Fangasi ya ukeni husababishwa na fangasi aina ya Candida albicans. Ugonjwa huu huitwa vaginal candidiasis kwa kiingereza na ni kati ya magonjwa ambayo husumbua wanawake mara kwa mara.
Maambukizi
Fangasi ya ukeni huambukizwa kwa njia ya;
Vyoo vichafu.
Kuchangia nguo za ndani na taulo.
Sababu
Uwezekano wa kupata fangasi ya uke au fangasi ya uke kujirudia rudia unaongezeka pale ambapo mwanamke ana;
Kisukari.
Ujauzito.
Anatumia antibiotics kwa muda mrefu
Ukimwi.
Joto, unyevu mwingi na nguo za kubana huchangia pia kutokea kwa fangasi ukeni. Ugonjwa huu haumbukizwi kwa njia ya ngono.
Dalili
Fangasi ya ukeni inaweza kuleta dalili zifuatazo kwa wagonjwa wenye maambukizi;
Kuwashwa sehemu za siri hasa wenye uke na mashavu ya uke.
Kutokwa na maji maji meupe mfano wa maziwa kutoka kwenye uke ambayo hayana harufu mbaya.
Maumivu wakati wa kukojoa kwa baadhi ya wagonjwa. Mara chache hali hii hutokea, ikisabaishwa nakuchubuka wakati wa kujiwasha.
Matibabu
Matibabu ya fangasi ya uke hutumia dawa za kuua fangasi (antifungals). Mara nyingi dawa za kuingiza kwenye uke (vaginal pessaries) hutumika kwa muda wa siku 3 mpaka 6. Wakati mwingine dawa za kunywa zinaweza kutumika kutibu fangasi hii.
Muone daktari kwa ajili ya uchunguzi, dawa na dozi sahihi.Cotrimazole na ketoconazole ni kati ya dawa zinazotumika mara kwa mara.
Kinga
Pamoja na matibabu kuna hatari ya maambukizi ya fangasi hawa kujirudia, hivyo ni muhimu kupata tiba hospitali na kurudi unapoona inajirudia. Vitu vingine muhimu kuzingatia ni;
Usafi wa nguo za ndani; kuvaa safi iliyofuliwa kila siku na kuanikwa juani (au kupigwa pasi).
Vaa nguo za ndani zilizokauka vizuri. Epuka zenye unyevunyevu au mbichi.
Vaa nguo za ndani zilizotengezwa kwa pamba (hupunguza joto na hivyo hatari ya fangasi kuzaliana)
Usafi wa sehemu za siri na kujikausha viruzi baada ya kuoga.
Usafi wa choo ni muhimu sana.
Read and Write CommentsReferences:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE