SMS ya kumtumia mpenzi wako kumtakia mahangaiko mema ya kazi
Ukipata tutakula na wala usijali mpenzi wangu.
Ukikosa tutalala na hiyo itabaki siri yanguuuuuuuu.nakupenda mpz
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Ukipata tutakula na wala usijali mpenzi wangu.
Ukikosa tutalala na hiyo itabaki siri yanguuuuuuuu.nakupenda mpz
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Mbolea ya kunyunyiza ni nzuri kwani inasaidia kuupa mmea virutubisho moja kwa moja kupitia kwenye majani au shina ambapo ndipo chakula kinahitajika.
Faida za mbolea ya maji ni pamoja na kuongezeka kwa kiwango cha mavuno, uwezo wa mimea kukabiliana na wadudu pamoja na magonjwa, kuvumilia ukame, na kuongeza ubora wa mazao.
Mbolea ya maji hutengenezwa kwa kuchukua kiroba kilichojazwa samadi, aina mbalimbali ya mimea yenye virutubisho na inayoaminika kuwa dawa ya mimea. Kiroba hicho kinafungwa kwenye kijiti, na kutumbukiza kwa kuningโinia kwenye pipa lililojazwa maji.
Kiroba hicho ni lazima kichukue kati ya kilo 30-50 za samadi pamoja na aina nyingine za mimea kwa maji lita 200 (tazama mchoro). Unaweza kushika upande mmoja wa mti na kunyanyua na kushusha kila baada ya siku tano ili kuchanganya na kuharakisha kutolewa kwa virutubisho zaidi.
Kwa kawaida mchanganyiko huo unakuwa na harufu kali sana maana Nitrojeni nyingi inayopatikana hugeuka kuwa Amonia. Ni vizuri kufunika pipa ili kuzuia kuyeyuka kwa nitrojeni. Harufu ikishaisha, ujue mbolea yako ipo tayari kwa matumizi.
Ongeza maji na utingishe vizuri kabla ya kutumia. Nyunyizia mimea yako kila wiki mpaka utakapoona mabadiliko.
Mbolea hii hutengezwa kwa kuchukua majani mabichi na kuyakatakata na kisha kuyachanganya na maji kidogo.
Baada ya kuchanganya na maji unaacha kwa siku tatu au nne ambapo utatikisa mchanganyiko wako kila siku.
Baadae utatikisa na kuchanganya na maji na kunyunyiza shambani.
Vilevile Unaweza kutumia mbolea ya majani ambayo itakuwa kama dawa ya kuulia wadudu, kwa kutumia aina ya mimea kama vile mivule, mibangi mwitu, majani ya minyanya, mwarobaini, mashona nguo, pamoja na vitunguu saumu. Aina hii ya mimea inasaidia sana katika kuzuia magonjwa, wadudu na kutoa virutubisho muhimu kwa mimea vinavyosaidia mkulima kupata mazao bora bila gharama ya ziada ya kununua virutubisho.
Ili upate matokeo mazuri wakati wa kunyunyiza mbolea ya maji unatakiwa kufuata vigezo vifuatavyo:
โข Inashauriwa kutumia mbolea iliyochanganywa vizuri ili kuepukana na kuunguza mimea.
โข Acha maji utakayotumia kuchanganyia mbolea yako nje katika pipa lililowazi usiku kucha, hii inasaidia kutoa madini hatarishi, na kufanya mchanganyiko wenye faida kwa mimea.
โข Unatakiwa kutingisha vizuri mbolea yako ya maji kabla ya kunyunyiza. Chembechembe ndogo ambazo hazikuyeyuka zinaweza kuziba mdomo wa bomba la kunyunyizia.
โข Matokeo mazuri yanaweza kupatikana endapo mbolea imechanganywa vizuri na kunyunyiziwa wakati hakuna upepo.
โข Unatakiwa kunyunyizia mbolea wakati wa asubuhi au jioni wakati hakuna joto na upepo ukiwa umepungua.
Angalizo
Kabla ya kunyunyiza dawa au mbolea uliyoitengeneza mwenyewe shambani nyunyiza kwenye eneo dogo au mimea michache kwanza ili uone kama inaunguza au haiunguzi. Kumbuka kuwa mchanganyiko mwingine ukiwa cream au ukikolea sana unaweza kuchoma. Kwa hiyo kuepuka hili nyunyiza mahali padogo kwanza.
Kutifua udongo ni jambo la muhimu sana ili kuufanya udongo kuwa bora.
Umuhimu wa kutifua udongo ni kama ifuatavyo
1. Hulainisha udongo ili kuruhusu mizizi ya mimea kupenya kwa urahisi.
2. Kutifua kunaboresha uwezekano wa kupenya kwa nitrogen na oxygen kutoka kwenye hewa.
3. Kunawawezesha viumbe hai waliopo kwenye udongo kufanya kazi zao ipasavyo.
4. Kunasaidia Kuandaa sehemu ya kuwekea mbegu.
5. Kutifua kunauongeza uwezekano wa maji kupenya kwenye udongo na kupunguza uyeyukaji wa maji.
6. Kuchanganya mabaki ya mimea na samadi kwenye udongo
Tumeamriwa tutunze uhai wetu na wa watu wengine tangu mwanzo hadi mwisho. (Mwa 4:10-11)
Kwa sababu uhai wa watu wote umetoka kwa Mungu
Haki ya binadamu iliyo ya msingi kupita zote ni uhai wake ambao ni lazima uheshimiwe na kulindwa tangu siku ya kutungwa mimba
Anayetemda dhambi dhidi ya amri ya tano ya Mungu ni yule;-
1. Anayemuua mtu au anayejiua mwenyewe
2. Anayemdhuru mwingine kwa namna yoyote ile
3. Anayeua Mimba na kuharibu nguvu za uzazi
4. Anayesaidia kuua, kumdhuru mtu au anayesaidia kutoa/kuharibu mimba
5. Anayeharibu mazingira yaliyomuhimu kwa uhai
6. Anayetetea au kuendeleza mifumo ya ya dhuluma, uhasama na vita.
Kila mtu ni mrithi wake yeye mwenyewe. Mafanikio yako ya baadae ni urithi wako ulioutengeneza hapo awali. Utajiri wako wa sasa unatokana na uliyoyawekeza miaka ya nyuma na utajiri wako ujao ni yale unayoyawekeza sasa.
Unga vikombe 2 ยผ
Siagi 250g
Sukari kukaribia kikombe ยฝ (au takriban vijiko 10 vya kulia)
Baking powder ยฝ kijiko cha chai
Ute wa yai 1
Vanilla 1 kijiko cha chai
Sukari Ya Kunyunyizia na rangi mbali mbali.
Kagawa sukari katika vibakuli utie rangi mbali mbali uweke kando.
Changanya siagi na sukari katika mashine ya kusagia keki upige mpaka ilainike iwe nyororo.
Tia ute wa yai vanilla uhanganye vizuri.
Tia unga na baking powder kidogo kidogo uchanganye upate donge.
Sukuma donge ukate kwa kibati cha shepu ya kopa.
Pakaza siagi katika treya ya kupikia kwenye oveni upange biskuti
Nyunyizia sukari za rangi rangi kisha pika katika oven moto mdogo wa baina 180 โ 190 deg F kwa takriban robo saa.
Epua zikiwa tayari.
Jamaa mmoja dereva wa bajaji alianguka, sasa bajaji ikawa imem’bana akawa anafurukuta bila mafanikio Cha ajabu watu wakawa wanampita bila kumsaidia, Kumbe Nyuma ya Bajaji yake alikua Kaandika “NIACHENI KAMA NILIVYO, HII NDIO STYLE YANGU”ย ๐๐๐ย Mpaka sasa nimemwacha bado yuko hapoย *Sipendagi Ujinga mimi* ๐ถ๐ฝ๐ถ๐ฝ๐ถ๐ฝ๐ถ๐ฝ๐ถ๐ฝ
Kila jambo lina Mkono wa Mungu juu yake hata kama limefanyika bila kupangwa au kukusudiwa. Mbele ya Mungu hakuna kitu kinachofanyika kwa Ajali au bahati mbaya.
Kuchagua vyakula sahihi kwa mlo wako inaweza kuwa changamoto na tungependa kuamini kwamba kupungua uzito ni jambo tu la kula kalori chache na kufanya mazoezi zaidi. Hata hivyo, si mara zote zoezi hili linakuwa rahisi. Kama ni lengo lako kupunguza uzito, kuchagua chakula gani ule ni muhimu kama kuchagua kiasi gani cha chakula ule.
Ukweli ni kwamba , baadhi ya vyakula vinauwezo wakusaidia kupunguza uzito kutokana na tabia zake za kuunguza mafuta mwilini.
Mafuta ya nazi yanapanda chati kwa haraka kabisa na kufanya kuwa mojawapo ya vyakula bora kabisa kwa afya ya binadamu.
Mojawapo ya vitu muhimu kabisa katika mafuta haya ni uwezo wake wa kupunguza uzito wa mwili.
Mafuta ya nazi ni yana kemikali yenye mlolongo wa kati wa mafuta (โMedium Fatty Chain Acidsโ) ambayo humengโenywa tofauti na yale yenye mlolongo mrefu wa mafuta (โLong Fatty Chain Acidsโ)
Kemikali zenye mlolongo mrefu wa mafuta(โLong Fatty Chain Acidsโ) hupatikana kwa wingi katika vyakula vingi vya mafuta kaa vile nyama, chips n.k.
Kemikali zenye mlolongo wa kati wa mafuta hutumiwa na mwili kwa ajili ya nishati badala ya kuhifadhiwa kama mafuta katika mwili.
Hii ndio sababu mafuta ya nazi ni moja ya vyakula vyenye uwezo wa kuchoma mafuta mwilini na kusaidia kupungua uzito.
Siki ya Apple ina kiwango kikubwa cha kemikali za amino (amino acids) ,kemikali za kumengโenya chakula na madini na vitamini. Utafiti unaonyesha kwamba kutumia Siki ya Apple kabla ya kula vyakula vya wanga inasaidia kupunguza kupanda kwa insulin hivyo kusaidia kutopata hamu ya kula mara kwa mara.
Utafiti unaonyesha kuwa kiasi cha vitamini C mwilini kinahusiana na uzito wa mwili.
Watu wenye viwango vya kutosha wa vitamini C wana uwezo wa uwezo wa kuvunja asilimia 30 zaidi ya mafuta wakati wa mwili unapofanya shughuli za nguvu kama kazi za nyumbani,shambani na mazoezi kama kutembea, kuliko wale walio na kiwango cha chini cha vitamini C.
Kama una dhamira ya kupungua uzito, basi fikiria kuanza siku yako kwa kunywa glasi moja ya maji yenye ndimu au limao au anza kutumia siki(vinegar) kwenye kachumbali au saladi unapokula chakula.
Balungi yana kiasi kidogo cha kalori , kiwango cha juu cha tindikali za kumengโenya chakula na inaweza kukufanya usijisikie njaa kwa muda mrefu.
Watafiti wamegundua kwamba kula nusu ya balungi kabla ya mlo ni inachangia sana kupoteza uzito . Pia kula nusu tu ya balungi kabla ya mlo inaweza kusababisha kupungua kwa kiasi cha glucose-insulin katika muda wa masaa mawili tu.
Kama wewe unahitaji kupungua uzito zingatia kula vyakula vinavyo kata mafuta na ongeza vyakula hivi vilivyotajwa katika mlo wako.
Kwa mafanikio ya muda mrefu , kazania kula vyakula kamili (vyakula visivyo kobolewa au kusindikwa) na kufanya mazoezi ya mara kwa mara.
Wanawake nilianza kuwachukia tokea shule ya msingi.
Ni pale mwanamke wangu aliponiacha na kwenda kwa jamaa mwenye kichongeo kipya โฆinauma sanaaโฆ
WANAWAKE SIO WATU WA MCHEZO MCHEZO ASEEE Bac tuu
Fangasi ya ukeni husababishwa na fangasi aina ya Candida albicans. Ugonjwa huu huitwa vaginal candidiasis kwa kiingereza na ni kati ya magonjwa ambayo husumbua wanawake mara kwa mara.
Fangasi ya ukeni huambukizwa kwa njia ya;
Vyoo vichafu.
Kuchangia nguo za ndani na taulo.
Uwezekano wa kupata fangasi ya uke au fangasi ya uke kujirudia rudia unaongezeka pale ambapo mwanamke ana;
Kisukari.
Ujauzito.
Anatumia antibiotics kwa muda mrefu
Ukimwi.
Joto, unyevu mwingi na nguo za kubana huchangia pia kutokea kwa fangasi ukeni. Ugonjwa huu haumbukizwi kwa njia ya ngono.
Fangasi ya ukeni inaweza kuleta dalili zifuatazo kwa wagonjwa wenye maambukizi;
Kuwashwa sehemu za siri hasa wenye uke na mashavu ya uke.
Kutokwa na maji maji meupe mfano wa maziwa kutoka kwenye uke ambayo hayana harufu mbaya.
Maumivu wakati wa kukojoa kwa baadhi ya wagonjwa. Mara chache hali hii hutokea, ikisabaishwa nakuchubuka wakati wa kujiwasha.
Matibabu ya fangasi ya uke hutumia dawa za kuua fangasi (antifungals). Mara nyingi dawa za kuingiza kwenye uke (vaginal pessaries) hutumika kwa muda wa siku 3 mpaka 6. Wakati mwingine dawa za kunywa zinaweza kutumika kutibu fangasi hii.
Muone daktari kwa ajili ya uchunguzi, dawa na dozi sahihi.Cotrimazole na ketoconazole ni kati ya dawa zinazotumika mara kwa mara.
Pamoja na matibabu kuna hatari ya maambukizi ya fangasi hawa kujirudia, hivyo ni muhimu kupata tiba hospitali na kurudi unapoona inajirudia. Vitu vingine muhimu kuzingatia ni;
Usafi wa nguo za ndani; kuvaa safi iliyofuliwa kila siku na kuanikwa juani (au kupigwa pasi).
Vaa nguo za ndani zilizokauka vizuri. Epuka zenye unyevunyevu au mbichi.
Vaa nguo za ndani zilizotengezwa kwa pamba (hupunguza joto na hivyo hatari ya fangasi kuzaliana)
Usafi wa sehemu za siri na kujikausha viruzi baada ya kuoga.
Usafi wa choo ni muhimu sana.
Kitendawili…
Nikizidi nalaumiwa, nikipungua nadharauliwa
JIBU: Chumvi
Upendo wa kweli hauambatani na chuki. Huwezi kusema una Upendo wakati kuna watu wengine unawapenda na wengine unawachukia. Ni sawa na kusema kitambaa ni cheupe lakini kina madoa doa, maana yake sio cheupe.
“Cannibalism,”
Kudonoana kwa kuku ni tatizo linalo wa sumbua wengi, ni moja ya athari ya lishe duni. Ni kisema lishe duni na maanisha chakula wanacho kula kukosa vurutubisho muhimu vya madini au kuku kutokula chakula cha kutosha.
1.Kuku kukaa wengi kwenye eneo dogo
2. Tabia yao
3.Ubaguzi wa rangi
Hii Mara nyingi hutokea kwa kuku weusi ukiwachanganya na kuku mweupe au rangi ingine tofauti, kuku weusi Mara nyingi huwa ni wakali sana Kwahiyo ukiona kuku bandani kwako kadonolewa chunguza kwa makini chanzo ninini! Kama ni ubaguzi wa rangi unaweza watenga hao weusi.
4. Kuku kutokupata chakula cha kutosha
5.Upungufu wa madini ( protini)
6. Kukosa kitu walicho kizoea au kuboreka
Kwa mfano kuku ukiwazoesha kuwa changanyia Damu kwenye chakula , siku utakapo punguza kipimo au kuacha kabisa kuwa changanyia damu ambayo umewazoesha kuwa changanyia lazima watadonoana.
Kuku ukiwa zoesha kuwa fungia mchicha hasa wale kuanzia mwezi mmoja hadi wa miezi 4 siku utakapo acha kuwafungia mchicha inaweza sababisha wakadonoana.
Kuku hupenda kuparuaparua na kuzunguka zunguka. Wakikosa nafasi na vitu vya kudonoa donoa huanza kudonoana wenyewe kwa wenyewe.
7. Mwanga mkali
8. Msongo
Banda lenye joto sana na lisilo pitisha hewa vizuri huwapatia msongo/stress kuku, na kuku huweza kuanza kudonoana.
9. Uhaba wa vyombo bandani๐
Hii hutokana na kuwa na kuku wengi halafu vyombo vichache vya chakula , Kwahiyo wakati wa kula lazima watagombania na kudonoana
Kuku wa umri tofauti kuwekwa kwenye banda moja
Tumia Protini (Amino Acid) stahiki kulingana na tatizo.
Mfano: (methionine , lysine nk)
Changanya Proteni kiwango kizuri kwenye chakula cha kuku,chakula cha kuku kijumuishe virutubisho vyenye asili ya wanyama ambavyo ni chanzo kizuri cha Proteni
Hakikisha kuku wako wanakaa kwenye eneo la kutosha . hii inategemea aina ya kuku na umri wake.
Mungu ni Mwaminifu Sana na mwenye mipango na subira katika kila kitu hasa Sala na maombi yetu kwake. Tunaposali leo Mungu anatusikia na kujibu leo, kesho au hata miaka kumi ijayo. Inawezekana hata baraka zako za leo ni majibu ya Sala zako miaka kumi iliyopita. Sali bila kuchoka kwani hujui Sala zako zitakusaidia lini. Usitegemee majibu ya Sala zako wakati huo huo, amini katika uaminifu wa Mungu kwani anajua lini ni siku sahii ya kukujibu.
Unga 300gm
Siagi 225gm
Icing Sugar 60gm
Chokoleti iliyokoza (Dark Chocolate) 225gm
Vanilla 2 kijiko cha chai
Yai 1
Baking Powder ยฝ kijiko cha chai
Njugu za vipande ยฝ kikombe cha chai
Njugu zilizosagwa ยผ kikombe cha chai
1. Piga sukari na siagi katika mashine ya keki mpaka iwe laini
2. Kisha mimina yai na vanilla koroga vizuri
3. Mwisho mimina unga na baking powder polepole mpaka ichanganyike.
4. Kata kata umbo (shape) lolote unavyopenda (kama nyota, pembetatu,duara, kopa n.k)
5. Panga kwenye treya na choma kwa moto wa 350ยฐC , vikibadilika rangi kidogo tu vitoe
6. Yayusha chokoleti tia kwenye bakuli ndogo.
7. kisha paka kwa kijiko au chovyea upande mmoja mmoja wa biskuti kisha nyunyizia njugu za kipande na njugu ya unga.
8. Panga kwenye sahani tiyari kunywewa na chai ya maziwa au kahawa.
Mchele wa basmati – 3 Vikombe
Dengu – 2 vikombe
Viazi – 3 vikubwa
Kitunguu – 2 kubwa
Nyanya – 2
Pilipili mbichi kubwa – 3
Pilipilimanga – ยฝ kijiko cha chai
Garama Masala (bizari mchanganyiko) -1 kijiko cha chai
Supu ya vidonge (stock cubes) – 2 vidonge
Chumvi – kiasi
Mafuta – ยผ kikombe
Zaafarani – 1 kijiko cha chai
Dengu kama sio za tayari kwenye kopo, roweka na zichemshe hadi ziwive
Zaafarani โ iroweke katika maji ya dafu dafu (warm) ya chini ya robo kikombe weka kando.
Osha mchele, roweka.
Menya viazi na vitunguu, katakata vitunguu, na nyanya , weka kando.
Katakata viazi vipande vidogo vidogo kwa umbo la mchemraba (cubes).
Katika sufuria tia mafuta yakipata moto, tia viazi ukaange kidogo kwa moto mdogo mdogo hadi kukaribia kuwiva, toa weka kando.
Kaanga vitunguu hadi vigeuka rangi ya hudhurungi isiyokoza (light brown) kisha tia nyanya ukaange kidogo.
Tia vidonge vya supu (stock cubes) uvivuruge katika mchanganyiko, katakata pilipili mbichi kwa urefu tia, uendelee kukakaanga. Tia bizari, chumvi.
Zima moto, changanya dengu na viazi katika mchanganyiko huo.
Chemsha mchele kama kawaida ya kupika wali mweupe, kiini kiwe kimewiva nusu yake.
Chuja maji kisha changanya katika mchanganyiko wa dengu.
Nyunyizia zaafarani, uchanganye wali na mchanganyiko kidogo tu.
Funika acha uive katika mtoto mdogo mdogo au tia katika oveni hadi uive kama kawaida ya kupika wali.
Pakua katiha sahani na tolea na samaki yoyote wa kukaanga.
Recent Comments