Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Je, ngono/kufanya mapenzi ni jambo la faragha au unajisikia huru kuzungumzia kuhusu hilo?

Jambo la faragha kabisa ni ngono au kufanya mapenzi. Kila mtu ana hisia tofauti kuhusu suala hili. Wengine hujisikia huru kuzungumza kuhusu ngono na wengine huitazama kama jambo la kibinafsi kabisa. Hata hivyo, kuna umuhimu wa kuzungumza kuhusu ngono hasa kwa watu ambao wanaanza kujifunza kuhusu ngono.

  1. Kuzungumza kuhusu ngono kunaweza kuwasaidia watu kujifunza zaidi kuhusu afya yao ya kijinsia.

  2. Kuzungumza kuhusu ngono kunaweza kusaidia kupunguza hatari za maambukizi ya magonjwa ya zinaa.

  3. Kwa wapenzi, kuzungumza kuhusu ngono kunaweza kuwasaidia kuelewa mahitaji ya kila mmoja na kufurahia ngono zaidi.

  4. Kuzungumza kuhusu ngono kunaweza kuwa na manufaa kwa watu ambao wanakabiliwa na changamoto za kijinsia kama vile kutokuwa na hamu ya ngono au kutokujua jinsi ya kufurahia ngono.

  5. Kuzungumza kuhusu ngono kunaweza kuwasaidia watu kuwa na uelewa wa kina kuhusu jinsi ya kujikinga na mimba zisizotarajiwa na magonjwa ya zinaa.

  6. Kwa wapenzi, kuzungumza kuhusu ngono kunaweza kuwasaidia kuboresha uhusiano wao kwa kufurahia ngono zaidi na kupunguza tatizo la kutokuwa na hamu ya ngono.

  7. Kuzungumza kuhusu ngono kunaweza kuwasaidia watu kuelewa kwamba ngono ni jambo la kawaida na halina ubaya wowote.

  8. Kuzungumza kuhusu ngono kunaweza kuwasaidia wazazi kuzungumza na watoto wao kuhusu ngono na kusaidia watoto kujifunza kuhusu afya ya kijinsia.

  9. Kuzungumza kuhusu ngono kunaweza kuwasaidia watu kujenga ujasiri na kujiamini katika uhusiano wao.

  10. Kuzungumza kuhusu ngono kunaweza kuwasaidia watu kujifunza jinsi ya kufurahia ngono kwa usalama na kwa njia inayowafaa.

Unajisikia vipi kuhusu kuzungumzia ngono? Je, unaona kwamba ni jambo la faragha kabisa au unajisikia huru kuzungumza kuhusu ngono? Je, umewahi kuzungumza kuhusu ngono na mtu yeyote na jinsi gani ilikuathiri? Tafadhali shiriki mawazo yako kwa kutuandikia sehemu ya maoni hapo chini.

Nitafanya nini kuzuia dawa za kulevya na jinsi gani nitaepukana na marafiki wabaya?

Wakati mwingine ni vigumu kusema hapana ukiwa na
maana ya hapana. Jaribu kuwa mpole na usiwe mgomvi.
Jaribu kueleza sababu zako kwa upole na uwaeleze rafiki zako kile unachokijua na nini unachofanya. Hivyo utapata heshima kutoka kwa wanarika wenzako na rafiki zako. Kama vijana wenzako watakushawishi utumie dawa za kulevya wakati wewe hutaki, wanaweza kuwa marafiki wabaya. Kumbuka kwamba rafiki ni mtu ambaye anajali, analinda na kuthamini maisha ya rafiki yake. Kwa maana hiyo, kwa nini mtu anayekushawishi kwa makusudi kufanya kitu chenye madhara kwa afya yako awe rafiki wa kweli?!

Kuna aina ngapi za dawa za kulevya?

Tunatofautisha dawa za kulevya katika makundi mawili. Zile zinazokubalika na zile zisizokubalika kisheria. Tanzania, dawa za kulevya zinazokubalika kisheria ni pamoja na tumbaku na pombe, pia dawa zilizothibitishwa kwa maandishi na daktari. Dawa zinazotolewa kwa udhibitisho wa madaktari ni zile dawa za kutibu. Pale zinapotolewa kwa sababu nyingine mbali na matibabu au maelezo ya daktari zinakuwa dawa za kulevya. Miongoni mwa dawa zinazotumika vibaya hapa Tanzania ni valium, asprin na panado. Vimiminika kama petroli pia hutumiwa kama dawa za kulevya. Vitu hivi hutumiwa kwa njia ya kuvuta hewa yake kwa pua au mdomo.
Pia kuna vileo visivyoruhusiwa ambavyo hutengenezwa kienyeji kama vile gongo. Dawa za kulevya ambazo hutumika sana Tanzania ni pamoja na bangi, mirungi, mandrax, heroini na kokaini. Kokaini ambayo hupatikana katika hali ya ungaunga ulio mweupe, hutumiwa kwa njia ya kuvuta kwa pua au kuchanganywa na maji na baadaye kujidunga mwilini kwa kutumia sindano. Heroini pia hupatikana kama unga mweupe. Unaweza kuvuta heroini kama sigara au kuvuta hewa yake kwa ndani na pia kwa kujidunga sindano. Katika hali i i isiyo ya kawaida heroini vilevile inaweza kupatikana katika vipande vidogovidogo vya kahawia vijulikanavyo kama โ€œsukari ya kahawiaโ€.
Njia nyingine ya kuzungumzia dawa za kulevya ni kutokana na madhara yake. Yapo madawa ambayo hupagawisha au yanayozubaisha au kupoozesha kama vile kileo, nikotini, dawa za usingizi, kwa mfano valium na heroini. Dawa hizo zinamfanya mtumiaji kujisikia shwari, lakini pia huhuzunisha. Dawa zinazochamngamsha ni i kama mirungi, kokaini na zile za kuvuta, kwa mfano petroli, zina madhara ya kukufanya uhamasike na kujisikia kuwa na nguvu. Dawa zinazopagawisha zinaleta hisia, sauti, taswira, harufu kwa mtu japokuwa vyote hivyo havipo kweli. Bangi ni mojawapo ya dawa hizi.

Kulambana sehemu za siri ni salama kiafya? Je, tendo hili ni la kawaida?

Si rahisi kusema ni kitendo kipi kilicho cha kawaida na kisicho cha kawaida. Kulamba ni jambo linalofanyika

na kama wahusika wote wanalipenda ni sawa. Inashauriwa kuosha sehemu za siri kabla ya kufanya hivyo. Kwa kufanya hivyo, yaani kunawa kunafanya tendo hili kufanyika katika hali ya usalama kiafya. KAMA wote mtakuwa wazima bila kuwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa hasa kisonono (gono).

Ninawezaje kumsaidia mtu kuacha kuvuta sigara na kunywa pombe?

Jaribu kutafuta sababu zinazowafanya rafiki, ndugu na jamaa
zako kuwa na tabia ya kuvuta sigara na kunywa sana pombe.
Jaribu kuwa naye karibu na mshughulishe asipate muda wa
kuvuta na kunywa pombe. Kuwa naye kwa muda mrefu, fanya
naye kazi na mtambulishe kwa rafiki zako ambao hawatumii
sigara wala pombe. Mweleze umuhimu wa yeye kukaa mbali na
vishawishi. Mweleze kwa nini ni vigumu sana kushinda vishawishi
ukiwa katika hali ya ulevi, na unapotoa ushauri huo yakupasa
usiwe mlevi na mvutaji.
Inaweza ikatokea, jamaa unayemshauri kuhusu madhara ya
kunywa pombe na kuvuta sigara, akachukia au ukawa ndio mwisho
wa urafiki wenu. Usijilaumu, ujitahidi kumsaidia kadiri uwezavyo.
Wakati mwingine ni vyema ukavunja urafiki huo kwa usalama
wako na wa rafiki yako. Endapo kama itatokea akaanza kutambua
madhara na matokeo ya uvutaji sigara na unywaji pombe na
hatimaye kuchukua uamuzi wa kuelezea matatizo yake, itampasa
amtafute mtaalamu ili aweze kupata ushauri nasaha.

Shopping Cart
0
    0
    Your Cart
    Your cart is emptyReturn to Shop
    ๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About