Vichekesho Vya Wakaka Na Wadada

Mchaga mmoja kamtoa mke wake out mambo yakawa hivi

*Mchaga mmoja kamtoa mke wake out.*

*mchaga* : _chips yai bei gani?_

*mhudumu*: _elfu 2_

*mchaga* : _zina kachumbari?_

*mhudumu*: _ndio!_

*mchaga*: _kachumbari mnauzaje?_

*mhudumu*: _kachumbari ni bure._

*mchaga*: _ok basi naomba kachumbari sahani mbili, chips ziache tuuu_.๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ _SIPENDI UJINGA MIMI_๐Ÿ’ฅ

Hii ndiyo Ladha ya bia zote usiyoijua

Ladha ya bia ya 1 hadi ya 6..

Kwa wanywaji wazuri wa bia,

chupa ya kwanza ๐Ÿบ huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza kooโ€ฆ Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.

chupa ya pili ๐Ÿบ๐Ÿบ kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihiโ€ฆ.

Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Yanga bila kukosea.. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.

Bia ya tatu ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sanaโ€ฆ. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokezaโ€ฆ..

Bia ya nne ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikiaโ€ฆ.. bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.

Bia ya tano ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipuโ€ฆโ€ฆna kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; โ€˜Mi sipendwi mpaka leo sijaolewaโ€™ au โ€˜ Mume wangu sijui yukoje hanijaliโ€™

Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.

Kuanzia bia ya sita ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. โ€ฆโ€ฆ. โ€ฆKuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo fala na hajui kuendesha kampuni.

Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjikaโ€ฆโ€ฆ.

Ulevi noma! Angalia huyu mlevi alichomfanyia huyu jamaa usiku! Ungekua wewe ungefanyaje?

Jamaa alikuwa amelaa na mkewe saa tisa ya usiku akastuka baada ya kusikia mtu anabisha hodi kwenda kufungua mlango
Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao
JAMAA: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
MLEVI: Naomba uje unisukume.
Jamaa akiamini kuwa pengine kuna gari la huyu mlevi limezima jirani akamwambia subiri nikavae viatu. Baada ya kuvaa viatu akatoka na wakaanza kusindikizana na mlevi. Mlevi akaongoza njia
mpaka kwenye mabembea ya jirani akakaa kwenye bembea moja na kumgeukia jamaa na kumwambia.. Okay nisukume basi.

Utajuaje kama unachoangalia ni filamu ya kibongo!!!!

Angalia hivi

-Mlinzi wa Getini lazima awe chizi
-Mtu yupo kijijini, maisha magumu ana Wave
kichwani.
-Kama bosi atakuwa na kampuni basi ni lazima
itakuwa ya Clearing and Forwading au ya uuzaji
Magari.
-Lazima waende Kununua nguo.
-Jambazi lazima avae koti lefu jeusi na Miwani.
-Mtu akichapwa kofi huangukia kwenye kochi
ama kitandani.
-Actress huwa hawapiki hata chai.
-Kwa mdada akiishi maisha ya kitajiri lazima
avae nguo inayoishia mapajani.
-Actress even after 5 yeas utakuta staili ya
nywele na rangi za kucha ni zile zile.
-Anaweka Sumu alafu anaonja kama imekolea.
-Movie zote wapenzi huitana Baby..
-Main actor wote ni wafanya biashara na lazima
wataongelea mizigo kutoka bandarini.
-Wakinywa Soda basi lazima wabakishe.

Jinsi ya Kubana matumizi X-mass

Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.

๐ŸŽ€โœจMarry Xmas & Happy new year.โœจ๐ŸŽ€

Ameniomba nimfungulie akaunt facebook cheki nilichomjibu

Leo nimechoka zangu alafu shangazi amekuja anataka nimuunganishe facebook. Imebidi nimwambie
lazima awe na picha passport size 4 kwaajili ya kuweka profile picture, barua kutoka kwa afisa mtendaji na Atm card ya nmb bank. Alafu awe na marefa wanne ambao wamekuwa facebook for more than 3 years. Amesema
hataki tena kujiunga fb!

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Saa ivi niko zangu nimelala naendelea kupunguza uchovu

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About