Ndio nilikuwa nimeshuka kwenye basi la SAI BABA pale Ubungo, nina Begi kubwa Mgongoni na begi Dogo la Lap Top mkononi, sura inatazama Mbele Very Serious kama nipo kwenye Gwaride la Uhuru!..Mabega juu yanafanya Cheers na Mawingu!, natembea kwa madoidoโฆ..leo nimetoka Likizo Moshi,
“Brother Simu ya ukweli hii..kitu cha Tecno C9 bei poa” hii ilikuwa sauti ya Teja mmoja hivi!
Yaani huyu Teja Bwege kweli,anataka kumuuzia nani sabuni? mimi sio wa kuja!โฆkamwe Siwezi kuibiwa hapa Town,hakuna wizi au utapeli nisioujua!, Mimi nimezaliwa Mwananyamala kwa Manjunju, nikalelewa Tandale kwa Mtogole, Shule ya msingi nimesoma Turiani Magomeni, Hivi Mbwa gani aniibie?โฆkwa Style ipi?
Sipendi kabisa Upuuzi!, Wajinga ndio wataibiwa, sio Mimi!โฆsasa Kwa mwendo wa haraka nikatoka nje kabisa ya Stendi ya Ubungo straight mpaka Stendi ya dala dala za Kariakoo, hapo ndipo nikakutana na Vijana wawili wadogo wakiwa na mzani wa kupimia uzito,โฆhakika napenda sana vijana wanaojituma kama hawa na sio ile Mijizi ya kule ndani Stendi!!,โฆ.hapa sasa nikapata wazo!
“Dogo mnapima uzito kwa shilingi ngapi?”
“Mia mbili tu Kaka!”
”Ok”
Kwa mwendo wa kikakamavu nikapanda juu ya mzani,lengo hapa ni kujua uzito wangu, Mtori niliokula mwezi mzima kule kwa Mshekuu sio mchezo, hapa nahisi nacheza kwenye kg za John Cena,
“Mama wee! Dogo mzani mzima huu kweli? Mbona nina kilo 134?” (Nilihamaki)
“Aaah! Brother huoni umepanda na Mabegi juu ya mzani?”’
Hahaha! kweli nimechanganyikiwa!โฆSasa nikatoa mabegi yote mawili na kurudi juu ya Mzani, hapa ndipo Uzito ukashuka kutoka kg 134 mpaka kg 56!โฆMy God kweli Body la “One Pack ” haliongopi! thats means mabegi yaliniongezea kg 78! duh hii ni hatari!
“Yaani we Dogo kitambi chote hiki kg 56? huu Mzani Mzima kweli?”
Kimyaโฆ
“Dogo huu Mzani vipi?”
Kimyaโฆ
Dogo ana dharau huyu!โฆSasa ndio nikabandua macho yangu toka kwenye kioo cha mzani ili nimtazame huyu dogo asiyejibu!โฆ.ndipo macho yangu yakakutana na Kigoda tupu kilichochongwa Mvomero!โฆDogo hakuwepo!โฆ.na Mabegi pia hayapo!โฆlap top haipo!โฆ.NIMEPIGWA!
Ni dhahiri watoto wa Mjini walikuwa wameniacha juu ya Mzani, wamechukua Lap top ya Milioni na wameniachia Mzani chakavu wa elfu 40, what a stress!โฆ.sasa nilirudisha macho kwenye kioo cha uzito na sasa kilisoma KG 38!โฆyaani dakika hii hii nimepungua kilo zingine 18, Hakiyamama nahisi hata utumbo wangu wamebeba!โฆniitieni Ambulance!
๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ
Recent Comments