Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Jinsi ya kutumia kondomu ya kike

Kondomu ya kike inafahamika kwa jina la „care“ na “Lady Peteta”. Hapa Tanzania hazipatikani sehemu zote na bei yake ni kubwa kidogo.
Kondomu ya kike huingizwa ukeni kabla ya kujamiiana. Kama unatumia kondomu ya kike, chana kwa uangalifu pembezoni mwa pakiti. Kondomu ina pete mbili za plastiki na uwazi upande wa juu. Pete moja imelegea ni ndogo na iko kwa ndani, upande usio na uwazi. Pete ya pili ni kubwa zaidi, imeshikiliwa na iko upande wa tundu. Shikilia kondomu upande uliozibwa na minya pete ya ndani kwa dole gumba na kidole cha pili na cha kati. Mara nyingine inaweza ikakuponyoka, (kuteleza) lakini endelea kujaribu hadi umeiminya vizuri. Tafuta mkao mzuri na ingiza kondomu ya kike. Huku bado unaminya kwa vidole vyako iongoze kondomu ndani ya uke wako. Ukiiachia pete ya ndani itashikilia kondomu ndani ya uke. Sasa ingiza kidole chako kwenye kondomu, sukuma pete mpaka inapogota kwenye mlango wa uzazi.
Kondomu ya kike inaweza kuvaliwa saa kadhaa kabla ya kufanya ngono na pia inaweza kuvuliwa baada ya muda wa kufanyika ngono kupita. Ili kuhakikisha kuwa uume umeingia sehemu husika, msaidie mwenzi wako kuongoza uume kuingia kwenye uke ili usipenye pembeni.
Baada ya kujamiiana, vua kondomu kwa uangalifu. Tupa kondomu iliyotumika kwenye choo cha shimo au uichome. Usitupe kondomu iliyotumika ovyo.
Kama ilivyo kwa kondomu ya kiume, kondomu ya kike itatumika kwa mafanikio zaidi pale ambapo wahusikia wanakuwa na makubaliano na maelewano juu ya matumizi yake.

Kwa nini watu wasio na ualbino wanaogopa kuoa Albino kwa imani kuwa watawazalia watoto Albino?

Ualbino ni hali ya
kurithi, hii inamaanisha
kuwa unapata ualbino
kutoka kwa wazazi
wako. Watu wawili
weusi wanaweza kupata
Albino endapo kila
mmoja wao atakuwa
na kinasaba cha ualbino.
Hali hii huwezi kuiona
au kuijua. Unaweza tu
kuitambua baada ya
kujifungua. Takribani
mtu mmoja katika watu
70 ana kinasaba cha
ualbino lakini si rahisi
kujua ni nani anacho.
Endapo Albino ataoa
mwanamke mweusi,
uwezekano wa kuzaa
Albino ni mdogo sana.
Albino wengi waliooa au
kuolewa na watu weusi
wamepata watoto
ambao ni weusi.

Kwa upande mwingine, wanandoa ambao wamekwisha
pata mtoto Albino kuna uwezekano wa kupata mtoto mwingine
Albino katika uzazi wa pili.
Kuzaliwa Albino ni lazima mtoto huyo arithi vinasaba vya
ualbino kutoka kwa wazazi wote wawili, yaani mama na baba.

Nini matatizo ya macho ya Albino?

Mboni katika macho ya Albino haina pigimenti ya rangi. Kwa
hiyo, ni rahisi macho yao kuathiriwa na mwanga. Kwani mboni
ndiyo inayolinda jicho la ndani lisipatwe na mwanga mkali.
Vilevile kama mboni inavyolinda jicho dhidi ya mionzi ya jua,
inakuwa vigumu kuona kwa usahihi utofauti katika picha. Kwa
hiyo uwezo wa kuona unatiwa mawingu mawingu. Hivyo basi, ni
muhimu sana kukwepa inavyowezekana mionzi ya jua na kulinda
macho kwa kuvaa miwani ya jua.

Albino mara
nyingi hawaoni
vizuri, na hii
i n a t o f a u t i a n a
k w a m m o j a
hadi mwingine.
Inawezekana ni
kutoona mbali,
kutoona karibu au kuona mawingumawingu (ukungu).
Matatizo haya hutofautiana katika Albino. Ukweli ni kuwa
Albino anaweza kushiriki katika michezo mbalimbali, baadhi
wanaweza kuendesha magari na wengi wanaweza kusoma
maandishi ya kawaida.

Sababu za ukeketaji

Hakuna hata mmoja anayejua hasa kwa nini, na lini desturi
imeanza. Jamii inatoa maelezo tofauti kwa nini wasichana
wanatakiwa watahiriwe. Sababu zifuatazo zimetolewa kufanya
desturi hii: mila na utamaduni, dini, usafi, kulinda ubikira, kukaa
bila kuzini.
Kila mara sababu zinazotolewa za kuondoa au kukata kisimi
ni kupunguza nyege au starehe kwa mwanamke. Kwa makosa,
baadhi ya watu huamini kuwa kwa njia hii wanawake watakuwa
waaminifu kwa waume zao.
Kiafya hakuna sababu ya kumtahiri msichana, kinyume chake
inaweza kusababisha idadi ya matatizo ya afya. Ukeketaji
hautakiwi na dini yoyote. Hatakiwi na Koran wala Biblia.
Ukeketaji ni desturi na mila ambayo imepitishwa toka kizazi
kimoja hadi kizazi kingine.

Je,mwanaume akitoa uume nje ya uke kabla ya kumwaga shahawa anaweza kuambukizwa yeye au mwanamke na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Ndiyo, hata akitoa uume nje ya uke kabla ya kumwaga mbegu anaweza akaambukizwa Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Ni hatari kwa mwanamke na pia kwa mwanaume, kwa sababu vijidudu vimo ndani ya majimaji ukeni na uumeni. Hasa kama mmoja kati ya wapenzi ana vidonda au michubuko midogo sehemu za siri, Virusi vya UKIMWI. huingia kwa urahisi.

Kutoa uume nje ya uke kabla ya kumwaga shahawa siyo njia salama ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

Msichana ambaye hajawahi kujamiiana anaitwa bikira, je mvulana huitwaje?

Neno “bikira” ni mtu yeyote ambaye hajawahi kujamii ana maishani mwake, awe mwanamke au mwanaume.
Zamani, watu walimtambua msichana bikira kwa njia ya kuhakikisha kwamba kile kiwambo chembamba ndani ya uke kipo. Lakini kwa sababu ngozi hii huweza kuchanika kwa njia nyingine zaidi ya kujamii ana, siyo kipimo kizuri cha kumtambua msichana ambaye hajajamii ana kabisa (yaani bikira).
Katika jamii nyingi ni kawaida kuwaita `bikira` wanawake ambao hawajawahi kujamii ana. Pia, jamii nyingi wanasisitiza umuhimu wa mwanamke kuwa bikira mpaka siku ya kuolewa. Hata hivyo, neno “bikira” hutumiwa kwa wanawake na wanaume.

Vijana Albino wafanye nini ili kulinda ngozi yao?

Pamoja na matatizo ya kuona, ngozi ya Albino ni rahisi sana
kudhurika kwa mionzi ya jua. Hatima yake ikiwa ni uwezekano
mkubwa wa kupata saratani ya ngozi. Hivyo basi, kila Albino
anashauriwa daima kujikinga dhidi ya mionzi ya jua kwa kuvaa
nguo za mikono mirefu, kuvaa kofia pana, kuvaa miwani ya jua na
kwa wale wenye uwezo kujipaka mafuta maalumu yanayosaidia
kukinga ngozi dhidi ya mionzi ya jua.

Ukubwa wa kondomu

Kuna aina kondomu za ukubwa mbalimbali. Kwa wastani ukubwa wa kondomu unafaa kwa wanaume watu wazima karibu wote na vijana balehe waliokomaa. Mara chache sana, kondomu ni ndogo kwa wanaume fulani, lakini wakati mwingine wanaume wanaringa tu kuwa na uume mkubwa au wanatumia kisingizio tu kwa sababu hawataki kutumia kondomu.
Kwa upande wa vijana, balehe kondomu zinaweza kuwa ndogo ukilinganisha na ukubwa wa uume wao. Kwa vijana, ambao uume bado mdogo, ni vizuri zaidi wangeacha kujamiiana badala yake watumie njia nyingine za kumaliza hamu ya kutaka kujamiiana kama vile kukumbatiana na kubusu.

Je, kuna njia salama ya kutoa mimba?

Hatari inategemea na mazingira ambapo mimba inatolewa. Kama ni hospitalini na i inatolewa na mtaalamu aliyesomea na kama mazingira na vifaa ni safi, uwezekano wa kutoa mimba salama ni mkubwa. Lakini, hata katika mazingira hayo, shida zinaweza kutokea.

Msingi wa kukumbuka ni kwamba kutoa mimba mwenyewe au hata kwa mtu asiyesomea ni hatari sana. Kwa wanawake wanaojaribu kutoa mimba kuna uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi katika via vya uzazi na baadhi yao hutoboa mfuko wa uzazi. Matatizo haya ni hatari sana. Matatizo yanayohusiana na kutoa mimba ni mazito, kama mfuko wa uzazi kuharibika, maambukizi yasiyotibiwa katika via vya uzazi, kutoa damu nyingi, ugumba au hata kifo kwa mwanamke aliyehusika.

Kwa hiyo ni vizuri zaidi na tena salama kuacha kutoa mimba. Unaweza kuzuia kupata mimba i isiyotarajiwa, ama kwa kuacha kujamii ana au kwa kutumia njia za uzazi wa mpango kujikinga. Pia kumbuka kuwa utoaji mimba hauruhusiwi hapa Tanzania.

Jinsi mimba inavyopatikana

Ukitaka kuelewa jinsi mimba i inavyopatikana, lazima uelewe mzunguko wa hedhi wa mwanamke. Baada ya kuvunja ungo (yaani kupata hedhi kwa mara ya kwanza) msichana hupata hedhi mara moja kila mwezi. Kwa wanawake wengi ni kila baada ya siku 28, hata hivyo wengine huweza kupata hedhi chini au zaidi ya siku hizo.
Siku ya kwanza ya hedhi huhesabiwa kama siku ya kwanza ya mzunguko. Baada ya damu kutoka, yai moja linaanza kukua ndani ya kokwa. Na vilevile utando ndani ya mfuko wa uzazi huanza kujengeka i ili ukaribishe mimba. Kati ya siku 11 au 14 yai hupevuka ndani ya kokwa na halafu husafiri kwenye mrija

wa kupitisha mayai hadi mfuko wa uzazi. Mwanamke anapata mimba kama yai litaungana na mbegu ya kiume ndani ya mrija wa kupitisha mayai. Ina maana kwamba endapo atajamii ana kipindi cha siku chache kabla ya yai kupevuka au siku yai linapopevuka na kutoka kwenye kokwa, linarutubishwa wakati linaelekea kwenye mji wa mimba, na linapofika hapo kwenye mji wa mimba linatulia kwenye utando wa mji wa mimba. Mtoto anahifadhiwa na kukua ndani ya mji wa uzazi mpaka siku ya kuzaliwa. Kama yai halikurutubishwa, basi yai hufa na hutoka pamoja na utando wa mfuko wa uzazi na hutoka nje ya mwili wa mwanamke kama damu ya hedhi. Yaani, mwanamke atapata hedhi kama kawaida na atafahamu kwamba hajashika mimba.

Kuna fikra kuwa Albino ni watu wa kawaida je, kisayansi hii ni kweli?

Hii ni kweli kabisa. Watu wanaoishi na ualbino ni watu wa
kawaida kama binadamu wengine wote na wanaweza kuwa
wa aina tofauti kama binadamu wengine. Wanaweza kuwa
wadogo au warefu, wanene au wembamba, warembo au wasio
warembo, wenye vipaji au wa wastani. Wanaweza kuwa na
uthubutu au wenye aibu, wachangamfu au jeuri, wenye tabia ya
ushirikiano au wenye tabia ya uhasama.
Kumbuka kuwa utofauti wao upo tu kwenye muonekano wa ukosefu
wa rangi kwenye ngozi, nywele na macho. Wakati umefika kwa
jamii kujifunza kuwakubali Albino kama binadamu wengine, wenye
hisia, mahitaji, uwezo na wanastahili haki zote za binadamu kama
alivyo mtu mwingine yoyote.

Sabau za ubakaji

Ni vigumu kuelewa nini kinamfanya mtu aweze kubaka mwingine.
Ubakaji ni aina nyingine ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia
ambao utaleta madhara mengi kwa muhusika kwa hiyo hakuna
msamaha kwa ubakaji.
Ubakaji mara zote ni kosa la mbakaji. Hakuna maelezo
mazuri ya kuwaelezea watu ambao ni, au wanajihusisha na
ubakaji. Ubakaji unatendeka kwa sababu mbalimbali. Baadhi
ya wabakaji ni wagonjwa wa akili, wanaume wengine wanabaka
kwa sababu wanafikiri wanawake wako pale ili kuwaridhisha
wao katika masuala ya kujamiiana, na kumwadhibu msichana au
wameshawishiwa na wengine.
Hii ni kosa maana hauheshimu haki ya binadamu na thamani ya
muhusika. Dawa za kulevya na pombe yanaweza vinashawishi
tabia ya ubakaji maana vinawafanya watu kushindwa kujizuia
kuhusu tabia zao.

Jinsi ya Kuwa na Tarehe ya Ushirikiano na Msichana

  1. Anza kwa Kujijenga Kimaumbile
    Kabla ya kumwomba msichana tarehe ya ushirikiano, ni muhimu kujijenga kimaumbile. Hakikisha unajitunza na kujitunza kwa kutunza afya yako, kuoga na kuvaa mavazi safi na yenye kuvutia. Hii itaashiria kuwa unajitambua na unathamini afya yako.

  2. Jenga Uhusiano Mzuri
    Ili kuwa na tarehe ya ushirikiano na msichana, ni muhimu kujenga uhusiano mzuri kwanza. Piga simu yake mara kwa mara, mpe text na mualike kutoka nje. Kukutana na marafiki zake na kuwa karibu na familia yake inaweza kumsaidia kukuamini na kukupenda zaidi.

  3. Muulize kwa Ustaarabu
    Baada ya kujenga uhusiano mzuri, sasa inakuwa rahisi kukaribisha msichana kwenda nje. Muulize kwa ustaarabu na kwa hisia nzuri. Mfano, "Je, ungependa kutoka nje leo jioni na mimi?" Kwa njia hii, utamwonyesha kuwa unaheshimu hisia zake na unataka kufanya jambo sahihi.

  4. Chagua Mahali Pazuri
    Chagua mahali pazuri kwa tarehe yenu ya ushirikiano. Kama unamjua vizuri, unaweza kuchagua sehemu ambayo anapenda. Hii inaweza kuwa mgahawa wa kupendeza au sehemu ya mandhari nzuri. Kumbuka kuwa mahali unachochagua lazima iwe salama na rahisi kufikia.

  5. Kuwa Mwenyewe
    Kuwa mwaminifu na kuwa mwenyewe. Msichana anaweza kukuona kama mtu wa kweli na wa kuaminika ikiwa utakuwa wazi na mahiri kuhusu maisha yako na malengo yako. Kumbuka kuchukua muda wa kumjua msichana na kuonyesha upendo wa kweli.

  6. Kuwa Mwanaume wa Kuvutia
    Kuwa mwanaume wa kuvutia na wa kimapenzi. Jaribu kumfurahisha msichana kwa kutoa zawadi ndogo ndogo kama maua au chokoleti. Jifunze kuhusu maslahi yake na mazungumzo ya kuvutia. Kwa njia hii, utajenga uhusiano mzuri na msichana na kuwa na tarehe nzuri ya ushirikiano.

Kwa kufuata vidokezo hivi, utakuwa na mafanikio katika kuwa na tarehe ya ushirikiano na msichana. Jihadhari na kuwa mpole, mvumilivu na mwenye kujitambua. Kumbuka kuonyesha upendo na kujali kwa msichana. Mwishowe, hakikisha unafurahia tarehe yako ya ushirikiano na msichana!

Nini kifanyike ili kurekebisha matatizo ya macho ya Albino?

Kuishi kwa kushindwa kuona sawasawa ni changamoto ya
msingi waliyonayo Albino, inaathiri elimu yao (hususan katika
usomaji), katika kujumuika (ikiwemo kushiriki katika michezo
na kukubalika na rika lao) na katika uwezo wa kutembea katika
mazingira magumu. Matatizo huanzia pale ambapo udhaifu huu
usipotambuliwa na marekebisho yoyote yasifanywe na familia
au jamii. Kama marekebisho yatafanyika ama kwa kutumia
miwani ya macho, au kuwa na vitabu vyenye maandishi makubwa
au kutumia lensi ya kukuza maandishi au kwa kuwapa nafasi ya
mbele darasani watoto Albino wanaweza kufanya vizuri kama
watoto wengine.

Je, kuna umuhimu wa kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wakati wa ngono/kufanya mapenzi? Ndiyo! Kwa sababu kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wakati wa ngono/kufanya mapenzi kunaweza kuboresha uzoefu wako wa ngono na kufanya iwe salama zaidi kwa hivyo hakikisha unakaa nami hadi mwisho wa makala hii.

Kabla ya kuanza, ni muhimu kuelewa kuwa kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wakati wa ngono/kufanya mapenzi sio sawa na kuwa mtaalam wa afya ya uzazi. Kwa hivyo, usijaribu kufanya kazi ambazo unahitaji ujuzi wa kitaalamu.

Hapa kuna sababu na faida za kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wakati wa ngono/kufanya mapenzi:

  1. Kuelewa jinsi mwili wako unavyofanya kazi: Kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wako wakati wa ngono/kufanya mapenzi kunaweza kukusaidia kuelewa jinsi mwili wako unavyofanya kazi. Unaweza kujifunza jinsi ya kufikia kilele, jinsi ya kuongeza hamu ya ngono, na jinsi ya kutumia vizuri viungo vyako vya uzazi.

  2. Kupunguza hatari ya maambukizi: Kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wako wakati wa ngono/kufanya mapenzi kunaweza kusaidia kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Unaweza kujifunza jinsi ya kutumia kinga za kujamiiana, jinsi ya kuzuia maambukizi, na jinsi ya kutambua dalili za maambukizi.

  3. Kupunguza maumivu: Kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wako wakati wa ngono/kufanya mapenzi kunaweza kukusaidia kuepuka maumivu wakati wa ngono. Unaweza kujifunza jinsi ya kutumia mafuta ya kulainisha, jinsi ya kuepuka kuumia, na jinsi ya kufurahisha mwenzi wako.

  4. Kuongeza hamu ya ngono: Kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wako wakati wa ngono/kufanya mapenzi kunaweza kusaidia kuongeza hamu yako ya ngono. Unaweza kujifunza jinsi ya kuchochea viungo vyako vya uzazi, jinsi ya kumfanya mwenzi wako apate hamu ya ngono, na jinsi ya kudumisha mahusiano yako ya ngono.

  5. Kujisikia vizuri: Kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wako wakati wa ngono/kufanya mapenzi kunaweza kukusaidia kujisikia vizuri juu ya mwili wako na kujiamini katika mahusiano yako ya ngono. Unaweza kujifunza jinsi ya kuelewa mwili wako, jinsi ya kudumisha afya ya uzazi, na jinsi ya kufurahisha mwenzi wako.

  6. Kukuza utafiti: Kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wako wakati wa ngono/kufanya mapenzi kunaweza kukusaidia kufanya utafiti wa ziada. Unaweza kujifunza kuhusu utafiti wa kisayansi unaohusu ngono, jinsi ya kupata vifaa vya kujifunzia, na jinsi ya kujitolea kwa taasisi za kijamii.

  7. Kujifunza jinsi ya kutumia teknolojia: Kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wako wakati wa ngono/kufanya mapenzi kunaweza kukusaidia kujifunza jinsi ya kutumia teknolojia. Unaweza kujifunza jinsi ya kutumia programu za kufuatilia afya ya uzazi, jinsi ya kutumia vifaa vya uzazi wa mpango, na jinsi ya kutumia simu za rununu na vidonge kwa usalama.

  8. Kujifunza jinsi ya kufurahisha mwenzi wako: Kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wako wakati wa ngono/kufanya mapenzi kunaweza kukusaidia kujifunza jinsi ya kufurahisha mwenzi wako. Unaweza kujifunza jinsi ya kumfanya mwenzi wako asisitize, jinsi ya kumfanya mwenzi wako ashinde kilele, na jinsi ya kumfanya mwenzi wako ajisikie vizuri juu ya mwili wake.

  9. Kujifunza jinsi ya kudumisha afya nzuri ya uzazi: Kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wako wakati wa ngono/kufanya mapenzi kunaweza kukusaidia kudumisha afya nzuri ya uzazi. Unaweza kujifunza jinsi ya kudumisha usafi wa uzazi, jinsi ya kuzuia magonjwa ya zinaa, na jinsi ya kupanga uzazi.

  10. Kudumisha mahusiano yako: Kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wako wakati wa ngono/kufanya mapenzi kunaweza kukusaidia kudumisha mahusiano yako. Unaweza kujifunza jinsi ya kuelewa mwenzi wako, jinsi ya kumfanya mwenzi wako awe na furaha, na jinsi ya kudumisha mahusiano yako ya ngono.

Kwa hivyo, kama unatafuta kuboresha uzoefu wako wa ngono, kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wako wakati wa ngono/kufanya mapenzi ni hatua nzuri. Kwa kuwa unajua faida ya kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wako wakati wa ngono/kufanya mapenzi, unaweza kuchunguza zaidi kwa kusoma vitabu, makala, na kuhudhuria mafunzo ya ngono. Kumbuka, lengo ni kuboresha uzoefu wako wa ngono na kufanya iwe salama zaidi. Je, umejifunza nini kuhusu anatomi ya mwili wako wakati wa ngono/kufanya mapenzi? Je, ni nini ambacho umepata kibaya? Au kuna jambo lingine unataka kujifunza? Hebu tuzungumze juu ya hilo kwenye maoni hapa chini!

Je, nikitoa au kupata damu hospitalini, itakuwepo hatari ya kupata virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Katika swali hili lazima tutofautishe kati ya kutoa damu na kuwekewa damu. Kutoa damu hakuleti hatari, kama mtaalamu wa afya aliyechoma sindano kwa ajili ya kutoa damu anatumia sindano na vifaa vilivyochemshwa.
Kwa kawaida hakuna matatizo kuongezwa damu, kwa sababu damu i inapimwa kabla ya kumuongeza mgonjwa hospitalini. Iwapo damu i imepimwa na sindano zilizochemshwa zimetumika hakuna ubaya wowote katika kuongezwa damu.

Je, nikiambukizwa virusi vya UKIMWI na UKIMWI nifanye nini?

Jambo la msingi ni kutokukata tamaa na kuwa na matumaini. Mara nyingine i inasaidia kama utakuwa na mazungumzo na watu ambao tayari wanaishi na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI au marafiki na ndugu unaowaamini. Jaribu kuongea na mwenzi wako i ili kumfahamisha juu ya hali yako ya maambukizi. Yeye pia anaweza kuwa ameambukizwa na angependa kupima. Ni muhimu kuzingatia kanuni muhimu za afya nzuri kama vile kula vyakula vyenye mlo kamili na kujiweka katika hali ya usafi. Kwa mantiki hiyo hiyo ni lazima kuharakisha kutibu maradhi mengine yatakayojitokeza. Watu wanaoishi na virusi i vya UKIMWI wanashauriwa wasitumie pombe wala kuvuta sigara, kwa sababu vyote hivyo huchangia katika kudhoofisha mwili. Kama watafanya ngono, ni lazima watumie kondomu i ili wasiambukize wengine.
Aliyeambukizwa, baada ya miaka kinga ya mwili i wake i itaanza kupungua na atatakiwa kupata dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ARV).
Kama mtu aliyeambukizwa na virusi vya UKIMWI atazingatia masharti haya, kuna uwezekano wa kuishi na kufurahia maisha kwa miaka mingi.

Je, kuna madhara gani ya kunywa pombe kwa vijana hasa kijana Albino?

Athari za pombe kwa mtu anayeishi na ualbino ni sawa na zile
zinazowapata watu wengine.
Mtu akiwa katika hali ya ulevi anaweza kuzembea katika
kufanya uamuzi sahihi kwa mfano kuhatarisha maisha yake
kwa kuendesha baiskeli yake kimchoromchoro, kujamiiana
bila kuvaa kondomu na kadhalika. Mbali na hayo, watu wenye
matatizo ya kunywa pombe husahau kujiweka katika hali nzuri
kwa maana hawajali kula chakula. Tabia hii inamuweka katika
hatari ya kuandamwa na maradhi.
Pombe zinaweza pia kuingiliana na maisha/uhusiano wa kimwili.
Mwanzo kabisa pombe inaweza kukusisimua na kukufanya
mchangamfu (kutoona aibu), lakini kadiri unavyoendelea
kunywa unaanza kusinzia na kwa upande wa wanaume wengine,
uume kukosa nguvu. Unaweza kushawishika kutoa aibu uliyo
nayo kwa kunywa pombe lakini mara nyingi hii haileti mvuto
kutoka kwa wenzi wako.

Kunywa pombe pia kunaleta uharibifu wa kudumu kwenye ubongo
ambao unamfanya mtu kupata matatizo ya kumbukumbu.
Pombe imewekwa kwenye kundi la vilevi tegemezi. Mwili
ukishazoea pombe, ni rahisi sana watu kutumia pesa zote
kwa ajili ya pombe na kusahau kufanya mambo mengine
yatakayomletea maendeleo katika maisha yake.

Mambo usiyoyajua kuhusu mimba na wasichana

Je, mimba hupatikanaje?

Ukitaka kuelewa jinsi mimba i inavyopatikana, lazima uelewe mzunguko wa hedhi wa mwanamke. Baada ya kuvunja ungo (yaani kupata hedhi kwa mara ya kwanza) msichana hupata hedhi mara moja kila mwezi. Kwa wanawake wengi ni kila baada ya siku 28, hata hivyo wengine huweza kupata hedhi chini au zaidi ya siku hizo.
Siku ya kwanza ya hedhi huhesabiwa kama siku ya kwanza ya mzunguko. Baada ya damu kutoka, yai moja linaanza kukua ndani ya kokwa. Na vilevile utando ndani ya mfuko wa uzazi huanza kujengeka i ili ukaribishe mimba. Kati ya siku 11 au 14 yai hupevuka ndani ya kokwa na halafu husafiri kwenye mrija wa kupitisha mayai hadi mfuko wa uzazi. Mwanamke anapata mimba kama yai litaungana na mbegu ya kiume ndani ya mrija wa kupitisha mayai. Ina maana kwamba endapo atajamii ana kipindi cha siku chache kabla ya yai kupevuka au siku yai linapopevuka na kutoka kwenye kokwa, linarutubishwa wakati linaelekea kwenye mji wa mimba, na linapofika hapo kwenye mji wa mimba linatulia kwenye utando wa mji wa mimba. Mtoto anahifadhiwa na kukua ndani ya mji wa uzazi mpaka siku ya kuzaliwa. Kama yai halikurutubishwa, basi yai hufa na hutoka pamoja na utando wa mfuko wa uzazi na hutoka nje ya mwili wa mwanamke kama damu ya hedhi. Yaani, mwanamke atapata hedhi kama kawaida na atafahamu kwamba hajashika mimba.

Ni siku gani katika mzunguko wa hedhi yai linapoweza kurutubishwa?

Yai mmoja hupevuka siku 14 kabla ya hedhi i i inayofuata. Baada ya yai kukomaa ndani ya kokwa la upande wa kulia au wa kushoto, yai husafirishwa kwenye mrija wa kupitisha mayai mpaka kwenye mfuko wa uzazi.
Yai likijiunga na mbegu ya kiume ndani ya mrija wa kupitisha mayai siku zilezile, linaweza kurutubishwa. Yaani, endapo mwanamke anajamii ana kipindi cha siku chache kabla ya yai kupevuka au siku yai linapopevuka anaweza akapata mimba.
Kwa sababu wasichana wengi hawapati hedhi ya kawaida, yaani mzunguko wa siku 28 katika kila mwezi, ni vigumu sana kwao kufahamu tarehe ya hedhi i i inayofuata. Hivyo ni vigumu kujua lini litakuwepo yai linalongojea kurutubishwa.
Mzunguko wa hedhi kwa msichana unaweza kuathiriwa na mfadhaiko, huzuni, safari au mabadiliko mengine katika maisha ya msichana. Hata kama msichana ana mzunguko wa kawaida wa hedhi hali hiyo inaweza kubadilika ghafla na ukawa sio wa kawaida. Wanawake wengi na hasa wasichana hawawezi kutegemea kuhesabu siku kama njia ya kuzuia mimba, kwa sababu hawawezi kuwa na uhakika i iwapo lipo yai linalongojea kurutubishwa au la. Hakuna siku salama za kuepukana na mimba!

Ninaweza kupata mimba wakati nipo kwenye hedhi?

Ili mwanamke aweze kushika mimba, i inabidi yai lililopevuka likutane na mbegu za kiume. Yai pevu linapokosa mbegu hufa na kwa vile utando kwenye tumbo la uzazi ulishajiandaa kupokea yai lililorutubishwa hubomoka. Kwa pamoja, yai na utando hutoka kama damu kupitia ukeni na i le damu huitwa hedhi.
Hedhi ni dalili, kwamba yai halikurutubishwa na hivyo limeshakufa na kutoka. Kwa kawaida, wakati huo halitakuwepo yai jingine lililopevuka kuweza kurutubishwa na kwa hiyo uwezekano wa kupata mimba hautakuwepo. Lakini, mara chache kuna hitilafu katika mzunguko wa hedhi na yai jingine linakuwepo tayari kwa kurutubishwa, hata ukiwa kwenye hedhi. Kwa hiyo uwezekano wa kupata mimba wakati wa hedhi upo, hata kama ni mdogo.

Je, inawezekana msichana akapata mimba kabla ya kuvunja ungo?

Ndiyo, msichana anaweza kupata mimba kabla ya kuvunja ungo, yaani kabla ya kuona hedhi kwa mara ya kwanza. Kwa uhakika utajiuliza kwa nini.
Kabla ya kuona hedhi, yai ndani ya kokwa linapevuka na kusafiri kutoka kwenye kokwa mpaka tumbo la uzazi. Hedhi yenyewe ni dalili kwamba lile yai pevu halikurutubishwa na kwa hiyo linatoka pamoja na utando wa tumbo la uzazi kupitia ukeni.
Kuna maana kwamba hata kama msichana hajavunja ungo, i inawezekana kwamba ndani ya tumbo lake yai limeshaanza kupevuka. Lile yai linaweza kurutubishwa na msichana anaweza kupata mimba, hata kama hajaona hedhi yake kwa mara ya kwanza.

Je, msichana akijamiiana mara moja tu anaweza akapata mimba?

Ndiyo, msichana anaweza kupata mimba akijamii ana mara moja tu. Inategemea na mzunguko wa hedhi. Kama ndani ya tumbo la msichana lipo yai pevu ambalo ni tayari kwa kurutubishwa, na siku i ileile msichana anajamii ana na mvulana anaweza kupata mimba. Isitoshe, anaweza kupata mimba hata kama ni mara ya kwanza ya kujamii ana

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Kuwa na Hamu ya Kufanya Ngono?

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Kuwa na Hamu ya Kufanya Ngono? 😊🙌

Leo tutajadili jinsi ya kukabiliana na hisia za kuwa na hamu ya kufanya ngono kwa njia ambayo inafuata maadili ya Kiafrika. Kama kijana mwenye maadili mema ya Kiafrika, ni muhimu kutambua umuhimu wa kusubiri hadi ndoa kabla ya kujihusisha kimapenzi. Hapa kuna vidokezo 15 vya kukusaidia kufanya hivyo:

  1. Kujielewa: Elewa ni nini kinachochochea hisia hizo za ngono ndani yako. Je, ni kutokuelewa, mazingira au shinikizo za kijamii? Kwa kujielewa, utakuwa na uwezo wa kushughulikia hisia hizo kwa njia sahihi.

  2. Kujifunza kuhusu afya ya uzazi: Kuelewa hatari na matokeo ya ngono kabla ya ndoa ni muhimu. Kujifunza kuhusu afya ya uzazi na athari za ngono zisizodhibitiwa, itakusaidia kuthamini thamani ya kusubiri hadi ndoa.

  3. Kuweka mipaka: Jiwekee mipaka na kushikilia maadili yako ya Kiafrika. Jua ni wapi unapovuka mipaka yako na jinsi ya kuiweka.

  4. Kuwa karibu na marafiki wanaofuata maadili sawa: Kuwa na marafiki ambao wanashiriki maadili yako na kusaidiana kufuata njia sahihi inaweza kuwa na athari kubwa katika kukabiliana na hisia hizo.

  5. Kuweka malengo na mipango: Kuwa na malengo na mipango ya kujenga mustakabali wako itakusaidia kuzingatia mambo muhimu katika maisha yako kuliko kufanya ngono kabla ya wakati.

  6. Kujihusisha na shughuli za kujenga: Kujihusisha na shughuli zenye kujenga kama michezo, kusoma, kufanya kazi, na kuchangia katika jamii kunaweza kukusaidia kuondoa mawazo ya ngono.

  7. Kujenga uhusiano mzuri na Mwenzi wako wa maisha: Kuwa na uhusiano mzuri na mwenzi wako wa maisha kunatoa nafasi ya kujenga upendo wa kweli kabla ya kujihusisha kimapenzi.

  8. Mafunzo ya maadili: Jifunze kuhusu maadili ya Kiafrika na umuhimu wake katika maisha ya kijamii. Kuelewa maadili haya itakusaidia kujenga utambuzi mzuri wa thamani ya kusubiri hadi ndoa.

  9. Kuepuka mazingira hatarishi: Epuka mazingira ambayo yanaweza kuchochea hisia hizo za ngono, kama vile sinema zenye maudhui ya ngono na mitandao ya kijamii yenye picha za ngono.

  10. Kuwa na mawazo chanya: Kuwa na mawazo chanya na matumaini kuhusu mustakabali wako itakusaidia kujikumbusha umuhimu wa kusubiri hadi ndoa.

  11. Kusoma hadithi za mafanikio: Kusoma hadithi za watu ambao wamesubiri hadi ndoa kabla ya kujihusisha kimapenzi na wamepata mafanikio, kunaweza kukusaidia kuona umuhimu wa kusubiri.

  12. Kuwa na malengo ya muda mrefu: Kuwa na malengo ya muda mrefu katika maisha yako, kama vile kujenga familia na kufanikiwa katika kazi yako, kunaweza kuimarisha azma yako ya kusubiri hadi ndoa.

  13. Kuwa na mazungumzo na wazazi au walezi wako: Mazungumzo na wazazi au walezi wako juu ya thamani ya kusubiri hadi ndoa yanaweza kukusaidia kufahamu maoni na ushauri wao kuhusu suala hili muhimu.

  14. Kukumbuka thamani na heshima ya mwili wako: Kukumbuka kuwa mwili wako ni zawadi muhimu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na unapaswa kutunzwa. Kusubiri hadi ndoa ni njia ya kuonyesha heshima kwa mwili wako.

  15. Kusubiri hadi ndoa kabla ya kujihusisha kimapenzi: Mwishowe, njia bora ya kukabiliana na hisia hizo za ngono ni kusubiri hadi ndoa kabla ya kujihusisha kimapenzi. Hii itahakikisha unakuwa na uhusiano thabiti na wa kudumu, na pia itaepusha hatari zinazohusiana na ngono kabla ya ndoa.

Kumbuka, kusubiri hadi ndoa na kubaki safi ni baraka kubwa na inajenga msingi imara kwa mustakabali wako. Je, una maoni gani juu ya kusubiri hadi ndoa kabla ya kujihusisha kimapenzi? Je, una njia nyingine za kukabiliana na hisia hizo? Tungependa kusikia kutoka kwako! 😊👍

Asante kwa kusoma na kumbuka, uko kwenye njia sahihi. Endelea kusubiri hadi ndoa na kujenga maisha yenye thamani na furaha! 🙌🌟

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About