Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya

Jinsi ya kupika vitumbua inavyotakiwa

Mahitaji

Unga wa mchele ( Vikombe 2 vikubwa)
Sukari (Nusu ya kikombe kikubwa)
Hamira ( Nusu ya kijiko cha chai)
Hiliki (Nusu ya kijiko cha chai)
Tui la nazi ( Kikombe kimoja kikubwa)
Unga wa ngano (Vijiko viwili vya chakula)
Mafuta ya kuchomea (Vegetable oil)

Matayarisho

Unachanga unga, sukari, hamira, hiliki, unga wa ngano na tui la nazi pamoja katika bakuli la plastiki. Kisha unaukoroga mpaka mchanganyiko unakuwa kama uji mzito. Kava bakuli lililokuwa na mchanganyiko kisha hifadhi katika sehemu yenye joto kwa muda wa masaa matatu.

Jinsi ya kupika

Weka chuma cha kuchomea vitumbua katika moto wa wastani, kisha weka mafuta kwenye chuma cha kuchomea ( Kijiko kimoja cha chai) mafuta yakisha pata moto tia uji wako (upawa mmoja) katika kila shimo la chuma cha kuchomea. Acha mpaka kitumbua kikauke kisha geuza na tia mafuta. Acha upande wa pili wa kitumbua mpaka uwe rangi ya kahawia na hapo kitumbua kitakuwa kimeiva utakitoa. Rudia hatua hizo kwa vitumbua vyote vilivyobaki.

Jinsi ya kupika Magimbi Kwa Nyama Ya Ngโ€™ombe

Vipimo

Majimbi (Eddoes) kiasi 6 au 7

Nyama ngโ€™ombe ยฝ kilos

Tangawizi ilosagwa 1 kijiko cha kulia

Haldi (bizari manjano/turmeric) ยฝ kijiko cha chai

Tui zito la nazi vikombe 2

Chumvi kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Safisha nyama kisha weka chumvi, bizari ya manjano, tangawizi mbichi, ukaushe kwanza katika sufuria kwa kukaanga kaanga.
Ikianza kukauka, weka maji funika uchemshe iwive.
Menya majimbi ukate kate na uweke katika sufuria nyengine.
Mimina supu na nyama katika majimbi uchemshe yawive majimbi.
Mwisho weka tui zito la nazi uchanganye vizuri kisha weka katika moto kidogo tu bila kufunika yakiwa tayari.

Mapishi ya Biskuti Za Mayai

VIAMBAUPISHI

Unga 3 Vikombe

Sukari ya unga (icing sugar) 1 Kikombe

Siagi 250 gm

Mayai 3

Vanilla 2 Vijiko vya chai

Baking powder 1 Kijiko cha chai

JINSI YA KUPIKA

Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy).
Tia mayai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini.
Tia unga na baking powder changanya na mwiko.
Tengeneza round upange kwenye tray utie nukta ya rangi.
Nyunyuzia sukari juu ya hizo round ulizotengeneza kabla huja choma.
Pika (bake) katika oven moto wa 350ยฐF kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.

Jinsi ya Kujiandaa kwa Chakula cha Wiki Nzima cha Lishe Bora

Jinsi ya Kujiandaa kwa Chakula cha Wiki Nzima cha Lishe Bora ๐Ÿฅ—

Hakuna jambo bora kuliko kujihusisha na maisha yenye afya na lishe bora. Kwa wengi wetu, changamoto kubwa ni jinsi ya kujiandaa kwa chakula chetu cha wiki nzima ili tuweze kula vyakula vyenye virutubisho muhimu. Kama AckySHINE, mtaalamu wa lishe, ninafuraha kukushirikisha njia kadhaa ambazo unaweza kutumia kuandaa chakula chako cha wiki nzima cha lishe bora! ๐ŸŒฑ

Hapa kuna orodha yangu ya 15 ya hatua unazoweza kuchukua kufanikisha lengo hili:

  1. Tengeneza orodha ya ununuzi: Kupanga ni muhimu sana. Andika vyakula vyote unavyotaka kuwa nayo katika chakula chako cha wiki nzima. ๐Ÿ“

  2. Tafuta mapishi: Tafuta mapishi mbalimbali yanayokusisimua na yenye lishe bora. Kuna tovuti nyingi na programu za simu ambazo zinaweza kukusaidia kupata mapishi haya. ๐Ÿ“ฑ

  3. Nunua vyakula vyenye virutubisho muhimu: Nunua mboga mboga, matunda, nafaka na protini zenye lishe bora. Epuka vyakula vyenye sukari nyingi au mafuta mengi. ๐Ÿฅฆ๐Ÿ“

  4. Panga ratiba yako: Jijengee ratiba ya kushughulikia maandalizi ya chakula cha wiki nzima. Hii itakusaidia kuwa na mpango mzuri wa wakati na kufanya kazi yako vizuri. โฐ

  5. Fanya maandalizi ya kabla: Jitahidi kuandaa sehemu ya chakula chako kabla ya wiki kuanza. Kwa mfano, unaweza kuosha na kukata mboga mboga, na kuandaa mlo wa asubuhi kwa kuyaweka kwenye kontena. ๐Ÿ‘ฉโ€๐Ÿณ

  6. Pika mlo wa kwanza: Anza kwa kupika mlo wako wa kwanza wa wiki. Unaweza kuwa na chakula cha kiamsha kinywa, chakula cha mchana na chakula cha jioni tayari katika kontena au sahani zilizogawanyika kwa siku zote za wiki. ๐Ÿณ

  7. Tumia vyombo vya kuhifadhia: Vyombo vya plastiki au glasi vyenye sehemu tofauti vinaweza kukusaidia kuweka chakula chako salama na safi kwa muda mrefu. Hakikisha kuandika tarehe za kumaliza mlo wako kwenye vyombo hivyo. ๐Ÿฅฃ

  8. Fanya chakula kuwa kiburudisho: Hakikisha kuwa chakula chako cha wiki nzima kinakufurahisha. Jaribu mapishi mapya na ubunifu ili uweze kula vyakula tofauti kila siku. ๐Ÿฝ๏ธ

  9. Tumia vifaa vya kuongeza lishe: Kwa kuongeza lishe, unaweza kutumia viungo kama vile mbegu za chia, karanga, na tasty na vinywaji vya afya kama vile smoothies au matunda ya kuchoma. ๐ŸŒฐ๐Ÿฅค

  10. Hakikisha unakula kwa wingi: Ni muhimu kuhakikisha unapata mlo wa kutosha kwa siku nzima. Tenga sehemu yako ya kila mlo na kuzingatia uwiano sahihi wa protini, wanga na mafuta. ๐Ÿฝ๏ธ

  11. Panga vinywaji vyako: Hakikisha unakunywa maji ya kutosha kwa siku nzima. Weka chupa ya maji karibu nawe ili uweze kuinywa mara kwa mara. ๐Ÿšฐ

  12. Fikiria kuhusu uchumi: Kujiandaa kwa chakula cha wiki nzima kunaweza kukusaidia kuokoa pesa, kwani huwezi kutumia pesa nyingi kununua chakula nje. ๐Ÿช™

  13. Saidia familia na marafiki: Unaweza kuwahimiza familia na marafiki wako kujiunga na wewe katika kuandaa chakula cha wiki nzima. Inaweza kuwa ni jambo la kufurahisha na kuwapa motisha. ๐Ÿ‘จโ€๐Ÿ‘ฉโ€๐Ÿ‘งโ€๐Ÿ‘ฆ

  14. Uwepo wa akili: Kujiandaa kwa chakula cha wiki nzima kunahitaji subira na nidhamu. Kuwa na akili nzuri na uzingatia lengo lako. ๐Ÿ’ช

  15. Badilisha mapishi yako: Usiogope kubadilisha mapishi yako na kujaribu vitu vipya. Hii itakupa uzoefu mpya na kuongeza furaha yako ya kula chakula chako cha wiki nzima cha lishe bora. ๐ŸŒŸ

Kwa hivyo, kama AckySHINE, na mtaalamu wa lishe, ninaamini kuwa kujiandaa kwa chakula cha wiki nzima cha lishe bora ni njia nzuri ya kuboresha afya yako na kufurahia chakula chako kwa njia ya kipekee. Je, umeshawahi kujaribu kuandaa chakula chako cha wiki nzima? Je, unayo mbinu zako za kujiandaa? Nishirikishe mawazo yako katika sehemu ya maoni hapa chini! ๐Ÿ‘‡

Asante kwa kusoma, na kuwa na wiki njema ya lishe bora! ๐Ÿฅ—โœจ

Jinsi ya kupika Biskuti Za Tende Na Ufuta

Viambaupishi

Unga 3 Vikombe vya chai

Baking powder 1 ยฝ Vijiko vya chai

Sukari 1 Kikombe cha chai

Siagi 1 Kikombe cha chai

Mayai 2

Maji kiasi ya kuchanganyia

Tende 1 Kikombe

ufuta ยผ kikombe

Jinsi ya kuandaa na kupika

1. Changanya unga, siagi, baking powder, na sukari katika bakuli

2. Tia mayai, na maji kidogo uchanganye vizuri.

3. Sukuma kiasi kama unavyosukuma chapati duara kubwa.

4. Tandaza tende juu yake halafu kunja hadi mwisho.

5. Paka mayai juu yake halafu mwagia ufuta kisha kata kata vipande kama katika picha.

6. Vipange kwenye treya ya oveni kisha choma(bake)moto wa 350ยฐF kwa muda wa nusu saa takriban.

7. Ziepue katika moto naziache zipowe. Panga katika sahani.

Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Chumvi

VIAMBAUPISHI

Unga – 3 Vikombe vya chai

Siagi – 250 gms

Baking powder – 3 Vijiko vya chai

Mayai – 2

Chumvi – 1 kijiko cha chai

Maziwa – 1/2 Kikombe

Pilipili manga ya unga 1 Kijiko cha chai

MAANDALIZI

Katika bakuli la kusagia (blender) au mashine ya keki, tia siagi, chumvi na mayai, piga mpaka iwe kama malai (cream).
Tia Unga, baking powder, pilipili manga.
Tia maziwa.
Kata usanifu (design) unayotaka na sokota au kunja kwa usanifu unaopenda.
Pika (bake) katika moto wa 350ยบ C โ€“ usiviache vikawa rangu ya udongo (brown) sana.

Mapishi ya Dagaa wa nazi, nyanya chungu na bamia

Mahitaji

Dagaa waliokaushwa (dried anchovy 2 kikombe cha chai)
Bamia (okra 5)
Nyanya chungu (garden egg 5)
Tui la nazi (coconut milk 1 kikombe cha chai)
Nyanya (fresh tomato 2)
Kitunguu (onion 1)
Curry powder 1/2 ya kijiko cha chai
Turmeric powder 1/2 kijiko cha chai
Limao (lemon 1/2)
Chumvi (salt kiasi)
Pilipili (scotch bonnet 1)
Mafuta (veg oil)

Matayarisho

Safisha dagaa na uwaweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia dagaa wakaange kidogo kisha tia chumvi, pilipili, curry powder, turmeric, bamia na nyanya chungu, koroga vizuri mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri kisha tia nyanya na ufunike. Pika mpaka nyanya iive kisha kamulia limao,na pia hakikisha nyanya chungu na bamia zimeiva kidogo(usiache mpaka ziive sana manake zitavurugika pindi utakapotia tui la nazi) kisha malizia kwa kutia tui la nazi na uache lichemke mpaka rojo ibakie kidogo. Hakikisha nyanya chungu na bamia zimeiva ndo uipue. Na hapo dagaa wako watakuwa tayari kwa kuliwa na wali au ugali.

Mapishi ya Maini ya kuku

Mahitaji

Maini ya kuku 1/2 kilo
Vitunguu vikubwa 2
Hoho 1
Pilipil 1
Limao 1/2
Swaum/tangawizi 1 kijiko cha chai
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia

Matayarisho

Safisha maini weka pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu,swaum na tangawizi pamoja (hakikisha vitunguu visiwe vya brown), kisha tia maini, curry powder, pilipili, chumvi ,hoho na limao kisha changanya vizuri na ufunike. Pika mpaka maini yaive na hakikisha yanakuwa na rojo kidogo. Baada ya hapo ipua na yatakuwa tayari kwa kuliwa na chochote upendacho kama vile chapati, chips, ugali, wali.

Mapishi ya Ndizi Za Supu Ya Nyama Ya Ngโ€™ombe

Mahitaji

Ndizi – 15 takriiban

Nayma ya ngโ€™ombe – 1 kilo

Kitunguu maji – 1

Nyanya – 3

Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa – 1 kijiko cha supu

Tangawizi mbichi ilosagwa – 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi ilopondwa – 2

Jira/cummin/bizari ya pilau ilosagwa – 1 kijiko cha chai

Ndimu – 1

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Chemsha nyama kwa ndimu, chumvi na tangawizi mbichi na kitunguu thomu.
Menya ndizi na zikatekate vipande kiasi, weka katika sufuria.
Katakata kitunguu na nyanya utie katika ndizi.
Tia jira na chumvi.
Nyama ikiwiva mimina pamoja na supu yake ufunike ndizi ziwive na kuwa tayari kuliwa.
Ukipenda tia pilipili mbuzi zichemke pamoja na ndizi.

Mapishi ya Chapati za Kusukuma kitaalamu

Mahitaji

Unga wa ngano (plain flour 1/2 of kilo)
Siagi (butter vijiko 2 vya chakula)
Yai (egg 1)
Chumvi (1/2 ya kijiko cha chai)
Hiliki (ground cardamon 1/4 ya kijiko cha chai)
Maji ya uvuguvugu (warm water)
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Weka unga wa ngano katika bakuli la kukandia, kisha tia chumvi na hiliki na uchanganye kwanza, baada ya hapo tia siagi na uichanganye vizuri na unga mpaka ipotee. Baada ya hapo tia tena yai na uchanganye vizuri. Mchanganyiko ukishachanganyika vizuri sasa unaweza kutia maji ya uvuguvugu kidogo, kidogo huku ukiwa unauchanganya ili kupata donge. Baada ya hapo anza kukanda hilo donge mpaka mabuje yote yapotee na unga uwe mlaini, ambapo itakuchukua kama dakika 15. Baada ya hapo tawanyisha unga katika madonge ya wastani (yasiwe makubwa sana au madogo sana) Ukimaliza hapo, andaa kibao cha kusukumia chapati kwa kukitia unga kidogo ili chapati isinatie kwenye kibao. Sukuma donge moja la chapati mpaka liwe flat na kisha weka kijiko kimoja cha mafuta na usambaze. ukisha maliza ikunje (roll). Fanya hivyo kwa madonge yote yaliyobakia.
Baada ya hapo andaa chuma cha kuchomea (fry-pan) katika moto wa wastani. Kisha anza kusukuma chapati (ni vizuri ukaanza na zile ulizozikunja mwanzo ili kuzipa nafasi zile za mwisho ziweze kulainika) ukiwa unasukuma hakikisha zinakuwa flat (na zisiwe nene sana au nyembamba sana) Ukishamaliza hapo tia kwenye chuma cha kuchomea. Acha iive upande mmoja then igeuze upande wa pili. Tia mafuta ama kijiko kimoja kikubwa upande wa chini wa chapati na uanze kuukandamiza kwa juu uku ukiwa unaizungusha. fanya hivyo uku ukiwa unaigeuza kuiangalia kwa chini ili isiungue. ikishakuwa ya brown, geuza upande wa pili na urudie hivyohiyvo mpaka chapati iive. Rudia hii process kwa chapati zote zilizobakia.

Siri ya chapati kuwa laini ni kutia siagi au mafuta ya kutosha kipindi unazikanda na pia kuzikanda mpaka unga uwe laini.

Mapishi ya Wali, samaki wa nazi na kisamvu

Mahitaji

Mchele
Kisamvu kilichotwangwa
Samaki
Mbaazi
Nyanya chungu
Vitunguu
Nyanya ya kopo
Tangawizi
Kitunguu swaum
Vegetable oil
Curry powder
Tui la nazi (kopo 2)
Chumvi
Pilipili
Limao

Matayarisho

Safisha samaki kisha wamarineti na kitunguu swaum, tangawizi, pilipili, chumvi na limao kwa muda wa masaa 3.Baada ya hapo wakaange na usiwakaushe sana na uwaweke pembeni kwa ajili ya kuungwa.Katakata vitunguu maji, saga tangawizi na kitunguu swaum. Baada ya hapo injika sufuria ya mchuzi jikoni na mafuta kiasi ya kupikia, mafuta yakisha pata moto, tia vitunguu maji na vikaange mpaka viwe vya rangi ya brown. kisha tia kitunguu swaum na tangawizi.kaanga kidogo kisha tia nyanya ya kopo moja na ufunike. acha mpaka nyanya ziive. Kisha tia chumvi na curry powder na uache ikaangike kwa muda wa dakika 2 kisha tia samaki na nyanya chungu nakisha kamulia nusu ya limao. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia tui la nazi kopo moja na uache ichemke mpaka mchuzi uive.

Baada ya hapo chemsha kisamvu pamoja na mbaazi Kikisha iva, kaanga kitu na nyanya pembeni mpaka ziive kisha tia kisamvu. geuza mchanganyiko mpaka uchanganyike vizuri kisha tia tui la nazi na chumvi na aacha ichemke mpaka tui liive kisha ipua.malizia kwa kupika wali ambapo utachemsha maji kisha tia mafuta,chumvi na mchele na uupike mpaka uive kisha sevu na mboga ulizopika na mlo wako utakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Wali Wa Nazi Kwa Mchuzi Wa Samaki Na Rojo La Bilingani Na Viazi/Mbatata

Wali Wa Nazi

Mpunga – 4 vikombe

Tui la nazi – 6 vikombe

Chumvi – Kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mchele kisha
Bandika tui jikoni likichemka tia mchele na chumvi.
Funika uchemke, tui likikauka wacha moto mdogomdogo hadi wali uive ukiwa tayari. Ikiwa unatumia mkaa unapalia juu yake.

Mchuzi Wa Samaki Nguru

Samaki – 4

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi – 2 viijiko vya supu

Kitunguu maji kilokatwakawa – 2 slice ndogo

Nyanya/tungule – 4

Nyanya kopo – 3 vijiko vya supu

Pilipili mbichi – 2

Kotmiri ilokatwakatwa – 3 msongo (bunches)

Bizari ya mchuzi (simba 2) – I kijiko cha chai

Ndimu – 1 kamua

Mafuta – ยผ kikombe

Chumvi kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Katakata samaki mkaange kwa kumtia viungo.
Weka mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu. Vinapogeuka rangi thomu na tangawizi mbichi, nyanya, nyanya kopo, kitunguu na bizari ya mchuzi endelea kukaanga.
Tia maji kiasi na ndimu, pilipili mbichi ilosagwa kisha tia kotmiri.
Mwisho tia nusu ya samaki alokaangwa ukiwa tayari

Bilingani Za Kukaanga Na Viazi

Bilingani – 4 madogodogo

Viazi/mbatata – 3

Nyanya – 3

Majani ya mchuzi/mvuje/curry leaves – kiasi 6-7

Nnyanya kopo – 2 vijiko vya supu

Methi/uwatu ulosagwa – 1 kijiko cha chia

Rai/mustard seeds – 1 kijiko cha supu

Bizari ya manjano/haldi/turmeric – 1 kijiko cha chai

Chumvi – kiasi

Mafuta ya kukaangia – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1. Weka mafuta ya kukaangia katika karai

2. Katakakata bilingani vipande vipande vya mraba (cubes) kaanga katika mafuta ya moto hadi yageuke rangi. Eupa weka kando.

3. Katakataka viazi/mbatata vipande vidogodogo vya mraba (cubes) Kaanga hadi viive epua weka kando.

4. Ondosha mafuta yote katika karai bakisha kidogo tu kiasi ya vijiko 2 vya supu.

5. Kaanga rai kisha majani ya mchuzi, na methi/uwatu kisha kaanga nyanya.

6. Tia nyanya ya kopo kisha changanya pamoja bilingani na viazi ikiwa tayari.

Jinsi ya kupika mkate wa sembe

Mahitaji:

Unga sembe glass 1
Unga ngano glass 1
Sukari glass 1 (unaweza kupunguza kidogo)
Maziwa glass 1
Mafuta 1/2 glass
Mayai 4
Iliki iliosagwa 2tbs
Bp 2tbs

Jinsi ya kupika:

Saga sukari yako uweke kwenye bakuli safi pamoja na mayai. Tumia mashine ya cake kusagia hadi ifure/ivimbe.
Weka mafuta saga, weka maziwa saga, weka unga wa ngano na bp(bp imix kwenye unga kabla kumimina kwenye mchanganyiko) changanya vizuri halafu malizia kwa kuweka unga sembe na iliki usage vizuri.

Chukua trey au sufuria safi weka baking paper Mimina mchanganyiko wako na uoke.

Ukiwiva utoe na uwache upoe. Mkate wa sembe utakua tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Pasta za cream na uyoga

Mahitaji

Pasta (2 na 1/2 vikombe vya chai)
Uyoga (mashroom 2 vikombe vya chai)
Cream (1 kikombe cha chai)
Mafuta (vegetable oil)
Kitunguu (onion 1)
Chumvi
Majani ya basil (dried basil leaves 1/2 kijiko cha chai)

Matayarisho

Chemsha maji ya kutosha kisha tia chumvi na mafuta kidogo katika hayo maji na baadae tia pasta na uzichemshe mpaka ziive kisha uzichuje maji na uziweka pembeni. Baada ya hapo weka mafuta kidogo katika sufuria kisha tia uyoga uliokatwa na uupike mpaka uive. Baada ya hapo tia majani ya basil, chumvi na cream kisha acha ichemke kisha weka vitunguu na upike kwa muda wa dakika 4 kisha malizia kwa kutia pasta. Zichanganye vizuri na mchanganyiko wote kisha zipike kwa muda wa dakika 5. Na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Unaweza kupika nyama ya kuku (chiken breast) iliyokatwa vipande vidogo vidogo kama saizi na shape ya pasta. Vizuri kuikaanga pembeni mpaka iwe brown na kuiva alafu kuimix kwenye chakula baada ya uyoga na vitunguu kuiva alafu unamix cream kumalizia mapishi.

Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Tende Na Ufuta

MAHITAJI

Unga – 3 Vikombe vya chai

Baking powder – 1 ยฝ Vijiko vya chai

Sukari – 1 Kikombe cha chai

Siagi – 1 Kikombe cha chai

Mayai – 2

Maji – kiasi ya kuchanganyia

Tende – 1 Kikombe

ufuta – ยผkikombe

MAPISHI

  1. Changanya unga, siagi, baking powder, na sukari katika bakuli
  2. Tia mayai, na maji kidogo uchanganye vizuri.
  3. Sukuma kiasi kama unavyosukuma chapati duara kubwa.
  4. Tandaza tende juu yake halafu kunja hadi mwisho.
  5. Paka mayai juu yake halafu mwagia ufuta kisha kata kata vipande.
  6. Vipange kwenye treya ya oveni kisha choma(bake)moto wa 350ยฐF kwa muda wa nusu saa takriban.
  7. Ziepue katika moto naziache zipowe. Panga katika sahani.

Mapishi ya Kabichi

Mahitaji

Kabichi 1/2 kilo
Nyanya ya kopo 1/2
Kitunguu 1
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Chumvi
Olive oil

Matayarisho

Kwanza kabisa bandua magada ya juu ya kabichi, kisha ioshe na uikaushe maji baaba ya hapo katakata kabichi (inapendeza zaidi kama ikikatwa nyembamba) kisha saga pamoja nyanya na kitunguu. Baada yahapo tia katika sufuria ya kupikia, ipike mpaka maji yote yatakapokauka kisha tia chumvi, curry powder na mafuta pika kwa muda kiasi kisha tia kabichi na upunguze moto. Pika mpaka kabishi itakapoiva kisha ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila kwa wali au ugali.

Jinsi ya kupika Wali Wa Sosi Ya Tuna

Viambaupishi

Sosi Ya tuna

Tuna (samaki/jodari) 2 Vikopo

Vitunguu (kata kata) 4

Nyanya zilizosagwa 5

Nyanya kopo 3 Vijiko vya supu

Viazi (vilivyokatwa vipande vidogo – cubes) 4

Dengu (chick peas) 1 kikombe

Kitunguu saumu(thomu/galic)&Tangawizi iliyosagwa 1 Kijiko cha supu

Hiliki 1/4 kijiko cha chai

Mchanganyiko wa bizari 1 kijiko cha supu

Chumvi kiasi

Pilipili manga 1 Kijiko cha chai

Vipande cha Maggi (Cube) 2

Wali

Mchele 3 Vikombe vikubwa (Mugs)

Mdalasini 2 Vijiti

Karafuu chembe 5

Zaafarani kiasi

*Jirsh (Komamanga kavu au zabibu kavu -raisins) 1/2 Kikombe

Jinsi ya kuandaa na kupika

1. Kosha Mchele na roweka.

2. Kaanga vitunguu hadi viwe rangi ya hudhurungi (brown) chuja mafuta uweke kando.

3. Kaanga viazi, epua

4. Punguza mafuta, kaanga nyanya.

5. Tia thomu/tangawizi, bizari zote, vipande vya Maggi, nyanya kopo, chumvi.

6. Mwaga maji ya tuna iwe kavu, changanyisha kwenye sosi.

7. Tia zaafarani kidogo katika sosi na bakisha ya wali.

8. Chemsha mchele pamoja na mdalasini na karafuu.

9. Karibu na kuwiva, chuja maji utie katika chombo cha kupikia katika jiko (oven)

10. Nyunyizia zaafarani, mwagia vitunguu, viazi, na dengu juu ya wali.

11. Mwagia sosi ya tuna na pambia jirshi (au zabibu).

12. Funika wali na upike katika jiko moto wa 450ยบ kwa muda wa kupikika wali.

* Jirsh (komamanga) kavu zioshwe vizuri kutoa vumbi au tumia zabibu kavu (raisins)

Jinsi ya Kupika skonzi

Mahitaji

Unga wa ngano (self risen flour 2 vikombe vya chai)
Sukari (sugar 1/2 kijiko cha chakula)
Chumvi (salt 1/2 kijiko cha chai)
Hamira (yeast 1/2 kijiko cha chakula)
Baking powder 1/2 kijiko cha chai
Siagi (butter 1/4 ya kikombe cha chai)
Maziwa (fresh milk 3/4 ya kikombe cha chai)(unaweza kutumia maji badala ya maziwa)

Matayarisho

Pasha maziwa yawe ya uvuguvugu kisha weka pembeni, pia yeyusha siagi na uweke pembeni.Baada ya hapo tia kila kitu kwenye bakuli la kukandia kasoro maziwa, na uchanganye vizuri kisha tia maziwa kidogo kidogo katika mchanganyiko huo kisha ukande. Ukimaliza uweke kwenye sehemu ya joto na uache uumuke. Ukisha umuka utawanyishe katika madonge saba Kisha .pakaza mafuta au siagi katika chombo cha kuokea kisha yapange hayo madonge katika hicho chombo na uyaache yaumuke tena (kwa mara ya pili). Baada ya hapo pakaza mafuta juu ya hayo madonge na uyaoke (bake) katika oven (moto 200ยฐC ) kwa muda wa dakika 25 na hapo scones au maskonzi yatakuwa tayari

Mapishi ya Wali Wa Zaafarani Na Kuku Wa Kupaka

Vipimo

Wali:

Mchele – 3 Vikombe

Kitunguu kiichokatwa – 1

Pilipili boga nyekundu iliyokatwa vipande – 1

Mafuta – ยผ Kikombe

Zaafarani – 1 kijiko cha chai tia kwenye kikombe na maji robo roweka

Chumvi – 1 kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Katika sufuria, tia mafuta, kaanga kitunguu mpaka kiwe kidogo rangu ya udongo (brown)
Tia pili pili boga.
Tia mchele, kaanga kwa muda wa dakika 3, tia zaafarani na chumvi.
Tia supu uliyochemshia kuku iwe imoto.
Pika wali katika moto mdogo hadi uwive.

Kuku

Kuku Mzima -1

Mayai ya kuchemsha – 6

Namna Ya Kupika Kuku

Mchemshe kuku mzima na chumvi mpaka uhakikishe ameiva vizuri.
Mtowe na muweke pembeni. Supu yake tumia katika wali kama ilivyo hapo juuu.
Chemsha mayai, menya na kata vipande viwili kila yai moja weka kando

Vipimo Vya Sosi Ya Kuku Ya Nazi

Kitunguu – 1

Nyanya iliyokatwa vipande – 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi – 1 kijiko cha supu

Garam Masala – ยฝ kijiko cha supu

Bizari ya manjano – ยฝ kijiko cha chai

Chumvi – kiasi

Pilipili masala ya unga – ยฝ kijiko cha chai

Nyanya ya kopo – 1 kijiko cha supu

Nazi ya unga – 1 kikombe

Maji ya ukwaju – ยผ kikombe cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Tia Mafuta vijiko 2 vya supu katika sufuria
Kaanga kitunguu maji mpaka kiwe rangi ya udongo (brown).
Tia thomu na tangawizi.
Tia nyanya nzima iliyokatwa katwa.
Tia garam masala, manjano, pilipili ya unga, nyanya ya kopo, kaanga vizuri.
Changanya kwenye sufuria na ukwaju. Iache ichemke vizuri.
Changanya nazi ya unga na maji vikombe viwili.
Mtie kuku mpike vizuri na hilo tui.
Mtie kwenye oveni kidogo.

Kupakuwa katika Sinia

Pakuwa wali kwanza katika sinia
Muweke kuku juu ya wali.
Pambia mayai

Mapishi ya Ugali, dagaa (wabichi) na matembele

Mahitaji

Dagaa wabichi (Fresh anchovies packet 1)
Unga wa ugali (corn meal flour 1/4 kilo) (unaweza kutumia unga wa choice uipendayo)
Matembele ya kukaushwa (dried sweet potato leaves, handful)
Nyanya ya kopo (tin tomato 1)
Kitunguu maji (onion 2)
Limao (lemon 1/4)
Pilipili mbuzi nzima bila kukata (scotch bonnet pepper1, do not chop)
Chumvi (salt 1/2 ya kijiko cha chai)
Mafuta (vegetable oil)
Hoho (green pepper 1)
Kitunguu swaum (garlic 5 cloves)
Tangawizi (ginger 1 kijiko cha chai)
Binzari ya curry (Curry powder 1/2 kijiko cha chai)

Matayarisho

Safisha dagaa kwa kutoa vichwa na utumbo kisha waoshe na uwakaushe na kitchen towel na uwaweke pembeni. Baada ya hapo katakata, vitunguu na hoho kisha weka pembeni. Baada ya hapo weka sufuria jikoni na utie mafuta yakisha pata moto tia dagaa na uwakaange mpaka wawe wa brown, kisha tia kitunguu swaum,curry powder na tangawizi, kaanga kidogo kisha malizia kwa kutia vitunguu maji, hoho,pilipili,chumvi na ukamulie limao. Kaanga kwa muda wa dakika 3-4 na hakikisha vitunguu na hoho haviivi sana na hapo dagaa watakuwa tayari.

Baada ya hapo yaoshe na uyaloweka matembele (kama ni makavu) kwa muda wa dakika 15, Kisha yatoe na uyaweke kwenye sufuria pamoja na kitunguu, nyanya, chumvi ,kamulia limao kidogo, pilipili na maji kiasi. acha matembele yachemke kwa muda wa dakika 20 na uhakikishe yameiva kwa kuwa laini. Baada ya hapo yapike mpaka maji yote yakauke na mafuta yatok na hapo matembele yatakuwa tayari.

Ukisha maliza kupika dagaa na matembele andaa chungu cha ugali. Kwanza unatakiwa kuchemsha maji ya moto, kisha koroga pembeni unga kiasi katika maji ya baridi na utie kwenye maji yanayochemka, Fanya kama unatengeneza uji, uji wa ugali ukishachemka tia unga na uanze kuusonga mpaka ugali uive. Ukisha iva pakua na usevu na mboga tayari kwa kuliwa.

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About