Vichekesho Vya Jumatano

Cheki huyu mzee alichomfanyia muuzaji wa pharmacy

Mzee kaingia pharmacy,
MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu naomba uonje nitakulipa
MFAMASIA: Kitu gani?….Mzee akatoa kichupa na kijiko akaweka …majimaji yaliyomo kwenye
kichupa kwenye kijiko na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia akatia yale maji mdomoni na kuyazungusha zungusha mdomoni akionja;

MZEE: Nipe jibu, ina utamu wa sukari au chumvi au pilipili?
MFAMASIA: Kama chumvichumvi
MZEE: Hakuna sukari
MFAMASIA: Sukari hakuna kabisa
MZEE: Loh asante chukua hii alfu tano nashukuru sana, dokta alinambia nipime mkojo wangu kama nina kisukari, kumbe sina asante bwana mdogo

Cheki jamaa alivyoumbuka baada ya kuhudhuria semina isiyomuhusu

Jamaa kavamia semina ya wasomi iliyokua inafanyika maeneo ya ubungo plaza bas wakaanza kujitambulisha
1. Naitwa Anna niko SUA mwaka3 nasoma agriculture
2. Naitwa Stella niko UDSM mwaka2 nasoma public relation

3. Naitwa Emmanuel niko UDOM mwaka3 nasoma computer science
bas jamaa nae akainuka kwa kusuasua huku akijishtukia akasema”Naitwa Elisha niko Tanesco mwaka wa 7 nasoma mita”

Mke alichomfanyia mme wake kabla ya kwenda safari, Chezea mawaifu walokole wewe!

JAMAA alimuaga mke wake mlokole kuwa anaenda semina ya siku tatu, kumbe anakwenda kwa bi mdogo.

Mke akamwambia mumewe; “Tupige magoti tusali”,

Wakapiga magoti…:
MKE: Eee baba msaidie mume wangu afike salama safari yake.
MUME: Emen…

MKE: Mpe nguvu katika yote atakayoyafanya huko.
MUME: Emen…

MKE: Akitaka kufanya uasherati ashindwe.
MUME: Kimya…

MKE: Akifanya uasherati apatwe na janga baya kwa uwezo wako bwana.
MUME: …….!!

MKE: Yaani akifanya uasherati afie hukohuko kwa mateso makali.
MUME: Maombi gani sasa hayo!!?. Haya basi siendi semina ufurahi wewe.

Chezea mawaifu walokole wewe!

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About