Vihoja Vya Kukuparaha
Kilichotokea baada ya bibi na babu kukumbukia mahaba ya ujanani
Mzee wa miaka 60 alimwambia mkewe, leo nataka tukumbukie enzi zetu kutongozana, mke akajibu sawa, inabidi unisubiri mwembeni saa 1 usiku nitapita, mzee akafika saa 1 alikaa hadi saa 5 usiku, aliporudi nyumbani akamuuliza mkewe kwa hasira; sasa tumepanga nin halafu haujatokea ?
Mke; leo mama alinikataza nictoke nyumbani usiku nijisomee ! Babu hoiiβ¦
Wadada lenu hili. Mimi sipo
Wadada kama una sura mbaya subiri NEEMA YA BWANA..Sio kutuambia mna uzuri wa Ndani usioonekana..Sisi ni Wanaume,Sio MINYOO
ππππ
Sababu ya watu kupenda mapenzi kuliko vita
Mwalimu aliuliza swali
“Kwanini watu wanapenda MAPENZI kuliko VITA?
Mwanafunzi mmoja akajibu:-
“Kwa sababu CONDOM ni bei rahis kuliko BUNDUKI.
Wanafunzi wote: Ndioooooβ¦!!
Eti kwa nini Watu hawapostigi hii? Hata selfie sijaonaga
Vijana mkiwa mnaendesha magari mna post mukiwa mpo beach mna post mkiwa kwenye masherehe mna post Lakin mkiwa mmeenda kwa mganga siwaoni kupost mitunguli na vibuyu vya mganga unakuwa je wa zee tena. ππππ
Jambo la kufanya ukitaka mwanaume akusaidie kazi jikoni
Fanya hivi
Ukitaka mwanaume akusaidie kazi jikoni mwambie “NAOMBA CM YAKO NIWASHE TOCHI TAA IMEUNGUA”
atakusaidia kumulika mpaka unamaliza kazi zako zooteπ
Kilichotokea kati ya mkaka na mdada walipokutana hotelini
Mkaka aliingia kwenye hoteli moja akaketi meza moja na mdada mrembo maarufu sana;
MKAKA: Samahani dada sijui saa ngapi?
MDADA: Nani kakwambia saa yangu ndio ya kuangalia kila mtu?
MKAKA: Samahani sanaβ¦.jamaa akachukua Galaxy yake akapiga simuβ¦.aise saa ngapi saa hizi? mi ndio nimeingia toka USA nataka kurekibisha saa yangu ifwate muda wa huku. Na wewe uwahi kuchukua iPad nimekuja nazo tatu tu za zawadi. Halafu ntafutie mtoto mzuri nimumwagie midola niliyokuja nayo, ok ciao tuonane badae.
MDADA: Kaka samahani saa hizi ni saaβ¦..
MKAKA: Achana na mimi wewe
Ha ha ha ha haaaaa!!
Kifahamu Kidada kimbea kilichofukuzwa kazi
Unafahamu?
Kile kidada kimbea kinachosemaga salio lako halitoshi kimefukuzwa kazi saivi kupiga simu ni bure mjulishe na mwenzako
π² π²
Utani kwa wadada wembamba
πππππππππππ
Wadada wembamba hebu nenepeni basi mnatupa tabu kusoma maneno ya kwenye kanga jamanii β¦β¦β¦mnaviringisha kanga mwili mara 3 mpaka maandishii hayaonekanii
π€£π€£π€£π€£
Angalia kilichomkuta huyu msanii wa mziki na mashabiki wake
Msanii mmoja anaitwa ”KINYA” alikuwa ana perfom jukwaan..!!!
Kawaida kila msanii lazima ajitambulishe, mfano:-
”YEAH NI TEMBA hapa au
YEAH NI CHEGE hapaβ¦!!!
Yeye akasema: “YEAH NIKINYA HAPAβ¦!!!”
Watu wakapiga kelele ”UTAZOAAA” mwenyewe bwenge wee
JE, WEWE UNGEJITAMBULISHAJE NAITAJI JIBU LAKO TUONEβ₯
Kapresha kakiamua kuja kanakujaga tuu, cheki kilichompata huyu mme wa mtu mpenda michepuko
Kimchepuko chako kinakuandikia meseji kama hiiβ¦
β¦Samahani baby kama unavyojua nimeokoka ,nimetubu kanisani lakini nabii kaniambia niwaombe msamaha wote niliowakosea.
Nimemkosea sana mkeo kwa kumwibia mumewe na nimepanga kuja kumwomba msamaha kesho ntakuja na nabii na Mchumba wangu mpya nilie mpata kanisani.
Samahani kwa usumbufu uliojitokeza lakini hilo ni kwa ajili ya utukufu wa bwana!!!
Wako Manka wa Magorofaniπ π
Madenge hakosi visa. Soma hii
MADENGE
HAKOSI
VISA
baada ya kumaliza form four baba akamwambia achague zawadi yoyote aipendayo
MADENGE: naomba pesa nikamuoe bibi maana siku nyingi amekuwa akiniita mchumba wake.
BABA: Shenzi, yule ni mama yangu mzazi huwezi kumuoa.
MADENGE: Mbona wewe umemuoa mama yangu mzazi sijasema kitu ww inakuuma? lazima nilipize kisasi ikikuuma muache mama yangu kila mtu akae na mamayake. πππ
Swali la kizushi kwa wadada wanaovaa mawigi
Hivi wadada mnaovaa mawigi.
ππ½Β Utajisikiaje siku Boyfriend wako anaingia chumbani halafu anatundika NDEVU kwenye hengaπ€£
Cheka kidogo, angalia anachosema huyu mchaga
Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?
MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee.
MALAIKA: Kwa nini?
MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni.
Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?
Kali ya mwaka iliyotokea Benki Baada ya wezi kuiba
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuniβ¦unaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuniβ¦ππππ
Analia kilichompata huyu jamaa baada ya kubadili jinsia yake kichawi
Jamaa alimpa ujauzito mwanafunzi akashtakiwa kumbe yule jamaa ana bibi yake mtaalam wamambo yetu ya Jadiβ¦
Jamaa akaongea na bibi yake amuwekee jinsia ya kike ili akashinde Mahakamani na akitoka arudishiwe mambo yake kama kawaida.
Bibi akampachika jamaa jinsia ya kike alipofika mahakamani kuhojiwa akasema mi sijampa ujauzito kwasababu minina jinsia ya kike piaβ¦!
Kwa kuthibitisha akajifunua nguo, basi jamaa akashinda kesi.
Jamaa akawa anarudi Home, lakini wakati anakaribia kufika akaona watu wengi wamejaa home wanalia akauliza kulikoni akaambiwa “Bibi amefariki”!
Vuta picha hapoβ¦!!!
Kilichotokea baada ya babu mzee kuibiwa nauli kwenye daladala
Mzee mmoja alipanda Gari Stend;
Wakati wa kugombania Siti,
Akaibiwa Nauli.
Akasimama katikati ya Gari-Akasema; “Jamani Naomba Aliyeniibia Pesa yangu Arudishe Haraka,
Tena Fasta kabla Sijafanya Tukio kama Nililofanya 1977″
Abiria kuskia hivyo wakaogopa.
Ikabidi Mwizi Ajitokeze,
Akarudisha Pesa na Kuomba Msamaha! Mtu Mmoja akauliza,
Mzee,
Kwani 1977 Ulifanya nn?
Si nilienda kwa Miguu mpaka Nyumbani!
Uscheke Peke Yako, wa2mie na wengine ili nao wacheke!
Hali za ndoa
Kuna kijana alikua anajua kuwa mke wake
anatoka nje ya ndoa basi akamwuliza mke,
mkewe akakataa, akamwambia baba yake
akaambiwa na babaake tulia mwanangu ndoa
zina mengi! akawa kila siku analalamika kwa
babaake, mwisho babaake akamwambia basi
ntakusaidia. Itabidi ujifanye unaumwa sana hoi
hujiwez halafu nitakuonyesha jawabu!
Basi kijana akajifanya anaumwa mzee akaitisha
kikao cha ndugu wote pande 2,
Mzee akaanza kueleza jaman kijana wetu
anaumwa amepata ugonjwa wa utata hospital
zote umeshindikana hivyo tumeenda kwa mganga
wa jadi amenipa dawa na ina masharti, inatakiwa
atakaye iandaa hii dawa awe mwanamke mwenye
ndoa ambaye hajawah kutoka nje ya ndoa tangu
alipoolewa ndo kijana wetu atapona!
Kama ametoka nje ya ndoa asiandae dawa hii
kwa sababu tukimpa kjana wetu watakufa wote!
Je kina mama nani ataandaa? Walitoka nje
wamama mmoja mmoja hadi mkewe na mamake
mzazi wakatoka, akafata mama ake kijana,
mashangazi na dada zake, mwisho wakabakia
wanaume peke yao! Mzee akamwambia
mwanangu umeona hali za ndoa zilivyo?
Acha kujisumbua tulia na mkeo nadhani
umejionea hali halisi.
Cha zaidi omba Mungu sana juu ya ndoa yako!
Kijana akazimia!
SOMA TENA KISHA MTUMIE NA MWENZIO.
Januari kweli ngumu, soma hii
Januari kweli kiboko
Hii january sabuni za kuogea ni zile za kuoshea vyombo, yani unakutana mjini na mtu ana mchicha shingoniβ¦π



















I’m so happy you’re here! π₯³


























































Recent Comments