SMS Nzuri: Meseji za Vituko Vya Kenya
Nilichomfanyia huyu aliyenizingua nilipomuazimisha pasi
🙄🙄🙄🙄🙄🙄
Jana nimeenda kuazima pasi chumba jirani, ili ninyooshe nguo zangu, Jamaa wakaniambia nichukue nguo nikanyooshe room kwao maana hawataki pasi yao itoke.
Sasa leo amekuja mmoja wao kuazima mopper akasafishe room, nimemwambia aje adekie humu humu…
Jamaa ameondoka nadhani atakua ameenda kuchukua maji
🤒🤒🤒
Angalia kilichotokea baada ya dogo kupewa ada na kuitumia kubeti
Dogo kampigia simu baba yake;
DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa
nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti
BABA : Unasema nini we mpumbavu mshenzi
mkubwa? Nimekukanya mara ngapi kuhusu kubeti?
DOGO : Lakini baba
BABA : Lakini baba nini ngoja urudi utaona
ntakachofanya.
DOGO : Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda
shilingi milioni 3
BABA : Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu
sana kwanini hukutumia laki nzima kubeti? Si
ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi niwataarifu
ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua
haraka mwanangu mpenzi…
😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Read and Write CommentsBaada ya mwanamke kukataa kufungua mlango angalia kilichomkuta
MUME: Fungua mlango!
MKE: Leo sifungui! Nimechoshwa na ulevi wako.
MUME: kama hufungui najitupa kwenye hili shimo nife kabisa.
MKE. Kufa huna faida yoyote duniani!
MUME kachukua jiwe kubwa kalitupa kwenye shimo chubwiiiiiii!
MKE kajifunga kanga, kafungua mlango. Ghafla mume kaingia ndani na kumfungia mke nje.
MKE: Nifungulie la sivyo nitapiga kelele majirani waje.
MUME: Piga kelele na wakija uwambie unakotoka usiku huu na khanga moja.
Read and Write CommentsNilichokifanya jana baada ya kushuka kwenye basi Ubungo
Jana nateremka kwenye BASI UBUNGO nataka nichukue TEKSI hadi KIMARA naambiwa sh.15,000/=.
Wakati niponatafakari hiyo bei, nikasikia “Moro, Moro,Morogoro sh.6,000/=”
Nikaamua nipande niende zangu MOROGORO.
Kwenda na kurudi sh.12,000/=.
Wakati wa kurudi nikamwmbia KONDA aniteremshe KIMARA.
SIPENDAGI UJINGA MIMI NA BEI ZA TEKSI.
Read and Write CommentsHuyu mwanamke kazidi sasa
Jamaa: Mambo honey, upo ok?
Mrembo: Sipo ok my dear
Jamaa: Una tatizo gani baby?
Mrembo: Nimetoka hospitali kupima, nna mimba.
Jamaa: Weeh usiniletee balaa hiyo mimba imeingiaje wakati huwa tunatumia kinga?
Mrembo Kwani nani kakwambia mimba ni yako, hebu tuliza mshono huo.
😆😆😆😆😆😆😆
MTATUUA
Kali za leo: Misemo ya kuchekesha na kuvunja mbavu
1. Ati wee ni m-black mpaka ukiingia kwa dinga(gari), dirisha zinakuwa tinted!
2. Kwenu kuchafu mpaka mende zinatema mate.
3. Vile wewe mfupi, ukipiga picha ya passport inatokea full.
4. Ati(house) yenu ina gate lakini hakuna fence.
5. Baba alienda ku buy ngombe akaona ikikojoa akasema sitaki hiyo imetoboka.
6.Wee mblack mpaka ukikutana na mzungu afternoon anakusalimia: Good evening.
7. Mko wengi kwa house mpaka kuna rush hours na kukinyesha kunakuwa na jam.
8. Paka yenu noma mpaka ikishika panya inaomba chumvi, fork na pilipili.
9. We ni mrefu mpaka ukikunywa maziwa inafika kwa tumbo ikiwa mgando.
10.Wewe ni mweusi ukikanyanga makaa unawacha footprint nyeusi.
11. Kwenyu mkikunywa maji mnaitisha toothpick
12. We ni mbishi hadi ulikataa kuzaliwa uchi
13. Kwenu kuna insecurity ikifika usiku hadi geti mnaingiza ndani
14. Kwenu ni wengi sana hadi mmeweka round about ndani.
15. Wewe ni mlafi hadi maji uliyochemshia mayai unayafanya supu.
16. We ni mjinga sana hadi blood test ulifeli.
17. Una chogo refu hadi ukigeuka haraka unaweza kuliona.
18. Una kichwa kikubwa hadi ukiingia kwenye daladala konda anakwambia “abiria usiingie na mizigo, tunaweka juu kwenye carrier
Read and Write CommentsDuh! Angalia alichokula huyu mwizi! Wizi mwingine bwana!
Baada ya mwizi kuvunja mlango huko Tarime, akaingia kwenye stoo akaona vinyama kwenye bakuli vikiwa vimekauka. Akaonja 1 akaona kitamu na kina chumvi! Akavila vyote. Alipomaliza akaangalia juu ya mlango akaona pameandikwa; “chumba cha UKEKETAJI WANAWAKE”. Unafikiri atakuwa amekula nini?
Read and Write CommentsSababu ya mwanaume kunya kitandani alipokuwa kalala na mke wake
Jamaa flani alikuwa amelala na mkewe. Mara akamuona mtu amesimama kitandani.
Jamaa akafoka, “Toka hapa, we ni nani mpaka unakuja kitandani mwangu?”
Yule mtu akajibu, “Mi ni malaika na hapa sio kitandani mwako uko mbinguni!”
Jamaa, “Huh! Inamaana nimekufa,mbona mi bado kijana… naomba nirudishwe!”
Malaika, “Inawezekana lakini siwezi kukurudisha kama mtu labda urudi kama mbwa ama kuku.”
Jamaa akakumbuka mbwa wanavyopata taabu ya kulinda, akaonelea arudi kama kuku.
Malaika akamgeuza kuku, akamwambia ajifunze kutaga kabla hajapelekwa duniani.
Akachuchumaa na kuanza kujikamua; yai la kwanza likatoka. akajikamua tena, yai la pili likatoka. Akajikamua tena mara ya tatu.
Wakati yai la tatu linatoka… akashtukia amepigwa konde ikifuatwa na sauti ya hasira ya mkewe, “Pumbav*! Balaa gani hii…. unakuny* kitandani!!”
Read and Write Comments
Recent Comments