekuita DARLING na wewe ukaniita HONEY. Yani kwa maana nyingine unamuita mama yangu NYUKI. Huheshimu wazazi wangu, fungasha kilicho chako. its over.

😄😂😄😂😄😂😄😂😄

Madhara ya kuvaa miwani ya Urembo maarufu kama miwani ya Jua

Miwani za urembo maarufu kama miwani za jua zimetajwa kuwa na madhara kwa watumiaji wake kutokana na watu kutofahamu saizi za namba ambazo wanapaswa kuzivaa kabla ya kununua.

Akifafanua kwenye kipindi cha Supamix kinachorushwa East Africa Redio, Daktari Ningwa wa Upasuaji wa macho kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk.Neema Daniel Kanyaro amesema watu wengi amekuwa wakivaa miwani pasipokjua kwamba zinaweza kuwasababishia matatizo ya kuona.

Dk. Kanyaro amesema kwamba watu wamekuwa wakivaa miwani za jua kama urembo pasipo kwenda kupima kujua ni aina gani ya miwani wanazotakiwa kuzitumia lakini pia bila kujua kama miwani hizo zina namba ambazo kila mtu ana namba kutokana na uono wake.

“Miwani ni dawa lakini usivae bila kupima kwani inaweza kukusababishia matatizo ikiwemo uoni hafifu. Unaweza kukuta unavaa miweani nyeusi lakini kumbe siyo namba yako. Kama hujijui unaweza kuta ukitazama unaona giza kumbe umeshaua macho kwa urembo” amesema.

Akizungumzia kuhsu presha ya macho Dk. Kanyaro amesema kwamba ugonjwa huo hauna dalili za moja kwa moja bali ni lazima kupima na huathiri watu wa rika zote.

Mapishi ya Biriyani Ya Kuku

Vipimo

Mrowanishe kuku na viungo hivi kwa muda mdogo tu

Kuku (Mkate kate Vipande) – 4 LB

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi – 2 Vijiko vya supu

Chumvi – kiasi

Pilipili nyekundu ya unga – 1 Kijiko cha supu

Bizari ya manjano (Haldi au Tumeric) – 1 Kijiko cha chai

Bizari ya pilau ya powder (Jeera) – 1 Kijiko cha chai

Gilgilani powder (Dania) – 1 Kijiko cha chai

Ndimu – 1 Kijiko cha supu

Mchele na vitu vya Masala:

Mchele (Basmati mzuri) (rowanisha) – 7 cups

Mafuta ya kupikia – kiasi

Vitunguu Vilivyokatwa – 8

Nyanya iliyokatwa katwa – 3

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi – 1 Kijiko cha supu

Garam Masala -1 Kijiko cha supu

Hiliki powder – ½ Kijiko cha chai

Tomatoe paste – 1 Kijiko cha supu

Pilipili mbichi zipasue katikati – 4

Chumvi – kiasi

Mtindi – 4 Vijiko vya supu

Kotmiri iliokatwa (Chopped) – ½ Kikombe

Mafuta ya kunyunyuzia katika wali – 3 Vijiko vya supu

Zaafarani au rangi ya biriani – kiasi

Namna Ya Kutaarisha Na Kupika

Weka kuku aliyerowanishwa na viungo vyake katika Foil tray au chombo chocote utakachomwagia wali humo humo na kupikia biriani, kisha mchome (Bake) mpaka awive na awe mkavu kiasi.

Wakati kuku anapikika, kaanga vitunguu katika karai au sufuria mpaka viwe brown na epua nusu yake weka kando.

Punguza mafuta yabakie kiasi tu, ongeza Thomu na tangawizi, na viungo vyote vya hapo juu isipokuwa Mtindi na kotmiri, endelea kukaanga hadi tomatoe zilainike.

Ongeza chumvi, malizia mwisho kwa kutia mtindi, kotmiri na vile vitunguu ulivyoweka kando. Masala yako tayari.

Mwagia masala juu ya kuku uliyekwishmpika changanya vizuri.

Chemsha Mchele uwive nusu, chuja na mwagia juu ya masala.

Nyunyiza mafuta kidogo juu ya mchele na zaafarani au rangi ya biriani.

Bake katika moto wa 350 – 400 kwa muda wa 15 – 20 minutes. Biriyani imekuwa tayari kuliwa.

Mtindi wa kutolea Biriyani:

Mtindi – 1 kikombe

Pilipili mbichi – 1 ndogo

Kitunguu saumu(/galic) thomu – chembe mbili

Nanaa – kiasi

Chumvi – chembe tu

Weka kwenye Blender na uchanganye, kisha mimina katika bakuli

Mapishi ya Chicken Curry

Leo wapendwa nitaenda kuzungumzia mapishi ya mchuzi wa kuku (chicken curry).

Mahitaji

Kuku mzima
Nyanya kubwa 3
Karoti mbili
Pilipili hoho
Kotmiri
Tangawizi
Kitunguu maji
Kitunguu saumu kidogo
Ndimu
Mafuta ya kupikia
Chumvi (pilipili ukipenda)

Matayarisho

1. Menya vitunguu saumu na tangawizi na uvitwange pamoja.
2. Katakata kuku vipande vidogo kisha ukamulie ndimu na kupaka mchanganyiko wa tangawizi na vitunguu saumu (kiasi tu).
3. Katakata vitunguu maji na pilipili hoho uweke pembeni.
4. Grind (Kwangua) kwenye grater nyanya na karoti pia uweke pembeni.
5.Katakata kotmiri vipande vidogo uweke pembeni.
6. Andaa kikaango na jiko.

Mapishi

1. Bandika kikaango jikoni na mafuta kiasi, yakishachemka weka vitunguu maji na kaanga hadi vimelainika na kuiva (hakikisha haviungui).
2. Weka pilipili hoho na karoti na endelea kukoroga hadi vyote viive na kulainika, Kisha weka chumvi.
3. Sasa weka vipande vya nyama koroga na funikia kwa dakika 3, kisha weka nyanya zako ulizo grind na koroga ili zichanganyike vizuri, vikishachanganyika weka kotmiri na pilipili kama utapenda. Acha vichemke kwa dakika 5. Hakikisha moto sio mkali sana.
4. Angalia kama nyama zimeiva vizuri kisha epua mchuzi wako.
5. Pakua kwenye bakuli na katakata kotmiri uweke kwa juu.
Unaweza kula kwa ugali, wali, ndizi rost au chipsi.

Maswali na Majibu kuhusu Sala

Sala ni nini?

Sala ni kuinua mioyo yetu kwa Mungu na kuongea nae. Kuongea maana yake ni kusema na Kusikiliza. Sala sio kuongea tuu, sala ni kuongea na kusikiliza. Mungu anatualika tuongee nae kwa kusema na kusikiliza. Kwenye Biblia tunasoma Hivi;
“Niite, nami nitakujibu na kukuambia mambo makubwa yaliyofichika ambayo hujapata kuyajua”.(Yeremia 33:3)
Vile tunavyokuwa na juhudi ya kusali kwa kusema mbele ya Mungu ndivyo hivyo hivyo tunatakiwa tuwe na juhudi ya kumsikiliza Mungu kile anachotuambia.
Tunaweza kumsikiliza Mungu ndani kabisa ya Mioyo yetu, mara nyingine kwa kupitia dhamira zetu, kupitia watu wengine na kupitia neno lake (Biblia). Tuombe neema ya kutambua sauti yake anaposema nasi ili tuweze kumsikiliza na kutengeneza mahusiano mazuri kati yetu na yeye.
Mungu ni Baba yetu, anatupenda sana na yupo tayari kutusikiliza wakati wote ndio maana Mungu anatualika kwa kutuambia;
“Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu”. (Isaya 1:18)
Tudumu katika sala daima kwa sababu njia ya sala ndipo tunaweza kusema yale tunayotaka mbele ya Mungu na kusikia yale anayotaka Mungu.


Kwa nini tunasali?

Tunasali ili kudumisha mahusiano yetu na Mungu na ili kutimiza wajibu wetu Mbele ya Mungu. Sababu kuu za kusali ni;
  1. Kumwabudu Mungu,
  2. Kumshukuru Mungu,
  3. Kuomba neema na baraka kwa ajili yetu na wenzetu,
  4. Kuomba msamaha,
  5. Kumsifu na kumtukuza Mungu

1. Kumwabudu Mungu

Tunasali ili kumwabudu Mungu, yaani kumpa heshima ya mwisho juu ya kila kitu. Kuonyesha kuwa ni mkuu na wa kipekee kuliko mtu au kitu chochote.

2. Kumshukuru Mungu

Tunasali ili kumshukuru Mungu kwa yale yote aliyokwisha kuyatenda, anayoyatenda na yale atakayoyatenda. Tunamshukuru Mungu kwa yote kwa kuwa yote anayoyafanya anayafanya kwa Mapenzi/ Matakwa yake Matakatifu. Nia ya Mungu ni njema daima ndio maana tunapoona ameruhusu mambo ambayo kwa akili zetu tunayaona ni magumu na sio mema tunapaswa kushukuru kwa sababu ameyafanya kwa makusudi mema.
Biblia inatuambia hivi;
16 Furahini siku zote; 17ombeni bila kukoma; 18shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. (1 Wathesalonike 5:16-18)
Tunatakiwa kumshukuru Mungu kwa Kila jambo na kumshukuru huku ni kwa njia ya sala.

3. Kuomba neema na baraka kwa ajili yetu na wenzetu

Tunasali kwa kuomaba neema na baraka kwa ajili yetu sisi wenyewe na kwa ajili ya wenzetu. Tunamuomba Mungu baraka na Mkono wake katika yale tunayoyafanya na kwa yale wanayoyafanya wengine.
Maombi yetu ili ykubalike mbele ya Mungu ni lazima yawe katika mapenzi yake na yawe na nia njema. Tunafundishwa hivi katika biblia;
3Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu. (Yakobo 4:3)
Tunatakiwa tusali kwa kuomba mema na kwa nia njema ili tuweze kupata yale tunayoyaomba kwa Mungu.

4. Kuomba Msamaha

Tunasali ili kuomba msamaha mbele ya Mungu kwa yote mabaya tuliyoyafanya. Mungu ni mwaminifu hasa kwenye kutusamehe na kutuondolea dhambi zetu.
9Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. (1 Yohana 1:9)
Vilevile Tunatakiwa kusali katika mapungufu yetu na kuwa na matumaini.
9Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. (2 Wakorinto 12:9)

6. Kumsifu na kumtukuza Mungu

Tunasali ili kusifu na kumtukuza Mungu. Mungu anapenda kusifiwa na kutukuzwa. Kwa njia ya sifa tunapokea neema na baraka hata ambazo hatujaziomba.
1Mfanyieni BWANA shangwe, dunia yote;
2Mtumikieni BWANA kwa furaha;
Njoni mbele zake kwa kuimba;
3 Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu;
Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake;
Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
4Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru;
Nyuani mwake kwa kusifu;
Mshukuruni, lihimidini jina lake;
5 Kwa kuwa BWANA ndiye mwema;
Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake vizazi na vizazi. (Zaburi 100:1-4)


Nani anapaswa kusali?

Watu wote wanapaswa kusali, wema na wabaya. Sala ndiyo njia pekee ya kumuunganisha Mwanadamu na Mungu. Tunapaswa kusali Katika hali yoyote. Tunapokuwa katika hali ya neema tunapaswa kusali vivyo hivyo tunapokuwa katika hali ya dhambi tunapaswa kusali.
Tunapokuwa katika hali ya neema tunapaswa kusali. Tunasali ili tuweze kudumu katika hali ya neema. Hatupaswi kuacha kusali kama tunajiona hali yetu ya kiroho ipo vizuri. Hatupaswi kuacha kusali kama tumepata neema ya kusimama vyema mbele ya Mungu.
Tunapokuwa katika hali ya dhambi tunapaswa kusali. Tunasali ili tuweze kurudi katika hali ya neema. Hatupaswi kuacha kusali kama tunajiona tupo katika hali ya dhambi. Kwa njia ya sala ndipo tutakapoweza kutoka katika hali ya dhambi.
Mungu yupo tayari kusikiliza ukiwa katika hali ya neema au kama ukiwa katika hali ya dhambi. Ndio maana tunapaswa kumwelekea Mungu katika hali yoyote tulio nayo.
14Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. 15Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba. (1 Yohane 5:15)
Tena Mungu anasubiri tumuombe ili furaha yetu itimilike.
24Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. (Yohane 16:24)
Hata kama tuna dhambi Mungu yupo tayari kutupokea na kutusikiliza.
“Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu”. (Isaya 1:18)
Mungu yupo tayari kutusikiliza hata tunapokuwa wadhambi kwa kuwa haziweki dhambi zetu na makosa yetu mbele yetu. Huruma yake ni kubwa kushinda dhambi zetu.
12 Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,
Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.
13 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake,
Ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao. (Zaburi 103:12-13)
Mungu anatuwazia mema daima ndio maana tunapaswa kusali kwake
11Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. 12Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. 13Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. (Yeremia 29:11-13)


Yatupasa kusali lini?

Yatupasa kusali kila siku bila kukata tamaa (Lk 18:1) Sala ndiyo njia pekee ya kutuunganisha na Mungu.
Tunatakiwa tusali daima Kama Yesu alivyotuhimiza kwa mfano huu;
1 Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.
2 Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu.
3 Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu.
4 Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu,
5 lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima.
6 Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu.
7 Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?
8 Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani? 
(Lk 18:1-8)
Kwa hiyo basi, Tusali daima kila siku, kila saa na katika hali yoyote. Tusichoke kusali hata kama maombi Yetu hayajajibiwa. Mungu ni mwenye Hekima na anajua lini hasa akujibu kile unachokiomba kwa manufaa yako wewe. Usipopewa Leo kile ukiombacho unaweza kukipata kwa wakati ufaao tena bila ya Kukiomba.

Sala ni Hazina

Sala ni hazina. Kusali ni kujiwekea hazina. Sala unayosali leo inaweza kukunufaisha wakati usioutarajia.

Maana ya Sala kwa Mkristo Mkatoliki

Maana ya sala kwa Mristu Mkatoliki sio kuomba tuu. Sala kwa Mkatoliki ni zaidi ya kuomba. Kwa Mkatoliki sala inamaanisha kufanya haya;
  1. Tunasali kushukuru,
  2. Tunasali kuomba,
  3. Tunasali kusifu na Kutukuza,
  4. Tunasali kumshirikisha Mungu Furaha zetu na huzuni zetu,
  5. Tunasali kuomba Toba na Msamaha,
  6. Tunasali kumshirikisha Mungu Juhudi zetu na Mipango yetu,
  7. Tunasali kumshirikisha Mungu changamoto zetu.
Tuna kila sababu ya Kusali kila Siku na Kila saa. Maisha yetu yote yanatakiwa yawe Maisha ya Sala. Usifikiri kwamba Wakati wote unaposali lazima utamke maneno Mengi sana ili uwe umesali, Sala haipimwi kwa Maneno. Sala inapimwa kwa nia yake na Kujiweka wazi mbele ya Mungu.
Kila Usalipo Jijengee Tabia ya kunuia, kuwa wazi na kusali kwa ukweli wa Moyo wako. Hata kama ni sentesi Moja fupi Kabisa itamke kwa Upendo na Imani. Kwa Mfano, kuna wakati inatosha kabisa kusema Ee Mungu wangu ninakushukuru kwa hili, hii inaweza kuwa sala Yenye nguvu Kama imetamkwa kwa Imani, Shukrani na Mapendo ya Kweli. Maneno machache yanayotamkwa kwa Imani na Mapendo yanaweza kuzidi Mkesha wa Kusali Usiku Mzima huku unasinzia.
Pamoja na kwamba sala fupi ni nzuri na inafaa sana, kuna haja pia ya kujitengea Muda wa Kutosha Kusali na Kutafakari Huku tukiungana na Mungu. Kila siku tunanye mambo yote mengine lakini tusisahau kuwa Tunahitaji kuwa na Muda wa Kusali.
Tusali daima, Kila wakati na Maisha yetu yawe ni Maisha ya Sala.
Mungu Akubariki sana, Azijibu sala zako na Akujalie Neema ya Kuwa Mtu wa Sala.


Yatupasa kusali namna gani?

Yatupasa kusali kwa Unyenyekevu, Ibada, Matumaini na kwa Saburi. Yesu alitufundisha kuhusu kusali kwa kutumia mfano huu;
9 Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote.
10 Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.
11 Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.
12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote.
13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
14 Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa. 
Luka 18:9-14
Tunatakiwa tusali kwa nia njema na kwa kufuata Mapenzi ya Mungu ili sala zetu zipate kibali mbele za Mungu. Tunapoomba kwa nia mbaya ya tamaa na majivuno hatuwezi kupata kile tukiombacho.
3Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu. Yakobo 4:3
Mungu anajibu sala zetu kulingana na nia ya kile tunachokiomba. Watu wote waliofanikiwa Katika sala zao walifanikiwa kwa sababu ya nia ya kile walichokiomba.
Sala sio kutamka manano tuu, sala ni kutamka maneno kwa kunuia. Tena tusalipo yatupasa kujua kuwa tunaongea na Mungu na sio tuu kwamba tunatamka maneno. Tusisahau nia kuu ya kusali ambayo ni mawasiliano Yetu na Mungu.
Tunaposali Tunapaswa Kukumbuka na kuzingatia haya;
  1. Nia na Imani (Kuamini na Kuwa na Uhakika na Unachokifanya)
  2. Unyenyekevu wa Kweli
  3. Ibada na Uchaji
  4. Upendo na Uwazi (Honest)
  5. Matumaini na Saburi (Subira)
Kila unaposali jiulize unasali kwa kwa sababu gani? Kila ubapoomba, jiulize unamuomba Mungu ili nini? Sababu yako ndio kibali cha sala yako.
Mungu Akubariki kwa Kukujalia Imani, Unyenyekevu, Ibada, Uwazi na Matumaini Usalipo. Uwe na Amani.


Sala zipo za namna ngapi?

Sala zipo za namna tatu,
1. Sala ya sauti
2. Sala ya fikara
3. Sala ya taamuli


Sala ya Taamuli ni nini?

Sala ya taamuli ni sala ya kumtazama tuu Mungu kwa upendo mkubwa moyoni


Sala ya sauti ni nini?

Sala ya sauti ni sala asaliyo mtu au kundi kwa kutamka maneno


Sala ya fikara ni nini?

Sala ya fikra ni sala asaliyo mtu peke yake au akiwa na wengine kimya kimya akimuwaza Mungu


Sala ya kanisa ni nini?

Sala ya kanisa ni sala maalumu wasaliyo Maklero, Watawa, na Walei kwa ajili ya Kanisa zima


Ni nyakati gani zafaa kwa sala?

Nyakati zote zafaa kwa sala hasa:
1. Asubuhi na jioni
2. Kabla na baada ya kula
3. Kila Dominika
4. Sikukuu za amri
5. Kabla na baada ya kazi
6. Katika kishawishi


Yesu alitufundisha sala gani?

Yesu alitufundisha sala ya Baba Yetu (Mt. 6:9-13)


Je, yatupasa kuombea wengine?

Ndiyo. Yatupasa kuwaombea watu wote hasa wenye shida, wakosefu na hata maadui zetu.


Vyanzo vya sala za Kikristo

Vyanzo vya sala za kikristo ni;
1. Neno la Mungu
2. Litrujia ya kanisa
3. Fadhila za Kimungu
4. Matukio ya kila siku


Je, ni sahihi kusali sala kwa kurudia rudia mfano Novena?

Ndiyo, Hii ni kwa sababu sala nyingi za kurudia ni za Ahadi na zinasaliwa ili kutimiza ahadi ile. Mfano Novena husaliwa kwa siku 7 au 9 kwa nia ya kupata kile kilichoahidiwa au kinachodhamiriwa. Mungu alishawahi kuwaagiza Waisraeli wafanye Ibada maalumu kwa kurudiarudia mfano wakati walipoangusha kuta za Yeriko walifanya Ibada maalumu kwa siku 7 (Saba).
“Waisraeli walipopita waliagizwa na Mungu kuzunguka Mji wa Yeriko 2Kisha BWANA akamwambia Yoshua,“Tazama, nimeitia Yeriko mikononi mwako, pamoja na mfalme wake na watu wake wa vita. 3Zunguka mji mara moja pamoja na watu wako wote wa vita. Fanya hivi kwa siku sita. 4Uwe na makuhani saba wakibeba mabaragumu ya pembe za kondoo waume mbele ya sanduku. Siku ya saba, mzunguke mji mara saba, nao makuhani wakipiga baragumu hizo. 5Utakaposikia makuhani wamepaliza sauti kubwa ya baragumu, watu wote wapige kelele kwa sauti kuu, kisha ukuta wa mji utaanguka na watu watakwea, kila mtu aingie ndani moja kwa moja kutokea pale alipo.’’ (Yoshua 6:2-5).
Naamani aliambiwa na Nabii Elisha aoge mara saba kwenye mto Yordani ili apone.
14Hivyo akashuka na kujizamisha ndani ya mto Yordani mara saba, kama vile huyo mtu wa Mungu alivyokuwa amemwambia, nayo nyama ya mwili wake ikapona na kutakasika kama ya mwili wa mvulana mdogo. (2 Wafalme 5:14)
Yesu alisali sala ya kurdia rudia kama tunavyosoma,
39Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akaomba, akisema, “Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniepuke, lakini si kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo Wewe.’’ 40Kisha akarudi kwa wanafunzi wake na kuwakuta wamelala. Akamwuliza Petro, “Je, hamkuweza kukesha pamoja nami kwa saa moja? 41‘‘Kesheni na mwombe, msije mkaanguka majaribuni. Hakika roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.’’ 42Akaenda tena mara ya pili na kuomba, “Baba yangu, kama ikiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, mapenzi yako yafanyike.’’ 43Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. 44Hivyo akawaacha akaenda zake tena mara ya tatu na kuomba akisema maneno yale yale. (Mathayo 26:39-44)

Je ni makosa kurudia sala maneno yale yale kwa Mfano Rozari?

Hapana sio Makosa. Kwa Mfano Biblia inatuambia kuwa Malaika humtukuza Mungu kwa maneno ya kurudia rudia.
“8Kila mmoja wa hawa viumbe wenye uhai wanne, alikuwa na mabawa sita na kujawa na macho pande zote, hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawakuacha kusema: ‘‘Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.’’ (Ufunuo 4:8).
Vile vile tunasoma katika kitabu cha Isaya kuwa malaika walikua wakimsifu na kumtukuza Mungu kwa sala/ maneno ya kurudiarudia. “Katika mwaka ule mfalme Uzia alipokufa, nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu na kilichotukuzwa sana, nalo pindo la joho lake likajaza hekalu. 2Juu yake walikuwepo maserafi, kila mmoja alikuwa na mabawa sita: Kwa mabawa mawili walifunika nyuso zao, kwa menngine mawili walifunika miguu yao na kwa mawili walikuwa wakiruka. 3Nao walikuwa wakiitana kila mmoja na mwenzake: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni BWANA Mwenye Nguvu, Dunia yote imejaa utukufu wake.”
Kama Malaika humtukuza Mungu kwa maneno ya kurudia rudia kwa nini sisi tukifanya hivyo tuwe tunakosea? Na sisi tunaweza kumuomba, kumsifu na kumtukuza Mungu kwa sala au maneno ya kurudiarudia kama walivyofanya malaika. Kwa hiyo sala za kurudia rudia sio makosa.
Tukiangalia Zaburi ya 136 inarudia maneno “kwa maana fadhili zake zadumu milele” mara 26 yaani kwenye mistari yake yote. (Zaburi 136:1-26)
Yesu pia allimuomba Mungu Baba kwa kurudia maneno yale yale kama tunavyosoma,
39Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akaomba, akisema, “Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniepuke, lakini si kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo Wewe.’’ 40Kisha akarudi kwa wanafunzi wake na kuwakuta wamelala. Akamwuliza Petro, “Je, hamkuweza kukesha pamoja nami kwa saa moja? 41‘‘Kesheni na mwombe, msije mkaanguka majaribuni. Hakika roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.’’ 42Akaenda tena mara ya pili na kuomba, “Baba yangu, kama ikiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, mapenzi yako yafanyike.’’ 43Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. 44Hivyo akawaacha akaenda zake tena mara ya tatu na kuomba akisema maneno yale yale. (Mathayo 26:39-44)

Sala kwa Mkatoliki ni nini hasa? Tunaposema sala tunamaanisha nini hasa?

Sala ni kuongea na Mungu. Sala kwa Mkatoliki inajumuisha maombi, tafakari, ibada, taamuli, shukrani na sifa. Maana ya sala kwa Mkristo Mkatoliki sio kuomba tuu kama wanavyotafsiri watu wasio wakatoliki. Wengi wa wasio Wakatoliki wanaposema Sala wanamaanisha Maombi.
Kwa hiyo kwa Mkatoliki, Sala ni zaidi ya Maombi. Ndiyo maana kwa mkatoliki kuna sala za namna mbalimbali kama vile za Tafakari, za Maombi za Sifa na za kushukuru. Mfano sala ya Atukuzwe Baba sio maombi bali ni sala ya kumtukuza Mungu kwa maana hiyo sio Maombi, ndiyo maana husaliwa baada ya sala au matukio fulani kama ishara ya kumtukuza Mungu na kutambua ukuu wa Mungu

Yesu alifundisha tusali vipi?

Kisha Yesu akawapa wanafunzi Wake mfano ili kuwaonyesha kuwa yawapasa kuomba pasipo kukata tamaa.
2Akawaambia, “Katika mji mmoja alikuwapo hakimu ambaye hakumwogopa Mungu wala kumjali mtu. 3Katika mji huo alikuwako mjane mmoja ambaye alikuwa akija kwake mara kwa mara akimwomba, ‘Tafadhali nipatie haki kati yangu na adui yangu.’ Wa Mjane Asiyekata Tamaa 4“Kwa muda mrefu yule hakimu alikataa. Lakini hatimaye akasema moyoni mwake, ‘Japokuwa simwogopi Mungu wala simjali mwanadamu, 5lakini kwa kuwa huyu mjane ananisumbuasumbua, nitahakikisha amepata haki yake ili asiendelee kunichosha kwa kunijia mara kwa mara!’ ” 6Bwana akasema, “Sikilizeni asemavyo huyu hakimu dhalimu. 7Je, Mungu hatawatendea haki wateule Wake wanaomlilia mchana na usiku? Je, atakawia kuwasaidia? 8Ninawaambia, atawapatia haki upesi. Lakini je, Mwana wa Adamu atakapokuja ataikuta imani duniani?” (Luka 18:1-8)


Roho Mtakatifu ana nafasi gani katika sala?

Roho Mtakatifu ndiye Mlezi wa ndani wa sala ya Kikristo


Ni ipi sala kubwa ya Kanisa?

Sala kubwa ya Kanisa ni Misa Takatifu


Ni ipi sala bora kwa Bikira Maria? Kwa nini Tunasali kwa Bikira Maria?

Sala bora kwa Bikira Maria ni Rozari Takatifu

Kwa nini watu wengi wanaomba kwa Bikira Maria?

Watu wengi wanaomba kupitia Bikira Maria kwa sababu wanashuhudia sala zao kujibiwa kirahisi zaidi wanaposali kupitia Bikira Maria kwani Bikira Maria anatuombea kile tunacho mwomba. Bikira Maria anasimama Kama mwombezi wetu mbele ya Mungu hasa pale tunaposhindwa kusali Inavyotakiwa.

Bikira Maria anatuombea kwa jina na mamlaka ya nani?

Bikira Maria anatuombea kwa jina la Yesu Kristu na kwa mamlaka ya Yesu Kristu aliye mwanaye. Hakuna Sala yoyote inayotolewa kwa Bikira Maria moja kwa moja kwani Sala zote kwa Bikira Maria zinatolewa kwa kusema utuombee ikimaanisha kuwa utupelekee Maombi yetu kwa Mungu. Bikira Maria hatusaidii sisi moja kwa moja bali anatusaidia kwa kutuombea msaada kutoka kwa Mungu.

Je ni halali au ni sawa kwa Bikira Maria kutuombea kwa Jina la Yesu? Na Je tunajuaje kuwa Bikira Maria anaushirika na Yesu?

Ni halali na nisawa kabisa Bikira Maria kutuombea. Tunajua kuwa Bikira Maria anaushirika na Yesu kwa kuwa Yesu mwenyewe alituambia kuwa “asiyepingana na sisi yupo upande wetu”. Biblia iintuambia…
“Yohane akadakia na kusema “Umemwona Mtu mmoja akifukuza pepo kwa kutumia jina lako, nasi tukajaribu kumkataza kwa kuwa si mmoja wetu.” Lakini Yesu akawaambia, “Msimkataze kwani asiyepingana nanyi yupo upande wenu” (Luka 9:49-50).
Kwa hiyo Bikira Maria anapolitumia jina la Yesu bila kupingana na sisi wala Yesu ni ishara tosha kuwa ni mshirika wa Mungu (Yesu)

Je ni kweli kwamba Bikira Maria ni Malkia wa Kipepo?

Sio kweli kwamba Bikira Maria ni Malkia wa Kipepo/Kishetani
Sababu hizi zifuatazo zinadhihirisha kuwa Bikira Maria sio Malkia wa kipepo;
1) Kuomba kwa jina la Yesu: Angekua ni Malkia wa Kipepo asingeomba kwa Jina la Yesu. Kama ilivyoelezwa hapo juu. Biblia iintuambia linapotamkwa Jina la Yesu mapepo hukimbia. Sasa iweje yeye alitumie Jina hilo kutuombea Kama yeye ni pepo? (Luka 10:17)
2) Hafundishi uovu/dhambi: Mbali na kuomba kwa jina la Yesu, vilevile Yesu alituambia tuzichunguze roho na tutazitambua roho hizo kwa matendo yake. Kwa lengo hili tukichunguza kuhusu Bikira Maria tutaona kuwa Bikira Maria ni Mtakatifu aliye upande wa Mungu kwa sababu Mara zote alipowatokea watu amekuwa akifundisha na kuelekeza watu kuishi maisha ya utakatifu na kumfuata Mungu kweli kwa kutii amri zake na kufuata mafundisho ya mwanae ambayo ni yakuelekea katika utakatifu. Hakuna hata Mara moja mafundisho ya Bikira Maria yalihusishwa na vitendo viovu au vya kuvunja Amri za Mungu.
3) Mafundisho yake yanaendana na Neno la Mungu (Biblia): Bikira Maria hajawaji hata mara moja kufundisha na kuelekeza vitu vilivyo nje ya Mafundisho ya neno la Mungu (Biblia). Hakuna hata Mara moja mafundisho ya Bikira Maria yalikinzana na Mafundisho ya Neno la Mungu.
4) Anahubiri Wema, Unyenyekevu, Upole na Utii: mambo ambayo ni alama ya kudhihirisha Utakatifu.
5) Anasisitiza Upendo kwa Binadamu wenzetu na kwa Mungu: Anahubiri Upendo hasa kwa Maadui zetu na wale wanaoipinga Imani ya Kikristu na wanaomkataa Yesu Kristu. Anasisitiza mara zote Tumpende Mungu na kumtii.
6) Anahubiri Amani: Anahubiri Injili ya Amani na Mara zote anasisitiza tuombe amani ambapo amani ndio Ishara ya Utakatifu.
7) Hajitukuzi mbele ya Mungu bali anajinyenyekesha: Hajawahi kufundisha kwamba tumtukuze yeye au tumuheshimu yeye. Mara zote anahubiri tumheshimu Mungu pekee na kumtukuza Mungu. Amekua akijishusha kwa unyenyekevu huku akituelekeza tuige mfano wake wa unyenyekevu wa kumuelekea Mungu aliye Baba wa huruma na upendo.
8) Anaongeza imani kwa Mungu: Kwa sala na Ibada za Bikira Maria waumini wanapata kuongezewa Imani na Uchaji wao kwa Mungu. Wengi wanabadili maisha yao ya dhambi na kuelekea Maisha mema ya utakatifu ya Kumtumikia Mungu.
9) Sala Ibada yake inachanganyika na Ibada nyingine za Kikristu: Hakuna mgongano/ushindani wa Ibada kwa Bikira Maria na Ibada nyingine za Kikristu. Kama angekua ni pepo kamwe Ibada yake isingechanganyika na Ibada Takatifu.
10) Ibada kwa Bikira Maria Imedumu: Haikufifia wala kupotea bali ilizidi kuendelea vizazi hata vizazi. Hii inadhihirisha kwamba kuna Neema ya Mungu.
Kwa sababu hizi unaweza ukaona kwamba Bikira Maria anaushirika na Mungu na ni Mtakatifu.


Ni zipi sala Muhimu kwa Mkristo?

Sala muhimu kwa Mkristo ni;
1. Misa Takatifu
2. Baraka ya Sakramenti Kuu
3. Litania Takatifu
4. Njia ya Msalaba
5. Rozari Takatifu
6.Novena


Ipi ni shule ya kwanza ya sala?

Familia ni shule ya kwanza ya sala


Mahali gani panafaa kwa sala?

Mtu anaweza kusali mahali popote lakini Kanisani ndipo mahali Rasmi pa sala


Mwenye kusali anakutana na majaribu gani?

Anakutana na Majaribu haya;
1. Mtawanyiko wa Mawazo
2.Ukavu wa moyo
3. Uvivu na Uregevu
Ndiyo maana kwa Wakatoliki sala nyingi zimeandikwa ili kutuongoza hasa tunapokuwa majaribuni katika sala.


Neno “Amina” katika sala lina maana gani?

Neno “Amina” katika sala lina maanisha “Na iwe Hivyo” (Hesabu 5:22)


“Aleluya” katika sala, hasa zaburi ina maana gani?

“Aleluya” katika sala, hasa zaburi ina maanisha “Msifuni Mungu”


Ishara ya msalaba ni nini?

Ishara ya Msalaba ni tendo la mtu kugusa panda la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na kutamka “Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”


Kwa kugusa paji la uso tuna maana gani?

Kwa kugusa paji la uso tuna maana ya kukubali kwa akili


Kwa kugusa kifua tuna maana gani?

Kwa kugusa kifua maana yake ni kuupokea na kuukubali msalaba moyoni.


Kwa kugusa mabega tuna maana gani?

Kwa kugusa mabega maana yake ni kuwa tayari kuubeba msalaba kwa nguvu zetu zote


Kwa nini tunafanya Ishara ya Msalaba?

Tunafanya Ishara ya Msalaba kwa nia ya kumkiri Mungu mmoja katika Nafsi Tatu. Pia msalaba ni Ishara ya Ukombozi wetu


Ishara ndogo ya Msalaba juu ya panda la uso, mdomo, na kifua kabla ya Injili ina maana gani?

Maana yake ni kama Ahadi kuwa, Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu kwa akili yangu, Nitalitangaza kishujaa kwa Midomo yangu, Nitalipenda na kulishika kwa Moyo wangu wote.


Sala zina faida gani? Kwa nini watu tunasali?

Sala zina faida hizi;
1. Zinaleta neema nyingi
2. Zinatuimarisha ili kushinda vishawishi na dhambi
3. Zinatuunganisha na Mungu
4. Zinatudumisha katika kutenda mema


Mazinguo ndiyo nini?

Mazinguo ni sala za kupungia mashetani ili kuepusha watu na balaa au madhara, hasa kama wamepagawa nao.
“Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu” (Mk 5:8).
“Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena!” (Mk 9:25).
Yesu ameliachia Kanisa mamlaka yake juu yao.
“Aliwaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu” (Mk 6:7).
“Paulo alisikitika, akageuka akamwambia yule pepo, ‘Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu’. Akamtoka saa ileile” (Mdo 16:18).


Ikiwa sala ni maongezi ya Mungu na mtu, kwanza tufanye nini?

Ikiwa sala ni maongezi ya Mungu na mtu, kwanza tumsikilize kwa makini na kutafakari alichosema ili tukifanyie kazi. Tukisema peke yetu si sala, kwa kuwa ukisema upande mmoja tu si maongezi.
“Nena, Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikia” (1Sam 3:10).
“Nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku” (Zab 63:6).
“Sheria yako naipenda mno ajabu, ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa” (Zab 119:97).
“Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu” (Yer 15:16).


Kielelezo cha sala yetu ni nani?

Kielelezo cha sala yetu ni Yesu Kristo.
“Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, ‘Bwana, tufundishe sisi kusali” (Lk 11:1).
Yeye kama binadamu alichota humo uaminifu kwa wito wake wa pekee.
“Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe” (Yoh 17:1).
“Aba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe” (Mk 14:36).


Kama binadamu Yesu alijifunza kusali kwa nani?

Kama binadamu Yesu alijifunza kusali kwa Mama yake na kwa mapokeo yote ya Israeli, yaliyojitokeza hasa katika Zaburi.
“Wazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka. Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuu” (Lk 2:41-42).
“Saa tisa Yesu alipaza sauti yake kwa nguvu, ‘Eloi, Eloi, lama sabakthani?’” (Mk 15:34).
“Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu” (Lk 23:46).


Je, sala ya Yesu inatokana na utu wake tu?

Hapana, sala ya Yesu haitokani na utu wake tu, bali katika huo Mwana wa milele ndiye anayemuelekezea Baba yake sala kamili ya kitoto.
“Saa ileile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, ‘Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili, umewafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza” (Lk 10:21).
“Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote” (Yoh 11:41- 42).
“Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo” (Lk 23:34).


Yesu alisali vipi?

Yesu alisali kila mahali na kila wakati, akidumisha ushirika wa upendo kati yake na Baba katika Roho Mtakatifu.
“Saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu” (Yoh 4:23).
Pamoja na kushiriki kiaminifu ibada za taifa lake, mara nyingi alijitafutia mahali pa faragha.
“Aliongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani” (Lk 4:1).
“Alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba” (Lk 5:16).
“Aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu” (Lk 6:12).
Ndiyo sababu ametuambia,
“Wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini” (Math 6:6).
Tusipojua kuongea na Baba moyo kwa moyo, tutawezaje kuongea naye kati ya umati?


Yesu ametufundisha kusali vipi?

Yesu ametufundisha kusali akitueleza misimamo ambayo tuwe nayo.
“Upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako… Waombeeni wanaowaudhi… Msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu” (Math 5:24,44; 6:5).
“Mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipigapiga kifua akisema, ‘Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi’. Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki” (Lk 18:13-14).
Hasa ametutia Roho Mtakatifu atuongoze kama alivyomfanyia yeye.


Je, Yesu ametufundisha maneno ya sala pia?

Ndiyo, Yesu ametufundisha maneno ya sala ya ‘Baba Yetu’, kamili kuliko zote. Maombi yake saba yanategemea utangulizi ambao tunamuendea Mungu kwa ujasiri na furaha kama watoto wake, ndugu kati yetu.
Maombi matatu ya kwanza yanalenga atukuzwe, atawale, apate ushirikiano wetu. Maombi manne ya mwisho yanalenga tupate chakula cha roho na cha mwili, msamaha wa dhambi, ushindi katika vishawishi, usalama dhidi ya yule Mwovu.
“Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. Basi ninyi salini hivi…” (Math 6:8-9).


Je, sala inategemea maneno?

Hapana, sala haitegemei maneno mengi mazuri, bali kujijenga
“juu ya imani… na kuomba katika Roho Mtakatifu” (Yud 20).
“Mkiwa katika kusali, msipayukepayuke, kama watu wa mataifa; maana hao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi” (Math 6:7).
Hii haituzuii tusirudie maneno yetu kwa dhati zaidi na zaidi.
Yesu “alikwenda, akaomba mara ya tatu, akisema maneno yaleyale” (Math 26:44).
Tunaweza kusali kimoyomoyo pia.
“Hana alikuwa akinena moyoni mwake, midomo yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe… ‘Nimeimimina roho yangu mbele za Bwana’” (1Sam 1:13,15).
“Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee Bwana” (Zab 19:14).


Je, sala yetu inasikilizwa daima?

Ndiyo, sala yetu inasikilizwa daima kwa kuwa imeunganika kwa imani na ile ya Yesu, njia pekee ya kumuendea Baba.
“Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata, furaha yenu iwe timilifu” (Yoh 16:24).
Lakini Baba, kwa ujuzi na upendo usio na mipaka, anaweza akatupatia mambo tofauti na yale tuliyomuomba.
“Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, ‘Nipe maji ninywe’, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai” (Yoh 4:10).
“Ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je, Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?” (Lk 11:13).
Imani yetu ikubali kwamba aliyotupatia ni bora zaidi.


Je, sala inaweza kumuendea Yesu?

Ndiyo, sala inaweza kumuendea Yesu, Bwana wetu na kaka yetu, aliye hai mbinguni, kama ilivyomuendea na kusikilizwa alipokuwa duniani.
Mhalifu alisema,
“‘Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako’. Yesu akamwambia, ‘Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi” (Lk 23:42-43).
Stefano aliomba,
“‘Bwana Yesu, pokea roho yangu’. Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, ‘Bwana, usiwahesabie dhambi hii’” (Mdo 7:59-60).
“Roho na Bibi arusi wasema, ‘Njoo!’. Naye asikiaye na aseme, ‘Njoo!’… Na uje, Bwana Yesu!” (Ufu 22:17,20).


Roho Mtakatifu anatusaidiaje kusali?

Roho Mtakatifu anatusaidia tusali kama Yesu, akiwa mlezi wa ndani na kutumia vipaji vyake saba.
“Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, ‘Aba!’ yaani, ‘Baba!’” (Gal 4:6).
“Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo; lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa… huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu” (Rom 8:26-27).
Ndiyo sababu Kanisa linatuhimiza tumtamani na kumualika kila mara, ‘Njoo, Roho Mtakatifu!’ yaani kumuomba Baba kwa njia ya Mwana amtume zaidi na zaidi ndani mwetu.


Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha hadi wapi?

Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha hadi muungano wa dhati na Mungu.
“Yeye awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake, katika utu wa ndani. Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu” (Ef 3:16-19).
“Huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote” (Yoh 16:13).
Safari hiyo inategemea sana sala isiyoishia katika maneno bali inalenga kupenya mafumbo kwa imani na upendo.


Je, sala inaweza kuwaendea Mama na marafiki wa Yesu (Watakatifu)?

Ndiyo, sala inaweza kuwaendea Mama na marafiki wa Yesu, walioungana naye kuwa mwili mmoja, wasiweze kutenganishwa na chochote.
“Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine chochote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Rom 8:38-39).
“Kwangu mimi kuishi na Kristo, na kufa ni faida… Ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo” (Fil 1:21,23)
.
Kwa kuwa hao wako na Kristo mbinguni, wanatuombea mfululizo pamoja naye.
“Niliona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, ‘Ee Mwenyezi, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini…’” (Ufu 6:9-10).
Tunawaomba wazidi kutuombea kwa Mungu, kama tunavyowaomba wenzetu waliopo duniani.
“Mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; pia na kwa ajili yangu mimi” (Ef 6:18-19).


Je, Yatupasa kumwomba Roho Mtakatifu?

Ndiyo, kwani twataka kwake maonyo na msaada. Tusipokuwa na neema yake hatuwezi kutenda jambo jema la kufaa kutuokoa. (Yoh 16:13)
Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About