Vituko Vya Ijumaa

Hawa wanaume wanaopenda wanawake hovyo barabarani wamepatikana, hawatarudia ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Marafiki wawiliย (Jose na Ben)ย walikuwa wanatembea mtaani akatokea mwanamke akarusha busu kwa mmojawapo kupitia dirishani katika jengo la ghorofa tatu.

Wakaanza kujadiliana kama ifuatavyo:

Ben:ย Muone yule mrembo amenirushia busu

Jose:ย tafadhali achana na huyo mwanamke, usimjali..

(baadae yule mwanamke akamuashiria aende)

Ben:ย yule mwanamke ameniita!

Jose:ย Rafiki yangu, usiende. Nakutafadhalisha.

Ben:ย Kwa nini unaniambia nisiende Wakati mrembo kama yule ananiita? Huo ni wivu

Jose:ย Ben, Ninakutafadhalisha tena, usiende, tafadhali usiende kuleย (akihisi kutotiliwa maanani)

(Rafiki yake alimpuuza na alienda kwa yule mwanamke, mwanamke alishuka kukutana naye na wakapanda juu. Ghafla wakiwa wanataka kuanza taratibu za kula uroda, wakasikia mlio WA gari getini).. ๐Ÿ”Š๐Ÿ”Š

Lady:ย _(akiangalia kupitia dirishani)_
Oooh! Yule ni mume wangu!!

Ben:ย Mama yangu !
Nipo matatani, kweli ? ..!!

Lady:ย Usiwe na khofu, jifanye kuwa Dobi na anza kupiga pasi hizo nguo

(akimuonyesha lundo la nguo)

(Ben alitumia masaa matano kukamilisha kunyoosha zile nguo kwa sababu yule mume hakutoka tena siku ile)

(Siku iliyofuatia Ben alikwenda kwa Rafiki yake)

Ben:ย Kaka, unaweza kuamini Jana nimepiga pasi nguo kwa masaa matano???

Jose:ย Lakini nilikwambia usiende. Nguo zote hizo ulizonyoosha,ย Nilizifua Mimi Juzi!!
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

When an experienced person speaks โ€ฆ ๐Ÿ‘‚you must listen..!

Mkalimani alivyoharibu ibada ya leo

Leo nikaamua niingie misa ya asubuhi kwenye kanisa moja la kilokole kulikua na ugeni wa mchungaji kutoka Bulgaria, Mahubiri yameanza saa 1 asubuhi hali ikawa kama hivi:

MCHUNGAJI: My name is Pastor Livingstone
MKALIMANi: Kwa jina naitwa mchungaji Jiwe linaloishi
MCHUNGAJI: We thank God for All goals we set by our hands
MKALIMANI: Tunamshukuru Mungu kwa Magoli yote tuliyoweka kwa Mkono

Hivi navyoongea kanisa halina viti waumini wote tumekimbia nje naona Mkalimani amebaki na kiatu cha kushoto tu.
Sunday joke

Cheki huyu mzee alichomfanyia muuzaji wa pharmacy

Mzee kaingia pharmacy,
MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu naomba uonje nitakulipa
MFAMASIA: Kitu gani?โ€ฆ.Mzee akatoa kichupa na kijiko akaweka โ€ฆmajimaji yaliyomo kwenye
kichupa kwenye kijiko na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia akatia yale maji mdomoni na kuyazungusha zungusha mdomoni akionja;

MZEE: Nipe jibu, ina utamu wa sukari au chumvi au pilipili?
MFAMASIA: Kama chumvichumvi
MZEE: Hakuna sukari
MFAMASIA: Sukari hakuna kabisa
MZEE: Loh asante chukua hii alfu tano nashukuru sana, dokta alinambia nipime mkojo wangu kama nina kisukari, kumbe sina asante bwana mdogo

Mke alichomfanyia mme wake kabla ya kwenda safari, Chezea mawaifu walokole wewe!

JAMAA alimuaga mke wake mlokole kuwa anaenda semina ya siku tatu, kumbe anakwenda kwa bi mdogo.

Mke akamwambia mumewe; “Tupige magoti tusali”,

Wakapiga magotiโ€ฆ:
MKE: Eee baba msaidie mume wangu afike salama safari yake.
MUME: Emenโ€ฆ

MKE: Mpe nguvu katika yote atakayoyafanya huko.
MUME: Emenโ€ฆ

MKE: Akitaka kufanya uasherati ashindwe.
MUME: Kimyaโ€ฆ

MKE: Akifanya uasherati apatwe na janga baya kwa uwezo wako bwana.
MUME: โ€ฆโ€ฆ.!!

MKE: Yaani akifanya uasherati afie hukohuko kwa mateso makali.
MUME: Maombi gani sasa hayo!!?. Haya basi siendi semina ufurahi wewe.

Chezea mawaifu walokole wewe!

Padri Akimbia wakati wa kuungamisha, chanzo ni hiki

Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
“Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sana.”
Padri, “Endeleaโ€ฆ”

“Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia
amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema
nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa
kufungwa.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu,nikatoa bastola nikamuuaโ€ฆ.. Yesu atanisamehe?”

Padri: “Utasamehewa.”
“Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango
unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona
kilichotokea akasema anapiga polisi simu.
Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuua na yeye piaโ€ฆ Yesu atanisamehe hilo?”
Padri: “Utasamehewa.”

Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi
akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa
bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuuaโ€ฆ.. Yesu atanisamehe?”
Padri:”Utasamehewa.”

“Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda
nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi
akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi
nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya
babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye
wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua?
Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.

Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke
yetu, nikamuuaโ€ฆ.. Yesu atanisamehe na hilo?”

Kimyaaโ€ฆ.
“Padri yesu atanisamehe?”
kimyaโ€ฆ.

Jamaa akatazama kwenye confession booth padri
hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo
za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.

Jamaa, “Sasa baba mbona umekimbia?”
Padri kwa taabu akajibu, “Nilitazama huku na huku
nikagundua tuko wawili peke yetuโ€ฆโ€ฆ.”

Kichekesho cha mtalii na mbongo

Duh! Sikubali bora mbavu zituume wote!

Watalii wana dharau sana bana, Mtalii alikodi boti akazunguka nayo kwenye mto Rufiji kuangalia mandhari, akamuuliza kijana anayeongoza boti, “Do you know Biology, Psychology and Anthropology?” Kijana akajibu “NO,” Mtalii akamwambia “nothing you know under the sun? You are useless, and u’ll die with your illiteracy!” baada ya muda boti ikaanza kuzama, kijana akamwambia mtalii “Do you know kuogelealogy and kusepalogy from mambalogy? Mtalii akajibu huku ametoa macho “No” kijana akamwambia “You will kufalogy and mambalogy wil eat your matakology because of your bad-mdomology..๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Alichojibu dalali baada ya kufumwa na mke wa mtu ndani ya nyumba ya kupanga

Dalali aliwatafutia jamaa chumba Buguruni karibu na reli, nyumba nzuri sana. Jamaa na mkewe wakahamia kwa furaha, lakini furaha yao iliisha walipokuja gudundua nyumba ile iko karibu mno na reli treni ikipita mpaka kitanda kinacheza.

Siku hiyo dalali akapita mke akamwita na kumwambia tatizo wakati treni inapita, wakaanza kubishana, yule mama akamwambia dalali kwa kuwa kuna treni itapita sasa hiviโ€ฆ njoo ndani uone mwenyewe.

Bahati mbaya wakiwa wamejilaza kitandani ili dalali aone adhabu wanayopata, Mzee mwenye mali alirudi ghafla, akauliza,

‘Nyie mnafanya nini hapa?’

Masikini dalali kwa woga mkubwa akajibu’ Tunangoja treni’

Kweli tamaa ni mbaya, mke wa mtu kaponzwa na tamaa, ndio basi tena

Jamaa kaenda kwa mke wa rafiki yake:
JAMAA: Shem nakupenda!
MKE: Hebu toka hapa! Je rafiki
yako akijua? tena koma!
JAMAA: Ntakupa milioni 1!
MKE: Basi njoo kesho mchana
mume wangu akiwa kazini!

Kesho yake Jamaa kaja
na milioni 1 wakamalizana na mke wa rafki yake,
jioni ilipofika
Mume akarudi home na
kumuuliza Mkewe, “Rafki yangu SAM kaleta hela yangu milioni 1?”
MKE akajibu kwa unyonge, “Ndio!”
MUME: Yes! Ndio maana nampenda SAM kanikopa asubuhi jioni karejesha!!!!
Mke hoiโ€ฆโ€ฆ

Angalia huyu boyfriend alivyomuweza huyu msichana wake

Siku moja msichana alikuwa anapita maeneo ya A.T.M gafla
akamuona boyfriend wake anatoa pesa kwenye A.T.M binti
akaamua kujificha na kumtumia boyfriend wake sms ya
kimahaba
“Honey kama upo nyumbani umelala naomba unitumie ndoto
zako,
Kama unakula nitumie chakula, Kama unacheka nitumie kicheko
chako,
Kama unalia nitumie machozi yako,Kama unatoa pesa kwenye
A.T.M nitumie pesa.” Boyfriend akajibu “NIKO CHOONI LABDA
NIKUTUMIE KINYESI MPENZI!!

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About