Vichekesho vya Zuzu
Angalia wanachokifanya Zuzu na msichana chumbani kwenye giza
Zuzu: Mambo Anna!
Anna: Poa!
Zuzu: Kuna kitu nataka nikuonyesheโฆ
Anna: Kitu gan?
Zuzu: Twende chumbani kwako (wakaenda)
Anna: Haya nionyesheโฆ
Zuzu: Funga mlango na madirisha kwanza (akafunga)
Anna: Haya nionyeshe sasa!..
Zuzu: Zima taa kwanza (akazima)
Anna: Mhmโฆnionyeshe sasa!
Zuzu: Haya njoo hapa kitandaniโฆ
Anna: Ok, nionyeshe!
Zuzu: Ona nimenunua saa ambayo inawaka yenyewe gizaniโฆ Acha mawazo mabaya ww???
Angalia huyu mwanafunzi anachomjibu huyu mwalimu wake
1. Ticha:”Punda ni mnyama anaefugwa nyumbani,lakini akiwa mwituni anaitwa pundamiliaโฆ.Je sungura anayeishi mwituni anaitwaje?”
ZUZU:”Sunguramilia.”
2.Ticha:”Rais wa kwanza wa kenya aliitwa KENYATTAโฆJe rais wa kwanza wa
Tanzania aliitwaje?”
ZUZU:”TANZANIATTA.”
3. Ticha:”Kuku yuko katika jamii ya NDEGEโฆJe samaki yuko katika jamii ya nini?”
ZUZU:”MELI.”
4. Ticha:”Coach wa Arsenal anaitwa ARSENE,wa Man-city anaitwa MANCINIโฆ.Je wa
Liverpool anaitwaje?
ZUZU:”LIVER.”
5 Ticha:”Ukiwa na mbuzi 10,wezi waje waibe 5,utabaki na nini?”
ZUZU:”Hasira nyingi sana!”
Kwa nini vitu vunavyoanza na “K” ni vitamu sana?
Zuzu kaniuliza, “Anko, unajua vitu vinavyoanzia na K ni vitamu sana.”
Nikashtuka, “Astaghafilulah we mtoto! Niondolee wehu wako hapa!”
Zuzu akatabasamu. Akaendelea kuongea kabla sijafanikiwa kumzuia. “Kweli kabisa anko. Vitu vinavyoanza na K ni vitamu sana kwa mfano kuku, kalimati, keki, kabab, katleti, kashata, kisheti na karoti.”
Nikashusha pumzi. “Ahaa! Kumbe ndo hivyo, ni kweli!”
Zuzu akanitupia swali. “Kwani we anko ulidhani nini?”
Huyu dogo nimsaidieje? Cheki alivyojichanganya
Nimekutana na dogo mmoja hivi hapa analia,namuliza analia nin??ananambia ”ALIPEWA MIA TANO ZIPO MBILI,MIA TANO MOJA YA NYANYA na MIA TANO NYINGINE YA VITUNGUU sasa KAKOSEA KAZICHANGANYA HAJUI TENA IPI NI YA NYANYA na IPI NI YA VITUNGUU!!!
.
.
NA PESA ZOTE ANAZO KAZISHIKA MKONONI,
Angalia huyu demu alivyo mbulula
Jamaa aliamua kumtoa demu wake out kwaajili ya chakula cha usiku kufika hotelini wakakaa mezani mhudumu akaja,
Mhudumu: kaka nikuhudumie nini,
Jamaa: afathal NILETEE MENU LISTI
Mhudumu: dada na wewe?
Demu akajibu kwa pozi tena kwakujishaua, “NA MIMI NILETEE MENU LIST ILA USIWEKE CHUMVI NYINGI”
Chezea mbulula weweโฆ!!!
Huyu jamaa bonge la bwege, ungekua wewe ndiyo rafiki ake ungemwambiaje?
RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu
JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu
RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana
JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana
ananificha, mi naita huu ni usaliti wa ndoa.
RAFIKI: Nini tena?
JAMAA:Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia
RAFIKI: Kitimoto? We umejuaje?
JAMAA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kwenda kazini, simu ya mke wangu ikalia, nikaamua kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya mwanaume mmoja akauliza, โHuyo nguruwe umeshamuondoa?โ Hebu we fikiria nilivyoshtuka, yaani mpaka sasa nashindwa kuamini kuwa mke wangu ananizunguka anafanya biashara ya nguruwe hajaniambia hata siku moja
Wavuta bangi wa Colombia watoa mpya
Asubuhi ya leo huko nchini Colombia baada ya serikali kuidhinisha matumizi ya bangi kuwa halali +++ Wavutaji bangi wamepanda basi la gorofa wengine juu wengine chiniโฆ.
Waliopanda chini wanawauliza wa juu huko speed ni ngapi maana huku ni 80.
Wajuu wakajibu huku mpaka sasa hatujui dereva bado hajajaโฆ. ๐๐๐
Sababu ya jamaa kujiita fara ugenini
MZEE:”sasa huyu mgeni sijui alale wap?”
MKE:”saa hizi ni usiku akalale na Bebi.”
jamaa akaona huyo Bebi pengne mtoto anakojoa kitandani au akalia asije msumbua usiku
JAMAA:”msipate tabu mi ntalala hapa kwenye kochi” akalala
asubh wanakunywa chai akaibuka mrembo,jamaa akapigwa bumbuwazi almanusra ajimwagie chai.
BINTI:”Naitwa BEBI,we unaitwa nani?”
Jamaa akasema mimi naitwa Faraโฆ..!
Bangi si mchezo, Angalia kilichowakuta hawa
Bangi si mchezo!
Jamaa kaikoleza si ikamtuma avue nguo!
Akavua nguo zote akaenda kwenye kioo, kujitazama akaona kama kavaa suti!
then akaenda kama alivyo zaliwa kwa masela wenzake akawauliza vp suti imenikaa? Mvuta bangi mwenzie akamwambia “imekutoa kinyama ila tai umeifunga chini sana”.
Recent Comments