Vihoja Vya Msimu
Ungekua wewe ndio boss wa huyu jamaa ungempa kazi? Ungemjibu nini?
*Boss*:-kijana unataka nini ndani ya ofisi zangu?
*Jamaa*:-Samahani naomba kazi ya ulinzi ndugu.
*Boss*:-umesoma mpaka wapi?
*Jamaa*:-mpaka form four.
*Boss*:-unajua kingereza?
*Jamaa*:-kwani hao wezi wanakuja na wazungu???.
😅😅😅😅😅😅
Sio kwa wivu huu
Wanawake nilianza kuwachukia tokea shule ya msingi.
Ni pale mwanamke wangu aliponiacha na kwenda kwa jamaa mwenye kichongeo kipya …inauma sanaa…
WANAWAKE SIO WATU WA MCHEZO MCHEZO ASEEE Bac tuu
Huyu mtoto kaongea point kweli, angalia anachomwambia baba yake
Mtoto alimwuuliza baba yake,
Mtoto: Baba unaweza kumwachia hilo gari lako house boy/girl akaliendesha?
Baba: siwezi kumwachia gari langu hili aliendeshe ni ghali sana.
Mtoto: je mnaweza kumwachia chumba chenu house boy/girl kikiwa wazi na mkaenda kazini?
Baba: haiwezekani kamwe kuna vitu vya gharama na pia heshima haitakuwepo.
Mtoto: unaweza ukampa house boy/girl ATM CARD yako na namba ya siri ukakuchulie pesa?
Baba: mtoto unatafuta balaa sasa, unataka siku akiiba hii card akachukue pesa zote tuwe maskini, sithubutu.
Mtoto: aahaaaaaa, kumbe hauwezi kumkabidhi chochote chenye thamani house boy/ girl, sasa kwa nini mnanikabidhi mimi kwa house boy/girl na nyie mnaenda kazini mpaka mnarudi kumbe mimi sina thamani kwenu eeeeh!
Mzee wa kichaga na hela zake. Angalia anachofanya
Mzee moja alikuwa kila usiku anapita mbele ya bank anasimama,kisha anapiga honi,akitoka askari mlinzi,anaondoka.Hilo jambo likamkera sana askari mlinzi, askari akawa na mvizia yule mzee wa kichaga ,siku alipokuja tena akamkamata, akamuuliza kwa nini unakuja unapiga honi kisha unakimbia? Mzee akasema: Haki ya mungu babaangu , Nina pesa zangu ktk account hapa bank naogopa usilale usingizi ndo maana kila siku usiku napita kukuangalia kama umelala!!
😂😂😂😂😂😂
Madhara ya kubeba nauli kamili tuu. Cheki kilichonipata
Kubeba nauli kamili nayo ni shida
Yani nimepanda daladala
Kondakta mmoja akaingia kwenye Gari amevaa suti za blue za daladala na miwani Kisha akakusanya pesa Gari Zima alafu akakaa siti ya nyuma baade Kondakta mwingine akaanza kukusanya pesa watu wakalalamika na kusema tayari tumelipa na kumuonyesha tuliemlipa Kondakta akacheka na kusema huyo tuliemlipa ni kipofu na alikuwa anaomba msaada..!!
Tofauti kati ya Binti wa Kizungu na Binti wa Kibongo mwanamme anapotoka kuoga
Tofauti ya Binti wa Kizungu na Binti wa Kibongo pale ambapo Mwanaume wake atokapo kuoga.
Binti wa Kizungu: Baby you look nice and fresh.
Binti wa Kibongo: Naona safari imeiva, Mwanaume hupumziki kama nesi wa zamu
😆😆😆😆
Ujanja alioutumia msichana wa kazi ili apandishiwe mshahara na mama mwenye nyumba
Msichana wa kazi alitaka mama mwenye nyumba ampandishie mshahara….. Mama mwenye nyumba akamwambia msichana ampe sababu tatu za kutaka kupandishiwa mshahara.
Msichana: Napika vizuri kuliko wewe.
Mama: Nani kakuambia?
Msichana: Baba kaniambia.
Mama: ok. Sababu ya pili?
Msichana: Napasi nguo vizuri kuliko wewe
Mama: Nani kakuambia na hili?
Msichana: Baba pia kaniambia
Mama: ok, na sababu ya tatu?
Msichana: Najitahidi kitandani kuliko wewe.
(Hapa mama kaonekana kutaka kujua zaidi na akawa tayari kujiandaa kumrukia akate kichwa cha binti mara moja)
Mama: Mume wangu kakuambia na hili pia?
Msichana: Hapana ni Shamba boy kaniambia mimi najitahidi kitandani kuliko wewe.
Mama: Tafadhali punguza sauti baba yako asisikie. Nitakupandishia mshahara wako mara tatu…….
Je, hili nalo ulilipitia ulipokua Shuleni?
Hakuna Kitu Kilikua Kinaniumizaga Kipindi Nipo Shuleni.
Time Mmetoka Kwenye Mitihani Wa Mathematics Halafu Mpo Kikundi Fulani Either Mnarudi Nyumbani Au Mnapumzika Kwa Ajili Ya Next Exam.
Unasikia Jamaa Wanabishana Pale Jibu Lilikua 4 Mwingine Anasema 5, Na Wewe Ulijaza 80.
SMS Mafua ndiyo hii
JE UMESHAWAHI KUONA SMS MAFUA?
Cheki hii hapa……..
“Mabo dugu yagu mziba? Bwada nasubuliwa sada na bafua baka dashindwa kuadika beseji do hayo dugu yagu.
Diobeeni dipone
😂😂😂😂😂😂😂😂
Hapana Chezea
Bafua
Jinsi Baba na mtoto wanavyoweza kuwaziana
Duh! Maisha
Ile time unawaza baba angekua MO DWEJI baba ako na ye anawaza mwanangu angekua MBWANA SAMMATA
Ni shetani tu anajaribu kucheza na akili zenu
😂😂😂😂
Hawa wanaume wanaopenda wanawake hovyo barabarani wamepatikana, hawatarudia 😂😂😂
Marafiki wawili (Jose na Ben) walikuwa wanatembea mtaani akatokea mwanamke akarusha busu kwa mmojawapo kupitia dirishani katika jengo la ghorofa tatu.
Wakaanza kujadiliana kama ifuatavyo:
Ben: Muone yule mrembo amenirushia busu
Jose: tafadhali achana na huyo mwanamke, usimjali..
(baadae yule mwanamke akamuashiria aende)
Ben: yule mwanamke ameniita!
Jose: Rafiki yangu, usiende. Nakutafadhalisha.
Ben: Kwa nini unaniambia nisiende Wakati mrembo kama yule ananiita? Huo ni wivu
Jose: Ben, Ninakutafadhalisha tena, usiende, tafadhali usiende kule (akihisi kutotiliwa maanani)
(Rafiki yake alimpuuza na alienda kwa yule mwanamke, mwanamke alishuka kukutana naye na wakapanda juu. Ghafla wakiwa wanataka kuanza taratibu za kula uroda, wakasikia mlio WA gari getini).. 🔊🔊
Lady: _(akiangalia kupitia dirishani)_
Oooh! Yule ni mume wangu!!
Ben: Mama yangu !
Nipo matatani, kweli ? ..!!
Lady: Usiwe na khofu, jifanye kuwa Dobi na anza kupiga pasi hizo nguo
(akimuonyesha lundo la nguo)
(Ben alitumia masaa matano kukamilisha kunyoosha zile nguo kwa sababu yule mume hakutoka tena siku ile)
(Siku iliyofuatia Ben alikwenda kwa Rafiki yake)
Ben: Kaka, unaweza kuamini Jana nimepiga pasi nguo kwa masaa matano???
Jose: Lakini nilikwambia usiende. Nguo zote hizo ulizonyoosha, Nilizifua Mimi Juzi!!
😂😂😂😂😂😂😂😂😂
When an experienced person speaks … 👂you must listen..!
Cheki wanachokisema vichaa baada ya kuona ndege inapita angani
Vichaa wawili walikuwa wamekaa sehemu ghafla ikapita ndege angani kichaa mmoja akasema ndege ile hitakua imembeba rais kichaa mwenzake akajibu hapana ile imebeba wazungu kama ingekuwa imembeba rais ungeona mapikipiki mbele
Hapo sasa patamu, cheki jamaa alivyowezwa na huyu dogo
Mfugaji mmoja alikwenda kwa mfugaji mwenzake (ambae pia ni bwana mifugo wa eneo lao) asubuhi moja. Alipobisha hodi mtoto wa kiume wa umri upatao miaka 12 akamfungulia mlango. Mazungumzo yafuatayo yakafuatia:
Mkulima: Baba yako yupo?
Mtoto: Hapana Mzee, amekwenda mjini.
Mkulima: Mama yako?
Mtoto: Nae kaenda mjini na baba.
Mkulima: Kaka yako Howard yupo?
Mtoto: Nae hayupo, wote yeye, baba na mama wamekwenda mjini. Kwani una shida gani? Kama kuna kitu unahitaji niambie maana nimeachiwa funguo na najua vifaa vinapowekwa.
Mzee akawaza kidogo halafu akasema: Kwa kweli nilitaka kuongea na baba, mama au kaka yako kwa kuwa kaka yako amempa mimba binti yangu.
Mtoto akafikiria kidogo halafu akasema: Kusema ukweli itabidi umsubirie baba, ila kwa kukusaidia ni kuwa baba hulipisha shilingi laki moja kwa kupandisha dume la ng’ombe na elfu hamsini kwa beberu. Ila sijui baba hutoza shilingi ngapi kwa Howard akifanikiwa kutia mimba.
Kingereza sio mchezo, angalia huyu anavyojichanganya
Jamaa fulani alikuwa ame2lia beach mzungu akapita akamuliza “Are u relax ? Jamaa akawa hamuelewi akamjibu No! Mzungu mwengine akapita akamuliza vilevile akajibu No!
Akaona hapa anasumbuliwa akasogea mbele kidogo ya maji akamuona mzungu mmoja alikuwa ame2lia. Akamuliza “are u relax? Mzungu akajibu yes jamaa akamkata makofi mawili na kumwambia kumbe we ndo relax inuka unatafutwa na wenzako…..Shenz mkubwa mie nasumbuliwa na wenzako kule we umejikausha!!
Jinsi nilivyogundua kuwa nina kipaji leo
LEO NIMEPITA MTAA FULANI NIKAKIMBIZWA NA MBWA, NDIO NIKAJUA NINA KIPAJI KINAPOTEA TU………
SIO CHA KUKIMBIA, NI KUPIGA KELELE😆😆😆😆😆😆
Cheki tabia za kuandika vimaneno vya ajabuajabu kwenye pikipiki na bodaboda ilivyomponza huyu
Jamaa mmoja dereva wa bajaji alianguka, sasa bajaji ikawa imem’bana akawa anafurukuta bila mafanikio Cha ajabu watu wakawa wanampita bila kumsaidia, Kumbe Nyuma ya Bajaji yake alikua Kaandika “NIACHENI KAMA NILIVYO, HII NDIO STYLE YANGU” 😂😂😂 Mpaka sasa nimemwacha bado yuko hapo *Sipendagi Ujinga mimi* 🚶🏽🚶🏽🚶🏽🚶🏽🚶🏽
Misemo ya kina dada
Misemo ya kina dada
walianza na halohalooo!
Wakaja unalo babu weee!
Ikafuata utajijuuu!
Ikafupishwa utajiJJ!
Mara ghafla kantangazeee!
Haikukaa sana kansajiriii!
Ikatoka nyingine nishiiiiida!
Unaijua iliyotoka Leo?
Heh! Heh! Heeeh! MB zenyewe 8 nikudownload unanini?
Recent Comments