Vituko Vya Kukupa Mudi Mpya
Watoto wa siku hizi ni shida! Angalia huyu mtoto anachomwambia baba yake
Ka ni wewe?
DOGO: baba mi siendi tena shule inaonekana walimu hawana uhakika na majibu yao.
BABA: Kwanini unasema hivyo?
DOGO: juzi walisema 3+4= 7, jana wakasema 1+6=7, halafu leo wanasema 5+2=7 sasa huoni kama wanatuchanganya.
ungekua wewe ungemjibu nini
Staili nyingine za michepuko ni shida
Mtu na mkewe walikuwa bado wamelala asubuhi, mtu akapiga hodi mke akaenda kufungua mlango, si akakuta mchepuko wake,
MKE: Unataka nini we mpumbavu?
MUME: Nani huyo unamtukana?
MKE: Kuna mtu hapa anakichwa kama nenda urudi badae
MCHEPUKO:Nawewe pua kama poa
MKE:Miguu kama masaa mawili
MCHEPUKO:Masikio kama sichelewi
MKE: Ondoka hapa mjinga we. β¦β¦ Akafunga mlango
MUME: mwambie ana macho kama sitoki leo ng’oo
SIPENDI UJINGA MM nikiwa na my love pr
Hii ndiyo sababu ya kumfanya huyu jamaa kujiita fara
MZEE:”sasa huyu mgeni sijui alale wap?”
MKE:”saa hizi ni usiku akalale na Bebi.”
jamaa akaona huyo Bebi pengne mtoto anakojoa kitandani au akalia asije msumbua usiku
JAMAA:”msipate tabu mi ntalala hapa kwenye kochi” akalala
asubh wanakunywa chai akaibuka mrembo,jamaa akapigwa bumbuwazi almanusra ajimwagie chai.
BINTI:”Naitwa BEBI,we unaitwa nani?”
Jamaa akasema mimi naitwa Faraβ¦..!
Cheki tabia za kuandika vimaneno vya ajabuajabu kwenye pikipiki na bodaboda ilivyomponza huyu
Jamaa mmoja dereva wa bajaji alianguka, sasa bajaji ikawa imem’bana akawa anafurukuta bila mafanikio Cha ajabu watu wakawa wanampita bila kumsaidia, Kumbe Nyuma ya Bajaji yake alikua Kaandika “NIACHENI KAMA NILIVYO, HII NDIO STYLE YANGU”Β πππΒ Mpaka sasa nimemwacha bado yuko hapoΒ *Sipendagi Ujinga mimi* πΆπ½πΆπ½πΆπ½πΆπ½πΆπ½
Huku ndiko kuumbuka bila chuki
Umeenda kutembea ukweni kwako baada ya chakula chausiku unapewa chumba chakulala inapofika usiku unatakakutoka kwenda kujisaidi kwasababu taa zimezimwa unapamia vyombo vya chakula sebleni kipindi unajalibu kupapasa uviweke sawa mala taa inawashwa na mama mkwe anaona umeshika vyombo anakwambia, baba kama ukushiba ungesema
Eti kwani wewe ni turubali?
Unakuta MTU mwaka Mzima
Umehudhuria,Β birthday parties 20 ,Β misiba 30,
Mikutano kanisani 40, Ndoa 80 na bado uko Single Kwani wewe ni turubai jaman??
πππππππππππ
Wanawake wa leo mbele ya hela. Hii ni hatari
MDADA: Baby nikwambie kitu
MKAKA: Yeah Baby Uko huru nambie
MDADA: nilikua naomba hela babyβΊ
MKAKA: WW nae kwa kupenda hela jana tu nmekupa hela Leo unaomba ya nn π
MDADA: hapanaπ Bby sio hivyo nlikua nataka nikashuhudie tetemeko la ardhi BUKOBA nasikia huko linaonekana vizur .
ππππππππ
Wanawake kumbukeni sio vizuri
Wasichana wa leo
Jamaa yupo ndani ya Range rover yake mpya na msichana ambaye ni mpenzi wake.
#Jamaa: kuna siri flani nimeitunza moyoni mwangu kwa muda mrefu na nikaona kama nitakuambia lazima utaniacha.
#Msichana: siri gani hiyo mpenzi wangu?
#Jamaaa: nimeoa.
#Msichanaa: HΙΙΙΙΙΙΙΙ! We umenishtua sana,mm nilifikiri hili gari sio lako!
πππ€π€
Duh, Ukisikia ngoma droo ndio hii
Ni noma!
Baada ya Talaka mke kamtumia mume meseji:- “Nasikitika kukujulisha kuwa binti uliyemlea kwa miaka 20 sio mtoto wako” Mume akamjibu:- “Duh! Nashukuru Mungu kwani nilikuwa nikiumia rohoni kila siku kwamba nazini na binti yangu” πππππππππ πππππππππ
Angalia huyu msichana alichonifanyia
Kuna siku nilichalala kipesa nikaamua kuomba dem wangu aniazime 10,000/= akanipa.
Baada ya siku mbili nikapata pesa zaidi ya laki nne hivi, nikaamua kumpa 100,000/= mpenzi wangu bila yeye kuniomba.
Baada ya siku 3 akaja kuniambia:- “Bae, ile 10,000/- niliyokuazima mwenyewe amekuja kunidai, so kama unayo naomba unipe nimrudishie maana ananisumbua leo siku ya 3.”
SAA HIZI NIPO ZANGU SINGLE NATAFUTA DEM MWINGINE
Cheki kilichotokea stesheni ya treni, mambo mengine ukipaniki inakula kwako kama huyu jamaa
Jamaa Wawili Walifika Stesheni, wakakuta Treni ndo kwanza inaondoka. Wakaanza Kuikimbiza. Mmoja akafanikiwa kupanda akaondokaβ¦
Yule aliyebaki akaanza kucheka sanaa mpaka machozi yakamtoka. Watu wakamuullza, unacheka nini sasa wakati umeachwa? Akawajibu: “kinachonichekesha, yule aliyepanda alikuwa ananisindikiza.
Utani wa wahindi, cheka kidogo
Mhindi afaulu mtihani wa Kiswahili
(1) Mfa maji ?β¦β¦β¦β¦β¦β¦.. Tampa life jacket.
(2) Mwenda pole?β¦β¦β¦β¦ Tachelewa fika.
(3) Usipoziba ufa ?β¦β¦β¦.. Mizi taona mpaka dani.
(4) Usilolijua ?β¦β¦β¦β¦β¦β¦ Uliza google.
(5) Mbio za utelezini ?β¦β¦. Chafua guo yako.
(6) Ukipenda boga ?β¦β¦β¦ Ngoja mezi ya ramzani tapata.
(7) Ukiona vinaelea ?β¦β¦.. iko nyepesi hiyo.
(8) Maji yakimwagika ?β¦β¦ Mambie dada tapiga deki.
(9) Chelewa chelewa ?β¦β¦β¦ Takosa guo ya sikukuuβ¦
(10) Kila ndege ?β¦β¦β¦β¦.. β¦Hutua Airport
(11) Bandu bandu ?β¦.. β¦β¦.Rafiki yake Jecha
(12) Mtaka cha Mvunguni ?β¦ Ondoa tanda
(13) Simba mwenda kimya?β¦.Kama sio gonjwa basi haina njaa.
(14) Aisifuye mvua ?β¦β¦β¦. Najua iko Mkulima hiyo
(15) Barabara ndefu ?β¦β¦.. Ongeza mwendo au tachelewa fika.
(16) Mlanawe hafi nawe ila?β¦. Takimbia
(17) Asie sikia la mkuu ? β¦β¦.. Tapeleka jela
(18) Hasira za mkizi ? β¦β¦β¦β¦..Tatafuna veve
(19) Mchamba wima ?β¦β¦.. Karibu ya Hurumzi
(20) Akumurikae mchana ?β¦.Kipofu hiyo
(21) Mficha maradhi ?β¦β¦.. Taenda Loliondo
(22) Mkataa wingi ? β¦β¦β¦.Taenda Chadema
(23) Bendera ?β¦β¦β¦β¦β¦. Kama sio ya CCM, ya CUF
(24) Baniani mbaya ?β¦β¦. Peleka Bombay Lakini sio HB kweli, naonea tu
(25) Akili nyingi ?β¦β¦β¦. Tapasi mtihani yote
(26) Penye kuku wengi ? β¦β¦.. Chija bili tatu ivi, hapana mtu najua.
Ukimuona mbwa kwenye harusi hii ndiyo maana yake
Hili nalo neneo.
Ukimuona mbwaπΆ harusini usimpige mawe wala kumfukuza inawezekana kilichomleta pale ndicho kilichokupeleka na wewe hapo
BREAKING NEWS!!! Nyoka wa ajabu agundulika
HABARI MPASUKO..
jana katika taasisi ya wanyama pori ya Nat Geo ilitangazwa kuwa ametokea Nyoka hatar san Ambaye hajawah kutokea duniania.. wanadai kwamba nyoka huyo anaongezeka ulrefu wa 0.5sm kila akila chakula na huwa anakula chakula kuanzia sekunde 30 kurudi nyuma.. mpaka sasa hakuna siraha ya kuweza kumuua nyoka huyo isipokuwa akiji uma mwenye ndo anaweza kufa, wanasayansi hao walieleza japo uchunguz zaid bado unaendelea⦠huyu ni nyoka anayeua kuliko nyoka wote waliowah kutokea katika historia ya maisha ya mwanadam..
nyoka huyu hupatikana katika simu pekee za nokia toch katika sehem ya game inaitwa snake xenzia..
asanteni kwa kufurah na umakin mkubwa katika usomaji wa matini hiiβ¦
haya ni mambo ya wikiend jaman na iwe njema kwenu wote
Angalia huyu mwanafunzi anachomjibu huyu mwalimu wake
1. Ticha:”Punda ni mnyama anaefugwa nyumbani,lakini akiwa mwituni anaitwa pundamiliaβ¦.Je sungura anayeishi mwituni anaitwaje?”
ZUZU:”Sunguramilia.”
2.Ticha:”Rais wa kwanza wa kenya aliitwa KENYATTAβ¦Je rais wa kwanza wa
Tanzania aliitwaje?”
ZUZU:”TANZANIATTA.”
3. Ticha:”Kuku yuko katika jamii ya NDEGEβ¦Je samaki yuko katika jamii ya nini?”
ZUZU:”MELI.”
4. Ticha:”Coach wa Arsenal anaitwa ARSENE,wa Man-city anaitwa MANCINIβ¦.Je wa
Liverpool anaitwaje?
ZUZU:”LIVER.”
5 Ticha:”Ukiwa na mbuzi 10,wezi waje waibe 5,utabaki na nini?”
ZUZU:”Hasira nyingi sana!”
Sababu za kumuacha mke kama umemchoka
Ukimchoka mkeo, waweza kumtaftia sababu za kumuacha kama hizi
_
1. Missed calls 16? Umeua betri la simu yangu. Kwa hiyo hata mimi unaweza kuniuaβ¦ It’s Over!!!
_
2. Hata hunieshimu. Mi naongea na wewe lakini we upo bize unavuta pumzi? It’s over!
_
3. Nimekupigia umepokea simu hapohapo. Huna subira. Itβs over!!
_
4. Nilikwambia huwa napenda chakula cha moto lakini hujanipashia ice cream. Hunijali. It’s over!
_
5. Nimekupa mayai mawili, moja uchemshe jingine ukaange. We umekaanga ambalo ulitakiwa kuchemsha na umechemsha ulilotakiwa kukaanga. Huniheshimu, Itβs over!
_
6. Nimekuita DARLING na wewe ukaniita HONEY. Yani kwa maana nyingine unamuita mama yangu NYUKI. Huheshimu wazazi wangu, fungasha kilicho chako. its over.
πππππππππ
Angalia ndoto nyingine zilivyo na Majanga
Ndoto zingine bwana usiombe zikupate
Mimi usiku wa kuamkia Leo nikiwa nimelala nimeota naendesha gari Yangu aina ya BMW mpya Mara gafla ikakwama kwenye tope .hivyo ikabidi nishuke ili kuisukuma loh! Yani kudadeki ile kuamka nikakuta nimesukuma kitanda hadi sebleni Daaa ilinisikitisha sana jiangalie sana sese hivi ndio narudisha kitanda chumbani .angalizo angalia ndoto unazo ota unaweza kuota upo baharini ukaamka unajikukuta unaogelea kwenye Jaba la Maji shauri yako.












































































I’m so happy you’re here! π₯³
Recent Comments