Vichekesho Vya Kukuchekesha
Usichokijua kuhusu shamba lako
Je wajua?.. Shamba lako likipatikana na dhahabu ni mali ya serikali..ila likipatikana na bangi ni mali yako
😂😂😂😂
Je, hili nalo ulilipitia ulipokua Shuleni?
Hakuna Kitu Kilikua Kinaniumizaga Kipindi Nipo Shuleni.
Time Mmetoka Kwenye Mitihani Wa Mathematics Halafu Mpo Kikundi Fulani Either Mnarudi Nyumbani Au Mnapumzika Kwa Ajili Ya Next Exam.
Unasikia Jamaa Wanabishana Pale Jibu Lilikua 4 Mwingine Anasema 5, Na Wewe Ulijaza 80.
Duh! Tamaa mbaya, cheki kilichompata Huyu
HAHAHAHAHAAAAAA DUH TAMAA MBAYA
Muokota makopo katika uokotaji wake wa makopo akaona chupa ambayo ndani kuna ki2, alipoifungua likatoka jitu la ajabu. Huku akitetemeka lile jitu likamwambia kijana asante sana kwa kuniokoa omba vi2 viwili sasa hivi. Kijana kwa hofu akaomba pesa za kumiliki magari na majumba ya kifahari. Ghafla fuko la hela na pete ya bahati vikadondoka. Akaambiwa ombi la pili,akasema nibadilishe niwe kivutio ili nipendwe sana nakina dada Hapohapo akageuzwa akawa chipsi yai.!!😂🤣🤣🤣
Kilichotokea baada ya mzungu na mbongo kukaa siti moja, bongo wasanii wengi
Mzungu akamdharau sana Mbongo nakujiona anajua kila kitu duniani!,
Akamwambia Mbongo waulizane maswali na Mbongo akishindwa anatoa sh.500 na endapo yeye atashindwa atatoa 100,000/=.
Mzungu akauliza ni nchi ipi ilishindwa kwenye vita kuu ya kwanza ya Dunia?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hajui.
Na yeye akamuuliza Mzungu ni kitu gani kikienda juu kina miguu minne na kikirudi chini kina miguu mitatu?
Mzungu akafikiria akakosa jibu akatoa 100,000/= kuashiria hajui ila akataka kujua, akauliza ni nini hicho?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hata yeye hajui!.
SHARE na marafiki kama umemkubali Mbongo kwa ujanja. Lakini unafikiri Mbongo huyu kwa akili hizi atakuwa ametokea mkoa gani!?.
Huyu jamaa kawaweza wapenda vya bure
Jamaa kaingia mgahawani kwa fujo
JAMAA : Nipe soda moja na kila mtu mpe yake maana ninapokunywa soda napenda kila mtu anywe
WATU : Ha! Ha! Ha! Haaaa!
JAMAA : Nipe mchemsho na kila mtu mpe wa kwake maana ninapokula mchemsho napenda kila mtu ale wake
WATU: Watu weweeee! Tena safari hii Na makofi juu..
JAMAA : Mhudumu, nipe bili na kila mtu mpe yake maana ninapolipa bili napenda kuona kila mtu analipa yake
😂😂😂😂😂😂😂
Angalia nilivyoingizwa mjini na ujanja wangu wote
Ndio nilikuwa nimeshuka kwenye basi la SAI BABA pale Ubungo, nina Begi kubwa Mgongoni na begi Dogo la Lap Top mkononi, sura inatazama Mbele Very Serious kama nipo kwenye Gwaride la Uhuru!..Mabega juu yanafanya Cheers na Mawingu!, natembea kwa madoido…..leo nimetoka Likizo Moshi,
“Brother Simu ya ukweli hii..kitu cha Tecno C9 bei poa” hii ilikuwa sauti ya Teja mmoja hivi!
Yaani huyu Teja Bwege kweli,anataka kumuuzia nani sabuni? mimi sio wa kuja!…kamwe Siwezi kuibiwa hapa Town,hakuna wizi au utapeli nisioujua!, Mimi nimezaliwa Mwananyamala kwa Manjunju, nikalelewa Tandale kwa Mtogole, Shule ya msingi nimesoma Turiani Magomeni, Hivi Mbwa gani aniibie?…kwa Style ipi?
Sipendi kabisa Upuuzi!, Wajinga ndio wataibiwa, sio Mimi!…sasa Kwa mwendo wa haraka nikatoka nje kabisa ya Stendi ya Ubungo straight mpaka Stendi ya dala dala za Kariakoo, hapo ndipo nikakutana na Vijana wawili wadogo wakiwa na mzani wa kupimia uzito,…hakika napenda sana vijana wanaojituma kama hawa na sio ile Mijizi ya kule ndani Stendi!!,….hapa sasa nikapata wazo!
“Dogo mnapima uzito kwa shilingi ngapi?”
“Mia mbili tu Kaka!”
”Ok”
Kwa mwendo wa kikakamavu nikapanda juu ya mzani,lengo hapa ni kujua uzito wangu, Mtori niliokula mwezi mzima kule kwa Mshekuu sio mchezo, hapa nahisi nacheza kwenye kg za John Cena,
“Mama wee! Dogo mzani mzima huu kweli? Mbona nina kilo 134?” (Nilihamaki)
“Aaah! Brother huoni umepanda na Mabegi juu ya mzani?”’
Hahaha! kweli nimechanganyikiwa!…Sasa nikatoa mabegi yote mawili na kurudi juu ya Mzani, hapa ndipo Uzito ukashuka kutoka kg 134 mpaka kg 56!…My God kweli Body la “One Pack ” haliongopi! thats means mabegi yaliniongezea kg 78! duh hii ni hatari!
“Yaani we Dogo kitambi chote hiki kg 56? huu Mzani Mzima kweli?”
Kimya…
“Dogo huu Mzani vipi?”
Kimya…
Dogo ana dharau huyu!…Sasa ndio nikabandua macho yangu toka kwenye kioo cha mzani ili nimtazame huyu dogo asiyejibu!….ndipo macho yangu yakakutana na Kigoda tupu kilichochongwa Mvomero!…Dogo hakuwepo!….na Mabegi pia hayapo!…lap top haipo!….NIMEPIGWA!
Ni dhahiri watoto wa Mjini walikuwa wameniacha juu ya Mzani, wamechukua Lap top ya Milioni na wameniachia Mzani chakavu wa elfu 40, what a stress!….sasa nilirudisha macho kwenye kioo cha uzito na sasa kilisoma KG 38!…yaani dakika hii hii nimepungua kilo zingine 18, Hakiyamama nahisi hata utumbo wangu wamebeba!…niitieni Ambulance!
🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼
Angalia huyu mvulana anachomwambia huyu daktari baada ya rafiki yake wa kike kupata ujauzito
😂😂😂😂
MVULANA: Daktari, rafiki yangu wa kike ni mjamzito, lakini mara zote nimekua nikitumia kinga. Inawezekanaje hii?
DAKTARI: Ngoja nikusimulie hadithi. Kulikua na Muindaji ambaye alikua anabeba bunduki kila aendako. Siku moja, alichukua mwamvuli badala ya bunduki na akaenda nayo. Ghafla akatokea Simba mbele yake. Ili amtishie Simba, muindaji akatumia mwamvuli na kummiminia risasi Simba. Simba akafa palepale!
MVULANA: Sio kweli!! Lazima kulikua na mtu mwengine pembeni aliyempiga risasi Simba.
DAKTARI: Nashukuru umeelewa somo!!😂
😂😂😂😂😂😂😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃
Dingi kauzu kuliko wote duniani ndiyo huyu hapa
Mtoto: Baba nitumie pesa ya matumizi huku shuleni hali ni mbaya sana la sivyo najinyonga.
Baba: Huku nyumbani hali ni mbaya kuliko huko shuleni kwahiyo kama unajinyonga utapunguza Bajeti, kopa Kamba dukani kwa Mangi nitalipa nikija kuchukua Maiti yako, Mungu akulaze mahali pema peponi Mwanangu…..
Gari na mke nini muhimu?
GARI YA MILIONI 50
UNALAZA NJE…
mke wa laki sita
unalala nae ndani….
BANGI SI NZURI JAMAN
😂😂😂😂😂😂😂😂
Kiingereza kinashida kweli, Angalia alichokisema huyu mwalimu
Kiingereza shidaaaa……!
Mwalimu wa chakula alipokuwa anaongea na wapishi akiwaeleza maharage kutoungwa vizur
Tcha: these beans are not well connected,,😂😂😂
Huyu mama mkwe kazidi sasa
Eti kuna mkaka alitembelewa na mama yake mzazi. Wakiwa sebuleni yeye, mama na mke wake, mke wake akaanza kuonekana tofauti kama vile anajiskia vibaya. Akaenda chumbani. Baada ya muda mfupi yule mkaka akamfuata. Wakakaa sana huko kisha mkaka akarudi sebuleni kuendelea kuongea na mama yake. Lakini zipu ya suruali yake ilikuwa wazi. Mama akamuuliza, mkeo anaendeleaje? Akamuambia, anajisikia vzr sasa. Nimempa panadol. Mama akatabasamu na kumwambia mwanaye, sawa. Lakini siku nyingine ukishatoa panadol ukumbuke kufunga pharmacy😂😂
Huyu Jamaa ubahili umezidi kwa hiki anachomwambia huyu dada
Kama ni ubahili hapa umezidi
mdada Bby naomba hela nimpeleke mdogo wangu hospital kang’atwa na nyoka
JAmaa embu mpe huyo nyoka cm niongee nae.. maisha yanakaba..😂😂
Kuna watu makauzu ila huyu kazidi.. Soma hii!
Kakubaliana vizuri na msichana fulani hivi kuwa aibuke gheto, mchizi kajipanga vizuri kabisa…. mara saa nne hivi mdada kasema hana nauli.
Mshkaji kajikunja kamtumia Elfu tano maana mwenye shida alikuwa ni yeye……
Baada ya nusu saa yule dada akamtumia meseji.
“Jamani mpenzi, kumbe baba hatoki nilijua atatoka… sorry bae sitaweza kuja kwa leo… sooo sorry!”
Mshkaji jiii! hajajibu kitu…..
Baada ya muda kidogo meseji ikaingia katika simu ya binti, akajua mchizi kajibu. Mh! kutazama ni meseji kutoka Mpesa.
“CA90F0511 IMETHIBITISHWA Tshs 5000 ILIYOTUMWA KIMAKOSA KATIKA ACCOUNT YAKO IMETOLEWA SALIO LAKO NI Tshs 5”
Halafu ndo ikaingia meseji ya mshkaji.
“BASI POA SIKU NYINGINE KAMA VIPI”
#dada wa watu mashavu yakamshuka… hakuamini kilichotokea…. yaani jamaa keshawapigia Voda na pesa fasta imezuiliwa……
Cha kufanya mpenzi wako akikuacha
Kumkomoa…
MPENZI WAKO AKIKUACHA BILA SABABU CHUKUA SIMU MPIGIE MAMA AKE MWAMBIE MWANAO AMEKUFA UWEZI…. KULIA PEKE YAKO🤒
Kilichompata sista duu bishoo wakati akijidai kununua pete
Mwanamke mmoja aliingia duka la vito vya thamani, akaona pete moja ya dhahabu nzuri sana amabayo ilikuwa kwenye shelf ya chini, wakati anainama apate kuitazama vizuri kwa bahati mbaya (au nzuri!), shuzi likamtoka- druuuuuu, soni ikamuingia huku akigeuka haraka kuangalia kama kuna yeyote dukani pale ameliskia shuzi lake, macho yakagongana na mwenye duka ambaye alikuwa karibu huku uso ukiwa umejaa tabasamu zito, mwana mama hakuwa na uhakika kama amesikika au hakusikika, akaona atumie nafasi ile kuyeyusha…Akauliza “Hii pete bei gani?” . Jamaa mwenye duka, huku akiangua kicheko, akajibu “Umeiona tu umejamba, je nikikuambia bei yake si utakunya kabisa?”
Misemo 17 ya kuchekesha
1) gari la kuvutwa halina overtake
2) kisigino hakikakai mbele
3) wimbo wa taifa haupgwi disko
4) feni haiwashwi beach
5) mshkaki hauchomwi kwa jiko la ges
6) mganga haagiz tembele
7) hata bibi alikuwa bint
8) mke wa mtu sumu,mume wamtu maziwa
9) kipara bila pesa ni kovu
10) mbwa hanenepi migiuu
11) picha ya rais haina bodyguard
12) mjini shule kijiji tuition
13) saa ya ukutani haivaliwi mkonon
14) heshima pesa shkamoo makelele
15) ulinz pesa bastora mzgo
16) kuku ni kuku jogoo mbwembwe
17) kusoma kuelewa kukesha mbwembwe
Angalia sababu ya mwanamme kubadili jina na Kuitwa jina la kike, hii dunia ina mambo kweli
Rashidi alimpa ujauzito mwanafunzi, akashtakiwa.
Kumbe Rashidi ana bibi yake mtaalamu wa yale mambo yao ya Sumbawanga, akampachika Rashidi i jinsia ya kike.
Alipofika mahakamani kuhojiwa Rashidi akasema sijampa ujauzito kwa sababu mimi pia nina jinsia ya kike.
Kwa kuthibitisha Rashid wakaenda kumkagua basi akashinda kesi, kufika nyumbani Rashid akawakuta watu wamejaa wanalia, akauliza kulikoni?
Akaambiwa bibi yako amefariki. 😭😭😭😭😭😭😰😰😰😆😆😆😆😆😆
Kwa sasa Rashid anaitwa Leila😀😀😀
Baada ya kuulizwa nani anapenda kwenda peponi, haya ndiyo yalikua majibu ya wanafunzi
Wanafunzi waliulizwa na mwalimu nani angependa kwenda peponi? Wote wakanyosha ila mmoja tu alipokwenda nyumbani akamuelezea mamake, mamake akamuuliza je wewe ulinyosha mtoto hapana mama yule mama akamuuliza kwanini.
mtoto kwa sababu mama uliniambia nikitoka shule nije moja kwa moja mpaka nyumbani nisiende kokote
Angalia anachokisema Madenge sasa
MWALIMU kaingia darasani na kusema. “Wanaojijua wajinga wasimame”.
MADENGE akasimama peke yake.
MWALIMU: Wewe ndio mjinga?
MADENGE: Hapana, ila nimeona umesimama peke yako nikaona usijisikie vibaya angalau tuwe wawili.
Recent Comments