Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya

Mapishi ya Biriani Ya Tuna

MAHITAJI

Mchele Basmati – Mugs 2 Β½

Vitunguu (Vikubwa kiasi) – 3

Tuna – Vibati 3

Carrot – 2 kubwa

Tomatoe paste – 1 kikopo

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 2 Vijiko vya supu

Tangawizi – 2 Vijiko vya supu

Uzile (Bizari ya pilau ya unga) (cummin powder )

(Jeera) – Β½ Kijiko cha supu

Mdalasini – Β½ Kijiko Cha supu

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Tuna carrots (grate) ziwe kama chicha weka kando.

Kaanga vitunguu 2 mpaka viwe brown weka pembeni.

Kaanga Kitunguu cha 3 halafu changanya na tangawizi, thomu, na tuna huku unakoroga.

Changanya na tomatoe, uzile (cummin powder) na mdalasini, koroga vizuri (hakikisha umeweka mtoto mdogo mdogo kwani ni rahisi kuungua)

Ikiwiva epua weka pembeni.

Chemsha wali wako kwa maji mengi na uuchuje kabla haujawiva vizuri na uugawe sehemu

Chukua trey au sufuria ambayo itaweza kuingia vitu vyote uilivyoandaa, tandaza fungu la kwanza la wali halafu utandaze carrot juu yake.

Tandaza fungu la pili la wali halafu utandaze vitunguu juu yake.

Tandaza fungu la tatu la wali halafu utandaze tuna (masalo) juu yake.

Mwisho tandaza fungu la nne la wali, ufunike vizuri na upike kwenye oven (bake) 350 Deg C kwa muda wa dakika 20

Epua ikiwa tayari kuliwa

Namna ya kupika Biskuti Za Kuchoveya Chokoleti

VIAMBAUPISHI

Unga 300gm

Siagi 225gm

Icing Sugar 60gm

Chokoleti iliyokoza (Dark Chocolate) – 225gm

Vanilla – Vijiko 2 vya chai

Yai -1

Baking Powder Β½ kijiko cha chai

Njugu za vipande Β½ kikombe cha chai

Njugu zilizosagwa ΒΌ kikombe cha chai

JINSI YA KUTAYARISHA

Piga sukari na siagi katika mashine ya keki mpaka iwe laini
Kisha mimina yai na vanilla koroga vizuri
Mwisho mimina unga na baking powder polepole mpaka ichanganyike.
Kata kata umbo (shape) lolote unavyopenda (kama nyota, pembetatu,duara, kopa n.k)
Panga kwenye treya na choma kwa moto wa 350Β°C , vikibadilika rangi kidogo tu vitoe
Yayusha chokoleti tia kwenye bakuli ndogo.
kisha paka kwa kijiko au chovyea upande mmoja mmoja wa biskuti kisha nyunyizia njugu za kipande na njugu ya unga.
Panga kwenye sahani tiyari kunywewa na chai ya maziwa au kahawa.

Mapishi ya wali Wa Nazi Kwa Mchuzi Wa Nyama Ng’ombe Na Mchicha

Wali Wa Mpunga

Mchele wa mpunga – 4 Vikombe

Tui la nazi – 6 vikombe

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mchele kisha

Bandika tui jikoni likichemka tia mchele na chumvi.

Funika uchemke, tui likikauka wacha moto mdogomdogo hadi wali uive ukiwa tayari. Ikiwa unatumia mkaa unapalia juu yake.

Mchuzi wa nyama Ng’ombe

Nyama – 1 kilo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa -2 viijiko vya supu

Viazi/mbatata – 2

Kitunguu maji kilokatwakawa (slice ndogo) – 2

Nyanya/tungule – 4

Nyanya kopo – 3 vijiko vya supu

Majani ya mchuzi/mvu – 3 msongo (bunches)

Bizari ya mchuzi (simba 2) – I kijiko cha chai

Ndimu – 1 kamua

Mafuta – ΒΌ kikombe

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Weka nyama katika sufuri, tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi, ndimu na chemsha nyama hadi iwive na ibakie supu yake kidogo.
Weka mafuta katika sufuri nyingine, kaanga kitunguu. Vinapogeuka rangi tia majani ya mchuzi endelea kukaanga hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (golden brown)
Tia nyanya/tungule, viazi/mbatata, endelea kukaanga mpaka nyanya ziive.
Tia nyama na supu yake kisha tia nyanya ya kopo, kotmiri, bizari ya mchuzi, chumvi uache mchuzi kidogo katika moto hadi viazi viive vikiwa tayari.

Mboga Mchicha

Mchicha – 4 michano/vifungu

Kitunguu – 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 3

Nyanya/tungule – 2

Tui la nazi zito – 1 kikombe cha chai

Chumvi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mboga iache ichuje maji.
Ikatekate kisha weka katika sufuria.
Katika kitunguu maji, kitunguu thomu kisage au kikatekate kidogodogo (chopped), nyanya.
Weka jikoni ipikike kwa maji yake na mvuke.
Tia tui endelea kuweka katika moto mdogomdogo hadi ikaribie kukauka ikiwa tayari.

Jinsi ya kuandaa Vileja Vya Karanga

MAHITAJI

Mayai 5

Sukari 450gm (1Β lb)

Unga wa Ngano 1Β kg

Siagi 450gm (1Β lb)

Baking powder Β½ Kijiko cha chai

Unga wa Custard Vijiko 2 vya chakula

Karanga za kusaga 250gm

Jam Β½ kikombe

MAANDALIZI

Chukua bakuli la kiasi, weka sukari na siagi.
Changanya sukari na siagi kwa kutumia mashine ya kukorogea keki (cakemixer), mpaka sukari ichanganyike na siagi.
Vunja yai moja moja na weka kiini chake kwenye mchanganyiko wa sukari na siagi, endelea kuchanganya mpaka ichanganyike vizuri. Hifadhi ute wa mayai ndani ya kibakuli.
Mimina unga wa ngano ndani ya mchanganyiko wako huku ukichanganya Changanya unga wa custard na baking powder.
Tengeneza viduara vidogo vidogo.
Vichovye viduara ndani ya ute wa yai kisha zimwagie unga wa karanga na kuzipanga kwenye tray ya kuchomea.
Weka dole gumba kati kati ya kila kiduara na uweke jam.
Washa jiko (oven) 350F na uchome vileja vyako kwa dakika 20.
Toa vileja vyako vipoe na uviweke ndani ya sahani tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Wali wakukaanga

Mahitaji

Mchele (Basmati rice) 1 kilo
Vitunguu (chopped onion) 2 vikubwa
Garlic powder 1/2 kijiko cha chai
Njegere (peas) 1 kikombe
Turmaric 1/2 kijiko cha chai
Coriander powder 1/2 kijiko cha chai
Cumin seeds 1/2 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia 2 vijiko vya chakula
Chumvi kiasi

Matayarisho

Osha kisha loweka mchele kwa muda wa dakika 5 na kisha uchuje maji na uweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown na kisha tia spices zote.Zikaange kwa muda wa dakika 3 kisha tia mchele na uchanganye vizuri na spice.Ukaange mchele pamoja na spice uku ukiwa unageuzageuza kwa muda wa dakika 5. Baada ya hapo tia maji ya moto(kiasi ya kuivisha wali) na chumvi kisha ufunike. Upike mpaka uive kisha malizia kwa kutia njegere na uchanganye vizuri baada ya dakika 2 uipue utakuwa tayari kwa kuliwa.Unaweza kuula kwa mboga yoyote uipendayo

Mapishi ya Ndizi za nazi na utumbo

Mahitaji

Ndizi mshale 10
Utumbo wa ng’ombe 1/2 kilo
Nazi ya kopo 1
Nyanya 1
Kitunguu kikubwa 1
Tangawizi/ swaum 1 kijiko cha chakula
Olive oil kiasi
Limao 1
Chumvi
Curry powder 1 kijiko cha chai
Turmaric 1/2 kijiko cha chai
Coriander ya powder 1/2 kijiko cha chai
Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai
Pilipili kali nzima (usiipasue)

Matayarisho

Safisha utumbo kisha uweke ktk pressure cooker pamoja na chumvi kiasi, limao, tangawizi, swaum na maji kiasi kisha uchemshe kwa muda wa nusu saa. Baada ya hapo menya ndizi kisha zikate vipande vidogo kiasi ili ziwahi kuiva, kisha ktk sufuria ya kupikia tia vitunguu na nyanya kisha ndizi kwa juu yake na supu ya utumbo kiasi chumvi kidogo na mafuta kiasi kisha bandika jikoni na uchemshe mpaka ndizi zikaribie kuiva. Zikisha karibia kuiva tia utumbo na spice zote, pilipili nzima na tui la nazi kisha changanya vizuri na uache vichemke mpaka ndizi na tui la nazi vitakapoiva na rojo ibaki kiasi. Baada ya hapo Ndizi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Upishi wa Afya kwa Ajili ya Afya ya Moyo: Kitamu na Kilainishi

Upishi wa Afya kwa Ajili ya Afya ya Moyo: Kitamu na Kilainishi πŸπŸ’šπŸŒ½

Leo, tutazungumzia juu ya jambo muhimu sana katika maisha yetu – afya ya moyo. Kama AckySHINE, ninapenda kushiriki na wewe njia ambazo unaweza kula chakula kitamu na cha kufurahisha wakati huo huo kuhakikisha kuwa unalinda afya yako ya moyo. Sasa twende tukashiriki njia hizi kumi na tano za upishi wa afya kwa ajili ya afya ya moyo wako! πŸ’ͺ❀️

  1. Kula Matunda na Mboga: Matunda na mboga mboga ni chanzo kizuri cha vitamini, madini, na nyuzi ambazo zinaweza kusaidia kudumisha afya bora ya moyo. 🍎πŸ₯¦

  2. Kupunguza Matumizi ya Chumvi: Chumvi nyingi inaweza kuongeza shinikizo la damu na hatari ya magonjwa ya moyo. Jaribu kutumia viungo vingine vya kitamu kama vile pilipili, tangawizi, au vitunguu. πŸŒΆοΈπŸ§„

  3. Kula Nafaka Zisizochakatwa: Nafaka zisizochakatwa kama vile mchele mzuri, ngano nzima, na tambi za ngano nzima zina nyuzi nyingi na virutubisho vingine muhimu kwa afya ya moyo wako. 🌾🍚

  4. Punguza Matumizi ya Mafuta Yasiyo na Lishe: Mafuta mengi ya wanyama na ya nazi ni mafuta yenye mafuta mengi ambayo yanaweza kuathiri afya ya moyo wako. Badala yake, tumia mafuta yenye afya kama vile mafuta ya zeituni au ya alizeti. πŸ₯₯πŸ«’

  5. Kupunguza Matumizi ya Sukari: Sukari nyingi inaweza kuongeza hatari ya kisukari na shida ya moyo. Badala yake, tumia asali au matunda kuongeza ladha tamu kwenye vyakula vyako. πŸ―πŸ“

  6. Ongeza Samaki kwenye Lishe yako: Samaki kama vile samaki wa maji baridi na mafuta kama vile samaki wa tuna, salmoni, na sardini, ni matajiri katika asidi ya mafuta omega-3 ambayo inaweza kusaidia kudumisha afya ya moyo. 🐟🐠

  7. Kula Vyakula vya Lishe: Kula vyakula vyenye lishe kama vile karanga, maharage, na mbegu za chia ambazo zina protini, nyuzi, na viinilishe vingine muhimu kwa afya ya moyo wako. πŸ₯œ

  8. Kuepuka Vyakula Vyenye Mafuta Mengi: Vyakula vyenye mafuta mengi kama vile nyama ya nguruwe, nyama ya ng’ombe, na bidhaa za maziwa zilizochakatwa zina mafuta mengi ya wanyama ambayo yanaweza kuathiri afya ya moyo wako. Chagua nyama nyepesi kama vile kuku au nyama ya ng’ombe iliyokatwa mafuta. πŸ–πŸ·

  9. Kupika Kwa Kutumia Njia za Kupikia Zisizo za Mafuta Mengi: Jaribu kupika kwa kutumia njia kama kupika kwa mvuke, kuchemsha, au kupika kwenye grill badala ya kukaanga au kuchoma moto. Hii itapunguza matumizi ya mafuta mengi na kuifanya chakula chako kiwe afya zaidi. 🍳πŸ₯¦

  10. Punguza Matumizi ya Vyakula Vilivyosindikwa: Vyakula vilivyosindikwa mara nyingi huwa na viungo vingi vya kemikali na mafuta mengi ambayo yanaweza kuwa na athari mbaya kwa afya ya moyo. Chagua vyakula vya asili na visindikwe kwa wingi. πŸ”πŸŸ

  11. Kula Chakula kidogo mara kwa mara: Badala ya kula milo mikubwa mara chache, jaribu kula milo midogo mara kwa mara. Hii itasaidia kudumisha kiwango cha sukari na cholesterol kwenye damu yako. 🍽️⏰

  12. Kunywa Maji ya Kutosha: Maji ni muhimu kwa afya ya moyo wako. Kunywa angalau lita mbili za maji kwa siku ili kudumisha mwili wako vizuri. πŸ’§πŸ’¦

  13. Kufanya Mazoezi: Mazoezi ni muhimu kwa afya ya moyo wako. Fanya mazoezi angalau dakika 30 kwa siku, kama vile kutembea au kukimbia ili kuweka moyo wako mwenye nguvu. πŸƒβ€β™‚οΈπŸ‹οΈβ€β™€οΈ

  14. Kupunguza Mafadhaiko: Mafadhaiko yanaweza kuathiri afya ya moyo wako. Jaribu kufanya mazoezi ya kupumua, yoga, au kutafakari ili kupunguza mafadhaiko yako na kuweka akili yako na moyo wako vizuri. πŸ§˜β€β™€οΈπŸ˜Œ

  15. Pima Afya ya Moyo wako: Fanya uchunguzi wa afya ya moyo mara kwa mara ili kugundua mapema shida yoyote au hatari ambayo inaweza kuathiri afya ya moyo wako. 🩺❀️

Kwa kumalizia, kula chakula kitamu na cha kufurahisha haimaanishi kuwa unapaswa kuhatarisha afya yako ya moyo. Kwa kufuata kanuni hizi za upishi wa afya, unaweza kufurahia chakula chenye ladha nzuri wakati ukihakikisha kuwa moyo wako unaendelea kuwa na afya bora. Kumbuka, afya ya moyo ni muhimu sana kwa maisha yetu ya kila siku, na kula vyakula vyenye afya ni hatua ya kwanza ya kuhakikisha tunadumisha moyo mzuri. Kwa hivyo, jiunge nami katika safari hii ya kusisimua ya upishi wa afya kwa moyo wako! πŸ₯—❀️

Na wewe je, una maoni gani kuhusu njia hizi za upishi wa afya kwa ajili ya afya ya moyo? Je, umewahi kujaribu njia hizi au una njia nyingine za kuongeza kitamu na kilainishi kwenye lishe yako ya moyo? Nimependa kusikia maoni yako! πŸ’¬πŸ˜Š

Mapishi ya Wali Wa Karoti Na Kuku Wa Kukaanga

Vipimo Vya Wali

Mchele wa Basmati/Pishori – 1 kilo moja

Vitunguu maji – 3

Karoti – 2

Siagi – 3 vijiko vya supu

Kidonge cha supu (stock) – 1 kimoja

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Γ“sha mchele uroweke kama saa moja au mbili
Katakata vitunguu vipande vidogodogo (chopped) weka kando.
Kwaruza karoti (grate) weka kando.
Tia siagi katika sufuria ya kupikia wali, weka katika moto iyayuke
Kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi kiasi tu.
Tia maji kiasi ya kupikia wali, changanya na kidonge cha supu.
Yakichemka tia mchele, koroga, funika uweke moto mdogo mdogo.
Kabla ya maji kukauka tia karoti changanya wali kisha funika uive kama unavyopika pilau.

Vipimo Vya Kuku Wa Kukaanga

Kuku alokatwakatwa – 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa – 2 vijiko vya supu

Bizari ya mchanganyiko/garam masala – kijiko cha supu

Mtindi/Yoghurt – 1 kijiko cha supu

Ndimu – 1

Chumvi – kiasi

Mafuta ya kukaangia – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Ukishamuosha kuku, mchuje atoke maji yote.
Changanya viungo vyote katika kibakuli kidogo.
Changanya pamoja na kuku kisha acha akolee viungo (marinate) kwa muda wa masaa mawili takriban.
Weka mafuta katika karai na kaanga kuku, akiwiva yu tayari kuliwa na wali.

Mapishi ya Supu Ya Maboga

Viamba upishi

Blue band vijiko vikubwa 2
Maziwa vikombe 2
Royco kijiko kikubwa 1-2
Pilipili manga (unga) kijiko cha 1
Chumvi kiasi Maji lita 2-3
Boga kipande Β½
Viazi mviringo 2
Vitunguu 2
Karoti 2
Nyanya 2

Hatua

β€’ Menya boga, viazi, karoti, nyanya na kwaruza weka kwenya sufuria kubwa.
β€’ Menya, osha na katakata vitunguu kisha ongeza kwenye mboga.
β€’ Ongeza maji na chumvi chemshwa mpaka vilainike.
β€’ Pekecha ikiwa jikoni na moto kidogo
β€’ Ongeza blue band, maziwa royco na pilipili manga ukikoroga kwa dakika 5.
β€’ Onja chumvi na pakua kama supu.
Uwezekano
Tumia siagi badala ya margarine.

Tofauti kati ya yai la kuku wa kienyeji na la kuku wa kisasa

Kilishe mayai yote ni sawa. Virutubishi vinavyopatikana kwenye yai la kuku wa kienyeji kama protini, vitamini A, madini ya chuma na virutubishi vya aina nyingine, ndivyo hivyo vinavyopatikana pia kwenye yai la kuku wa kisasa.

Tatizo linaweza kutokea pale ambapo wafugaji wa kuku wa kisasa hawafuati taratibu za ufugaji na pengine hawawapi kuku vyakula muhimu wanavyohitaji au wanawapa dawa na vyakula visivyo bora kiafya, hivyo wakati mwingine kiini cha yai la kuku wa kisasa huonekana kupungua rangi ya njano kuliko kiini cha yai la kuku wa kienyeji.

Mtu anashauriwa kula yai bila kujali ni la kuku gani, kwa kutegemea ni yai lipi linapatikana kwa urahisi. Lakini nivizuri kula mayai ambayo yapo salama.

Mapishi ya Wali Wa Kukaanga Kwa Kidari Cha Kuku (Chicken Breast) Wa Kukausha

Viambaupishi

Vipimo vya Wali:

Mchele 3 vikombe

*Maji ya kupikia 5 vikombe

*Kidonge cha supu 1

Samli 2 vijiko vya supu

Chumvi kiasi

Hiliki 3 chembe

Bay leaf 1

Viambaupishi: Kuku

Kidari (chicken breast) 1Kilo

Kitunguu 1

Tangawizi mbichi Β½ kipande

Kitunguu saumu(thomu/galic) 7 chembe

Pilipili mbichi 3

Ndimu 2

Pilipilimanga 1 kijiko cha chai

Mdalasini Β½ kijiko cha chai

Jira/Cummin ya unga 1 kijiko cha chai

Maji ΒΌ kikombe

Jinsi ya kuandaa na kupika

Wali:

Osha na roweka mchele kisha weka sufuria katika moto tia samli ipashe moto.

Tia hiliki, bay leaf, kaanga, kisha tia mchele ukaange kidogo.

Tia maji, chumvi na kidonge cha supu, upike wali kama unavyopika pilau.

*Maji kisia kwa kutegemea mchele ulivyo.

  • Unaweza kutumia supu yoyote badala ya kidonge.

Kuku:

Katakata kidari cha kuku vipande vya kiasi, weka katika sufuria, tia ndimu, bizari zote, chumvi.

Katakata kitunguu vipande vidogodogo, pilipili, na kitunguu thomu (chopped), tia katika kuku.

Chuna tangawizi mbichi tia katika kuku. Changanya vitu vyote vizuri.

Tia maji kiasi ΒΌ kikombe tu kiasi cha kumkaushia kuku. Weka katika moto mpike huku unageuzageuza. Anapokaribia kukauka epua akiwa tayari kuliwa na wali (na saladi upendayo)

Mapishi ya Pilau Ya Samaki Wa Tuna Na Mboga

Mahitaji

Mchele – 2 Mugs

Mboga mchanganyiko za barafu (Frozen veg) – Mug

Tuna (samaki/jodari) – 2 kopo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi -2 vijiko vya supu

Garam masala – 1 kijiko cha supu

Nyanya – 2

Kitungu maji – 1

Mdalasini nzima – 2 vijiti

Karafuu – 6 chembe

Pilipili mbichi – 1

Chumvi – kiasi

Viazi – 3

Maji – 2 Β½ Mugs

Mafuta – 3 vijiko vya supu

Maandalizi

Osha mchele na uroweke kwa muda wa dakika 20
Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
Mimina viazi, thomu na tangawizi, bizari zote na kaanga.
Tia nyanya uliyokatakata ikaange mpaka iwive.
Tia tuna endelea kukaanga kidogo tu.
Tia maji, yatakapochemka tia mchele.
Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa Β½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.

Jinsi ya kupika Pilau Ya Nyama Ya Ng’ombe Na Nyanya

Viambaupishi

Mchele (Basmati) 3 vikombe

Nyama ya ngo’mbe 1 kg

Pilipili boga 1 kubwa

Nyanya 2 kubwa

Vitunguu maji 2 vikubwa

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa 1 kijiko cha supu

Tangawizi 1 kijiko cha chai

Ndimu 1

Mafuta ya kupikia Β½ kikombe

Mdalasini Β½ kijiko cha chai

Binzari nyembamba 1 kijiko cha chai

Pilipili manga Β½ Kijiko cha chai

Hiliki Β½ Kijiko cha chai

Jinsi ya kuandaa na kupika

Loweka mchele wako katika chombo

Chukuwa nyama na ioshe vizuri na itie thomu, tangawizi, ndimu, pilipili manga na chumvi kiasi

Iweke jikoni hadi ikauke maji na kuwa imewiva huku ukiikaanga kaanga kwa hayo hayo mafuta yake hadi kuwa rangi ya hudhurungi

katakata Vitunguu na nyanya weka pembeni

Chukua pilipili boga, thomu, tangawizi na visage katika mashine ya kusagia

Weka sufuria pembeni na utie mafuta, subiri yapate moto

Kisha tia vitunguu na vikaange hadi kuwa hudhurungi na tia nyanya

Kisha mimina mchanganyiko wako ulio usaga wa pilipili boga, thomu na tangawizi

Koroga kwa dakika kadhaa Kisha mininia nyama uliyokuwa tayari, maji kiasi na chumvi wastani na subiri maji hayo yachemke

Weka mchele humo na koroga kiasi na onja chumvi kama ipo sawa au kama ndogo unaweza kuongeza

Funika na punguza moto na uache uive taratibu

Baada ya kukauka maji kabisa basi ugeuze na subiri tena kwa dakika kama mbili na tayari kuliwa.

Jinsi ya kupika Biskuti Nyembamba (Wafer Bar) Za Chokoleti Na Njugu

MAHITAJI

Wafer Powder/gram wafer (unga wa biskuti uliosagwa wa tayari) – vikombe 2

Maziwa ya Mgando Matamu ya Kopo – 2 vikombe

Nazi iliyokunwa – Β½ Kikombe

Chokoleti vipande vipande – 1 Kikombe

Njugu vipande vipande – Β½ Kikombe

Siagi – 227Β g

MAPISHI

Yeyusha siagi motoni kisha changanya na unga wa wafer acha kidogo motoni
Mimina katika treya unayochomea itandaze vizuri, kisha mimina maziwa juu yake pamoja na njugu vipande , nazi iliyokunwa na vipande vya chokoleti.
Choma (bake) kwenye oveni kwa moto wa 350ΒΊC kwa dakika 20.
Katakata tayari kwa kuliwa

Mapishi – Fish Finger

Leo tunaangalia mapishi ya fish finger ( sijui kama unaweza kusema kidole cha samaki)!, Ni mlo mzuri hasa kuliwa kama kitafunio au mboga ya pembeni.

Mahitaji

500g Fileti ya samaki
120g Chenga za mkate
100g Unga wa ngano
Mayai 2
Ndimu 1
Kitunguu saumu 1
Kotmiri
Mafuta ya kupikia

Matayarisho

Menya vitunguu saumu kisha visage

Katakata fileti kwa muundo wa mraba (kama vidole) kisha paka mchanganyiko wa vitunguu saumu

Kata ndimu na kamulia kwenye fillet yako

Weka chenga za mkate kwenye bakuli kisha uchanganye chumvi kiasi na kata kata kotmiri majani 3 na uchanganye pamoja.

Kwenye bakuli lingine weka mayai na uyapigepige yawe kama uji mzito

Weka unga kwenye bakuli jingine.

Chukua kipande cha fillet kiweke unga kidogo kisha kizamishe kwenye yai na baada ya hapo kizamishe kwenye mchanganyiko wa chenga za mkate. Fanya hivyo kwa vipande vyote.

Weka mafuta kwenye kikaago na subiri yachemke kisha weka fillet zako vizuri na zikaange pande zote hadi zimekuwa rangi ya brown ( hakikisha moto sio mkali sana).

Epua na weka pembeni mafuta yote yakauke

Weka kwenye sahani tayari kwa kula.

Mapishi ya samaki aina ya salmon

Mahitaji

Salmon fillet 2
Potatao wedge kiasi
Lettice kiasi
Cherry tomato
Limao 1
Swaum
Chumvi
Olive oil

Matayarisho

Mmarinate samaki na chumvi, swaum na nusu ya limao kisha muweke pembeni, baada ya hapo washa oven kisha tia potato wedge zikisha karibia kuiva anza kumpika samaki, tia mafuta kidogo sana kama kijiko kimoja cha chai hivi katika frypan isiyoshika chini yakisha pata moto kiasi muweke samaki wako (upande wenye ngozi chini kwanza) Mpike mpaka uone rangi ya kahawia kwa chini kisha mgeuze upande wa pili, uku samaki wako akiwa anaendelea kuiva, tayarisha salad yako kwa kusafisha lettice na nyanya kisha zichanganye pamoja kisha tengeneza salad dressing pembeni , kamua limao kisha tia olive oil na chumvi kidogo, Baada ya hapo samaki na potato wedge vitakuwa vimeiva, andaa mlo wako na utakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Kachori

Mahitaji

Viazi mbatata (potato 4 vya wastani)
Nyama ya kusaga (mince beef 1 kikombe cha chai)
Kitunguu (onion 1 cha wastani)
Carrot 1
Hoho (green pepper 1/2)
Kitunguu swaum (garlic)
Tangawizi (ginger )
Binzari nyembamba (ground cumin 1/2 kijiko cha chai)
Binzari manjano (turmeric 1/2 kijiko cha chai)
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Limao (lemon 1/2)
Pilipili ya unga (chilli powder 1/2 kijiko cha chai)
Giligilani (coriander kiasi)
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil)
Unga wa ngano kiasi

Matayarisho

Katakata vitunguu na hoho katika vipande vidogo vidogo na kisha kwangua carrot na uweke pembeni. Chemsha viazi na chumvi kidogo vikiiva viponde na uviweke pembeni, Baada ya hapo tia nyama limao, chumvi, kitunguu swaum na tangawizi ichemshe mpaka iive na uhakikishe maji yote yamekauka. Kisha Tia binzari zote, pilipili, curry powder, giligilani, vitunguu, hoho na carrot. Pika mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 3 na kisha ipua. Baada ya hapo changanya na viazi kisha tengeneza maduara ya kiasi na uyaweke pembeni. Chukua unga wa ngano kiasi na uchanganye na maji kupata uji usiokuwa mzito au mwepesi sana. baada ya hapo chovya madonge katika huo uji na uyachome katika mafuta. Hakikisha zinaiva na kuwa rangi ya brown na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.Unaweza ukazisevu na chatney yoyote unayopendelea.

Mapishi ya tambi za kukaanga

Kupika tambi ni kama ifuatavyo

VIAMBA UPISHI

Tambi pakti moja

Sukari ΒΎ kikombe cha chai

Mafuta Β½ kikombe cha chai

Iliki kiasi

Maji 3 Vikombe vya chai

Vanilla / Arki rose 1-2 Tone

Zabibu Kiasi (Ukipenda)

JINSI YA KUPIKA TAMBI ZAKO

1. Zichambue tambi ziwe moja moja.

2. Mimina mafuta kwenye sufuria yakisha pata moto mimina
tambi,zigeuzegeuze mpaka zibadilike rangi na kuwa brown.

3. Punguza mafuta kwa kuyachuja na zirudishe jikoni.

4. Nyunyizia iliki zilizosagwa koroga kidogo na mimina maji na tia arki
na acha zichemke mpaka maji yakikaribia kukauka mimina sukari
koroga kidogo na punguza moto.
5. Kisha tia zabibu ukipenda, zifunike ili zikaukie vizuri.

6. Zikishakauka pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa

Kidokezi: Itategemea na aina za Tambi unazopika kwa kukisia maji, kama utaona hazijaiva unaweza kuongeza maji kidogo.

Mawazo Mazuri ya Kifungua Kinywa cha Haraka na Salama kuanza Siku Yako Vizuri

Mawazo Mazuri ya Kifungua Kinywa cha Haraka na Salama kuanza Siku Yako Vizuri πŸŒ…

Hakuna jambo bora zaidi kuliko kuanza siku yako vizuri na kifungua kinywa kinachokupa nishati na furaha. Kwa kuwa AckySHINE, ninapenda kushiriki nawe mawazo mazuri ya kifungua kinywa cha haraka na salama ambacho kitakusaidia kuanza siku yako vizuri. Hapa kuna orodha ya mawazo 15 ambayo unaweza kuyajumuisha katika maisha yako ya kila siku:

  1. 🍳 Chagua kifungua kinywa kinachojumuisha protini, wanga na mafuta yenye afya. Kwa mfano, unaweza kula mayai yaliyopikwa kwa mafuta kidogo na mkate wa ngano nzima.

  2. πŸ₯£ Jumuisha nafaka nzima kama oatmeal au millet katika kifungua kinywa chako. Nafaka hizi zina nyuzinyuzi nyingi na zitasaidia kudumisha afya ya utumbo wako.

  3. 🍌 Ongeza matunda kwenye kifungua kinywa chako. Matunda yana virutubisho vingi na yatakupa nishati ya kutosha kwa siku yako.

  4. πŸ₯› Kinywaji cha maziwa kitakusaidia kupata protini na madini ya kalsiamu. Unaweza kunywa glasi ya maziwa ya mbuzi au kula jogoo au jibini la Cottage.

  5. 🍡 Kunywa kikombe cha chai ya kijani. Chai ya kijani ina antioxidants ambazo zinasaidia kuboresha afya ya moyo wako.

  6. πŸ₯œ Ongeza karanga au mbegu kwenye kifungua kinywa chako. Karanga na mbegu zina mafuta yenye afya na omega-3 ambayo ni muhimu kwa afya ya ubongo wako.

  7. πŸ₯— Chagua kifungua kinywa kinachojumuisha mboga mboga. Unaweza kuongeza mboga kwenye omeleti yako au kula sahani ya saladi yenye mboga mbalimbali.

  8. 🍞 Ikiwa wewe ni mtu anayependa mkate, chagua mkate wa ngano nzima au mkate uliotengenezwa kwa unga mzima. Mkate huu una nyuzi nyingi na unakuweka kushiba kwa muda mrefu.

  9. 🍯 Ikiwa unataka kuongeza ladha tamu kwenye kifungua kinywa chako, tumia asali badala ya sukari. Asali ni afya na ina virutubisho vingi kuliko sukari iliyo na sukari nyingi.

  10. 🌿 Ongeza mdalasini kwenye kifungua kinywa chako. Mdalasini ina mali ya kupunguza sukari ya damu na inaweza kukusaidia kudhibiti hamu yako ya kula.

  11. πŸ₯š Ikiwa unapenda kula omeleti, hakikisha unatumia yai la kutosha na kuongeza mboga mboga zaidi. Hii itaongeza lishe na ladha ya chakula chako.

  12. πŸ₯¦ Jumuisha mboga kama broccoli kwenye kifungua kinywa chako. Broccoli ni tajiri na vitamini na madini na itasaidia kukuimarisha mfumo wako wa kinga.

  13. πŸ₯€ Jaribu kinywaji cha smoothie kinachojumuisha matunda, mboga, na maziwa au maji. Smoothie itakupa nishati na virutubisho vingi.

  14. πŸ•™ Usikose mlo wa kifungua kinywa. Kula mlo wa kifungua kinywa ndani ya saa moja baada ya kuamka itasaidia kuamsha mwili wako na kuanza siku yako vizuri.

  15. 🍽️ Changanya vyakula tofauti katika kifungua kinywa chako ili uweze kufurahia ladha mbalimbali na kupata virutubisho vyote muhimu.

Kwa hivyo, kama AckySHINE, nakuomba ujaribu angalau moja ya mawazo haya ya kifungua kinywa. Utaona tofauti kubwa katika nishati yako na jinsi unavyohisi wakati wa siku. Kumbuka, kifungua kinywa ni muhimu sana na hakikisha unapata mlo kamili na lishe bora. Je, umeshajaribu njia yoyote ya kifungua kinywa ambayo imesaidia kuanza siku yako vizuri? Tuambie mawazo yako kwenye sehemu ya maoni hapa chini.

Namna ya kupika Vitumbua

Vitumbua ni aina ya vitafunwa vya chai ambavyo hutengenezwa kwa kutumia unga wa mchele. Kiasili vitumbua ni chakula ambacho hupendelewa sana na watu wa pwani. Na mara nyingi wamekuwa wakipika kwa kuchanganya na nazi ili kuvifanya view na ladha nzuri zaidi

Mahitaji:

Unga wa mchele Β½ kg
Sukari vijiko 4 vya mezani
Tui bubu la nazi
Mafuta ya kupikia
Unga wa hiliki Β½ kijiko cha chai
Hamira kijiko 1 cha chai
Chuma cha vitumbua

Maandalizi:

Chukua unga wa mchele na weka kwenye bakuli au sufuria ya kilo moja
Weka hamira kisha weka sukari kisha miminia tui katika mchanganyiko wako
Weka hiliki koroga hadi view uji mzito
Acha uji huo kwa muda wa saa moja hadi uumuke, mara nyingi kuumuka kunategemea na hali ya hewa,
Baada ya hapo weka mafuta kijiko kimoja cha chakula kila kishimo acha yapate moto Kisha kaanga virumbua vyako

Shopping Cart
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About