Vichekesho Vya Asubuhi Hii

Cheki masifa yalivyomponza huyu, Sifa nyingine ni mbaya jamani

Mbongo, Mganda, na Mkenya walikamatwa na makosa Uchina.

Wakaambiwa adhabu ni ama kifo cha moja kwa moja au adhabu nyingine ambayo atakayeifaulu atakuwa huru, atakayeshindwa atauawa.

Basi wao wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao.

Wakapelekwa msituni wakaambiwa kila mmoja aende kwa njia yake halafu arudi na matunda kumi ya kufanana.

Wakaingia msituni kila mtu njia yake.

… Mganda akarudi wa kwanza na machungwa kumi. Akaambiwa adhabu yake ni kumeza moja moja likiwa zima bila kufumba macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa mpaka yote kumi yaishe. Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili, akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi akafa.

Mkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogo kama pili vilaini. Akasomewa masharti. Akaanza kumeza bila kufumba macho wala kulia, wala nini… alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa.

Wakiwa kuzimu Mganda akamwuliza Mkenya, “Vipi, mbona ulishindwa kuvumilia wakati kilibaki kitunda kimoja tu?”

Mkenya akamjibu: “Mkuu, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mbongo anakuja na matikiti maji!”

Kilichotokea Baada ya mlevi na mchungaji kukutana

MCHUNGAJI; “Unakunywa bia!?
MLEVI; “Ndio.
MCHUNGAJI; “Kwa siku unakunywa bia ngapi!?

MLEVI; “Nakunywa bia tano!
MCHUNGAJI; “Bia moja bei gani!?
MLEVU; “2500/
MCHUNGAJI; “Ulianza lini kunywa bia!?
MLEVI; “Miaka 18 iliyopita!

MCHUNGAJI; “Kwa hiyo kwa siku unatumia zaidi ya 10,000??
MLEVI; “Ndio!
MCHUNGAJI; “Kama u gekuwa unatunza hiyo pesa 10,000 kwa siku leo hii si ungekuwa na Range Rover!?
MLEVI; “Samahani, naweza kukuuliza swali!?
MCHUNGAJI; “Uliza!
MLEVI; “Unakunywa bia!?
MCHUNGAJI; “Hapana!
MLEVI; “Nionyeshe Range Rover yako!
MCHUNGAJI; “akasepa”

Faida 3 za uvutaji wa sigara

Ni hizi

1. Mvuta sigara hazeeki
2. Mvuta sigara haumwi na mbwa
3. Mvuta sigara nyumbani kwake haingii mwizi

UFAFANUZI

1. Hazeeki kwa sababu hufa mapema kwa kifua kikuu

2. Haumwi na mbwa kwa vile kifua na mapafu yanapooza na hulazimika kutembea na bakora

3. Nyumbani kwake haingii mwizi kwa kuwa inafika wakati ambapo halali:
atakohoa usiku kucha hivyo mwizi anajua yupo macho
kumbe kikohozi tu!

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About