Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya

Mapishi ya mboga mchanganyiko

Mahitaji

Viazi ulaya 4 vya wastani
Hoho jekundu 1/2
Hoho la njano 1/2
Hoho la kiajani 1/2
Njegere 1 kikombe cha chai
Carrot 1 kubwa
Broccoli kidogo
Cauliflower kidogo
Kitunguu 1
Nyanya 1/2 kopo
Swaum/tangawizi 1 kijiko cha chakula
Curry power 1 kijiko cha chakula
Coriander powder 1 kijiko cha chai
Tarmaric 1/2 kijiko cha chai
Olive oil
Chumvi
1/4 ya limao

Matayarisho

Katika sufuria isiyoshika chini kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia swaum/tangawizi na spice zote kaanga kwa muda mfupi kisha tia nyanya na chumvi. pika mpaka nyanya ziive kisha tia vegetable zote na vimaji kidogo sana na kisha kamulia limao, baada ya hapo punguza moto na kisha funika na zipike mpaka vegetable zote ziive na rojo ibakie kidogo. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kuandaa Ndizi Mbichi Za Supu Ya Nyama Ng’ombe

Mahitaji

Ndizi mbichi – Kisia

Nyama ng’ombe – ½ kilo

Pilipili ya kusaga – 1 kijiko cha chai

Tangawizi ya kusaga – 2 vijiko vya supu

Thomu (garlic/saumu) – 1 kijiko cha supu

Bizari mchuzi – 1 kijiko cha chai

Nazi ya unga (ukipenda kuongezea) – 2 vijiko cha supu

Chumvi – Kiasi

Ndimu – 1 kamua

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Weka nyama ng’ombe katika sufuria, tia tangawizi, thomu, pilipili mbichi, bizari, chumvi. Roweka kidogo ukipenda kisha ikaushe yenyewe kwa maji yake
Ongezea maji ya kiasi yasizidi mno, kisha funika na chemsha.
Menya ndizi, ukatekate.
Nyama ikikaribia kuiva, weka ndizi uendelee kupika mpaka viive vyote.
Tia nazi ya unga kidogo tu ukipenda. Koleza kwa bizari mchuzi, pilipili, na ndimu
Epua mimina katika chombo cha kupakulia zikiwa tayari.

Jinsi ya kupika Eggchop

Mahitaji

Mayai yaliochemshwa 4
Nyama ya kusaga robo kilo
Kitunguu swaum
Tangawizi
Limao
Chumvi
Pilipili
Breadcrambs
Carry powder
Binzari nyembamba ya unga
Yai moja bichi
Mafuta

Matayarisho

Marinate nyama na pilipili, kitunguu swaum, tangawizi, limao, chumvi, carry powder, binzari nyembamba na breadcrambs pamoja. Kisha vunja yai moja bichi kwenye kibakuli na ulikoroge kisha tia kwenye mchanganyiko wa nyama.Gawanisha matonge manne kwa ajili ya kuzungushia kwenye mayai .Chemsha mayai kwa muda wa dakika 20. Yakisha iva acha yapoe na kisha yamenye maganda na uyaweke pembeni. Baada ya hapo chukua yai moja lililochemshwa na ulizungushie donge moja la mchanganyiko wa nyama. fanya hivyo kwa mayai yote yaliobakia. Baada ya hapo paka mafuta kwa nje ya hizo eggchop na kisha paka mafuta kwenye sinia la kuokea na uziokee kwenye oven kwa moto wa kawaida, kwa muda wa dakika 20.Na eggchop zako zitakuwa tayari kwa kuliwa

Mapishi ya Viazi vya nyama

Mahitaji

Viazi (potato) 1 kilo
Nyama ya ng’ombe 1/2 kilo
Nyanya ya kopo iliyosagwa 1/2 tin
Vitunguu maji 2
Tangawizi/ swaum 1 kijiko cha chai
Hoho 1
Curry powder 1 kijiko cha chai
Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/2
Chumvi
Coriander
Mafuta ya kupikia

Matayarisho

Safisha na katakata nyama ktk vipande vidogovidogo kisha weka pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia nyama, swaum/ tangawizi, chumvi na limao. Ichanganye vizuri kisha funika na uipike mpaka iive na maji yote yakauke yani yabaki mafuta tu. Baada ya hapo tia viazi vilivyokatwa vipande vya wastani vikaange kwa muda wa dakika 10 kisha tia pilipili na curry powder na nyanya. Funika na punguza moto.Pika mpaka nyanya iive vigeuze kisha tia vimaji kidogo vya kuivishia viazi. Viazi vikikaribia kuiva(hakikisha vinabaki na rojo kidogo) tia hoho na upike kwa muda wa dk 5 kisha malizia kwa kutia coriander. Changanya vizuri kisha ipua na viazi vyako vitakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kutengeneza biskuti za Matunda Makavu Na Cornflakes

VIAMBAUPISHI

Unga – 4 Vikombe

Sukari – 1 Kikombe

Baking powder 1 kijiko cha chai mfuto

Siagi – 454 gms

Mayai – 2

Matunda makavu (tende, zabibu, lozi) – 1 Kikombe

Vanilla – 2 Vijiko vya chai

Cornflakes – ½ kikombe

JINSI YA KUANDAA

Changanya sukari na siagi katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy)
Tia yai moja moja huku unachanganya mpaka iwe laini kama sufi. (fluffy)
Tia unga, baking powder, matunda makavu, changanya na mwiko.
Chota mchanganyiko wa biskuti kwa mkono kama (kiasi cha kijiko kimoja cha supu) fanya duara na uchovye katika cornflakes iliyopondwa kwa mkono (crushed)
Zipange katika treya ya kupikia na zipike (bake) katika moto wa 375°F kwa muda wa kiasi dakika 15 huku unazitazama tazama.

Jinsi ya kupika Pilau ya Mpunga Na Nyama Ya Ng’ombe

Mahitaji

Mpunga – 4 vikombe

Nyama – 1 kilo moja

Kitunguu maji – 3

Mbatata/viazi – 7 vidogodogo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa 3 vijiko cha supu

Bizari nzima/ya pilau/uzile/cumin – 3 vijiko vya supu

Mdalasini – 3 vipande

Hiliki – 7 punje

Pilipili manga nzima – 1 kijiko cha supu

Chumvi kiasi

Mafuta – ½ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mchele weka kando
Katakataka vitunguu slice ndogo ndogo.
Weka mafuta katika sufuria kisha ukaange vitunguu pamoja na mdalasini, hiliki pilipilimanga.
Vitunguu vikigeuka rangi unatia kitunguu thomu na tangawizi.
Tia supu kidogo na nyama, kisha tia bizari ya pilau/uzile, na viazi/mbatata.
Maliza kutia supu yote, na ikiwa ni kidogo ongeze maji kiasi cha kuivisha mchele. kisha tia mchele ufunike hadi wali uwe tayari.
Ikiwa unatumia mkaa palia juu yake, ikiwa hutumii uache uive kwa moto mdogo mdogo.

Mawazo ya Chakula cha Usiku cha Dakika 20 kwa Familia Yote

Mawazo ya Chakula cha Usiku cha Dakika 20 kwa Familia Yote 🌮🍝🍗

Kama AckySHINE, leo nataka kushiriki mawazo ya chakula cha usiku ambayo yanaweza kuandaliwa kwa haraka na kwa urahisi katika dakika 20 tu! Nimepata maswali mengi kutoka kwa watu ambao wanahitaji chakula cha jioni kinachoweza kupikwa haraka, lakini bado ni kitamu na kinachofurahisha kwa familia nzima. Hivyo, leo nitaenda kupendekeza chaguzi kadhaa ambazo naamini zitakufurahisha na familia yako.

  1. Tacos za Kuku 🌮
    Tacos za kuku ni chaguo bora kwa chakula cha jioni cha haraka. Unaweza kuandaa kuku wa kusaga, kuongeza viungo vya ladha kama vile pilipili, chumvi, tangawizi na vitunguu. Kisha, unaweza kuchoma kuku huyo na kuweka katika taco, na kuongeza nyanya, avokado, na jibini. Bila shaka, usisahau kuongeza limao kwa ladha ya ziada!

  2. Pasta ya Kuku na Mchuzi wa Krimu 🍝
    Pasta ni chakula rahisi cha jioni ambacho kina ladha kubwa na familia yote. Kwa mfano, unaweza kuandaa pasta ya kuku na mchuzi wa krimu. Chukua kuku uliyomaliza na kuongeza vitunguu, kitunguu saumu, pilipili, na tangawizi. Kisha, unaweza kuongeza mchuzi wa krimu na kuweka pasta ambayo tayari imepikwa. Hakika familia yako itafurahia ladha hii ya kitamu!

  3. Vitumbua vya Kuku 🍗
    Vitumbua vya kuku ni chaguo jingine la haraka na rahisi la chakula cha usiku ambalo linaweza kuandaliwa katika dakika 20 tu. Unaweza kuandaa kuku wa kusaga na kuongeza viungo kama vile vitunguu, pilipili, chumvi, na tangawizi. Kisha, unaweza kutengeneza vitumbua na kuchoma kwenye sufuria. Ikiwa una watoto, unaweza kuwauliza wakusaidie kufanya vitumbua hivi, hata watafurahi kushiriki katika mchakato wa kupika!

  4. Pizza ya Familia 🍕
    Pizza ni chakula maarufu cha jioni kinachopendwa na watu wengi. Kwa nini usijaribu kuandaa pizza ya familia yako mwenyewe? Unaweza kununua mizinga ya pizza tayari kutoka dukani na kuongeza toppings unazopenda. Kwa mfano, unaweza kuongeza jibini, nyama ya nguruwe, pilipili, na vitunguu. Basi, weka pizza kwenye oveni na uipike hadi iwe dhahabu na crispy. Familia yako itafurahi kula pizza ambayo wamelihusisha katika mchakato wa kupika!

  5. Saladi ya Kuku 🥗
    Saladi ni chakula kingine cha jioni ambacho kinaweza kuandaliwa haraka na kwa urahisi. Unaweza kuanza kwa kuchemsha kuku na kisha kukiharibu vipande. Kisha, unaweza kuongeza mboga mboga kama nyanya, pilipili, vitunguu, na karoti. Kisha, unaweza kuongeza vijiko vichache vya mchuzi wa saladi kama vile mafuta ya mizeituni na asali. Hakika familia yako itafurahi kula saladi yenye afya na kitamu!

Nimepata furaha kushiriki mawazo haya ya chakula cha usiku cha dakika 20 kwa familia yote. Kuna chaguzi nyingi za chakula ambazo zinaweza kuandaliwa kwa haraka na bado zina ladha nzuri na ya kuridhisha. Kwa mfano, tacos za kuku, pasta ya kuku na mchuzi wa krimu, vitumbua vya kuku, pizza ya familia, na saladi ya kuku. Chagua moja ambayo inakuvutia zaidi na ujifurahishe na familia yako katika chakula cha jioni cha dakika 20!

Je, una mawazo mengine ya chakula cha usiku cha haraka kwa familia yote? Tafadhali nishirikishe katika sehemu ya maoni hapa chini! ✨🍽️

Mapishi ya Mchuzi wa kambale

Mahitaji

Kambale 2
Nazi kopo 1
Nyanya kopo 1
Vitunguu 2
Curry powder 1 kijiko cha chai
Turmaric 1/2 kijiko cha chai
Binzari nyembamba ya unga 1/2 kijiko cha chai
Swaum/ tangawizi 1 kijiko cha chakula
Giligilani kiasi
Limao 1/2
Chumvi
Olive oil

Matayarisho

Loweka samaki katika maji ya moto kwa muda wa muda wa nusu saa.Baada ya hapo Saga pamoja nyanya, vitunguu, swaum na tangawizi kisha vibandike jikoni na uvipike mpaka maji yote yakauke kisha tia mafuta. Pika mpaka nyanya zitengane na mafuta kisha tia spice zote.Zipike kwa muda mdogo kisha tia tui la nazi, maji kiasi, samaki, pilipili nzima, chumvi na kamulia limao. Pika mpaka tui la nazi litakapoiva na samaki pia wawe wameiva na mchuzi ubakie kiasi. Baada ya hapo ipua kisha tia giligilani iliyokatwa na mchuzi utakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuulia kwa chochote kile upendacho. Mi hupendaga kuulia na ugali mlaiiini au na wali pia.

Jinsi ya kupika Visheti Vyeupe Na Vya Kaukau

VIPIMO:

Unga wa Visheti

Unga 4 Vikombe vya chai

Siagi 1 Kikombe cha chai

Hiliki ½ Kijiko cha chai

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1. Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi na hiliki.

2. Changanya vizuri isiwe na madonge.

3. Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu.

4. Halafu utakata sampuli unayopenda mwenyewe.

5. Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. .

6. Ukipenda gawa visheti sehemu mbili, na shira pia igawe sehemu mbili

7. Changanya nusu ya visheti kwa shira nyeupe.

8. Nusu ya shira nyingine ibandike tena motoni na tia cocoa vijiko viwili vidogo vya chai. Inapochanganyika cocoa vizuri changanya nusu ya visheti ulivyogawa kupata visheti vya shira ya cocoa.

Shira:

Sukari 2 Vikombe vya chai

Maji 1 Kikombe cha chai

Vanilla ½ Kijiko cha chai

(cocoa ukipenda kugawa visheti aina mbili) 2 Vijiko vya chai.

Jinsi ya kutengeneza Biriani Ya Nyama Ya Ng’ombe

Mahitaji

Nyama – 2 Ratili (LB)

Chumvi – kiasi

Mafuta – 1 Kikombe

Samli – ½ Kikombe

Kitungu (Kata virefu virefu) – 3 Vikubwa

Nyanya (kata vipande) – 2

Nyanya kopo – 1 Kijiko cha chakula

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 1 Kijiko cha chakula

Tangawazi – 1 Kijiko cha chakula

Pilipili mbichi iliyosagwa – 1 Kijiko cha chai

Pilipili ya unga nyekundu – ½ Kijiko cha chai

Kotmiri iliyokatwa – 2 Vijiko vya chakula

Viazi – 6

Gram masala – 1 Kijiko cha chai

Mtindi – ¼ Kikombe cha chai

Namna Ya kutaarisha Na Kupika

1. Kwenya karai au (sufuria) mimina mafuta na samli. Yakishapata moto mimina vitunguu vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi. Vitowe viweke pembeni.
2. Kaanga viazi na viweke pembeni.
3. Chukua sufuria tia nyama, thomu, tangawizi, pilipili, nyanya, nyanya ya kopo, mtindi, na pilipili ya unga. Chemsha mpaka iive.
4. Tia vile vitungu ulioyovikaanga, tia viazi, gram masala, kotmiri na yale mafuta uliokaangia vitunguu kama ¼ kikombe, acha moto mdogo mdogo kama ¼ saa, epua weka pembeni.

Vipimo Vya Wali

Mchele – 5 Magi (Kikombe kikubwa)
Hiliki nzima – 4
Mdalasini mzima – 1
Zafarani – ½ kijiko cha chai
Rangi ya biriani – ¼ Kijiko cha
Mafuta yaliyokaangiwa vitunguu – ½ Kikombe
Chumvi – kiasi
Roweka zafarani na rangi kwenye kikombe na ¼ kikombe cha maji. Roweka kabla ya robo saa.

Namna Ya Kutaarisha

Osha mchele uroweke kwenye maji muda wa dakika 20.
Chemsha maji kwenye sufuria kama magi 10.
Tia hiliki na mdalasini.
Yakishachemka unatia mchele,chemsha usiive sana, unamwaga maji.
Unamimina tena ule mchele ½ yake kwenye sufuria, unatia rangi na zafrani kidogo, halafu unamimina
mchele uliyobakia unatia rangi iliyobakia.
Mafuta yake unayachemsha mpaka yachemke unamimina juu ya mchele, unarudisha motoni unaweka
moto mdogo ukisha kuiva, tayari kupakuliwa.
Unapakuwa wali unaweka chini kwenye sahani na juu yake sosi ya nyama

Mapishi ya Pilau Ya Nyama Na Mtindi

MAHITAJI

Nyama iliyokatwa vipande – 1 Ratili(LB)

Mchele Basmati – 2 Magi

Chumvi ya wali – kiasi

Kitungu kilichokatwa katwa – 1 kikubwa

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi – 1 kijiko cha supu

Mtindi (yogurt) – ½ kikombe

Mchanganyiko wa bizari ya pilau ya tayari – 2 vijiko vya supu

Mafuta kidogo yakukaangia

Rangi ya manjano (ukipenda)

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Osha mchele na roweka nusu saa .

Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi (brown).

Tia thomu na tangawizi na ukaange kidogo.

Kisha weka bizari ya pilau halafu nyama huku unakaanga hadi nyama isiwe nyekundu tena.

Tia maji gilasi 1½- 2 ichemke mpaka nyama iwive na karibu kukauka.

Mimina mtindi na iachie moto mdogo ikauke kidogo.

Kwenye sufuria nyingine chemsha mchele pamoja na chumvi na mafuta kidogo mpaka uive.

Mimina wali juu ya nyama, kisha nyunyiza rangi (ukipenda) kama vile wali wa biriani na ufunike kwa dakika kumi hivi.

Changanya wali na nyama pamoja ikiwa tayari kuliwa.

Mapishi ya Ugali Kwa Mchuzi Wa Samaki Wa Kuchoma

Vipimo Vya Ugali

Unga wa mahindi – 4 vikombe

Maji – 6 kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Tia maji kiasi katika sufuria wacha yachemke hasa

Tia unga kidogo kidogo huku ukikoroga mpaka ukamatane

Punguza moto huku ukiendelea kuusonga

Endelea kusonga kwa dakika kadhaa mpaka uanze kuchambuka

Kisha mimina kwenye bakuli au sahani na itakuwa tayari

Vipimo Ya Upishi Wa Mchuzi Wa Samaki Wa Kuchoma Wa Nazi

Samaki:

Samaki wa Nguru – kiasi vipande 5 – 6

Pilipili mbichi – 3

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 5 chembe

Tangawizi mbichi – 1 kipande

Bizari ya samaki – 1 kijiko cha supu

Pilipili nyekundu ya unga – 1 kijiko cha chai

Ndimu – 3 kamua

Chumvi – kiasi

Ukipenda mkate samaki vipande kiasi.
Saga vipimo vyote vinginevyo katika mashine. Mchanganyiko ukiwa mzito ongezea ndimu
Changanya pamoja na samaki upake vizuri vipande vya samaki
Acha kwa muda wa nusu saa vikolee mchanganyiko
Panga samaki katika treya ya kupikia ndani ya oveni, kisha mchome (grill) samaki huku ukigeuza hadi viwive.
Epua weka kando.

Kuandaa Mchuzi:

Nyanya/tungule – 3

Kitunguu – 2

Bizari ya manjano/haldi – ¼ kijiko cha chai

Mafuta – 3 vijiko vya supu

Tui la nazi zito – 3 vikombe

Chumvi – kiasi

Katakata vitunguu na nyanya vidogodogo (chopped) weka kando

Weka mafuta katika karai au sufuria, kaanga vitunguu hadi vianze kugeuka rangi

Tia nyanya kaanga pamoja na tia bizari ya njano/haldi .

Tia tui la nazi, chumvi koroga .

Mwishowe tia vipande vya samaki na rojo lake litakalobakia katika treya, mchuzi uko tayari

Mapishi ya Kabichi

Mahitaji

Kabichi 1/2 kilo
Nyanya ya kopo 1/2
Kitunguu 1
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Chumvi
Olive oil

Matayarisho

Kwanza kabisa bandua magada ya juu ya kabichi, kisha ioshe na uikaushe maji baaba ya hapo katakata kabichi (inapendeza zaidi kama ikikatwa nyembamba) kisha saga pamoja nyanya na kitunguu. Baada yahapo tia katika sufuria ya kupikia, ipike mpaka maji yote yatakapokauka kisha tia chumvi, curry powder na mafuta pika kwa muda kiasi kisha tia kabichi na upunguze moto. Pika mpaka kabishi itakapoiva kisha ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila kwa wali au ugali.

Jinsi ya kutengeneza Mkate wa mayai

Mahitaji

Slice za mkate 6
Mayai 3
Chumvi
Olive oil

Matayarisho

Vunja mayai yote katika sahani kisha tia chumvi kidogo sana na uyapige mpaka chumvi ichanganyike. Kisha chukua frying pan na utie vimafuta kidogo na uweke jikoni. Mafuta yakishapata moto kiasi,chovya slice za mkate katika hayo mayai na uzipike pande zote zikishaiva zitoe na uziweke katika kitchen towel ili kukausha mafuta.Na baada ya hapo mikate yako itakuwa tayari kwa kuliwa na chai.

Mapishi ya Mlenda wa bamia na nyanya chungu

Mahitaji

Bamia (okra) 20
Nyanya chungu (garden eggs) 5
Magadi soda (Bicabonate soda) 1/4 ya kijiko cha chai
Nyanya (fresh tomato) 1
Chumvi (salt) kidogo
Pilipili 1/4

Matayarisho

Osha bamia, nyanya chungu na nyanya kisha vikatekate katika vipande vidogovidogo. Baada ya hapo vitie kwenye sufuria na vitu vyote vilivyobakia na kisha tia maji kidogo.Chemsha mpaka bamia na nyanya chungu ziive na vimaji vibakie kidogo sana. Baada ya hapo ziponde na mwiko kidogo kisha zikoroge na uipue na mlenda utakuwa tayari kwa kuliwa na ugali.

Mapishi ya Pilau Ya Samaki Wa Tuna Na Mboga

Mahitaji

Mchele – 2 Mugs

Mboga mchanganyiko za barafu (Frozen veg) – Mug

Tuna (samaki/jodari) – 2 kopo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi -2 vijiko vya supu

Garam masala – 1 kijiko cha supu

Nyanya – 2

Kitungu maji – 1

Mdalasini nzima – 2 vijiti

Karafuu – 6 chembe

Pilipili mbichi – 1

Chumvi – kiasi

Viazi – 3

Maji – 2 ½ Mugs

Mafuta – 3 vijiko vya supu

Maandalizi

Osha mchele na uroweke kwa muda wa dakika 20
Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
Mimina viazi, thomu na tangawizi, bizari zote na kaanga.
Tia nyanya uliyokatakata ikaange mpaka iwive.
Tia tuna endelea kukaanga kidogo tu.
Tia maji, yatakapochemka tia mchele.
Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa ½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.

Jinsi ya kutengeneza Nangatai

MAHITAJI

Unga wa ngano – 2 – 2 ¼ Vikombe

Siagi – 1 ½ Kikombe

Sukari – 1 Kikombe

Yai – 1

Vanilla -Tone moja

Baking Powder -kijiko 1 cha chai

Chumvi – Kiasi kidogo (pinch)

Unga wa Kastadi – 2 Vijiko vya supu

MATAYARISHO

Changanya vitu vyote isipokuwa unga.
Tia unga kidogo kidogo mpaka mchanganyiko uwe sawa.
Kisha fanya duara ndogo ndogo uzipange kwenye treya na utie rangi katikati.
Halafu zichome katika moto wa 300°F kwa muda wa dakika 20 – 25 na zisiwe browni .
Kisha panga kwenye sahani tayari kuliwa na chai.

Jinsi ya kupika kisamvu bila nazi

Kisamvu ni aina ya mboga ya majani inayopatikana kwa wingi na kwa urahisi katika mikoa takriban yote nchini Tanzania.
Pia aina hii ya mboga hupikwa katika mapishi ya aina mbalimbali kulingana na mahitaji ya mpishi.

Aina hii ya mboga kama zilivyo mboga zingine za majani ni nzuri na muhimu kwa afya ya binadamu. Aina hii ya mboga huleta virutubisho mbalimbali mwilini.
Hapa tunaenda kuona mapishi ya kisamvu kwa kutumia mafuta bila nazi kama ilivyozoeleka na wengi.

Mahitaji :

• Kisamvu kilichotwangwa na kuwa laini
• Kitunguu maji
• Kitunguu swaumu
• Kunde mbichi
• carrots
• Mafuta ya kula
• Chumvi kiasi

Maandalizi :

• Chemsha kisamvu ukiwa umechanganya na kunde mpaka uhakikishe vyote vimeiva. Baada ya kuiva weak pembeni.
• Chukua sufuria kavu, weak mafuta kasha weak katika jiko na yakipata moto weak kitunguu na koroga mpaka kibadilike rangi kasha weak kitunguu swaumu na endelea kukoroga kwa muda baada ya hapo weak carrots na kisha weka kisamvu chako ambacho kimechanganywana kunde.
• Endelea kukoroga kwa muda na kasha acha kichemke mpaka uhakikishe mboga yako imeiva vizuri.
• Mboga hii iko tayari kwa kulikwa na inaweza ikaliwa na wali au ugali.

Jinsi ya kutengeneza Bisikuti Za Kaukau Na Kahawa (Cocoa Coffee Biscuits)

MAHITAJI

Maji baridi – kikombe 1

Biskuti za kawaida – paketi 2

Kaukau (cocoa) – vijiko 3 vya kulia

Kahawa ya unga – kijiko 1 cha kulia

Njugu mchanganyiko zilokatwakatwa – kikombe 1

Sukari – kiasi upendavyo

MAANDALIZI

Changanya maji na kaukau na kofi na sukari
Katakata biskuti kisha tia paketi moja na nusu uchanganye vizuri.
Kisha nusu ya biskuti zilobakia katakata vipande vikubwa na weka juu ya mchanganyiko, kisha changanya kidogo tu.
Weka katika foil paper na zungusha (roll)
Kisha fungua umwagie njugu au mkassaraat zilosagwa
Kisha roll katika foil paper na uweke katika freezer mpaka igande
Kisha kata kata slices na iko tayari

Shopping Cart
2
    2
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About