Visa Vya Kileo

Hii ndio maana ya Matatizo, usiombee hili likukute

Matatizo ni nini???

`Matatizo ni pale unapokuwa umefika ukweni usiku na haja kubwa ikakubana na hukuwa unajua choo kilipo, ukatoka nje na kujisaidia kwenye majani kumbe ni mboga asubuhi ukasikia mama mkwe anasema kuna mjinga kajisaidia kwenye mboga na kaangusha pochi yake hapohapo haa! Vile unajisachi pochi hamna na kulikuwa na passport,vitambulisho, kadi ya benki, pesa zaidi ya laki 2 na nusu, funguo za nyumba yako, `
๐Ÿค’๐Ÿค’๐Ÿค’๐Ÿค’๐Ÿค’๐Ÿค’๐Ÿค’๐Ÿค’๐Ÿค’

Walahi haya ndo matatizo๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…

Hii ndiyo Ladha ya bia zote usiyoijua

Ladha ya bia ya 1 hadi ya 6..

Kwa wanywaji wazuri wa bia,

chupa ya kwanza ๐Ÿบ huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza kooโ€ฆ Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.

chupa ya pili ๐Ÿบ๐Ÿบ kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihiโ€ฆ.

Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Yanga bila kukosea.. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.

Bia ya tatu ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sanaโ€ฆ. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokezaโ€ฆ..

Bia ya nne ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikiaโ€ฆ.. bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.

Bia ya tano ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipuโ€ฆโ€ฆna kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; โ€˜Mi sipendwi mpaka leo sijaolewaโ€™ au โ€˜ Mume wangu sijui yukoje hanijaliโ€™

Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.

Kuanzia bia ya sita ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. โ€ฆโ€ฆ. โ€ฆKuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo fala na hajui kuendesha kampuni.

Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjikaโ€ฆโ€ฆ.

Mzee wa kichaga na hela zake. Angalia anachofanya

Mzee moja alikuwa kila usiku anapita mbele ya bank anasimama,kisha anapiga honi,akitoka askari mlinzi,anaondoka.Hilo jambo likamkera sana askari mlinzi, askari akawa na mvizia yule mzee wa kichaga ,siku alipokuja tena akamkamata, akamuuliza kwa nini unakuja unapiga honi kisha unakimbia? Mzee akasema: Haki ya mungu babaangu , Nina pesa zangu ktk account hapa bank naogopa usilale usingizi ndo maana kila siku usiku napita kukuangalia kama umelala!!
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Huu ndio mlolongo wa michepuko kuwahi kutokea kati ya mke, mume mwanafunzi na boss

BOSS anamwambia sekretari wake: Wiki hii tutaenda wote Serena Hotel kwenye mkutano fanya mipango yote.
SEKRETARI (anamuaga mumewe): Tunaenda na bosi Serena hotel kwenye mkutano for 1 week.
MUME (anampigia mpango wa kando): Mambo safi, wife anaenda kikazi Serena, jitayarishe tujipe raha for 1 week
(Mpango wa kando) anamwambia mwanafunzi wake wa tution: wiki hii nina kazi fulani hakuna tution mpaka week ijayo.
MWANAFUNZI anampigia simu sugar daddy wake ambaye ndo (BOSS): Dear hakuna tution wiki hii nakuja kwakoโ€ฆ..

BOSS anamwambia sekretari wake: Siendi Serena tena coz mjukuu wangu atanitembelea.
SEKRETARI: Mume wangu hatuendi Serena
MUME (anampigia Mpango): dah! mpenzi, huyu mke wangu haendi tena. Shit! So hadi next time plz
Mpango wa kando a.k.a teacher (anampigia mwanafunzi): Darasa kama kawaida sorry for the earlier message.
MWANAFUNZI: darling tution inaendelea kumbe, so nakuja wiki ijayo!!
BOSS: Sekretari sorry jitayarishe ile safari ya Serena iko palepaleโ€ฆโ€ฆ

Maisha ya Pwani ni Shidaaaaah

๐Ÿ˜†๐Ÿ˜† ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Jamaa kagombana na mkewe, akasusa kula๐Ÿฝ๐Ÿจ kurudi kazini kamkuta mkewe amevaa kanga imeandikwaย ukisusa wenzio walaย ilipofika asubuhi mke akavaa kanga imeandikwaย ukitoka ๐Ÿšถ๐Ÿšถmwenzio anaingia๐Ÿ’ƒ๐Ÿ’ƒ

jamaa akagoma kwenda kazini ๐Ÿ˜ฌ๐Ÿ˜ฌ mke akabadili kanga na kuvaa iloandikwaย nimemdhibiti ndo mana hatoki๐Ÿšท jamaa akaenda kuomba ushauri kwa rafiki yake akaambiwa twende nyumbsni kwako, walipofika walimkuta mke kavaa kanga imeandikwaย ulidhani rafiki yako kumbe adui yako๐Ÿค”๐Ÿค” jamaa akaamua kusafiri siku tano ili kupunguza hasira. Aliporudi akamkuta mke amevaa kanga imeandikwaย ni bora nimpe jirani kuliko kiozee ndani
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

hata kama hupendagi ujinga kwa maneno ya kwenye kanga utasanda tu

Huyu panya wa tatu ni noma

๐Ÿ€ ๐Ÿ€ ๐Ÿ€ย Panya watatu walikua wakibishana nani Ni noma zaidi

Panya 1:ย jamani mimi ni noma Wiki hii nimekula rat rat(sumu ya panya) mara tatu na sijadedi !!!

Panya 2ย Wewe unasema nini, mimi nimekula nyama ikiwa
kwa mtego mara 5 nasijawahi dakwa

RAT 3ย Mmemaliza? Mie hata sijui mnabishana nini? Mimi hii mimba niliyo nayo ni ya paka !!!

Panya WA 1 na 2 wakazimia๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†
Panya wa 3 huwa hapendi ujinga kabisa

Angalia wanachokifanya Zuzu na msichana chumbani kwenye giza

Zuzu: Mambo Anna!
Anna: Poa!
Zuzu: Kuna kitu nataka nikuonyesheโ€ฆ
Anna: Kitu gan?
Zuzu: Twende chumbani kwako (wakaenda)
Anna: Haya nionyesheโ€ฆ

Zuzu: Funga mlango na madirisha kwanza (akafunga)
Anna: Haya nionyeshe sasa!..
Zuzu: Zima taa kwanza (akazima)
Anna: Mhmโ€ฆnionyeshe sasa!
Zuzu: Haya njoo hapa kitandaniโ€ฆ
Anna: Ok, nionyeshe!
Zuzu: Ona nimenunua saa ambayo inawaka yenyewe gizaniโ€ฆ Acha mawazo mabaya ww???

Cheki huyu jamaa anavyoungama kwa padri sasa

JAMAA: Baba Padri nimekuja kuungama
PADRI: Haya
JAMAA: Niliiba kamba
PADRI: Kamba?
JAMAA: Ndio, kamba lakini kule mwisho kulikuwa kumefungwa ng’ombe
PADRI: Kwa hiyo uliiba ng’ombe?
JAMAA: Kiukweli nilikuwa nina lengo la kuiba kamba, kwa bahati mbaya mwisho kulikuwa na ng’ombe
PADRI: Mi naona mueleze Mungu direct, mi sikuelewi kabisaaa

๐Ÿ™ˆ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜‚๐Ÿ™Š

Angalia wadada walivyoumbuka kwenye hii test

Ticha katangaza test , Akatoa Masharti; Ukiandika jibu hamna kufuta au kukata.

Swali la kwanza,
Taja vyakula vi3 ambavyo ukienda hotelini umelipiwa utapenda kula (marks 1)

WAVULANA wakajaza; wali, ugali, mihogo.
WADADA wakajaza; burger, pizza, egg chop. Swali la

2: Eleza jinsi ya kupika kila chakula ulichotaja hapo juu. (marks 99)
wacha wadada waanze kuhangaika kukata majibu ya mwanzo!

Hii ndio ndoto ya harusi ya kila msichana anayotamani

GIRL: Baby, hebu niambie harusi yetu itakuwaje?
BOY: Yaani hii haijawahi kushuhudiwa, ngoja nikupe kionjo kidogo tu
GIRL: Enheeโ€ฆ
BOY: Kwanza siku ya kupeleka mahari nitaswaga zizi zima la ng’ombe napeleka kwa babu yako
GIRL: Ooh baby u care..
BOY: Siyo hivyo tu, baba yako ntamnunulia Range Rover Sport na mama mkwe ntampa Range Rover Evoque
GIRL: Baby u are awesomeโ€ฆ
BOY: Halagu mdogo wako wa kiume ntampa Prado Tx, na hapo nimesukutua tu mdomo sijaanza kulaโ€ฆ.
GIRL: Enheeโ€ฆna sisi??

BOY: Sisi tutachukua mtaa mzima Oysterbay, kila wiki tutaishi nyumba tofauti
Halafu siku ya harusi yetu tutakodi zile meli zinabeba makontena ndiyo iwe ukumbi wetu, itatupeleka hadi Maldives
GIRL: Baby I love you
BOY: Tukitoka hapo tunaenda honeymoon Bahamasโ€ฆ.halafu tunaenda Taiwan shopping ya fenicha, kisha Japan shopping ua electronics, halafu tunaenda Dubai nikununulie vito vya thamani
GIRL: Ooh my sweetheartโ€ฆhalafu tukitoka huko??
BOY: Tukitoka huko nachukua ndoo ya maji nakumwagia uzinduke usingizini na ndoto yako imeishia hapo

Shopping Cart
16
    16
    Your Cart
    ๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About