Kiingereza kinashida kweli, Angalia alichokisema huyu mwalimu
Kiingereza shidaaaaβ¦β¦!
Mwalimu wa chakula alipokuwa anaongea na wapishi akiwaeleza maharage kutoungwa vizur
Kiingereza shidaaaaβ¦β¦!
Mwalimu wa chakula alipokuwa anaongea na wapishi akiwaeleza maharage kutoungwa vizur
1. Awe na pesa nyingi
2.Siyo lazima awe mzuri wa sura
3. Ajenge ukweni
4.Awe mpole
5.Asimuonee wivu mke wake
6.Awe mwenye upendo wa dhati
7.Asishike simu ya mke wake.
8.Akimkuta na mwanaume apite tu, akitaka kujua ni nani asubiri nyumbani
9.Awe anamskiliza mke wake kwa kika kitu.
10.Asipende mwanamke mwingine zaid yake
UKIMPATA MWANAUME MWENYE SIFA HIZO KAPIME DNA LAZIMA ATAKUWA NI BABA AKO.
ππππππππ
MZEE:”sasa huyu mgeni sijui alale wap?”
MKE:”saa hizi ni usiku akalale na Bebi.”
jamaa akaona huyo Bebi pengne mtoto anakojoa kitandani au akalia asije msumbua usiku
JAMAA:”msipate tabu mi ntalala hapa kwenye kochi” akalala
asubh wanakunywa chai akaibuka mrembo,jamaa akapigwa bumbuwazi almanusra ajimwagie chai.
BINTI:”Naitwa BEBI,we unaitwa nani?”
Jamaa akasema mimi naitwa Faraβ¦..!
Jambazi mmoja aliingia kanisani na bunduki akapiga risasi juu ya bati akasema “asiyempenda YESU atoke nje” wakatoka wote ispokuwa Mchungaji na Wazee wawili.
Jambazi likamwambia Mchungaji “unaweza kuendelea na ibada, nilikuwa nakuondolea wanafiki”, Mchungaji akasema “ungewaacha kwanza nichukue sadakaβ¦!
Ticha: Wa kwanza kujibu swali langu ataenda Home mapema..
John kusikia hivyo….Karusha begi la daftari nje…..`Β
`Ticha akauliza: Nani karusha begi nje!?!`*
`John: Mimi….. Kwa herii Mwalimu……` ππ,ππ
Ulishawahi kutana na hiiβ¦.
Issa: mambo
Jeni:poa vp
Issa:poa nambie:
Jeni:poa aje ww:
Issa:poa nambie
Jeni:poa
Issa :bas poa
Jeni:poaβ¦.
Issa:poa badee basi
Jeni:haya
Issa:bai
ππππβ¦β¦..HII KIITALIANO INAITWA LACK OF SOUND ENGINEERING NA HII INASABABISHWA NA UOGAβ¦β¦
Umeenda kutembea ukweni kwako baada ya chakula chausiku unapewa chumba chakulala inapofika usiku unatakakutoka kwenda kujisaidi kwasababu taa zimezimwa unapamia vyombo vya chakula sebleni kipindi unajalibu kupapasa uviweke sawa mala taa inawashwa na mama mkwe anaona umeshika vyombo anakwambia, baba kama ukushiba ungesema
Miaka 13: Usipende wavulana ni wabaya.
Miaka 18: Sitaki nikuone na yule mvulana tena!
Miaka 23: Lini utatuletea mchumba wako?
Miaka 26: Wenzio wanaolewa.
Miaka 30: Tumekuambia kwamba acha
kuchagua sana wanaume, hutaki kusikia!
Miaka 33: Kuna mtu wa Mungu yupo kule
anaombea unaweza kupata mchumba
Miaka 36: At least pata mtoto mmoja.
Miaka 39: We will take care of all the wedding
billsβ¦yeyote ni sawa sisi tutagharamia kila kitu mwanetu wee mlete tu .
Miaka 45: hivi kweli nani alikuroga.?
πππ changamkia fulsa umri ukifika
Rashidi alimpa ujauzito mwanafunzi, akashtakiwa.
Kumbe Rashidi ana bibi yake mtaalamu wa yale mambo yao ya Sumbawanga, akampachika Rashidi i jinsia ya kike.
Alipofika mahakamani kuhojiwa Rashidi akasema sijampa ujauzito kwa sababu mimi pia nina jinsia ya kike.
Kwa kuthibitisha Rashid wakaenda kumkagua basi akashinda kesi, kufika nyumbani Rashid akawakuta watu wamejaa wanalia, akauliza kulikoni?
Akaambiwa bibi yako amefariki. πππππππ°π°π°ππππππ
Kwa sasa Rashid anaitwa Leilaπππ
NAJISIKIA NIMEBOEKAβ¦
SIJUI NIENDE KAMBI YOYOTE YA JESHI NITEREMSHE BENDERA
ALAFU NITOKE MBIOβ¦..
πππππππΎππΎππΎππΎππΎππΎ
Chizi kakaa ukingoni mwa bahari analia kwa masikitiko na huku kakamata kijiko cha chai. Mwezake akamuuliza mbona unalia mwenzangu. Chizi akajibu nimetia vijiko vitatu vya sukari baharini, kila nikionja bado ina chumvi. Mwenzake akacheka sanaaaaaa akamwambia. Hujakoroga!!!!ππππππ
Kuna mtu kanikeraΒ et nmemkubalia urafiki Leo tuΒ Facebook anataka kujua kabila langu
Bac akajifanya mjanjaa etΒ akaniuliza mbu kwenu mnawaitaje
Mimi nkamjibu hatuwaiti wanakujagaΒ wenyewe
πππππππ
Si kwamba cjamuelewa ila sipendagi Ujinga Mimi
Baba na mama baada ya kurudi safari pamoja wakakuta BARUA iko mezani SEBULENI ikisemaβ¦. “Baba na mama, ni matumaini yangu kuwa mtasoma ujumbe wangu huu kwenye karatasi niliyoiweka
juu ya meza, naomba msishtuke mana ni mambo ya kawaida kwenye maisha tunayoishi, najua mtaumia kwa vile bado nasoma na ndiyo nipo kidato cha kwanza⦔ Napenda kuwajulisha kwamba sasa hivi mnaposoma hii barua sipo nyumbani, nimetoroka mana nimegundua
nina uwezo wa kujitegemea kwa sababu mi ni kijana mwenye umri wa miaka 14 na ninajua kipi chema na kipi kibaya.
Tangu mwezi mmoja uliopita nilikuwa na uhusiano nabinti mmoja aliyeitwa Rachel, mwenye umri wa miaka 27 na kwa sasa
ndo naishi naye kwenye chumba alichopanga. Nilipokuwa nyumbani sikuwa napata hela za kutosha ila sasa nimeanza kushika noti za shilingi 10,000β¦ Msichana niliyenaye ni mzuri sana wa umbo na ninampenda sana, amenifundisha njia za kutafuta hela.
Amenipangia kazi ya kuuza madawa ya kulevya na yeye ikifika
usiku anaenda kuuza mwili wake, basi kila siku tunapata hela ya kutosha, huyu mchumba wangu ni msichana mwenye bidii, kwa siku analala masaa 6 tu maana mwanaume yeyote akija lazima awe naye
chumbani kwa muda wa masaa 3.
Msiwe na hofu, nipo salama kabisa na nimeamua kumwoa Rachel mana ni kila kitu kwangu. Pia amenunua gari la kubebea mbao kwahiyo biashara inaenda vizuri.
Rachel ameenda kupima afya na amekutwa na upungufu wa kinga
mwilini, mara nyingi namridhisha anapotaka kitu flani, iwe kufanya naye mazoezi ya viungo au kufanya naye mapenzi, si mnajua unapokuwa na mgonjwa unakuwa naye karibu.
Ila mi pia sijihisi vizuri mana kila saa nakohoa tu na sina uhakika kama nimeathirika. Tumepanga baada ya miaka miwili tutawatembelea, nadhani mpaka miaka miwili iishe atakuwa
ameshajifungua, na ni furaha yangu mtamwona mjukuu wenu. Wazazi wangU, sina la kuongeza kwaherini Mungu
akipenda tutaonana.
NB: “Baba na mama, mimi nipo chumbani kwangu najisomea,
mnachokisoma ni h/work ya mwalimu wa kiswahili alituambia tutunge hadithi fupi ya kusisimua, naomba muiangalie kama kuna
makosa!”
Ingekuwa wewe hapo ndi baba au mama ungefanyaje? SHARE na wenzako wasome.
Recent Comments