SMS Nzuri: Meseji za Vituko Vya Kujienjoi Leo
Kilichotokea baada ya mzungu na mbongo kukaa siti moja, bongo wasanii wengi
Mzungu akamdharau sana Mbongo nakujiona anajua kila kitu duniani!,
Akamwambia Mbongo waulizane maswali na Mbongo akishindwa anatoa sh.500 na endapo yeye atashindwa atatoa 100,000/=.
Mzungu akauliza ni nchi ipi ilishindwa kwenye vita kuu ya kwanza ya Dunia?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hajui.
Na yeye akamuuliza Mzungu ni kitu gani kikienda juu kina miguu minne na kikirudi chini kina miguu mitatu?
Mzungu akafikiria akakosa jibu akatoa 100,000/= kuashiria hajui ila akataka kujua, akauliza ni nini hicho?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hata yeye hajui!.
SHARE na marafiki kama umemkubali Mbongo kwa ujanja. Lakini unafikiri Mbongo huyu kwa akili hizi atakuwa ametokea mkoa gani!?.
Mambo ya kijijini haya!
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuniβ¦unaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuniβ¦ππππ
Angalia anachokisema Madenge sasa
MWALIMU kaingia darasani na kusema. “Wanaojijua wajinga wasimame”.
MADENGE akasimama peke yake.
MWALIMU: Wewe ndio mjinga?
MADENGE: Hapana, ila nimeona umesimama peke yako nikaona usijisikie vibaya angalau tuwe wawili.
Tabia za wachepukaji
WACHEPUKAJI WENGI WANATABIA HIZI
1.Hachezi mbali na simu yake kila wakati.
2.Inbox na sending items hufutwa kila
wakati.
3.Ukimuomba simu yake ghafla lazima
akwambie hebu
kwanzaβ¦β¦.
4. Kamwe haiiti always vaibration.
5. Namba nyingi ha save.
6. Kuna simu hapokei hata
iwejeβ¦.anapenda sms zaidi
7.Majina mengi kwenye simu yameseviwa
kwa majina ya
kufikirika.
8.Muda mwingi ni mtu wakujihami.
9.Anapenda password na anabadili mara
kwa mara.
10.Akiazima simu yako, akitumia tu
anafuta dial no
haraka.
11.Always yuko na simuβ¦..hadi bafuni
ikibidi.
12. Anajazba ukimuuliza chochote kuhusu
simuβ¦.anajishtukia.
13. Akiwa anachati anakuangalia mara kwa
mara
kiwiziwizi
14. Hana jeuri ya kukuweka profile picture
na akikuweka
humalizi masaa anakudampu huko
Hapa kuna ukweli asilimia millioni moja
kabisa
Share na washikaji zakoπππππ
Misemo 17 ya kuchekesha
1) gari la kuvutwa halina overtake
2) kisigino hakikakai mbele
3) wimbo wa taifa haupgwi disko
4) feni haiwashwi beach
5) mshkaki hauchomwi kwa jiko la ges
6) mganga haagiz tembele
7) hata bibi alikuwa bint
8) mke wa mtu sumu,mume wamtu maziwa
9) kipara bila pesa ni kovu
10) mbwa hanenepi migiuu
11) picha ya rais haina bodyguard
12) mjini shule kijiji tuition
13) saa ya ukutani haivaliwi mkonon
14) heshima pesa shkamoo makelele
15) ulinz pesa bastora mzgo
16) kuku ni kuku jogoo mbwembwe
17) kusoma kuelewa kukesha mbwembwe
Jambo la kufanya ukitaka mwanaume akusaidie kazi jikoni
Fanya hivi
Ukitaka mwanaume akusaidie kazi jikoni mwambie “NAOMBA CM YAKO NIWASHE TOCHI TAA IMEUNGUA”
atakusaidia kumulika mpaka unamaliza kazi zako zooteπ
Mimi ndio nimeelewa hivi!
Leo nimepishana na Vitz imeandikwa, “Never trust women”
Nikajua huyu mtu lazima alikuaga na Range Rover
ππππππ
Kweli shilingi yaua, Huyu jamaa kapatikana, angalia anachomjibu mke wake,
Jamaa alikuwa anagombana na mkewe,hatimae
akamwambia kwa ukali
“Unajua nimechoka sasa, haya kusanya nguo
zako naβ¦β¦..
Kabla hajamalizia sentensi simu
ya mkewe ikaita, kumbe alikuwa ni baba yake.
Basi mzee akaanza kuongea na binti yake huku
jamaa anasikia
“Aisee mwanangu nimebahatika kuuza ile
nyumba yangu sasa nimeona niwatumie milioni
20 mjaribu kuanzisha mradi na mwenzio.
Haya mwambie yeye nitampigia kesho kama
ana mradi mwingine nimpe hela kidogo”.Baada
ya simu kukatwa mke akamgeukia jamaa
akamuuliza,”eeenhee!!! ulikuwa unasema
umenichoka nikusanye nguo zangu halafu
iweje? Jamaa kwa upole akajibu “Nilikuwa
nasema ukusanye nguo zako na unipe nifue”.
Wanawake wa leo mbele ya hela. Hii ni hatari
MDADA: Baby nikwambie kitu
MKAKA: Yeah Baby Uko huru nambie
MDADA: nilikua naomba hela babyβΊ
MKAKA: WW nae kwa kupenda hela jana tu nmekupa hela Leo unaomba ya nn π
MDADA: hapanaπ Bby sio hivyo nlikua nataka nikashuhudie tetemeko la ardhi BUKOBA nasikia huko linaonekana vizur .
ππππππππ
Wanawake kumbukeni sio vizuri
Alichokisema mtoto baada ya kusikia baba na mama wakiongea mambo yao usiku
MUME: Mke wangu naomba nikubusu
MKE: Sitaki
MUME: Ntakununulia pete ya gold
MKE: Staki
MUME: Ntakununulia gari
MKE: Sitakiβ¦.mtoto wao aliyekuwa kalala alisikia haya maneno ya mwisho
MTOTO: Baba basi nibusu mimi uninunulie baiskeli
BABA: Pumbafu lala huko mjinga mkubwa
Wazo la asubuh – penzi la kuku
Wazo la asubui
πPenzi la kuku sekunde 2 ila vifaranga kibao.Lakini binadamu masaa kibao mtoto 1 au 2. Sasa binadam na kuku nani JEMBE? Ukimwona JOGOO popote piga SALUTI!ππππππππukinuna poa tu!!!!!ππππππππππππππ
Wanaume ni noma, Angalia huyu alivyomdanganya huyu π§ girlfriend wake
Jamaa kamdanganya girlfriend wake kuwa anasomea HOTEL MANAGEMENT. Siku huyo girlfriend akamkuta jamaa anaosha vyombo kwa MAMA NTILIE.
Girlfriend akamuuliza jamaa βbeby vipi mbona uko hapa?β Jamaa bila woga akajibu βNIPO FIELD.
Wanaume hatupendi ujinga sisi π π π
Angalia huyu mwanafunzi anachomjibu huyu mwalimu wake
1. Ticha:”Punda ni mnyama anaefugwa nyumbani,lakini akiwa mwituni anaitwa pundamiliaβ¦.Je sungura anayeishi mwituni anaitwaje?”
ZUZU:”Sunguramilia.”
2.Ticha:”Rais wa kwanza wa kenya aliitwa KENYATTAβ¦Je rais wa kwanza wa
Tanzania aliitwaje?”
ZUZU:”TANZANIATTA.”
3. Ticha:”Kuku yuko katika jamii ya NDEGEβ¦Je samaki yuko katika jamii ya nini?”
ZUZU:”MELI.”
4. Ticha:”Coach wa Arsenal anaitwa ARSENE,wa Man-city anaitwa MANCINIβ¦.Je wa
Liverpool anaitwaje?
ZUZU:”LIVER.”
5 Ticha:”Ukiwa na mbuzi 10,wezi waje waibe 5,utabaki na nini?”
ZUZU:”Hasira nyingi sana!”
Angalia huyu ticha wa Hesabu alichofanyiwa
Looku Looku* ππ
*Ama Kweli Mkuki Kwa Nguruwe kwa Binadamu Mchungu Skia Hiiβ¦.!!*
*Ishawahi kutokea Pale nilipokutana njiani na mwalimu aliyekufundisha MATHS secondary afu akaniambia nimuelekeze njia ya kwenda sehemu fulani.*
*_Nenda mbele kama 2KM hivi kisha kata kushoto,ila hakikisha ANGLE inakuwa ni 30.5 KUSINI MASHARIKI.Kisha tumia PYTHAGORAS na hakikisha una FOUR FIGURE ili kupata thamani ya ANGLE._*
*Mwalimu alisonya na kuondoka.*πππππ
*Stakagi ujinga kabisa mimi, wakati ananichapa alifikiri sifa*ππ
π ππ½ππ½ *Mniache Tuu Mimi Sio Kwa Bifu Ilo Aiseee*ππΎ
Jinsi Baba na mtoto wanavyoweza kuwaziana
Duh! Maisha
Ile time unawaza baba angekua MO DWEJI baba ako na ye anawaza mwanangu angekua MBWANA SAMMATA
Ni shetani tu anajaribu kucheza na akili zenu
ππππ
Baada ya kunitumia SMS usiku ikawa hiviβ¦.
Jana usiku kuna Jirani yangu..kanitumia text “mambo vipi?”β¦halafu tunakaa nae mtaa mmoja nikaona nikimjibu ni uharibifu wa hela nikaenda kumgongea mlango saa 7 usiku. Alipofungua nikamjibu “shwari”halafu nikarudi nyumbani kulala zangu..
Sipendagi kuchezea salio..
πππππ
Hawa ndio wanaume wanaoweza kushinda vishawishi
Wanaume wenye kushinda vishawishi ni;
Wanaume ambao mnaweza kula wali hadi mwisho bila kugusa nyama nyie ndio mnaweza kushinda vishawishiπ€£π€£π€£π€£π€£
πββπββπββπββπββπββ
Recent Comments